Tuwe Baraka kwa viongozi wetu kiroho!!

pastor

TUWE WA BARAKA KWA VIONGOZI WETU KIROHO ILI NAO WAFIKE MBINGUNI

Shalom!

Kuna umuhimu kuhakikisha tunakua wa baraka kuingia na kutoka kwetu chini ya Watumishi (Wachungaji) walioaminiwa na Bwana kutulea, ili kusaidia kuweka mazingira mazuri, wafanye kazi ya BWANA kwa amani, utulivu wa moyo na akili,kuwawezesha kua na UMAKINI KUMSIKIA MUNGU KWA USAHIHI AZUNGUMZAPO NAO mambo ya utumishi na kwa ajili yetu na hatimaye wafanyapo yale waliyoagizwa na si vinginevyo, basi wahesabiwe kua ni  Watumishi watiifu na ivyo wao pia wafike mbinguni kama vile sisi kondoo tunavyopenda tufike.Katika somo ili, tuangalie hali/tabia ya Wapendwa wa kanisa la jangwani walivyotenda isivyo vema mbele za Bwana na Mchungaji wao Musa, ikawaletea hasara kubwa wao na Mchungaji wao.

Japokua sisi sote ni spesheli wa Bwana-1Petro.2:9-10 na tumetengwa toka dunia hii au kati ya Watu kwa kusudi maalumu(Kumwabudu na Kumtumikia Jehova-Kut.8:1), ni ukweli mwingine pia kua kutoka kati yetu tuliotengwa kwa makusudi ya  Bwana mwenyewe, wanatengwa baadhi/WANATOLEWA-wanakua APPOINTED – 1Wakor.12:28-30, Waf.4:11-12 ili watuhudumie roho zetu-Ebran.13:17, kufanya kazi permanently hemani-Hesb.18:1-32 na pia kulihudumia Neno muda wote-Mdo.6: 4 

Ugumu, Unyeti wa kazi/jukumu la wenzetu hao, unatokana na kweli kama Mungu mwenyewe ndiye anayewa-appoint kwa toka kati yetu kwa iyo special task, Roho Mtakatifu kuwasemelea uzito na unyeti wa kazi yao kwa kiasi hiki-Wabr.13:17 kua LAZIMA watatoa hesabu ya JUKUMU ILO MBELE ZA MUNGU na pia ukweli kua wao pia ni wanadamu kama sisi-Yak.5:17 na kwakua si malaika ivyo kuingiwa huzuni, kuchoka, kukosea,kujuta,kuchoka, kukata tamaa,kuchanganyikiwa-1Wafalme.19:1-10, kushawishika kujitoa ktk utumishi, kutiwa kasirani, kuchukizwa, kukwaza vibaya nk ni mambo yanayoweza tokea/wapata ikiwa hatuta angalia ili tuwe wa baraka kwa ingia,kaa-kaa na toka yetu tukiwa  chini ya ulezi wao, lakini  tukihakikisha tunawatia moyo na kusisima nao kama wana kwa baba wa kiroho, hata kuwahurumia, kuchukuliana nao na kuwarehemu kama wanadamu wenzetu maana wana jukumu nzito, na kama viungo ktk mwili mmoja-1Kor.12:12-27, tukapendana na kushirikiana, basi tutakua tumefanya vema kabisa hapa na mbele za Bwana.

Kama kuna Mchungaji wa ajabu kwa uzuri, mzigo na upendo wa kuitenda kazi ya BWANA kwa kujitoa maisha yao yote kulea kondoo, aliyewahi kuwepo ktk uso wa dunia baada ya Yesu basi na Musa naye anayagusa na kuya-challenge maisha yangu sana kabisa.

Ni wazi Mungu alimuita-Kut.3:1-20 wala HAKUJIITA!!!!! Alichunga kundi ambalo hata Yesu mwenyewe anadokeza kua lilikua na shingo ngumu hadi kupelekea Musa kama kiongozi wa kiroho kuwatengenezea utaratibu (by-law) wa ku-handle mambo yao ya ndoa tofauti na original plan ya Mungu(main-law)-Marco.10:4-6.

