Kama una Mashaka na Huamini huduma ya mtumishi fulani…

church

KAMA UNA MASHAKA NA HUAMINI HUDUMA YA MTUMISHI FULANI, USIFUNGUE MDOMO KUMSEMA AU KUWASHAWISHI NA WENGINE WAWE NA CHUKI NAYE; KWA KUFANYA VILE, HATA KAMA UNACHOKISEMA NI SAHIHI, LAKINI TAYARI HAUJAKIFANYA KWA KANUNI ZA KIMUNGU, CHUKI YAKO NI SAWA NA UUAJI!

NJIA RAHISI YA KUSHUGHULIKA NA HUYO AMBAYE WEWE UNA MASHAKA NA HUDUMA YAKE AU HUAMINI KWAMBA NI MTUMISHI WA MUNGU, FANYA HAYA YAFUATAYO:

1.Yesu Alisema “TUTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO” (Mathayo 7:15-23) Yaani Tutawatambua Kwa “KILE WANACHOZALISHA” Yaani Kama “WANACHOTOA KINAJENGA UFALME WA MUNGU”, “KINAMTANGAZA YESU NA MSALABA”, “KINALETA WATU TOKA DHAMBINI KUINGIA KWENYE UTAKATIFU”, “KINATOA WATU KWENYE MIKONO YA ADUI KUWAINGIZA KWA BWANA YESU”
Angalia Huyo Mtumishi Anafanya Yafuatayo:
-Anaamini Na Kuhubiri Kuhusu Wokovu Kupitia Msalaba; Ulazima Wake, Umuhimu Wake Na Madhara Ya Kutookoka Hapa Duniani Na Maisha Baada Ya Kifo.
-Anakubali Na Kufundisha Kuhusu Umuhimu Wa Maisha Ya Utakatifu Na Kumcha Mungu Kwa Washirika Wake Na Watu Wengine.
-Anaiamini Na Kuiheshimu Biblia Kama NENO LA MUNGU Na MAAGIZO HALALI YA MUNGU Nakadhalika.

2.Kama Kimetoka Kwa Mungu “KITASIMAMA” Na Kama Hakijatoka Kwa Mungu “KITAKUFA”… Hauhitaji Kushindana Na Mtumishi Yeyote Wa Mungu, Au Anayejiita Wa Mungu: Hii Ni Kanuni Ya Kimungu Ya Kuamua Mambo, Chochote KISICHOTOKA KWA MUNGU KITAKUFA; ILA KILICHOTOKA KWA MUNGU HAKIWEZI KUFA, KADRI KINAVYOPIGWA VITA NDIVYO KINAVYOZIDI KUSTAWI NA KUONGEZEKA… Matendo 5:34-39.

3.Kama Unajua “WEWE UKO VIZURI NA MUNGU” Yaani Unajiona Wewe Ni Mkamilifu Na Rafiki Wa Mungu, Basi “OMBA HUYO NDUGU NA HUDUMA YAKE WANG’OLEWE” Maana “KILA PANDO ASILOPANDA BABA WA MBINGUNI LITANG’OLEWA” Lakini Ukiona “UMEOMBA NA KUKAZANA KUMNG’OA LAKINI BADALA YAKE NDIO ANAZIDI KUSTAWI NA KUONGEZEKA NEEMA NA NGUVU” Ujue “WEWE NDO UNA MATATIZO” Na Ujue “ULIKUWA UNASHINDANA NA MUNGU” Na “UMESHALIKOROGA”

4.Kama Una HEKIMA ZAIDI: Tumia BUSARA Aliyoitoa Yesu “KWENYE MFANO WA NGANO NA MAGUGU” Yaani “VIACHE MAGUGU NA NGANO VYOTE VIKUE PAMOJA” Halafu “MUNGU ATAFANYA MWENYEWE KAZI YA KUTENGA NA KUTOFAUTISHA NGANO NA MAGUGU”
Usijaribu Kufanya Kazi Ambayo Si Yako!

Ile tu Kwamba Mtumishi Fulani “HAHUBIRI AU KUFUNDISHA” Kama “MCHUNGAJI AU ASKOFU WAKO” Haimfanyi Kutokuwa MTUMISHI WA MUNGU… MUNGU ANAYETENDA KAZI NDANI YA WOTE NI MMOJA; LAKINI KWA KILA MTU MUNGU ANATENDA KAZI KWA NAMNA TOFAUTI… Usije Kujiingiza Matatani Ka Kutumia Vigezo Vyako Vya Macho Na Masikio Ya Utafiti!

