Breaking News: Wakamatwa wakifanya mazoezi ya Kigaidi Mtwara!!

alshabab

Vijana 11 wamekamatwa Mkoani Mtwara wanafanya mazoezi katika msitu wa Makolionga na CD zenye mafunzo ya kigaidi za Al Qaeda na Al Shabab pamoja na zana za hatari.

–ITV

…………………………..

Habari kamili

POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab.
Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen ameuambia “mtandao wa Kusini Leo” kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema: “CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al-Shabaab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd Amin na Mogadishu Sniper,” alisema Stephen.
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha Sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.
Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary (39) mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail (27). Abdallah Y. Hamisi (32), Salum Wadi (38), Fadhili Rajabu (20), Abbas Muhidini (32), Ismail Chande (18), Said Mawazo, Issa Abeid (21), na Ramadhani Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha Likokona.
Kuhusu vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda Zelothe alisema, “Tumekamata mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi, Betri, Simu za kiganjani 5, Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu, Vitabu mbalimbali wa dini ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150 na virago vya kulalia. Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima.

Kanisa zidisha maombi……

Advertisements

2 thoughts on “Breaking News: Wakamatwa wakifanya mazoezi ya Kigaidi Mtwara!!

  1. HEE HALELUYAAAA!! HUO NI WAKATI WA BWANA WA MABWANA KUJITUKUZA!!!! ITAJULIKANAJE KAMA MUNGU WETU ANAWEZA? LAZIMA FARAO AWAFUATE WAISRAELI KISHA ATUMBUKIE KWENYE BAHARI YA SHAMU. SASA KUMEKUCHA JAMANI KAZI NI TATU, KUWA WATAKATIFU, TUSIJICHANGANYEEE!!!! TUSOME NENO LA MUNGU ILI TUWE NA SILAHA, KISHA KUTUPA MAKOMBORA MBONA WATASIMULIA?!!! LA MSINGI UKICHOKA TUMIA DAMU YA UKOMBONZI YA YESU KRISTU MWANA WA MUNGU ALIYEHAI BOMOA KWA KUTUMIA DAMU YA YESU, HARIBU, FARAKANISHA, FUNIKA MAKANISA YOOTE KWA DAMU YA YESU! USISAHAU KWENDA KINYUME NA KISASA CHA HUYO IBILISI HARIBU NA CHENYEWE KWA DAMU YA YESU KISHA SIKILIZIA!! WATAOKOKA TUU! MAANA KULE WATAKUWA WANAPIGANA WENYEWE KWA WENYEWE NA HUKU KWETU AMANI TELE WATAKUJA WENGI HAOOO! KISHA YESU ANAVUNA WATU WAKE WENGIIII!!!.
    Mungu awabariki sanaaa!!!

  2. me naona wakati wa mavuno umefika jamani, tukazane kuwa watakatifu ili Mungu atakapokuja atukute tayari. Hata tukiomba sana Neno lake halita dondoka mpk limetimia alichokisema yeye. lakini sio ninasema usiombe hapana ombeni bila kukoma ili atakapo kuja mwana wa Adam akukute tayari.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s