Ukombozi sio tukio ni safari!!

Pastor Carlos Kirimbai.

Kuna wimbi kubwa sana la huduma za ukombozi ambalo limeibuka katika siku za hivi karibuni. Zingine ni halisi lakini nyingi sio hata kidogo. Sasa sio nia ya post hii kuhukumu huduma ya mtu maana sina mamlaka hiyo ila ni nia ya post hii kusaidia japo kwa sehemu kuwa na msingi wa kimaandiko kwa ajili ya huduma ya ukombozi. Nisingependa kuingia katika unaga ubaga wa kama ukombozi ni sahihi kwa walio okoka au la ila ningependa kuweka chini msingi wa kimaandiko wa huduma ya ukombozi. 

Ninaposoma maandiko, kwanza kukombolewa ni jambo ambalo limewekwa ndani ya package ya wokovu.

Pia huu ukombozi sio jambo ambalo linatokea tu mara moja bali ni jambo ambalo linajidhihirisha katika maisha ya mtu kwa kadiri anavyokua katika kuijua kweli na kutembea katika hiyo.

Yesu alisema maneno haya:

Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. (YN. 8:31, 32 SUV).

Yesu alikuwa anasema na watu waliyomwamini. Ukisoma alichowaambia ni wazi kuwa Yesu alikuwa anadhihirisha kuwa kumwamini ni mwanzo tu wa safari. Yale uyafanyayo baada ya kumwamini ndo yanaamua ubora wa maisha katika Yeye utakayofurahia. Ukimwamini alafu huendelei katika neno Lake kuna kiwango cha uhuru katika Yeye hutafurahia. Na ni wazi huu uhuru anaouzungumzia hapa hauji kwa njia ya kumwamini tu bali unakuja kwa njia ya kuijua kweli Yake na kuiishi pia.

Sasa wengi wetu katika huduma ya ukombozi tunawafunza tu watu kufunguliwa na vifungo vya adui, kuvunjiwa laana nk bila ya kuweka msisitizo wa kuishi maisha ya kulisoma neno na kuliishi neno. Yesu aliweka wazi TUTAIJUA KWELI NA HIYO KWELI ITATUWEKA HURU. Uhuru wowote unaokuja katika maisha ya mwamini unatunzwa na kweli aijuaye na kuiishi. Sasa sijajua katika huduma za ukombozi kama msisitizo huo unawekwa. Maana watu wanaenda tu kuombewa ambayo sio mbaya lakini hawawajibiki binafsi na maisha yao na matokeo yake huduma ya ukombozi badala ya kuwasaidia ndo inawaharibu.

Kwanini nasema hivyo.

Soma haya maneno ya Yesu hapa:

Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya. (MT. 12:43-45 SUV).

Sio mimi nimesema maneno haya. Ni Yesu ndo kayasema. Pepo likishatolewa kwa mtu kwa njia ya huduma ya ukombozi, litaenda alafu kuna siku litarudi. Kama huyu mtu aliyetolewa mapepo hajajua jinsi ya kujipanga anaweza akawa amejiweka katika hali ya hatari sana. Kinachomfanya pepo arudi alipotoka ni pale ajapo na kukuta nyumba imefagiwa na kupambwa lakini tupu. Ni ule utupu wa maisha ya mtu ndo unamweka katika hali ya hatari sana. Kinachoweza kujaza maisha ya mtu sio maombi endelevu na huduma endelevu ya ukombozi ni neno la Mungu na neno la Mungu peke yake.

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. (KOL. 3:16 SUV).

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. (ZAB. 119:11 SUV).

Hatuwezi kukwepa wajibu wa kulijaza neno la Mungu ndani ya maisha yetu.

Na halijai kwa kulisoma tu linajaa kwa kulisoma na kuliishi.

Sijui kama tunaona jinsi ilivyo hatari kufunguliwa kwa njia ya maombi peke yake bila msisitizo kuwekwa katika maisha ya usomaji na kuliishi neno.

Hali ya mwisho ya huyu muathirika au mhanga ni mara saba mbaya kuliko ya kwanza.

Katika agano la kale ambalo ni kivuli cha agano jipya, Mungu aliwaambia wana wa Israel maneno haya:

Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi. (KUT. 23:28-30 SUV).

Cjui tunaona hayo maneno. Mungu anasema hatawaondoa wote mara moja. Ukweli ni huu japo unauma. Huwezi tu kwenda mahali na matatizo yako yoooooote yakaondoka mara moja. Ondoa dhana ya kuwa nitaenda mahali kuombewa, kutolewa mapepo, sijui kufanyiwa ukombozi na matatizo yangu yataisha. Mungu mwenyewe anasema hatayaondoa mara moja maana akifanya hivyo wanyama wa bara wataongezeka kukusumbua. Yaani ni kama kuyaondoa matatizo yote mara moja ni kufungulia matatizo makubwa zaidi. Yeye anaahidi kuyaondoa kidogo kidogo kwa kadiri sisi tunavyoongezeka na kuirithi nchi aliyotupa au ahadi alizotupa. Kuongezeka katika kimo ni muhimu mno.

Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; (1 PET. 2:2 SUV).

Kuongezeka au kuukulia wokovu ni matokeo ya neno na neno peke yake linaloingia maishani mwako kwa njia ya kulisoma, kufundishwa na hatimaye kuliishi. Ndipo unaanza kukua kiroho. Na matokeo ya kukua kiroho ni:

Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. (LK. 1:80 SUV).

Kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyoongezeka nguvu rohoni.

Angalia maneno ya Paulo kwa wazee wa kanisa la Efeso:

Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. (MDO 20:32 SUV).

Neno la Mungu unapolisoma, kufundishwa na kuliishi ndilo linalokujenga na ndilo linalokupa urithinpamoja na wengine waliyotakasea kama wewe.

Tumeweka msisitizo mkubwa kuliko kwenye huduma ya ukombozi, kuvunja laana na kutoa mapepo bila ya kuweka mkazo wa kutosha katika kuwajibika binafsi katika kulisoma neno, kupata mafundisho sahihi na kuishi kila kinachofunuliwa kwetu tusimapo na tufundishwapo. Iko kama tunainua kizazi cha watu waliyookoka ambao hawapo tayari kulipa gharama ya kulijua na kuliishi neno ili kutembea katika ukamilifu wa uhuru ambao Yesu alienda msalabani kuununua kwa ajili yao.

Kila aliyeokoka ni mrithi pamoja na Yesu wa ahadi zote za Mungu. Lakini kama Paulo asemavyo:

Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; (GAL. 4:1 SUV).

