Mwigizaji Jim Iyke maarufu kama “play boy” ampa Yesu maisha yake!

6

Baada ya kuwa na personality ya u-playboy kwa muda mrefu hivi sasa Jim Lyke ni mfuasi mzuri wa dini ya kikristu na aliingia kanisani weekend iliyopita kuombewa, hapo ndiyo mapepo yakaanza kumtoka. Watu wengi hawakuamini kumuona Jim akienda kuombewa, lakini amepata support kubwa kutoka kwa mchungaji maarufu TB Joshua. Hizi ni picha nyingine na alichosema TB Joshua baada ya Jim Lyke kuamua kwenda kanisani kuombewa.

Jim-Iyke-Synagogue-Delivearnce2

Screen-shot-2013-09-29-at-21.59.51

Jim-Iyke-Synagogue-Delivearnce3

–Millard Ayo

Advertisements

4 thoughts on “Mwigizaji Jim Iyke maarufu kama “play boy” ampa Yesu maisha yake!

 1. Mtu mmoja alitoa kisa hiki kifuatacho;
  “Siku moja baba mmoja mstahiki, aliangukia kwenye mikono ya majambazi. Mzee huyo alivuliwa nguo na kufungwa kamba na hao maharamia na kisha kumpiga na kumtesa kadri walivyoweza. Maharamia hao, walimuumiza sana kwa kumchomachoma miiba, misumari, viisu na vitu vyenye ncha kali mwili wake wote. Damu zilimtoka sana mwili wote. Alikuwa hajiwezi kabisa. Baada ya vitendo hivyo viovu, maharamia hao walimtelekeza huyo mzee katika eneo hilo.
  Baada ya muda kupita, watoto wa huyo mzee walizipata taarifa za baba yao. Mtoto wake wa kwanza na wengine pamoja na ndgu jamaa na marafiki wengine wote waliongozana kwenda mahali pa tukio hilo. Walipofika hapo walimkuta mzee yuko katika hali mbaya sana. Walitafuta usafiri wa haraka wa kumuwahisha hospitali. Baada ya kuuguzwa hospitalini kwa muda, hali ya mzee huyo ilizidi kuwa mbaya. Kadri siku zilivyonga, hali ya mzee ilizidi kuwa mbaya zaidi.
  Siku moja na katika saa wasiyoitarajia, watoto wa huyo mzee pamoja na ndugu, marafiki na jamaa wote, walimshuhudia mzee huyo akiwa katika hatua ya kulala na wazee wake. Walimshuhudia jinsi alivyokuwa akihangaika hapo kitandani alipokuwa katika hali ya kukata roho. Walimshuhudia jinsi alivyokuwa akitupatupa mikono, miguu na kulia kwa sauti ya maumivu makali, “ Baba yabgu, nakufa mie, nakufa mie jamaniii.. Nisaidieni, nakufa mie…”. Walimshuhudia kukoroma na kuvuta pumzi kwa mara ya mwisho kwa huyo mzee wao. Hatimaye alikata roho.
  Baada ya kufariki, walimchukua na kwenda kumzika kwa taratibu zote za kijadi. Baada ya miaka mingi kupita, yule kijana mkubwa aliwaita ndugu zake wote wa damu, majirani, marafiki, na watu wengine wote walioweza kufikishiwa mwaliko huo ili wakukusanyike nyumbani kwa kusudi la kuwaonesha jinsi baba yake alivyohangaika wakati wa kifo chake. Walipokuwa wameketi vizuri na kwa utulivu mkubwa, alisimama akawaambia, ‘ leo tutaonesha jinsi baba yetu marehemu alivyokuwa anahangaika pindi alipopatwa na masaibu yaliyosababisha kifo chake. Tutaonesha kwa kuigiza hatua zote alizozipitia kwenye tukio hilo hadi umauti ulipomfika.
  Akiwa na vijana aliokuwa amewachagua kuonesha igizo hilo, walijiandaa vizuri ili kuanza kuigiza kifo cha baba yake. Walianza kuigiza jinsi mzee huyo alivyotekwa, kuvuliwa nguo mbele za halaiki ya watu, kupigwa na kuchomwa vitu vya ncha kali mwili mzima wakitumia vifaa bandia. Vijana wenzake walimfanya vyote alivyofanywa baba yake. Hatimaye huyo kijana alipelekwa hospitali ya kuigiza hapohapo wakati wakifanya mchezo huo wa kuigiza.
  Ilipofikia hatua ya kukata roho, waigizaji waliwatangazia watamazaji kuwa sasa wanapaswa kukodoa macho vizuri maana waigizaji wanaelekea sehemu muhimu sana ya igizo hilo. Watu walikaa kimya kusikiliza huku wakitazama kila hatua ya igizo hilo. Kijana mwigizaji alianza kukoroma kama baba yake alivyofanya. Aliigiza mitupo yote ya mikono, miguu na kilio cha sauti kali kwa uchungu na huzuni kubwa aliyokuwa akiitoa baba yake, ‘Baba yangu, nakufa mie, nakufa mie jamaniii.. Nisaidieni, nakufa mie…’. Aliendelea kukoroma kwa muda kitambo na baadaye alivuta pumzi ya mwisho na kujifanya anakata roho kama baba yake alivyokata roho”. Hapo ikawa mwisho wa igizo hilo.
  Maswali ya kujiuliza;
  1. Je, ungekuwa wewe kuwa ndiye yule kijana mkubwa, ungeigiza kifo cha baba/mama yako kama yule kijana alivyofanya?
  2. Ungemwona huyo kijana wewe kwa macho yako, ungemwambiaje?
  3. Nini mtazamo wako kuhusu kisa hiki?

