Kiingilio kwenye Semina!!

ukumbii

Shalom naamini mnaendelea vyema kwa neema ya Mungu, popote mlipo watumishi wa Mungu naomba mnisaidie kunielimisha juu jambo hili, mara nyingi nasikia watumishi wa Mungu wanasema Mungu amewapa ufunuo fulani ili wawasaidie watu wanaoteseka ktk jambo fulani na wanaandaa semina na kualika watu ili waende wakajifunze, na hapo wanatangaza kuwa kutakuwepo na KIINGILIO kwenye semina hiyo je ni halali watu kulipa pesa kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu? na unakuta semina hiyo imeandaliwa kwenye kanisa fulani, je ina maana wasio na na pesa hawaruhusiwi kwenda kujifunza?

Mara nyingi nimeona watu wanazuiliwa kwenye milango kisa hawana hela, kama ni kufidia gharama kwenye semina kunakuwepo na sadaka mbalimbali ambazo zinaweza kufidia gharama, za maandalizi. tumepewa bure ni kwa nini tuwauzie watu ujumbe au maono uliyopewa na Mungu?

–Emmanuel

Advertisements

122 thoughts on “Kiingilio kwenye Semina!!

 1. Mpendwa Lwembe,

  Ahsante kwa kutamathisha mabishano yako. Kiukweli dalili ya ukosefu wa hoja ilikufikia katika makala yako ya huko nyuma. Ulipoona nimenyamazia oungo wako kwa kuwa uliomba masamaha ukajikuta kutofurahi kwani ulikuwa umejivua joho lako, sasa hapa nimedaka conclusion yako na nimeiheshimu. Mim sina tabia ya kutukana. Umesema “…lakini kuhusu haya, ninaamini binafsi nimefikia mwisho…” Nami sikushurtishe kuleta hoja usiyo nayo. Ulijitaabisha uwezavyo kwa hila na uongo, sasa umechoka; pole sana.

  Rafiki yangu, kwa kumaliza nitakupa tu shauri ndogo pia shairi ya kukusaidia:
  1)Shauri:
  -Unapojadili, umpe Mungu nafasi, Yeye ndiye akuongoze. Kwa hila na uongo huwezi eleweka ili ulichokisoma na kukielewa uweze kielewesha wengine, kwani kidogo tu uongo na hila vinaingia. Nafikiri unafahamu kama nuri na giza haviikae pamoja.
  -Kama msomi, nafikiri unafahamu ile alama inayoitwa ya kushangaa inatumiwa je. Unafahamu yaweza kuwa inamaanisha yowe(kuita ukiomba msaada), kushangaa kawaida, kushangaa ya hudhuni, kuamuru, …. Kinachokusumbua si kwamba ninatumia jina “Jesus” bali ni kwamba ninamtegemea wakati wewe unamdharau; hii inakusukuma kumuita torati na kumfanya dhaifu asiweze samehe wala kuyatimiza yaliyotabiriwa na manabii tangu zamani. Yeye Mungu anaechunguza roho zetu anaona. Nawe usihukumu usije ukahukumiwa.
  -Hiyo tamko yako “FOR ETERNITY” katika setensi yako, mimi siikutakie. Kaa kimya, Mungu akupe siku nyingi za kuishi hapa duniani, utajitambua bila mtu kukuhubiri.
  -Enenda moja kwa moja na mafundisho ya biblia, usitafsiri sana.Yeyote anaekusoma atagundua mara moja kama makala yako ni tafsiri tu kama vile walioandika Bible hawakukamilika.
  -Uongo isiendelee kukutawala kiwango hata umsingizie Paulo. Kwani wewe unapima viringisha maandiko yake ukidhani utasifiwa. Nadhani hii mda imekusaidia na umegundua kama hiyo method haikukusaidia kwa chochote.
  -Nakusihi udake “FOR ETERNITY” (nakunukuu), kama injili inahubiriwa. Mafundisho ni jambo lingine. Injili inaleta Imani, lakini mafundisho yanaongeza ufahamu. Wengine wanaenda kutafuta ufahamu kwenye vyuo vya kiteolojia hata kama wameamini! Si hao wote wanalipa? Fahamu kama alieita ule mkutano “semina” hakukosa ufahamu wa kuuita tu “Injili”. Injili inapewa bure kila fasi. Ile uidake na isikuponyoke kaka yangu. Na iwepo kuna watumishi wa Mungu wanaochanga Injili na Semina, basi wale tuwaachie namna yao ya kuiandaa.
  -Usiwe na tabia ya kuhukumu watumishi wa Mungu bila sababu.
  -Usiwe na tabia ya kukubali kitu kiisha ukikane kwa hila. Kwa mfano wewe mwenyewe ulihakikisha kam yeye Yohana Mbatizaji alitamathisha unabii kihuduma, kiisha nimekuona ukirudi nyuma kukanusha, kama jinsi uliomba masamaha baadaye ukasema hukuomba.

  2) Shairi:
  Ujithahidi usome maandiko haya, pengine yatakusaidia. Nayaweka si kwamba nina uhakika hujawai kuyasoma, lakini sasa ukiwa na mda utayasoma tena. Sikuombe kunijibu kwani nimeheshimu uliposema umefika mwisho.

  2 Petro 2:22
  Luka 11:26
  Yohana 15:15
  1 Wakorintho 16:1-24
  Ufunuo wa Yohana 1:8
  Ufunuo wa Yohana 21:6
  Mathayo 19:14
  Mathayo 23:36-37

  Tukingoja kukutania kwenye mijadala ingine,

  Mungu wa Mbinguni akubariki.

 2. Ndg Ziragora,

  Haya, sasa tukirudi ktk Injili, katika maelezo yako ya 03/02/2014, umeorodhesha takribani mambo 6. Kati ya hayo, matano ni ngonjera zako za kawaida, kwahiyo ninaliendea hilo la 6 ambalo naliona angalau lina mantiki!

  Katika hili, maelezo yako yanaonesha kwamba licha wewe kuwa ni mkweli kwa kiasi unachokijua kuhusu mambo haya tunayoyazungumzia, lakini kimsingi huna unalolijua, zaidi ya lile ulilolikiri kuhusu Mathayo 11:12-15
  “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15 Mwenye masikio, na asikie.”
  Kuhusu vifungu hivi, umekiri kwamba Maandiko haya yanathibitisha kwamba Yohana Mbatizaji ndiye nabii wa MWISHO na hivyo HAKUNA tena nabii wa jinsi ya akina Isaya au Danieli nk, jambo ambalo si kweli!!!

  Na kwa vile hii ndiyo imani inayokushikilia, basi si ajabu kwamba imekuzuia kuijua Kweli ya jambo hilo, kulingana na Maandiko! Bali ukweli wa jambo hili ndio huo kwamba Huduma ya manabii wa jinsi ya akina Isaya, bado inaendelea kama ilivyoahidiwa!!!

  Niliirejea Huduma ya Kristo kulingana na Isaya 61:2 ili tu kukuonesha jinsi ambavyo sentensi moja ya unabii inavyoweza kugawanyika katika kutimia kwake. Lakini naona hili lililojepesi limekushinda kulielewa! Bali Maandiko yako hivyo unavyoyaona, hiyo Luka iko hivyo kwa miaka zaidi ya elfu mbili, nayo Siku Iliyokubaliwa ndiyo hii tunayoiishi leo hii mimi na wewe, na Injili inayolibeba jambo hilo ndiyo hii inayowaitia watu wokovu mpaka leo hii, kuanzia siku ile ktk Luka alipoitangaza Siku hiyo kwamba Maandiko hayo aliyoyasoma kutoka kitabu cha Isaya YAMETIMIA masikioni mwao! Luka hiyo ndiyo inayopaswa kukuongoza kuyaelewa hayo kama yalivyotangazwa, yakikurudisha huko kwa Isaya kuona yalivyotabiriwa. Zimetabiriwa siku mbili, Siku Iliyokubaliwa na Siku ya Kisasi; Usizichanganye Siku hizo ni siku halisi, nenda pole pole na Maandiko utaelewa tu!!!!

  Hiyo Mt 24 inaambatana na hao manabii wawili kwa Israeli, Kanisa halihusiki na Siku hiyo ya Kisasi, labda uwe ulimkosa huyo Eliya ambaye Huduma yake ingekutayarisha kuondolewa, kwahiyo kwa kuikosa utaishia kuipitia hiyo Siku ya Kisasi, ambayo ndiyo tamati ya Dhiki Kuu utakayoianza baada ya Kanisa kuondolewa! Au mwenzangu unaijua Siku hiyo ya Kisasi ilipotimia? Hiyo Mt 24 ni UNABII unaoihusu Siku hiyo tu, ukipewa mandhari yake!!!

  Basi, Huduma ya Elia ktk Malaki 4:6 iko hivyo pia, imegawanyika; nusu kabla ya Siku Iliyokubaliwa, ndiyo hiyo Huduma ya Yohana Mbatizaji aliyeigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto, akiwatayarisha wazee wa Torati kumpokea Kristo, (na hapo sasa akiitangaza ktk hiyo Luka akiisha kupokelewa); na sehemu ya pili itakuwa kabla ya Siku ya Kisasi, ili kuiondoa migawanyiko na mafundisho ya uongo kama haya uliyoaminishwa, ili Kanisa liwe tayari kuondolewa ktk Unyakuo kuipisha hiyo Siku ya Kisasi. Na pia nilikuambia kuwa Kristo akiisha kuliondoa Kanisa lake uwanjani, ndipo anawarudia Israeli ndugu zake, na hao manabii wawili ni katika Huduma hiyo, mtazame Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake, mkewe alikuwa ghorofani huko juu tayari! Hata nikakuambia kuwa hao hawawezi kuwa Kristo wala Yohana Mbatizaji kama unavyolazimisha kutokana na maudhui ya Huduma yao!

  Sina namna ya kuyaelezea mambo haya zaidi ya yanavyojifunua ktk Maandiko. Hakuna Shuruti inayoweza kumpa yeyote yule Ufahamu wa jambo, isipokuwa unyofu wa moyo wake ktk kujifunza!

  Nakushukuru sana kwa kuutoa muda wako katika kulitazama jambo hili la manabii!

  Kuhusu mambo ya KIINGILIO, nadhani kimsingi tulikwisha kulimaliza na jibu langu la mwisho nilikuambia ni “FOR ETERNITY” kwamba sioni ni kwa jinsi gani unaweza kumkosea adabu mtumishi wa Mungu, kama mtume Paulo, kwa kuzifananisha CHANGIZO alizo ziamuru na VIINGILIO vyenu ktk jinsi yoyote ile! Aliyekosa Heshima kaikosa na Hekima pia; ndio maana umeshindwa hata kupambanua maudhui ya mambo mawili hayo, kwamba Changizo huja baada ya Injili kuhubiriwa, wahubiriwa wakiwa Convinced ndipo wanakuwa Concerned; lakini kwa Viinglio ni tofauti, unatoa pesa kwanza halafu ndio unapewa Injili!!! Pretex yoyote, au excuse yoyote ile ya KUTOZA Viingilio, is not worthy of the Gospel, it is just plain VANITY!!!

  Basi ndg yangu, kama kuna jambo jingine, nitafurahi kulisikia kutoka kwako, lakini kuhusu haya, ninaamini binafsi nimefikia mwisho, sina tena rejea za Maandiko za kuongezea, labda mambo ya mtaani, ambayo sioni manufaa yake kiungu;

  Bwana akubariki sana ktk jitihada zako za kumfanania Yeye,

  Asante sana,

  Over & Out!!

 3. Ndg Ziragora,

  Asante sana kwa maelezo mapya uliyoyaleta, yamenifurahisha sana maana naona yamelifumua duku duku ulilonalo moyoni mwako na kulimwaga nje, hilo ni zuri kwa afya!!

  Juu ya hayo umenisikitisha ktk jambo moja tu, kwamba unanisisitizia kuwa unaendelea kulitumia Jina la Bwana kama kibwagizo chako cha starehe ya uandishi na maongezi ktk namna ya exclamation, “Jesus !!!!” Kama ulivyosema, hushurutishwi, ni kweli hakuna anayekushurutisha kuiacha tabia hiyo, hata Yuda Iskariote ulipofika wakati wake wa kumsaliti Kristo, aliambiwa aende akatimize azma yake, na kwa ujeuri akaondoka kwenda kuitimiza, kwahiyo nawe endelea tu ndg yangu, “Sikio la kufa halina dawa”! Lakini kaa ukijua kwamba hali yako ni sawa na ya mtu aliyejivisha kitanzi kwa ujinga wa mashindano, kisha anakisukuma kiti alichosimamia kuivaa hiyo kamba!

  Unapolitaja Jina la “Yesu”, jua kwamba kikosi cha malaika wapiganaji hushuka kuja kukusikiliza hitaji lako; basi wakifika hapo wanakukuta uko kwenye mizaha yako ya kujionesha umaarufu wako ktk Injili! Deployment of forces ni very costly, na ikiwa “war cry” yenyewe ni mockery, basi hata sijui nikwambie nini, ndio maana Mungu ametukataza kulitaja Jina lake bure, inamgharimu sana Amani yake kwa jambo la kipuuzi!!

  Asante!

 4. Ndugu Lwembe,

  Kutofahamu kwako kusikusukume kujipatia maarifa usiyo nayo. Kusema “Jesus…” naendelea, lakini sishurtishwe kusema sentence moja. Hata huko unaposema sikuweka sentence moja. Ninapoita Yesu ni kwani ninamjua. Wewe uko shabik wa torati, ninakufahamu. Ndiyo maana mtu anapomuita Yesu unashikwa na kigugumizi.

  Unasema ume clear wingu ya uongo? Kwa taarifa yako umehakikisha wewe ni muongo kiasi umetambulikana na takriban watu wote. Hata wewe umeifahamu ile pale iliposema kwa lugha yako sanifu kwamba:”Lakini kwa upande mwingine nakushukuru, kwani hila ulizozitumia, hutumika sana na watu wa jinsi yako, kwahiyo at least wenye kukusoma watakuwa wamepata mfano mzuri wa kuyabaini hayo.” Nafahamu hukupenda sema hila, ulimaanisha ufahamu. Na watu wa jinsi yangu ni walokole wala si wanatorati/wanasheria kama Lwembe. Si tena siku ingine ukaleta orodha bila kuimaliza ya waliyonisikiliza, nilipokuuliza waliokusikiliza ukawakosa!!!! Ndio maana hawo unaowasema, ukitazama vizuri wanayoandika utawakuta wamejazwa RM. Hii ni uhakikisho ya kuwa hii ni kanisa inayoombewa usiku kama mchana ili mbwa mwitu asiingie, au kam aliingia awe si kitu. Bwana Yesu asifiwe!

  Shika vizuri, wala usisahau:”Kiingilio na Semina vina lengo moja”. Nilipokuambia nawe uendeshe semina, uli paste tu pale lakini ukisoma yote utakuta pale ndipo jibu zote ziko. Ni hapo ndipo nilikukemea nikikuambia uache kudhulumu watumishi wa Mungu. Na kama una namna nyingine za kuendesha semina uwe mfano, uindeshe kwa namna unayoshurtisha wengine. Usitukane mtu wakati huwezi kufanya tofauti yake bwana!!! Unapashwa uwe mtendaji wala si msemaji tu.

  Nataka nikumbushe msomaji ili usilete udanganyifu. Wewe unasema Paulo hakutoa amri kwani adhabu haikuwepo, are you serious? Hapo Nyuma sikujulisha kama adhabu ilikuepo na alieshikilia maamzi ni RM mwenyewe. Nikakuonyesha kama Anania na Safira walikufa tu katika kukosea ile changizo. Lwembe, hapa si uwanja wa uongo. Ni kanisani, wateule wa Bwana wanaombea usiku kam mchana hii blog. Hivi usicheze na moto Lwembe. Unaposema kila mara “watoto”, wewe ulizaa nani ili umuite “mtoto”. Ni mtoto yupi anaeandika maneno ya upako kama hii na kubabaisha Lwembe anaejidai kuwa mwandishi wa lugha sanifu, pia kujionyesha kuwa mufarisayo akishika kwa kuiga tu torati bila kuifahamu vizuri.

  Lwembe, fahamu hii:”Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”
  Kila mara utakapodharau maneno ya Yesu, ufahamu una tatizo kubwa.

  Asante.

 5. Ndugu Lwembe,

  Naami hujambo kaka yangu!

  Dan! una hofu kiwango hiki? Hivi umeijibu kwa hoja gani ndugu yangu? Hebu linganisha unayoandika na hoja inayoendelea. Come down Lwembe, uwe mzima. Unadaka setences tofauti za kila makala ya zamani, yangu, yako na ya wengine, ambapo unafikiri utapata haki, ukizidisconnect na mantiki yake; hivi unafikiri ndipo utakuwa sahihi kweli? Lwembe, si unaona kama umeogopa hoja yangu, sasa umetupa ufahamu? Uwe tu muungwana ukiri kutofahamu.
  Wewe si Richard, tena kwa kuwa hakuja kujitetea ina maana aliandika pasipo kuchunguza na hiyo si tatizo, hio ndio nilikemea, sawa jinsi nimekukemea kwa uongo wako na hila yako; lengo ikiwa kwamba uokoke. Ufahamu vile kama anaesaidia muongo naye ni muongo, sasa akifanya ile pasipo kujua , wakati anapopata makemeo/msaada na kujirekebisha, sisi tuliyookolewa tunasema “Haleluya”.

  Sasa, ili uhalalishe hila yako ya kuwa umeomba masamaha kwa hila, umebandika ile ambayo ilikutumbukiza ndani ya uongo. Umetimiza hili andiko; “2 Petro 2:22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”

  Hii yote, kaka Lwembe, ni upungufu wako wa kushindwa kukiri kutofahamu. Umeacha hoja yako juu ya manabii pasipo kukiri kama umetosheka na umekimbilia kujiosha, kwa hila, ile uongo yako ambayo kwa kuomba masamaha tayari ulikuwa umesamehewa. Ndugu yangu, sitakulazimisha kusamehewa, baki pale pale.

  Nilikuambia mara nyingi ujitahidi kutofautisha uongo na hoja/fikara/maoni. Uongo ni kuhakikisha kitu unachojua kama si kweli kwa lengo la kujiweka, kwa hila, ndani ya kweli/ushindi. Kwa mfano, tulipozungmuzia Semina, ulipoona hoja hangu imemeza yako ukasema kama mimi ninaendesha semina makusudi wanaotusoma wasione tena ukweli bali waone kama najitetea mwenyewe. Nikakuuliza uliniona wapi nikiendesha semina, ukashindwa. Ukatafutisha jibu kwa siku nyingi, hukupata, ndipo ukatafutisha hila iliyokupeleka mahala uliposema “Unapoitetea hoja yoyote ile, basi jua ya kwamba, moja kwa moja unakuwa umejitambulisha na hiyo hoja kwa mema na mabaya yote yanayoihusu”.
  Sikiliza Lwembe, hiyo unayoleta ni utani. Hapa semina haitetewi kwani haikushindwa wala haiko mahakamani. Ndiyo maana unakuwa mbishi sana. Kama ninatetea Mungu ndiye aliyeumba Mbingu haimaanishe kama mim ndiye niliyeiumba. Kama ninatetea kam nabii wa kweli analeta maneno ya Mungu haimaanishe mim ni nabii. Kam Lwembe anatetea kina Eliya atafika kwa mfano wa Yohana Mbatizaji, haimaanishe kam Lwembe ndiye Yohana Mbatizaji; na iwepo mtu atasema Lwembe=Yohana Mbatizaji, itakuwa uongo kabisa. NK.

  Ok sasa ukipenda vunja msamaha na kurudi huko nyuma, hebu nenda na utafutishe hila nyingine ili uthibitishe ushujaa wako katika uongo na hila, ukifahamu kama muongo na baba yake Ibilisi walitayarishiwa jehanum:

  “3. Uongo wako: “ulisema mim naendesha semina”, uliniona wapi? Ukasema “kuamuru” haihusiane na kutoa “amri”, jambo ambalo linakunasa popote. Ukasema “mim nilisema asiyetoa kiingilio analaaniwa”, nakuomba ufanye copy –paste ya ile tamko yangu. Ukasema nililazimisha KIINGILIO na CHANGIZO kuwa ni neno moja , copy-paste exactly lile tamko langu.”

  Usikwepe swali:
  1. Niliendesha semina wapi na siku gani?
  2. Taja dictionary inayosema kama kuamuri si kutoa amri.
  3. Wapi ulipo paste “asiyetoa kiingilio analaaniwa”?
  (Fahamu kama copy-paste si tafsiri fulani, ni exactly lile tamko)
  4. Wapi ulipopaste “nililazimisha KIINGILIO na CHANGIZO kuwa ni neno moja”?
  (Fahamu kama copy-paste si tafsiri fulani, ni exactly lile tamko)
  Kaka Lwembe, kama si kukimbiakimbia tu, kweli una hoja tena?

  Kwa mwisho, uwe na tabia ya kukiri makosa yako na kuwa mtu wa nuru. Unayofanya ni mambo ya kinyokanyoka, unaposhindwa kujibu unaandika mambo yasiyoeleweka. Nilikuambia tena kama ukisema mtu ni muongo na unashindwa kuonyesha uongo wake, wewe ni muongo zaidi. Nikakushawishi kuto repeat tu kiupofu maneno yangu kama “uongo”, “jela”, “hila”. Mim ninayatumia kwani nina ufahamu. Usiigeige tu.
  Ndugu yangu, okoka kwani hujue siku wala saa Mwana wa Adam atakapofika.

  Bwana Yesu akusaidie.

 6. Ndg Ziragora,

  Katika umbali tuliofika, napenda niyaweke sawa machache ili yakusaidie ktk mtazamo ambao ninauona umejiinua ktk hila mpaka umeuzoelea ukiamini kwamba uko sawa, na hila yako kukupofua kabisa!!

  Umerudia rudia mara nyingi sana kwamba mimi ni “muongo” ktk jitihada zako za kuwaaminisha watu kwamba Kiingilio ni sawa na Changizo kwa hila ya kuyageuza niliyoyasema kwamba ni uongo. Labda ngoja niirejee orodha yako ili tuitazame pamoja, tupate uhakika wa hili ninalotaka ulione, hili hapa bandiko lako la tarehe 22/10/13 kuhusu uongo wangu kwa sehemu:
  “”3. Wongo wako:
  A: “Ulisema mimi naendesha semina”, uliniona wapi?
  B: Ukasema “kuamuru” haihusiane na kutoa “amri”, jambo ambalo linakunasa popote.
  C: Ukasema “mimi nilisema asiyetoa kiingilio analaaniwa”, nakuomba ufanye copy –paste ya ile tamko yangu.
  D: Ukasema nililazimisha KIINGILIO na CHANGIZO kuwa ni neno moja , copy-paste exactly lile tamko langu””

  “A”
  Nina kopi na kupaste jibu nililokuletea kuhusiana na “A”, huko kuendesha semina (28/10/13), nikikuongezea ufahamu juu ya majadiliano, najinukuu:
  “”Ngoja nikuongezee ufahamu katika majadiliano: Unapoitetea hoja yoyote ile, basi jua ya kwamba, moja kwa moja unakuwa umejitambulisha na hiyo hoja kwa mema na mabaya yote yanayoihusu. Kwahiyo, nilipokuambia kuwa unaendesha semina za viingilio, ilikuwa ni katika maana hiyo na si kwamba mimi nilikukuta mahali fulani ukiendesha semina, kwahiyo usikazanie sana kwamba nimeongopa, si kweli!!!!””
  Halafu ktk kipimo chako ulichoamulia kunilalamikia kuwa mimi ni “muongo”, hebu nipe nawe jibu la kauli yako hii unaponiambia, “” Si vema zaidi uendeshe wewe pekee semina …” (21/10); Uliniona wapi naendesha semina????” Kumbe wewe ndiwe “Muongo”!!!!

  “B”
  Kuhusu hili la “B”, pia nilikwisha kukujibu kulingana na ufahamu nilionao, kuendelea kwako kulidai jambo hilo naona ni ile hila endelevu unayozidi kuilea, hili hapa jibu langu FOR ETERNITY, kuhusu vifungu ulivyovinukuu kwa alichokifanya mtume Paul! Najinukuu 21/10/13:
  “” KUAMURU ni Kutoa Agizo, nalo Agizo likiambatana na Sharti hugeuka kuwa Amri! Bali Agizo la Paulo haliwezi kuwa Sheria au Amri kwa sababu haliambatani na Adhabu, ni Agizo lililojifunga katika Upendo na si Hukumu ya Sheria kama unavyotaka kulazimisha! I Wakorintho 16:1-3 “Kwa habari ya ile CHANGIZO kwa ajili ya WATAKATIFU, kama vile NILIVYOAMURU makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
Siku ya kwanza ya juma KILA MTU kwenu na aweke akiba kwake, KWA KADIRI YA KUFANIKIWA KWAKE; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue HISANI YENU mpaka Yerusalemu.”

  Maelezo “KWA KADIRI YA KUFANIKIWA KWAKE” yana denote UPENDO unaoiondoa Amri, kama unaweza kuelewa! Jitahidi kwanza uujue Moyo wa Mungu kwa wanae! Ingawa hutaki matumizi ya vocabulary, lakini hebu tafuta maana ya neno HISANI uone ni nini, maana naona tumerefusha majadiliano kwa wewe tu kuikosa maana ya maneno, KIINGILIO na CHANGIZO ukiyalazimisha kuwa ni neno moja, ili usimamishe fundisho la kuhalalisha KIINGILIO, kwa kuwatishia watoto wa Mungu kwa LAANA wasipoyatii mafundisho yako yasiyo na rejea ya Maandiko! Ndg yangu Mungu hana shida na hekima yako, na wala hakuna technology inayomshtua Mungu, usijidanganye na tumaendeleo twa sayansi twa leo; FUATA instructions! Mungu anataka UTII kuliko hivyo Viingilio vyako!!!””

  “C”
  “””Sasa nakuona wewe Lwemba na wapambe wako mukichagua laana!!!”” (18/10 at 5:21 PM)

  “D”
  “” Sasa wewe Lwembe, acha mambo ya kitoto na uonyeshe kikweli tofauti kamili ya Paulo na walimu wanaoleta semina. “” (18/10)!!!

  Unafiki huzaa hila ya kulitafsiri Neno la Mungu kinyume na uhalisi wake ili kuwapandikizia “Uongo” wapate kuwatumikisha watoto wa Mungu ktk utumwa wa dini, wakiyageuza maneno na kuyatoa ktk maana yake halisi ili kukidhi mafundisho yao, na hata kuikataa vocabulary! Vitisho pia ni sehemu ya hila hiyo na hata ikibidi ukatili hutumika ili kulifanikisha lengo hilo.

  Hebu angalia ulichomjibu ndg Richard, uone kama kina hata chembe ya upendo:
  RICHARD (4/11):
  “”Iko hivi;
Lwembe hajapinga changizo wala sadaka ya kuwalisha/tunza/na kuwasafirisha watumishi na hata sadaka za kuchangia gharama na ndio maana amenukuu vifungu vilivyovyomuonyesha Paulo akifanya hivyo na hata wakati huu hayo mambo yapo makanisani huwa mara nyingi ajapo mtumishi kutoka nje ya nchi, mkoa, au hata jimbo huwa tunatoa sadaka ya kumsafirisha.
na kama ni semina mbona wapo watumishi wengi tu wanazifanya tena ni kubwa tu lkn ni bure? mfno mwalimu C.Mwakasege semina zake huwa zinachukua nafasi kubwa mfano hakuna.
mbona ni free tuu?””
  SOOOOO INNOCENT a remark!!

  ZIRAGORA:
  “” Richard,
  Sijui kama umetumbukia tu au kama umetusoma vizuri. Au umejichanganya usijue unaeandikia.
Richard, play with your Lwembe, not with me.
  Thank you.””
  SOOOOO SAINTLY an answer!!!!!???????

  Yako mambo mengi sana yaliyonidhihirishia kuwa unafanya hila ya kulivuruga Neno la Mungu, ukitumia vitisho, hekima ya kibinadamu ukiibadili na Neno la Mungu, nk, ndipo ikanilazimu kutumia kale kahila kadogo, kama kale tunawafanyia watoto wadogo, ili labda tuwanyang’anye wembe wanaochezea mdomoni, ndipo nikakuambia kuwa nimetubu! Hebu yasome tena niliyoyaandika, nimemuandikia mtoto mdogo ktk Injili, mtu mzima ataona upesi tu kuwa nataka nikurudishe kwenye majadiliano nikiisha kukunyang’anya “Ubwana Jela” unaojifichia kujibu maswali!

  Lakini kwa upande mwingine nakushukuru, kwani hila ulizozitumia, hutumika sana na watu wa jinsi yako, kwahiyo at least wenye kukusoma watakuwa wamepata mfano mzuri wa kuyabaini hayo. Na pia nikupongeze kwamba angalau umejifunza jambo kutoka kwa “robot” wa Injili, tangu nikuonye kuhusu kulitaja taja kwako Jina la Mungu bila sababu, kama ulivyojizoelesha ukilifanya ni kibwagizo cha uheshimiwa wako, eti, ” Jesus !!! Sasa Lwembe unataka tukufanyeje?” bali sasa sijakuona tena ukikitumia kibwagizo chako hicho, licha ya kunichachamalia, lakini umeunyookea usawa wa Injili!!!!

  Mwisho, kuhusu Kiingilio, ukiziacha sifa za mtaani, hakina uhusiano wowote na matoleo wala sadaka wala changizo; kuyaleta kwako mambo hayo kuwa yana maana moja au faida moja, au kwamba yanafanana kimantiki, ni BANKRUPTCY of The Gospel!

  Ninaamini nime clear wingu la “”Wewe ni specialist wa uwongo kwani hata lililokweli unaligeuza uwongo” kwa kuzionesha HILA za wingu hilo ambalo umekuwa ukilitandaza kila unapopita, your great companion, otherwise lets turn to the Challenges of The Gospel!!!

  Asante,
  &
  The Lord bless u, my beloved brother in Christ!

 7. Ndugu Lwembe,

  1. Unachokipokea, ukukitupia kunguru utafikia kujitupia kunguru wewe mwenyewe.

  2. Wewe unafurahia kuandika novel. Nikufahamishe kama novel si ukubwa wake bali namna inavyozunguushwa kwa kufikia lengo moja. Ninachofurahia ni kwamba umebadilika kiwango aliekusoma katika makala yako ya zamani ana tatizo ya kutambua kama ni wewe Lwembe wa zamani au ni Lwembe mwengine. Nitaendelea kukupongeza kwa mabadiliko hadi utakapoandika (mengi wala machache) bila kujichanganya kwa lengo. Sasa upende usipopenda umeshawishika tu. Sikudai kuikiri, unapojitahidi kwa kutimiza ni sawa.

  3.Nilikuuliza kama uko ndani ya dini au la? Hivyo tukusifie kama wewe huwezi danganywa wakati wengine wote wanadanganywa na dini zao. Nafikiri, sisi sote tunapekua maandiko. Hii isiwe sababu yako ya kukwepa hoja.

  4.Kukwepa, uko professional. Unakwepa kwa namna yote na unaweka sababu zisizoitikiwa. Kwa mfano kama swali ina alama ya ulizo, na unaona alieuliza ana akili za kitoto, kwa nini usimpe jibu pia umfunze ili naye akuwe? Au kwa nini usinyamaze basi kwa yote wakati unapoona anaejadili nawe hastahili? Unatumia hila kwa kukwepa.
  Tena tukirudia huko juu, utagundua kama Lwembe alikiri anataka kaa na kujifunza. Sasa, mwalimu anapomswali ili afahamu kama mwanafunzi ana ufahamu kiwangi kipi, mwanafunzi anajibu eti sitaki leta jibu kwani swali ni ya kitoto! Lwembe, utaendelea shindwa!!!!
  Anyway, Lwembe umejifunza kupanga majibu yako, inayobaki ni kuondoa hila.

  5.Unaendelea kuzusha uongo, nilipokuuliza mahala nilipoandika kama “changizo” na “kiingilio” vina maana sawa, ukashindwa. Tena unasema una lugha sanifu. Ina maana kwako lugha sanifu ni uongo? Kwa kuwa uliomba ufunzwe, nakukumbusha kama kiingilio na changizo vina lengo sawa lakini kama tamko si sawa.

  6.Kuhusu yanayothibitisha kama Yesu amemaliza kazi yake iliyotabiriwa na manabii, nikikuuliza aliposema kama hakumaliza unanipa ile ile shairi ya Luka 4:21-27 alipofungua kiile chuo cha Nabii Isaya, wewe ukimshurtisha Yesu kusema yote kwa dakika moja wakati alikuwa na wakati yote ya kuendelesha. Hivyo ukakwepa niliokutolea inayothibitisha kama aliendelea siku nyingine na kumaliza yote.
  Kuhusu hawo manabii wawili unaoshurtisha bible kuenenda na fikara zako, naona hukuongeza jambo lolote lifaalo licha ya kuwa nimekutolea maandiko haya:
  “Mathayo 24: 1….29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, JUA LITATIWA GIZA, na MWEZI HUTATOA MWANGA WAKE, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
  30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
  31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”
  Pia ninaendelea kuuliza, hawo manabii wawili unaojiumbia watafika baada ya jua kutiwa giza?

  Asante

 8. …. inaendelea

  Ndg Ziragora,

  Kuhusu manabii wawili waliotabiriwa, yaani Yohana na Kristo, hawa ni kweli kwamba wamekwisha kufika na wameyatimiza yote yaliyoandikwa kuwahusu kulingana na Programu ya Mungu kama ilivyoainishwa ktk Maandiko. Kwahiyo swali unaloniuliza kwamba, “…kwa nini hukunipa maandiko inayoonyesha kama wao wenyewe walikiri kama hawakuweza kutimiza shurti zao?” Maandiko kuhusu jambo hilo yako wazi, labda hukuyatazama vizuri tu, bali yapo hapo hapo ktk Biblia yako.
  1. Kuhusu nabii Eliya, Malaki 4:5-6:
  “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. 6Naye ATAIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO WAO, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

  Sehemu ya Yohana Mbatizaji ktk unabii huo:
  Lk 1:17:
“Naye atatangulia mbele zake katika ROHO YA ELIYA, na nguvu zake … KUIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.”

  Nikakuambia kuwa Torati/Sheria ndiyo iliyokuwa ikiwaongoza Israeli ndio baba yao, hata ukiendelea kuyaangalia Maandiko vizuri utaona kuna “mapokea ya wazee” yaliyowashikilia pia kwa kujishikiza pamoja na Torati, Mk 7:5 ” 5Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee.” Ujumbe wa Yohana Mbatizaji uliwatayarisha makundi hayo kumpokea Kristo, huyo mtoto, mwana wa Daudi, akiwageuza mioyo yao kumuelekea! Mdo 19:4 “Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, AKIWAAMBIA WATU WAMWAMINI YEYE ATAKAYEKUJA NYUMA YAKE, YAANI, YESU.”!!!

  Jaribu nawe kuyaangalia Maandiko kuona iwapo ktk huduma hiyo kuna watoto waliogeuzwa mioyo kuwaelekea baba zao, labda hapo mbele kidogo walipogeuzwa mioyo Wasabato kuirudia Torati ktk huduma ya manabii wao!

  Kwahiyo si suala la nabii kukiri kama unavyotaka bali ni suala la nabii kutimiza lililoandikwa kumhusu, maana Mungu ndiye anayeyasimamia yote ktk Kuahidi na Kutimiza alichokisema kulingana na alivyokisema!

  2: Kuhusu Kristo:
  Nilikurejesha ktk Lk 4:17-21
“Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21Akaanza kuwaambia, LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU.”!!!

  Hapo ndipo alipoikiri Huduma yake katika siku hiyo aliyokuja. Kulitangaza jambo ni kuwaambia watu jambo hili limewafikia. Ukiyarudia Maandiko, hutaiona sehemu yoyote ile ambayo kuna nabii yeyote yule au kuhani au yeyote yule si wachawi wala waganga wa kienyeji waliowahi kumponya kipofu yeyote yule; Israeli wanalijua hilo; Kristo alipofika ndipo hayo yalimdhihirisha kuwa ndiye!

  Kama walivyoponywa vipofu ktk siku ya ujio wake wa kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, vivyo siku ya kisasi itafika, watakaokuwepo hawataikosa, hakuna hila inayoweza kufanyika ktk siku hiyo kama zile hila za mwaka uliokubaliwa, huu ambao tunaendelea kuuishi tukiyafitini Maandiko, siku hiyo si ya kuiombea ikufike!

  Hii Yn 6:40 si siku ya kisasi, ni siku ya Rehema tunayopewa Uzima wa milele kama inavyojishuhudia, inakazia huo mwaka uliokubalika! Bali hii Isaya nusu ya pili ya kifungu cha pili ambayo ALIIACHA HAKUISOMA, labda inakuchanganya hapo inaposema, ” kuwafariji wote waliao…”; lakini hao waliao ni hawa hapa, Ufu 5:9-10, ” Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?”

  Nayo Mt 24 uliyoinukuu ameielezea kuwa itakuwa hivyo bali HAJAITANGAZA kwa maana kuwa ndio imeanza, “kutangazwa” kunakozungumziwa humo ktk Biblia kuna ambatana na kudhihirika kwake, ndio kusema siku hiyo bado haijaja, ikifika ATAITANGAZA tena, katika namna hiyo anayoielezea, tukiwepo tutaisikia sote ndg yangu!

  Manabii hao wawili wa Ufu 11, si Yohana Mbatizaji wala Yesu, tena hawaji kwa Mataifa, hao wanakwenda kwa Israeli, lakini wanatanguliwa na Eliya anayelijia Kanisa la Mataifa na Ujumbe utakaoligeuza mioyo kuwaelekea baba zao mitume, wakiyabwaga mafundisho yote ya kulipa viingilio vya semina, Salamu Maria umejaa neema, Asante Yesu x 666, na uongo mwingine mwingi wa dini; sasa wakirejeshwa ktk Injili waliyoihubiri Mitume, na kujazwa RM wa Kweli atakayewaongoza ktk Njia iendayo Uzimani, nahivyo kuwa tayari kwa kuipisha Hukumu ya Mungu, hicho Kisasi!

  Pia umeniambia, ” Sasa utuonyeshe neno lilitoka kinywani mwa Yesu linalotupasha kama alitenda kazi kwa nusu kabla hio siku ya kuogofya.” Hili ndio hiyo Lk 4:17-21!!!

  Asante kwa leo!

  Gbu!

 9. Ndg Ziragora,

  Ndugu yangu, ninakushukuru sana kwa majibu yako yenye sehemu tatu. Ninakusifu kwa jitihada uliyonayo katika Neno la Mungu; nina uhakika kwamba ukiendelea ktk unyenyekevu unaweza kufanikiwa sana ktk kumlingania Kristo, kwa kadiri ya nafasi atakayokuweka!

  Kwa ile sehemu ya kwanza ya majibu yako, kwa vile haina hata punje ya Neno la Mungu, nami ninaiacha ielee hewani kwa ajili ya kunguru na matumbusi wenye kupenda mizoga!

  Sehemu ya pili na ya tatu, hizi ni njema maana zinatoa fursa ya kujifunza Neno la Mungu, nitaziendea hizo kwa ajili hiyo kama ulivyoziorodhesha.

  1: Ila nina jambo fulani:
-Nakushawishi kutoridhika na kuandika novel ili watu waone kama unajua andika.
-Ni almost kila siku unaandika kama wengine wanadanganywa na dini zao. Nimejizuiza siku nyingi, lakini ninaamua leo nikuambia. Una uhakika? Wewe huko ndani ya dini? Nayo inakudanganya? Una uhakika uko sahihi na yote unayosema? Na kama ndiyo kwa nini unakwepa logic ya mazungumzo?

  JIBU: Ushawishi wako kwamba nisiandike novel ni wa kinafiki zaidi kuliko kimantiki, kwahiyo siupokei. huko nyuma ulishawahi kulalamikia “kuandika mingi” halafu wewe mwenyewe ukaishia kuandika zaidi ya mingi na nikakuonesha, bali nilikuambia kuwa umeandika mingi kwa sababu unayo mingi ya kuandika!!!

  Kuhusu kuwa ndani ya dini, nina uhakika na ninayoyasema! Niliwahi kukuambia huko nyuma kuwa hapa tunayatazama zaidi Maandiko kuliko misimamo ya dini, na nikakukumbusha ujitahidi kuiepuka misimamo ya dini au ukishindwa basi uwe tayari kuitetea na si kuwalazimisha watu waipokee kama unavyojitahidi!
  Kuhusu kwamba eti nakwepa logic ya mazungumzo, ni absurd statement! SIJAWAHI KUKWEPA hata mara moja, labda kama ni mambo ya kitoto, kama hili uliloling’ang’ania kwamba CHANGIZO na KIINGILIO vina maana sawa, licha ya kukuonesha maana zake ktk lugha sanifu! Sasa, sijui utaendelea kujadili nini na mtu aliyeikataa maana ya maneno ktk lugha mnazozitumia, hata hiyo logic mtaitoa wapi nje ya maana ya maneno? Ndio maana nilikuaga baada ya kuona ni upuuzi kuendelea na mjadala ktk grotesque setting kama hiyo ambayo inawapeleka ktk kufuru msizozitarajia, kama hiyo mizaha kwamba Changizo alizoziamuru mtume Paul ni sawa na Kiingilio!!!!!