Mrithi anapoendelea kuwa mtoto, hata afanyiwa huduma ya kufunguliwa kiasi gani, hata avunjiwe laana kiasi gani, hata atolewe mapepo kiasi gani, ataendelea tu kuwa kama mtumwa ingawa ni Bwana wa yote. Tumeitiwa kuwa bwana wa yote lakini adui mkubwa wa kutuzuia tusiyaone hayo sio mapepo, sio laana sio vifungo. Ni utoto. Na utoto ni matokeo ya kutoijua na kuiishi kweli.

Kama tunataka kuona ubora wa uzima ambao Kristo aliulipia pale msalabani ukiwa halisi maishani mwetu, tuache kukimbizana na huduma hii na ile na ile tukidhani kuna moja itaweka majibu yote mikononi mwetu tena kwa kuombewa tu na maombezi. Tulia mahali ambapo unajua Mungu amekuweka, tia mizizi yako chini hapo na kua katika kumjua Yeye na utaona uhru wako ukiachiliwa katika maisha yako hatua kwa hatua.

Nimalize kwa maneno haya ya Yesu:

Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. (MT. 24:26-28 SUV).

Yesu hapa anatuonya kuhusu kichaa kitakachoibuka siku za mwisho za watu kuambiana yupo huku, au kule au pale. Yesu keshasema tusiwasadiki. Alafu akasema maneno magumu sana ambayo sijui kama huwa tunayaelewa, akasema palipo na mzoga, tai hukusanyika. Kiswahili chetu hakikutenda haki hapa. Maana isemapo tai unaweza haraka ukafikiri ni yule ndege kwa kiingereza tunamwita eagle lakini ndege anayetajwa hapa ni vulture ambaye ni ndege ambaye anasekiaga harufu ya mizoga au kuna namna anajua mnyama anapokaribia kufa alafu wanasogea. Hawa ndege hawali vilivyo hai. Wanakula tu vulivyokufa. Ni mbaya sana mzoga unapokusanya na bahati mbaya mzogo haukusanyi ila ndege na wanyama waliyo maarufu kwa kula mizoga. Huko kukimbia kimbia kwako usije ukawa msaka mizoga.

Sasa kusema hivyo haimaanishi kuwa kila palipo na uwingi wa watu kilichowakusanya ni mzoga. Hapana. Kuna huduma nyingi kubwa nazijua ambazo zimekusanya watu kwa sababu ya kitu cha kipekee cha kiMungu kilichopo hapo na watu wanakifuata. Ila pia zipo nyingi zinazojiita “huduma” ambazo zinakusanya kwa sababu ni mzoga unaovutia tai.

Mzoga ni mrahisi sana kuujua. Unatoa harufu mbaya.

Asomaye na afahamu.

Pastor Carlos Kirimbai

……………………………………………………………..

Mafundisho mengine yanayokubali Kufunguliwa yaliwahi kujadiliwa bila kupata majibu sahihi

https://strictlygospel.wordpress.com/2011/09/08/kufunguliwa-kutoka-katika-ndoa-ya-mapepo-au-majini-mahaba/

https://strictlygospel.wordpress.com/2013/07/22/balaa-laana-na-mikosi-ya-kifamilia/

Advertisements

21 thoughts on “Ukombozi sio tukio ni safari!!

 1. Baraka,

  Ubarikiwe kwa kuelewa kuhusu uandishi ingawa bado vituo vikuu vinatapakaa kila sehemu! Sijui unaandikaje na unaandikia nini aisee! la!

  Asante kwa majibu kiasi ILA nakungoja UMALIZIE MASWALI yangu ndio niseme nami…Unaweza ukajibu vema hatua kwa hatua kwa mpangilio nadhifu kama nilivyo yapanga ili iwe rahisi kukufuatilia? Itabariki zaidi, jaribu kidogo iyo.

  Ukikosa muda kwa yaliyobaki, basi jibu kwa nini Petro kt Wagal.2 alifanya ovyo mpaka Paul akamkemea na wakati aishabatizwa kwa Roho na maji na hata kuzaliwa mara ya pili?

  Kama utaona vipi, maswali yangu na majibu yako, tunaweza yahamishia kt mada naona imekua revived hapo ya Kuzaliwa mara ya pili

  Aya malizia majibu kama ni hapa au kule mada ya Kuzaliwa mara ya pili, mimi nakungoja na kukufuatilia

  Pia maswali kuhusu Kuzaliwa mara ya pili ni muhimu sana, yajibu plz.

  Press on.

 2. sasa kaka waweza kuona YESU alisema magugu yakue na ngano yeyeatayangoa,hivyo Yuda lilikuwa gugu lilipewa toba likamwamini YESU likabatizwa yaani kutakaswa lakini bado lingali gugu,hilogugu halikuweza kuzaliwa mara ya pili kama wenzake pale pentekoste yaani ile nguvu hakupata.hivyo mpendwa roho ya Yuda ipoleo makanisani hata wakiombewa hawatafikia hatua kama za wenzao walio simama.sasa utaona kuzaliwa mara ya pili sikubatiza kwa maji bali mdo,11:15:18 sasa kaka hapo ndo watu huchanganya mambo,hii hatua ya tatu kwa mwamini ni MUNGU mwenyewe humpamtu amtakaye aliyejitoa kwa bwana hata uwezi kuwa Mchungaji bila kuzaliwa mara ya pili ndo utasikia amezini na washirika au amekimbia kundi nk,nakusihi fundisha neno onya kalipia lakini mayuda wamo na BWANA atayangoa,kwani ukitumia mawazo yako kungoa utaharibu na ngano.bwana awajua walio wake tena wakiokoka hawasumbui,barikiwa mtumishi wa Bwana.

 3. kaka Edwin nashukuru kwa msaada wako kuusu uandishi ubarikiwe.sasa mpendwa jua kuna hatua 3 mtu hupitia ktk wokovu,anapo amini anahesabiwa haki kwanjia ya toba,pili anatakaswa kwanjia ya ubatizo,tatu hujazwa Roho Mt.sasa kaka utaona mitume kabla yesu ajaondoka hatua 2 za mwanzo wote walipata,rakini haikuwasaidia bado walikuwa uovundani yao,acha Yuda,Petro hakuwa na imani na uwezo wa MUNGU hata akatumia upanga.sasa angalia baada ya kuzaliwa mara 2 pale siku ya pentekoste kaka hata wewe unajuamoto uliofuata,hakukua na udhaifu tena.mdo.2.1.4 luk,24:49 sasa huo ndio ubatizo wa ROHO MT.luk.3:16:17 sasa kaka siokila mwamini anazo hatua zote,wako kwa hatua kama ulivyoona wapo kina Yuda wameishia hatua 2 za awali wapo wanaoendelea hadi 3 MUNGU huwatumia.sasa kaka anayezaliwa mara ya pili kwenyehiyo 3 ,kaka utawatambua kwa matendo yao maana YESU yumo ndani yao nitaswira ya BWANA kaka wamekomaa ktk imani.YESU hakumwombea Yuda kwani alijua wazi kuwa hato badilika yer,1:4:5 rum 8:30 wake anawajua onawake Petro alitubu.