  Mtazamo wa Sampuli ya msimuliaji
  Wasikillizaji wengi wa kisa hiki walitoa maoni na mitazo hasi juu ya kijana huyo ya kwamba alikuwa ni kichaa, tahira, mpumbavu, mwehu na kadhalika. Kimsingi, yalikuwa ni majibu ya kulaani kitendo alichokuwa amekifanya huyo kijana.
  Je, ikiwa tunaona kuwa ni jambo lisilofaa asilani kufanya maigizo ya jinsi wazazi wetu wa kimwili walivyokufa, ni kwa namna gani ilivyo vibaya sana na uovu ulioje, kumwigiza Yesu Kristo jinsi alivyozaliwa, kukua, alivyoishi kwa kuhubiri na kuponya wasiojiweza, alivyokamatwa, kuteswa, kuvuliwa nguo, kupigwa mijeledi na kuchomwa vitu vya ncha kali, kuangikwa msalabani,alivyolia, Eloi, Eloi, Lamathabakithani yaani Mungu wangu Mungu mbona umeniacha?” Kama kuna dhambi na uovu ulio mkuu kupindukia katika ulimwengu wa Kikristo, ni kuigiza maisha, kifo, kufufuka hadi kupaa mbinguni kwa Kristo. Shetani amefaulu sana kuidhalilisha sana tena kwa kiwango kikubwa sana KAFARA YA KRISTO PALE MSALABANI na mpango mzima wa wokovu wetu. Kristo na msalaba wake, amedhalilishwa, dhalilishwa sana sana. Kama tunaonesha nidhamu na heshima kubwa ya KUTOIGIZA MAISHA kwa wazazi wetu wa kimwili, je, ni kiasi gani tunapswa kuonesha nidhamu na heshima zaidi kwa mzazi wetu wa kiroho – Yesu Kristo aliyetuumba na baadaye kutukomboa baada ya kupotelea dhambini?
  Biblia inasema, “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani” – Isaya 9:6. Ni tendo la kukosa adabu kiasi gani kuthubutu kuigiza mambo aliyoyapitia Baba wetu wa milele, Yesu Kristo pale msalabani? Ni nani anapaswa kupewa heshima kwanza kati ya Baba yetu wa milele na wazazi wetu wa kimwili? Kama kuna mtu anapenda kuigiza kifo cha Kristo, ni vyema aende akaanze na kuigiza kifo cha baba/mama/mtoto wake kipenzi jinsi alivyokufa tena kafanye igizo hilo sokoni penye watu wengi sana. Kama ataweza na watu watampongeza kwa hilo, na aje aigize kifo cha Kristo.
  Kama kuna familia, mtu, kanisa au jamii ya watu wanaopenda kuonesha watoto picha za maigizo ya visa vya kibiblia kikiwemo na kisa cha Kristo, ingependeza mtu, familia au jamii hiyo ikaanza kuwaonesha watoto wao visa vya vifo vya mababu/mabibi zao kwanza. Kama watahimili kufanya hivyo, basi wawaoneshe watoto wao na vile visa vya kibiblia.
  Tofauti na hapo, neno la Mungu limekataza na wala hakuna mfano wowote ndani ya Biblia, wa watu waliotumia maigizo au maonesho katika kuihubiri injili. Kama tulifanya hivyo kwa kipindi kilichopita, ni wakati sasa wa kufanya matengenezo katika maisha yetu, familia zetu na makanisa yetu. Biblia inaema “Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu”.
  Mungu awabariki sana mnapochukua hatua katika hili.
  Wakatabahu!!