  Lakini jambo la Injili, kama lipo ambalo sijalijibu, nitafurahi kulijibu!

  Novel itaendelea ….

  Gbu!

 10. Ndugu Lwembe,

  -Neno la Mungu kwa Agano jipya ni katika imani na neema itokayo kwa Yesu Kristo. Wewe unaiweka kwenye “changamsha akili”, ndiyo maana mambo ya kiroho yanakushinda.
  -Hiyo wakati ya mwisho ambayo Daniel alitabiri ndiyo siku ya mwisho iliyoonyeshwa Yahana. Na Yule aliemuonyesha ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo.
  “Ufunuo wa Yohana 1: 1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako UPESI; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;
  2 aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.
  3 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati U KARIBU.”

  Bwana Yesu asifiwe!

  Lwembe, Yesu ndiye mwanzo na mwisho. Huo ufunuo unaesoma ni wa Yesu Kristo kwa makanisa, akieeleza jinsi ile siku yaja upesi na jinsi mambo yatakuwa. Kwani yeye ni mwanzo na mwisho, ndiyo maana utakuta katika hii kitabu kinachofunga Biblia mambo ya huko mwanzoni, na inaendelea mpaka mwisho.

  Shika Injili Lwembe, usije ukaangamie! Acha kumpinga Kristo!

  Asante

 11. Ndugu yangu Lwembe,

  Nimeyaona makala yako mengine, nashukuru sana.

  1)Ila nina jambo fulani:
  -Nakushawishi kutoridhika na kuandika novel ili watu waone kama unajua andika.
  -Ni almost kila siku unaandika kama wengine wanadanganywa na dini zao. Nimejizuiza siku nyingi, lakini ninaamua leo nikuambia. Una uhakika? Wewe huko ndani ya dini? Nayo inakudanganya? Una uhakika uko sahihi na yote unayosema? Na kama ndiyo kwa nini unakwepa logic ya mazungumzo?

  2) Neno tulilozungumzia kwa hii period ni kwamba hawo manabii wawili wamefika au hawajafika? Nadhani ulileta tu history lakini hukuingia rohoni na kufwatilia logic ya topic hii.
  – Umekubali walifika, nao ni Yohana Mbatizaji na Yesu Kristo, ila ukasema walitimiza kwa nusu. Je ,bila kudharau yote ulioandika, kwa nini hukunipa maandiko inayoonyesha kama wao wenyewe walikiri kama hawakuweza kutimiza shurti zao?
  – Je huone kama unajifunza Yesu scientifically? Unaposema hakutimiza hii “2 Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao…” umesoma vizuri Biblia? Na hii ni nini? “Yohana 6:40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Mathayo 24: 1….29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, JUA LITATIWA GIZA, na MWEZI HUTATOA MWANGA WAKE, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
  30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
  31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”

  Lwembe, kweli, unaona Yesu hakutangaza ile siku ya kuogofya? Na hawo manabii wawili watakaokuja namna ya kiroho mara ya inne watafika kwa siku ipi? Siku ambapo jua litakuwa tayari limetiwa giza? Lwembe, jaribu kuwa mkweli.

  -Kuna jambo la kiroho ambalo hujaeleza katika fumbo ya kuwa miyoyo ya baba itageukia watoto wao. Ulitakiwa sema kama itaonekana kivipi katika ulimwengu wa roho au wa mwili ndipo ulete swali kama hiyo imekwisha tokea au la.
  -Kufwatana na logic ya mjadala, nafikiri huna hoja ingine juu ya kiingilio, si ndiyo kaka yangu?
  -Hiyo yote unayodai italetwa na manabii wengine, imekwisha tokea. Ona tena hapa:“Kumbukumbu la Torati 18:18 Mimi nitawaondokeshea NABII miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia MANENO YANGU kinywani mwake, naye atawaambia YOTE nitakayomwamuru.”
  Kinachosemwa si manabii, lakini ni nabii (mmoja).
  Lwembe, Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu, hakuna lingine. Hata ukisoma Yohana 1, utakuta hakuna lingine Neno la Mungu lisilo Yesu Kristo. Sasa utuonyeshe neno lilitoka kinywani mwa Yesu linalotupasha kama alitenda kazi kwa nusu kabla hio siku ya kuogofya. Si wewe tu Lwembe unaemfanya Yesu kuwa hakutimiza wakati yeye mwenyewe ameyasema yote?

  Ubarikiwe ndugu yangu.

 12. Ndugu Lwembe,

  Nafurahia sana jibu lako tena nahudhunika kuona unajipoteza kirahisi. Katika fumbo ya ile sentence yangu ndogo sana ambayo ulishindwa elewa, ndimo unathibitisha kama una hofu nyingi na kama huna tena hoja. Unabaki tu na kelele. Nafikiri umefahamu kama uungwana hupatikani kirahisi, na kama huna uchambuzi wa mambo!
  Huwezi endelea wakati umepigana sana na Neno la Mungu kwa kutofahamu. Umejivunja mifupa ya miguu na mikono, kiisha umeanza tumia kichwa chako, ndio maana unakipoteza. Unaposema kunyolewa,sawa, abarikiwe kwa kujivunia hila, lakini wewe utanyolewa kile usichokuwa nacho? Hivi sasa, ndugu yangu, kwa nini nisikulilie ninapoona ukijimaliza wewe mwenyewe? Lwembe, kumbe uko empty kiwango hicho?
  1)UMESHINDWA MADA YA KIINGILIO kwa kutoweza kujibu kwa makala yangu ya 22/10/2013.
  2)Uliendelea na kelele isiyo na lengo, LAKINI UKAENDA KIRI KUSHINDWA KWAKO katika makala yako ya 04/01/2014; ukaomba masamaha.
  3)NIKAKUSAMEHE katika makala yangu ya 06/01/2014 na kukupa uhuru wa kuweza kuelimishwa zaidi, ukipata jibu kwa swali lako juu ya unabii ambayo ilikuwa kipengele kidogo katika hoja yangu ya zamani wakati wa upekuzi wa mambo. Hiyo ilithibitisha kama nilikusamehe kabisa, sivyo singelikujibu wakati ulikuwa tayari umeshindwa.
  4)Tangu ile makala yangu, ulibaki hojaless mpaka unapokwamia kwa neno “moderator” kwa kutofahamu, kwani unazoea ku repeat maneno yangu kama tu mwanafunnzi mdogo sana. Kwa nini usiseme AMEN kwa Neno la Mungu ambalo nakutolea?
  Anyway, can Lwembe repeat 3 times “moderator”, please! Nafikiri umefurahi zaidi kwa lile zowezi, si ndio?
  5)Ndiyo maana unastahili kupumzishwa kwani unalia kwa kushindwa na kilio chako kinaleta kelele. Sivyo ungelijibu kwa hoja, wala hungelisema maneno yasiyo na lengo. Lwembe, unashikwa na hofu kiisha unashindwa kiri upungufu ? Uwe tu muungwana kama ulivyojaribu 22/10/2013 ; sivyo litakutimilikia lile neno lipatikanalo ndani ya 2 Petro 2:22.
  6) Ungelikuwa na hoja si ungelijibu kwa hoja inayokukabili, hiyo yangu ya 14/01/2014 uliyokwepa kwa kushindwa kusema «AMEN » ? Sasa hii unayoandika hapa 16/01/2014 ni mada ya kujadili, au ni mchezo, au mzaha, au ukosefu wa uungwana tu ?

  Pole sana Lwembe, huna hoja tangu zamani, nyamaza tu !

 13. ….Haya tunapoendelea

  Hebu itazame tena siku hiyo hapa ktk Isaya, ambayo nayo inashabihiana kiutimiaji na hiyo Malaki. Isaya 61:1-3:
  “1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao…”
  Huu ni unabii alioutoa nabii Isaya, kwamba jambo hilo lingetimia siku fulani huko mbele, haijalishi ni lini, lakini kutimia ni lazima. Unabii huu ulitolewa karibu miaka 700 kabla ya Kristo. Nacho kifungu hicho cha kwanza na nusu ya kifungu cha pili vinatimia katika Ujio wa Kristo kwa ushahidi wa Maandiko, Lk 4:17-21
  “Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
  Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”
  Hakuendelea kusoma, “Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.”!!!

  Sehemu ya pili ya kifungu hicho inahusu siku ya kisasi, hiyo unayosema unaingoja ndg Ziragora, ndiyo hiyo siku ya Bwana iliyo Kuu na Kuogofya! Hiyo koma inayokigawa kifungu hicho cha 62, ni miaka zaidi ya 2000 sasa tangu hiyo nusu ya kwanza itimie ktk ujio wa Kristo, nusu ya pili bado, hiyo ya kisasi!! Basi na hicho kifungu cha Malaki nacho kiko hivyo kama unaweza kujifunza! Nusu ndiyo hiyo aliyoitimiza Yohana, na nusu iliyobaki tunamtazamia mjumbe huyo! Ni jambo la kusikitisha kwamba unaingoja siku hiyo!

  Lakini Kanisa lina ahadi tofauti, hiyo siku haitalikuta Kanisa, kwani akija huyo Eliya, atayarejeza yote yaliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu na tunutu …! Nao mti wa Bibi Arusi kuwa kamili na tayari kwa kuungana na Bwana Arusi, ndio huko kunakoitwa kunyakuliwa kwa Kanisa! mtakaobaki Ole wenu!!!

  Hivi ndg yangu Ziragora, ni nani atakayekufungulia yaliyofungwa ktk Biblia?
  Utayajuaje haya?:
  1: Dan 12:4
  “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho”
  Yanapaswa kufunguliwa ktk siku za mwisho ili uyajue Mapenzi Makamilifu ya Mungu!
  2:Ufu 10:4
  “Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.”
  Hutaki kuyajua hayo aliyoambiwa Yohana?
  3:10:5-7
  “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; 7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; HAPO NDIPO SIRI YA MUNGU ITAKAPOTIMIZWA, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.”
  Acha woga ndg yangu, hutaki kuyajua mambo safi kama haya!!!

  Changamsha akili hiyo ndg yangu & Enjoy the Gospel!!!

  Gbu!

 14. Ndg Ziragora,

  Kuhusu Ahadi ya ujio wa Eliya, licha ya kwamba nimekupa rejea za Maandiko zinazoliongoza jambo la kumtegemea tena Eliya, naona umeshindwa kudaka chochote, huenda ni kutokana na uoga wa kusahihishwa, au upofu unaotokana na dini kwa kuyazoelea sana mafundisho yake na hivyo kila unapoifungua Biblia yako kuisoma, ukizifikia sehemu kama hizo, wewe huzisoma moja kwa moja kutoka akilini, ukiamini ndivyo ilivyoandikwa, kama Wasabato!

  Bali jambo hili liko katika Biblia yako, kama utachukua wasaa kulikagua. Hebu tuitazame tena Ahadi iliyoko ktk Malaki 4:5-6, kifungu cha 5 ndicho kinachoitoa Ahadi hiyo:
  “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.”
  Hapa ndipo ilipo hiyo Ahadi na wakati wake wa kutimia ni Kabla ya siku ile ya Bwana, hiyo iliyo kuu na kuogofya! Elia atakuja kufanya nini, Huduma yake imeorodheshwa ktk kifungu cha 6:
  “Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

  Sasa, ulikumbuke jambo hili la kwamba hii Ahadi tunayoisoma ktk kitabu cha mwisho cha Agano la Kale, kifungu chake cha mwisho, ndiyo inayotoa ahadi ya ujio wa nabii huyo wa jinsi ya akina Isaya. Hakuna mahali ambapo Isaya alitabiriwa kuja hapo alipokuja, wala Eliya Mtishibite hakuwahi kutabiriwa bali alizuka tu! Kwahiyo ni vizuri ukayafahamu maudhui ya ujio wa manabii ili usiishie kujichanganya kama ninavyokuona. Neno la Mungu ni endelevu, ndio maana unaliona katika wakati wake lilifikia kutoa Ahadi, likiisha kuwaleta watangulizi ili kupitia hao aziweke hizo Ahadi na kuzitimiza, hata hizo za ujio wa manabii!

  Kwahiyo, Mungu alipofikia kuitimiza Ahadi aliyoitoa ktk hiyo Malaki, alimtuma malaika Gabrieli kutoa Habari za kulitimiza hilo kupitia Yohana Mbatizaji, Lk 1:17:
  “Naye atatangulia mbele zake katika ROHO YA ELIYA, na nguvu zake …”
  Haleluya! Kama hawa viongozi wa kawaida wanatanguliwa na wafuasi wao, si zaidi aliye Bwana wa mabwana! Huduma yake ni ipi?:
  “… KUIGEUZA MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.”
  Neno la Mungu ni Kamili, halibahatishi, lina dove-tail! Kama unayaamini Maandiko, basi ndiyo hayo hapo yakijishuhudia yenyewe, na si Lwembe! Naye Kristo analithibitisha hilo kwa wanafunzi wake ili wajue kilichofanyika wasikae Gizani. Hakuna anayeweza kumthibitisha Nabii isipokuwa Mungu, ndio maana wote walitoka kapa kuhusu Huduma ya Yohana, hakuna aliyejua kuwa lile Andiko la Malaki lilikuwa likiwatimilia, si makuhani wala maaskofu, bali Paulo, huyo aliyemdhirisha Kristo ktk mwili alijua, Mdo 19:4 “Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.”!!!

  Mara nyingi tunapoisoma Ahadi ya ujio wa Eliya ktk Malaki, huwa hatufikii kuifuatilia kwa umakini utimiaji wake, ndio maana mafundisho kama hili ulilolileta Ziragora hupata nafasi ktk mioyo yetu kutokana na uzembe wa dini unaotufunika. Uko mfano mwingine unaofanana na huu wa Malaki 6 ambao nao koma inayokigawa kifungu hicho ina gap ya zaidi ya miaka 2000 katika kutimia kwake. Yaani ni sawa na hicho kifungu cha 6 kinaposema, “Naye ataigeuza MIOYO YA BABA IWAELEKEE WATOTO WAO, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, …” kati ya kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto na kuigeuza mioyo ya watoto kuwaelekea baba zao, ni gap ya zaidi ya miaka 2000! Unaona, si jambo lililofanyika katika mlolongo mmoja, ni vipindi viwili tofauti, kimoja kwa Israeli na kingine ni kwa Kanisa!

  Uking’ang’ana kwamba hayo yote yalitimia kwa Yohana Mbatizaji, basi itakubidi ugushi Huduma yake kwa kuiingiza Huduma ya kuigeuza mioyo watoto kuwaelekea baba zao! Na pia utueleze hao akina baba waliogeuzwa mioyo ni wepi, mioyo hiyo waliwaelekezea watoto hao ni akina nani? Na kwa upande mwingine hao watoto nao waliogeuzwa mioyo ni akina nani, na hao baba zao ni wepi?

  Hata ukilitazama vizuri jibu la Kristo kuhusu Eliya, ktk Mt 17:11 hapo anapowaambia, “Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote…” kabla hajaendelea kuwaambia kuwa amekwisha kuja, ukiirudisha sehemu ya jibu hilo ktk ulinganishi na Huduma aliyoifanya Yohana, sidhani kama utaiona sehemu hiyo ktk hiyo Huduma, huko kutengeneza yote (restore all things); ni yapi hayo aliyoyarejeza? Sehemu hii ya hili jibu inahusu nusu ya pili ya unabii wa Malaki!!! Yaani Eliya atakutangulia tena kuja kwa pili kwa Bwana kama yanavyosema Maandiko, ayarejeshe yote yaliyopotoshwa, kanisa lililo kamili liondolewe na kisha ndio ije hiyo Siku unayoingojea ndg yangu Ziragora!!!!

  ….. novel inaendelea!

 15. Ndg yangu Ziragora,

  Asante kwa kuipokea ‘novel’ niliyokuandikia na majibu yako mafupi!

  Kuhusu Biblia nilisema kwamba iko kamili na HAKUNA kilichosazwa nje kiasi kwamba kuhitaji ainuliwe nabii mwingine akilete hicho ambacho hakikuandikwa humo, na hivyo kuifanya Biblia kutokuwa kamili! Hivi ndivyo ninavyoamini kwa udhihirisho wa Maandiko.

  Lakini Ukamilifu wa Biblia ni pamoja na kutimia kwa yote yaliyo ahidiwa humo, pamoja na ujio wa hao manabii waliotabiriwa kuja. Ndio maana nikasema ilimradi nabii ametabiriwa kuja, basi na huduma atakayoifanya NI LAZIMA iwe imeorodheshwa! Katika mlolongo huo ndio nikakutajia nabii Eliya kulingana na Malaki 4. Nikakuonesha Huduma aliyoifanya ktk Yohana Mbatizaji, kwamba kulingana na Ahadi, Huduma hiyo ni nusu, imewageuza mioyo akina baba kuwaelekea watoto tu, yaani waliohudumiwa hapo walikuwa ni Israeli tu, nusu ya pili inawahusu Kanisa, huo ndio ukweli wa Maandiko kama unaweza kuyaamini!

  Halafu, pia unapaswa ufahamu kwamba nabii sio mwinjilisti wala pasta au askofu nk, nabii humuwakilisha Mungu kwa kulileta Neno kutoka Uweponi, likiisha kuletwa ndipo wainjilisti, makuhani na wahubiri wote hulichukua hilo, kisha hulisambaza na kulisimamia! Basi ahadi ya nabii inapaswa itazamwe katika jicho hilo, kwamba kuna jambo ambalo Mungu atasema nasi ktk kipindi kijacho, hapo atakapomleta nabii wake; ndio maana nikakuambia kuwa Neno haliendagi kwa pasta au askofu bali nabii! Nilikuambia manabii wa karama Mungu amewaweka ktk kila kusanyiko, hawa ni kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu waliomo ktk makusanyiko yao, lakini hao walio ktk ahadi niliokutajia wanahusika na kulileta Neno kwa Kanisa lote la dunia (kijiografia!).

  Kwahiyo ukisema Hakuna tena nabii wa jinsi hiyo, hilo litakusababishia kubaki huko nje kwa kutompokea nabii huyo, nawe utakatiliwa mbali kama ilivyokuwa kwa wale ambao hawakumpokea Kristo kulingana na Ahadi iliyotolewa kwa kinywa cha Musa!

  Kuhusu hao manabii wawili waliotajwa ktk Ufunuo 11 unaniambia, “Wale uliowasoma ktk ufunuo ukawalinganisha na Musa na Eliya ni Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji.” Lakini hili si kweli, umechapia tu, au unalazimisha jambo nje ya ufahamu! Siku zote, chochote kinachotabiriwa, hutambulika kwa sifa na si kwa sura wala hisia za dini! Mimi niliwataja hao kuwa ni Elia na Musa kutokana na sifa zinazo wahusu, Ufu 11:5-6
  “Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.”
  Mambo ya kushusha mioto na kuzifunga mbingu mvua isinyeshe, kama utakumbuka, ni mambo ya Eliya Mtishibite!! Na mapigo ya kuyageuza maji kuwa damu na mapigo mengine, Musa ndiye mtaalamu wa hayo, rudi kule Misri unaweza kuyaona hayo kwa uwazi zaidi!

  Yohana Mbatizaji hakuwahi kufanya muujiza wowote ule wa mwilini, bali wa Rohoni tu! Sijui umetumia kigezo gani unapotuambia kuwa ni mmoja wa hao! Hata Yesu Kristo, hatuna Ahadi ya yeye kuja tena na kufanya kazi hiyo na kisha kufa tena na mzoga wake kuwapo hapo njia panda “kwa siku tatu u nusu”; haya ni mafundisho ya Uongo! Tena basi, wajumbe hawa si kwa Kanisa, litakuwa limekwisha kuondoka, liko Utukufuni yanapotendeka mambo haya kwa Israeli.

  Hebu niishie hapa kwanza, nikiamini nimeijibu sehemu ya uliyoyauliza, sehemu iliyobaki, hiyo inayohusu zaidi unabii kuhusu Eliya, nitaiendea, huenda kwa kadiri ya tafakari, tutafika mahali sote tukayaelewa vizuri yanalihusu.

  Gbu!

 16. Hahahahahaha….!
  Mtu mkubwa Ziragora acha mambo ya kitoto! Wewe ndiye uliyelileta fundisho hili linaloifunga Huduma ya Unabii kwamba hakuna tena ktk AJ ndani ya mada hii ya KIINGILIO KWENYE SEMINA, sasa tunakuuliza kuhusu hilo, kwa hila unakimbilia kumuita Moderator akuokoe kutoka aibu ya kufundisha Uongo, kama si Unafiki ni nini hiki unachofanya???

  Kwani ulipotuchomekea Fundisho hilo ulikuwa hujui kwamba kuna Moderator? Ni wapi Yohana Mbatizaji alitoza Kiingilio hata ukamuunganisha kwenye hii mada?

  Acha kuukimbia ukweli, wewe kaa sawa ukatetee kafundisho kako haka wakati kanabamizwa kwenye Mwamba, kama unalia we lia tu si umekaleta mwenyewe!

  Unaponyolewa, tulia!!!!

 17. Pia nikunukuu tena:

  “Manabii na Torati ndio Agano la Kale, na katika order hiyo Yohana ndiye wa MWISHO, na si mwisho wa manabii! Kama unazijua “mbio za vijiti”, zile ambazo wakimbiaji hupokezana kijiti, unaweza kulielewa vizuri jambo hili, nacho Kijiti akiwa ndiye Kristo, lile Neno lililotabiriwa na kuwa laid down na manabii na Torati, Yohana ndiye wa mwisho, ndiye anayekirudisha Kijiti hicho kwa KIJITI mwenyewe mwanzilishi wa mbio hizo, aliyekuwa manifested in the Flesh!!!! Na katika Order hiyo Roho ya Eliya ndiyo inayomaliza, ndio maana unamuona Kristo akikufunulia jambo hilo, kwamba huyo Yohana ndiye Eliya!!!!”

  Unatuletea literature full of truth lakini kwa hila tu unashindwa ihalalisha kwa kusema wazi kama unabii iliendelea kitofauti kwa huduma!!!

  Wewe mwenyewe unathibitisha kama hiyo Roho ya Eliya iliyomjia Yahana Mbatizaji,kwa kumaliza agano la kuchakaa na kuanzisha agano jipya, NDIYO INAYOMALIZA. Huone pale umetia fullstop? Unaenda wapi tena Lwembe isipokuwa utani? Na kama umetambua hiyo una swali gani tena? Labda useme kama hapa huna tena hoja na tuendelee na makala mengine kwani mada ni “kiingilio” na siyo “unabii” Ina maana ukipungukiwa hapa haimaanishe kama kwa mada yote ni vile tu. Ndugu yangu, kuna wakati ni faida kuitika upungufu! Daka hiyo kiisha tuendelee.

  Hivi Lwembe, kungelikuwa moderator anaehusika kuamua juu ya discussion kwa namna ya upekee, si kama alikwisha kukunyamazisha zamani?

  Ubarikiwe.

 18. Ndugu Lwembe,

  Bwana Yesu Asifiwe sana !

  Nakushukuru kwa kuniandikia novel. Hawo waandishi ndiwo wanaandika mengi ili msomaji atoshe somo ndogo.

  ULIYOANDIKA YOTE INATHIBITISHA KAMA UNA TATIZO LA KUSEMA « NDIYO » AU « AMEN ».

  1)Unasema : « …Hivyo ilivyo iko Kamili, HAKUNA kilichosazwa nje kiasi kwamba kuhitaji ainuliwe nabii mwingine akilete hicho ambacho hakikuandikwa humo, na hivyo kuifanya Biblia kutokuwa kamili!»
  OK, Lwembe, bila kuridhika na kuandika tu, wewe mwenyewe si umesema kama hakuhitajiki nabii mwengine kwani Neno la Mungu, Biblia, linaenea ? Kwa nini usibaki na ile kauli tangu mwanzo hadi mwisho ? Kwa nini unajipinga mwenyewe ?
  Sasa hawo manabii waliotumiwa kwa kujenga Nyumba(Bible), na hawa wa kukaa ndani tu wako sawa ?

  Kuna mifano mingi ya tamko fulani lakini nitakupa moja : Si wote waitwao madaktari ni madaktari kwa mfumo wa shule. Waliofanya takriban miaka 6 ya chuo kikuu wanaitwa nao madaktari, lakini daktari wa kweli ni yule aliefanya miaka isiyopungua 7 zaidi ya hawo wengine. Hii mfano inaweza kukuweka sahihi kabisa ili uongeze uhakikisho kwamba hawa manabii wote si sawa.

  Waliojenga wanao siri ya nyumba, anaekaa ndani anapata tu taarifa. Utambue kama wanaoitwa manabii kwa leo wanasema mambo manabii wa kale wanaowapasha, hata wewe umekubali. Sasa sijue unacheza mchezo gani.

  2) Wayahudi kama hawakubali Yohana Mbatizaji siyo kigezo cha kuwa yeye hakuwa ao kam siye yule Eliya. Nakushangaa wakati unapolenga kiroho !!! Labda anadhani kuna anayesahau kama Eliya aliishi kimwili kabla Yahana Mbatizaji azaliwe. Kuna mambo ambayo mtu kama ni muungwana hatakiwe sema kwa kujipendeza tu. Unaposema ile unahakikisha ungali chini sana.

  Sasa wayahudi walimkubali Yesu ? Na kama hawakumkubali, iweje tu wakubali Yohana aliefika kumtayarishia mapito ? (Yohana 1:11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.), (Warumi 11:25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.)

  3) Unasema Eliya anatajwa mara tatu, yes, yeye binafsi katika mwili, ya pili ni kwani Elisha alitaka awe na ROHO ya Eliya maradufu (2 Wafalme 2:9 Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.), na ya tatu ni ile iliyotabiriwa na Nabii Malaki. Umbalimbali na hawo hakuna mwengine wa inne, na wa tano. Walio na masikio wamesikia kama mara tatu inasema nini. Usiandike kwa fikara zako ingine ya ine na ya tano ambayo unatengeneza ndani ya akili zako. Hiyo tafsiri ya TM version inaonyesha wazi kama Yohana Mbatizaji ndiye Eliya ambaye ALITARAJIWA. Yesu hakushindwa sema kama ni nusu ya Eliya, na Malaki hakushindwa sema kama wakina Eliya watafika mara mbili katika roho. Hii ni ushahidi ambayo haitoke kwangu; ni kwa Yesu Kristo na Malaki. Sasa kama wayahudi hawakumbali yeye Yohana kama Eliya haishangaze kwani Yesu naye hakubaliwa. Kinachonifurahisha ni kwamba hukukana kama yote iliyo ndani ya ufunuo si kwamba haijatokea bado. Wewe unasema hawa manabii wawili watafika kabla ile siku ya kuogofya, na hivyo ndivyo ilivyo: Yohana Mbatizaji(ELIYA) na Yesu Kristo (Musa) walikuja kabla ile siku. Sasa ile siku yaja!!! Paulo aliwaambia wafilipi:” Wafilipi 4:5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. »
  Pia Kama uko myahudi, utujulishe. Lakini sote twajua kama wayahudi wana dini yao ya kiyahudi isiyokubali agano jipya kwani wao wanangoja mkombozi mwengine asiye Yesu Kristo, atakayefika kama mfalme kisiasa. Ina maana wao si wakristo.

  4) Siyo kusema eti uko wa kiroho, na wengine wote wako wa kimwili itakayokufanya wewe kuwa mkweli, au kuwa wa kiroho wakati huna matunda ya roho. Hivi unaweza hakikisha kama wewe una paste tu maneno ya Bible bila kueleza chochote? Lwembe, try to be honest, hapo ndipo utakuwa muungwana.

  5) Lwembe, discussion yako inaonyesha huna lengo la kuhubiri au kufundisha neno la Mungu lakini unayofanya inaonekana kuwa utafiti ili upate elimu ukitumia hila. Uwe huru, tutakusaidia tu katika utafiti wako, kaka; kwani ina faida gani ufanye utafiti yuu ya Neno la Mungu na baadaye ukose uzima wa milele? Tafadhali, usishikwe na kifafa kwani umetambulikana!!!

  6. Hayo maswali, uyalete tu, nikiona yanastahili majibu nitajibu

  Asante, na Mungu akubariki.

 19. ….
  Kuhusu Yohana Mbatizaji kuwa ndiye Eliya, nilikueleza kuwa Malaika Gabrieli ndiye aliyezileta Habari hizo, Lk 1:17 ““Naye atatangulia mbele zake katika ROHO YA ELIYA, na nguvu zake”; na nikakuambia kuwa Kristo analirejea Neno hili, hapo anapowathibitishia wanafunzi wake kama ulivyoyanukuu Maandiko, “”Matthew 11: 13 For all the Prophets and the Law prophesied until John. 14 And if you are willing to accept it, he is the ELIJAH who WAS to come. 15 He who has ear, let him hear.”

  Umeelewa context ya “And if you are willing to accept it, he is the ELIJAH who WAS to come.”? Yohana Mbatizaji hawezi kuwa ndiye Eliya kimwili, ndio maana anasema if you are willing to accept, yaani anawaspiritualize wanafunzi wake akiwaingiza ktk dimension nyingine ambako ndiko mambo hayo yanaeleweka, kwamba huyu Yohana mtoto wa kuhani ndiye Eliya mnayemsubiri Israel wote, “Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?! Israeli wote walikuwa mwilini ktk siku hizo licha ya kwamba waliokusudiwa waliuitikia wito wa Yohana lakini hawakumjua kuwa ndiye Eliya, na wala hawakujua kuwa ile Huduma ya kugeuzwa mioyo ilikuwa ikiwatimilia, mpaka walipofunuliwa kwamba Roho ya Elia na nguvu zake vilikuwa juu ya Yohana, ndio maana mlishuka kule mtoni!!!! Neno la Mungu huenda kwa nabii na si mchungaji wala askofu!

  Umeiona Roho ya Eliya, hiyo hapo mara tatu: kwa Eliya mwenyewe, kisha kwa Elisha na hapa kwa Yohana Mbatizaji; sasa hao si akina Elia watatu, kama umeelewa!!!

  Na pia ni vizuri tukayasikiliza zaidi Maandiko yanachokisema, kuliko kujijaza ufahamu usioendana na Maandiko. Hayo Maandiko unayoyalazimashi kuwa ndio yanayoifunga Huduma ya Unabii kwa Agano Jipya, mbona yako wazi sana katika kujieleza mpaka inasikitisha kwamba unaweza kuyatafsiri mbali sana na yalicho! “For all the Prophets and the Law prophesied until John.” (“Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.) Kwamba wewe kifungu hiki unakiona kikikomesha Huduma ya Unabii, ni kukosa Understanding, au umepokea mafundisho potofu nawe unayaendeleza bila kujua!

  Manabii na Torati ndio Agano la Kale, na katika order hiyo Yohana ndiye wa MWISHO, na si mwisho wa manabii! Kama unazijua “mbio za vijiti”, zile ambazo wakimbiaji hupokezana kijiti, unaweza kulielewa vizuri jambo hili, nacho Kijiti akiwa ndiye Kristo, lile Neno lililotabiriwa na kuwa laid down na manabii na Torati, Yohana ndiye wa mwisho, ndiye anayekirudisha Kijiti hicho kwa KIJITI mwenyewe mwanzilishi wa mbio hizo, aliyekuwa manifested in the Flesh!!!! Na katika Order hiyo Roho ya Eliya ndiyo inayomaliza, ndio maana unamuona Kristo akikufunulia jambo hilo, kwamba huyo Yohana ndiye Eliya!!!!

  Nimeipenda ile translation ya TM version, ambayo inasema “But if you read the books of the Prophets and God’s Law closely, you will see them culminate in John, teaming up with him preparing the way for the Messiah”

  Bali, mimi naona kwamba books of the Prophets and God’s Law and John CULMINATED in Christ, Jn 3:30 “ He must increase, but I must decrease”!
  Christ is ALL the Prophets and the Law!!!

  Ninayo maswali juu ya yale uliyoyaandika, lakini ninayareseve kwa sasa ili niione response yako kwanza ndipo tuendelee katika tafakari ya jambo hili!

  Asante ndg yangu,
  &
  Gbu!!!

 20. Ndg Ziragora,

  Shalom!
  Asante kwa majibu yako, lakini naona kuna jambo ambalo unaliunganisha ktk wazo lako ingawa ni tofauti na wazo langu. Hili wazo lako kwamba “nabii kwa Agano jipya ni tofauti ya wale wa Agano la kale kihuduma” halijajengeka juu ya Msingi wa Neno la Mungu, ni mawazo yako tu! Unabii ni kipawa, kinatumika wapi na kwa namna ipi, hilo ni kulingana na Mapenzi na Mpango wa Mungu.

  Kwamba unaniambia “Ndiyo maana umeshindwa kunitajia katika Agano jipya nabii kama Isaya au Yohana Mbatizaji, … ambaye alikuwa au ni mwakilishi wa Mungu duniani.” Hili laonesha kwamba hujafahamu sawa sawa kuhusu jambo hili la manabii.

  Biblia haiko ktk jinsi ilivyo kwa kudra, bali ni Mpango Mkamilifu wa Mungu katika jinsi ya Kujifunua kwake kwetu sisi. Hivyo ilivyo iko Kamili, HAKUNA kilichosazwa nje kiasi kwamba kuhitaji ainuliwe nabii mwingine akilete hicho ambacho hakikuandikwa humo, na hivyo kuifanya Biblia kutokuwa kamili!

  Kristo ndiye Roho ya Unabii. Nalo Neno la Unabii ndilo linalomtambulisha Nabii. Nao mitume ndio waliokuwa na Neno hilo la Unabii (2Petro 1:19), hao ndio manabii wako wa kwanza katika Agano Jipya!!! Na hao wengine watakao kuja, NI LAZIMA wawe wametabiriwa katika Maandiko na Huduma watakayoifanya iwe imeorodheshwa humo ili uweze kuikagua maana Biblia IMEFUNGWA! Ndio nikakuonesha wale manabii wawili katika Ufunuo na Eliya ktk Malaki 4, kwamba kulingana na Huduma yake iliyo orodheshwa, kwa ushahidi wa Maandiko na matukio nikakuambia kuwa kuna sehemu ya Huduma hiyo haijakamilika!

  Maelezo yako yanayolikataa jambo hilo lililowazi ktk Maandiko, yanaonesha kwamba wewe unataka Maandiko ndio yakufuate uyaongoze badala ya wewe kuongozwa nayo, nakunukuu:

  ““-Nafikiri Yesu Kristo si kama sisi ili ajidanganye hata herufi ndogo, wala Malaki hakusema kama kutafika wa Elia wawili, mmoja kwa nusu na mwengine kwa ingine nusu. Hiyo ni tafsiri yako isiyo na msingi. Ni yule tu Yohana Mbatizaji na hakuna mwengine aliyetajwa. Tatizo ni kwamba kila andiko linaposomwa ndani ya ufunuo, watu huwaza kama halijatokea bado!!! Je hujue kam kuangushwa kwa shetani duniani inaandikwa ndani ya ufunuo ikiwa ni jambo lililotendeka mwanzoni? Wale uliowasoma ktk ufunuo ukawalinganisha na Musa na Eliya ni Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji.””

  Tukiyatafakari hayo uliyoyaandika, kwa kuyarudisha ktk Maandiko, labda unaweza kuona ni kwanini nasema umemtangulia Mungu mbele! Usiyachukue Maandiko bila Roho, yanaua!

  Ktk Malaki Mungu anasema “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.” Basi ukiwa ni mtu wa kujichukulia tu Maandiko, ni lazima uishie katika mawazo kama yako, kwamba Yohana ndiye aliyekuwa Elia na ukakomea hapo ktk mtazamo wa kimwili kama unavyokiri kwamba “Malaki hakusema kutakuja Elia wawili…”!!

  Mambo ya Mungu ni ya Rohoni maana yeye ni Roho, bali hudhihirika katika mwili. Ndipo ili uweze kuyaelewa vizuri unapaswa kuyarudisha Rohoni kwanza ndipo uendelee nayo mwilini! Elia, Mtishbite, yeye akiisha kuondolewa uwanjani, roho yake, Mungu ameendelea kuitumia. Baada ya yeye kuondoka, Mungu aliiweka juu ya Elisha, kama si wa rohoni huwezi kuliona hilo, utabaki kuusubiri ule mwili wa Elia nje ya mpangilio! Hebu watazame hawa walio wa kiroho uone walichokiona, 2 Fal 2:15
  “Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.”
  Umeona, unadhani wanamuinamia nani, Elisha?? Hao wameiona Roho ya Eliya!!

  ….inaendelea!

 21. Ndugu Lwembe,

  Hahahahaaaah!!!!
  Nadhani hapa tu ulitaka tucheke ukapita humo ndani na huko pembeni ukipiga chakacha. Nakupigia nami saluti kwani kuchekesha watu nayo ni karama. Tumecheka pamoja na Mungu wetu apewe sifa.

  -Kuwa umekubali kama wanaoitwa nabii kwa Agano jipya ni tofauti ya wale wa Agano la kale kihuduma, ile imekuleta kwenye tafsiri yangu. Hivi hakuna cha kuongeza, na nikiendelea nitakuwa nikipenda Lwembe aandike nukta kwa nukta kama Ziragora, jambo ambalo haliwezekani kwani ni watu wawili tofauti kimwili. Hivi umekubali mtazamo wangu, nasema tena asante. Vile vile nakushukuru kwa tamko yoyote uliyoongeza, na Mungu akubariki.

  -Nafikiri umekubali kama Agabo hakuleta jambo jipya. Hiyo ndiyo inamuweka kwenye unabii wa kipawa tofauti na ule wa huduma. Ktk makala yangu mengine nilikuambia kam anaeitwa nabii kwa leo anarudilia tu ile iliosemwa kabla yeye aseme. Na huyu Agabo hakukwepa hiyo statement. Ndiyo maana umeshindwa kunitajia katika Agano jipya nabii kama Isaya au Yohana Mbatizaji, … ambaye alikuwa au ni mwakilishi wa Mungu duniani. Si pengine nawewe ulisema wa interpreters wa maandiko, wakiwa chini ya uongozi wa wachungaji? Ni nabii kwa lugha ya kiteolojia lakini si nabii kwa huduma.

  -Nafikiri Yesu Kristo si kama sisi ili ajidanganye hata herufi ndogo, wala Malaki hakusema kama kutafika wa Elia wawili, mmoja kwa nusu na mwengine kwa ingine nusu. Hiyo ni tafsiri yako isiyo na msingi. Ni yule tu Yohana Mbatizaji na hakuna mwengine aliyetajwa. Tatizo ni kwamba kila andiko linaposomwa ndani ya ufunuo, watu huwaza kama halijatokea bado!!! Je hujue kam kuangushwa kwa shetani duniani inaandikwa ndani ya ufunuo ikiwa ni jambo lililotendeka mwanzoni? Wale uliowasoma ktk ufunuo ukawalinganisha na Musa na Eliya ni Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji.

  Uniruhusu niweke lile andiko tunalozungumzia kwa lugha ya kingereza katika NIV version:
  Kama Yohana Mbatizaji ndiye nabii wa mwisho na ni yeye yule Eliya alietabiriwa:”Matthew 11: 13 For all the Prophets and the Law prophesied until John. 14 And if you are willing to accept it, he is the ELIJAH who WAS to come. 15 He who has ear, let him hear.”
  Tena nitaiandika kwa TM version:
  “Matthew 11: 13 But if you read the books of the Prophets and God’s Law closely, you will see them culminate in John, teaming up with him preparing the way for the Messiah of the kingdom. 14. Looked at this way, John is the “ELIJAH” you’ve all been expecting to arrive and introduce the Messiah. 15 “Are you listening to me? Really listening?”

  Ndugu yangu, asiyesikia, ina maana hana masikio. TM version ingali ikiuliza kama watu wanasikiliza hili neno au la!

  Ile siku ya Bwana yaja. Tujiweke tayari.Wale manabii walipita, vita kali ya kiroho ilianza na itaendelea mpaka ile siku.

  Acha nikuwekee chakula kingine ndugu yangu, nakupendaga sana!
  Musa anayetajwa ndiye Yesu:
  “Kumbukumbu la Torati 18:18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.”
  Jumlisha na:
  “Yohana 1:45 Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.”

  Nafikiri umetosheka kabisa.

  Ndugu yangu, nina shauri ndogo kwako: Vaa kofia yako vizuri wala usiyivike wengine. Hivi hujatambua kama ni wewe unaeendelea na tafsiri tu tangu mwanzo hadi mwisho?

  Kwa kumaliza, nakushukuru, uko mwanaume kabisa, hauko wa kusemasema AMEN, una jinsi yako ya kuitika mambo.

  Hii topic kidogo imemalizika kwa usalama, tukizama sote ndani ya Injili.

  Anae swali lingine alilete nalo tulitazame pamoja.

  Haleluya!!!

  Na mada inaendelea…

  Ubarikiwe kaka yangu.

 22. Ndg Ziragora,

  Bwana Yesu Asifiwe!
  Ninakushukuru kwa kulipokea ombi langu, yote uliyoyasema nimeyasikia, na ninaamini kwamba yanaufunga ukurasa. Asante na Bwana akubariki!