 4. Baraka Charles,

  Nakupa ushauri wa BARAKA sana KiBiblia na kiunadhifu kua TAFADHARI SANA UNAPOANDIKA MUNGU, YESU, ROHO MTAKATIFU, tumia herufi kubwa kwa herufi zote au herufi ya kwanza..mfano unaweza andika ‘YESU’ au ‘Yesu’. Never ever use these..yesu,roho mtakatifu, bwana nk, Kibiblia huyu..’’yesu’ au huyu ‘bwana’ SI SAWA na huyu ‘Yesu’ au ‘Bwana’!!. Na hata pia majina ya Watu au sehemu, anza na herufi kubwa mfano Petro si petro!! au Mitume si mitume. Pia baada ya kituo kikuu, anza na herufi kubwa!

  Baada ya kusema hayo, nina maswali kidogo hapa kutokana na mchango wako

  Umesema, ‘sio kila mwamini amezaliwa mara ya pili
  Maswali:
  (a) Una maana Mtu akiokoka(Kua mwamini Yesu) anakua bado anahitaji kitu kingine tena kinaitwa kuzaliwa mara ya pili?

  (b) Nini tofauti ya Watu hao ukiwatazama na kuishi nao kati ya aliyekua mwamini(ameokoka) na aliyezaliwa mara ya pili?

  (c) Unaweza nionyesha katika Biblia kwa kutumia Wanafunzi wa Yesu, walikuaje walipokua Waamini tu na ilikuje Walipozaliwa mara ya pili au vice versa?

  (d) Kwani hata ivyo kama uliyosema ni kweli, kipi kinatangulia chenzake, Kuokoka au Kuzaliwa mara ya pili?

  Umesema Mtu akibatizwa na Roho Mt, ndio kushinda dhambi ataweza
  MaSwali:
  (a) Dhambi zipi labda pengine maana Kibiblia dhambi ni uasi dhidi ya Mungu, ni kutofanya jambo jema wakati ulijua ulipaswa, ni kila tendo lisilotokana na imani, ni mambo ya machukizo mbele za BWANA na kiujumla dhambi ni kutolitii Neno la Mungu, sasa unaongelea dhambi kwa maana/mantiki ipi kati ya izo au zote?

  (b) Una uhakika na ulilosema kwa kuzingatia alichofanya Petro hapa wakati alisha jazwa nguvu na ni mtumishi wa nguvu..Wagal.2:11-14?

  Umesema jambo la udadasi mzuri hapa na nimelipenda, sikuwahi kuwaza ivyo, hongera kwa reasoning safi sana kua kama ni ivyo Yesu angemuombea maombi ya ukombozi Yuda maana alikua mwizi, wow! great thought lakini nina swali

  Swali: Kwa iyo kwakua Yesu hakuwahi muombea/kumfanyia deliverance jamaa ili ivunje roho ile ya wizi, unataka kusema nini hasa? Au ku-conclude nini kwa herufi kubwa?

  Press on

 5. wapendwa tatizo kubwa ni watu kutumia mawazo yao na siokumwacha roho mt.atuongoze,mf.siokila mwamini amezaliwa mara ya pili,mtu kuamini na kubatizwa siokipimo cha wokovu,unaweza kuwa na hatuahizo na bado ni mwovu au akanena kwa lugha nabado ni mwovu,sasa wakiona hayo wanasema anahitaji hiyo delevalence,bilakujua kuwa hakuna mtuanayeshinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe.mfn.mitume walipitia yote hayo lakini bado petro alimkana bwana,hivyo ona walipoipata ilenguvu baadaye walisimama hadimwisho.sasa tatizo hiyohatua kama mwamini hajaifikia unataka matatizo yamwishe kweli?ubatizo wa roho mt.ndounatakiwa ilimtu ashindedhambi na sio maombezi,mat 3.11:12. mdo 2.1:4 mwamini anapobatizwa na roho mt.hapo huwezakuishinda dhambi bilamaombi ya mtu,hivyo hudumanyingine za miujiza ya ukombozi nk ni upofu tu,nakama ndivyo yesu angemfanyia yuda msaliti huduma hiyo kwani alikuwa mwizi nk au haikuwa ni roho kama hizi mnazoombea leo?wapendwa hubirini watu waache dhambi.

 6. HILI somo bab kubwa Mzee, hata ukiwa mbishi namna gani hapa lazima uelewe tu! MUNGU WA HERUFI KUBWA Akubariki Postor Sungura.

 7. Sungura,

  Nimecheka sana hii…. Ha ha aha ha…. ‘’’Sasa kama na wewe Seleli huwa ukisikia kuwa kuna mtu katapika nyoka mzima mahali fulani unavutwa kwenda huko, basi na wewe umo kwenye hilo kundi! ACHA UTANI MBAYA! Tehe… umenichekesha kweli wewe kiumbe aisee.

  On Mindset elaborations and cooking……. job well done , you made tangible great senses indeed.

  Press on

 8. Seleli,
  Wa salaam!

  Nafikiri suala la mzoga na tai umelisemelea sawasawa, japo mimi hata sikuwa nimeliwekea manani yoyote katika kuchangia kwangu.
  Nafikiri Yesu hakuwa anataka tuangalie sifa ya mzoga na sifa ya tai, bali ile dhana nzima jinsi walio wake watakavyomkusanyikia siku ya mwisho.
  ……….
  Kuhusu suala la mindset ya kichawi, nitalijibu kwa jumla si kwa a,b, c…..!

  Kwanza nimesema wana mindset ya kichawi siyo ya uchawi! maana hayo maneno mawili hayana maana sawa.

  Kuna dada mmoja ameokoka, lakini alikuwa house girl kwa muda wa zaidi ya miaka kumi. Kwa hiyo akazoea ile hali ya kutokukaa mezani kula na boss wake,yaani wakati boss anakula yeye bado anashughulikia hiki na kile,na mwishoe boss na familia wanamaliza kula hivyo yeye kulazimika kula peke yake tena jikoni.