 2. Ni jambo la kutia moyo tunapomwona mtu fulani kampokea Kristo na kuanza safari nyingine nzuri ya imani akipambana ana kwa ana sasa na mamlaka ya giza kuliko ilivyokuwa hapo awali. Binafsi namshukuru sana Mungu kuwaona baadhi ya marafiki na wapendwa wetu angalao wanatambua kuwa huko walikokuwa awali, siko na sasa wanapaswa kumtafuta Mungu. Tunamshukuru Mungu kwa Jim kumpokea Kristo, japo bado ana safari ndefu ya kwenda zaidi ya hapo.
  Changamoto inabaki kwetu ambao ni waumini wa muda mrefu kanisani, lakini bado tu wapenzi wakubwa wa hayo maigizo na maonesho. Wengi wetu tumekuwa wapenzi sana wa kutazama maigizo na sanaa za maonesho huku tukijua kabisa kuwa wanaofanya hivyo kimaadili ya dini, wamepotoka. Swali la kujiuliza, inakuwaje sisi tunaomwamini Kristo tufurahishwe na waliopotoka-waigizaji au wasanii???
  Wengine wanaweza kufikiri mbona kuna maigizo ya kidini? Mbona kuna mikanda ya watu walioigiza habari za watu wa kale katika Biblia kama vile akina Musa, Ibrahimu, Samson nk? Mbona hata agano jipya watu wameigiza? Leo hii kuna mikanda ya maigizo ya Yesu kuzaliwa hadi kupaa mbinguni, mikanda ya akina Paulo na sila, Petro nk. Yote haya yanafaa kwetu kama wakristo? Je, neno la Mungu linaweza kufundishwa kwa kuigiza au usanii?
  Kuna madhumuni makubwa mawili makuu ya kuigiza au kufanya usanii. 1. Kufundisha jamii na 2 ni kupata pesa. Jambo la kujiuliza, ni kwa kiasi gani maigizo hufundisha jamii? Bila ya kumumunya maneno, maigizo hayafundishi uadilifi wowote ktk maisha ya jamii, na badala yake yamekuwa ni chanzo kikubwa sana cha kuchochea uovu. Huchochea tamaa mbaya za kimwili pamoja na kuamsha nia ya kuendeleza kutenda uovu huo unaoigizwa. Ni neno la Mungu peke yake ndilo linaweza kumfanya mtu kuwa mwadilifu kama Paulo asemavyo; “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. – 2 timothy 3:16-17

  Je, maigizo yanayofanywa na wakristo(yaani maigizo ya Kikristo), Mungu anayakubali? Je, Kristo aliagiza wanawafunzi wake wakaihubiri injili duniani kwa njia ya kuigiza? Je, utukufu wa Mungu waweza kuonekana ktk michezo na maigizo kama hayo? Aya ifuatayo inajaribu kutoa majibu ya maswali haya.
  Hakuna hata aya moja ndan ya Biblia inayoonesha kuwa watu walifundishwa neno la Mungu kwa njia ya maigizo. Mtu anayeigiza kwa kusingizia kuwa anafundisha maadili, amefilisika kiroho. Ana kifaduro cha kiroho, Ukiro- Upungufu wa Kinga Rohoni. Yeyote anayetaka kuihubiri injili, sharti afanye kama Paulo aagizavyo; “…ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha. Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia”. – 1 timothy 4:13-16

  Sababu ya 2, watu wanaigiza ili wapate pesa. Hapa ukiangalia kwa makini, Mungu huwekwa pembeni ili waigize kile kisichoendana na neno la Mungu ili kiuzike. Hata hao wanaoigiza habari za Biblia, kama wachungaji nk, lengo lao kubwa huwa si kuihubiri injili bali huwa ni maslahi tu. Maana ni dhahiri wanajua kuwa, injili haihubiriwi kwa maigizo. Wamejidai kusahau kuwa, wote wanaomtumikia Mungu, hawapaswi kuyatafuta ya ulimwengu huu, bali wamtafute Mungu na haki yake na mengine watazidishiwa.
  Lakini bado kuna watu wanaposoma makala/mchango huu wanaendelea kuhoji ndani ya mioyo yao; na pengine wengine kuendelea kushikilia mitazamo yao hasi. Wengi watapotea si kwa sababu ya kutokujua, bali kwa sababu ya kiburi. Neno la Mungu linapowafikia, na hata linapoonekana likipinga michezo hiyo mibaya, wao hulipinga sana. Lakini Mungu anabaki palepale na ukweli wake unabaki palepale na utadumu milele wakati wapinzani wa neno la Mungu wataangamizwa milele.
  Mtumishi wa Kristo, anapaswa kuwa mtu wa sala, mcha Mungu, mchangamfu na hapaswi kuwa mtu wa ovyo, mwenye utani, au mtu mwenye kufanya mambo ya upuuzi. Mtu mwenye tabia za upuuzi, masihara na uchekeshaji usomaana, havifai kwa mtu aliyeitwa na Mungu kwa ajili ya kuzitangaza fadhili zake kuu- uzima na mauti!! Wanaoitwa kwa jina la Bwana, sharti wawe nuru kwa ulimwengu wote.

 3. Sifa na utukufu ni kwa Mungu peke yake, yeye atupaye hata yale tusiyoweza kuomba wala kuyafikiria. Lakini mmmmmm! haya.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s