  Tukirejea katika kujifunza, kwanza nikushukuru kwa majibu yako na rejea zake za Maandiko. Nimeyatafakari with an open mind ili niweze kulifikia wazo lako katika hayo uliyoyaandika katika msingi wa kile kifungu cha Mathayo 11-13-15, bado nashawishika kwamba maelezo uliyoyatoa, yaani hiyo tafsiri au interpretation ya kifungu hicho, HAIOANI na kifungu chenyewe!
  “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15 Mwenye masikio, na asikie.”

  Maelezo yako yanaifunga Ofisi ya Unabii, yaani kwamba HAKUTAKUWA na nabii tena, hao wa aina ya akina Isaya nk, baada ya Kristo;
  “Nafikiri ulisoma vizuri nilioandika. Utagundua kam unabii wa leo si kama unabii wa zamani . Ule wa zamani uliisha na Yohana Mbatizaji. Unabii wa zamani ulikuwa professional/kazi/huduma.”
  Lakini Maandiko yanazumgumzia ukomo wa Manabii na Torati, kutokea huko walikoanzia, huko unakokuita zamani, yaani Agano la Kale, kwamba ukomo wa makundi hayo, yanaishia na Yohana, huyu ndiye anayelifunga Agano la Kale kwa kumkaribisha Masihi, huyo ambaye habari zake zimetabiriwa Agano la Kale looote! Kifungu hiki hakisemi kwamba Mungu hatainua tena na nabii wa jinsi hiyo, bali Kristo, huyo aliyewavuvia Manabii na Torati, anasema kazi waliyoifanya, yeye ndiye udhihirisho wa yote hayo, manabii na Torati, kwahiyo anapaswa asikilizwe Yeye sasa; ndio maana alipoongozana na wale wa Emausi aliyarejea hayo ya manabii na Torati ili kuwafungua wale wanafunzi wake kuhusu Yeye!

  Ni jambo jema kwamba umemtambua Agabo kuwa ni nabii. Kwamba alizaliwa kabla au baada ya Yohana, hili naona liko wazi kama unavyolisoma ktk Biblia yako, halihitaji kuumiza kichwa, huduma yake imeonekana baada ya Yohana Mbatizaji, nayo Maandiko, hicho kifungu cha Mt 11:13 kinathibitisha kwamba Yohana ndiye nabii wa mwisho kwa AK! Tukumbuke pia kwamba hakuna nabii wa kweli anayekuja na ujumbe wake binafsi, bali Mungu ndiye humpa Ujumbe kwa ajili ya watu wake, awe wa Karama au Professional! Agabo akiwa ni nabii, yaani “muonaji”, aliwaletea kusanyiko habari za yatakayomfika Paulo!

  Kunena kunakozungumziwa ktk 1 Wakorintho 14:29 “Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.” Hili ninaamini linahusiana na kunena kwa lugha, kukiwa na ujumbe wa kinabii kwa kanisa na hivyo kuhitaji kupambanuliwa, otherwise kuna manabii katika makusanyiko kama hao wa Efe 4:11 ambao ni waonaji na kusanyiko huwatumia hao wanapotaka kuwasiliana na Mungu juu ya jambo linalowatatiza au kupata maelekezo, au Mungu hapo anapotaka kuwasiliana na wanae, hawa huwaga ni lugha iliyonyooka. Bali utaratibu wa huduma hii huwa ni chini ya mchungaji wa kusanyiko na si vinginevyo!

  Kuhusu Malaki 4:5, ni sawa kwamba Yohana Mbatizaji alilitimiza Andiko hilo, bali ni kwa sehemu tu. Biblia inapomtabiria mtumishi, huainisha na shughuli atakayoifanya. Yohana Mbatizaji alipoulizwa wewe ni nani, alijibu mimi ni “Sauti ya mtu aliaye nyikani” akiurejea unabii wa nduguye, Isaya!

  Kwamba Kristo anawaambia wanafunzi wake kwamba Yohana ni nani, hilo lina faida kubwa sana kwa watu walio katika tegemeo fulani. Wako Wayahudi ambao wanamsubiri Eliya mpaka leo hii, kwa Huduma aliyoimaliza Yohana!

  Ili kulipata vizuri jambo hili la Yohana kuutimiza nusu ya unabii, ni lazima kuyachunguza Maandiko ili kuyaona haya ninayotaka uyaone, yamo humo ktk Biblia yako, ni suala la kuamini tu hicho unachokisoma na kukiacha kijitafsiri chenyewe!

  Kuhusu Eliya aliye katika Ahadi ya Malaki haya hapa maelezo yanayomuhusu, Mal 4:5-6
  “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. 6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

  Kauli ya Kristo inayomtambulisha Yohana Mbatizaji kuwa ndiye Eliya inatokana na Neno hili alilolileta malaika Gabrieli ktk Lk 1:17 likimzungumzia Yohana Mbatizaji:
  “Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.”
  Kwa kadiri utakavyoyatafakari Maandiko haya, utaona kwamba Yohana alitimiza nusu ya kifungu cha 6 cha hiyo Malaki, “Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao” ndiyo hii hapa ktk Lk, “Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto” Torati inaishia hapo, wanapaswa sasa wamsikilize Kristo huyo mtoto aliyetabiriwa ktk Isaya!

  Yohana HAKUIMALIZA Huduma yote iliyotabiriwa kwa Eliya, kama aliitimiza yote basi iwapi ile siku ya BWANA? Haijaja kwasababu huduma iliyotabiriwa haikukamilika ktk wakati huo. Waligeuzwa mioyo watu wa Torati tu kuifuata Injili, hao watoto! Eliya anapaswa aje tena kwa kazi ya kuigeuza mioyo ya watoto waliozaliwa kwa Injili, sisi ambao leo hii tumevurugika kuliko mkorogo, kila kundi na mafundisho yake halafu kila mmoja wetu anangoja kunyakuliwa; Mungu ameahidi kuturejeza, akiigeuza mioyo yetu kuwaelekea baba zetu wa imani, mitume ili kuufunga wakati, hapo kanisa litakapoifikia Imani moja na Roho moja kwa kugeuzwa huko! Hiyo ndiyo kazi ya Eliya, kwa ile nusu iliyobaki!

  Pia, ukisoma ktk Ufu 11,utaowaona manabii tena akina Musa na Elia, upande huu wa Agano Jipya!!

  Waaaaaa! Enjoy the Gospel!

  Asante, & Gbu!

 23. Tumaini,

  Asante sana kwa comment, nimefurahi kukusoma!
  Ni kweli kwamba tunajifunza mambo mengi saaana ya Wokovu hapa; binafsi toka nifike hapa, I have enjoyed every bit of it! Wakati mwingine tuna lock horns, swords flying, and things, but NEVER seeking to pierce the hearts, for we do it in Love, ndio maana nikimsikia mtu anasema ANAONDOKA, huwa namshangaa sana, nadhani its a weakness not befitting a soldier, especially a Christian soldier, How can you walk away from the Communion Table???

  Unajua, God is daring us to go to Him like He did Peter kule baharini! Lets GO for the Word without flinching, lets walk the water, this time bila kuzama, maana ukizama ndio mchezo umekwisha!!!! Lete “Mkate” Tumaini!!!!

  Basi ndugu yangu, kuna misemo au slogan ambazo ni maarufu hapa, denoting the bonding spirit:
  “Tuendelee Kujifunza”
  “Press On”
  “ Keep on Digging”
  and finally, the Famous “Twende Kazi” from Siyi, the Granite!!!
  Hahahahaha… not forgetting “Ufahamu ni Chembe ya Uhai!!

  Enjoy the Gospel,
  &
  Gbu my brother, for the Soothing Balm!!!

 24. Lwembe nimekukubali mjol wa Mungu!Umeonyesha ukomavu wa Kiroho na umeonye kwamba S.G cyo sehemu ya maigizo au sehemu ya kuuza sura bt ni sehemu ambayo 2naweza kujifunza tena hata kubadilika pia!unyenyekevu uliyouonyesha umenibariki sana tena nimejifunza mambo makubwa sana ktk hili.Mungu aendelee kukutia nguvu ktk kuisongesha injili BIG UP.Some tymez nilikuwa naboreka sana kuona baadhi ya wapendwa kutokutaka kujifunza kwa wengine na kuamua kushikilia kile anachokiamini hata kama wapo kwenye njia ya upotevuni!bt 4rom now naona umeonyesha njia so wapendwa wengine tutabadilika na kukubali kujifunza kutoka kwa wengine.Nakupa Saluti.BE BLESSED.

 25. Ndugu yangu Lwembe,

  Bwana Yesu asifiwe!
  Nafurahi sana kwa majibu yako. Naamini umeomba msamaa wa dhati. Nami nimekusamehe yote kwa dhati. Kiukweli ni kwamba hata mimi nilijikuta ndani ya “Jela” tofauti kwani nilikosa namna ya kuendelea mjadala licha ya kuwa nilipenda nijifunze na niendelee kuleta mchango wangu. Hali kama hii ingenisukuma pengine kuaga SG. Hivi unayofanya ni ungwana kabisa, Mungu akubariki. Kuwa watu watafurahi, sina masito. Nadhani ni wote kabisa. Hatutakiwe hata kuwa na vikundi, sisi sote ni kuelimishana tu. Wanaojadili si wengi sana, wengine wanaleta mchango kidogo bila kuendelea, na wengine wanaweka posts zao tu kiisha hawarudie kutuambia kam wametosheka au la.
  Kwa hivi, pengine nawe nilikukwaza, zaidi niliposema juu ya ujinga. Samahani kabisa. Nilijieleza lakini lile neno liliendelea jitokeza. Sikulenga mtu kama mjinga bali lililomponyoka akiandika.Hivi naamini kwa upande wako vilevile utasahau iliyokukwaza yote.
  Sasa kwa ukubali wako pamoja na wandugu wengine imetupasa tujenge juu ya msingi mpya kuanzia hii mwaka 2014. Izikwe uongo na hila ili tutembee kwa utaratibu tukitegemea Neno la Mungu na kuheshimiana. Ninafikiri ni vema zaidi ku debate neno na kulimaliza kwa salama, au tukikosa jibu nasi tunaomba wengine msaada hata kwa kuipost upya. Hapa nataka nikuombe kujisikia huru kujadili kulingana na mtazamo wako.Naamini kam uongo huwezi tena kujiingiza pahali ungwana uko.

  Ngoja basi nikujibu:

  A. Ninaanza nikitia swali lako nikikunukuu.

  “Ifuatayo ni sehemu ya kauli yako katika maelezo yako ktk mada hii (18/10/2013):
  “”Na tena kuna kutofamu juu ya mambo ya unabii. Leo hakuna nabii kwa jina kama ya zamani. Yesu yeye pekee alisema kama Yahana ndiye aliekuwa nabii wa mwisho. Ndio maana tunakataa yule anaeleta unabii ingine. Leo ni mitume (wachungaji, wainjilisti,wazee, Askofu, nk). Humo ndimo Mungu anachipusha ufafanuzi wa neno lake na hii ndio tunayosema unabii kwa leo. Lakini ukiona vizuri ni tafsiri ao maelekezo ya ile iliosemwa na manabii tangu zamani (Ina maana, unabii wa leo ni ukumbusho wa unabii wa zamani).
  Yesu anasema hivi:
“Mathayo 11-12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15 Mwenye masikio, na asikie.”
  Asiongee kitu usichokijua, acha wanaojua maana ya semina wasaidie alieleta mada. Inatakiwa kutoa kiingilio ili uingiye kwenye semina.””
  Ndipo nikakuuliza maswali machache kuhusu hayo uliyonifundisha:

  1: Maandiko katika Efe 4:11 yanazungumzia huduma ya manabii kuendelea, “11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa MANABII; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu”
  Je, Andiko hili ni uongo??
  2: Mdo 21:10-11 “Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.”
  Unasemaje kuhusu nabii huyu pia, ni wa Agano la Kale?
 Je, unajua kwamba jambo hili lilitokea kama alivyolitabiri huyo nabii?
  3: Mal 4:5 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.”
  Je, amekwisha kuja nabii huyu aliyeahidiwa kuletwa?
  Ninakushukuru kwa kuutoa wakati wako kusawazisha matuta haya! »

  B. Yafwatayo ni majibu yangu.

  0.Ndugu yangu, mtu akikuletea shairi ya biblia inaomba uizungumzie kwanza, pengine uonyeshe kunapo upungufu na kwa nini ile upungufu, ndipo uweke shairi ingine ya kuelimisha zaidi. Lakini mtu akileta neno na wewe unaweka lingine tu bila kuongelea uliyowekewa itaonekana biblia inajipinga na hii siyo sahihi kabisa katika mjadala wa wakristo. Inatakiwa kupekuwa kwanza uliyotolewa kabla uweke changamoto ingine. Kwani hapa sione mahala unapotupilia mbali andiko nililokuletea. Hivi sasa mimi nafikiri hili andiko lililotoka kinywani mwa Yesu likisema kama manabii wote walitabiri mpaka Yohana ulilikubali na maelezo yangu pia. After that ukasoma nafasi nyingine ambapo hukuelewa kuambatanisha na hilo andiko. Hivi nataka nilete mwangaza kwa ile sikitiko lako.

  1.Nafikiri ulisoma vizuri nilioandika. Utagundua kam unabii wa leo si kama unabii wa zamani . Ule wa zamani uliisha na Yohana Mbatizaji. Unabii wa zamani ulikuwa professional/kazi/huduma. Na kati ya nabii na Mungu hakuwa mtu mwengine kwa huduma yoyote au conditions nyingine zitokazo kwa mtu mwengine. Unabii wa leo ni kipawa tena mtu anatabiri mambo yaliyotabiriwa zamani, wala si mapya. Utanisikia zaidi nitakapofika kwa ile swali ya pili inayosema juu ya Agabo. Utaona kama wakati wa mitume, alieitwa nabii hakuruhusiwa kuleta unabii wake kama huchunguzwe na mitume. Sasa umekwisha kuona wapi katika agano la kale mahala nabii anategemea mtu mwengine kiroho? Au una uhakika unawezataja majina ya manabii wengine kihuduma kabisa waliowekwa na Mungu waziwazi kama Yohana Mbatizaji, Elia, Elisha, Hosea, Isaya, nk? Ndugu yangu ukitazama vizuri, utaona tu inayoitwa unabii ni karama tu inayojitokeza kwa mtu pengine hata siku moja tu kufwatana na jinsi RM anapenda. Lakini zamani ilikuwa huduma mpaka kufa.
  Soma:
  1 Wakorintho 14:37 Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana
  1 Wakorintho 14:29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.
  1 Wakorintho 13:9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

  2. Nabii Agabo :
  -Yeye hatujue kama alizaliwa mbele au nyuma ya Yohana Mbatizaji.
  -Hakunena jambo jipya. Alirudilia ambayo Yesu aliambia Mitume. “Luka 21:12 Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.”
  Nafikiri umeona kama Agabo hakusema neno lipya kama jinsi nilivyosema katika ile hoja yangu ya 18/10/2013

  3. Mal 4:5.
  Nadhani hungeliniswali wakati unayo jibu ndani ya ile niliokuandikia na uliyonukuu wewe mwenyewe. Acha tu ni paste sehemu ndogo ktk ile ulionukuu:
  “Mathayo 11-12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye ELIYA atakayekuja.
15 Mwenye masikio, na asikie. »
  Si unaona kama ule Eliya ambaye Nabii Malaki aliemtaja ni Yohana Mbatizaji ?

  Ahsante, na Mungu akupe maisha mazuri.

 26. Ndg Ziragora,

  Nimefurahi kukuona tena ktk Mwaka Mpya huu! Ni mategemeo yangu kwamba umeongezeka katika umri na hekima!

  Jambo la kwanza nisilopenda kuingia nalo ktk Mwaka huu Mpya wenye matumaini makubwa ni hali yangu ya “Kuwekwa Jela”; kwahiyo ninakuomba unisamehe “Uongo wangu” na “Ujinga wangu” wote; Pia ukupokee kushindwa kwangu kuyajibu maswali yako kama changamoto ya kuzidi kunifundisha hayo niliyoyashindwa ili wokovu unaonitamania unifikie na niweze kuufikia ufahamu kama wako ktk hayo unayonifundisha na mengineyo utakayoyaleta!

  Pia, ninatarajia sasa kwa kuacha “Uongo wangu”, wana SG wote wanafuraha kubwa kama ulivyosema au unavyotaraji, kwa uhakika kabisa najua walio na furaha ya kupitiliza watakuwa ni Seleli na Sungura na Mabinza, pamoja na wote, nawaombeni radhi nyote!

  Basi kwa imani nikiwa nimekwisha kutoka “Jela”, ninakusubiri ndg yangu Ziragora, uniweke sawa katika hayo niliyokuuliza pamoja na majibu sahihi ya maswali yako ili tuendelee kujifunza!!!

  Ubarikiwe ndg yangu!!!

 27. Lwembe,

  Maswali yangu yanayohusu ibada na sadaka hujayajibu brother, imeweka mkazo kwenye maelezo mengine tu.

  Kuhusu suala la sadaka ya upatanisho, na lenyewe umebabaisha kidogo kwenye kujibu. Kristo si sadaka tunayotoa sisi, bali ni sadaka ambayo Mungu katoa kwa ajili yetu.

  Halafu Isaka hakuwa anatolewa kama sadaka ya dhambi katika lile tukio, maana Ibra hapo alikuwa hamtoi kwa ajili ya kutubia dhambi yoyote ile mbele za Mungu, bali alikuwa anamtoa tu kama sadaka ya upendo na utii kwa Mungu. Na nia ya Mungu haikuwa Isaka kuchinjwa kweli, bali ilikuwa ni kupima moyo wa Ibra wa upendo kwa Mungu. ndio maana biblia inasema Mungu alimjaribu Ibrahim

  Ndio maana wanaokomaaga leo kuwaambia watu ati wamtoe Isaka wao, mimi huwa nawashangaa. Maana aliyemtoa Isaka, mwisho wa siku hakumteketeza bali alirudi naye nyumbani, sasa sijui wanapotuambiaga tutoe vile vitu tunavyovipenda sana kama mwisho wa siku nasi tutarudi navyo nyumbani kama Ibra alivyorudi na Isaka wake

  Anyway, asante kwa majibu yako.

 28. Ndugu yangu Lwembe,

  Usijali, tuko tu pamoja. Sorry kabisa, nimechelewa kufika. I was not online. Asante kwa kunitakia mwaka mzuri, jambo ambalo nilikutakia katika mada ingine kabla sijawa offline.

  Ndugu yangu, usife moyo. Unapojitazama ni wewe mwenye kushindwa, hii ni kawaida. Kumbuka jinsi unazoea kuniita mwalimu. Nilikuambia ndani ya mada ingine kama nimeelewa kumbe mimi ni mwalimu wa Lwembe. Nilitambua tena kama neno kubwa ninalokufundisha ni kutosema uongo na kuutofautisha na hoja/fikara/tafsiri. Kama utaacha uongo itakuwa furaha kubwa kwa wana SG wote.
  Sasa fikirini kama wewe ni mwalimu na katika class yako unajikuta uko na mwanafunzi aitwae Lwembe na tayari amepata chini ya % 50. Huyu mwanafunzi utasema hakushindwa hata kama alipata juu ya % 0? Pengine alishindwa kwani anakosa ufahamu au tu kwani kwa mtihani fulani ali cheat na akanaswa; lakini iwe hii au ile kilicho wazi ni kwamba alishindwa tu. Sasa ndugu yangu hatutauingilia ubishi, unafahamu kama kilichokuleta “kushindwa” ni ule uongo wako ambao ni cleary identified ndani ya mada hii. Kinachoonekana ni kwamba pahali pa kutubu ile uongo unaendelea tu kuuweka hadharani na kuimbaimba ile neno “uongo”. Unatakiwa pia ufahamu kutofautisha uongo na tafsiri/msimamo/mafikara/hoja. Tunaweza ongelea mengine yote lakini tubu kwanza uongo, ndugu yangu. Hapo ndipo utapata mafasiriyo juu ya unabii kwani tunaongea tunachofahamu.Mambo ni mengi yanayokungoja; wewe tu jirekebishe, wala usiwaze kam huwezi leta hoja nzito pasipo uongo. Lwembe, unatakiwa uwe mtaratibu.

  Licha ya kuwa kushindana si vibaya kulingana na aina za mashindano, hapa si kwa kushindana kwani mwalimu hana mashindano yoyote na mwanafunzi. Huyu mwanafunzi hata akileta kelele hataweza badili cheti chake, na hana jinsi ya kujiweka katika class ya juu. Ya kufanya ni kuitika kushindwa na kulirudilia lile class. Kam ni Lwembe tu hapo itakua rahisi kumrekebisha kwani mwalimu atamfwatilia kirahisi ili mwanafunzi afaulu. Kwa mtazamo mzuri, utaona kam ninachotakia Lwembe ni wokovu. Na kwa huo mtazamo nadhani ile wokovu ni karibu, kwani nafikiri Lwembe si mtu wa upotevu.

  Hence, unatakiwa uwe unazungumzia unayofahamu maksudi usijichanganye mwenyewe. Ndugu yangu, kila mara nakutolea maonyo kwa upendo, wala si kwa kushindana. Ukosefu wa ungwana kwa upande wako ndiwo unakuleta kushindwa. Hukulazimishwa kushindwa wala hatuifurahie. Uyarudilie niliyokuandikia hapo mbele utakuta nimekusaidia sana. Na kujifanya kushindwa inakuleta kupoteza kwa sisi sote utamu wa mada. Utambue vizuri kam kila mara ulipoanguka nilikuandikia kwa hudhuni.

  Unachotakiwa kufanya ni kutazama mada jinsi ilivyo. Kama hoja fulani imekupita ufahamu, usitafutishe ili usitumbukie ndani ya uongo. Uwe muungwana kam wengine, sema mapema kam hoja imekuwa nzito kwako, ndipo ulete swali lingine. Hapo kila mtu atakuona kuwa mwenye maarifa. Hebu pima kusoma mada zote, utaona jinsi tulienenda hata kwa kukiri kutofahamu jambo fulani. Hiyo ndiyo ushindi wakati wewe unaitafutia kwa mashindano. Nafikiri unafahamu kama wakombolewa wa Bwana Yesu ni hata zaidi ya washindi! Hii ni kwani wao hujishusha na Yesu kawainua. Sasa jiweke huru kiisha uinue hoja, iwe ya zamani au ya sasa.

  Kwa ile unayoita swali, uwe na tabia ya kuheshimu wengine. Wewe rudilia niliokuandikia 22/10,24/10, 29/10, 5/11, 11/11, 12/12/2013. Ni mara mingi nilikuandikia nikikuambia kam hujalipa garama ya uongo, yote mengine unayoongea si hoja bali mazungumzo tu ambayo hayana lengo . Ina maana huna swali. Ikiwa kweli unayo itakuwa kam mwanafunzi alieshindwa kiisha kaingia class ya juu akitumia kelele na hila. Usione haya kusema “sorry”, “sifahamu”, “unisaidie”, nk. Ndugu yangu Lwembe, ni katika hii maneno ndimo ungwana unapatikana, usitafutie mbali. Hata wewe si unaona matukio, ndugu yangu?

  Usikilivu mwema na Mungu akubariki kaka yangu.

 29. Ndg Ziragora,

  Pia,
  kuna maswali niliyokuuliza yaliyotokana na uliyoyafundisha, ninasikitika kwamba hujayajibu; bali inapendeza zaidi na ni uungwana kusawazisha mabonde ya ufahamu uliyoyazalisha! Ngoja niyarudie tena, maana ulichokifundisha kingali kinasimama, pamoja na maswali yake.

  Ifuatayo ni sehemu ya kauli yako katika maelezo yako ktk mada hii (18/10/2013):
  “”Na tena kuna kutofamu juu ya mambo ya unabii. Leo hakuna nabii kwa jina kama ya zamani. Yesu yeye pekee alisema kama Yahana ndiye aliekuwa nabii wa mwisho. Ndio maana tunakataa yule anaeleta unabii ingine. Leo ni mitume (wachungaji, wainjilisti,wazee, Askofu, nk). Humo ndimo Mungu anachipusha ufafanuzi wa neno lake na hii ndio tunayosema unabii kwa leo. Lakini ukiona vizuri ni tafsiri ao maelekezo ya ile iliosemwa na manabii tangu zamani (Ina maana, unabii wa leo ni ukumbusho wa unabii wa zamani).

  Yesu anasema hivi:
“Mathayo 11-12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15 Mwenye masikio, na asikie.”

  Asiongee kitu usichokijua, acha wanaojua maana ya semina wasaidie alieleta mada. Inatakiwa kutoa kiingilio ili uingiye kwenye semina.””

  Ndipo nikakuuliza maswali machache kuhusu hayo uliyonifundisha:

  1: Maandiko katika Efe 4:11 yanazungumzia huduma ya manabii kuendelea, “11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa MANABII; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu”
  Je, Andiko hili ni uongo??

  2: Mdo 21:10-11 “Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.”
  Unasemaje kuhusu nabii huyu pia, ni wa Agano la Kale?
 Je, unajua kwamba jambo hili lilitokea kama alivyolitabiri huyo nabii?

  3: Mal 4:5 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.”
  Je, amekwisha kuja nabii huyu aliyeahidiwa kuletwa?

  Ninakushukuru kwa kuutoa wakati wako kusawazisha matuta haya!

  Nakutakia Heri na Fanaka ktk sikukuu ya Xmas na mwaka mpya 2014!!!

 30. Ziragora,

  Umenipa ‘Pole sana’, nami nimeipokea hiyo pole, asante sana!

  Katika muda wote tuliolijadili jambo hili, nimepata tabu sana nikijaribu kukutafakari kuwa wewe ni mtu wa namna gani!!! Yaani unafikaje hata kujiaminisha kwamba Kiingilio ni sawa na Changizo, licha ya tafsiri ya kikamusi iliyo wazi ikiyatofautisha maneno hayo; isitoshe neno Kiingilio halijawahi kutumika ktk Biblia, basi inakuwaje hata wewe kulifanya neno hilo kuwa sehemu ya Maandiko????

  Ndio nilikuwa ninakushangaa sana, lakini namshukuru Mungu kwamba amekulazimisha mpaka umejitambulisha wewe ni nani; kumbe muda wote uko katika MASHINDANO!!! Unashindana kulipinda Neno la Mungu liseme unachokitaka ili ujitangaze Mshindi!!!! Hiyo ndiyo roho ya UNIKOLAI!!!!

  Mimi napenda kujifunza, hata ikiwa ni katika tofauti za kimtazamo, huwa bado ninajifunza hata nikazijua tofauti hizo; ila wewe nilishindwa kukubaini kutokana na kukataa kwako hata yaliyo dhahiri kilugha, kumbe masikini uko katika ushindani usio na tija, ndio maana una makelele mengi sana na kujibaraguza kwingi!

  Ninakushukuru sana, bali ushindi unaojidhanisha ni wa kufikirika tu, “Kiingilio” ni neno ambalo haliko ktk vocabulary ya Mungu, hebu litafute ulikolitoa, na ukiweza lirudishe huko huko!

  Nakutakia Heri na Fanaka ktk sikukuu ya Xmas na mwaka mpya 2014!!!

 31. Pole sana!!! Hapa si wapo waliyoshindwa zamani? Yote iliofwata kushindwa ni maongezi tu wala si hoja.

 32. Sungura,

  Kuhusu sadaka umeniuliza maswali mawili/matatu:
  1: -Je leo tunatakiwa kutoa sadaka ya upatanisho, kama ni ndiyo, ni ipi hiyo?
  JIBU:
  Ndiyo, kila Mkristo anapaswa kutoa sadaka ya upatanisho kwa ile Dhambi iliyopelekea Hukumu ya Kifo! Sadaka hiyo ni Mwana Kondoo asiye na waa aliyetolewa na Mungu kwa ajili yetu ili awe Sadaka yetu kwa ajili hiyo. Unaweza kukiona kivuli chake hapo ktk Mwa 22:13-14
  “Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.”

  Basi kama nilivyokuambia huko nyuma, kwamba ili uwe umeitoa Sadaka hiyo, ni lazima uwe UMEIPOKEA Injili ya mitume bila reservations, ndipo utahesabiwa kuitoa Sadaka hiyo iliyotolewa mara moja kwa maisha yetu yote, haitolewi mara mbili mbili! Umemuona Isaka alivyokuwa mtii mpaka kifo? Soma Isaya 53 uzione na tabia za Mwana Kondoo huyo, kisha ujilinganishe naye uone kama ule Uhai wake umeubadili wako, huo tuliourithi kwa baba zetu!
  1Pet 1:18-19 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.”

  2: a) Nami nakuuliza Lwembe, wapi biblia inasema kuwa hakuna ibada bila sadaka?
  b) Tena hebu niambie, wewe unapofanya ibada nyumbani kwako na familia yako au chumbani kwako pekee yako, au ofisini kwenu, huwa unatoa sadaka?
  c) Halafu niambie hizo dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo (1Pet 2:5), ni zipi ambazo wewe huzitoa kila unapofanya ibada?

  Jambo zima la Ibada na Sadaka, linategemea iwapo Uliungana na ile Sadaka mbadala aliyotuletea Mungu tuitoe, ambayo kwako wewe na mimi ni Injili iliyohubiriwa na Mitume, Yaani Kristo. Sadaka hiyo ndiyo inayotutenganisha na Dhambi kikamilifu hata kutuwezesha kufanya Ibada iliyo safi. Mt 26:28
  “…kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” Hakuna sadaka inayoweza kuondoa Dhambi zaidi ya Damu ya Kristo. Hata huko nyuma ktk Torati, damu ndiyo yenye kusafisha, Ebr 9:22
  “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.” Ukiendelea kifungu cha 28 kinasema, “…kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi…”

  Basi ni katika hali hii pekee, yaani ukiwa ni yule aliyeipokea Injili ya mitume, ukawa umetengwa na Dhambi, ndiposa hii 1Pet 2:5 inakuwa halisi badala kuwa nukuu tu;
  “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”

  Hilo lawezekana hivyo kwa sababu umeipokea kweli inayokutakasa, 1Pet 1:22-23 Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli… Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.” Haleluya, huyo mwenye kuzaliwa mara ya pili ndiye pekee aliyejengwa ili awe nyumba ya Roho na kuzitimiza kazi za ukuhani mtakatifu!

  Na kupitia huyo aliyezaliwa mara ya pili, Roho Mtakatifu atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, kwasababu ulimwengu wa dini haukuiamini kikamilifu Injili waliyoihubiri mitume na hivyo ibada na sadaka zao HAZIPOKELEWI kama ilivyokuwa kwa Kaini na Mafarisayo waliomkataa Kristo; Rum 15:15-16
  “…kwa neema ile niliyopewa na Mungu, ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.”

  Unauona umuhimu wa kuipokea kikamilifu Injili waliyoihubiri mitume? Kuikataa sehemu yoyote ya Injili hiyo kunazaa UNBELIEF, and my beloved brother, Unbelief is an insult to the divine veracity!!!

  Gbu!

 33. Sungura,

  Huu msemo ulionifananisha nao, hata mimi nimeupenda sana, kwamba, “Ukikataa kujifunza unakuwa funza!” Hahahahaha, Funza ni wengi sana, hata wakipelekwa chuo cha Biblia, wanatoka Funza kama walivyoingia!!!

  Kuna msomi wa chuo, nadhani atakuwa mkufunzi wako mmojawapo, nilimuuliza, anaonaje pastor wao akipelekwa kusoma ktk chuo cha Kikatoliki? Akanishangaa sana, kwamba Mlokole akasome ktk chuo cha Kikatoliki, haiwezekani! Unalionaje hilo, huyo anayegoma kwenda kusoma katika chuo hicho, si atakuwa Funza!

  Unajua Paulo alikuwa ni msomi, tena si usomi wa kubabaisha kama wetu, mara tumenunua mitihani, au tunafanyiwa, kisha tunatoka vyuoni humo tukingali Funza; Paulo alikuwa kamili, na anakuambia kuwa elimu yote aliyoipata anaihesabu kuwa mavi! Basi linapokuja suala la Funza nadhani wanakaaga kwenye mavi! Otherwise elimu ni nzuri sana haswa unapopata Ufunuo wa jambo fulani basi ile elimu uliyoipata kuhusu jambo hilo inakuwa kipimo kizuri sana cha kuujua Utukufu wa Mungu!

  Sasa hebu wewe mwenyewe jihakikishie jinsi Ufunza unavyofanya kazi:
  Kuhusu ile kauli ya Paulo niliyoinukuu kimaelezo (not a straight quote), “”Mtazame Paulo, anasema asiyefanya kazi na asile,”” ukailinganisha na ile halisi kama ilivyo ktk Biblia, na ukauliza, “Je kusema kuwa ‘asiyefanya kazi na asile, ni sawa na kusema kuwa ‘ikiwa mtu hataki kufanya kazi asile (neno chakula nimeliacha)?”
  UKAISHIA HAPO!!!

  Nikakujibu kuwa mimi sioni tofauti ya kimantiki ya kauli hizo mbili, labda ukinihakikishia kuwa watu wanakulaga na mawe! Na nikakuambia kuwa tusipokuwa makini, tutaishia katika irrelevancy!

  Jibu uliloniletea kuhusu jambo hilo la “Asiye fanya kazi na asile” hili hapa:
  “”Nilijua hicho kimstari kitakusumbua sana. Neno chakula nililiacha kwa sababu si hilo lililobeba maana iliyo kwenye huo mstari ambayo wewe hujaiona. Hata tukiliongeza kwenye paraphrase yako, na tukaliacha liendelee kuwepo kwenye mstari wenyewe, si hilo lililobeba amabacho nakwambia hujakiona.

  Unapomzomea mtu, hakikisha umejiridhisha kwa 100% kuwa uko sahihi katika unachosema.

  Nataka wewe mwenyewe kwanza uangalie na useme tena kama kuna tofauti kimaana au hakuna kati ya sentensi: ”asiyefanya kazi na asile chakula”, na ”ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”
  Na naomba wadau wengine pia waangalie hizo sentensi, kisha waseme, kama zina maana sawa kama ambavyo Lwembe amenizomea kuwa sijawa makini, hivyo naishia kwenye irrelevancy!
  Baada ya kufanya hivyo ndipo tutagundua vile ambavyo watu hudhani wamesema vile biblia inasema na kumbe wamesema maneno ya kwao yenye kufanana na ilivyosema biblia.””
  Katika hili jibu nalo, UMEISHIA HAPO!!!

  Umeandika zaidi ya makala tatu na zote unajizungusha bila kulisema kikamilifu hilo ulilosema unalijua tofauti na nilivyolitumia; basi, kujizungusha kwako huku kama sio Gospel Irrelevancy ni nini hiki unachokifanya???

  Gospel Irrelevancy ndio FUNZA brother, na naona tumekwisha fika huko!!!

 34. Lwembe,

  Kuna msemo unasema kuwa Ukikataa kujifunza unakuwa funza. Naona wewe kama hujawa funza umekaribia kabisa kuwa funza.

  Lwembe, usiendelee kupuuza elimu ya biblia, wewe huna akili kuliko wale waliogundua huko zamani kuwa elimu hiyo ni ya muhimu.

  Ninavyoiona akili yako ndivyo hivyo kabisa wakristo wengi walivyo, wale wenye kusema hawahitaji kwenda shule kujifunza, ila Roho mt. anatosha.

  Nilijua hicho kimstari kitakusumbua sana. Neno chakula nililiacha kwa sababu si hilo lililobeba maana iliyo kwenye huo mstari ambayo wewe hujaiona. Hata tukiliongeza kwenye paraphrase yako, na tukaliacha liendelee kuwepo kwenye mstari wenyewe, si hilo lililobeba amabacho nakwambia hujakiona.

  Unapomzomea mtu, hakikisha umejiridhisha kwa 100% kuwa uko sahihi katika unachosema.

  Nataka wewe mwenyewe kwanza uangalie na useme tena kama kuna tofauti kimaana au hakuna kati ya sentensi: ”asiyefanya kazi na asile chakula”, na ”ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”

  Na naomba wadau wengine pia waangalie hizo sentensi, kisha waseme, kama zina maana sawa kama ambavyo Lwembe amenizomea kuwa sijawa makini, hivyo naishia kwenye irrelevancy!

  Baada ya kufanya hivyo ndipo tutagundua vile ambavyo watu hudhani wamesema vile biblia inasema na kumbe wamesema maneno ya kwao yenye kufanana na ilivyosema biblia.

  Kuhusua sadaka, nisengependa maneno mengi yenye longolongo kama uliyosema hapo juu. Nataka useme kwa uwazi mfupi:

  -Je leo tunatakiwa kutoa sadaka ya upatanisho, kama ni ndiyo, ni ipi hiyo?

  Umezidi kusistiza haya maneno kuwa ”HAKUNA Ibada isiyo na Sadaka, hata huko mwanzo tunakorudishwa, bado kulikuwa na sadaka na inaendelea hata leo hii, labda uwe umejichanganya! ”

  Kauli hii ya hakuna ibada bila sadaka inasemwa na wakristo wengi sana. Nami nakuuliza Lwembe, wapi biblia inasema kuwa hakuna ibada bila sadaka?

  Tena hebu niambie, wewe unapofanya ibada nyumbani kwako na familia yako au chumbani kwako pekee yako, au ofisini kwenu, huwa unatoa sadaka?

  Halafu niambie hizo dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo(1Pet 2:5), ni zipi ambazo wewe huzitoa kila unapofanya ibada?

  Lwembe nakupa ushauri wa kweli kabisa hapa, kuwa wewe kwa jinsi nilivyokuona kiufahamu, hasa katika suala zima la uwezo wa lugha, ukikubali kujifunza elimu ya biblia unaweza kuwa mwalimu mzuri sana.

  Lakini kama utaendelea na msimamo wako wa kuona kuwa elimu ya biblia ni upuuzi, basi utaendelea kuwa funza!

  Asante sana!

 35. Sungura,

  Naona wakati mwingine huwa unaflow tu!!! Hivi mtu akisema “asiyefanya kazi na asile”, na mwingine akasema, “ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”; kwa mawazo yako, hayo ni mawazo mawili tofauti? Au kwa kuliacha neno “chakula”, inaleta utofauti wowote ule mtu anapokuambia “usile”? Au ulishawakuta watu wanakula mawe!!! Unajua, tusipokuwa makini tutaishia katika irrelevancy!

  Kuhusu sadaka ndg yangu, bado ninaamini kwamba ni jambo pana na linalohitaji UFUNUO! Unapotoa sadaka yako, kama unatoaga, ni lazima ujue ni kwa minajiri gani unaitoa sadaka hiyo. Je, ni ya upatanisho, au ni ya shukurani, au unasaidia yatima au wajane nk, au ni ya nini? Au ni Kiingilio kwenye semina?? Unauona umuhimu wa Ufunuo juu ya jambo hili, ukiliendea bila Ufunuo unaweza kuishia kutoa sadaka zako kama Kaini!

  Hata hivyo, jaribu kwenda pole pole ktk tafakari yako ya Neno la Mungu ili uweze kuyaoanisha yote unayoyasoma maana ni kitu kimoja! Unaniambia kwamba,
  “Ibada hata kabla ya anguko ilikuwepo. .. Mungu alikutana na Adamu wakati wa jua kupunga ndio ibada yenyewe sasa au kwa lugha rahisi inaitwa ‘FELLOWSHIP’. Wala wakati huo haikuambatana na sadaka…. Leo huhitaji kutoa sadaka yoyote ya upatanisho ili kukamilisha ibada…”

  Mawazo yako ni mazuri, lakini hayana msingi wa maelekezo ya rohoni anayopewa muaminio ili ayapokee na kuyatimiza! Unajua kuna sehemu ktk Biblia Mungu anauliza kuhusu hizo sadaka zetu, Je, ni yeye huwa anazila au sisi ndio hula hizo? Unaona, sadaka ni Symbol inayoonesha utii wa maelekezo uliyopewa, na pia huwatofautisha waigizaji kama Kaini! Kwa taarifa yako sadaka huungana na mtoa sadaka. Ukimleta kondoo wako, basi anapochinjwa unapaswa uwe umemshika ili uuone ule uhai wa kondoo unaotolewa badala yako! Ndipo Kristo akiwa ndiye Sadaka, basi tunalo sharti la kuungana naye ili awe hiyo Sadaka kwa ajili yetu. Nako kuungana naye ni kuliamini Neno la Mungu lote, ambalo ndilo Kristo, na si Neno nusu nusu, hili umelipokea na hili umelikataa, hapo hawi Sadaka kwako; ndio maana tunazitubia dhambi zile zile kila wakati, leo umezini, kesho unautubia uzinzi wako na mwezi ujao tena hivyo hivyo!!! Kwanini? Sadaka haikukamilika, umemeza nusu dozi, wakufunzi wako wamekudanganya kwa mafundisho yao yasiyo jengwa juu ya Msingi wa Neno, wengi wetu tungali tunashikiliwa na Torati kwasababu hiyo, maana unapolipokea Neno lote ndipo nguvu ya Torati hukoma!!!! Inahitajika Sadaka Kamili ili ile Nguvu ya KUKUBADILISHA, ile inayoweza kuku CONVERT iifanye kazi hiyo; ile NGUVU ya kumsukuma mtoto azaliwe, hata akiwa ni wa kiroho!!!