  Baadae dada aliolewa hivyo akawa na familia yake. Kilichotokea ni kwamba akishaivisha chakula alikuwa anamkaribisha mezani mume wake pamoja na watu wengine waliopo, lakini yeye anaendelea kushughulikia hiki na kile, hivyo kushindwa kukaa mezani na mume wake.

  Mume wake akimwambia aje akae mezani wale pamoja alimjibu kuwa waendelee tu kuna kitu anamalizia kufanya baadae atakwenda kukaa mezani pamoja nao, lakini mwishoe watamaliza kula kabla yeye hajakaa.

  Ndipo mume alipofuatilia akagundua kuwa huyo dada wakati akiwa house girl hakuwa anakaa mezani na familia ya boss wake, kwa hiyo hiyo hali ikawa imemkaa kichwani mwake.

  Hiyo ndio mindset juu ya jambo fulani ambalo mtu amekaa katika mazingira yake muda mrefu.

  Ilimchukua Mungu miaka 40 kuwafanya Waesrael wasiwaze kama wamisri japo walishatoka Misri tayari- mindset!!

  Watu wengi wameishi maisha yao wakiwa wamezungukwa na matukio ya kichawi na waganga wa kienyeji. Wakiokoka akili zao zinaelewa na kuvutiwa kirahisi zaidi na lugha zinazosema mambo ya pepo la chuma ulete, kuibiwa nyota yako, kuna wachawi wanakufuatilia, n.k, maana inafanana na yale ambayo siku zote wamekuwa wakiyasikia masikioni mwao.

  Ndio maana wanatakiwa wafanywe upya akili zao( mindset) – which is a process!!

  Watu wengi wanavutiwa na mambo ya mauzauza katika movie za kinigeria kuliko hicho kiingereza chao. Na wachaza movie wa bongo kwa kulijua hilo wameamua na wao kutengeneza movie za mauzauza kama za kinigeria, na matokeo yake movie za kinigeria soko lake Tz limeshuka.

  Nilitolea tu mfano wa mindset za uchawi, lakini kama ulivyosema hata mindset za uzinzi zipo tu za kutosha. Ndio hao watu ambao mwanamke akivaa suruali kwao ni shida.
  Nami huwa nawauliza swali ‘what do u see when u look at a woman’?- hiyo ndio mindset niliyomaanisha.

  Ukiwa msomaji mzuri utangundua kirahisi kabisa kuwa niliposema watu wengi waliookoka wana mindset za uchawi, simply nilimaanisha wale waliokoka wanaovutwa na upepo wa mauzauza yanayoendelea sehemu mbalimbali. Sasa kama na wewe Seleli huwa ukisikia kuwa kuna mtu katapika nyoka mzima mahali fulani unavutwa kwenda huko, basi na wewe umo kwenye hilo kundi!

  Suala la Si kila aliyeokoka anahitaji huduma ya ukombozi, lakini pia si kila aliyeokoka hahitaji huduma ya ukombozi,na yote yaliyofuatia baada ya hapo katika makala yako, tuliiongea sana wakati tunajadili suala la balaa na laana katika mada iliyohusu kauli ya Mch. Gwajima.

  Kwa hiyo kuendelea kulisema hapa ni kufanya marudio yasiyo ya lazima!

  Vinginevyo asante!

 9. Hahaaa, Yusha!

  Naona Seleli amekuchokoza kidogo lakini hukumwona vizuri ukadhani ni Sungura.

  Umenifanya nikumbuke kisa fulani cha mtu mmoja kufanyiwa kitu bila kujua aliyefanya, yeye akageuka tu nyuma na kumpa kofi aliyekuwa nyuma yake.

  Siyo mimi Yusha, ni Seleli ndo kakuchokoza!!!

 10. Sungura

  Ninahitaji kuelewa yafuatayo tokana na post zako mbili! Kuna mambo umeongea, mengine yanatisha sana na kusitua vibaya sana aisee! da! na some ya kawaida tu ila yanahitaji clarifications kiasi.

  Kuhusu Waliozaliwa mara ya pili kua wengi bado wako na Mindset ya uchawi!

  Maswali:

  (a) Inawezekana vipi Mtu aliyezaliwa mara ya pili, akajazwa RM na ana Neno la Mungu, anaukuliwa wokovu akawa na mindset ya kichawi?

  (b) Kama Uchawi uko sana ktk mazingira ndio unamfanya Mwana wa Mungu awe na mind set ya kichawi, vipi ile nguvu ya kufanywa upya kama Biblia inavyosema, ya kale yamepita, sasa ni mapya, haijafanya kazi nguvu iyo?

  (c) Lakini pia ktk mazingira kunatawala mengi si uchawi tu, ivyo ni kusema tuna mind set za kizinzi, ufisadi, madeal ya rushwa, chuki, ukabila nk maana hayo nayo yamekamata mazingira yetu yote kuanzia nyumbani, ofisini, mitaani, ktk taasisi, kwa biashara,shuleni, vyuoni nk

  (d) Lakini pia mambo mabaya, uchafu, zambi, uovu na madude yote ya kidevo na kibinadamu yanatawala mazingira hapa duniani yalikuwepo, yapo na yatakuwepo mpaka Yesu anakuja, so when tutakua na mindset nyingine ikiwa yaliyo ktk mazingira yanamu-affect ivyo mtoto wa Mungu?

  (e) Na umefikijae conclusion iyo kua ni WENGI wa wana wa Mungu wana mindset ya kichawi? Does that if true, include you? I guarantee mi simo katu katu!

  Kuhusu kupenda kuangalia movies za KiNigeria kama uthibitisho wa Watu kuwa na mind set za kichawi

  Swali:

  (a) Je hakuna wanaovutiwa kuona utamu wa story, vipaji vya uigizaji stori iyo, ujumbe mzuri unaotumwa kwa jamii via uigizaji ule, mila na desturi za makabila/wanadamu wengine, yaani hata namna Waafrica wa West, wanavyoongega ile Kiingereza yao ya my brodaa and my sistoooo, yaani full raha na burudani-mmoja wao mie, izo mind-set za kiwanga ziko wapi hapo? wasemaje?