Siku Njema,

Mwl D.C.K

Advertisements

31 thoughts on “Kama una Mashaka na Huamini huduma ya mtumishi fulani…

 1. Brother Seleli,

  This is nice indeed. Nakupenda rafiki yangu. Unacheka panapostahili. Tungelikuwa tukionana macho kwa macho kam tumecheka mpaka mwovu ananaswa na kigugumizi.

  Right, hatutatishwa na vyeo wanavyo makanisani. Tutachukia maovu yao, tutawaonya kabisa, wakikataa wabebe wao wenyewe damu yao. Mambo mengine tuyaachie Mwenyezi Mungu.

  Kwa hiyo, usijizuize kabisa kunichallenge. I’m strong, na aneenipa nguvu ni Bwana kam Yule anaekupa nguvu. Nilipendezwa sana na hoja yako, RM alikuongoza ili wasiojua kusema “sorry”, “samahani”, nk wajifunze hapa. Lakini wasiitumiye kwenye haistahili au kwa kusemasema tu. Iwe ina sababu ya kiroho. Haleluya!!! Ndugu Seleli, mimi sione tatizo kam tukiwa na maoni tofauti, hiyo ndio inaleta msaada. Nikiona nimetosheka siwezi kuwa na haya ya kusema “asante” au “sorry”, jambo ambalo unalifanya na wewe. Nisaidie ndugu yangu, unafahamu kwa nini wapendwa wetu wengi wanaendelea kukamatilia hata kam wameshindwa?

  Nataka turn off kidogo: Lakini, anyway, nilipima jibu kwa yote, ao kunayo iliobaki ili tuendelee peana mafikara? Ndugu Seleli, tumeitwa kufanya kazi hii ya Bwana; miiba iwe au isiwe tutakachapa tu. Hivi tusichoke kabisa.

  KUNA MSIMAMO FULANI NILIWAI SOMA HAPA KAM “TUKIMBIE MAKANISA AMBAMO WAONGOZI NI WABAYA”. WEWE WASEMAJE? MIM KWA UPANDE WANGU SIWEZI KIMBIA, NITANGOJA MDA WA BWANA WA KUYABOMOA MADHABAHU YALIYOCHAFUKA ILI KUWEKA MADHABAHU MATAKATIFU KAM VILE MANABII WALIVYOFANYA.

  Wale ambao maneno yao inawaingiza jela, wa kina Lwembe na Siyi, nao nawapenda sana. Kuna siku wataokoka (na hii ndio itakuwa furaha kubwa yangu) kwani siku moja watafahamu kam si lazma wangoje niwaarifu mara nyingi pasipo wao kujitambua. Brother Seleli, kweli kuna aliyewai okoka bila kwanza kujitambua? Naamini watajitahidi kuacha uongo. Kam bado kufunzwa kam waongo wote nafasi yao ni katika ziwa la moto, hapa wako wanapata training kiwango itakuwa vigumu tena wanasike kirahisi ktk uongo.

  Hahahaha…, acha nikuchekeshe. Angalia pale karibu kwa mwisho wa rejea za waislamu katika mjadala wa “Ukristo/Uislamu”. Utaona jinsi muislamu mmoja alivyokuwa amekwisha tandika viboko vya hila takrian vitatu vya kufwatana ndugu yangu mukristo mpendwa tena mwenye kuwa na upako. Nilipofika, nikamtandika viboko vya ukweli huyu muislamu. Tulijibiana tu mara mbili kiisha akajitambua na kukimbia, wala hakuna muislamu mwingine aliejitokeza tena. Huyu muislamu hakungoja awe tajiri wa uongo mpaka aingizwe jela kwani alijua imani yake tayari imemuingiza kule. Na kam akijitokeza tena nitamtandika tu. Nikipungukiwa kidogo, najua utamtandika vilevile. Na wengine wanao upako kam wa kina Sungura watamtandika. Haleluya!!! Najua kuna wengine wanao upako, nao sikuwasahau. Mungu awabariki.
  Sasa kam muislamu anakimbia kunaswa, mukristo ndiye ataendelea kujihatarisha? Naamini Lwembe iko karibu kutubu kwani naona yeye anasema anafuata Paulo wakati pengine angali akifuata Saulo!