  HAKUNA Ibada isiyo na Sadaka, hata huko mwanzo tunakorudishwa, bado kulikuwa na sadaka na inaendelea hata leo hii, labda uwe umejichanganya! 1Pet 2:5

  “… mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”

  Unaiona sadaka hiyo, au umezoea minyama tu? Sadaka hii hutolewa na Mkristo aliyekufikia kuzaliwa mara ya pili, huyo ambaye aliungana na ile Sadaka iliyotolewa na Mungu tena, akajivisha lile Vazi, ile Ngozi (Neno lote); kama Biblia ilisema yule mwanamke mchawi alimpandisha Samweli, unaliamini hilo hivyo, kama Biblia ilisema mwanaume asifunike kichwa chake asalipo, unaliramba hilo hivyo, na si kuleta ubishi wa akina Kora!!

  Kwahiyo, ni lazima tuelewe kwamba kuifahamu Dhambi ndiko kunakoweza kukupa kuishinda. Huwezi kumshinda adui usiye mjua! Neno la Mungu ndilo linaloifunua Dhambi! Je, Neno likijaa kwa wingi ndani yetu, kuna jambo gani litakalokuwa geni kwetu ilihali yote ya Utupu mbele yake? Kama Kristo ndiye Neno, basi hilo linalojaa kwa wingi ndani yetu, ukilimeza LOOOOTE, hauoni kwamba ndiko kuwa pamoja naye alikokusema? Nia ya Kristo ni Neno lake; Hayuko mbali tukilitii hilo Neno, yeye yuko tu hapo nje akiugonga mlango wa mioyo yetu, tukimfungulia ataingia, na siku hiyo tutajua kuwa yu ndani yetu nasi tu ndani yake!!!

  Ubarikiwe!

 36. Lwembe,
  Sijakushangaa ulivyonishangaa kukuuliza hilo swali kama una uhakika Paul alisema hivyo.
  Ulichotakiwa tu kugundua mapema ni kwamba, siwezi kukuuliza swali jepesi kiasi hicho kwa pupa, hivyo ulitakiwa udadisi kwa makini kuwa kuna nini ndani ya hilo swali jepesi.

  Wewe ulidhani natania au nimeshuka kiufahmu.
  Kwa taarifa yako nilikuwa sitanii wala sina mpango wa kushuka kiufahamu, bali nilishangaa tu kuona na wewe uko kwenye kundi la wakristo wenye kukiri kile ambacho biblia haisemi.

  Ona tofauti ya ulichosema:

  Ulichokiri kuwa Paul alisema ni hiki: ”Mtazame Paulo, anasema asiyefanya kazi na asile,”

  Ulichonukuu kwenye biblia ni hiki : ”2The 3:10 – ….. kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile (chakula).”

  Je kusema kuwa ‘asiyefanya kazi na asile, ni sawa na kusema kuwa ‘ikiwa mtu hataki kufanya kazi asile(neno chakula nimeliacha)?

  Hebu angalia vizuri kisha uone kama ufahamu wangu umeshuka,au kama ninatania!

  Ok,
  Usichanganye sadaka aliyotoa Mungu na sadaka waliyotoa wanadamu (Kaini na Habili). Tunaongelea sadaka ya mwanadamu kwa Mungu, kwamba sadaka za hao jamaa ndo zilikuwa sadaka za kwanza mwanadamu kumtolea Mungu.

  Kwa hiyo bila shaka umeona ulivyokuwa umechanganya kati ya suala la sadaka na ibada. Leo hatuhitaji kutoa sadaka za upatanisho tena, sadaka hiyo ameshaitoa Mungu mwenyewe.

  Sisi kutoa sadaka za upatanisho ni kurudi kwenye yaleyale ya Adamu na Eva, ya kutengeneza vazi la majani, ambalo halikuweza kuwasitiri ipasavyo. Lakini lile la ngozi ya kondoo (sadaka ya Mungu), liliweza kuwasitiri kwa kudumu.

  Na ndiyo hizo sadaka za wanyama zilizoendelea kabla ya sadaka ya Mungu ambayo ni Kristo. Hazikufanya kitu cha kudumu,lakini yenye kufanya kitu cha kudumu ilipofika, hizo zilikoma.

  Lwembe, mpaka hapo unasemaje kuhusu kauli yako hii ”ibada yoyote inajumuisha sadaka”?

  Karibu!

 37. Sungura,

  Hivi unatania au umeshuka kiufahamu kiasi hiki? Au ndio kule kunyang’anywa hata kidogo ulichonacho kunakutimilia? Tazama unachoniuliza:
  “”Je una uhakika Paul alisema ‘asiyefanya kazi na asile’ au umesema tu kwa kusikia wengine wakisema?””
  Haya nikujibu kwamba nimewasikia wahubiri wengi wakikirejea kifungu hiki, nami nikakisoma na kukielewa kama nilivyokitumia.
  2The 3:10 “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.”
  Nao wajibu wa Mkristo umejengeka ktk Mafundisho haya.

  Kuhusu Ibada, nilichokisema kiko wazi sana katika mantiki ya kinachoendelea leo hii. Ukirudi Edeni kabla ya Anguko na kuitafakari ile Fellowship, ambayo ilikuwa Mungu ndiye anayeshuka ili kukutana na Adamu. Sijapaona mahali ambapo Adamu alimtafuta Mungu! Au umewahi kusoma popote pale ambapo Adamu alifunga?

  KUABUDU vs IBADA! Ninaliona ni jambo pana, kwahiyo inategemea unaelezea hali gani. Ukisema Fellowship, hiyo ndiyo iliyowapotea baada ya Anguko. na jinsi gani wafanye ili waweze kusitirika mbele ya Uwepo wa Mungu, ndio yale majani walliyojishonea, ile hekima ya kibinadamu, baada ya Uwepo wa Mungu kuwaacha!

  Sadaka ya kwanza basi itakuwa ile aliyoitoa Mungu kwa ajili ya Adamu na mkewe, yule kondoo aliyemchinja na kuwavika ngozi! Hiyo ndiyo jinsi pekee ya vazi lenye kusitiri unaloweza kujiwakilisha mbele za Mungu na ukapokelewa na kusikilizwa, VAA Neno la Mungu, usimsogelee Mungu ukiwa umejivisha yale ma rags ya dini uliyojishonea kwa mapokeo na akili zako!

  Kwahiyo, baada ya Anguko, ili kujirudisha ktk Fellowship na Mungu, aweze tena kutujia hiyo saa ya jioni, inatubidi tuwe katika Vazi alilotutayarishia, Neno lake. Kwahiyo inakubidi uwe msikivu ili ukijue kinachotakiwa, ambavyo usikivu huo utaupata iwapo utakuwa ktk Fellowship na Mungu kama Habili! Na sasa, leo hii Mungu alishuka tena saa ya jioni ili KULIKAMILISHA VAZI letu la Kukutania, hilo linaloturejesha tena Edeni, akailipa Deni yetu ya Dhambi tupate kuwa HURU tena!

  Basi angalieni msijichafue tena na dini zenu zinazowafundisha kulitafsiri Neno la kinabii walilokabidhiwa mitume badala ya kulipokea, LIWABADILISHE!

  Ubarikiwe!

 38. Lwembe,

  Tunakungoja tu utubu. Hiyo yote mambo ya kiingilio au changizo, haina problem dhidi ya sheria au neema. Hakuna alieikataza wala kuishurtisha, lakini discussion inapokupeleka kwenye uongo kama ule, Lwembe, Lwembe, Lwembe si utajiangamiza kwa kukosa ufahamu?

  Kwanza hakuna yeyote aliyewai leta amri ya Mungu inayokataza hiki au kile. Kushutumu watumishi wa Mungu, Lwembe is number one!!! Nani amekuroga Lwembe? Ndugu yangu, sisi tunakupenda, ndio maana tunajitaabisha kukuleta kwa Yesu hata kama wewe unatutukana.

  Lwembe, tubu, huna ingine njia.

  Yesu Kristo akufundishe.

 39. Lwembe,

  Unajua kweli kuongea na kupangilia maneno rafiki yangu hongera sana.

  Ngoja nianze hivi:

  Je una uhakika Paul alisema ‘asiyefanya kazi na asile’ au umesema tu kwa kusikia wengine wakisema?

  Soma tena niliposema ‘kila mmoja wetu atawajibika kwa Mungu’ utagundua kuwa hukuipata sawasawa maana ya nilichokisema.
  Kwa urahisi tu, nilichomaanisha ni kwamba wewe hutatoa hesabu kwangu, wala mimi sintatoa hesabu kwako, bali mimi na wewe wote tutatoa hesabu zetu kwa Mungu.

  Kwa hiyo sikuwa naongelea suala la Mungu kuwajibika kwetu kwa habari ya mahitaji yetu.

  Hakuna kitu cha maana sana ulichosema kuhusiana na suala la sadaka na ibada.

  Ibada si kwa ajili ya kujipatanisha na Mungu baada ya anguko. Na wala wakati Habili na Kaini wanatoa sadaka kwa Mungu haikuwa ibada ya kwanza hiyo, ispokuwa zilikuwa sadaka za kwanza.

  Sijui kama unaelewa maana ya Ibada, na kama maana ya ibada unayoilewa wewe ni hii uliyosema (Ibada ni jitihada za kujipatanisha na Mungu baada ya Anguko) basi ndio maana unadhani ukamilisho wa kila ibada ni sadaka hiyo ya upatanisho.,

  Ibada hata kabla ya anguko ilikuwepo. Hicho unachokisoma kwenye Mwanzo kuwa Mungu alikutana na Adamu wakati wa jua kupunga ndio ibada yenyewe sasa au kwa lugha rahisi inaitwa ‘FELLOWSHIP’. Wala wakati huo haikuambatana na sadaka.

  Na kama baada ya anguko ilikuwa ni lazima kutoa sadaka ya upatanisho, basi hiyo nayo ilikoma pale Kristo alipoutoa mwili na uhai wake uwe hiyo sadaka ya upatanisho, ambayo kwa lugha nyingine ni dhabihu/Kafara.

  Leo huhitaji kutoa sadaka yoyote ya upatanisho ili kukamilisha ibada. Na ibada leo ni kitu ‘continuous’, siyo tu pale mnapokutanika sehemu fulani. Hapa ninapoandika hivi nafanya ibada.

  Ndio maana nilikuuliza, ni sadaka ipi ambayo kwenye kila ibada lazima ijumuishwe?

  Hayo mambo mengine ya kusema siwezi kuelewa suala la mmepata bure toeni bure, sihitaji kupoteza muda kulisemea maana tayari nilishaeleza maana ya hiyo statement, kwa hiyo mwenye kusoma atahukumu kama maelezo yangu hayako sahihi.

  Hayo maneno ya bwana jela, na mengine ya aina hiyo, huo ni mzaha wako,mimi hata hayanihusu maana hata sihitaji kuelewa nini unamaanisha hapo.

  Vinginevyo , asante!

 40. Lwembe,

  Kam unaemwita Jela ni yule aliegundua kam wewe ni muongo professional basi imeonekana umeridhika kuwa ndani ya jela iliyowekewa waongo. Na hapa si mwisho, ungali utanaswa tu kwani umefanya moyo wako kuwa mgumu. Hapa umenasika mapema, sivyo uongo wako uliendelea tililika, inayo maana orodha ingekuwa ndefu sana. Itakapofika kila mtu akunase utakimbia SG. Dawa tu ni moja: kuomba masamaha ili uwe huru kwa kujadili. Wala unataka tu uwe hojaless!!! Hii uongo yako ndio inakusukuma kukosa jibu kwa swali la Ndugu Sungura. You’re out of mind. Na kwa upande mwengine you’re right kwani muongo hadaiwe jambo lingine lolote la kujadili.

  Bwana Yesu Kristo akusaidie.

 41. Sungura,

  Naona una tatizo la consistency katika kujadili mambo! Unapoteza mwelekeo mapema sana, na hilo linasababisha kila wakati uulize maswali yaliyokwisha kujibiwa! Hata jambo la versions za Biblia, nililiweka wazi kulingana na nilivyozisoma na kuelewa, nikavielezea vifungu na muktadha wake na unapobadilika kutoka jambo la kujikimu kuja jambo la kuihubiri Injili, kama hujaelewa sikulaumu, bali mimi siwezi kuacha nililolielewa nilifuate lisiloeleweka!

  Kama ni jambo la Kiingilio, hili tulikwisha limaliza pale wewe na “Bwana Jela” mlipolazimisha kuwa KIINGILIO ni sawa na CHANGIZO na SADAKA!! Mkasema hilo liko hivyo, mkaikataa na tafsiri logical ya maneno hayo, jambo ambalo linaufanya msimamo wenu wa kuyageuza maneno hayo ya lugha mkiyaleta ktk maana moja kuwa ni MAFUNUO! Mjadala ukifika ktk mafunuo hapo ndipo hukomea!!!!

  Tuliendelea ktk kipengele cha Paulo na kauli yake ya kwamba ameihubiri Injili “Free of Charge”; wewe na “Bwana Jela” mkasema hiyo “Free of Charge” inahusiana na kujikimu vya madhabahuni ambavyo yeye Paulo alikataa kujikimu kwavyo. Ndipo nikakuambia usome vizuri mchango wa “Bwana Jela” utaona amemnukuu Paulo akiwaagiza wamsafirishe yeye na alioongozana nao, kwahiyo suala la yeye kutokula vya madhabahuni linafia hapo, na kwavile vyote vinaangukia ktk Kiingilio ndio kusema Paulo alitoza gharama kwa Injili Haikuwa Bure kama anavyojigamba!!!! Hili pia tumelimalizia hapo.

  Hata mambo ya samaki na mikate, muktadha wake ulikuwa kuonesha ukarimu wa kujitoa na kuthibitisha MUUJIZA unaoambatana na huko kujitoa ktk Upendo, ili uweze kuona kwamba Mungu akiwepo hakuna kitachowapungukia, haikuwa ili tuanze kujadili miujiza ya samaki wala hali za hao waliopewa samaki! Kwahiyo wewe kuniambia kuwa:
  “”… ukitaka kufanya semina mambo ya gharama kama ukumbi, umeme, usafiri, vyombo, n.k Mungu atavileta mwenyewe, endelea kuamnini hivyo. Mwisho wa siku hakuna atakayewajibika kwa mwenzake, bali ni kila mtu kuwajibika kwa Mungu.””
  Labda nikusahihishe, si mimi ninayewajibika katika hilo bali Mungu ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha mambo yote yanalipiwa kwa kazi yake aliyonituma!!!

  Kuhusu mimi kumuomba Mungu anipe mkate wangu, nilikuambia hivi:
  “”…riziki ya mtoto wa Mungu iko katika jitihada yake ya kuliishi Neno la Mungu. Mtazame Paulo, anasema asiyefanya kazi na asile, na Mungu alisema “Kwa jasho lako…”, basi mkristo hutoka nje kwenda kulitimiza hilo ndipo Mungu huwajibika kwake”” Maisha ya mtoto wa Mungu yako hivyo ndg yangu, haijalishi watu wa dunia wanaishi ktk abundancy kiasi gani, mtazame Nabali na Daudi, unaweza kujifunza kitu!

  Suala la “mmepewa bure toeni bure”, huwezi kufikia kulielewa hilo as long as umeshindwa kuyatofautisha maneno ya kawaida ya mtaani ambayo hata mtoto wa darasa la pili anayaelewa vizuri sana! au wewe mwanao kila jumapili huwa anakuomba KIINGILIO anapokwenda kanisani? Hiyo kauli aliyoitoa Kristo ni ya Rohoni, it went before them, na wote ambao receptors zao zilikuwa live and vibrant they picked up the message and laid in wait!!!! Achana na carnality, huwezi kuyaelewa hayo, mwisho wa siku utaishia kuyakanyaga Maandiko to your own detriment!

  Kuhusu sadaka, hata sielewi nikujibu nini, lakini ngoja niendelee pengine hilo laweza kukusaidia. Ibada ni jitihada za kujipatanisha na Mungu baada ya Anguko, kulingana na maelekezo tunayopewa na Mungu mwenyewe ili kukufikia kupatanishwa huko, iwapo uliwahi kuyasikia hayo maelekezo!

  Ibada ya kwanza hii hapa, Mwa 4:3-4
  “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama.”
  Umeiona? Inaambatana na sadaka, na nyingine hii hapa,1Pet 2:5
  “… mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”
  Haya ndiyo “Mapokeo” tuliyoyapokea na tunayaishi mpaka yamekuwa ni sehemu ya maisha yetu!

  Asante sana pastor, mjadala ulikuwa ni wenye manufaa sana, ingawa mimi nimefikia upeo wa maelezo yangu, kama unalo jambo jingine basi nitafurahi kulisoma!

  Ubarikiwe!

 42. Lwembe,

  Kuna mambo mengine ni rahisi sana kuyafanyia maamuzi, moja wapo ni mada kama hii!

  Unajua msingi wa ubishani katika mada hii ulijikita kwenye mmepewa bure toeni. Na nilikuuliza kuwa ni nini hicho kilichotolewa bure, ulikwepa sana kunijibu kwa sababu uliojua kua hicho kilichotolewa bure si hicho ambacho watu hukitolea kiingilio.

  Ukaja suala la Paul kuhubiri injili ‘free of charge’, hapo napo tumefafanua vitu vingi tu.Lakini umeamua kulazimisha kuwa tafsiri zilizo kwenye version zingine haziko sawa, ispokuwa ya KJV.

  Lakini katika kuhitimisha hitimisha kwako naona umeamua kusimamia tu mawazo yako unayodhani wewe kuwa ndivyo inavyotakiwa kuwa, hujagusia tena suala la mmepata bure toeni bure.
  Na bado nazidi kusisitiza kuwa nilivyolifafanua suala la 1cor 9, niko sawa,na huo ndio msingi wa kuamini ninavyoamini kuhusu hii mada, yaani vile nilivyofafanua.

  Hivyo basi, maamuzi niliyosema hapo juu kuwa ni rahisi kuyafanya ni haya, kwamba, kuweka kiingilio kwenye semina sio kutotoa bure kile tulichopewa bure. Kuna vitu vingi sana ambavyo tunatakiwa tuvigaramie kwa habari ya injili, na huwa tunafanya hivyo, tena hufanya hivyo kwa hiari zetu kama ambavyo kiingilio huwa natoa kwa hiari yangu, maana hata kwenda kwenye hiyo semina ni hiari yangu.

  Niliwahi kusema kuwa biblia yenyewe ambayo ndio habari njema haswa, huwa haigawiwi bure, bali inauzwa, na bei yake hujipangii kwa kujisikia kwako wewe unayeinunua, bali unakuta imepngwa. Hivyo basi mnunuzi una hiari ya kununua hiyo biblia au kuacha, na wala Mungu hajawahi kuweka sheria kuwa kila mwamini lazima anunue au awe na biblia.

  Kama wewe unaamini kuwa ukitaka kufanya semina mambo ya gharama kama ukumbi, umeme, usafiri, vyombo, n.k Mungu atavileta mwenyewe, endelea kuamnini hivyo. Mwisho wa siku hakuna atakayewajibika kwa mwenzake, bali ni kila mtu kuwajibika kwa Mungu.

  Suala la Yesu na samaki, naona umeamua kuongea maneno yoyote vivihivi, Yesu aliwalisha watu samaki na mkate tena kwa muujiza kwa sababu hapakuwa na namna wangeweza kupata chakula katika hayo matukio. Ndio maana unayakuta sehemu mbili tu japokuwa ni mara nyingi tu watu walikusanyika kumsikiliza Yesu.

  Na kumwambia Mungu atupe mkate wetu wa kila siku, maana yake si sisi kuamka asubuhi na kuingia kwenye maombi hayo kisha tukifumbua macho mkate unakuwa mbele yetu. Ni ishara tu ya kumwonyesha Mungu kuwa katika yote tunamtegemea yeye na yeye ndiye hutufanya tupate yote tuhitajiyo. Maana kuna watu wengi sana hata huwa hawafanyi hayo maombi lakini hawajawahi kukosa chakula. Nani huwa anawapa?
  ……………………………………
  Lakini kuna kitu umekisema hapo mwishoni mwishoni, hiki hapa: ”….ibada yoyote inajumuisha sadaka, hiyo ndiyo order uliyopaswa ufundishwe ulipoamua kuwa mkristo”

  Lwembe ni sadaka ipi hiyo unayosemea kwamba katika ibada yoyote lazima hiyo sadaka iwepo? au ni yaleyaele mapoke ambayo huwa mnayasema tu kwa mazoea bila kuzingatia undani wake?

  Asante!

 43. Lwembe,

  Sikushangae kwani najua pale ulipo. Wewe umejiingiza jela wewe mwenyewe. Nitegemee basi una akili zaidi ya ile? Hivi umependezwa ndani baki ndani tu. Wala kusiwe wa kukuchokoza ndugu yangu. Kitu ninachokukumbusha ni kwamba siwezi ambatana na waongo. Anaekupenda yeyote akuletee msaada wa toba.

  Asante.

 44. Sungura,

  Hahahahaha….! Acha ujanja wa maneno!!!

  Wewe tukubaliane jambo moja, kuwa piga ua, ninyi, semina ni lazima mtoze Kiingilio, mwanzo mwisho!!

  Mungu kukutangulia ni reality na si jargon kama unavyosema brother! Mungu asipokutangulia basi jua kuwa hiyo ni jitihada yako mwenyewe, tena ukimaliza semina yako bila madeni, au ukapata faida kubwa, jipongeze sana!!! Yatazame Maandiko haya kama yatakusaidia:
  Isa: 45:2 “Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma”

  Kum: 31:3 “BWANA Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako.”
  8 “Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.”

  Mt 28:20 “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

  Lakini ikiwa kazi ni ya Mungu, yeye ndiye huzibeba gharama katika namna tunayoiona katika Biblia, kwa Changizo au Sadaka kutoka kwa wanae, ule Mwili wake!

  Hata unapozungumzia kuwa Kristo aliwaambia msichukue chochote cha kujikimu, kwa mantiki yako ya kutoza, ndio tuseme kwamba waliyapata mahitaji yao kutokana na viingilio walivyoviweka kwa kila mkutano waliofanya? HAWAKUTOZA! Basi unapozifikiria hizo gharama zako unazozihofia sana, hebu niambie, yaliwezekanaje hayo? Watoto wa Mungu ni jeshi kubwa sana, wewe njoo na Sauti ya Mungu tu, utashangaa!

  Pia naona unadhani kuwa haukuwa wajibu wa Yesu kuwapa wale watu samaki, sasa ilikuwaje akawapa? Ni pale walipotaka kuugeuza wajibu huo kuwa ni Tozo lao la kuisikiliza Injili ndipo akawatolea nje!!! Bali wajibu wa Yesu kuninunulia chakula au kunipa pesa za kuniwezesha katika hilo, ungali uko juu yake ndio maana kila siku mimi humkumbusha jambo hilo: “ Baba yetu … Utupe leo riziki yetu …”; Halafu usichukue tafsiri ya kiswahili ya riziki iliyoegemea sana ktk udhaifu, riziki ya mtoto wa Mungu iko katika jitihada yake ya kuliishi Neno la Mungu. Mtazame Paulo, anasema asiyefanya kazi na asile, na Mungu alisema “Kwa jasho lako…”, basi mkristo hutoka nje kwenda kulitimiza hilo ndipo Mungu huwajibika kwake, lakini ukitaka kumnafiki Mungu, eti ule bila jasho, ulete mipango yenu ya mjini na matangazo yenu ya fix uwavute watu waje uwakamue Viingilio, unakuwa huna tofauti na wale waliotaka kumseti Kristo wawe wanakula mikate na samaki bure!!!

  Unapomzungumzia Paul na Haki ya kujikimu aliyoikataa ukiileta katika kile kifungu cha 1Cor 9:18, halafu kwa hila ukachomeka “gharama za Injili” yaani kumbi, umeme, vyombo, askari wa mlangoni nk ukiudhihirisha ulazima waTozo kuzilipia hizo huduma, basi ninakushauri uisome vizuri michango ya “Bwana Jela” Ziragora ili uoanishe vizuri na wazo lako huenda jibu utakalo pata litakufikisha hatua ya juu zaidi. Maana yeye “Bwana Jela” hiyo Haki aliyoikataa Paulo, alituletea Maandiko anayotaka ahudumiwe na Kanisa, yeye Paulo pamoja na hao alionao, akatuhakikishia kuwa hilo jambo ni Tozo!!! Ndio kusema hicho kifungu cha 18 hakisemi kweli kuhusu hiyo “Free of charge” maana alihudumiwa, nanyi mkiwa huduma hizo mmezifanya Tozo yaani “Charge”!!!!

  Vinginevyo ktk ku “charge” ni lazima kuweko na kubadilishana kwa bidhaa, kama medium of exchange ni pesa basi unatoa hizo nawe unapewa bidhaa hiyo hata ikiwa ni Injili! Lakini kujikimu vya madhabahuni si hivyo, hakuna ku exchange chochote, ibada yoyote inajumuisha sadaka, hiyo ndiyo order uliyopaswa ufundishwe ulipoamua kuwa mkristo. Ukileta ujeuri kuwa oh kumbe Mungu naye ana charge Neno lake, basi jua umepotea mlango! Rudi katika Biblia yako ujaribu kuona ni wapi Mungu aliwahi kushuka na kuondoka na sadaka zenu, hakuna! Sisi wenyewe ndio huzitumia kwa ruksa yake ktk Mapenzi yake Makamilifu!

  Biblia ni “Barua ya wapenzi”; nenda nayo taratibu, wewe AMINI tu kama mtoto mdogo, au kama umekuwa mkubwa basi jitegemee na hizo Tozo zako!

  Karibu sana, Sungura!

 45. Richard,

  Sijui kama umetumbukia tu au kama umetusoma vizuri. Au umejichanganya usijue unaeandikia.
  Richard, play with your Lwembe, not with me.

  Thank you.

 46. ZIRAGORA

  Iko hivi;
  Lwembe hajapinga changizo wala sadaka ya kuwalisha/tunza/na kuwasafirisha watumishi na hata sadaka za kuchangia gharama na ndio maana amenukuu vifungu vilivyovyomuonyesha Paulo akifanya hivyo na hata wakati huu hayo mambo yapo makanisani huwa mara nyingi ajapo mtumishi kutoka nje ya nchi,mkoa,au hata jimbo huwa tunatoa sadaka ya kumsafirisha.
  na kama ni semina mbona wapo watumishi wengi tu wanazifanya tena ni kubwa tu lkn ni bure? mfno mwalimu C.Mwakasege semina zake huwa zinachukua nafasi kubwa mfano hakuna.
  mbona ni free tuu?
  ishu ipo kwenye KIINGILIO YAANI KIMA MAALUM kwamba uwe nacho au usiwe nacho bila hicho kima maaul huwezi kusikia lile neno la Mungu. Huyo Paulo aliwaambia wachange lkn hakuwawekea KIMA MAALUM
  Hilo ndilo tatizo ninaloliona kwenye kuweka kiingilio ktk semina.
  Baba yetu wa mbinguni awabariki
  aaaamen

 47. Sikia Lwembe,
  Huwezi nikamata kwa kutumia hila za uandishi rafiki yangu, nilishakwambia kuwa fasihi andishi unaiweza, kwa hiyo anayesoma ulichoandika akiwa mjinga tu unamkamata mateka ki ufahamu.

  Unachokisema wewe na ninachokisema kuhusu suala la wajibu viko tofauti.
  Wewe uliniambia kwamba nimesema ‘I dont care’ kama ametumwa na Mungu, lakini nikakwambia kuwa nilisema ‘I dont care’ kama Mungu kamwambia aniambie nitoe hicho kiasi cha pesa au thamani kwa ajili ya kuingia kwenye hiyo semina.

  Wewe msimamo wako ulikuwa umekaa kwenye mmepata bure toeni bure, lakini nimekwambia alichomaanisha Yesu hapo haikuwa mmepata bure nauli, mmepata bure gharama za umeme, mmepata bure gharama za malazi,chakula, ukumbi, n.k. kwa ajili ya semina. Lakini alimaanisha mmepata bure ile nguvu ya Mungu inayofanya kazi ndani yenu kwa ajili ya kuponya, kutoa pepo, kufufua wafu, n.k.

  Which means, usiletewe mfu ukawaambia waliomleta watoe pesa au kitu fulani ndipo umfufue, hiyo ni dhambi.

  Lakini gharama za injili hata Yesu wakati anawatuma wanafunzi aliwaambia wasichukue chochote pamoja nao, maana yake ni kwamba walienda kula cha hao waliopelekewa hizo habari njema.

  Lakini hiki kitu Paul yeye alikataa kukifanya ili apate nafasi ya kujisifia kwa habari ya kazi ya injili, pamoja na kwamba alikiita kuwa ni haki kwa mpeleka injili. Maana yeye kuhubiri injili haikuwa hiari bali amri, iwe isiwe yeye ilikuwa ni lazima ahubiri.

  Kwa hiyo wewe unaposema kuwa anayeweka kiingilio hajatumwa na Mungu ati kwa sababu Mungu akikutuma lazima akutangulie, naona umeamua tu kuweka msimamo wako ambao umeumix na ‘christian jargon inayosema ‘ Mungu akikutuma ni LAZIMA akutangulie’ ‘! Anakutanguliaje, unakuta kila kitu kimelipiwa wau anafanyaje?
  Huwezi kumfundisha Mungu njia ya kufanya jambo,wala hawezi kufanya tu kama ambavyo wewe unajua!

  Ahaa, kumbe Yesu huwa anagawa samaki bure! Vipi jana alikununulia chakula cha shilingi ngapi Lwembe?

  Mbona unajilazimisha kuwa asiyejua, huo muujiza wa samaki na mikate ndio unajaribu kuutumia kutaka kujiaminisha kuwa ni wajibu wa Yesu kuwalisha au kuwapa watu mahitaji yao ya mwilini?

  Basi Paul yeye alisema kinyume sasa, kwamba asiyetaka kufanya kazi na kula asile. Mkate wa mwilini hilo ni jukumu lako kuutafuta brother, ule pale ulikuwa muujiza tu, hayakuwa ndio maisha ya kawaida ya kila siku.

  Kama hukusoma vizuri,soma tena, ndipo utagundua kuwa hao waliolishwa samaki ndio hao kesho yake Yesu aliwapa makavu, na samaki hakuwalisha hiyo siku. Aliwaambia kazi yake si kuwapa samaki au chakula cha mwilini bali cha rohoni. Kama kazi yake ni kutupa cha rohoni then ni wajibu wetu kujipa cha mwilini.

  Isome hii hapa uone alivyowapa makavu John 6: 22-27a ( 26 – Jesus answered, “Very truly I tell you, you are looking for me, not because you saw the signs I performed but because you ate the loaves and had your fill. 27 Do not work for food that spoils, but for food that endures to eternal life, which the Son of Man will give you)

  Lwembe kwa habari ya tafsiri za biblia najua kuna tafsiri nyingi tu zenye mapungufu sehemu fulani fulani,ikiwemo ile tafsiri ya Kiswahili ya siku zote. Hata KJV siyo kwamba ndio the best, nayo ina mapungufu yake.

  Hata hivyo sioni kama kuna kutoshabihiana kwa hizo tafsiri kwa habari ya 1 cor 9, ni sisi tu tumetofautiana katika kuelewa.

  Na kama unafuatilia vema utagundua kuwa tunachotofautiana siyo suala la watu kutoa pesa kwa ajili ya semina,ispokuwa ni ile namna ya utoaji wa hizo pesa. Pesa kwa ajili ya injili lazima tutoe, maana watahubirije wasipopelekwa!

  Shida iko kwenye kuwaambia watu watoe kiasi fulani; wewe unaona hiyo inaondoa u hiari katika suala la kutoa ambao ndio msingi wa utoaji kwa agano jipya, lakini mimi pia naona kuwa hiyo bado haiondoi uhiari wa kutoa, maana mtu halazimishwi kwenda kwenye semina hiyo, wako walio tayari kwenda watatoa hicho kiasi kwa moyo wa kupenda.

  Nakushukuru pia Lwembe!

 48. Rafiki yangu Lwembe,

  Biblia inasema”kuogopa Mungu ni mwanzo wa maarifa”.
  Unasema “uniongezee ufahamu”, sawa, go ahead, sikuzuize kwani hii SG si yangu pekee. Ninachojua ni kwamba unayo bidii. Ungeliitumia kwa kuogopa Mungu, sijue ningemtukuza Mungu namna gani! Kinacholeta hudhuni ni kwamba hii bidii yako inakuongoza mpaka ujifunge wewe pekee mikono na miguu kwa kujitumbukiza ndani ya wongo. Dawa num 1 ya wongo ni kuikwepa mapema kama unavyoniona mimi hata bila kudai kam nina ufahamu kuliko wengine; lakini ukiisha ambatana nayo, dawa ni kutubu. Acha nikuache utubu kwanza. Nashangaa kuona mwanaume shujaa, anaejaa ufahamu kiwango aongezee wengine, ashindwe kutubu!!!
  Naona ungali na nia ya kujadili, kiri basi kosa lako, utoke jela kiisha uje tujadili, sitakataa kwani wewe tu ni ndugu yangu. Sivyo utakayoandika tu ni kulalamika kawaida kwa mtu yeyote ambaye anajikuta akiwa jela. Hakuna jinsi nyingine ya kukusaidia ndugu yangu kwani garama ya hii jela si pesa.

  Asante na Mungu wa Mbinguni akuwezeshe..

 49. Mpendwa Ziragora,

  Shalom!

  Unajua ndg yangu, tunayoyajadili hapa yanakuwa na maana iwapo yataiamsha ndani yako ari ya kuyatafakari Maandiko na si kukuingiza katika mzunguko wa mashindano yasiyo na tija wala mwisho kama ninavyokuona!

  Unaling’ang’aniza jambo la KIINGILIO kuwa sawa na CHANGIZO na SADAKA ukiishindwa hata akili ya kawaida ya kuitambua maana ya maneno, na kuidhihaki vocabulary, hiyo elimu inayoweza kukusaidia kuielewa Biblia yako unapoisoma.

  Ngoja nikuongezee ufahamu katika majadiliano: Unapoitetea hoja yoyote ile, basi jua ya kwamba, moja kwa moja unakuwa umejitambulisha na hiyo hoja kwa mema na mabaya yote yanayoihusu. Kwahiyo, nilipokuambia kuwa unaendesha semina za viingilio, ilikuwa ni katika maana hiyo na si kwamba mimi nilikukuta mahali fulani ukiendesha semina, kwahiyo usikazanie sana kwamba nimeongopa, si kweli!!!!

  Kama ni semina niliyokuona, labda iwe ni hii hapa kwenye blogu ambayo bado hujanidai pesa, hii unayonifundisha kuhusu unabii:
  “”Na tena kuna kutofamu juu ya mambo ya unabii. Leo hakuna nabii kwa jina kama ya zamani. Yesu yeye pekee alisema kama Yahana ndiye aliekuwa nabii wa mwisho. Ndio maana tunakataa yule anaeleta unabii ingine. Leo ni mitume (wachungaji, wainjilisti, wazee, Askofu, nk). Humo ndimo Mungu anachipusha ufafanuzi wa neno lake na hii ndio tunayosema unabii kwa leo. Lakini ukiona vizuri ni tafsiri ao maelekezo ya ile iliosemwa na manabii tangu zamani(Ina maana, unabii wa leo ni ukumbusho wa unabii wa zamani).
  Yesu anasema hivi:
“Mathayo 11 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15 Mwenye masikio, na asikie.”

  Asiongee kitu usichokijua, acha wanaojua maana ya semina wasaidie alieleta mada. Inatakiwa kutoa kiingilio ili uingiye kwenye semina.”” (18/10/13)

  Labda nikuulize maswali machache kuhusu hayo uliyonifundisha:
  1: Maandiko katika Efe 4:11 yanazungumzia huduma ya manabii kuendelea, “11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa MANABII; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu”

  Je, Andiko hili ni uongo??

  2: Mdo 21:10-11 “Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.”

  Unasemaje kuhusu nabii huyu pia, ni wa Agano la Kale?
  Je, unajua kwamba jambo hili lilitokea kama alivyolitabiri huyo nabii?

  Haya linganisha na kauli yako, ni nani anayeongea kitu asichokijua, mimi au wewe?

  Usipuuze elimu/maagizo, Mit 4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
  Mshike, maana yeye ni uzima wako.”!!!

  Soma Biblia yako kwa kituo, usisome kama gazeti, na usije kwenye mijadala na elimu za kidhehebu, kama walikudanganya kuwa hakuna tena nabii, kagua kwanza ktk Biblia yako, usije tu na kauli kama hizo za uongo, kwenye blogu ni semina za nje, watu wanayaheshimu Maandiko na si doctrines!

  Gbu my beloved brother in Christ!

 50. Sungura,

  Kwa bahati mbaya mchango wako huu wa mwisho nimeuona baada ya kutuma wangu, lakini hata hivyo kwa kuongezea niseme hivi, uelewa wako wa agizo la Yesu alilowapa mitume wake (Mt 10:1,7,8), utakuwa umebanwa katika wigo wa school of thought uliyonayo, ambayo iko limited kwenye tafsiri za mistari na si utendaji; kwahiyo unashindwa kulitanukia agizo hilo ktk mapana yake! Hiyo nguvu waliyopewa inaishikilia welfare yao yoooooooooote! Kama haulielewi hili, basi hakuna namna utayaelewa hata hayo mengine!!!

  Maelezo yako kuhusu 1Cor 9, haswa kifungu cha 18, mimi nilisema wazi kwamba hizo versions nyingine haziko sawa by themselves. Uungwana sio ku compromise Neno la Mungu!

  Tafsiri yako hii unayoitumia ktk mjadala,
  “”Mstari wa 18, anasema thawabu yake yeye ni kuihubiri injili bila kutoza gharama yoyote, na anafanya hivyo ili atimize lengo lake la kutokutumia haki zake zinazotokana na kuhubiri injili.””
  Inalingana na versions hizi mbili ambazo mimi sikuzitumia:
  -NIV: verse 18; What then is my reward? Just this: that in preaching the gospel I may offer it free of charge, and so not make use of my rights in preaching it.

  -English std version; verse 18 What then is my reward? That in my preaching I may present the gospel free of charge, so as not to make full use of my right in the gospel.

  Na ndio maana unaniambia:
  “”Unaona Lwembe, Paul alikataa kutumia hizo haki yeye kama yeye,wala haikuwa amri kwa kila mtu.
Ndio maana anasema mitume wengine walizitumia hizo haki.”

  Ndipo nikakuambia kuwa vifungu hivi by themselves haviko sawa contextually, kwa sababu neno FREE OF CHARGE haliendani na Haki ya kujikimu vya Injili, iwapo tutalichulia hivyo, basi ndio kusema wali CHARGE Injili walipojikimu kwa hivyo vya Injili! Jambo ambalo nikasema litayavuruga Maandiko yote, hata ninaamini mleta mada atakuwa ni muathirika wa mvurugiko huo!

  Bali nikasema KJV inajitosheleza katika maudhui, kifungu hiki kinajitosheleza katika maana yake chenyewe kuhusu ku Charge, ambako ndiko mnakokufanya, Sungura!
  “”18 What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, that I abuse not my power in the gospel.””

  Hivyo vifungu vingine vyote vinavyohusu Haki ya kujikimu, pamoja na maelezo yake, vimejengeka katika confusion ya hizo versions, na kama mlisema RM yupo kutuongoza, basi jaribuni kuvifuatilia hivyo vifungu mtaliona hilo, pia msisahau kuitumia vocabulary mliyojaliwa!

  Kulingana na tulivyolijadili jambo hili la KIINGILIO, kwa upande wangu sioni ni kwa jinsi gani naweza kuyavuka Maandiko ktk intructions zake, siwezi ku compromise hata yaliyo rahisi ktk lugha kwa kuyatafutia maana zisizo eleweka, kama KIINGILI kuwa sawa na CHANGIZO na SADAKA, ndipo tunalazimika kukubaliana kutofautiana katika jambo hili katika Upendo, ili ikiweko nafasi, basi Mungu atusaidie sote kuyajua Mapenzi yake katika hili!

  Pia niseme hivi, ni kweli kila mtu anayo Haki ya kuamini anacho kitaka katika namna anayoitaka, na kulingana na unachokiamini, ndicho kinachokutimilia!

  Nakushukuru Sungura, kwa fellowship!

  Gbu!

 51. Sungura,

  Baada ya kuyatolea maelezo malalamiko yako, ngoja nijaribu kuyajibu maswali yako ili twende sawa.

  Kuhusu jambo la wajibu, nadhani utakuwa hujaliangalia jambo ulilolisema katika mapana yake, nakunukuu:
  “Mimi Lwembe ‘I don’t care’, kama kuna kitu chenye kunifaa kinanenwa nitatoa chochote ninachoweza ili nikipate hicho. Sio wajibu wangu kujua kama anayekitoa Mungu alimwambia tunaokihitaji tutoe hicho kiasi cha pesa au thamani ambayo tumetoa…”
  Nilichokiandika kuhusu wajibu kinatokana na mtazamo niliouweka wazi tangu nilipoanza kuchangia ktk mjadala huu:
  “Basi kuweka kiingilio ni ishara kwamba kazi hiyo HUJATUMWA NA MWENYE KAZI! Mungu akikutuma ni LAZIMA akutangulie.”

  Kwahiyo, unaweza kuliona hilo kwamba mimi ninamhesabu mtumishi anayetoza kiingilio kuwa hajatumwa na Mungu, na wewe unaniambia you don’t care!