Ni kundi ambalo si tu Yesu alisema lilikua ni kazi kulichunga lakini Mungu Baba mwenyewe aliwahi kusema maneno ya uchungu kweli kuhusu ingia na toka yao mbele zake- Kut.32:9 Kut.33:33Hesb.14:11,20-23,26-35. Biblia ya Kiingereza NKJ ilivyoweka ukweli huo ktk mstari wa 9 wa Kut.32, nimependa- inasema kuhusu hali ya kanisa lile la jangwani kwamba-‘’Nimewaona Watu hawa, KWAKWELI au KWA HAKIKA ni watu wenye shingo ngumu!!!-imagine mpaka Mungu achoke ivyo na kushangaa/kuumia hata kusema ‘’INDEED = truly/certainly/for sure/actually/ no doubt/ definitely/ ….’’these people are stiff-necked’’. Kuna nyakati walinungunika na kuongea maneno mabaya sana, Mungu hakuvumilia, akatuma nyoka wa moto kuwauma, wakafa wengi- Hesabu 21:4-9, wakati mmoja pia hasira ya Bwana iliwaka, moto ukawaka na kuwateketeza baadhi nje ya malango-Hesb.11:1-2. Pia waliwahi hata kutaka fanya mapinduzi, kumng’oa kihuni na kwa jabza Mchungaji wao Kiongozi Musa-Hesb.14:3-4 ili kusimika mwingine na kutaka KURUDI MISRI-(utumwani/dhambini/matesoni/kwa miungu ya kigeni kuitumikia!), yaani KUIFANYA PLAN YA MUNGU KUWATENGA=KUWAKOMBOA IWE NULL AND VOID!!!!!!!!!,

Si ivyo tu hata walishawahi  kasirika mpaka  Mchungaji wao kuona wazi wako karibu kumuua! (piga mawe) Kut.17:4, Hesb.14:10-( can you imagine that for a second? kwamba wapendwa wanaheuka kiasi hicho hata kuonekana wanaweza fanya kitu mbaya  i.e. to KILL Mchungaji wao Kiongozi?!!!!!!), mbaya kuliko yote  ni wakati Mchungaji wao Musa amekawia toka ktk uweponi mwa Bwana mlimani, wao wakaona hamna haja ya kumngojea kupata maelekezo ya Bwana, wakaamua kujifanyia mungu kwa mikono yao wenyewe na hata kumu-infuence ‘Mchungaji Msaidizi’ kuingia ktk uasi na kufuru iliyovuka mipaka,akukubali kuwaongoza ktk mchakato wa kuumba ‘mungu ndama’  kisha kumuabudu, kumchezea na kumuimbia hata kumpa hadhi kubwa sana kua ndiye yeye aliyewatoa Misri wala si Mungu Yehova-Kut.32:1-6

Kwa mwenendo wa Wapendwa hao mbele za Mungu na Mchungaji wao ,ulipelekea  Mungu  KUTAKA FANYA MAAMUZI MAGUMU dhidi yao –Kut.32:10= kuwafuta wote mara moja!! wana bahati/neema kua na aina ya Mchungaji ambaye kweli alikua ameitwa, mwenye mzigo na kazi ya Bwana ya Kuchunga watu wake na moyo wa kuwasaidia wafike Caanan( Mbinguni) ndio maana akawakingia kifua kwa kumuendea Mungu kihoja –Isaya.43:25-26–  aka-mchallenge Mungu sana- Kut.32:11-14  mpaka ikamuingia/gusa na  Yehova akaghairi kuwatenda kitu mbaya mno, mfano,  ili kondoo wake wapone gadhabu ya Bwana wa majeshi, alimwambia Mungu kua yuko tayari yeye kufutwa toka kitabu chake Mungu-Kut.32:30-33. 