  Umesema haya:

  Wanaofanya deliverance, watafute jina jingine, hakuna Ukombozi wa pili kwa aliyeokoka labda amerudi nyuma, huwezi kua umeokoka ukawa hujakombolewa na kama hujakombolewa, hujaokoka

  Wokovu ni mchakato/safari, haukamiliki siku moja, wasiomuone mtu akiwa ktk safari iyo, jambo fulani bado kukawa sawa, wakamtaka afanyiwe ukombozi, safari aliyoianza ndio mchakato wenyewe, ujenzi unaendelea, huwezi lazimisha ‘finishing’ ya jengo wakati bado unatakiwa kuweka nguzo!

  Swali:

  Unaweza balance/harmonise vipi na sentence yako ya nguvu ya mwisho hapa chini-kisehemu chake cha pili na izo mbili za juu?

  ‘Si kila aliyeokoka anahitaji huduma ya ukombozi, lakini pia si kila aliyeokoka hahitaji huduma ya ukombozi!’’

  Kuhusu wanavyoamini kundi la kwanza kuwa mtu akishampokea Kristo mara moja mambo ya laana na ya kinguvu za giza yanakoma mara moja.

  Maelezo: MIMI NI MMOJA WAPO NAYEAMINI NA KUJUA KWA HAKIKA NA HOJA ZA NGUVU SANA NA HATARI NA KWELI TUPU KUA MTU AKISHAMPOKEA YESU MFALME WA NURU, ANAMKOMBOA NA KUMUHAMISHA TOKA NGUVU ZA GIZA( Uharibifu, uchawi, wanga, ulozi, laana, mikosi, mabalaa, nira,vifungo, minyororo, mateso, mikataba, mifuatayo/miandamo ya roho za kikoo na familia, kumilikiwa na mashetani,mizimu, mapepo, roho wachafu) KISHA ANAMUINGIZA KTK UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE-Wakol.1:13

  Ninaamini ikiwa Mtu anaokoka na bado akawa na magonjwa au shida, ITAKUA NI YA KIBAILOJIA tu and never TOTAL AND PURE UTAWALA WA DEVO LIVE OR LIVELY kwa Mtu huyo aliyemuingiza KING OF KINGS ndani. Ivyo mtu anaweza okoka na mguu kilema, maralia, mafua, tumbo la typhod, mgongo kuuma, upofu, ububu, ugonjwa wa ngozi, uziwi na yakabaki . Na sababu za shida/gonjwa izo si pepo au devo kabisa bali inaweza kua uchafu tu ivyo akishaokoka anashauriwa kuoga, usafi wa mazingira, kufua nguo, kufyeka majani kuzunguka nyumba na kufukia madimbwi ya maji kuzima mazalia ya mbu kisha kutumia net na kumeza ALU malaria over, kumeza codril na kunywa tangawizi moto-mafua kwa heri, kuomba mguu uote mpya kwa muujiza au kuvaa mguu bandia-kilema over au kinapunguza masaibu yake ya ulemavu, kuvaa vifaa vya kusaidia kusikia masikioni pengine alizaliwa kijijini, hakuna hospitali na alipougua masikio, hawakujua na hatimaye akawa kiziwi au hakukua na hospitali-ni extreme remote, vile vile macho hakuwahishwa hospitali au wazazi wao walikosa vitu fulani mwilini na wakati wako tumboni wakiwa vichanga, utengenezaji viungo haukukamilika, wakatokea duniani wako na ulemavu, hapo hakuna giza, devo, dhambi wala nini, ni normal occurrences pengine Mungu atukuzwe….angalia majibu ya YESU kuhusu kipofu huyu toka kuzaliwa-Yohana.9:1-41

  Swali:

  (a) Je wewe unaaaminije na kujuaje? kua Mtu akimpokea Yesu ile ya kweliiii, je bado ulozi aliologwa, gonjwa la kinguvu za giza alilotupiwa eg…mimba ya miezi 12 but no bebi and no kuzaa, nguvu ya uharibu/kuharibu aliokua nayo/iliyomkalia(laana), mizimu iliyoku imemshika na kummiliki, vifungo na nira za kipepo na uganga wa kienyeji na mazindiko, na madude, manyangalagata na maduduwasha yote ya pure kidevo/pepo/ulozi/laana, je yanabaki YESU NA RM na BABA WAKIINGIA kwa mtu?

  Press on

 11. Brother Sungura,am on line 24/7.what do you want me to do?the only problems is am not a religion person.I appreciat what is according to bible and refused what is coming in people is mind.

 12. Sungura,

  Great understanding kua si kila aliyeookoka anahitaji huduma ya ukombozi, lakini pia si kila aliyeokoka hahitaji huduma ya ukombozi!kulazimisha kuwa kila mtu anatakiwa kufanyiwa hiyo huduma si sahihi na kwamba wengine wanatakiwa tu kupewa ushauri eg. awe anasoma neno la Mungu

  Nimependa pia ukakamavu huu, a black and yellow statement….mtu anaaminishwa kuwa tatizo fulani haliwezi kuondoka mpaka akutane na mtu fulani- it is real ridiculous!!!!!!!! Hakuna mtumishi, black or blue mwenye hati miliki ya mambo ya Mungu, mtembeo wa nguvu zake na upaji wake.

  Nimecheka sana kua Waafrica wakisikia Mtu katapika nyoka mzima, kesho unajaza ‘’kanisa’’, well, I hope na Wazungu esp wakija uku wanapenda pia mauza-uza…nawafahamu weni kadhaa rafiki zangu, sema uko kwao hakuna Mitume/Manabii wa kuwafanyia hayo ‘’madude. I will balance liked this, si Waafrika mie, Carlos, na wewe ila Lwembe, Mabinza, Yusha I doubt! tehe tehe tehe! mis u guys!!!!!!!!! Yusha …debate is not a fight brother, uko wapi!

  Kuna vitu vingine umesema, imeleta maswali/confusions, I shall need clarifications, will post them later.

  Press on

 13. Wapendwa na ndugu zangu Lwembe, Sungura, na wengine wote,

  Nakumbuka mada hii imeiisha zungumzwa kwa kirefu katika Blog hii huko nyuma, na ilileta changamoto kubwa,

  https://strictlygospel.wordpress.com/2011/09/08/kufunguliwa-kutoka-katika-ndoa-ya-mapepo-au-majini-mahaba/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2013/07/22/balaa-laana-na-mikosi-ya-kifamilia/

  Nitachangia kidogo tu kwa leo, lakini Kila kitu muhimu kwetu sisi ni Je yasemaje Maandiko…? Je Kuna Deliverance kama inavyofanywa leo Katika Kitabu cha Matendo ya Mitume? Kuna Deliverance katika nyaraka za Paulo, Petro na mitume wengine…? Biblia inasemaje, hasa nini kinatendeka unapompokea Yesu…? Ni Kinatendeka katika utatu wa mtu (Soul, Spirit and Body) ? Roho wa Mungu anapoingia ndani yetu…? Tunasemaje kuhusu Kukua Kiroho ? Au kuukulia Wokovu…?