  Mwl wa mada hii, ana rejea nzuri, lakini pengine ni Mchungaji, sijue, naona harudie kujibu.

  Bwana Yesu Kristo awabariki.

 2. Ziragora,

  Wala husijali, sikua nimejisikia kukasirika ULIPONI CHALLENGE ila nilishangaa tu, napenda sana challenge coz name ninachallneg sana ili kuibua vitu, so my brother, don’t worry, relax man, mi ni aina ya wale wapendwa weather, peace, charming, social, free pia tough, straight, bold and I like be happy and enjoy life, that is my God given software.. ….kwa hiyo, ubarikiwe kwa kuomba masamaha but sikua na anything sema tu umefanya vema coz I can see una software ya unyeyekevu mwingi na kirahisi kuutumia-that is sweet spiritual quality-U CHALLENGE ME TOO now.

  Pia nimecheka sana ….h ha ha ha…..kuhusu Mtu akishaingia jela, hakuna haki…. Ha ha ha, kweli ni Lwembe ndio alitakiwa kusema sorry, na ole wake, akizubaa na akaingia jela, hakuna haki..hahaha, umeitowa wapi iyo tip tamu? kweli bwana ndani jela hata kama mjanja na maneno mengi ya Lwembe ya ivi ivi, utatiishwa na kunyamazishwa tu.

  Nimeona pia elaborations zako, ni powerful na hili angalizo naliweka ktk herufi kubwa nimelipenda sana… Tutakataa/Tutachukia matendo mabaya yao (ndio maana ya chuki hiyo) ILA TUTAENDELEA KUPENDA MTU-aisee, great balance, nimekusoma mno/nimekupata kabisa kwa iyo warning, ubarikiwe

  Press on

 3. Ndugu yangu Seleli,

  Hivi nikwishaomba masamaha, nimekuwa na nguvu tena. Nimechukua text moja yako tu: ambayo ninataka nizungumzie:

  “Nauliza, UNA UHAKIKA NA UNA MAANISHA BIBLICALLY, SPIRITUALY, pia KIHUDUMA ZILIZOPO, KIHALI-HALISI MAKANISANI, WATUMISHI WA LEO NA KILEO, kua hakuna haja ya kufanya alivyofanya Yesu -pasua-pasu ‘michezo michafu’ ya baadhi ya Wanadamu/Viongozi wa dini/imani/huduma kwa kua tu Yesu ameshajenga Kanisa ivyo hamna shida wala tabu?

  Kuhusu la chuki, nadhani nimeeleza vema ktk response yangu ya pili. Chuki uliyoelezea wewe ni tofauti na niliyomaanisha- I MEANT a natural or side effects baada ya Waaongozwaji na Waongozaji wa mambo ya imani, kujua Kweli ya Mungu, wako wanaoaibishwa uovu wao na wasingefurahi na wako pia wanaojisikia kukasirika kwa nini wanamedanagwa na hao walaghai kwa njia ya madhabau/dini/imani.”

  Naanza na hii ya mwisho.:
  Jinsi umetafsiri sasa hii “chuki”, una haki. Tutakataa matendo mabaya yao (ndio maana ya chuki hiyo). Ni kweli hapo tutachukia matendo lakini tutaendelea kupenda mtu. You’re right.

  Ya kwanza:
  Uhakika kuwa watumishi wote wako right sina. Lakini aliejenga yupo hakubaki kaburini. Yeye ndiye anayo mamlaka ya kujenga na kubomoa. Ndio maana ukitazama vizuri utaona Yesu akibomoa wale watumishi wabaya. Kwa mfano: mchungaji anaeabudu hela na wanawake, yule hawezikosa kuongoza vibaya waumini. Lakini omba na chunga kidogo utaona jinsi Mungu atampindua. Mim nimekwishafanya ile mara nyingi na nimeona matunda. Utaona Mchungaji kama yule akikamatika hadharani katika uasharati na kukimbia pasipo mtu wa kanisa kumgusa. Hii si kwa wachungaji tu, ni hata kwa kila yeyote anaeshikilia uongozi. Neno la Mungu linasema “Muwabariki, wala msiwalaani”. Amefanya vibaya kwani yeye ni mwanaadamu. Kuna njia mbili:
  -Wala wewe umeona tendo lake ni libaya kwa kukosa maarifa.
  -Wala kweli tendo lake ni mbaya.
  Ukitazama vizuri utakuta tu kimbilio ni Kristo; ukimuomba atanyoosha njia zako ao kam njia zako ni safi atashululika na njia za mchungaji.