U-shingo ngumu wa wapendwa dhidi ya Mungu na Viongozi wao Kiroho- Mchungaji Kiongozi na Wasaidizi-Joshua na Haruni, uliendelea na ingawa kuna nyakati Mungu aliwasamehe walipoomba na kuombewa rehema na Musa, lakini wakati mwingine alisamehe na kuadhibu pia-mfano siku ile ile walipovuka mipaka ya uovu na kufanya kufuru ya kutengeneza mungu ndama, Mungu kupitia Musa aliamuru wana wa  Walawi kuua ndugu, jirani na jamaa zao, wakafa watu alfu 3 mara moja!-Kut.32:26-28

Wapendwa hawakuwahi kujirekebisha maana hata siku ile  walipopata habari toka Wapelelezi 10 kuhusu Watu wanaoikaa Nchi wanayokwenda kuirithi kua ni ya majitu, wakaongea mbovu, Mungu akawapiga kwa tauni wakafa wale wapepelezi 10 walioleta habari na kusababisha kundi kulalamika-Hesb.14:36-37 na kisha akataka kwa mara nyingine kuwafuta wote kisha kupitia Musa, Mungu atengeneze-lizaliwe Taifa jipya kubwa na lenye nguvu zaidi. Ila Kama kawaida Mchungaji wa ukweli Musa, ingawa naye alikua anavurugwa na kuchoshwa na kondoo zake wale, bado ktk moyo wa ubaba/Uchungaji, alitoa hoja nzito mbele za Bwana kuwatetea Watu wake-Hesabu.14:11-20

Bahati mbaya neno likatimia kua aonywaye mara nyingi akishupaza…..ivyo mwishowe Mungu akafanya sasa MAAMUZI MAGUMU!-Wale wote waliokua na vurugu safarini, waliomtesa Mchungaji wao, kumsumbua, kukufuru, kulalamika na kunung’unika , Mungu aka APA kwa nafsi yake kua, hawatairithi Nchi aliowahaidia na  pia akasema atahakikisha wana wao ndio watarithi lakini wote kuanzia miaka 20 kuendelea isipokua Jushua na Kalebu, atahakikisha wanakufa wote jangwani, wana wao watazunguka jangwani miaka 40 wakati wakiwa wanachunga mifugo, wanapita uko na kule jangwani, watashuhudia maiti/mizoga ya Baba zao na watabeba uasherati wa wazazi wao walioufanya-Hesb.14:20-35

Masikitiko makuu ni kwamba, Mchungaji mzuri na wa ajabu kama Musa na msaidizi wake Haruni, masikini wa Mungu, AKAKOSEA KUSIKILIZA KWA MAKINI MAAGIZO ya Mungu ya namna ya kutatua tatizo la ukosefu wa maji wakati wana Israeli walipoanza tena kulalamika vibaya na kumkasirikia Musa walipopata kiu wakati hakuna maji-Hesb.20:1-12. Mungu alimwambia  AUAMBIE mwamba MBELE YA MACHO YAO nao utatoa maji, lakini akiwa amekasirika( bila shaka kama mwanadamu-alichoshwa na aina ya kondoo wale wasiobadilika na kuwa wa baraka kwake yeye kama kiongozi, akatokea mbele zao baada ya kusikia toka kwa Bwana, akiwaambia…’’Sikieni sasa enyi Waasi(wajua mpaka uwaite-address watu ‘enyi waasi’-alikua amekasirika na kuchoshwa kwelikweli), Je TUWATOKEZEE MAJI ktk mwamba huu? Kisha akainua mkono wake na KUUPIGA(si kuu-ambia) ule mwamba mara mbili….maji yakatoka tena mengi licha ya kwamba alifanya TOFAUTI NA MAAGIZO YA MUNGU!!!!!!!!! Ndipo Mungu akasema, kwa kua Musa na Haruni HAWAKUMWANI NA KUMSTAHISHA/HESHIMISHA mbele za Wana Israeli, kwa kosa hilo na wao HATAWAINGIZA Nchi ya ahadi. Mwisho wa Mchungaji mzuri kama huyo, unakua ivyo kwa masikitiko makubwa, kisa? aina ya Wapendwa wale, toka, ingia na kaa-kaa yao mbele ya Mungu na Kiongozi wao wa kiroho, wamekua wanamtia pressure/misuko-suko mingi muda mwingi vya kutosha hadi ikapelekea kutotenda ACCURATELY kama Mungu alivyoAGIZA.