  Kuhusu Injili kutolewa bure, haya unayoyasema yanaonesha kwamba mawazo yako yana hama hama! Nilisema Injili inatolewa bure kwa sababu huo ndio ukweli wa Maandiko, vinginevyo basi Maandiko ndiyo yaliyochanganyikiwa!!

  Kuhusu samaki naona unajichanganya, mimi nimezungumzia watu waliolishwa sio walionyimwa! Ukitaka kujua habari ya walionyimwa, hao pia ninaweza nikakuonesha leo hii wako wapi, ila usilalame tu, bali watu walilishwa na HAWAKUTOZWA gharama ya samaki waliokula wala Injili au Semina, kwanini tusimfuate huyo anayeweza kutupa samaki na Uzima wa Milele BURE!! Walionyimwa ndio hao wanaotumia maarifa yao kujikimu kwa Viingilio!!!!

  Pia mimi sijakwepa kukupa jibu la swali uliloliuliza, nimekujibu zaidi ya mara mbili ila naona ulitaka nikujibu ktk jinsi unayoitaka wewe ambayo mimi naiona ni nje ya maudhui. Uwepo wa Mungu, ambao ndio hiyo “NGUVU” unayoikiri kwamba walipewa mitume, ndiyo iliyowatangulia katika miji waliyokwenda na kufanya kazi ndani ya hao waliowapokea. Ndio maana ninawashangaa mnapotaka kuvitenganisha hivi vitu viwili ambavyo viko ktk package moja, kwamba unataka kuniambia kuwa kumponya kipofu ni rahisi kwa Mungu kuliko kuniongoza mimi Lwembe kuchangia milioni kumi ili kuzigharamia semina atakazo zifanya Paulo katika makanisa ya vijiji vya Sumbawanga???

  Mungu anayajua yooote, pamoja na hizo semina zetu, tusilazimishe mambo!
  Zab 37:5
  “Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.”

  Gbu!

 52. Kaka Sungura,

  Mpendwa Lwembe anayo shahuku ya kupindukia. Hata akiwa jela pamoja na waongo wote, anaendelea na hila.

  Wewe sijue utamweka wapi? Pengine chini ya jela!!!! Lakini hivi ulichukua hatua ya kumhurumia, hebu tuone kama atajitambua. Nami nitafurahia hiyo hatuwa yake nzuri.

  Asante

 53. Lwembe,
  Ulitakiwa kujibu mambo ya msingi yanayohusu mada husika siyo kutoa nasaha, m mimi sizihitaji brother!

  Nimekuonesha maana ya alichosema Yesu ‘mmepata bure toeni bure’. Na iko wazi kiasi kwamba ungekuwa muungwana ungekiri kuwa ulikuwa hujakiona hicho kitu ndio maana hilo swali nilikuuliza zaidi ya mara tatu-nne ukawa unakwepa kulijibu.

  Nimefafanua pia maudhui yaliyo katika maneno ya Paul kwa habari ya kuhubiri kwake injili bila kumlemea mtu. (1cor 9)
  Kama unaona kwamba mimi ninavyoelewa si sawa na unavyoelewa wewe ndio sawa, hakuna haja ya kupeana nasaha wala kuzodoana, amini unavyoona wewe kuwa ni sawa na mimi nitaamini ninavyojua kuwa ni sawa.

  Maana mwisho wa siku huwajibiki kwangu wala siwajibiki kwako, bali kila mmoja kwa zamu yake anawajibika kwa anayeamini anamtumikia.

  Nafikiri huna hoja zaidi juu ya mada hii, ndio maana safari hii umeongea manenomaneno tu!

  Asante sana!

 54. Sungura,

  Hahahaha … you can’t be so MEAN with the Gospel!!

  Kuna jambo ambalo inakubidi ujifunze ili kusoma kwako Biblia, katika maana ya kuitafakari au kujifunza, likusaidie! Kwanza uamini kwamba HAKUNA jambo jipya hapa duniani wala huko mbinguni ambalo Mungu hakulijua. Yaani hata kujadili kwetu Neno lake tunakokufanya leo hii, Yeye alikujua kabla hata hatujazaliwa. Ndipo, kama alitujua, basi tunayo nafasi katika Neno lake, nasi tumo humo katika Biblia tukilitimiza Neno lake!!!! Efe 1:4
  “…kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.”

  Sasa, pia unapaswa kufahamu kwamba licha ya kwamba tunaweza kuwa tunafahamiana katika mwili, hata labda tukawa ni wa kusanyiko moja, bado tutakuwa tunafahamiana haya makasha yanayotubeba tu, mpaka tutakapofika katika kuzungumza, ndipo tutafanya contact kujuana huyu ni nani, zile roho!!!

  Hivyo basi, kwa kadiri tunavyojadili, huwa jambo la kwanza ninaloliangalia ni nafasi yangu katika jambo hilo, je, nimeujua Moyo wa Mungu katika hilo? Kwahiyo huwa naendelea katika mindset hiyo nikiyachukua na majibu ya wenzangu kuyapima humo ili kuweza kuzijua roho, maana wakati mwingine roho za dini hutudandia mawazo yetu na kujiwakilisha katika mazungumzo yetu: Mt 16:22
  “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani…”
  Basi katika hili utasemaje, kwamba Petro alikuwa Shetani? Hata wewe si yule Simon!!!

  Ndipo katika majadiliano yetu, nilipojihakikishia kwamba kwenu ninyi KUTOZA VIINGILIO ni sehemu ya maisha yenu ya wokovu, na kwamba sadaka au changizo kwenu vyote ni TOZO; nikarudi katika Maandiko kuitafuta roho hiyo ilimpagaa nani, FOR THE FUN OF IT!!! Hata mimi ninapochemka huwa napenda kurudi ktk Biblia nimtafute aliyechemka kama mimi, otherwise if you can’t find yourself in the Book, then you just DON’T EXIST!

  Basi katika Biblia nikawakuta watu wawili waliokuwa na akili ya kufanyia biashara vipawa walivyopewa, Balaamu nabii na Simon mchawi aliyeuacha uchawi wake na kubatizwa, hawa ndio walikuwa na hesabu za kutoza!

  Unaona, si suala la kumshambulia mtu, ni suala la reflection tu ya tunachokijadili, hukupaswa kulichukulia hilo kwamba nilikulenga wewe, hatumjadili mtu bali views zetu on the subject katika reflection ya Maandiko, and if we trace the spirits from Genesis right thru Rev, we can’t miss them, not the people, they are all dead!

  Pia, pamoja na humor, ninafahamu kwamba kila ninaloliandika/sema nitalitolea hesabu, kwa hiyo Iam dead sincere abt wht I speak or write!

  Nimewaona wapendwa wengi huwa wana mawazo kama yako, lakini ni ule unafiki tu unao watawala! Utaona mtu anakulalamikia kuwa unaandika sana, the next thing you know, ameandika mara mbili yako and they don’t know it!! Au anakuambia kuwa wewe una ushetani, halafu mnapolitafakari hilo alilokuambia, akiona linamrudia, anageuka, anakuambia utayatolea hesabu unayoyasema!! Why so, kwasababu wengi wetu hatujaukulia wokovu invyopaswa, tumebeba mafurushi ya doctrines ambazo tunaamini ndilo Neno la Mungu, unapooneshwa tofauti, unashindwa kustahimili, unaanza kusaga meno kwa hasira na kulalamika kwingi!!!

  Sikiliza Sungura, “Good News” can’t be bitter; it is, only when it is tearing you apart to implant the Eternal Life into your precious soul, so bear it for a while!!!

  Gbu!

 55. Lwembe,
  Na kama wewe ni mwanafunzi mzuri wa biblia utagundua kuwa anachokisema Paul katika ile 1Cor 9, utagundua kiko tofauti kimaudhui na alichosema Yesu kwa habari ya kupokea bure na kutoa bure.

  Wala haihitaji kufunga na kuomba ili kuelewa anachokisema Paul, kama mtu unajua vizuri fasihi andishi inavyohusisha na kuunganisha matukio. Paul hakulisema hili suala la yeye kuhubiri injili bila mtu mwingine kuigharamia kama rejea ya maneno ya Yesu ya mmepata bure toeni bure. Ndio maana katika ile mistari ya juu amesema kuwa mitume wengine wao walikuwa wanatunzwa kutoka kwenye injili.

  Yesu aliongelea habari ya nguvu ya Mungu inayotenda kazi ndani ya anayehubiri ( yaani inayoponya wagonjwa, kufufua wafu, kutoa mapepo, n.k).
  Na Paul anaongelea habari ya mahitaji ya mwilini anayohitaji huyu anayehubiri hiyo injili( kusafiri, kula/kunywa, kulala, n.k)

  Ni mambo mawili tofauti kabisa yanayosemwa hapa.

  Yote anayoyasema Paul hapa yanatokana na watu fulani kumshambulia kwa habari ya huduma yake.
  Hivyo anajaribu kuwa-challenge kwa kuwauliza kama wanadhani yeye siyo mtume, au kama yeye hakumwona Yesu katika mwili.
  Na anawauliza kama yeye na Barnaba hawana haki ya kupata haki(za kula na kunywa n.k kutokana na kuinjilisha kwao) za kitumishi kama wale mitume wengine.

  Sasa uhusiano wa mstari wa 16-18 na ile mistari ya juu ni kwamba, katika hiyo mistari ya 16-18 Paul anaeleza kile ambacho kimemfanya yeye aamua kutokula na kunywa kunakotoka kwenye injili( Kuhubiri injili free of charge), tofauti na mitume wengine walivyokuwa wanafanya (yaani walivyokuwa wanakula na kunywa kutoka kwenye injili-ambako kimsingi ni haki yao kufanya hivyo).

  Sababu yenyewe ni kwamba Paul alifika sehemu kwake kuhubiri injili ikawa kama lazima(amri) ambayo amawekewa na Mungu. Ndio maana anajiambia ni ole wake kama hataihubiri injili.

  Wala Paul hakusema kuwa mitume wanaozitumia zile haki za kuishi kutokana na injili wanafanya makosa,wala hakusema kuwa na wao wafanye kama yeye alivyokuwa anafanya.

  Kwa hiyo kumlazimisha kila mtu ahubiri injili kwa mfumo kama wa Paul, wa kutokula,kunywa ,kusafiri, kulala, n.k, ni kuwafanya hao watumishi wavae viatu ambavyo si saizi yao,au wanywee kikombe ambacho hawajaitwa kukinywea.

  Na kama unataka tumfuate Paul kwa dhana hiyo, basi tusioe pia, maana yeye hakuoa na akashauri tusioe pia.

  Tujadili!

 56. Kaka Sungura,

  Pole sana na asante kumhurumia ndugu yangu Lwembe hata kam yeye haoni ile. Unampakaa malashi rafiki yangu: unasema anajua lugha? Anajua tu andika! Angelijua lugha kama anajuaga kile akiandikacho. Tena umemusaidia ukajibu wewe pekee kwa swali aliloshindwa kujibu. Tungoje, labda atasema “asante”. Jipe moyo kaka, labda atakengeuka.

  Ubarikiwe

 57. Kuna tu maneno tudogo tunashindaga watu wengi: “Sorry”, “samahani”, “sina ufahamu”, “unipe shauri”,”nitauliza kwanza”,”asante”, “nilikosa”, “sitaongeza na Mungu aniwezeshe”, nk.
  Hah!!!! kumbe kukamilika ni process kubwa!

 58. Lwembe,
  Acha kunishambulia mimi, bali chambua maandiko ili kupata ukweli wa tunachojadili hapa.
  Unaponifanisha na Simon mchawi, ni kukosa staha kwa mtu mliyetofautiana mtazamo. misho wa siku ‘we are all christians bought by blood of the lamb’.

  Wewe huwa ukisongwa kwa hoja unaanza kushambulia mtu.Mimi nimeokoka, sina mfanano wowote na Simon mchawi. Kumbuka maneno yasiyomaana kama hayo mwisho wa siku kuna kuyatolea hesabu. Hata hivyo nimekusamehe bure brothe,r hata kama hutaniambia samahani.

  Kuna maneno ulisema hapa, nakunukuu;
  ”..na pia huna wajibu wa kujua anayekuletea chakula hicho anatoka kwa Mungu au kokote kule, isipokuwa wajibu wako ni kupokea ulicholetewa..”

  Sasa linganisha na nilichosema mimi;
  ”.. Sio wajibu wangu kujua kama anayekitoa Mungu alimwambia tunaokihitaji tutoe hicho kiasi cha pesa au thamani ambayo tumetoa”

  Je nilisema sina wajibu wa kujua anayeniletea chakula kama ametoka kwa Mungu, au nilisema sina wajibu wa kujua kama Mungu alimwambia tutoe hicho kiasi cha pesa(kiingilio)? Hebu soma vizuri katikati ya hiyo mistari.
  Mpaka hapo jibu unalo bila shaka. Nachukulia tu kwamba ulipitiwa. Hapa napo nakusamehe bure.

  Lwembe ukihojiana na mtu asiyejua unaweza kumfanya mateka akadhani unachokisema kiko sahihi, kumbe ni maneno na lugha nzuri tu. Na hapo ndipo hufika wakati nikasema kuwa wewe umejaliwa uwezo wa kuandika na uwezo mzuri wa matumizi ya lugha basi.

  Tatizo siyo kujua biblia imeandika nini, bali ni kujua hicho kilichoandikwa kina maana gani. Wewe unajua sana biblia imeandika nini, lakini unakwama sana kwenye kujua sawasawa hicho ilichokiandika kina maana gani.

  Kama unajua kuwa injili inatolewa bure kwa nini ulisema kuwa hakuna cha bure? Au umechanganyikiwa kiasi cha kujichanganya hata wewe mwenyewe?

  Ndio maana nikakwambia useme kinachotakiwa kutolewa bure ni nini, umeshindwa kusema badala yake unaleta fasihi nyingii.

  Ule mfano wa samaki unayajua matokeo yake? Maana inaonekana nawe unawaza kama mmoja wa hao waliokula wale samaki na mkate na wakadhani ni wajibu wa Yesu kuwapa samaki na mikate.
  Ndipo walipovuka ile ng’ambo ya pili kumfuata Yesu wakitegemea kuwa ni wajibu wake kuwapa mikate bure wakakuta story tofauti. Aliwanyima mikata na akawapa makavu, akiwaambia hawajamfuata kwa sababu ya neno bali mikate.

  Alichokuwa anawajibika Yesu kuwapa bure ni neno la Mungu, uponyaji, utakaso n.k. Mikate ilikuwa ni wajibu wao kuilipia, kwa vile hapakuwa na namna ya wao kupata mikate hata kama hela walikuwa nazo, kwa vile pale ilikuwa ni jangwani, ndipo Yesu ikabidi afanye muujiza.
  Na hayo matukio mawili ya samaki na mikate ilikuwa ni kwa sababu maalum, ndio maana yanaitwa muujiza.

  Na hiki ndicho ulichokuwa unakwepa kujibu kuhusu kupewa bure na kutoa bure, kwamba tulichokipewa bure siyo ile pesa ya kugharamia ukumbi wa semina, gharama za umeme, gharama za vyombo, nauli kwa watakaohudumia hiyo semina, shooting, n.k. Bali ni ile NGUVU ya kufukuza roho chafu,kuponya magonjwa na maradhi yote, kutakasa wakoma, kufufua wafu,..

  Ndiposa biblia inasema ” Mt 1o:1 And when he had called unto him his twelve disciples, HE GAVE THEM POWER against unclean spirits, to cast them out, and to heal all manner of sickness and all manner of disease
…


  7 And as ye go, preach, saying, The kingdom of heaven is at hand.

  8 Heal the sick, cleanse the lepers, raise the dead, cast out devils:FREELY YOU HAVE RECEIVED, FREELY GIVE!”(nimwek herufi kubwa kukazia point tu)

  Gharama za kuandaa semina hazimo kwenye hicho kilichotolewa bure, na wala biblia haisemi kuwa ukitaka kupeleka injili utasubiri Bwana atende muujiza. Unatakiwa uwe na pesa mwenyewe au uweke mipango ya kupata hiyo pesa ili semina ifanyike.

  Tunaendelea kujadili!

 59. Sam,

  Nilipokuambia ninasubiri ushahidi wa kiMaandiko kuhusu KIINGILIO, jibu lako la kiMaandiko la jambo hilo, ulilonipa ninaamini ndilo hili hapa:
  ““”..hebu basi ww utupe ushahidi wa kimaandiko (neno kwa neno bila kutafsirisha) wa wewe kupiga mswaki, kuvaa raba&mokasi, kuwa na simu ya mkononi, kuangalia tv, etc””!!!!
  Sasa kwa vile ulisema unayo hekima na unafundishwa na RM, nikajua hilo jibu umelitoa kwake, ndio maana nikabaki katika mshangao!!!

  Lakini, kumbe ulikuwa nawe unaniuliza swali ili jibu nitakalokupa likusaidie kujua Kiingilio kimefundishwa wapi katika Maandiko; basi kukusaidia kirahisi usipoteze muda wako kutafuta katika Maandiko jambo ambalo HALIMO, ni sawa na kumtafuta nyoka wa jangwani Antarctica!

  Kwamba unataka ushahidi wa ki Maandiko wa mimi kupiga mswaki, au unauliza ni wapi Maandiko yamenifundisha umuhimu wa kupiga mswaki? Kama unauliza ni wapi nilipofundishwa, kama utaridhika, basi shina la kupiga kwangu mswaki liko katika ule UJUZI wa Mema na Mabaya nilioushiriki, Mwa 2:17 “…walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, …”

  Kama hujaridhika na jibu hilo, basi chukua hili ambalo linajibu mpaka swali nililokuuliza; ni kwamba ushahidi wa neno kwa neno wa ki Maandiko wa mimi kupiga mswaki SINA, ila ukiamini basi nimeyajua hayo kwa MAFUNUO, kama ambavyo nanyi mnatoza KIINGILIO kwa mafunuo ambayo wewe ulidhani ni Hekima itokanayo na RM!!!!

  Gbu!

 60. Ndugu Joseph,

  Uko mkweli kwa hofu kufwatana na yale uliyoyasoma. Lakini kanisa nzuri ni ile imani yako(roho yako). Ukifwatilia kanisa kama jengo ni hatari. Mim niliwai kuona kanisa iliyoanza kinyumenyume ya ile unayohofia. Mchungaji alijenga kanisa kwa msaada wa nje. Kanisa kama jengo iikajengeka vizuri sana lakini bila “waumini”. Ndipo akaanza propaganda ya kulipa hela kila anaeingia ndani ya ibada. Hapo akapata watu wengi. Baadaye hakulipa tena. Alianzatumika kam ingine makanisa. Kwa leo kanisa ingali, watu walioanza wengi walitoka, lakini wako wengine wengi walioamini baadae na wanaendelea. Hata leo alieanzisha ingawa angali pale, si yeye ndiye mchungaji.

  Hence, mambo tofauti usiyoweza elewa yanatendeka ndani ya makanisa mengi. Au ni “waumini” wanaoshurtishwa kulipa, au ni “wachungaji” wanaolipa “waumini”. Lakini kinachoendeka nyuma, RM anapoingilia kati wakati anapotaka mharibifu anakimbia.

  Si kila kitu kionekanacho mbele ya macho ya wanaadamu kama kizuri, ni kizuri mbele za Mungu. Mimi ningependa tuache critics. Huezi kudai una RM kiisha ushinde ukisemasema vibaya karibu watumishi wote wa Mungu. Unawezaonya kwa upole na mengine unamuachia Mungu. Tena Mungu wetu ni mkuu na hanyanyasike, wala haombi msaada wa mwanaadamu.

  Kwa hali ya semina na kiingilio, hilo ni jambo tofauti. Wanaoalikwa zaidi ni wale waliookoka, huko hawabatizi, na exceptions zinazopatikana (maumini wapya) wanaelekezwa ndani ya makanisa watakayochagua wawo wenyewe. Ina maana Semina na kanisa inatumia mfumo tofauti. Semina inaonekana kuwa ni ushirika wa waliookoka wanaokubali kuchanga sawasawa ili matukio iwe kwamba wanaelimishana zaidi na kizuri zaidi wanasaidia makanisa kufikisha neno mahali kanisa isingelifika, na mengine kam “kutafutia” makanisa waumini wapya. Inayomaanisha kanisa haliwezi kamata mfumo wa semina.

  Acha niweke shairi kidogo inayohusu sisi sote wana SG:

  “Mithali 14:12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.”
  “Mithali 16:2 Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu.”
  “Mithali 16:9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.”

  Kwa upande wangu, inabidi tuombe sana. Kuna mambo Mungu anafunulia watu, yule asiyeomba anawaza ni wendawazimu kwani kwake anaona haiwezekane.

  Jesus Christ bless you.

 61. Ndugu Tumaini,

  Siwezi puuzi ombi lako. Sorry kabisa. Nilipoona jinsi uliandika na jinsi tulivyoandika, sikuona swali katika maandiko yako kwani niliona ni kama maoni yako na mambo unayoweza soma nafasi nyingi ktk hii mjadala ambayo nami nilisisitiza kwa kusema kuna namna nyingi za utoaji, iwe ni kiingilio , iwe changizo, iwe sadaka ya kawaida, sadaka ya injili, sadaka ya majengo, zaka, nk. Ina maana kiingilio hua inatumika inapohitajika, na sadaka nyinine hali kadhalika. Hii kiingilio si kawaida kabisa na lengo lake si la kawaida, kufwatana na kazi inayofanya hata mafundisho yaweze kufika ndani ya nchi nyingine. Lakini, ndugu yangu, huezi weka kiingilio ndani ya Ibada ya juma pili. Isipokua pengine RM apane mipangilio ingine, ninachojua ni kwamba kiingilio kinasemeka tu ktk semina. Naweka hapa chini ulioniandikia kwa sababu tulikuwa tumekwisha fika mbali.
  Ninayo shauri kwako ni kwamba, uwekapo hoja, inaomba iwe clear kwamba ni swali kabisa, isionekane kama unajiswali binafsi, ao kwamba hata mtu mwengine anapoizungumzia si lazma ulieandikia airudilie tena.

  “Ndugu Ziragora cwezi kuwa vuguvugu ndugu na cpo hapa S.G kwaajili ya kuogopa awaye yoyote bt namheshimu kila mmoja na naheshimu wazo la kila mmoja so hiyo dhana yako ya kusema kuna point nimechangia kwa uoga imenishangaza sana coz nipo free 100% nikijua tupo hapa kwa nia njema kabisa ya kuelimishana hofu yangu ingekuwa kubwa sana kama niya yetu ingekuwa kutukanana kwakweli hapo ningehofu sana kumkosea MUNGU kwa hilo na wala nicngeweza kushiriki!Swala la kiingilio kuwa kama ni kanuni moja hapo ndiyo napata tabu kuwa MUNGU ni wa kanuni moja?inamaana leo hata wewe akikupa maono ili yatimie ni lazima kiingilio kionekane ndiyo njia peke ya kufanikisha maono hayo?MUNGU WETU NI WA NAMNA HIYO?hebu tuelimishane ndugu yangu!maana nahitaji kujua zaidi na zaidi!ili huu utata naoupata uondoke!NITABARIKIWA SANA NDUGU YANGU.”

  Ahsante sana ndugu Tumaini. Kama ungali na swali usichoke.

 62. CK Lwembe ulisema “Ninasubiri ushahidi wa KIINGILIO wa ki Maandiko!”

  ndio nami nikakuuliza “”..hebu basi ww utupe ushahidi wa kimaandiko (neno kwa neno bila kutafsirisha) wa wewe kupiga mswaki, kuvaa raba&mokasi, kuwa na simu ya mkononi, kuangalia tv, etc””

  …badala ya kunipa jibu la kimaandiko ukarukia mambo mengine….tafadhali naomba ushahidi wa kimaandiko wa swali langu!

  sam

 63. Wapendwa watoto MUNGU LWEMBE,SUNGURA,ZIRAGORA,HAULE,SAM na wana S.G woote naomba niseme hivi! mada hii ni nzuri na kama tukiwa fair kabisa pasipo kuweka itikadi zetu,misimamo yetu binafc na TUKASIMAMA NA NENO LA MUNGU NA TUKAOMBA UONGOZI WA RM KWAKWELI TUTAPATA VITU VIZURI VITAKAVYOTUSAIDIA SAANA KIROHO TENA SANA!BINAFC NATAKA NIPATE JIBU CLEAR KABISA KUHUSU KIINGILIO KUNA SWALI NIMELIULIZA KWA BR SUNGURA NA ZIRAGORA CJAJIBIWA NINGEBARIKIWA SAANA KAMA NINGEJIBIWA!then con sababu saana ya kupeana maneno maguumu ambayo yatatutoa kwenye uwepo wa MUNGU!yaana badala ya kujibiana hoja kwa kufuata hekima ya RM badala yake tutaenda kimwili zaidi!kuna cku nilishawahi kusema hakuna fundi wa neno la MUNGU bt RM pekee ndiye anayetufundisha!thn lazima tufahamu wote tupo kujifunza haijalishi nani ni mkongwe na nani ni kinda!coz neno la MUNGU NI JIPYA KILA CKU IITWAPO LEO!HEBU TUWE WANYENYEKEVU WAPENDWA NA TUACHE MAJIVUNO NA MIPASHO ICYO NA MSINGI!HIVI MPENDWA ALIYEOKOKA JANA ATAJIFUNZA NINI AKIONA COMENT ZETU?.GB ALL.

 64. 2 Corinthians 9:6-7 ” 6 But this I say: He who sows sparingly will also reap sparingly, and he who sows bountifully will also reap bountifully. 7 So let each one give as he purposes in his heart, not grudgingly or of necessity; for God loves a cheerful giver. ”

  Namshukuru Mungu leo nimekutana na kitu ambacho nilikuwa sijui kama kipo duniani…nasi tuangalie tusije tukafika huko…naomba msome link hizi (nimeona hiki kitu kwa mara ya kwanza leo)

  http://en.wikipedia.org/wiki/Church_tax

  http://en.mercopress.com/2013/10/23/german-catholics-can-only-remain-in-the-church-if-they-pay-membership-tax-rules-court

  Mi sina cha kuongeza kwenye hii mada…Mungu awe nanyi wote katika kujadili kwa nia ya kujifunza.

  Asanteni.

  “German Catholics can only remain in the Church if they pay membership tax, rules court
  Germany’s Roman Catholics can only remain part of the Church if they pay a membership tax, a court has ruled. All Germans who are officially registered as Catholics, Protestants or Jews pay a religious tax, worth an extra 8-9% of their income tax bill.

  by a retired law professor who said he wanted to remain a Catholic but not pay the tax. Last week, a new bishops’ decree warned that anyone not paying the tax would be denied the right to religious rites. The German church levy was introduced in 1803 in compensation for the nationalization of religious property.
  In 2011, the Catholic Church received 5bn Euros and the Protestant Church 4.5bn Euros from taxpayers, each adding up to the bulk of the churches’ income, the BBC’s Berlin correspondent Stephen Evans said.
  He added that this arrangement, whereby the state collects taxes on behalf of religious groups and then reimburses them, was unusual in Western secular societies.
  Hartmut Zapp, a retired professor of church law, filed a legal challenge in 2007, arguing that under Catholic doctrine, Church membership was determined by a person’s beliefs and not by a financial relationship. The Freiburg University academic said he wanted to continue praying and receiving Holy Communion without paying the religious levy.
  Judges at the Leipzig Federal Administrative Court, however, disagreed with Prof Zapp and ruled that there could not be partial Church membership. Their verdict follows a new bishops’ decree issued last week, according to which anyone failing to pay the tax will no longer have the right to Holy Communion and religious burial.
  Already alarmed by declining congregation numbers, the bishops were also pushed into action by Mr Zapp’s legal challenge. They said refusal to pay Church tax should be seen as a serious act against the community.
  Catholics make up around 30% of Germany’s population but the number of congregants leaving the church swelled to 181,000 in 2010, with the increase blamed on revelations of sexual abuse by German priests.
  “This decree makes clear that one cannot partly leave the Church,” Germany’s bishops’ conference said last week, in a decision endorsed by the Vatican.
  Unless they pay the religious tax, Catholics will no longer be allowed receive sacraments, except before death, or work in the church and its schools or hospitals.
  Without a “sign of repentance before death, a religious burial can be refused”, the decree states. Opting out of the tax would also bar people from acting as godparents to Catholic children.
  “This decree at this moment of time is really the wrong signal by the German bishops who know that the Catholic church is in a deep crisis,” said Christian Weisner from the grassroots Catholic campaign group We Are Church.
  But a priest from Mannheim in south-western Germany, Father Lukas Glocker, said the tax was used to do essential good works.
  “With kindergarten, with homes for elderly or unemployed, we’ve got really good things so I know we need the tax to help the German country to do good things.”
  While the decree severely limits active participation in the German Catholic Church, it does hold out some hope for anyone considering a return to the fold.
  Until now, any German Catholic who stopped payment faced eventual excommunication. Although the measures laid out in the decree are similar to excommunication from the church, German observers say the word is carefully avoided in the decree”

 65. Sungura,

  Tazama, katika maelezo yangu nilisema hivi Mungu hawezi kushiriki ku ABUSE Neno lake, hii ni kulingana na 1Kor 9:18 “What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, that I abuse not my power in the gospel.” Ambavyo ninafahamu kwamba hayo ni AMRI! Kwahiyo simtegemei Mungu ku improve, kwamba ilipofika katika nyakati za akina Sungura, Mungu akatambua kwamba kuweka Viingilio ni muhimu!!!

  Kuhusu suala la samaki wawili na hiyo mikate mitano, Mt 15:34 “…Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.” Wakaitoa kwa ajili ya makutano. Pia, mimi nilidhani unafahamu kwamba maisha ya mkristo yamejaa miujiza, hivyo kuwa sehemu ya maisha ya mkristo, kwamba hulijui jambo hili, haisikitishi sana, bali ninaamini ukikua utayajua hayo! Na ukiyasoma Maandiko niliyokunukulia, utamuona Yesu akiliitisha changizo hilo!!

  Na kuhusu, Changizo, Sadaka na Kiingilio kwamba vyote ni KUTOZA, kwa hili labda nikubaliane kutofautiana na wewe, kwani sioni ni kwa jinsi gani nitakueleza ili ufike katika kuelewa maneno mepesi ya kiswahili kama haya! Kwa kuikosa maana ya maneno hayo, ni dhahiri hutaweza kulielewa jambo hili, no wonder Changizo, Sadaka na Kiingilio mnayaona ni jambo moja, mpaka mnang’ang’aniza kuwa Paulo alitoza Injili!!!

  Jambo la kwamba wewe you ‘don’t care’ na pia huna wajibu wa kujua anayekuletea chakula hicho anatoka kwa Mungu au kokote kule, isipokuwa wajibu wako ni kupokea ulicholetewa, hilo ni sawa, hata mawazo yako yana reflect hilo!!

  Kuhusu wewe kutokuamini, najua huwezi kulikubali hilo kirahisi kwa sababu wewe unaamini kwamba unaamini, lakini ungekuwa ni mwenye kuamini basi ungeamini kwa urahisi na kufahamu kwamba Injili HAITOZWI, maana kule kutokuamini kwako kumeiondoa hata maana ya maneno rahisi moyoni mwako na kukuachia maana moja tu kwa maneno yote, ili upate KUTOZA Kiingilio ambacho unakiita ni Sadaka/Changizo; jambo ambalo linauvuruga mpangilio mzima wa Injili, likiuondoa Upendo na Shukurani uwanjani na kusimika PESA/MALI unazoweza kulipia Vipawa vya Mungu, sijui mtu wa jinsi hiyo ana tofauti gani na yule Simon aliyetaka kununua Vipawa!!!

  Kuhusu 1Cor 9:18, utakuwa hukuyaangalia vizuri majibu yangu niliyovifuatisha vifungu hivyo ulivyovileta. Nilikuonesha kwamba maelezo yaliyoanzia kifungu cha 13 yanaishia kifungu cha 15, akielezea juu ya Haki yake ya kula vya Injili kama watumishi wengine, kama hao akina Petro, na akamaliza kwa kusema yeye hajatumia haki hizo na hana mpango nazo!

  Kifungu cha 16 anaanza habari nyingine ihusuyo kazi ya kuihubiri Injili, akijigamba kuhusu hiyo na wajibu alio wekewa. Maelezo hayo anaendelea nayo verse 17, sasa akiingiza suala la Thawabu kwa kazi hiyo ya kuhubiri Injili. Sidhani kama THAWABU na HAKI yana maana sawa, labda kwa tafsiri zenu na Ziragora za kulazimisha! Lakini kwa mtu asiyejichanganya ni tofauti, Thawabu anayo mtoa Thawabu! Najua mnapata tabu kuelewa anachokisema Paul kutokana na mindset zenu kukaa “ki kula kula” pesa tu! Kwahiyo aliposema “without charge” mkajua ni zile Haki alizozizungumzia ktk verse13-15, and you completely missed the point!

  Mambo madogo ya changizo na sadaka na haki ya kujikimu vya Injili alimalizia kifungu cha 15, kuanzia verse 16 hadi hiyo 18 ni “Deep things of God” anazungumzia Kuihubiri Injili na Thawabu yake na si Haki ya kula pesa. Kinyume cha Thawabu ni Laana, sijui kwa tafsiri zenu, kwamba kuna Thawabu uki Abuse?

  Sasa hivi nimeanza kuhisi kwamba huenda tunajadili katika frequency tofauti sana! Hebu angalia hiki ulichokiandika:
  “”Ngoja niiseme hivi; Kama mamlaka anayokataa Paul kuyanajisi ni kule kuhubiri injili bure, basi wale mitume wengine (pamoja na Petro) waliyanajisi.”

  Halafu fanananisha na hiki nilichokisema kuhusu Paul (verse 18):
  “”Ndipo, akiwa ni mtu mwenye mamlaka ya Injili, hiyo inayopaswa kutolewa bure, basi akigeuka AKAWATOZA kwa ajili hiyo, jambo ambalo katika MAMLAKA aliyonayo angeweza kulifanya, labda akawaambia kila mtu alipie dola mia ili apate Wokovu, na wangelipa; kama Katoliki nao kwa mamlaka ya injili walivyowatoza watu viwango vya pesa kwa ajili ya indulgence; HUKU ndiko KUINAJISI mamlaka, lile Neno la Mungu!!!””
  Ni vitu viwili tofauti kabisa!!!

  Kuhusu kilichotolewa bure, nimeandika na kunukuu Maandiko zaidi ya mara mbili nikitegemea kuwa utaliona hilo, au mpaka tuitishe semina tuwatoze kila mtu laki unusu ndio mtatia akili?!! Ili chochote kile uwe UMEPEWA bila malipo, yaani BURE, ni LAZIMA awepo aliyekilipia ili wewe upewe bure! Na wewe uliyekipokea kitu hicho bila ya malipo una wajibu wa kukaa katika makubaliano ya kukipokea kwako bure kitu hicho ambayo katika hili tunalolizungumzia, sharti la kukipokea Bure ni kwa wewe nawe kukitoa Bure! Sina namna ya kulielezea hili unaloliuliza, zaidi ya yanavyojieleza Maandiko kuhusu hilo. Ngoja nikunukulie tena:
  Mt 10:
  
“1 And when he had called unto him his twelve disciples, he gave them power against unclean spirits, to cast them out, and to heal all manner of sickness and all manner of disease
…


  7 And as ye go, preach, saying, The kingdom of heaven is at hand.

  8 Heal the sick, cleanse the lepers, raise the dead, cast out devils: freely ye have received, freely give.”

  Halafu badala ya kupasuana vichwa, jaribu kuyaangalia maagizo yote yanayohusu kuihubiri Injili kama kuna TOZO lolote lililoambatanishwa, na kama unaona Sadaka ni tozo, sioni ni kwa vipi unakimbia kulipa Tozo la Zaka ambalo liko very specific kama KIINGILIO!

  Gbu!

 66. Sam,

  Unajua, kuna mizaha ambayo huwa tunaiendekeza mpaka tunaizoelea na kuiona ni kweli, kwa kule kujipumbaza kwetu kwa mizaha hiyo! Hebu lifikirie jambo hili, kwamba unatoka huko kwenye semina inayotoza kiingilio kinyume na Maandiko, halafu unasema eti “tuliambiwa RM atatufundisha yote”! Ni wapi mlipoambiwa kuwa RM atawafundisheni kuyakanyaga Maandiko yake? au mnasikiaga tu mtaani wakisema RM nanyi mmejiunga katika mzaha huo? RM ni Neno la Mungu, Yn 6:63
  “… maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Huwezi ukawa unalikanyaga Neno la Mungu, yaani ukawa kama nguruwe waliotupiwa lulu za thamani, halafu ukasema eti RM anakuongoza!

  RM hukuongoza kuliamini na kulithamini Neno la Mungu. Kama Paulo anasema ameihubiri Injili bila kutoza gharama, huyo ambaye amewekwa kuwa mwalimu kwetu watu wa Mataifa, tena akatuambia tumfuate yeye, basi sisi tunapotoza viingilio tunakuwa tumemfuata nani? Kama Paulo aliyanena aliyoyanena kwa RM, Mt 10:20 “Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”; basi usipoyatii hayo aliyoyanena, unatofauti gani na mpagani asiyeamini? Unaweza ukawa katika emotional frenzy, labda ukadanganyika kuwa umempata RM, lakini matunda yako yangekuonesha kuwa si kweli maana kutoza kwako viingilio ni ishara ya kutokuamini kwako, Yn 6:64 “Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini.”!!!

  Neno Mwili wa Kristo, haliishii katika namna ya kuhudhuria ibada na kuinjilisha au kushughulika ktk makusanyiko yetu, bali ni mjumuiko wa waaminio ambao Mungu huishi katikati yao. Hivyo hao huongozwa na uwepo wa Mungu, lile Neno lililojaa kwa wingi ndani yao. Hawa kunapokuwa na jambo lolote linalohusiana na Ufalme, Mungu huinua vipawa kati yao kwa ajili hiyo, Kut 35:30-35
  “Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; na kuvumbua kazi za werevu…” unaona, hata ikiwa ni semina, Mungu akihusika basi yote huwekwa sawa na si mambo ya kutumia hekima zetu, na kumlazimisha Mungu aliache Neno lake atufuate sisi!!!

  Tufikeni sehemu tuache kuheshimiana sisi kwa sisi kuliko tunavyomheshimu Mungu!

  Gbu!

 67. Ok, Lwembe.

  Unaposema kusiwe na tozo ili Mungu ahusike na hiyo semina una maanisha nini? Hasa hilo neno ‘Mungu kuhusika’.

  Unaposema suala la samaki watano, elewa unaongelea kitu kinachoitwa muujiza. Maana yake unataka kusiwe na kujiandaa, bali tukae tu tukingoja Mungu kutenda muujiza.
  Basi kama ni hivyo kuna sababu ya kujifunza kwa nini muujiza huwa unatokea.

  Halafu kwa nini hao samaki wawili unaliita CHANGIZO, nani alifanya hilo changizo?

  Lwembe kama hapa umesema hivi; Pia, unapaswa kuelewa kwamba HAKUNA KITU CHA BURE (japo hicho nilishakisema mapemaa),
  Halafu hapa tena ukasema hivi;
  ”- Kufanya changizo kwa ajili ya semina SI kutoza pesa.

  -Kuweka viingilio kwa ajili ya semina NI kutoza pesa.

  -Kukusanya sadaka kwa ajili ya semina SI kutoza pesa.”

  Basi jibu la hapo ni jepesi kwamba haujui unachokisema, ila umekisema tu vivi hivi.

  Mimi Lwembe ‘I don’t care’, kama kuna kitu chenye kunifaa kinanenwa nitatoa chochote ninachoweza ili nikipate hicho. Sio wajibu wangu kujua kama anayekitoa Mungu alimwambia tunaokihitaji tutoe hicho kiasi cha pesa au thamani ambayo tumetoa. Yeye ndiye mwenye kuwajibika kwa Mungu wake wala si mimi, mimi wajibu wangu ni kuhakikisha nakipata hicho.

  Kumbuka ninachokwenda kukipata katika hiyo semina kinaitwa ufalme wa Mungu. Na mwenye hekima hutoa chochote anachoweza ili aupate huo ufalme.

  ”Sungura Ingawa ninyi hamuamini kwamba Huduma ya Kristo kwa ukamilifu wake, iliendelea katika mitume wake….” Haya ni mamneno yako Lwembe. Ndio aina hii ya maneno ambayo mimi huyaita yaliyojaa hila.

  Unataka kuwaaminsha watu kuwa Sungura haamini kuwa huduma ya Yesu iliendelea ndani ya mitume? Hebu acha mzaha rafiki yangu!

  Waala, hujanijibu swali langu la mwanzo Lwembe, ulichokifanya ni kupiga brabra basi. Please nijibu; ni nini hicho kilichotolewa bure?
  Kimbuka wewe mwenyewe umesema hapo juu kuwa hakuna kitu cha bure.

  Hakuna nilichokosea katika kufafanua mstari wa 1cor 9:18. Wewe ndiye unayepindisha hiyo fafanuzi, maana unachokifanya ni kukomea tu kutafsiri kutoka kizungu kwenda Kiswahili. husemi kilichomaanishwa katika hayo maneno.

  Ngoja niiseme hivi; Kama mamlaka anayokataa Paul kuyanajisi ni kule kuhubiri injili bure, basi wale mitume wengine(pamoja na Petro) waliyanajisi.