  Kama hizo deliverance ministry ni kweli, kwa nini Paulo hakufanya katika kanisa la Wakorintho…….maana lilitaji kabisa deliverance kwa yale yaliyokuwa yakitendeka huko…..!!! Nyaraka za Paulo nyingi zilikuwa ni kushughulikia matatizo ndani ya Makanisa……..mbona hatuoni hata harufu ya huduma hii….? Au waumini wa kizazi hiki tuna matatizo sugu kushinda wenzetu katika Agano Jipya…? Je Mbona Yale makanisa saba katika Kitabu cha Ufunuo yaliambiwaTUBU….TUBU…..TUBU……na sio ifanyike ibada ya Deliverance.

  Lazima tujibu maswali kama “Kuwa ndani ya Kristo” ambako Mtume Paulo kafundisha mno katika Nyaraka zake maana yake ni nini…? Au “kuhamishwa kutoka nguvu za giza na kuingia katika Ufalme wa Mwana wa Pendo lake maana yake ni nini…? Biblia inasema……nita paraphrase Kama tukimpenda na kulishika Neno lake……Baba na Mwana watafanya Makao ndani yetu……! Au Sisi ni Hekalu la Mungu…….Tuna hazina (ROHO MTAKATIFU) ndani yetu…..Kama hii ni kweli kama yasemavyo Maandiko ……Ni nini kinamfikisha Muumini au ni kongwa gani ambalo linamfunga muumini ikiwa BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU AMEWEKA MAKAO NDANI YA MAISHA YETU….Kwenda KUFUNGULIWA ? Nini kinaweza kufunga NGUVU ZA MUNGU NDANI YA MUUMINI ZISIFANYE KAZI……!

  Kwa kifupi tu experiences zetu hazitakiwa kulazimisha UKWELI wa NENO la Mungu……..!!!! Hatuwezi kukunja maandiko yasema kutokana na experiences zetu…..hata ziwe za ajabu kiasi gani…….!

  Hivyo wanaosema Kuhusu huduma hii kupinga au kukubali……;leteni hoja za MAANDIKO……MAANDIKO TU…….wala sio experiences ……!

  TUBARIKIWE

 14. Pastor Carlos/Sungura/Lwembe,

  Nonetheless matumizi ya andiko la ‘’Palipo mzoga Tai watakusanyika’’, navyoelewa mie ni tofauti na ulivyoeleza na walivyochangia. You may wish to clarify more yours or reconsider mine and buy it cheerfully. Nina copy hapa baadhi ya mistari then I will make my point clear!!!!!!!!!!………………
  Mathayo 24
  1 Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. 3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

  Tuzingatie hoja izi:

  Kwanza Yesu anafundisha somo moja tu hapo … UJIO WAKE na DALILI ZAKE, akijibu swali la Wanafunzi walilouliza kwa faradha ktk mstari wa 3 ambalo naligawa ktk maswali madogo 3 namely
  (a) Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? (angalia jibu la Yesu mstari wa 2 kama itikio lake Bwana kwa kitendo cha Wanafunzi Mstari 1)

  (b) Nini dalili ya kuja kwako?

  (c) Nini dalili ya mwisho wa dunia ?

  Kwa mantiko iyo, kila alichosema Bwana hapo ni kuhusu subject iyo tu-nasisitiza point iyo kwa sabubu ya hoja zinazofuata!

  Pili, mistari 5, 23-26…Kabla, Wakati dalili zinaanza na kupea, Watakuwepo Wandanganyifu wakitaka KUVUTIA watu kua wao ndio Kristo au Bwana yuko kwao/kule/pale. The Key word hapo ni Wadanganyifu KUWAVUTIA/KUKUSANYA WATU KWAO

  Tatu, mistari 27 na 28 ni mapacha kabisa, ni side mbili za same coin… wa 27 ni kama intro na wa 28 ni kama matokeo/conclusion na hata ktk kanuni za lugha, mistari yote toka juu na hata hii miwili ni idea/blocks dropping on one another from the other kuhakikisha ONLY SUBJECT inaanza, jengwa kisha hitimishwa.

  Nne, Kwa iyo ukiunganisha mstari 27 wa radi/umeme kuonekana kwa haraka/kasi na clear ukiwaka toka upande mmoja kwenda mwingine ndivyo kuliko wazi kutakavyokua kuja kwa mwana wa Adamu then NDIPO ANAUNGANISHA KWA FLOW IYO IYO/CONCEPT IYO IYO/MANTIKO IYO IYO kua POPOTE kuliko mzogo ndipo tai/tumbusi watakusanyika yaani, atakapotokea/atakapokuwepo Bwana, basi walio wake watakusanyika au watakusanywa kwakwe au watakuwapo hapo. Mzoga kukusanya Tai ni lugha picha kuonyesha tukio la kuja Bwana na sisi kukusanyika kwake/naye….as simple and sweet as that na NAAMINI NDICHO SIMPLY YESU ALIMAANISHA NA WALIOMSIKIA WALIMUELEWA IVYO KIRAHISI KABISA WALA HAKUKUA NA MAFUNUO HAYA MLIYOSEMA. Nadhani kidogo ume-spiritualize sana mpaka kupiliza hata ile maana rahisi kabisa aliyomaanisha Bwana na ambayo wasikilizaji wake walivyomuelewa la sivyo WANGEULIZA maana si kitu kigeni wao wakishindwa jambo kuuliza.

  Ufunuo ni mzuri ila ukizidi sana au kufanywa/kudakwa/vutwa mechanically au kupenda ku-apply dhana delicate kua kila andiko lazima liwe na ufunuo, tutakua na Mafunuo mengi sana BUT yetu si ya au toka kwa RM.

  Press on

 15. Pastor Carlos, Shalom man of God,

  Msisitizo kuhusu kuweka jitihada binafsi kusoma na kuishi Neno na hoja kua ukiwa mrithi yet ukawa mtoto- bado utakua mtumwa, that is great, great , extremely very powerful truth/revelation am telling you, nimemeza iyo tamu sana , glory to God alleluyah.

  Pia angalizo kua huduma za deliverance kua kuna mahala na namna Watu wamepitiliza sana mpaka inakua kama mchezo wa wajanja, nayo nimependa kweli kweli.