  Karibu tena ndugu yangu.

  Ubarikiwe

 4. Lwembe,

  Uliyonukuu ni yangu wala si ya Seleli. Kumhusisha Seleli ni hila tu. Unachotakiwa kujifunza hapa kwanza ni kufahamu kam kuomba masamaha si jambo gumu. Sasa kam ulishindwa omba masamaha huko tulipokuwa, wakati ni wako hapa. Sikulazimishe kutaja moja kwa moja wongo uliyohusika nayo; ukisema tu “samahani kwa wongo ule wote”, ukiisema kwa dhati, utasamehewa. Sivyo kuna rights abazo huna ukiwa jela.

  Asante.

 5. Ndg Ziragora, Seleli

  Kuna jambo limenitatiza kidogo ktk inputs zenu, ambalo naona mmekubaliana ktk hilo, ndipo ninawaomba mnifafanulie kidogo ili sote tuweze kwenda sawa.

  Ngoja nikinukuu hicho alichokisema Ziragora”
  “”2. Yesu kuwasambua hao mafarisayo alitafuta jenga kanisa lake linalo msingi kefa. Limekwisha jengwa kwa limoja, na neno linasema kam hata nguvu za kuzimu haziwezi libomoa.
“Mathayo 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.””

  Basi kutoka maelezo hayo napenda kuuliza, Je, kuna makanisa mawili, moja likiwa ndilo hili lililo jengwa juu ya Msingi wa Kefa kulingana na maelezo hayo niliyoyanukuu, na jingine lililojengwa juu ya Msingi wa mitume na manabii, Efe 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.”??

  Na kama ni hivyo, nini tofauti ya makanisa hayo?

  Gbu!

 6. “Mwl” DCK na wapendwa mliolielewa somo,

  Mafundisho ni mazuri sana, lakini yanahitaji uangalifu maana jambo la ‘mashaka’ ni pana, au tusema ni matofali yanayotumika kujengea fensi ambayo ikikamilika ndipo yaweza kuwa Chuki, na si lazima iwe ni ile ya kuua, bali yaweza pia kuwa ni ile ya kuichukia dhambi uliyoiona imefanya makazi katika huduma hiyo!

  Point na 3 imenitatiza kidogo, unasema niombe kwa Mungu Huduma yake na yeye mwenyewe ving’olewe, halafu unasema nikiona wanashamiri basi nijue kuwa mimi ndiye niliyelikoroga! Sasa uhakika wa maombi yangu uko wapi katika hili, ni huko kushindwa kwangu? Kwamba hajang’olewa na dhambi ninaiona ingalipo, kwa ushauri wako napaswa kujiunga ktk dhambi hiyo kwa kule kushindwa kwangu?

  Mimi nadhani mwaminio akifika katika hatua ya kuwa na mashaka au kutokuiamini huduma ya mtumishi anayemuongoza, yaani akawa anajua kuliko labda pastor wake, kiutaratibu anapaswa AONDOKE katika kusanyiko hilo, tena akimuaga pastor wake ni vizuri zaidi, na iwapo pastor atampa nafasi ya kuliaga kusanyiko, sawa, bali yeye hapaswi kulivyruga kusanyiko hilo kwa kuanza kushawishi wengine!

  Pia watumishi nao hawapaswi kuwang’ang’ania waumini kwa vitisho vya laana nk ili mradi kuwatiisha wabaki hapo na kuyameza maovu yao!

  Basi kwa mfano, kama ambavyo mimi umenitatiza na kunizalishia mashaka kwa pointi hiyo na 3, kama nilivyoionesha, na pia kwa wewe kujitambulisha na kuitwa “mwalimu” kinyume na neno la Mungu katika Mt 23:8 “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu”; ndiyo kusema sasa hivi nianze maombi ya wewe na huduma yako mng’olewe au nikiwa na hekima nikuache ukue ungoje kuvunwa kama AU NIKUREJEZE??

  Gbu!

 7. Ndungu yangu Seleli,

  Najua unanifahamu hata kama hatujaonana macho kwa macho. Anyway Mungu akituwezesha tutaonana tu. Ina maana unajua ninachopenda. Nami nakufahamu vizuri rafiki yangu. Uko mwanaume; Tumejadili siku za kutosha na bado jijaona unadanganya; Kwani kuna wale wanachanganya kusimamisha maoni na kudanganya.