  Soma hapa; 1cor 9:4 Don’t we have the right to food and drink? 5 Don’t we have the right to take a believing wife along with us, as do the other apostles and the Lord’s brothers and Cephas? (NIV)

  Lwembe kama hukijui au hutaki kukijua kilichosemwa tukitoe bure maana tumekipewa bure, utapiga sana kelele hapa.

  Tuendelee!

 68. Ndugu Joseph,

  Pia nataka kukwambia kam kwa mtazamo wangu iwe semina ya kiingilio au changizo(sadaka) ndani ya makanisa, neno la Mungu linapewa bure. Kinachogaramiwa ni jengo, usafirishaji na vyombo vingine. Kwani neno la Mungu ni uzima ambao huna bei.

  Asante.

 69. Ndugu Joseph,

  Sijue kam labda hukusoma inayozungmuzia tangu mwanzo.
  Hapa hatuongelee sadaka ya kawaida kam ndani ya makanisa. Tunaongea semina. Nadhani unafahamu kam kanisani humo wana sadaka za aina mbalimbali, zaka nayo ikiwa humo humo.
  Semina si mkutano wa kawaida, inaandaliwa sana. Mara nyingi walimu wa semina si wachungaji wanaotumia makanisa zawo jinsi wanavyopenda.
  Sasa tuseme semina ingoje watakaoguswa ndani ha hiyo semina ndipo ianze, itaanzaje?
  Kitu ingine kuwa mtu haingie ndani ya semina haimaanishe kam hatapata ile maneno ya Mungu. Baadhi ya walimu wengi wanarikodi kanda na kuipeperusha kwenye radio kwa upako huohuo tu.
  Ile unayotofautisha, yote ni malipo tu bila kushurtishwa:
  -sadaka, changizo: unatoa kama ukitaka hapo unapokuwa ndani ya kanisa. Lakini kwa mambo ya Changizo tuliona kam Paulo alisema “KILA MTU”, hapa kuna sehemu ya kushurtisha idadi bila kushurtisha kiwango ya changizo kila mtu atakaetoa.
  -Semina: ukitaka unalipa kiingilio na unaingia ndani ya uwanja, nyumba, uliochanga kwa kulipa garama kupitia kiingilio, lakini anayekosewa hashurtishwe kulipa. Naye hawamsahau kwani ataweza baadaye kupata hilo hilo neno kupitia radio. Anataka awe akiisikia kila siku na kila saa apendae ndiye ananunua kanda hiyo, au kitabu.

  Hizo namna mbili zote ni kulipa, na utaona kama pote kuna wanaolipia wengine, wakilipia hata wakaidi.
  -Kwenye semina: waliolipa wanalipia bila kuhuzunika wale wote watakaosikia ile neno kwenye radio ndogo. Hii inafika hata ndani ya nchi za inje ya Tanzania. Hii inaenda mbali kwani imeandaliwa vizuri zaidi na walimu si wachoyo ili watiye tu mifukoni mwao. Kwa mfano: Ukifika Uganda, Rwanda,Burundi, Congo, … unaweza fwata mafundi ya Mwl Mwakasege na wengine unashangaa kusikia mafundisho kama yale yametoka Tanzania kufika nchi nyingine. Na kuna watu watokao huko wanaoshuhudia wokovu au ufungulivu wao kupitia hayo mafundisho. Mim namtaja tu kwani nina ile uhakika lakini si ushabik.
  -Ndani ya kanisa, mara nyingi ni wale walioingia ambao wanapata neno, hapo kukiwa watu wanaojitoa na wengine hawatoe kwa ukosefu au ughaidi.

  Yote mbili ina lengo moja, lakini ni huduma tofauti kidogo kwani wamoja hutafuta zaidi waumini, wengine hutafuta found zitakazowaruhusu kutafuta waumini watakaobatizwa ndani ya makanisa wanaochagua wao wenyewe. Ndio maana tunaongea hapa kwenye SG wengi tusipojua hata iligaramiwa je makusudi tupate sisi sote uwanja. Labda ukiuliza walioanzisha, watakuambia kam kwa mwanzo walikusanya kiwango fulani cha pesa namna sawasana; na leo sasa wanatuomba tuchange jinsi tunavyoweza. Kuna wale wanaochanga na wengine wasiochanga lakini sote tunajikuta tumebarikiwa na hii mtandao.

  Kumbuka tena, kam kuna mwenye ameokoka kupitia semina, anaambiwa ashiriki ndani ya kanisa atakayopenda haswa ya karibu yake. Hapo ndipo atakapo toa sadaka ya kawaida kama vile yule anayeokoka kupitia lile neno linalopeperushwa kwenye radio bila kutoachochote.
  Ukitazama vizuri ni mfumo tofauti, lakini lengo ni moja.

  Jambo linaloweza korifisha ile lengo ni wokovu wa Mchungaji kwa upande moja, na kwa upande Mwengine wokovu wa mwalimu wa semina. Kwani iwe huyu au ule, wakiwa ni watu wa hila, watajaza mifuko yao tu, yote itahuzunikisha mtoaji.

  Asante.

 70. Joseph,
  Mchango wako ni mzuri tu wala hauna shida, kulingana na ufahamu wako.

  Nifanyie tu upendeleao mmoja; nioneshe angalao maandiko matatu yanayosema kuwa mtu anatakiwa kutoa kulingana na alivyoguswa na Roho mtakatifu moyoni mwake!

  Pia unaposema kwamba wanaofanya semina za kile unachokiita ‘kulipia’ kwenye matangazo yao waseme pia kuwa wote wasio na uwezo wanakaribishwa na kutakuwa na namna ya kuwaingiza kwenye hiyo semina, wewe kichwani mwako unadhani hicho kiingilio huwa kinawekwa kwa ajili ya nini?

  Ni hayo tu kwanza.

  Karibu sana kwenye mjadala Joseph!

 71. Mpendwa Lwembe,

  Sikiliza, kucheka si vibaya, lakini kila wakati una majira yake. Mtu anaecheka pahali pa hudhuni anazo akili za kitoto.
  Unaposema « nikichekwa… » ina maana wewe kanicheka ? Na kama ni vile unahakikisha kuwa na hiyo haki mbele za Mwenyezi Mungu ? Hata vile sikuombe jibu. Nyamaza unifwate kidogo.

  Mim Ziragora nakupenda wewe Lwembe, tangu mbele nilikuarifu kama si vema kuweka wongo ndani ya mijadala(na si wengi wanaonasa waongo kirahisi), lakini ukaendelea kuibandika pasipo kujali. Si rahisi kupata mtu anaekuonya. Kwani fikiri kam unaendelea kuwa mwongo utaishia wapi. Nilikupatia orodha ya wongo uliohusika nawo. Nilitarajia pengine utajibu ukisema ndio samahani nilikosa lakini tuendelee na mada, au sikusema wongo bali wewe ulisikia hivi nami nilipenda niseme namna hii. Kwa mfano : unapodaiwa kuhusika na kwamba ulihakikisha mimi naendesha semina, ni wajibu wako kusema samahani, nimekurupuka tu, au unasema kam uliyoyasema ni kweli, uliniona mjini au vijijini fulani nikiendesha semina. Hakuna jinsi ingine ya kuzimisha ile. Lakini wewe ulikwepa ile orodha yote ukaendelea kama mwenye kucheka mpaka mwisho.

  Sijue kama ni kwa sababu ya hofu ; indeed umeshindwa hata kujibu kwa hoja zangu hata zilizotofauti na madai ya wongo. Yesu Kristo, saidia Lwembe !

  Ulijibu ukitafutisha chini-juu, hapo ukiungaunga sentenses ili upime kuonyesha kam nami ni mwongo kama wewe. Hapo kuna hatari mbili :
  -unasema niko mwongo bila uhakika ya wongo mwenyewe hapo ukiongeza wongo ku ingine
  -Hata ingelikuwa ni wongo haizimishe yako.

  Acha nipime kujifasiria hata kama isingelikuwa lazima, kwani inanibidi tu nikuchukulie:

  “KWA TAARIFA YAKO ANAESOMA ULIOANDIKA, ANAONA WAZI KAMA ULIKAMATA MITAZAMO YANGU INAYOTOFAUTIANA NA YAKO, PIA SHAIRI ZINAZOKUONYESHA UKWELI UNAYOKOSEWA, HIYO UKAIITA WONGO. NDIPO UKAUNGANISHA NA ILE NILIYOANDIKIA NDUGU TUMAINI. SASA KWA AKILI ZAKO UNAWAZA MANENO YA MUNGU YANA BEI? HEBU KAMA NI MIMI TU ULIEZOEA DANGANYA AMBIA WENGINE KAM MANENO YA MUNGU YANAPIMWA JE ILI YAPEWE BEI. NA ULINGANISHE NA JINSI NILIAMBIA TUMAINI KWAMBA ANAYOPATA NDANI YA SEMINA INAPITA ILE ANAYOLIPA KIINGILIO. KWA LAANA, NILIONGEA JUU YA KUKATAA KUKARIBISHA NA KUGARAMIA WATUMISHI WA MUNGU, NA NILILETA SHAIRI. KAMA HUSADIKI ILE SHAIRI HAIMAANISHE KAMA NI WONGO. UKADAI KAM NILISEMA MAFUNDISHO HUKO ZAMANI KAIKUFANYIZIKA KWA BURE. NI KWELI NILISEMA ILE NA NIKALETA SHAIRI HAPO NIKISISITIZA KAMA MANENO YA MUNGU TUNAYAPEWA BURE KUSUDI TUOKOKE. HEBU KAMA ULIOKOKA SEMA KAMA UMELIPA NGAPI KWA WOKOVU WAKO AU UTUAMBIYE ALIEOKOKA KUPITIA HELA YAKE, AWE AMEINGIYA NDANI YA MKUTANO WA CHANGIZO AU SEMINA YA KIINGILIO. KAMA ILE NI WONGO INA MAANA NI SHAIRI NDIO INASEMA WONGO.UNAENDELEA UKILETA KITU KAM HADISI NA UNAMALIZA UKIHAKIKISHA KAMA NILIJIKOROGA. KUJIKOROGA SIYO KUSEMA WONGO. KWA MWISHO UKAONYESHA KAM UMECHOKA KUYACHAKUA MAMBO YA UWONGO WANGU. UNAONA KAMA UMECHOKA PASIPO KUONYESHA HATA HERUFI MOJA YA UWONGO ULIOTOKA NDANI YA YALE NILIYOANDIKA? NILISEMA KAM MIM KABLA NIANDIKE NINAOMBA, NDIO MAANA UNACHOKA KUZUUNGUKA HOJA ZANGU LAKINI HUPATI KITU YA WONGO. HATA UNAPO CONNECT NA YALE NILIYOANDIKIA WENGINE HUPATI TU! UKITAFUTA HATA KATIKA INGINE MIJADALA HUTAPATA! ROHO MTAKATIFU NI WA AJABU!!!”

  Umeona kuna kinachofanana na ile orodha ya wongo wako? Jamani, kutubu hailete haya kwa mwana wa nuru!!!

  Kusema wongo ni kuhakikisha jambo usilowai kuona ao kusikia, tena kwa makusudi hapo ukiwa na lengo ya kudanganya tu kama ile mfano moja ya wongo wako nimekwisha kurudilia. Acha niirudilie tena: “Ulisema NINAENDESHA SEMINA makusudi ya kudanganya ili uonyeshe wengine kama ninajadili kwa faida yangu”. Sasa hii ni moja kati ya orodha ya mambo takriban mane. Rudi kwenye zizi bwana!!! Yesu Kristo anakupenda.

  Ninakushawishi kutosemesha wongo tena hapa kwenye SG. Kwa kukusaidia nataka nikuonyeshe kinachokuleta wewe kusema wongo pengine pasipo kujua. Ona jinsi kila mara wanaojadili nawe wakiwa na maoni tofauti na yako kam Ndugu Sungura wanarudilia wakisema kam hukuwajibu. Na hata mtu mwingine anapochunguza anagundua tu hukujibu. Kinachoendelea ni kwamba unakwepa hoja lakini unabandika tu maoni mengine marefu. Inayomaana unajibu kwa hoja unayotengeneza wewe mwenyewe hapo ukikwepa unayodaiwa. Unaona hata kam hapa, ulikwepa kuzungmuzia uliodaiwa kuwa mwongo ukatafutisha wongo wangu ambao kwa kweli huwezi pata. Kilichojitokeza ni kwamba uliongeza wongo ingine ambayo sikufwatilia kwani mtu aliejiingiza jela kwa wongo kawaida simdai tena chochote.

  HII CONCLUSION NDIYO INAYOBAKI KWA SASA KAMA HOJA YANGU:
  “UTALIALIA, LAKINI USIPOTAFUTA DAWA YA WONGO WAKO UTAKUWA UKIJICHOKESHA BURE. HAIKO MCHEZO WA WORD JUGGLER NDIO ITAKUTOA KULE ULIPOJIUNGANISHA NA WONGO; BABA YA WAONGO AKIWA IBILISI SHETANI. TENA MIM NINASEMA HII KWA HUDHUNI NYINGI WALA SI KWA KUCHEKA. NINACHOHOFIA NI KWAMBA MJADALA HUWEZI TOA MATUNDA MEMA WAKATI SHETANI AMEINGILIA KATI TENA AKIVAMIA MFANYA KAZI MKUBWA KAM NDUGU YANGU LWEMBE.

  NITAKACHOFANYA NI KUKUOMBEA HAPO NIKIKUNGOJA TENA KWANI SITAACHA KUKUPENDA.

  KARIBU TENA KAMA UMEJITAMBUA.

  ROHO MTAKATIFU AKUWEZESHE.”

 72. Kwa habari ya kutoa kiingilio ili uingie kwenye semina…ukitaka kujua watu wanatoa kwa moyo au kwa kupenda…njia rahisi ni kwa hao watumishi wanaofanya hivyo watangaze siku kuwa kutakuwa na semina kisha atakayependa atoe kiasi fulani mlangoni na ambaye anajisikia kuingia bila kutoa apite tu mlangoni ni ruhusa!…matokeo ya siku hiyo yatatoa picha halisi.

  Nijuavyo kumtolea BWANA mara nyingi kunaendana na jinsi mtu alivyoguswa na Roho Mtakatifu moyoni…ila kutoa kiasi fulani ili kuqualify kuattend semina ni kama kupay the price for service or product!…ndio maana matoleo ya sadaka jumapili yale ya makanisa yanayomaanisha..huwezi kuta kuna kufuatiliana mtu ametoa kiasi gani…ni yeye na Mungu wake…

  Hivi kwenye matangazo ya hizi semina za kulipia uwa wakishasema kuwa Kiingilio cha semina ni Shilling XXX/- uwa kwenye tangazo wanasema PIA kuwa wote wasio na uwezo wa kulipia wanakaribishwa na kutakuwa na namna ya kuwaingiza kwenye hiyo semina??

 73. Sungura,

  Ingawa ninyi hamuamini kwamba Huduma ya Kristo kwa ukamilifu wake, iliendelea katika mitume wake, kule kuwa pamoja nao mpaka mwisho wa dahari alikokusema na kukutimiza, ule ujio wa RM aliousema, lakini kwa kutokuamini kwenu inawagharimu katika ufahamu wa Huduma inayoendelea kwa kuwakosesha kupata flow nzima ya Good News!

  Tazama hapa Kristo anachokisema:
  Mt 10
“1 And when he had called unto him his twelve disciples, he gave them power against unclean spirits, to cast them out, and to heal all manner of sickness and all manner of disease.
….

  7 And as ye go, preach, saying, The kingdom of heaven is at hand.
  8 Heal the sick, cleanse the lepers, raise the dead, cast out devils: freely ye have received, freely give.”

  Basi iwapo Kristo yu pamoja na watumishi wake akiwaongoza, je, unategemea wawe na kauli tofauti? Haiwezekani, ndio unamuona Paulo akisema, 1Kor 9:18 “What is my reward then? Verily that, WHEN I PREACH THE GOSPEL, I MAY MAKE THE GOSPEL OF CHRIST WITHOUT CHARGE, that I abuse not my power in the gospel.” Unaona? Ni Roho yule yule aliyeyasema hayo huko nyuma, ktk Mt 10 na sasa akiendelea kuisimamia kauli yake kiutendaji bali akiliweka wazi hilo kwa ajili yetu!

  Ndipo, akiwa ni mtu mwenye mamlaka ya Injili, hiyo inayopaswa kutolewa bure, basi akigeuka AKAWATOZA kwa ajili hiyo, jambo ambalo katika MAMLAKA aliyonayo angeweza kulifanya, labda akawaambia kila mtu alipie dola mia ili apate Wokovu, na wangelipa; kama Katoliki nao kwa mamlaka ya injili walivyowatoza watu viwango vya pesa kwa ajili ya indulgence; HUKU ndiko KUINAJISI mamlaka, lile Neno la Mungu!!! Kama Mungu amekuambia TOA BURE, wewe kwa kisingizio chochote kile ukageuka ukatoza, unakuwa hauna tofauti yoyote ile na Sauli aliyeambiwa usichukue nyara chochote, bali yeye alipowaona wanyama walionona, akaingia tamaa ambayo ikamuongoza kujidanganya kumtolea Mungu sadaka sehemu ya nyara hizo alizokatazwa, tamaa ikiisinyalisha akili yake hata kudhania Mungu ataridhika tu; sadaka yake na yeye mwenyewe VIKAKATALIWA kama ambavyo watoza semina leo nao walivyokataliwa kwa kulinajisi Neno la Mungu! Jambo hili haliwezi kuwa tofauti kwa sababu “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele”!!!

  Kuhusu versions, well, maelezo yako niliyoyanukuu katika maana ya tafsiri ulizoziweka, yalikuwa ni yale ya KJV. Kwahiyo ile tafsiri uliyokiwekea hicho kifungu cha 18 ikawa haishabihiani kabisa na maelezo yake, wewe mwenyewe unaweza kuyaona, ndipo nikasema utakuwa umeyapata kutoka sehemu nyingine, ie hizo versions, ambazo niliyaona yanaendana, ndipo sikuelewa kwanini umechukua maelezo ya version nyingine na kuyabandika katika KJV uliyotiririka nayo vizuri sana, kwa uzoefu nikajua ni zile hila!

  Sikulazimishi ubaki ktk KJV, au version yoyote nyingine, bali msingi wa maelezo yangu, huko nilikotoka nayo, ulikuwa katika version hiyo, na kimaudhi ninaiona iko more perfect, otherwise version zote zinafaa, na ROHO yupo kutufunulia iwapo shauku yetu iko katika kulielewa vizuri Neno lake!

  Nadhani nitakuwa nimekujibu maswali yako yote, pamoja na lile la nyuma, karibu sana kaka!

  Gbu!

 74. Sungura,

  Ninachokisema ni hiki:
  SI SAHIHI kuweka TOZO lolote katika jina lolote kwa kazi ya Mungu inayohusiana na kuihubiri Injili kwa muongozo wa Maandiko!!

  Kilicho sahihi katika uendeshaji wa semina, watu wanapaswa wakaribishwe bila TOZO lolote kama inahusu Neno la Mungu, ili Mungu ahusike nayo, kutoza chochote kile ni ku ABUSE mamlaka mliyonayo katika Injili, kama Maandiko yanavyosema!

  Pia semina siyo jambo linaloshitukiza, bali hupangwa mapema. Kwahiyo maandalizi yanaweza kufanyika kwa KUAMURU changizo kwa ajili hiyo, si katika tamaa ya pesa kama Yuda Iskariote, bali katika Upendo wenye kuwakusanya watakatifu ili kuumega Mkate, kulingana na Ahadi ya Mungu katika Kristo! Ukisoma jibu la Haule kwa swali lako, katika tafakari waweza kukielewa ninachokisema; jaribu kuliwazia lile CHANGIZO la samaki wawili na mikate mitano, wakalishwa watu elfu tano (tena hiyo ni hesabu ya Kiyahudi, ambayo wanawake na watoto hawajahesabiwa, licha ya kwamba walikuwepo pia)!!!

  Tofauti ya KUTOZA na SADAKA katika context ya Neno la Mungu ni moja tu, TOZO, Mungu halitambui, kwahiyo wote waliolipia Huduma hiyo WAMEPOTEZA wakati wao na pesa zao, katika yote yanayohusiana na Roho, labda ya mwilini! SADAKA, Mungu anaipenda saana, na huwabariki wote wenye kutoa kwa moyo safi!

  Pia, unapaswa kuelewa kwamba HAKUNA KITU CHA BURE! Lakini pia mafanikio yetu katika maisha hayatugawi katika Baraka za Mungu. Kwa mfano wewe Sungura ukiwa Askofu Mkuu na Ziragora akawa Msaidizi wako, nyote mkiwa ni wale mliotukuka katika utumishi wenu kwenye kazi ya Mungu, basi mimi nikiwa ni lile busati la kufutia miguu mnapoingia maofisini mwenu, hilo lingeufurahisha sana moyo wangu kwamba ninawafuta miguu watukuka wa Bwana na kuwatakasa, sote tukiwa ni sehemu ya kusanyiko hilo; basi iweje mnitenge? Kutoza Viingilio ni UBAGUZI, unaozaliwa na roho ya Choyo inayowatawala watumishi wengi hata wanaishia kutawaliwa na njaa ya pesa!

  Pia, labda uwe ni mwenye kupenda kujidanganya au uliyedanganyika kwa kwa fix za waandaaji wa semina, kuwa Kiingilio unacholipia ni Mchango wa uwezeshaji, lakini:-
  – Kufanya changizo kwa ajili ya semina SI kutoza pesa.

  -Kuweka viingilio kwa ajili ya semina NI kutoza pesa.

  -Kukusanya sadaka kwa ajili ya semina SI kutoza pesa.
  Kuyaelewa haya ni suala la lugha, jihakikishie zaidi kwa kuyatafakari maneno hayo, Changizo, Viingilio na Sadaka ili uone kama yote yana maana moja, maana ukikosa kuyaelewa haya, basi utakuwa mteja mzuri wa semina za viingilio!

  Gbu!

 75. Lwembe,
  Kuhusu ule mstari wa 1cor 9:18, umetumia neno ‘kunajisi’. Unaweza sasa ukaniambia ni kwa namna gani Paul angeinajisi mamlaka yake katika injili?

  Na bila shaka uliposema kuwa hiyo tafsiri/maelezo yake nimeyapata toka sehemu nyingine ulimaanisha kuyapata toka kwenye version zingine za biblia tofauti na KJV.

  Nafikiri version zote nilizotumia ziko kwenye komenti yangu husika. Na wala siko bound kutumia KJV tu. Unaweza ukafuatilia na wewe tafsiri ya version zingine.

  Sioni nilichokosea katika fafanuzi zangu Lwembe!

 76. Ziragora,

  Ukichekwa, unawaka moto sana, lakini unastahili kuchekwa kwa sababu una mambo ambayo ni zaidi ya kitoto! Tazama unachoniambia:
  “”Unaongea « kiingilio » tangu mwanzo haadi mwisho.””!!!
  Kama unavyonishangaa kwa kuongelea “Kiingilio, tangu mwanzo hadi mwisho” nami ndivyo ninakushangaa kwa kuongelea “CHANGIZO mwanzo hadi mwisho” katika mada ya KIINGILIO, sasa sijui ni nani kati yetu aliyekosa maarifa na ufahamu!

  Hebu zitazame kauli zako hizi halafu uitafute nafasi yako ktk Injili.
  Ulimuandikia Tumaini maeneno haya:
  “”…unayopata kwenye semina inapita ile kiingilio. Ukilipishwa kikwelikweli yale maneno, nyimbo, pambio, kiti, nk, utapata? Sasa jumlisha na baraka utakazopata, au jumlisha na laana kam utapinga!!!!””
  Nami ukaniambia, “Sasa nakuona wewe Lwemba na wapambe wako mukichagua laana!!!”
  NI WAPI BIBLIA INAFUNDISHA KWAMBA ATAKAYEPINGA KULIPA KIINGILIO ATALAANIWA?

  Pia umemwambia Tumaini:
  “”Acha nikuonyeshe kama hata huko zamani mafundisho haikupewa bure. Soma “1 Wakorintho 16:2 Siku ya kwanza ya juma KILA MUTU kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;”. Hivi huone namna Paulo alikuwa akiwaambia washiriki watayarishe michango yao kabla aje? Hiyo ndiyo garhama. Sasa inategemea namna semina imendaliwa. Paulo yeye anasema kwa kadri ya kufanikiwa, lakini mwengine ataweka amount ya kadiri anayoona watu wengi wanaweza ifikia.””

  HUU NI UONGO USIO NA AIBU, AIDHA UFAHAMU WAKO ULIKWISHA TEKWA NA SASA UNATUMIKA KULIHARIBU NENO LA MUNGU!! Na kama unasema kwamba wewe si muongo, basi Paulo ndiye muongo maana yeye anasema ameihubiri Injili BURE, ““Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama,…”

  Unaendelea:
  “”Ni heri ueelewe kama jinsi Paulo alitoa bure neno licha ya kuamuru KILA MTU atoe changizo, vile vile semina inatolewa bure licha ya kuomba ANAETAKA atoe KIWANGO FULANI cha hela. Tena nikakuambia : pima kueleza mbele ya wakati shida ya ukosefu wako kifedha uone kama hutagaramiwa na kuingia kwenye semina. Jesus !!! Sasa Lwembe unataka tukufanyeje ?

  Nilijaribu kukuelezea lakini unakua kam mwenye kutosikia. Nilikuonyesha kama kazi changizo ilioamriwa na Paulo na hivi viingilio inafanana kwani yote ni kwa lengo inayofanana. Mim sikukwambia kam kwa maneno tu kiingilio na changizo si maneno mawili tofauti.””
  UNAUONA MKANGANYIKO UNAOUKOROGA BILA YA AIBU? NI MJINGA GANI UNAYEFIKIRI ATAYAAMINI MAFUNDISHO YAKO HAYA POTOFU YANAYOIDHALILISHA INJILI?

  Sikiliza, nikisema niyachukue mambo yako ya uongo yote uliyoyaandika hapa, haitamsaidia mtu yeyote zaidi ya kuwachosha kusoma mambo yasiyoeleweka! Nilikuambia ukae chini ya walimu wakufundishe ukanijia juu, halafu bila ya aibu unaniambia eti walimu wa semina watanifundisha kuukulia Wokovu! Kama semina zenu mnafundishwa kwamba “Paulo alitoza Injili aliyoihubiri” hauoni kwamba mnapelekwa kuzimu? Ni Mungu gani atakayewapokea ninyi wenye kuwadhalilisha watumishi wake vipenzi?

  Kati ya mimi niliyelikataa “Fundisho la Kutoza Viingilio kwenye semina za Neno la Mungu”, kwa ushahidi wa Maandiko, na wewe uliyeyachukua Maandiko yanayowafundisha watu kuchangia Huduma na wanyonge, ukayafanya kuwa yalikuwa ni MALIPO kwa Huduma na kuwafundisha watu waendelee kulipia Injili; ni nani kati yetu mwenye roho ya kishetani? Ni nani kati yetu mwenye kuubomoa Msingi wa Injili alioujenga Paulo? Usitoke kufundisha jambo usilolijua, tena jitahidi uwe na roho ya unyenyekevu kwa Neno la Mungu! Pia jaribu kuwa msikivu, unapofundishwa mambo ya Mungu usiyoyajua!

  Soma michango ya wengine ujifunze, uongeze ufahamu, soma huo mchango wa ndg John Haule unaweza kukusaidia sana, ukaokoka na Hukumu unayojipeleka kwa upofu wa kuyachezea Maandiko bila kujua! Maana kwa kadiri nilivyoisoma michango yako, ni kwamba HUJUI ila UNAJITUTUMUA tu kwa hasara yako!!!

  Bwana na akupe unyenyekevu!

 77. Lwmbe,
  Ni utoto kuambizana kuwa wazo fulani ni mambo ya kitoto! Hakuna jambo la kitoto hapa, bali ni tofauti tu ya mitazamo.

  Hebu sema ni nini hasa unachosema siyo sahihi:

  -Je ni kuwatoza watu pesa kwa ajili ya semina?
  -au je, ni kuwatoza watu kiingilio kwa ajili ya semina?

  Na nini hasa unachosema kuwa ni sahihi:

  -Je ni kwamba kwenye semina watu waingie bure?
  -Je, ni kuwa watu wagharamie semina lakini kwa michango ya hiari pamoja na sadaka?

  Tofauti hapa ni nini basi, kwani anayetolewa hiyo sadaka na michango ya hiari ni nani, na anayetolewa hicho kiingilio ni nani?

  Ukiangalia kwa umakini mzuri katika hii mada utagundua kuwa kiini cha mjadala hapa si kiingilio, bali ni mfumo unaotumika kutoza hicho kiingilio.

  Ukiandaa semina halafu ukawaambia watu watoe sadaka au michango ya hiari kugharamia hiyo semina, huwezi kusema kuwa hiyo semina ni ya bure.

  Tofauti yake tu na semina yenye kiingilio maalum ni kwamba, kwenye kiingilio mtu anakuwa limited kutoa kiasi fulani, na huku kwingine anakuwa na uhuru wa kuchagua atoe kiasi gani.

  Kwa hiyo:
  – Kufanya changizo kwa ajili ya semina ni kutoza pesa.
  -Kuweka viingilio kwa ajili ya semina ni kutoza pesa.
  -Kukusanya sadaka kwa ajili ya semina ni kutoza pesa.

  Kwa hiyo mpaka hapo hakuna semina ya bure.

  Kwako Lwembe.

  NB: Lwembe kulikoni hujibu lile swali langu,huna majibu au inakuwaje?

 78. Ndugu Sungura,

  Ukitazama vizuri utaona huyu Lwembe ni professionally mwongo. Pia nimeona hila zake zinamsukuma kutokuwa na mda wa kusoma mambo wengine wanaoandika, lakini ni mwepesi kwa kuandika jinsi anavyopenda kwa lengo ya kuvutia tu waliowachanga ndani ya Neno la Mungu. Pamoja na ile ana debate kam waislamu ambao wanasimamisha hoja kama za Lwembe wakisema :”Tutasadiki kama Biblia ni neno la Mungu mkituonyesha ndani ya Biblia kunapoandikwa neno BIBLIA kama vile ndani ya qu’ran neno qu’ran limeandikwa”. Ndio maana Lwembe hasomi maneno ya upako tunayompa, lakini anataka tu neno “kiingilio” liwe limeandikwa ndani ya Biblia.

  Mim namgoja , hapo nikimuombea, akanushe kwanza wongo yake, au aombe msamaha wasomaji wa SG wote, ndipo ajibiwe tena. Pengine anaweza okoka!!!

  Asante ndugu yangu Sungura.

 79. Sungura,

  Hivyo vifungu ulivyovinukuu kutoka hizo versions, na tafsiri ulizoviwekea, kwa kweli sijui niseme nini! Labda ngoja nikufuate nyuma ili nawe uone kama unakielewa sawa sawa unachokisema kutoka hayo aliyoysema Paulo.

  KJV; 1Cor 9: 13 “Do ye not know that they which minister about holy things live of the things of the temple? and they which wait at the altar are partakers with the altar?”
  (Katika kila hali jambo hili Paulo analirejea kutoka katika utaratibu wa Torati, ambao wahudumu walihudumiwa kutoka vitu vya hekalu na wahudumu wa madhabahu kutoka vitu vya madhabahu, na katika maelezo haya sioni tamko linaloashiria wahudumu hao kutoza chochote, labda unioneshe!)

  14 “Even so hath the Lord ordained that they which preach the gospel should live of the gospel.”
  UNASEMA: Unaongelea habari ya haki ya wanaohubiri injili kuishi kwa hiyo injili.
  (Haki ya kuishi kwa Injili inayozungumziwa hapa sidhani kama inajumuisha KUTOZA watu)

  15 “But I have used none of these things: neither have I written these things, that it should be so done unto me: for it were better for me to die, than that any man should make my glorying void.”
  UNASEMA: Kuwa Paul hajatumia hata moja ya hizo haki, na wala hasemi hayo sasa ili azitumie. Hajataka kuzitumia kwa sababu yeye alitaka ajivunie kutozitumia…
  (Haki anayoizungumzia hapa ni ile ya kuishi kwa vitu vya madhabahuni; bali sijui kama kuna madhabahu inayopokea TOZO, labda mnioneshe! Pia kifungu hiki ndicho kinalifunga jambo la kuishi kwake kwa Injili.)

  16 “For though I preach the gospel, I have nothing to glory of: for necessity is laid upon me; yea, woe is unto me, if I preach not the gospel!”
  UNASEMA: Unaeleza kuwa majivuno yake hayawi kwa sababu anaihubiri injili, maana kwake kuhubiri injili amewekewa na Mungu kama lazima/ amri.
  (Hapa mazungumzo yake yamebadilika, anazungumzia kujitukuza kwa kazi ya kuihubiri Injili, jambo hili halina uhusiano wowote na jambo la kula vya madhabahuni, hilo amelimaliza, he is not given to vain repetitions, hapa anazungumzia kazi ya kuihubiri Injili, ninaamini hapa ndipo mlipomkosa pamoja na watafsiri!!!

  17 “For if I do this thing willingly, I have a reward: but if against my will, a dispensation of the gospel is committed unto me.”
  UNASEMA: kama ameamua kuhubiri injili kwa hiari yake basi ana thawabu…
  (Hili ni sawa kwamba anaendelea na maelezo ya kuihubiri Injili na sasa anazungumzia THAWABU ya kazi hiyo…)

  18 “What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, that I abuse not my power in the gospel.”
  UNASEMA: Anasema thawabu yake yeye ni kuihubiri injili bila kutoza gharama yoyote, NA ANAFANYA HIVYO ILI ATIMIZE LENGO LAKE LA KUTOKUTUMIA HAKI ZAKE ZINAZOTOKANA NA KUHUBIRI INJILI.
  (Nusu ya kifungu hiki umenena sawa, lakini kipande hicho cha kumalizia, maelezo yake utakuwa umeyatoa sehemu nyingine, bali tafsiri halali ya maelezo haya, “that I abuse not my power in the gospel” ni hii hapa: “ili nisije nikainajisi mamlaka niliyonayo katika Injili”

  Hata hivyo, kauli yako hii, kwa kadiri ya ufahamu ulioupata wa nusu ya kifungu hiki cha 18, inatosha kukufundisha kuachana na kutoza viingilio kwa Neno la Mungu; “Anasema thawabu yake yeye ni KUIHUBIRI INJILI BILA KUTOZA GHARAMA YOYOTE”!!! Labda kama semina zenu ni za ujasiriamali!!!

  Hivi unajua kuwa Paulo alikuwa jasiri, tena mwenye kujivunia Bwana wake aliyemtia utumwani? He was a strongman! Hakuwa mtu wa kuomba omba, na hata makanisa aliyoyazaaa hayakuwa ‘lazybones’, aliwafundisha kuwa kama yeye, tofauti na walimu watoza viingilio na wafuasi wao! Mdo 20:32-35
  “Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.”

  Pokeeni nanyi huko kuwekwa katika mikono ya Mungu ili muondokane na roho ya hofu ya kukosa pesa na kuishia kutoza viingilio!

  Gbu my brother!

 80. Shalom….
  Mtumwa wa Bwana Sungura….

  Kama nilivyosema mwanzo kuwa sioni maandiko yanayonitangulia kutoa kiingilio ndipo nihubiriwe habari njema kwangu hakuna, kwa kweli niseme ni kusudi/mpango wa kibinadamu tu, kutoka moyoni si ukubali.

  Baada ya kusema hayo niyaendee yale yaliojiri na kuleta maswali na uthibitisho wa maandiko.

  Umeuliza:”Unaweza ukanithibitishia hayo maneno yako kibiblia”?

  Ndiyo…..Soma na tafakari….Mk6:31-42 ,Yoh 6 na Mk8:1-9

  Maandiko haya yanasimulia habari ya makusanyiko mawili makubwa ambayo yalilishwa.tunaona kwamba waandaaji wakishughulika na huduma kwa uongozi wa Roho Mtakatifu

  Huduma za zama zetu wanawaza kulisha kwanza chakula cha mwilini na gharama zitakazojiri kwa kutumia akili zao ndipo ile sauti weka kiingilio inaposisika masikioni mwao.

  Tunaona makutano kwa kupenda mafundisho na kutaka kwao kuijua kweli ya Mungu,waliitoa miili yao kuwa dhabihu takatifu wakapiga tatu kavu wakila chakula cha roho kilichoshuka toka mbinguni(Mk8:3)

  Wale wa kusanyiko la kwanza walishinda kutwa tena walikuwa wanafuata Yesu kwa miguu(Mk6:33)
  waandazi wa injili ya leo utawasikia usafiri utakuwepo lakini ni sh 1000,

  Nimebarikiwa na hili andiko mk6:36-37”wapeni chakula…yaani bure bila kulipa
  Haya ni mafunzo makubwa tunayapata ktk haya maandiko ili tuumalize mwendo vizuri.

  Bro Sungura linapogongwa GOMBO LA KWELI sioni haja ya kuweka kiingilio yote yatakuwa kama Bwana alivyotaka, Tatizo ni imani haba tunauwaza upepo wa mbisho nao unatuingiza mwilini
  “maandalizi ya moyo ni ya mwanadamu jawabu la ulimi latoka kwa Bwana”

  Uliuliza ‘Swali; kwani wanaotoa viingilio kwenye semina wanafanya hivyo kwa kulazimishwa au kwa moyo wa kupenda pia?
Na huko kutoa hicho kiingilio sio kumtolea Bwana?”

  Hili sina jibu Mpendwa mtumwa wa Bwana,Yeye achunguzae mioyo ndiye hajuaye,nisijitie nira na kitu ambacho sikijui na sina uhakika,kama kutoa kiingilio nayo ni matoleo kwa Bwana.

  “Tusikitendee kazi chakula kinachoharibika”

  Haya ndio kwa sehemu ninayoyafahamu

  Bwana akutunze mtumishi Sungura,

  Karibu……

  Amen.

 81. Sungura,

  Kujadili sentiments ni jambo gumu sana, maana haziishi kubadilika!

  Pia uungwana ni kufika mahali ukaukubali ukweli wa jambo unaojidhihirisha, kuliko kujibakiza katika assumptions zisizo na mashiko!

  Nimekopi mada na kupaste ili nikudhihirishie jambo la watu kuzuiliwa milangoni katika makanisa zinamofanyika hizo semina zenye viingilio, uungwana ni kufika mahali ukaliona hilo na kuubadili uelewa wako wa kukisia mambo kuwa “hakuna anayezuiliwa!”

  Kwamba unasema, “Nilitegemea labda mngeleta hoja za kuwaonya wale watumishi wanaotoza viingilio kwa manufaa yao binafsi wala si kwa ajili ya injili” hayo ni mambo ya kitoto! Kama unaweza kusoma katikati ya mistari, tumekuambia hivi: mtumishi anayetoza viingilio kwa Neno la Mungu huyo hajatumwa na Mungu! Na si kazi yetu kuwaorodhesha wasiotumwa na Mungu, isipokuwa tunatumia ujuzi wa Neno la Mungu kuyajua hayo na kujiepusha nayo!

  Tazama unachojifikirisha: “Kwani haiwezekani Mungu akakuambia ufanye semina mahala fulani lakini uwaambie watakaohudhuria watoe kiasi fulani kila mmoja kwa ajili ya ku-cover gharama zinazohitajika?” ukiisha jiingiza katika mtiririko wa mawazo kama haya, ni lazima utaishia kuliona jambo hilo kuwa ni jema, lakini Mungu hana mipango hiyo, mipango ya Mungu ni Changizo, Sadaka, na pia hajawazuieni kutoza malipo kwa Injili mtakayoifundisha!

  Halafu katika hiyo hila ya KUTOZA watu, siku hizi maelezo ya mafundi hao wa kutoza wameyachezesha kidogo na kuyafanya kama Changizo. Siku hizi kwa ule upako unaowatuliza waumini wao mithili ya kondoo anayenyolewa, ndipo utawasikia, “Bwana amenionesha kuna watu zaidi ya wanne hapa walio tayari kumtolea shilingi milioni moja moja, wapite mbele!!” watu hao wanatoka kumtolea Mungu, kisha wanaombewa baraka zaidi! Basi atashuka na hayo makundi akiwapiga sachi mpaka mtu wa mwisho mwenye ki mia chake!!!! Yote hayo ni kwa jina la INJILI!!!!

  Bali uwepo wa Mungu huyasawazisha yote yenye kuhitajika iwapo mko ktk Mapenzi yake Makamilifu, yaani mnaliamini Neno lake na mnaliishi hilo, siyo make-believe inayowaongoza kuuza Injili! Tazama hapa anachosema, Flp 4:19:
  “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.” That is if you Believe, kama mioyo yenu imejaa mashaka, basi TOZENI viingilio!!!

  Gbu!