  Press on

 16. Lwembe;
  Mchango wako uko vizuri nimeupenda.
  Unajua nilikuwa sikumbuki kabisa ‘vulture’ anaitwaje kiswahili, halafu nikasahau kufuatilia, na nilijua kuwa siyo tai kwa maana ya ‘eagle’.
  Hilo jina nimeliona nikacheka jinsi lilivyo ‘tumbusi’

  Na niongeze tu kitu kimoja kwamba, huduma hii ya ‘deliverance’ ya namna tunayoinina kwa wingi, iko sana afrika na mabara yenye kufanana na Afrika.

  Hii ni kwa sababu huduma hii ina mfanano mkubwa na huduma za kiganga ambazo mabango yake yamejaa Dar. yote mpaka mitaa ya Samora iliyo karibu kabisa ofisi kuu.
  Huduma hii inapata wateja sana,si kwa sababu ya wingi wa matatizo tuliyonayo Afrika, lakini ni kwa sababu waafrika wanapenda ginjangija za mauzauza na mazingaombwe.

  Wakisikia kuna mtu katapika nyoka mzimamzima wakati anaombewa, au ukianza kuwaambia kuna watu wanawawangia, au kuna mtu kaiba nyota zao, au kuna kitu wamelishwa n.k. hiyo ndiyo style mwafrika anapenda.

  Lakini ukiwaambia wasome neno la Mungu wao, au waingie kwenye maombi wenyewe kwa ajili ushindi katika eneo fulani la maisha yao, hapo utabaki mwenyewe,wala hawataipenda huduma yako.

  Idadi kubwa ya wakristo wa Afrika waliozaliwa mara ya pili bado wako na mindset ya uchawi,maana uchawi bado umetawala katika mazingira tunayoishi. Hebu fikiria tu zile movie za kinaijeria ambazo idadi kubwa ya watu ndo wanapenda kuangali!

  In fact, hicho kinachofanyika kwenye hizo huduma hata hakitakiwi kuitwa ‘deliverance’, kitafutiwe tu jina jingine. Maana kiukweli, hakuna ukombozi mwingine wa pili kwa mtu ambaye tayari ameokoka, labda kama alirudi nyuma.

  Huwezi ukawa umeokoka, halafu hapohapo ukawa hujakombolewa. Yaani kama hujakombolewa huna sifa ya kuitwa umeokoka.

  Lakini kwa kuwa wokovu ni mchakato/safari,kama alivyosema mleta mada, si kitu cha kukamilika siku moja . Sasa watu wasimwone aliye kwenye hiyo safari ana jambo fulani halijakamilika wakaanza kumwambia anahitaji ukombozi,huo mchakato alioanza ndio safari yenyewe ya ukombozi, ujenzi bado unaendelea

  Ni sawa na kulazimisha ‘finishing’ ya jengo wakati bado unatakiwa kuweka nguzo!

 17. “… Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.”
  (MT. 24:28).

  Pastor unasema “Kiswahili chetu hakikutenda haki hapa. Maana isemapo tai unaweza haraka ukafikiri ni yule ndege kwa kiingereza tunamwita eagle lakini ndege anayetajwa hapa ni vulture ambaye ni ndege ambaye anasekiaga harufu ya mizoga au kuna namna anajua mnyama anapokaribia kufa alafu wanasogea. Hawa ndege hawali vilivyo hai. Wanakula tu vulivyokufa.”

  Lakini ukweli wa jambo hili ni kama lilivyoandikwa, hata kimaudhui liko sawa tu, pastor utakuwa umekasirishwa sana na “mizoga” ya Deliverance inavyowavuta vultures, wale tumbusi kwa Kiswahili!!
  KJV inasema hivi: “Wheresoever the carcase is, there will the eagles be gathered together”
  Najua umetatizika na neno ‘mzoga”, lakini hii ndio mana yake halisi. Mzoga ni kiwiliwili/mwili wa mnyama aliyekufa au kuuawa, ambayo ni sawa na neno la kizungu “carcase” kama lilivyotumika ktk KJV:
  Carcase = the dead body of an animal, the trunk of an animal such as a cow, sheep, or pig, for cutting up as meat.

  Sasa sifa ya Tai ni kama ulivyoielezea, hawali nyamafu, yaani huyo ni ndege anayewinda, kwahiyo ni lazima ale alichokiua yeye au nduguye au mnyama mwingine kasha yeye amnyang’anye windo hilo. Kwa kifupi huo mzoga LAZIMA uwe unavuja damu au fresh!

  Nazo sifa za Vulture au Tumbusi, pia ni kama ulivyoziainisha, hawa wanakula nyamafu, yaani ni wasafisha mapori! Mnyama akijifia wao hufanya karamu, au akiwa anakaribia kufa labda anaumwa , basi hao humshukia, wanazijua dalili zote na pia hunusa harufu ya mizoga iliyooza. Na pia huvizia mabaki ya mawindo ya wanyama wengine! Basi mizoga ya jinsi hii, ni kweli huwakusanya saana vultures, and they love it, bali tai huipitia mbali mizoga hiyo!!

  Kwahiyo alipotajwa Tai, jambo hilo liliashiria mzoga unaovuja damu, lile Neno la Mungu lililo fresh, linalohusiana na wakati unaoishi, yaani fresh from the throne; kama ujumbe huu uliouleta wenye kuwafungua watu kutoka ktk vice ya Deliverance, iwapo hao si Vultures!!!

  Gbu!!

 18. Pastor, Sungura & all
  Somo ni zuri saana, kweli, asomaye na afahamu, habari ndio hiyo! “Kichaa cha siku za mwisho cha watu kuambiana yupo huku, au kule au pale”, tayari kimetufikia na ninaamini hali hiyo ndiyo iliyokusukuma ulilete somo hili, ni wakati muafaka!

  Na “kichaa” hicho kinapambishwa moto na hizo Huduma za Deliverance zinazoongezeka kwa kasi na kupendwa saana na wateja wake, hizo ni shortcut ya suluhisho za matatizo yao, zi karibu sawa na uganga wa kienyeji, lakini kwa hizi unaingia na utanashati wako na hakuna anayekushangaa! Jambo la kusikitisha ndilo hilo, kwamba wote wanaishia ktk “UTEJA” wa Huduma hizo, kimwili kwa mafanikio wanayoyapata, na kwa Kiroho, wanaishia ktk “umauti” maana hawakuongezeka katika “Kimo”!!!