  Niliona pia kam wanaojadili wako aina mbalimbali:
  -Wanaopost tu kiisha wanangoja wengine watoe maoni.
  -Wanaoomba shauri.
  -Wanaoswali, wakiisha pata jibu, basi.
  -WANAOCHALLANGE KWA WEMA ILI WAELIMISHANE.
  -Wanaochallenge ili chini-juu wapate haki.

  Nafikiri umeona nafasi yetu sisi wawili.

  Usijidharau Seleli, najua kuna wenye kuendesha shule yao ya Master ya kiteologia wakitafuta elimu kwa hii tunayojadili. Hapa kuna utafiti. Unajua kujadili ukiwa na RM inaleta mtililiko wa maneno ya Mungu ambayo huwezipata ndani ya shule.
  Je kwa nini nilikuwa kama nime give up? Ukinifahamu najua utafahamu kam napima kuwa mkweli. Ni hii mwelekezo ndiyo ningelipenda wana SG wakamate pamoja na ku challenge ili kuwe mtililiko wa maneno ya Mungu. Kuna wenye kujadili wakiweka wongo, kwao nasema never jadili with them.
  Kwako sivyo. Njoo maana nikakuomba kunisamehe. Nilitambua kama mim ndie nilisisimua kutonielewa kwako wakati niliposema “hoja yako haishitushe” wakati wewe ulieandika uliona ina shindo.

  Jambo lingine ni kwamba niliheshimu vilevile huyu Mwalimu kwani sawa jinsi uliona alileta mada ambayo alitengeneza vizuri.

  Kiukweli, nilipata mda ya kutosha kwa kujibu kwa yale ulioniandikia. Kwani nilifikiri sana, usiku na mchana.

  Sasa, nilipoona nimekuletea AMPB makusudi tu tusaidiane, nikakuona umenukuu tu ambayo nimekuandikia kutoka hio version, kiisha ukaendelea na version yako tu hapo ukiwa kama una ile AMPB lakini bila kujali nayo, kwani nafasi nyingine ulionipatia kwa mtililiko nayo ina tafsiri nyingi ktk AMPB, nikafikikiri kuwa nimekuumiza nikikuambia hoja yako haishitushe, hivi umeniwekea kikwazo makusudi nisiendelee kukusumbua. Ndipo nikaona sina jinsi ya kuendelea. Hata hivi sina namna rafiki yangu isipokuwa kam unaweza rudilia hata swali moja na tunaendelea polepole tukijua kinachofanyika. Naomba tena unisamehe kabisa. Kwangu kuomba masamaha kama ninaipewa au la ndio inanipa nguvu.

  Hence, nakushukuru sana namna ulivyoshikilia jibu langu na pendo ulilo nalo. You’re special.

  Hivi ndivyo inatakiwa wandugu kuongea wakiwa wakweli.

  Jesus Christ bless you.