 82. Lwembe,

  Sitakufwatilia kwa mambo yote yako unayotumia kam word juggler. Nitainuwa yaliyo na rejea inayosikilikana.
  Unaongea « kiingilio » tangu mwanzo haadi mwisho. Na unabandika tena suali ya “Kiingilio”, jambo nililokujibu zamani na nikaweka hoja nyingi ambazo ulikwepa kwa ukosefu wa maarifa.
  Pia unadaiwa mambo mengi ya wongo katika maandiko yako. Ndiyo inayoonekana kila mara kwa yeyote anaejaribu kuweka “danganya-jicho”. Ndio maana Ndg SAM akakupigia makofi akidhani ulinena kitu wakati reja zako zote ziko empty. Kwa taarifa yako, ukiwa muongozi, kuamuru mtu ni kumpa amri. Ifikapo kwa mtazamo wa kiroho, si mtume anaeleta adhabu, hiyo ni jukumu la Mungu. Ndio maana katika changizo tu Anania na Safira walipotia hitilafu wakapata chamutemakuni.
  Unayodaiwa ni hii kwa ufupi:
  1. Soma majibu tuliyokuletea.
  2. Jibu kwa hoja zetu.
  3. Jifasirie kwa wongo wako na usiongezee wongo kwa ingine kwani unaposema mtu amesema wongo na husemi ni wongo gani, hapo umekuwa muongo zaidi.
  Kwa urefu:
  1. Majibu juu ya kiingilio niliyaleta, ni wajibu wako kuyasoma wala si mim kuyarudilia.
  2. Jibu kwa hoja yangu, unakwepa tu, rudilia niliyoandika na ujibu.
  3. Wongo wako: “ulisema mim naendesha semina”, uliniona wapi? Ukasema “kuamuru” haihusiane na kutoa “amri”, jambo ambalo linakunasa popote. Ukasema “mim nilisema asiyetoa kiingilio analaaniwa”, nakuomba ufanye copy –paste ya ile tamko yangu. Ukasema nililazimisha KIINGILIO na CHANGIZO kuwa ni neno moja , copy-paste exactly lile tamko langu.

  Nangoja kabla nikamate hatua nyingine. Pengine utasoma vizuri ukiwa unatulia, baadaye uombe nikusamehe kwa wongo wako kiisha tuendelee. Naamini anamjua alie baba ya waongo.

  Mungu wa Mbinguni akuwezeshe.

 83. Lwembe, nazidi kukusisitiza kuwa hujaipatia hiyo tafsiri, japokuwa iko wazi.
  Unaweza ukasingizia ‘version’ iliyotumika kutafsiri haikuwa sawa, lakini ili kuuelewa mstari wa 18, unapaswa kusoma kuanzia mstari wa 13.

  Nainukuu KJV; 1Cor 9: 13 Do ye not know that they which minister about holy things live of the things of the temple? and they which wait at the altar are partakers with the altar?

  14 Even so hath the Lord ordained that they which preach the gospel should live of the gospel.

  15 But I have used none of these things: neither have I written these things, that it should be so done unto me: for it were better for me to die, than that any man should make my glorying void.

  16 For though I preach the gospel, I have nothing to glory of: for necessity is laid upon me; yea, woe is unto me, if I preach not the gospel!

  17 For if I do this thing willingly, I have a reward: but if against my will, a dispensation of the gospel is committed unto me.

  18 What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, that I abuse not my power in the gospel.

  -English std version; verse 18 What then is my reward? That in my preaching I may present the gospel free of charge, so as not to make full use of my right in the gospel.

  -NIV: verse 18; What then is my reward? Just this: that in preaching the gospel I may offer it free of charge, and so not make use of my rights in preaching it.
  ………

  Mstari wa 13 na 14 unaongelea habari ya haki ya wanaohubiri injili kuishi kwa hiyo injili.
  Mstari wa 15 unasema kuwa Paul hajatumia hata moja ya hizo haki, na wala hasemi hayo sasa ili azitumie. Hajataka kuzitumia kwa sababu yeye alitaka ajivunie kutozitumia.

  Na anasema ni heri afe kuliko kuzitumia hizo haki na kusababisha aonekane hana sababu ya kijivunia injili, au kusababisha kujivunia kwake injili kuwe bure.

  Mstari wa 16 unaeleza kuwa majivuno yake hayawi kwa sababu anaihubiri injili, maana kwake kuhubiri injili amewekewa na Mungu kama lazima/ amri.

  Mstari wa 17 unasema, kama ameamua kuhubiri injili kwa hiari yake basi ana thawabu, lakini kama anaihubiri kwa lazima basi anafanya hivyo kwa ajili ya kutimiza kazi ya uwakili ambayo imewekwa kwake. Kwa kifupi anasema kuhubiri yeye lazima ahubiri, no matter what.

  Mstari wa 18, anasema thawabu yake yeye ni kuihubiri injili bila kutoza gharama yoyote, na anafanya hivyo ili atimize lengo lake la kutokutumia haki zake zinazotokana na kuhubiri injili.

  Ili kujua vizuri baadhi ya hizo haki ni vema kusoma mistari hii: 1Cor 9: 5 Don’t we have the right to take a believing wife along with us, as do the other apostles and the Lord’s brothers and Cephas ?
  6 Or is it only I and Barnabas who must work for a living?

  7 Who serves as a soldier at his own expense? Who plants a vineyard and does not eat of its grapes? Who tends a flock and does not drink of the milk?

  8 Do I say this merely from a human point of view? Doesn’t the Law say the same thing?

  9 For it is written in the Law of Moses: “Do not muzzle an ox while it is treading out the grain.” Is it about oxen that God is concerned?

  10 Surely he says this for us, doesn’t he? Yes, this was written for us, because when the plowman plows and the thresher threshes, they ought to do so in the hope of sharing in the harvest.

  11 If we have sown spiritual seed among you, is it too much if we reap a material harvest from you?

  12 If others have this right of support from you, shouldn’t we have it all the more? But we did not use this right. On the contrary, we put up with anything rather than hinder the gospel of Christ (NIV).

  Unaona Lwembe,
  Paul alikataa kutumia hizo haki yeye kama yeye,wala haikuwa amri kwa kila mtu.
  Ndio maana anasema mitume wengine walizitumia hizo haki.

  NB: Nakukumbusha kuwa hujajibu swali langu Lwembe, sijui unashau au hutaki tu kulijibu.
  Hili hapa: ”ni nini hicho ambacho hao wenye kufanya hiyo huduma wamekipokea bure, hivyo wanatakiwa kukitoa bure pia?”

  I hope utalijibu na lenyewe!

 84. Lwembe,
  Uliyoniambia mengi ni porojo tu ambazo hata si za kupotezea muda kukujibu. Nitakujibu haya machache ya maana uliyoongea. Japo kama vile nilijua utatumia nguvu nyingi kuijadili mifano yangu ya Yanga na Simna,pamoja na harusi,ambayo hata hivyo haikuwa ya kuiongelea sana.

  Umesema kuwa mleta mada alisema hivi.”Mara nyingi nimeona watu wanazuiliwa kwenye milango kisa hawana hela, …”
  Na wewe katika tafsiri yako ulisema hivi; ”..Ukitaka kulipa zaidi, ujitolee, labda shs 70,000, yule mpokeaji atakataa kuchukua hiyo iliyozidi labda ufikishe iwe 100,000, ili akupe ticketi nyingine ambayo unataamua mwenyewe ufainyie nin.

  Ilikuwa yatosha wewe kusema tu kama alivyosema mleat mada kuwa ukiwa na hela pungufu hawakuruhusu kuingia. Lakini ukaongeza maneno yako kuwa hata ukitaka kutoa zaidi kwa kujitolea wanakataa. Hiyo si kweli, labda kama hukufuata utaritibu unaotakiwa. Huwezi kwenda kutaka kujitolea langoni, huko ni kuwa nje ya utaratibu.

  Na kama wamesema kuna kiingilio, kwa nini wewe uende bila hicho kiingilio huku ukitegemea kuingia, huo kama si ukorofi ni nini?

  Kama huna hela si nenda ofisini kwa wahusika ukaongee nao, nao wataangalia jinsi ya kukusaidia. Kwa nini wewe usubiri kwenda kutokeza mlangoni bila kitambulisho husika? kufanya hivyo ni ujinga na ukorofi.

  Na siwaelewi mnaopinga kiingilio, nini hasa mnataka kifanyike, au kosa la kiingilio ni nini. Nilitegemea labda mgeleta hoja za kuwaonya wale watumishi wanaotoza viingilio kwa manufaa yao binafsi wala si kwa ajili ya injili.

  Kwani haiwezekani Mungu akakuagmbia ufanye semina mahala fulani lakini uwaambie watakaohudhuria watoe kiasi fulani kila mmoja kwa ajili ya ku-cover gahrama zinazohitajika?

  Anyway cha muhimu sana kujibu kilikuwa ni kuhusu tafsiri ya maneno ya Paul. Na naomba nikijibu kwemye ukurasa wa peke yake…..

  P.T.O

 85. Ndugu yangu Tumaini,

  Nashukuru sana kwa jinsi umeniandikia. Kwa kweli sikutakie kuwa vuguvugu. Tukienenda namana hiyo tutakuwa hatusaidiane. Niliyosema ni “don’t be…”, ina maana nilionyesha wish nzuri kwako. Mara nyingine labda utakuwa wazi zaidi ktk unayoandika kama vile umenijibu mambo ambayo ni clear. Tunazungmuzia “kiingilio”. Hii ni neno tu iliyowekwa na watu ndio maana tunataka uhakika kam hio kiingilio inafanana au la na mojawapo wa sadaka, changizo, nk. Mim nilichunguza nikaona kam tukidaka tamko jinsi lilivyo tu pahali pa kuangalia lengo ya kinachoendeshwa, hatuwezi pata ufahamu. Hapo ndipo tukiwa Tanzania, kenya, uganda, Burundi, Congo, Somalia, nk tutajikwaa kwa namna ktk nchi yetu hatuoni Yerusalemu, Galatia, Korintho, Efeso, nk. Unaona kama tukifwatilia kila tamko kwa form yake tu tutakosa twende wapi. Iliyo muhimu ni lengo. Ninayotafuta mim ni ku debate ju ya lengo ya Kiingilio wakati anaeyeendesha mafundisho ya Semina iko serious. Kwani kusema changizo ni rahisi lakini kuwa serious katika mambo ya Mungu ni kuwa na RM. Ina maana mtu anawezaimba “Changizo” bila kuwa na RM. Tukienenda kwa kufwatilia tamko, tutajidanganya sana kwani hata kuzimu Shetani wanamuita mungu.
  HIVI NI VIZURI ZAIDI KUONYESHA WANAOTUSOMA LENGO MBAYA YA KIINGILIO NOT AS WORD BUT AS ACTION, KIISHA TUNAONA VILE MATUKIO MAZURI/ MABAYA TUKIKAMATA CHANGIZO NOT AS WORD BUT AS ACTION KWA MTAZAMO WA PAULO NDANI YA NCHI YETU, HENCE TUNAFANYA BALANCE TUKIWA TUMESHIRIKISHA RM.
  Kawaida mim natakia wanaochangia kuomba mbele waandike kwani kuna yanayoandikwa, ukiyachunguza ni ya kishetani.

  Jesus Christ bless you!

 86. Ndugu Ziragora cwezi kuwa vuguvugu ndugu na cpo hapa S.G kwaajili ya kuogopa awaye yoyote bt namheshimu kila mmoja na naheshimu wazo la kila mmoja so hiyo dhana yako ya kusema kuna point nimechangia kwa uoga imenishangaza sana coz nipo free 100% nikijua tupo hapa kwa nia njema kabisa ya kuelimishana hofu yangu ingekuwa kubwa sana kama niya yetu ingekuwa kutukanana kwakweli hapo ningehofu sana kumkosea MUNGU kwa hilo na wala nicngeweza kushiriki!Swala la kiingilio kuwa kama ni kanuni moja hapo ndiyo napata tabu kuwa MUNGU ni wa kanuni moja?inamaana leo hata wewe akikupa maono ili yatimie ni lazima kiingilio kionekane ndiyo njia peke ya kufanikisha maono hayo?MUNGU WETU NI WA NAMNA HIYO?hebu tuelimishane ndugu yangu!maana nahitaji kujua zaidi na zaidi!ili huu utata naoupata uondoke!NITABARIKIWA SANA NDUGU YANGU.

 87. My br Sungura nadhani utakuwa umenielewa vibaya kuhusu mtazamo wangu wa kiingilio!nimesema MUNGU ANAPOTAKA KUFIKISHA NENO LAKE HUWA ANA MPANGO KAMILI NADHANI HATA MPANGO WA UKOMBOZI MWANADAMU ALIUPANGA KAMA ULIVYOTOKEA KWA YESU KUWA KTK HALI YA KIBINADAMU MPAKA UKAKAMILIKA!SO NA MTUMISHI WA MUNGU YEYOTE ANAPOKUJA NA MAONO ALIYOPEWA NA MUNGU ANAKUWA TAYARI KUNA MPANGO KAMILI MUNGU AMEUANDAA HAIJALISHI WANADAMU WAUPINGEJE BT UTATIMIA SO KAMA MTUMISHI MPANGO WAKE UTAPITIA NJIA YA KIINGILIO KAMA KUSUDI LA MUNGU NI KUPITIA KIINGILIO BILA SHAKA UTAFANIKIWA!SHIDA YANGU NI KWAMBA INAMAANA KANUNI YA MUNGU NI MOJA TU KILA ANAYEKUJA NA MAONO NJIA YA KUFANIKISHA NI KIINGILIO TU?Yaani MUNGU AMEONA NJIA HII YA KIINGILIO NI KWA KILA MTUMISHI ANAYEMPA NA MAONO?KWA STAHILI HIYO HUONI KAMA MUNGU ANAKUWA WA KANUNI MOJA?Hebu tusaidiane kwa hilo Sungura nahitaji nijifunze zaidi.

 88. Sungura,

  Siku hizi unazeeka nini? Seleli kakuzeesha??!

  Ninakushangaa wewe pamoja na Ziragora, nawaona mmetoka katika mada na mmeleta sentiments zenu ndizo tuzijadili!!

  Kwamba Sungura unaijua habari ya simba na yanga kuhusu jambo la Kiingilio, halafu jambo hilo likija kanisani, unalibadili maana kwa kulipa uongo mwingine ili kuyapoza makali yake, mimi nilidhani mtu anayeibadili maana ya jambo kwa ajili tu ya kuwafanya wajinga wafuasi wake, huyo ndiye mwenye hila, kama wewe na Ziragora mnao ikataa tafsiri halali ya neno ili mpandikize ujinga ndani ya watu!

  Suala la ulazima wa mtu kuja katika semina au kutokuja kwa kushindwa kuwa na kiingilio silo tunalolijadili hapa, msizungushe akili za watu! Kama unajua kuwa kuna watu wanaoweza kushindwa kuja kwenye semina yako kwa kukosa kiingilio, usiwahukumu au kuwafanya wajinga au wachoyo, huo ni Ujinga wa Kiroho unaomkamata mtu asiye na Hekima! Niliwaulizeni kuhusu wale watu wa Yerusalemu ambao Paulo alichangisha pesa kwa ajili yao, kama wangeweza kulipia semina zenu hizo, ninyi wenyewe mnajua kuwa isingewezekana!

  Neno la Mungu halijengi tabaka, bali tamaaa ya pesa inajenga tabaka!

  Unazungumzia michango ya Harusi na hekima zake, kwa taarifa yako amewahi kushitakiwa bwana harusi aliyehamisha venue ya harusi kutoka Dar kwenda kijijini kwao, watu wakataka pesa zao zirudishwe! Na unapoifananisha michango ya harusi na Kiingilio cha semina, hapo ndipo unaponiacha hoi, naona hii ni zaidi ya hila!!!

  Lakini hii hapa ndio kubwa kuliko: kuhusu maelezo yangu ya KIINGILIO =ENTRANCE FEE, unasema,
  “”Tafsiri hii kwa rejesta ya kanisani haiko sawa, umeiweka hivi kwa ajili kutetea msimamo wako juu ya mada hii. Na hizi ni hila za kutokutaka kusema ukweli wa uhalisia wa kinachofanyika katika semina za kikristo zenye viingilio.
  Haya uliyosema wewe ni mambo yanayofanyika kwenye viingilio vya Simba na Yanga, sidhani kama kuna mtu alishawahi kutendewa hivi katika semina ya neno la Mungu.””

  Nilipokuuliza kuwa umezeeka, ilikuwa ni kutokana na kauli yako hiyo. Na kila nilivyojaribu kuwarudisha ktk mada, wewe na Ziragora, nawaona ni kama santuri iliyochubuka, mmekwamia kwenye hila ya Changizo, hata mlikotoka nayo haijulikani! Tazama hapa mtoa mada anachokisema, nina kopi na kupaste:
  “”“… mara nyingi nasikia watumishi wa Mungu wanasema Mungu amewapa ufunuo fulani ili wawasaidie watu wanaoteseka ktk jambo fulani na wanaandaa semina na kualika watu ili waende wakajifunze, na hapo wanatangaza kuwa kutakuwepo na KIINGILIO kwenye semina hiyo je ni halali watu kulipa pesa kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu? na unakuta semina hiyo imeandaliwa kwenye kanisa fulani, je ina maana wasio na na pesa hawaruhusiwi kwenda kujifunza?
  Mara nyingi nimeona watu wanazuiliwa kwenye milango kisa hawana hela, …”

  Haya, umeyaona mambo yako ya simba na yanga kanisani? Huku ndiko “kuyatazama mambo katika fikra ya majira na nyakati pia” unakokuita? Au ndiko “kupunguza uhafidhina wa kuyafikiri mambo haya” kwa kuyaleta mambo ya dunia kanisani?

  Kuhusu Paulo, sijui hila yangu iko wapi, mimi ninayaona Maandiko hayo kama yalivyo, isipokuwa nimesema wazi kuwa tafsiri ya Kiswahili haiendani kimaudhui na hayo yaliyoandikwa katika KJV, ni vitu viwili tofauti, au wewe unaona ni sawa? Ngoja nivinukuu vifungu hivyo:

  KJV: “What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, THAT I ABUSE NOT MY POWER IN THE GOSPEL.”

  SUV: “Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, BILA KUTUMIA KWA UTIMILIFU UWEZO WANGU NILIO NAO KATIKA INJILI.”

  BHN: “Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, BILA KUDAI HAKI NINAZOSTAHILI KWA KUIHUBIRI.”

  Hayo maelezo niliyoyacap, yana maana sawa?

  Maelezo hayo ya juu unayoniuliza kama sikuyasoma, ninaamini ndiyo yaliyowaongoza watafsiri kukitafsiri hiki kifungu cha 18 katika jinsi hiyo, lakini kifungu hiki kiko kama kilivyo katika hiyo KJV na ujumbe wake ndio huo! Usishangae sana ndg yangu, Mungu aliyajua yote haya mpaka viingilio vya semina, ndipo akaliweka neno hilo ili litusaidie kutuongoza katika Njia yake na kuufurahia Uhuru aliotupatia katika Kristo!

  Gbu!

 89. CK Lwembe Mungu amekupa hekima na ndio maana tukaambiwa Roho Mtakatifu atatufundisha yote. Si lazima yote unayoyafanya yawe yameandikwa neno kwa neno ktk bible hadi usubiri ushahidi wake kimaandiko…

  ..hebu basi ww utupe ushahidi wa kimaandiko (neno kwa neno bila kutafsirisha) wa wewe kupiga mswaki, kuvaa raba&mokasi, kuwa na simu ya mkononi, kuangalia tv, etc

  Sam

 90. Ziragora,

  Kuandika kwako mingi, mimi hakunikwazi maana najua unacho cha kueleza au kufundisha, sina unafiki wa kushutumu mikeka!

  Lakini tukirudi katika Mada, mimi nilitegemea katika maelezo yako utanionesha mahali popote katika Maandiko ambapo kulikusanywa KIINGILIO katika maana ya CHANGIZO, au Changizo katika maana ya Kiingilio!

  Unaponiambia “Sasa wewe Lwembe, kama hutaki, acha!” hii inadhihirisha uoga wa kukosolewa ulionao ambao unakuzuia hata kujifunza! Hapa hatujadili anachokitaka Lwembe, bali “KIINGILIO kwenye semina” je ni halali?!!

  Haya mambo mengine mengi uliyoyaandika, najua yanatokana na kuiogopa KWELI ya Maandiko, kama wale waliohubiriwa na Stefano, nawe nakuona ukiyaziba masikio yako na kupiga makelele sana yasiyo na rejea!

  “AMRI” ni SHERIA, na hakuna Sheria au Amri isiyo na adhabu, ukirudi katika Torati utalielewa vizuri zaidi jambo hili! Na kwa mtazamo wako Kiingilio ni Amri, na ndio ukatuambia tusiotoa Kiingilio kwenye semina tumelaaniwa! Bali hakuna jambo kama hilo, huu ndio Uongo uliozoelewa na kufundishwa na walimu wasio na ujuzi wa Neno la Mungu. Usifundishe jambo usilolielewa vizuri!

  KUAMURU ni Kutoa Agizo, nalo Agizo likiambatana na Sharti hugeuka kuwa Amri! Bali Agizo la Paulo haliwezi kuwa Sheria au Amri kwa sababu haliambatani na Adhabu, ni Agizo lililojifunga katika Upendo na si Hukumu ya Sheria kama unavyotaka kulazimisha! I Wakorintho 16:1-3 “Kwa habari ya ile CHANGIZO kwa ajili ya WATAKATIFU, kama vile NILIVYOAMURU makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
Siku ya kwanza ya juma KILA MTU kwenu na aweke akiba kwake, KWA KADIRI YA KUFANIKIWA KWAKE; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue HISANI YENU mpaka Yerusalemu.”

  Maelezo “KWA KADIRI YA KUFANIKIWA KWAKE” yana denote UPENDO unaoiondoa Amri, kama unaweza kuelewa! Jitahidi kwanza uujue Moyo wa Mungu kwa wanae! Ingawa hutaki matumizi ya vocabulary, lakini hebu tafuta maana ya neno HISANI uone ni nini, maana naona tumerefusha majadiliano kwa wewe tu kuikosa maana ya maneno, KIINGILIO na CHANGIZO ukiyalazimisha kuwa ni neno moja, ili usimamishe fundisho la kuhalalisha KIINGILIO, kwa kuwatishia watoto wa Mungu kwa LAANA wasipoyatii mafundisho yako yasiyo na rejea ya Maandiko! Ndg yangu Mungu hana shida na hekima yako, na wala hakuna technology inayomshtua Mungu, usijidanganye na tumaendeleo twa sayansi twa leo; FUATA instructions! Mungu anataka UTII kuliko hivyo Viingilio vyako!!!

  Watumishi wanaobomoka kwa KWELI ya Neno la Mungu, nawapa pole sana, lakini unaweza ukawahuisha kwa kuwapa Uongo waliouzoea, nalo ni jambo jema maana sharti wawepo kuwakusanya wote wa kupotea ili kusudi la Mungu litimie!

  Ninasubiri ushahidi wa KIINGILIO wa ki Maandiko!

  Gbu!

 91. Tumaini Tumaini…,
  Don’t be honnest and dishonnest at once. Hence, don’t be vuguvugu. Otherwise utatapikwa. Unasema: “MBONA MUNGU WETU ANAPOTAKA KUFIKISHA NENO LAKE HUWA ANAMIPANGO KAMILI?Ndiyo maana nikasema kama ni mpango wa MUNGU KUFANIKISHA NENO LAKE KWA NJIA YA KIINGILIO MAMBO YATAENDA KAMA ALIVYOKUSUDIA”
  After this unachanga hivi hapo ukiwa na hofu:”Na c swala la kusema ooh tutafanyaje semina tucpoweka kiingilio mara sadaka zenyewe hazitoshi kufanikisha huduma iliyokusudiwa!yaani kama tunatumia nguvu zetu vile badala ya kufuata maelekezo ya ROHO MTAKATIFU ANAYETOA “.

  Eh!!! Mungu akiisha panga, it means RM anaingia kati and there’s no “tufanyeje” kwani Mungu ame decide kwamba kiingilio ndio njia pekee mathubuti. Mwl wa semina hatafikiria sadaka ya kawaida kuwa ni kitu cha maana kuendesha semina. Ndio maana unapotazama utaona Semina zinafaulu namna usiyowazia. Hii inathibitisha uwepo wa RM.

  Yesu Kristo akusaidie.

 92. Tumaini rafiki yanagu;

  Mimi hata sikuelewi kusema kweli, maana umesema vizuri kabisa kuwa Mungu huwa hatumii njia moja.
  Lakini katika maelezo yako bado unataka Mungu atumie njia moja tu ya kuinua watu ili ku-support simina.

  Kwani kuna nini mbaya na hii njia ya viingilio Tumaini?

  Huo wasiwasi ulionao wa sauti za watu kusikika kuliko sauti ya Mungu katika vinywa vyao mimi sioni kama ni ya kweli.
  Mbona kuna watumishi wengi tu wanatumia sadaka vibaya, japokuwa watu wamezitoa kwa hiari bila kambiwa watoe kiasi gani?

  Unasema Mungu hahitaji kusaidiwa ili neno lake litimie, hapa napo naona unataka tu kupotosha. Kama unadhani kuweka viongilio ni kujaribu kumsaidia Mungu, basi kaa chini ufikirie kwa upya.

  Tunajua Mungu anaweza hata akatumia mawe yakahubiri, lakini je ulishawahi kuona akifanya hivyo?

  Na unataka kutuaminisha kuwa anayefanya kiingilio kwenye semina basi huyo hajaongoza na Roho mtakatifu? maana naona unasema huko ni kutumia nguvu zetu pasipokufuata maelekezo ya Roho.

  Maana ya kuongozwa na Roho mt.na kwenyewe sijui tunakuelewaje. Ivi lazima tusibiri Roho mt.mpaka atuambie kufanya kila jambo ndipo tufanye?

  Jaribu siku moja kukicha usiamke kitandani mpaka akuambie!

 93. Lwembe;
  Hujanijibu nilichokuuliza, halafu unasema ngoja unisikilize kwanza unajua nina neno!

  Tafadhali twende sawa Lwembe. Swali ni hili: ”ni nini hicho ambacho hao wenye kufanya hiyo huduma wamekipokea bure, hivyo wanatakiwa kukitoa bure pia?”

  Labda niongeze na jingine;
  Je tunachotakiwa kuangalia ni uwepo wa hicho kiingilio au matumizi yake ?

  Nangojea!

 94. Lwembe,
  Jaribu kuwa muungwana na kukumbuka kuwa huu si mdahalo wa nje ya nyumba ya Mungu.
  Ninasema uwe muungwana hasa katika kutoa fafanuzi ambazo hazina hila ndani yake. Kwa saehemu kubwa ulivyomjibu Ziragora, umemjibu kwa hila.

  Ona mfano huu wakati unafafanua maana ya kiingilio;
  ”KIINGILIO = ENTRANCE FEE (unalipa pesa mlangoni au kwa muuza ticket, kama ni elfu 50,000/= basi unalipa hizo ndio unaingia. Ukitaka kulipa zaidi, ujitolee, labda shs 70,000, yule mpokeaji atakataa kuchukua hiyo iliyozidi labda ufikishe iwe 100,000, ili akupe ticketi nyingine ambayo unataamua mwenyewe ufainyie nini. Na ukiwa na pesa pungufu, hauingii, askari wanakuzuia!)”

  Tafsiri hii kwa rejesta ya kanisani haiko sawa, umeiweka hivi kwa ajili kutetea msimamo wako juu ya mada hii. Na hizi ni hila za kutokutaka kusema ukweli wa uhalisia wa kinachofanyika katika semina za kikristo zenye viingilio.

  Haya uliyosema wewe ni mambo yanayofanyika kwenye viingilio vya Simba na Yanga, sidhani kama kuna mtu alishawahi kutendewa hivi katika semina ya neno la Mungu.

  Kisha ulimwambia kuwa changizo hazilazimishwi.
  Ni kweli hazitakiwi kulazimishwa, hata mimi nakubali Lwembe.
  Lakini je kwani viingilio vinalazimishwa? Ukiona kimesemwa kiwango ambacho humudu, kwani ni lazima uende jamani?
  Hakuna semina ambayo ilishawahi kufanyika kila mtu akaenda,iwe ya bure au ya kiingilio. Wengine wanataka mpaka na magari ya usafiri wapelekewe milangoni mwao ndipo waje kwenye semina, na huu mtazamo uko Afrika zaidi

  Halafu, neno changizo na neno kiingilio ni lugha za kifasihi tu, wala si maneno hayo yanayobeba dhana nzima ya tunachojadili hapa.
  Kwani ukiambiwa ili kuingia kwenye semina fulani lazima uchangie kiasi chochote ulichonacho, hicho hicho kiasi chochote tutakiita nini, changizo au kiingilio?
  Au ukaambiwa lazima uje na daftari la kuandika, ukiwa huna huingii. Hilo daftari ni kiingilio au sio kiingilio?

  Mbona kwenye harusi tunatoa sana maelfu ya pesa,mbona sijawahi sikia mtu anasema huwa tunalazimishwa kutoa hizo hela zinazoitwa michango wakati ni viingilio, si huwa tunatoa kwa kupenda kwetu? Unatoa laki moja unapata chakula kisichofika hata sh.elfu tano gharama yake.
  Na sina uhakika kama Yesu alikuwa amelipa mchango wa harusi pale mtaani kwao Kana ya Galilaya!

  Na je kijana Yesu angesikia kuna sehemu wanafanya semina,lakini lazima uchangie dinari 20, angeenda kwenye hiyo semina au asingeenda?

  Ni vizuri kuyatazama mambo katika fikra ya majira na nyakati pia. Mitindo na lugha za mambo hubadilika kulingana na wakati,lakini lengo hubaki lilelile. Ni vizuri tukapunguza pia uhafidhina katika kuyafikiri haya mambo.

  Lakini pia Lwembe umejaribu kufanya hila kwenye kuitafsiri hiyo 1Kor 9:18.
  Kwa kifupi ni kwamba, Paul kama alivyoamua kutokuoa,aliamua pia kutotumia haki zake fulani za kitumishi kwa ajili ya makusudi yake mwenyewe, kulingana na lazima ambayo Mungu alikuwa amemwekea (yeye Paul) moyoni mwake kwa ajili ya kuihubiri injili.

  Kwa hiyo Paul, aliikataa mwenyewe hiyo haki yake ya kitumishi ya kula kwa kazi ya injili. Sidhani kama Lwembe hujasoma kuanzia mstari wa 13-18.
  Ndio maana nahisi unafafanua vitu kwa hila.

  Asante Lwembe!

 95. Ndugu John Haule, binafsi nauheshimu mchango wako.

  Naomba tu unisaidie zaidi katika yafuatayo:

  Umesema hivi ”Injili ni bure kwa hao walengwa wa hiyo huduma haijalishi kuna chakula/AC/Usafiri.kuwaambia watakaoudhuria ni lazima uchangie ndipo upate huduma, Hayo ni makusudi yetu wanadamu si ya Mungu”

  Unaweza ukanithibitishia hayo maneno yako kibiblia?

  Tena ukasema;
  ”Wainjilisti wakubwa(wa Bwana)hawafanyi chagizo kwenye mikutano yao ya kupeleka injili kuna wanaobeba hiyo gharama kwa moyo wa kupenda/kwa kusudi la Bwana”

  Swali; kwani wanaotoa viingilio kwenye semina wanafanya hivyo kwa kulazimishwa au kwa moyo wa kupenda pia?
  Na huko kutoa hicho kiingilio sio kumtolea Bwana?

  Ubarikiwe!

 96. Lwembe,

  Kiukweli sione jinsi mtu mzima anawezajichanganya kwa mada hii akijiruhusu kuingia ndani ya vocabulary tu. Mim nitakuvumilia tu kwa kuchanganyikiwa kwako, kuwa na maoni tofauti, lakini ufikapo wakati unapojikazilia kunena wongo hiyo ni jambo lingine.

  Maneno kiingilio/viingilio na Changizo kam maneno tu siyo problem. Mtu mzima anafikiri ile hela inafanya nini. Ndio maana nikakuomba kuwauliza wanaoendesha hizo semina kama wanatumiaje hela. Na sasa unakurupuka tu kusema mim ninafanyisha semina. Umeniona wapi nikifanyisha semina ndugu yangu? Wewe Lwembe, unayo tatizo kubwa ya kutafuta chini-juu kuchonga uwongo !!! Usipime kufunika kutoelewa kwako kwa kutaka kuonyesha mimi natetea interests zangu. Kitu kinachonisukuma nijadili na wewe ni kukukataza kushawishi wengine wasifwate neno la Mungu kwani wewe Lwembe hutaki lipa kiingilio chako. Hiyo ni kupotea mara mbili kwani kwanza wewe unapotea kiisha unatafuta upoteze wengine.

  Kweli sikushurtishe kutazama vizuri kama wewe ni mwana wa upotevu. Lakini ukiwa umejaliwa neema itokayo kwa Mwenyezi Mungu, pima kuchunguza kama fedha hio inaenda wapi na inafanya nini. Pima vile vile kulinganisha maneno unayosema na ya wengine wote, wakiwa kwa upande wako au la, ndipo utajua kam unanena yaliyo uharibifu.

  Ni heri ueelewe kama jinsi Paulo alitoa bure neno licha ya kuamuru KILA MTU atoe changizo, vile vile semina inatolewa bure licha ya kuomba ANAETAKA atoe KIWANGO FULANI cha hela. Tena nikakuambia : pima kueleza mbele ya wakati shida ya ukosefu wako kifedha uone kama hutagaramiwa na kuingia kwenye semina. Jesus !!! Sasa Lwembe unataka tukufanyeje ? Isitoshe, semina inasaidia alieokoka kukua. Ina maana kam hujaokoka hutaielewa. Upande mwengine semina (kam mafundisho) inapewa bure. Kuna mambo Paulo alikuwa hafanye kufwatana na technology ya ile wakati, na Mungu hakuleta ile technology mapema angalau aliijua. Mungu anayo taratibu ya ajabu!!! Unajua, msaada kwa watakatifu hauna kipimo, lakini kurikodi kanda moja ni garama kamili, bei inajulikana. Ndio maana Mungu kwa uhuru wake katika kuongea na watumishi wake, pengine akawafunulia kutia kiingilio. Sina uhakika wowote kwa jinsi alivyoongea na watumishi wake kama vile wakati alipoambia Paulo juu ya changizo hakushirikisha mtu mwengine. Kitu ninachofahamu ni kwamba kinachoruhusiwa na Mungu kinafaulu na kinadumu. Unafikiri Mungu anaweza kubali jina lake lisemeke kiasi hicho kwa njia ya hila? Wanaotumikia Shetani nao wako, wanaweza tumia hata neno changizo lakini utawaona wakisema zaidi “mungu wangu akubariki”, wanaogopa kulitaja Jina la Yesu na hata wakati wanapima litaja wanaogopa weka “Kristo”. Tunawatambua bwana….

  Nilijaribu kukuelezea lakini unakua kam mwenye kutosikia. Nilikuonyesha kama kazi changizo ilioamriwa na Paulo na hivi viingilio inafanana kwani yote ni kwa lengo inayofanana. Mim sikukwambia kam kwa maneno tu kiingilio na changizo si maneno mawili tofauti. Lakini tukienenda kwenye utofauti wa tamko hata Biblia hatutazisoma kwani yawezekana katika tafsiri moja ya Biblia utakuta maneno tofauti ndani ya aya tofauti lakini ikiwa ina lengo moja. Sasa tunapofika kwenye tafsiri nyingine unakuta maneno ni tofauti zaidi. Ndio maana kwa mtu mzima, maoni yanasimamia kwenye lengo. Lakini wewe nakuona ukipoteza lengo na kuendelea kugaagaa ndani ya vocabulary. Hivi unawaza kuna afikae kwenye SG na hajue hii vacabulary inayokupotezea muda ?

  Nakuomba ukiwa na ya kukanusha kwa hii ninayotamka kwa num 1 & 2 go on :
  1. “Agizo la Paulo : Watu wote watoe, kadri ya mafanikio yao, ifanyike kabla awasiri, kwa kumgaramia na kugaramia wafanyakazi pamoja naye(usafirishaji na stay), sehemu ingine ipelekwe Yerusalemu kwa ajili ya kusaidia watakatifu”.
  2. “Wanaoendesha Semina: Mwenye kupenda atoe kiwango Fulani kinachojulikana, ifanyike kabla hajaingia, kwa kugaramia muendesha semina na wale wanaotumika naye(kulipa nafasi semina itafanyikia na usafirishaji wa watu na vifaa), sehemu inayobaki kwa kurikodi kanda itakayopeperushwa kwenye radio ili isaidie wale ambao hawakuweza pata ile hela na wengine wote labda ambao wako mbali ao hawakupata taarifa”

  Nimepima eleza kidogo lakini nafikiri wanaoendesha semina wana mingi ya kuongeza.

  Nataka uelewe kama Paulo hakugaramiwa kama Yona au Eliya. Mungu anatumia njia anayopenda, hapana kumtilia mipaka. Yeye Paulo alitafuta garama katika waumini. Lililo kweli ni kwamba alifanya iwezekanayo asilemee watu sana. Waendesha semina, sidhani kama wao wanalemea watu. Kwanza hawazifanye kila siku, ya pili hawashurtishe watu kulipa kiingilio. Hata mwenye amepinga, kwa mwisho mara nyingi anapata mafundisho kupitia radio ndogo sana anayo nyumbani, ao ndani ya simu yake ya mkono; very simple…

  Fikirini kam watu wa Mwanza, Moshi, Morogoro, nk wanaambiwa kam wachangie lakini wanayochangia ni kwa watakatifu na ni lazima ifike Dar!!! Unawaza watu hawataanza jiswali kwa nini tu Dar? Nasi hatuna watakatifu? Lakini inapotajwa Yerusalemu, unadhani ilikuwa neno rahisi kuzungumza au ni mapenzi ya Mungu kuliko kitu kingine chochote.

  Ukitazama superficially, utaona kuna tofauti, lakini isingelihesabiwa kwani pengine inafwatana na jinsi wakazi wako. Mwalimu wa semina pengine alionyeshwa kam ukiwaamuru wakazi wote kutoa hawatafanya. Na tena si jambo lifanyikalo kwa kanisa(jengo) moja. Hawezi amuru makanisa mbalimbali kuchangia. Ndio maana anatafuta wanaotaka tu. Sasa wewe Lwembe, kama hutaki, acha! Unafahamu kam hata wakati wa mitume, wa kina Anania na Safira walikuwepo. Kwenye Semina, Anania na Safira ni wale wanaosema eti walimu wameomba hela ambazo hawawezipata wakati wanazo nyingi.

  Unasema Mungu anajishughulikia, ndio, lakini alieleta mada hakusema kama waendesha semina hawafaulu kwani Mungu hakuwasaidia au kama wanalalamika kufwatana na jinsi hawafanikiwe. Nafikiri kama una tatizo kam lile hebu utuambie kama semina hazipati watu ao kama uwezo wa Mungu haudhihirike ndani ya semina ulizoshiriki binafsi. Ndugu, katika mijadala jaribu kuwa mkweli, itakusaidia na wakusomao watasaidiwa. Tena fahamu ya kwamba hata kunaweza kuwa tatizo, na mitume nao walipata tatizo licha ya msaada wa Mungu.

  Wewe ni specialist wa uwongo kwani hata lililokweli unaligeuza uwongo. Nakuomba ufafanue namna gani neno “KUAMURU” halihusiane na « AMRI ».

  Kwa maneno mengine kama nukuu ya Yesu, mimi nilisema kwa lugha yangu(style yangu) na sikulenga changizo, bali utoaji; changizo ikiwa mojawapo wa namna za utoaji. Nililenga kugaramia na kukaribisha. Kwa sababu unaendelea kukwaa kwa kutafutisha kwenye vocabulary kama mtoto mdogo aneona box bila kujali kilichomo, acha nimnukuu Yesu kama vile labda utakavyopenda, na msomaji aone kama kukaribisha na kugaramia watumishi wa Mungu ni baraka lakini kutowakaribisha na kutowagaramia ni laana. Na vile kwamba mtumishi wa Mungu anastahili ujira wake utokao kwa wale awahudumiae:
  “Luka 10:
  4 Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani.
  5 Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu;
  6 na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu.
  7 Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
  8 Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;
  9 waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.
  10 Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni,
  11 Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.
  12 Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.”

  Sasa wewe, kwa nini unashughulika na njama za kubomoa kazi ya watumishi wa Mungu bila kujenga hata nafasi moja. Unajua Shetani ndiye mwizi, mwongo na mharibifu. Si vema zaidi uendeshe wewe pekee semina ao namna ingine utakayoibandika jina kwa real copy ya wakati wa mitume kam jinsi unavyodai, kiisha uonyeshe tofauti ya ile yako na ya wale wengine? Unajua ndugu yangu, kuenenda kama unavyofanya kwa kudharau kazi ya watumishi wa Mungu hapa kwenye SG bila wewe kuonyesha unayoifanya hii si ungwana. Angalia vizuri usiwe na roho ya kishetani ya kuharibu tu.

  Ninajua nitakupata tu polepole. Usijali, kuna siku ambapo hutaweza nilazimisha kuandika mingi.

  Bwana wetu Yesu Kristo akuwezeshe.

 97. Sungura,

  Mt 10
  “1And when he had called unto him his twelve disciples, he gave them power against unclean spirits, to cast them out, and to heal all manner of sickness and all manner of disease.
  ….
  8Heal the sick, cleanse the lepers, raise the dead, cast out devils: freely ye have received, freely give.”