  Lakini, kisababishi cha hali hii ni makanisa yetu yenye kukiri Wokovu, pale yalipoliacha Neno na kuifuata hekima yao. Hebu fikiria, kwamba katika kila kusanyiko, angekuwepo nabii, yaani muonaji; mwalimu, huyo mwenye kulifungua Neno na Hekima yake; mwinjilisti, mwenye kuishitaki dhamira yako iliyopotoka; mtume, huyo mwenye ujuzi wa Injili na madhihirisho yake, hata kuyazaa makusanyiko; mchungaji, huyo mwenye kulihurumia, kulichunga na kulilisha kundi kwa Upendo; Je, uwapo ktk kusanyiko kama hilo, lenye Huduma ya Kristo ktk ukamilifu wake, ni nani awezaye kutangatangia huko kwenye ‘abracadabra’ za Injili?? Lakini kinyume na ukweli huu ndio hii hali tunayoiona, inawavuta woote, kama ilivyowavuta ile Huduma ya Deliverance ya kwa “Babu”, wengi hawakwenda kwa aibu tu na zile kelele za viongozi wao!!!

  Mkristo ni yule aliyekombolewa! Shetani anazifahamu Sheria zoote za Ukombozi kuliko maaskofu na wachungaji wetu wengi wa leo hii. Shetani huwa anarudi nyuma pale anapouona uwepo wa Mungu na si hadithi za Mungu!

  Kuna hatua Tatu katika jambo la kuukamilisha Ukombozi.
  Hatua ya Kwanza ni Kuhesabiwa Haki, hapo ulipohubiriwa Injili ya Kristo, nayo ikakuzalishia Imani ndani yako, ukaliamini hilo Neno, likakuongoza katika Ubatizo, ukaondolewa Dhambi zako – ule uhusiano uliokuwa nao na Shetani ukakatiliwa mbali- hivyo ukaondolewa kutoka ktk njia ya Mauti na kuwekwa katika Njia ya Uzima. Basi ukiisha Kuhesabiwa Haki, ni nani awezaye kukushitaki tena; maana Hakimu ndiye aliyekuhesabu wewe kuwa ni unayo Haki ya Uzima wa Milele, hivyo Mauti HAINA haki ya kukudai!!

  Hatua ya Pili, ni UTAKASO. Ukiisha Kuhesabiwa Haki, na kuwekwa katika hiyo Njia ya Uzima, sasa ndipo unaketishwa chini na kufundishwa yoote yanayohusu mwenendo wa mkristo, unapewa mila na desturi mpya, yaani kwa hilo Neno unalolishwa, makazi husafishwa, (Yn 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”)! “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote…”; Neno sasa likijazwa katika kiriba hicho kipya likizibadili tabia na hulka mbovu!!

  Hii ndio Hatua ambayo ina mikanganyiko mingi sana, maana hapa ndipo Mapokeo hujiwakilisha kama Neno la Mungu na kumrejesha Mautini mwaminio! Bali alipaswa kudumu katika Fundisho la Mitume, akiumega ule Mkate, lile Neno!

  Hatua ya Tatu na ya Mwisho, yaani hapo anapokuwa amekamilishwa katika Mafunzo na kufuzu, ndipo Mkaguzi huja na kumkagua, akiridhika humtia Muhuri wa bidhaa iliyokamilika, akimjaza RM, yaani Uzima wa Mungu sasa wakaa ndani yake!!!

  Basi mkristo wa jinsi hii, utamfanyia Deliverance gani? Au akikufikia wewe mwenye kuwafanyia watu hiyo, si utaishia kufanyiwa wewe!!!

  Gbu!!!

 19. Asante Mr. Kirimbai kwa udadavuzi mzuri!

  Kuna makundi angalao matatu ya watu kuhusiana na suala zima la ukombozi.

  Kundi la kwanza wanaamini kuwa mtu akishampokea Kristo mara moja mambo ya laana na ya kinguvu za giza yanakoma mara moja.

  Na kundi la pili wao wanaamini kuwa lazima kila mtu baada ya kumpokea kristo afanyiwe ukombozi.

  Kundi la tatu wao wanaamini kuwa si lazima kila aliyempokea Kristo afanyiwe tena maombi ya ukombozi. Lakini pia si kila mtu anapompokea kristo mara moja mambo yote ya laana na nguvu za giza hukoma mara.

  Mimi niko kundi la tatu.
  Nakubaliana na mtoa hoja kuwa ukombozi ni sehemu ya wokovu. Maana neno wokovu (sozo) ni neno la jumla au ‘inclusive’, lina vitu vingi sana ndani yake.

  Kuna uwezekano mkubwa kabisa mtu akatoka kumpokea Yesu leo na kesho yake akanywa pombe na kulewa,akatukana matusi ya nguoni, akaenda kulala kwa mpenzi wake,n.k.

  Hi ni kwa sababu kitu alichokianza (wokovu) ni safari ya kufanywa upya nia (akili). Na huku kufanywa upya kunafanywa na neno la Mungu. Kwa hiyo jinsi huyu mtu anapolielewa neno la Mungu na kulifanya liwe hai ndani yake, nia yake inazidi kufanywa upya.

  Sasa huu mchakato hutofautiana kati ya mtu na mtu.
  Kwa mfano; mimi huona kuwa ilimchukua Kristo muda mrefu zaidi kumbadilisha Petro kuliko muda alioutumia kumbadilisha Paul. Hii i kwa sababu Paul tayari alikuwa na ile concept ya kumtumikia Mungu, lakini ilikuwa katika mwelekeo usio sawa. Alipoufahamu mwelekeo sahihi alibadili na kuwa mtu safi saana.

  Hivyo basi, siyo sawa kwa wanaofanya huduma za ukombozi kulazimisha kuwa kila mtu anatakiwa kufanyiwa hiyo huduma, hasa wanaofanya ‘deliverance’ kwa njia ya maombi.
  Si kila mtu anatakiwa kufanyiwa ‘deliverance’ kwa njia ya maombi fulani, wengine wanatakiwa tu kupewa ushauri fulan, eg. awe anasoma neno la Mungu,basi tayari huyo anakuwa ameshapewa suluhisho.

  Lakini pia wasiwafanye watu wawategemee wao badala ya kumtegemea Mungu. Maana hicho ndicho ninachokiona sana siku hizi. Kwamba mtu anaaminishwa kuwa tatizo fulani haliwezi kuondoka mpaka akutane na mtu fulani.

  Si kila aliyeokoka anahitaji huduma ya ukombozi, lakini pia si kila aliyeokoka hahitaji huduma ya ukombozi!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s