Kwa vile jinsi tunavyoenenda ktk maisha yetu na Viongozi wanaotuchunga, inaweza kua na madhara hasi kiasi cha wao kutoingia Canaan( Mbinguni), basi ni muhimu sana tukajihoji, je tuwa baraka hapo tulipo au ni wasababisha matatizo, pressure mbaya, vurugu, mateso, majuto, shari,uasi, mapinduzi nk. Lakini ikumbukwe pia kua madhara hasi si tu yanaweza mpata Kiongozi wetu bali na sisi pia kama yalivyowapata wenzetu.Nawashawishi kua kila mmoja akusudie kua Mtu wa kubariki moyo wa Mungu na Watumishi pale tunapolelewa , kwa Baba zetu wa kiroho

Press on.

Edwin Seleli.

Advertisements

4 thoughts on “Tuwe Baraka kwa viongozi wetu kiroho!!

 1. somo zuri sana ,Mty 10:40-42 Hawa ni wanadamu Yesu anawaambia sio malaika, hawa ni wale waliobeba huduma tano Waefeso 4:11, hawa wanaotakiwa kubeba huduma hizi ni sisi (wanadamu). Bwana Yesu anasema na mitume, ukiwapokea hao umempokea yy, ukimpokea yy umempokea Mungu Baba, nimesoma nikaona Mungu hutuma mtu kwa ajili ya mtu .
  Matendo 10:5-6, Matendo 9:7-8, 10-19.
  Asanteni sana

 2. Seleli,
  Kwa vile hapa ni mitazamo tu, mimi naona hakuna haja ya kuendelea kumheshimu mchungaji anayepotosha Biblia. Hata kama atajiitaje mf, nabii, mchungaji mteule nk, kama anapotosha waumini, ni mchungaji anayeangalia mifuko ya waumini, haombei watu hadi wametozwa kikumi/chochote, ana vitisho tu kwa waumini wake,huyo si mchungaji wa kuheshimu.
  Kuwa Baraka kwao, ni kutoa zaka na kulishana neno la Mungu tu basi. Japo wachungaji wengine huwa hawakubali kuwa kuna waumini wanaowazidi uelewa wa neno. Utakuta wanataka kuheshimiwa tu kwa sababu wao ni wachungaji hata kama wanaburuza mambo kwa kutoelewa!!
  Mimi niko makini sana na wachungaji. Ndiyo maana, napendekeza kwa wanaSG kumheshimu mchungaji mmoja tu – Yesu Kristo. Wengine wana vyeo vya uchungaji lakini hawaendi popote.
  Huu ni mtazamo wangu tu

 3. Asante Seleli kwa fundisho lako.

  Biblia inasema:”Mathayo 26:31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.”

  Ina maana Ibilisi anawatafuta hasa wachungaji awanase ili waumini awapate kirahisi. Kuwahimiza wachungaji wetu ni kusaidiana kumpiga Ibilisi.

  Inatubidi kuwaheshimu wachungaji. Hawa ninaosema ni wale waliyoitwa kikweli na Mwenyezi Mungu.

  Lakini Bwana Seleli, Baraka ipi tutakuwa kwao? Fedha kam wengine wengi wanadhani, kuwatumikia na nguvu zetu, kuwatengenezea vyote ili wasichoke, kuwaombea, nk?

  Mungu akubariki.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s