  Yeye Kristo ndiye mwenye kuilipa gharama! Ndipo hakuna anayeweza kufanya lolote lile bila ya Yeye, sana sana utaishia kutoza viingilio au kuwatisha wateja wako watoe pesa la sivyo watalaaniwa! Au ukaishia kukiuza kipawa ulichokirimiwa, km ni cha kuombea wagonjwa nk; lakini Injili ilisema “kwa kupigwa kwake sisi Tulipona”! Hatuponi hapo tunapoombewa, bali tunaupokea tu uponyaji wetu tuliofanyiwa miaka 2000 iliyopita, sembuse hizi semina!!!

  Ngoja nikusikie kwanza, najua unalo neno!

  Gbu!

 98. To be honest jambo hili la kiingilio lipo complecated!nasema hivyo kwasababu MUNGU wetu c wa kanuni moja na inawezekanaje kila anayekuja na maono aone njia ya kufanikisha maono yake ni kuweka kiingilio?MBONA MUNGU WETU ANAPOTAKA KUFIKISHA NENO LAKE HUWA ANAMIPANGO KAMILI?Ndiyo maana nikasema kama ni mpango wa MUNGU KUFANIKISHA NENO LAKE KWA NJIA YA KIINGILIO MAMBO YATAENDA KAMA ALIVYOKUSUDIA!Wasiwasi wangu ni kwamba watu wanaweza wacwe waaminifu badala ya msauti ya MUNGU KUCKIKA KWENYE VINYWA VYAO INACKIKA SAUTI YA MAWAZO YAO THTSWHY UNAWEZA KUONA KILA MAONO YANAKUJA NA STAILI YA KIINGILIO!MUNGU ATUSAIDIE KWAKWELI KATIKA HILI!Naamini kabisa MUNGU WETU ANAWEZA SANA WALA HAITAJI KUSAIDIWA ILI NENO LAKE LITIMIE ANAWEZA KUINUA WATU ATAKAVYO ILI KUKAMILISHA KUSUDI LAKE!Na c swala la kusema ooh tutafanyaje semina tucpoweka kiingilio mara sadaka zenyewe hazitoshi kufanikisha huduma iliyokusudiwa!yaani kama tunatumia nguvu zetu vile badala ya kufuata maelekezo ya ROHO MTAKATIFU ANAYETOA MAELEKEZO SAHIHI.

 99. Ziragora,

  Usiwe mtu wa maneno mengi yasiyo na rejea! Unapochangia jambo jaribu kulielewa kwanza, usijikurupukie tu! Mada inazungumzia “KIINGILIO” wewe umeibadili mwelekeo na kuanza kutujadilisha CHANGIZO, huku ndiko kusoma superficially!!!

  KIINGILIO = ENTRANCE FEE (unalipa pesa mlangoni au kwa muuza ticket, kama ni elfu 50,000/= basi unalipa hizo ndio unaingia. Ukitaka kulipa zaidi, ujitolee, labda shs 70,000, yule mpokeaji atakataa kuchukua hiyo iliyozidi labda ufikishe iwe 100,000, ili akupe ticketi nyingine ambayo unataamua mwenyewe ufainyie nini. Na ukiwa na pesa pungufu, hauingii, askari wanakuzuia!)

  CHANGIZO = COLLECTIONS (ni michango inayotolewa kwa nia/kusudi fulani, haina kiwango, ni free will, kulingana na moyo na uwezo ulionao, haina masharti. Hii ndio aliyowaamuru Paulo, iwe ni kwa ajili ya KUWASAFIRISHA au kusaidia Watakatifu!)

  EliyaWilliam anasema hivi:” … Hivyo kuchangia kwa kutoa kiingilio hilo ni jambo zuri tu sioni kuwa ni tatizo.” Unaona ulivyochangia kumpoteza mwelekeo? Naye anasema kama wewe, eti UNACHANGIA KIINGILIO!!! Hivi kuchangia kiingilio ndio kitu gani?? Acheni hila za lugha!

  Umeandika mambo mengi sana yasiyo na uhusiano wowote na Mada! Nakuona unavyojaribu kuligeuza neno alilolisema Paulo, “Kwa habari ya ile CHANGIZO kwa ajili ya WATAKATIFU, kama vile NILIVYOAMURU…”, kwamba “ALIVYOAMURU” unataka kuligeuza jambo hilo kuwa ni “AMRI” na hivyo unaliambatanisha na ADHABU ya kulikiuka kuwa ni LAANA! Angalia unachoniambia: “Sasa nakuona wewe Lwemba na wapambe wako mukichagua laana!!!” Ni wapi Maandiko yanasema usipotoa changizo unalaaniwa! Ndg yangu usicheze na LAANA! Kwa aliyeondolewa katika Laana ya Sheria kwa Damu ya Kristo, akijirudisha huko, hakuna tena namna ya kutolewa humo! Kwa mfano, unapofundisha kuwa asiyetoa changizo analaaniwa, ni wapi Paulo amefundisha neno hilo? Usifundishe tofauti na mitume utaishia kulaaniwa bure!! Huku kucheza na Maandiko unakokufanya ndiko kujitoa muhanga!!!

  Changizo hazilazimishwi mtu na wala haziombwi! Hii habari ya kwenda kuwaomba wafanya biashara wasiookoka wachangie mambo ya ndani ya kanisa ni udhalilishaji wa kazi ya Mungu! Michango inatolewa na watu ambao wameshawishika na Injili na sasa INAWAHUSU! Na nimekuambia kwamba Mungu huwainua wote anaowataka kulishughulikia jambo lake, watoaji na wapokeaji, na kazi yake haijawahi kushindwa, kwahiyo usimuhusishe Mungu katika udhaifu wako wa kuukosa Ufunuo au Ono na hivyo kujiridhisha kwa viingilio! Hata nukuu ya Yesu alipowatuma wanafunzi wake umeitumia mahali ambapo si pake, Mt 10:12-15
  “Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi” sasa jambo hili lina uhusiano gani na Kiingilio cha semina? Kwamba Yesu aliwatuma wanafunzi wake wafundishe semina na kutoza viingilio? Usipandanishe mambo ndugu yangu, utajipoteza porini!

  Kuhubiri Injili au kutenda kazi ya Mungu si ‘lele mama’, ni lazima uwe na Uhakika wa mawasiliano na Mungu kwanza ndipo na Ujasiri udhihirike kwako kama unavyomuona Paulo Jasiri AKIAMURU machangizo na ndani ya huko KUAMURU, kumejaa UPENDO wa Kristo wenye kufurikisha Neema, mwenzako anayaona yote katika ulimwengu wa Roho yakitimia kabla hata hajayasema. Au wewe na semina zako za Viingilio, ukawa umekwenda Yerusalemu, je, kwa mawazo yako unafikiri wapendwa wale ambao Paulo anawakusanyia machangizo huku wangeweza kulipia semina zenu hizo?

  Huyu hapa Paulo, kwa Roho Mtakatifu anakataza Viingilio, 1Kor 9:18 “Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama …” Hii tafsiri ya haiko sawa sana, tazama hapa KJV, “What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, that I abuse not my power in the gospel.” Unaona, Viingilio ni kucharge! Paulo angeweza kucharge kama ninyi, lakini hataki kuitumia vibaya au kuichafua, au kuidhalilisha mamlaka aliyonayo katika Injili, kama mnavyofanya ninyi akina Ziragora!!

  Gbu!

 100. Lwembe,

  Nadhani unayo vile ya kujibu kwa Ndg Sungura. Lakini ninachoona zaidi ni kwamba unasoma very superficially maandiko ya wengine, na dalili ya kushindwa kwako ni kuchekacheka wakati tunapozungumza maneno muhimu hapo ukikosa jibu kamili.

  Kwa hivi siendi mbali wakati unapojiruhusu kudai kwamba Paulo alichukua changizo kwa ajili ya upendo wakati mimi nilionyesha kwa herufi kubwa mahali anapoamuru akisema kama ni kwa usafirishaji wake, na kwa stay yake anapofika eneo lile. Pamoja na usafirishaji wa Timotheo pia stay yake, na wengine wanaotumika pamoja naye.

  Paulo hasemi kam neno analowaletea lina bei, lakini kusafiri, kulishwa, kulala ilikuwa shurti. Tena akasema kila mtu afanye ile, na isitoshe afanye changizo kabla yeye Paulo hajawasiri. It’s very clear.

  Sasa wewe Lwembe, acha mambo ya kitoto na uonyeshe kikweli tofauti kamili ya Paulo na walimu wanaoleta semina. Tunaongea tunayoyaona kwanza, usijifiche kule ndani ya kiroho hapo ukidanganya; ile ni unafki.

  Kwangu nawaona wote wanaomba wasafirishwe, wapokelewe kivifaa, tena watu wote walete michango yao. Walimu wa semina hawafanye tofauti, nawo wanaomba viingilio. Uwaulize wanafanya nini na ile viingilio, najua hawatakuambia zaidi ya Paulo. Paulo hakusema kubaki hata mmoja atakaekosa changizo. Sasa wewe unaona tu tofauti ya kiingilio na changizo. Yote ni sawa, kwani inahusu watu wote bila kuwahurumia eti wao si matajiri. Paulo alijua kama hataenda kwa wana siasa au wafanya vyashara wasiookoka ndio warahisishe kazi ya injili. Kazi yake ilirahisishwa na wale atakaowahudumia. Full stop. Na wengine wenye kupana mifano ya wa akina Yona, Elia, ile ni mambo tofauti ambayo hatuoni tena ndani ya agani jipya ambapo si manabii, bali mitume ndio wanatumika. Ndio maana Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwaambia wasienda na kitu chochote. Watakapofika nafasi, atakaewahudumia atabarikiwa na aakaekataa atalaaniwa. Sasa nakuona wewe Lwemba na wapambe wako mukichagua laana!!!

  Lwembe, hata unafanya je hutabadili maandiko. Na kwa wengine wote, nawaomba kufungua macho vizuri muone ukweli.

  Asante.

 101. Hahahahaha … Ziragora!

  Najitoa muhanga, hapana; wanaolikataa au kulitafsiri Neno la Mungu wapendavyo ndio wanao jitoa muhanga!!

  Umenukuu vizuri sana Maneno ya Paulo, labda uyarudie tena ili uone kama yako sawa na hili tunalolijadili. Ninachokiona katika maelezo ya Paulo ni CHANGIZO kwa ajili ya Watakatifu, ALIWAAMURU wawachangie WATAKATIFU walio katika dhiki ya mahitaji huko Yerusalemu, lakini HAKUWAWEKEA KIWANGO specific! Yaangalie haya maelezo:
  Rum 15:25-27 “Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu; maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini. Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili.”

  2Kor 9:6-7 “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, WALA SI KWA LAZIMA; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”

  Halafu katika hivyo vifungu ulivyovinukuu, haukukiona kifungu hiki ambacho kingeyaweka sawa mawazo yako? “3 nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.” Unaona, hizo changizo zote zilikuwa ni HISANI!!! Hata katika kuwahudumia watumishi pia, mambo yao ya mwili, CHANGIZO ndizo hutumika na si VIINGILIO, maana viingilio ni sawa na kukiwekea“bei” kipawa cha Mungu ulichopewa bure!

  Pia elewa kwamba watumishi wa Mungu wanafanya kazi kwa UFUNUO, hawabahatishi! Uwepo wa Mungu huwatangulia, nao Watakatifu huwekwa katika hali ya kuwahudumia kama anavyofundisha Paulo hapo juu. Anachokifundisha Paulo ndio Mwongozo kwa Watakatifu, ukiona wanatoza viingilio tafuta kwanza kwenye Maandiko mahali Mungu alitoza kiingilio!

  Kabla ya kufanya jambo lolote, mtumishi yeyote hungojea maelekezo kutoka kwa Bwana wake, ndio maana Paulo anasema watamsafirisha kokote atakakoenda, ni lazima ayajue Mapenzi ya Mungu ni kwenda wapi! Hata hao wenye Semina iwapo wangekuwa ni wale wenye kutumwa na Mungu, wangesubiri maelekezo, maana Mungu huwatayarisha “samaki” wenye ‘gold coins’ kwa ajili ya kugharamia mambo ya watumishi wake, Paulo analifahamu jambo hilo! Litazame pia kaburi alilozikiwa Kristo, si unaona Yusufu alivyojitokeza katika saa aliyohitajika!

  Kutoza VIINGILIO ni ishara ya kutokuamini kwamba Mungu ataihudumia Semina! Huenda ni zile semina zinazoandaliwa kwa ushawishi wa waandaaji na makanisa kuhusishwa, hizo huishia kuwakamua waumini, na wakijua mnenaji anauzika, basi wao hupiga viingilio kwa lugha laini ya kuchangia gharama! Na kama watakuambia ni bure, basi robo tatu ya mahubiri itahusu sadaka na mafanikio ya mtoaji!

  Karibu & Gbu!

 102. Bwana Yesu asifiwe,

  Wachangiaji wote mmechangia vizuri, Bwana Yesu awabariki,
  Tofauti ya hoja zetu ipo kwenye njia ya kupata hiyo pesa ya kupeleka injili,

  Kuweka kiingilio hiyo siyo njia sahihi ya kibiblia,kama Kuna wito/kusudi la Bwana ktk huduma Bwana mwenyewe ataweka/atainua mzigo kwa watu wake ili hilo kusudi litimie kama ni semina ya ndani au makutano ya nje.

  Ukisoma LK 8:1-3 Utaona kulikuwa na wamama waliokuwa wanamuhudumia Yesu(huduma)kwa mali zao,

  Hata wakati wa Mitume kulikuwa na wamama wengi wamatajwa waliokuwa wanagharamia hizo huduma km Mariam mama yake Marko.

  Injili ni bure kwa hao walengwa wa hiyo huduma haijalishi kuna chakula/AC/Usafiri.kuwaambia watakaoudhuria ni lazima uchangie ndipo upate huduma, Hayo ni makusudi yetu wanadamu si ya Mungu,

  Wainjilisti wakubwa(wa Bwana)hawafanyi chagizo kwenye mikutano yao ya kupeleka injili kuna wanaobeba hiyo gharama kwa moyo wa kupenda/kwa kusudi la Bwana,

  Maandiko yanasema ukishamjua Bwana ni vizuri kutoa kuliko kupokea.

  Mbarikiwe ndugu wote ktk ushirika huu mtakatifu.

  Amen

 103. Lwembe;
  Naona una hoja,japokuwa bado umeifumbafumba.
  Na hoja hiyo ipo kwenye hilo andiko la Mt.10:8, hasa kile kipengere cha mwisho. (Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.)

  Hebu tujadili sasa, ni nini hicho ambacho hao wenye kufanya hiyo huduma wamekipokea bure, hivyo wanatakiwa kukitoa bure pia?

  Tujadili!

 104. Ndugu yangu Lwembe,

  Angalia pia ile aliobandika Ndg EliyaWilliam. Semina inafika kwa wale amboa tayari ni wakristo, wameokoka. Si rahisi yule ambaye hajaokoka, licha ya kuwa ana hela nyingi, azitoe kama changizo kwenye maandalizi ya semina. Ataziwapa malaya, atazitumia ndani ya vileo, na fasi ya music nyingine, nk. Ni wachache sana wa namna hiyo wanaojaribu kuingia kwenye semina. Semina inaviziya zaidi mukristo ili akue ndani ya neno la Mungu. Na moja wapo wa kukua ndani ya neno ni kujifunza utoaji kwani kupitia utoaji mna kumuogopa na kumtii Mungu. Sasa wewe unataka ukue lakini ukikwepa utoaji! Jesus!!!! Hii haitawezekana!
  Si vibaya semina iwe na lengo la kuonyesha kam wakristo wanao rights ya mafanikio.
  Kupitia semina, ile kiingilio inakusaidia kuendelesha injili bila kuwa muinjilisti anaejulikana na watu. Changizo lako linasaidia kwa kusafirisha muinjilisti, ku ricodi mafundisho na kuchapisha vitabu ambavyo vitawezafikishiwa watu mara nyingi kwa urahisi. Pima kulinganisha bei ya Biblia na ile ya dictionary, utaona kam Biblia inapatikana kirahisi, hata kam si kwa bure. Sasa kam ulichanga kwenye semina na hapo kukatoka kitabu kama kile, unafikiri Mungu hatakubariki? Ukidhani ni wengine tu watakaojitoa kwa kazi ya Mungu, wewe si mukristo. Na kama ni hivyo, utuambie tujue tunaongea na kina nani.

  Nimeona kama una shida ya kutofautisha semina na maandamano ya kiinjili. Semina kwa kiini chake haina lengo ya wokovu, lakini kwa sababu Mungu anaokoa anapotaka, kuna wachache ambao wanaingia sawa kwa mchezo tu na wanatoka wakiishaokoka.
  Maandamano ya injili ni kwa watu wote, yanafanyiziwa hadharani ao ndani ya makanisa, lakini haina kiingilio. Ile inalenga kuleta wasiyookoka kwa wokovu. Tazama vizuri,ndugu yangu, fanya uchunguzi, utaona hata wahuduma hawatumike sawa sawa kwani lengo ni tofauti. Na moja wapo wa semina ni vile vile kukufundisha namna ya kuleta watu kwa Mungu kwa namna zote.

  Wewe unasema yeye anaetayarisha semina atafute support nafasi nyingine, sasa Paulo alikuwa akisafirishwa na kugaramiwa na watu wengine isipokuwa wale anaowahudumia? Unawaza ile garama inatoka wapi? Kwa taarifa yako, kiingilio hakilipi semina(maneno inayojifunzwa), kinalipa nafasi inapofanyikia, usafirishaji wa vyombo na watu, chakula au kinywaji ikiwezekana. Unapoombwa kiingilio wewe unawaza unalipa Semina, nani akakwaambia vile? Kama hujue inafaa unauliza. Semina(mafundisho) haina bei na inapewa bure. Hio pekee ndio mhuduma anayo, aliipewa bure na anaitoa bure. Vifaa ni jambo lingine. Wenye walifwata Yesu, walijigaramia: aliyekuwa na ngamiya aliitumia, aliekuwa na mikate aliitwaa, aliekuwa na samaki halikadhalika. Na kufwatana na ile walikuwa nayo Yesu akaingiza baraka. Haleluya!!!

  Na tena kuna kutofamu juu ya mambo ya unabii. Leo hakuna nabii kwa jina kama ya zamani. Yesu yeye pekee alisema kama Yahana ndiye aliekuwa nabii wa mwisho. Ndio maana tunakataa yule anaeleta unabii ingine. Leo ni mitume(wachungaji, wainjilisti,wazee,Askofu, nk). Humo ndimo Mungu anachipusha ufafanuzi wa neno lake na hii ndio tunayosema unabii kwa leo. Lakini ukiona vizuri ni tafsiri ao maelekezo ya ile iliosemwa na manabii tangu zamani(Ina maana, unabii wa leo ni ukumbusho wa unabii wa zamani).

  Yesu anasema hivi:
  “Mathayo 11 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
  13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
  14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
  15 Mwenye masikio, na asikie.”

  Asiongee kitu usichokijua, acha wanaojua maana ya semina wasaidie alieleta mada. Inatakiwa kutoa kiingilio ili uingiye kwenye semina. Usihesabu kama umepoteza kwani utakayopata mi mingi zaidi(utapata baraka, elimu, utaburudishwa kwa nyimbo wala hukuchanga kwa ile music instruments, utaketi, na kam itadumu saa nyingi utapewa soda, nk). Hah! jamani…. kweli utakuwa umetoa changizo inayotoshelea?

  Jesus bless you!

 105. Ndugu Lwembe,

  Naona unataka jitoa muhanga ili unipinge pasipo sababu. Lakini utajikwaa kwenye maandiko. Acha nikupe ile maandiko kwa urefu. Kama unayo RM kabisa utaona Paulo hakupendelea huduma iwe pasipo mhudumiwa kuhusika kwa mapokezi, usafirishaji, nk. Isitoshe, hii ilikuwa agizo kwa kila mtu. Na hawa wenye kuendesha semina, wengi ni vile nanafanya. Hapa sijasema kama hakuna wanafki humo humo, wasio na RM, wenye kupenda fedha tu. Lakini wawe au wasiwe, ukweli unabaki pale pale. Unasema ni kwa upendo, ndio, sijaona vile vile mwenye kuendesha semina akilenga chuki. Anayotaka ni namna injili ifike fasi yote kwa mchango wako na wewe. Kwa nini unataka ule pasipo kutumika?

  “I Wakorintho 16: 1 Kwa habari ya ile CHANGIZO kwa ajili ya WATAKATIFU, kama vile NILIVYOAMURU makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
  2 Siku ya kwanza ya juma KILA MTU kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
  3 nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.
  4 Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.
  5 Lakini nitakuja kwenu, nikiisha kupita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.
  6 Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate KUNISAFIRISHA ko kote nitakakokwenda.
  7 Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.
  8 Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste;
  9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
  10 Lakini, Timotheo akija, angalieni AKAE KWENU pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe;
  11 basi mtu ye yote asimdharau, lakini MSAFIRISHENI kwa amani, ili aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.”

  Kwa upande wa Yesu, naye aliomba garama, apana ya hela lakini ya bidii kumtafuta. Ndio maana anasema anaingia mahali wanapofungua. Na siku moja akiwa hekaluni akatambua mjane alietoa zaidi kwani alitoa na moyo tayari. Pengine walimu wanaomba mingi sijue! Hebu pima kujieleza mbele ya wakati kam wewe huna kitu, labda utaingia tu. Lakini si vizuri ukae kimaskini na ujihuzishe na kuwatupia mawe hao walimu.

  Kwa siku za agano la kale mambo yalikuwa tu wazi:
  “Kumbukumbu la Torati 16:16 Mara tatu kwa mwaka na watokee wanawaume wako wote mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za Bwana mikono mitupu.”

  Kama wewe hutaki, utaona wenye kutaka ni wengi. Hata wakati wa Yesu si wote walimfwata. Ukitaka kumfwata, achilia, toa, Bwana!!!

  Tutaendelea.

  Asante.

 106. Mt. 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”

  Binafsi sidhani kwamba kuna tafsiri ya kifungu hiki inayokizidi kifungu chenyewe! Kama umepata “BURE” unapaswa nawe utoe BURE! Kanisa limejichanganya katika tafsiri za mitaani, mpaka limejiingiza katika biashara zenye kulifitini Neno la Mungu.

  Tunapozungumzia “Semina”, jambo la kwanza tulilopaswa kufanya ni kulitafuta chimbuko lake ki Maandiko, ni nini, ili itusaidie kuondokana na michezo ya lugha inayoweza kulibadilisha jambo la kawaida kuwa kitu kingine chenye kutugharimu kwa ushamba wetu tu!

  Mt 28:19-20 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, …. na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

  Basi kwa kadiri utakavyoyaangalia Maandiko haya, jambo la kwanza tunaloliona ni huko kufanywa kuwa wanafunzi, hii ndio hatua ya kwanza ambayo hutuingiza katika Wokovu. Baada ya hapo, kama kawaida ya wanafunzi ilivyo, huketishwa chini kufunzwa, ndiko huko “kufundishwa kuyashika yote yaliyoamriwa” ambako siku hizi ndio wanaziita “Semina”!!! Mpaka hapo jukumu la kuwafanya hao kuwa wanafunzi na kuwafundisha limewekwa juu ya mitume na si wanafunzi.

  Basi kuweka kiingilio ni ishara kwamba kazi hiyo hujatumwa na mwenye kazi! Mungu akikutuma ni LAZIMA akutangulie. Jaribu kujiuliza, ni nani aliyemgharimia Yona katika safari yake ya Ninawi? Hata nimeona ndg Ziragora akizungumzia michango aliyokuwa akiikusanya Paulo, akijaribu kuilinganisha kuwa ilikuwa ni “Tozo”, bali ni vitu viwili visivyohusiana kabisa, alichokikusanya Paulo kimefungamana na upendo na ‘viingilio’ ni hekima ya kibinadamu inayotokana na kutumia akili katika kutafuta namna ya kujikimu kigharama!

  Pia, kanisa kwa kuliacha Neno la Mungu, limeubadili Uongozi wa RM na hekima yake, ambayo imesababisha kuvikosa vipawa ambavyo Mungu alivikusudia kuwemo ktk kila kusanyiko lake, Efe 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.” Baada ya kuwa vipawa hivyo vimekosekana ktk makusanyiko, ndipo umuhimu wa kuokoteza “walimu’ na “manabii” na “wainjilisti” nk ulipokuja. Kwahiyo suala la kutoza viingilio ni la lazima ili kumudu gharama! Pengine “walimu” hao wametumia gharama kubwa kujisomesha nk kwa hiyo italipaje?

  Kwahiyo ndg Tumaini hayuko mbali na ukweli kwani mindset yake iko katika kulitazama Neno la Mungu na si mipango ya makanisa yetu. Mungu akikutuma kazi, hulisimamia jambo zima na kulifanikisha kulingana na kusudi lake, likiendana na Neno lake!

  Viingilio huwekwa kwa msingi wa kibiashara zaidi kuliko Neno la Mungu. Hebu wazia kwamba unatangaza “Semina ya Neno la Mungu, itafanyika katika ukumbi wa Mlimani City (ukumbi ni full A/C)” kiingilio shs 12,000/= Mnenaji ni Prof E Seleli DD, mada ni ZAKA; halafu siku hiyo hiyo kutakuwa na Semina pia mada ni ZAKA na mnenaji ni “mw” C Mwakasege, itafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee (una mafeni tu, yale mapanga boy!), kiingilio ni shs 100,000/=. Hao wa Mlimani City, nakuhakikishia, mnenaji na waandaaji wake, wote wataishia Diamond, maana hawatapata mtu!

  Gbu all!

 107. Hivi hapo mwanzo kama ingekuwepo hii dhana ya ‘michango’ kwa ajili ya kupokea neno lililotolewa bure …hii injili ingefika hapa tulipo? Just thinking aloud…ebu fikiria bwana wetu Yesu Kristo angesema kuja katika semina /mikutano yangu kiingilio shekeri fulani leo wokovu ungeenea? wokovu umeletwa kwa wanadamu wote…tujipange kuhakikisha lengo hili na si ujanja ujanja kupitia ‘semina’ . Kazi kweli kweli

 108. Sungura binafc mimi kinachonikwaza ni kiingilio tu yaani hilo neno kiingilio nililivyoliona likanipa tabu sana!thn nikajiuliza tena je kama wenye huduma wakajaribiwa kwenye eneo hilo la kiingilio pasipokuwa na maono mengine mfano kiingilio kitakuwa kwa kipindi gani je ni kila semina au ni kwa semina flani!bt still nimejiuliza jambo hilo bt nikapata jibu flan kwamba hudumu ambayo MUNGU ameilenga hata kama kunavikwazo it means itasimama tu kwani kuna kusudi la MUNGU.Na kama huduma hiyo ni ya kisanii lazima itafika sehemu itazima tu!nimejaribu kutafakari hata huduma ya Mwakasege ilivyoanza inamana haikuwa kama ilivyo nadhani alikuwa na maono ambayo ni haya aliyofikia!so kwa sasa naanza kupata amani kwa ile nia njema kama ni kusudi la MUNGU kuweka kiingilio na kwakuwa litakuwa ni kusudi la MUNGU it means amani ya BWANA ITATAWALA MION MWETU KUTOA KIINGILIO.Sam binafsi napenda saana kumtumikia MUNGU kwa shekeli na huwa cna utata kwa hilo!tupo hapa kuelimishana kujengana na kuwekana sawa tena kwa nia njema!

 109. Mara nyingi mtu anaekwenda kwenye semina tayar wokovu ameshaupata ila kule anakwenda kutafuta kukua zaidi kiroho.Hivyo kuchangia kwa kutoa kiingilio hilo ni jambo zuri tu sioni kuwa ni tatizo.Ndio maana kwenye matamasha ya nyimbo za Injili tunaingia kwa viinglio na wakati uimbaji nayo ni huduma kama zingne kwa ajil ya kujenga mwili wa Kristo.CD,Vitabu vya Injil tunanunua kiinglio ni right kutoa.

 110. Ndugu Tumaini,

  Tuliopewa bure ni wokovu. Na semina haimunyime mtu wokovu. Kam wewe ni mukristo si tayari umekwisha daka wokovu kwa bure?

  Jambo lingine ni ile namna ya kusikia neno “kwa bure”. Ina maana haina bei. Ndiyo maana unayopata kwenye semina inapita ile kiingilio. Ukilipishwa kikwelikweli yale maneno, nyimbo, pambio, kiti, nk, utapata? Sasa jumlisha na baraka utakazopata, au jumlisha na laana kam utapinga!!!! Au haujue kam laana nayo ina garhama kubwa inayofikia bei ya damu.

  Acha nikuonyeshe kama hata huko zamani mafundisho haikupewa bure. Soma “1 Wakorintho 16:2 Siku ya kwanza ya juma KILA MUTU kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;”. Hivi huone namna Paulo alikuwa akiwaambia washiriki watayarishe michango yao kabla aje? Hiyo ndiyo garhama. Sasa inategemea namna semina imendaliwa. Paulo yeye anasema kwa kadri ya kufanikiwa, lakini mwengine ataweka amount ya kadiri anayoona watu wengi wanaweza ifikia. Na kam kwa wakati ule hauna, ukiwa na kiu ya semina, kawaida kiingilio si hela nyingi; jikopeshe lakini usikose. Ile Imani yako itakuletea baraka, utalipa na utazidishiwa. Haleluya!!

  Asante.

 111. Tumaini Nelson mbona UNAZUNGUKAZUNGUKA hutaji vyanzo unavyoviona ww ni sahihi??..hizo kadi maalum unazosema wapelekewe watu wenye moyo wa kuchangia kwani WEWE si huyo mtu ambaye unatakiwa kuchangia kwa kulipa kiingilio?una uhakika gani kuna hao watu kama watu wote wana msimamo kama wako wa kutotaka kutoa hata kiingilio?..je hao unaowaita wenye moyo wa kuchangia wasipochangia?je semina zisifanyike kwasababu wenye moyo hawakuchangia gharama?

  ..inaelekea ndugu Tumaini unapenda kubebesha wengine mizigo wakati wewe binafsi ukisubiri vya bure na hii si sahihi kibiblia.!.umesema huduma zimevamiwa wengine wapo kimaslahi..je ni kina nani hao ambao wapo kimaslahi? maana unavyoongea ni kama vile una list ya hao walio kimaslahi..!

  ..ni vizuri hasa kwa watu waliokoka kuongea tukiwa na ushahidi na mambo tunayosema na si ku-generalize kila kitu kama wafanyavyo wengine…tukumbuke maneno huumba na tutayatolea hesabu siku ya mwisho…

  samwl

 112. Tumaini kinachokukwaza kenye viingilio ni nini hasa?
  Ni hicho ulichosema kuwa kama mtu hana kiingilio kwa hiyo asisikie neno la Mungu?

  Hebu fikiria kama semina inafanyika uwanja wa taifa hapa Dar, na mtu fulani anakaa Boko akataka aende kwenye hiyo semina lakini akashindwa kwa sababu ya nauli. Nani hapo kasababisha huyu mtu asisikie neno la Mungu?

  Ndio maana nilisema kuhusu biblia, kuwa haigawiwi bure. Kwa hiyo asiyekuwa na pesa ya kuinunua basi huyo hatasoma neno la Mungu. Sasa hapo sijui alaumiwe nani kwa kumfanya huyu mtu akose kusoma neno la Mungu.

  Nilishasema kuwa wachumia tumbo hao wapo tu siku zote!

 113. Nadhani nimesema wazi kabisa semina zina gharama na nikasema itafutwe njia sahihi ya kutafuta source of fund na c swala la kiingilio inamaana mtu kama hana kiingilio inamana hapati neno kwangu hainiingii akilini kabisa!brothr Sungura umesema semina za mwakasege zinaonekana kama ni bure bt zina gharama!huoni ametumia njia sahihi ya kutafuta vyanzo vya mapato kufanikisha semina na ndiyo maana watu wanaingia free!Mimi nadhan ni heri kungekuwa na kamati ambazo zinatakiwa zitafute mbinu sahihi za kupata fund!mfano inaweza kuandaa kadi maalumu ambazo zitapita kwenye semina ambazo yeyote atakayeguswa kuchangia huduma achangie kwa hiyari!na kamati inaweza kutafuta wadau mbalimbali ambao ni wapendwa wenye moyo wa kuchangia kufanikisha semina hiyo!thn lazima tutambue hizi huduma zimeingiliwa wengine wapo kimasilahi!unapoweka kiingilio how sure are u watu watakuja kama ulivyokadiria?je fedha ya kiingilio isopotosha au ikazidi inakuwaje?LET US THNK DEEP WAPENDWA!TUCWE WASHABIKI TU TUSEME ILE KWELI!

 114. Tumaini Nelson hebu tutajie hizo source nyingine unazozijua za kubuni ili kupata fedha ya kukulipia wewe uingie kwenye hizo semina bure…..kama unakwazika kwa kiingilio na kudai sadaka inatosha Je sadaka unayoitoa ww binafsi huwa unapiga hesabu kama inatosha kukulipia hata wewe mwenyewe??if yes kwann basi usigeuze hicho kiingilio kuwa sadaka yako?

  …au umesahau “Bwana Yesu alivyosema mwenyewe ni heri kutoa kuliko kupokea” – Matendo20:35…au kwako wewe dhana ya kutoa ipo kwa anayekupa wewe tu siku zote na si wewe kumpa?

  asante Sungura kwa ufafanuzi mzuri..

  samwl

 115. Yaacheni magugu yakue pamoja na ngano. Wachumia tumbo siku zote wapo tu katika ufalme wa Mungu. Hata kwa huduma ya Yesu walikuwemo, na Yesu aliwajua ila aliamua kuwapotezea tu. Hata kwa huduma ya Paul walikuwepo, na Paulo akasema potelea mbali iwe kwa hira au kwa nia njema alimradi injili inasonga mbele.

  Kuna umuhimu wa kuelewa maana ya mmepata bure toeni bure. Kwamba ni nini hasa hicho ambacho kimepatikana bure, na neno bure hapo linamaanisha nini- kwamba hicho kitu kimepatikana bila kulipiwa pesa, au ni bure kwa maana ya kwamba mtu hajakihangaikia kwa namna yoyote?

  Biblia zangu sikuzipata for free,tena zingine nimezinunua kwa pesa nyingi tu. Na ya kwako hata kama umeipata kwa njia msaada wa watu fulani (may be wazungu n.k), hawajakwambia tu ukweli, ni kwamba kuna mtu kaigharamia.

  Hakunaga kitu cha bure,ukiona unapewa kitu bila wewe kukigharamia jua kuna mtu katoa hiyo gharama kwa ajili yako.

  Daudi alikataa kupewa bure kiwanja cha kumjengea Bwana madhabahu,alitaka atoe kwa Mungu kitu ambacho kimemgharimu mwenyewe.

  Hebu fikiria, mtumishi kama Mayles wa Munroe akifanya semina akakwambia utoe kiingilio unaweza kulalamika kuwa hakutakiwa kutoza kiingilio. Lakini akisema badala ya kufanya hiyo semina basi atayaandika kwenye kitabu hayo amabayo angeyasema kwenye semina, na kitabu hicho kitauzwa. Hakuna atakayelalamika ati kwa nini anauza hicho kitabu badala ya kutugawia bure. U bure wanaousema wapendwa wengi ni mtazamo tu, wa kukiona kitu katika pande moja, kikigeuzwa pande nyingine huo mtazamo unabadilika.

  Kuna vya kutoa bure, na vingine lazima tuvilipie!

  Hata semina za Mwl. Mwakasege mara nyingi huonekana ni za bure, lakini kiukweli kuna watu wamezigharamia.

  Lakini wachumia tumbo wana kesi ya kujibu!

 116. Binafc cbarikiwi kabisa kwa swala zima la kuweka kiingilio kwenye semina!Nadhani walengwa wanaoandaa semina wanatakiwa wajipange ipasavyo kutafuta fund kwa ya kuendeshea semina kwa namna nyingini na kama ni semina za kila mwaka basi lazima kuwe na mpango kazi ambao utonyesha source of fund za mwaka huo lakini c swala la kuweka kiingilio!je tunauhakika gani kama wote wanaoandaa wanania ya dhati ya kutoa neno la kweli?maana wengine niwasanii!tumepewa huduma bure na MUNGU NASI YATUPASA KUTOA BURE!Tunajua huduma zina gharama basi inabidi wanaotoa huduma watafute njia sahii ya kupata fedha!unaweza sema sadaka zinazotolewa hazisaidii kitu cdhani kama ni kweli kwani katika kubuni source of fund zingine zilizosawa basi sadaka nayo iwe source of fund kuchangia semina hizo.KWAKWELI CBARIKIWI KABISAAA KUWEKA KIINGILIO!TUCWE WAVIVU KUFIKIRI KUBUNI MBINU SAHIHI ZA KUPATA FEDHA.MUNGU AWABARIKI WOTE.

 117. ndugu emmanuel labda tuanzie hapo kwako ww huwa unatoa sadaka kiasi gani ???maana mara nyingi watu walalamishi ndio hao utakuta wanatoa sadaka mia tano halafu wanataka kukaa kwenye ukumbi uliolipiwa seat, kiyoyozi,chakula&vinywaji, umeme,speakers,etc huku wakifikiri wengine ndio watalipia gharama zote..hv umeshawahi kupiga hesabu ya gharama hizo zote including ujira wa huyo mtumishi?au labda unafikiri mtumishi hana mahitaji na afanye kila kitu bure??

  sadaka hutolewa kwa siri na si guarantee kuwa watoaji watatoa kwa hali halisi ya gharama za hizo kumbi…ww kama unaona huwezi lipia basi subiri mikutano isiyo na kiingilio!

  Si vyema na sahihi kuwa walalamishi kwa watumishi wa Mungu kwa kila kitu…kama wao mioyoni mwao wameamua kufanya biashara injili basi hakika Mungu mwenyewe atawalipa lakini kama nia yao ni kukuletea habari za Mungu katika mazingira utakayo-enjoy basi ni haki ww kuchangia kwa kiingilio!

  sam

 118. Emmanuel,

  Good observation ila pia ni delicate issue kwa maana itahitaji ujasiri kusema kweli maana wanaohusika na seminar za aina izo kwa maana ile ya ujanja wakiona/soma baaadhi ya comments zinazopinga, wataona ‘’WANAVURUGIWA’’ channels za income!!!!!!!!

  Kuna side mbili ktk hili:

  Side A: Ikiwa lengo ni takatifu basi ni baraka sana kusaidiana kwa upendo na kwa kua huwezi ku- gurantee sadaka kama itakua na kilo za kutosha kumuda gharama kama- Mafuta ya magari, ticket za ndege kwa Wahubiri kama wamekaribisha wa Nje au hata wa ndani wanaotoka Mikoa ya mbali inayochukua siku 2-3 kufika Mkoa/Jijini alikoitwa kua mnenaji, guest house, posho kwa wanenaji, ukumbi-kama inafanyika nje ya jengo la kanisa, Walinzi maaulumu wakati wa seminar maana watakuja watu wengi, chakula kama ni ya siku nzima, waandishi wa habari na media kuitangaza nk, kwa ivyo, kwa mtazamo huu chanya, wa kitumishi, hatuwezi kua na mawazo machanga kua tunalipia au kama tunanunua Neno la Mungu, hapana!

  Side B: Kama ni mambo ya janja za mjini na jijini haya, kuwategesha Wanadamu wazilete noti, ole wao maana Ufunuo.20:12 haiachi chembe yoyote. By the way, huo ufunuo/maono spesheli au ujumbe wa ajabu kwa uzuri walionao au pata/pewa toka ‘’’Mbinguni’’’, JE HAUMO KTK BIBLIA? Imetoka wapi iyo SIRI mpaka iwe ya pekee kiasi icho na wawe nayo hao tu na kwamba kweli wanadamu wakiipata/sikia tu, kuanzia hapo mambo yanabadilika hakika, mateso kwisha na kwamba hata wao wanaokuja kuinena, wamebadilishwa na mambo yao super kabisa! Hawana mateso wala jambo tatizi ktk kila kona ya maisha yao! Na kama kila Watakachosema kimo ktk Neno-yaani kilisha nenwa/andikwa, so what is the deal then? Na kama wanachosema hakimo ktk Neno bali ni yale mafunuo wanayosema hua wanayapata straight toka kiti cha enzi ivyo si lazima sana yawemo ktk Neno, kuna haja gani hata ya kuwapa mic kunena? Si tuwafukuze tena haraka sana mara moja.!

  Press on

 119. Ni kweli semina nyingi huwa zinahusu viingilio, hili kwa kweli kwa upande mwingine halizuiliki kutokana na gharama za maandalizi hadi kufikia semina husika.

  Kikubwa ni kuwa kiingilio hicho hupangwa kulingana na gharama halisi bila kuongeza faida kwa waandaaji, hivyo mwendesha semina na mpata semina huwa wanasaidiaa kugharamia.

  nadhani utaratibu huu ni mzuri hasa kuepuka kugharamiwa semina na taasisi, vyomba au mashirika ambayo hayako upande mmoja na sisi kwenye malengo ( Hasa ya Kumtukuza Kristo wa Kweli ). Hali nii kwa kiasi kikubwa unatupa uhuru wa kupata injili safi isiyochujwa kwa matakwa ya aliyegharamia.

  huo ndio mtazamo wangu.

  Mwenye mtazamo tofauti simpingi nitamheshimu kwa dhati

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s