Live recording ya John Lisu ilipangiliwa vema!!

Ubora wa mandhari wa Live Recording pamoja na Itifaki ya Mtiririko wa waimbaji ndio uliosahaulisha machungu ya Maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam, Morogoro, Pwani , Zanzibar na nchi jirani Kenya waliochelewa kuingia ndani ya ukumbi wa CCC Upanga kufuatia utaratibu mpya wa usalama wakati wa kuingia kwenye Live Recording ya “Uko Hapa” ya Mwanamuziki John Lisu.

Siku ya Jana katika Ukumbi wa CCC Upanga Mwanamuziki wa Injili John Leonard Lisu ameandika historia kwa mara nyingine kwa kurekodi albam ya pili ya DVD katika Ukumbi huo. Kabla ya John Lisu kupanda na Kuanza kurekodi watumishi wengine wa utangulizi walianza kazi ya kusafisha njia hiyo. Wanamuziki waliohudumu ni pamoja na Mbomby Johnson, Neema Gospel Kwaya, Pastor Paul Safari, Paul Clement na Abedinego Hango.

John Lisu alipanda round ya kwanza na kurekodi nyimbo 12 mfululizo ambapo katika nyimbo hizo 12 amemshirikisha mwanamuziki maarufu wa Kenya Timothy Kaberia, pia amemshirikisha Mwanamuziki bora wa Injili Barani Afrika katika Ukanda wa Africa Mashariki Christina Shusho. Katika Collable hilo la John Lisu na Christina Shusho lilikuwa la aina yake na kukonga nyoyo za watu. Mwanamuziki John Lisu alirudi tena na kumalizia kurekodi nyimbo 6 na kutengeneneza jumla ya nyimbo 18.

John Lisu akiwa na ubavu wake Nelly Lisu wakijiandaa na recording.
John Lisu akiwa na music director wake Fred Kilago au mwite Masanja, jamaa ni kichwa cha muziki Tanzania inajivunia naye.
Fred akiwa na ubavu wa Ona mwite Tumaini.
Pastor wa DPC Abel akiwa anafunguwa event kwa maombi.
Jukwaa likipendeza na watu wakiwa wengi vijana wanakwambia nyomi.
Bomby Johnson akiwa Kikazi zaidi siku ya Jana.
Tumaini Ona akiwa natabasamu kali.
Pastor Paul Safari akimtukuza Mungu.
Christina Halai kulia akiwa sambamba na wenzake.
Milio yenye kubembeleza mweeee!
Hakika ilipendeza.
Neema Gospel Live Choir kutoka AIC Chang’ombe wakimsifu Mungu.
Kijana wa GWT, Paul Clement akiimba Mpenzi wa karibu.
Katibu Mkuu wa TAG Pastor Ron Swai akifungua rasmi Live Recording ya John Lisu
Ma MC wa tukio Godwin Gondwe kutoka IPP pamoja na Sam Sasali.
John Lisu akijiweka sawa kupanda jukwaani kuanza kazi huku mkewe akimwangalia.
Makofiiiiiii kwa John Lisu akipanda jukwaani tafadhaliiiii
Lisu akikimbia kuelekea jukwaani.
Kazi ilianza kwakishindo sauti zikapazwa.
Wee ilinoga sana.
Christina Halai akienda sawa, Sasali ameandika huyu dada huyuuu, hapana shaka waliokuwepo jana mnajibu.
Uncle jimmy the blogger akienda sawa na watu wengine kucheza na kumrudishia Mungu utukufu.
Wanaume wakiwa kazini mwe
Uweponi mwa BWANA kila goti litapigwa.
Godwin akiwa uweponi.
John Lisu na Timoth Kaberia toka Kenya wakiwa Kikazi zaidi
John Lisu na kundi lake wakipiga picha ya pamoja baada ya kazi nzuri. Picha by Samuel Sasali na Fred Kilago.
Advertisements

4 thoughts on “Live recording ya John Lisu ilipangiliwa vema!!

  1. Hongera sana kwa tukio kubwa na la baraka Mungu akuinue zaidi.Natamani kuipata hiyo copy ya DVD kwa upesi sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s