 8. Seleli,
  Maswali yako nimejaribu kuyajibu kiujumla sana. Jaribu kuyapitia majibu yangu, nina imani yatakupa picha tu na mwelekeo wa wewe kuchimba zaidi juu ya hicho nilichokisema kwenye majibu haya.
  Swali
  Wakolosai 4:6. Unaona nini hapo? Je umefanya sawa kulitumia kwa point yako kuhusu kuonya? We waonaje/Wajionaje hapo? uko sawa?
  Jibu
  Ndiyo nimeona. Na ninaona nimelitendea haki hilo fungu, maana liko sawa na niko sahihi na sawa kabisa.
  Baada ya hilo jibu tangulizi, sasa twende nikuelekeze kwa nini nimesema kuwa niko sahihi! Rejea kwanza…. Wagalatia.3:1,3.., Mathayo.3:7, Mathyo.16:1-4, Yohana.8:44
  Ukiangalia vizuri aya hizo hapo juu, ukiondoa ile ya Paulo kwa Wagalatia, utakuta Yesu akizungumza na walimu wa dini ambao kimsingi walikuwa ni wanafiki – Mafarisayo, masandukayo na waandishi (pritenders). Yesu alitumia lugha kali kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuona kile mtu akiwazacho. Waliwaza tofauti na walitenda/sema tofauti. Ndiyo maana Kristo alitumia lugha kali. Yesu aliyaona mashaka yao, kutokuamini kwao, kejeli zao, na mafikara yote mabaya yaliyokuwa yamesheheni ndani ya mioyo ya hao wanaume wanafiki. Hii ndiyo sababu kubwa iliyomfanya Yesu awakemee kwa lugha kali.
  Lakini ukiangalia sehemu ambazo Yesu alikutana na watu tofauti na wanafiki, Yesu alitumia lugha nzuri mno. Unakumbuka kisa cha Magdelene alivyoletwa kwa Yesu ili apondwe mawe? Kwa vile Magdalene alikuwa ni kahaba, tungetarajia Yesu amkaripie sana. Lakini Yesu alipoungalia moyo wa Magdelene ukijuta kwa lile alilokuwa amelifanya, lugha aliyotumia Yesu kwa mwanamke huyo ilikuwa ya upole tu-Yoh 8:1….
  Yesu alipokuwa kisimani na mwanamke msamaria…Fuatilia mazungumzo hayo. Fuatilia Yesu alipokuwa kwa dada zake Lazaro. Jaribu kufuatilia visa vya namna hii halafu ulinganishe na majibu ya Yesu kwa walimu wanafiki. Mf. mwingine nikupatie wa Marko 11: 27 Wakafika Yerusalemu tena; hata alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee,
  28 wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? 29 Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.
  30 Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni. 31 Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini? 32 Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, – waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi. 33 Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.

  Ukifikri haraka haraka, unaweza kusema jibu hili la Yesu lilikuwa ni jibu la jino kwa jino. La hasha! Walichokiuliza, sicho walichokitaka!!

  Hali kadhalika, na mitume nao walifuata njia ileile. Kwa vile wao hawakuwa na uwezo wa kusoma mioyo ya watu, wao walikuwa wakishughulika na watu vichwa maji. Watu wagumu wa kuelewa. Wasiobadilika. Walevi wa dhambi. Ukiangalia sehemu zote ambazo mitume walikuwa wameshafundisha halafu watu wakaonekana kurudia matapishi, mitume walionekana kutumia lugha kali ya kuonya. Mfano mmojawapo ni ule wa Wagalatia.3:1,3… Hili ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote anaporudia kukemea jambo kwa mara ya pili, tatu nk, sharti utumie shada(stress) tofauti na ile ya kwanza. Ndiyo maana nikakwambia kuwa, sisi tunaoliitia jina la Bwana, tunapaswa kuwa na lugha nzuri kwa hao wasiomjua Mungu, watu wanaotenda dhambi (kwa mara nyingine), bila ya kukusudia. Lakini kwa wale wanaotenda dhambi za makusudi na dhambi za uasi, hawa sharti tutumie lugha kali za kuonya, kukemea na kuwarudi. Ndiyo maana kwa nature ya kazi hii ilivyo(kufundisha), ilikuwa ni kazi ya wanaume tu tangu mwanzo, japo kwa sasa ibilisi amefanikiwa kuwapumbaza watu leo kuna wanawake wachungaji. Sitaki kwenda huko lakini najaribu kuonesha tu jinsi mambo yalivyokuwa.
  Swali:
  Nionyeshe the so called MANENO YALIYOKOLEA MUNYU HAPO KTK KUONYA ulikokumaanisha wewe ukianzia kwa statement ya Paul mwenyewe aliyosema kwa Wagalatia maana ndiye aliyesema kwa Wakolosai kuhusu maneno yaliyokolea munyu
  Jibu
  Kwa vile umesema nianze na Paulo, kwa kuzingatia maelezo hayo hapo juu, angalia kisa cha hubiri la Paulo ktk Matendo ya Mitume 17:23…. Ukisoma vizuri kisa hiki, Paulo kwa vile aliwakuta kwa mara ya kwanza wakiabudu mungu asiyejulikana, mtu huyo anaonekana kuwaingia kwa lugha positive kabisa na wao wanakuwa tayari kumsikiliza. Lakini angefika akawaaambia kama alivyofanya kwa wagalatia, wasingemsikiliza hata kidogo. Mifano mingine, jaribu kufuatilia kutengana kwa Paulo na Barnaba kwa sababu ya Yohana Marko(mdo 15….), Jaribu kuangalia lugha ya Paulo kwa Filemon kumhusu Onesmo(filemoni 1…). Lakini pia angalia Yohana Marko anaungana na Paulo na akina Barnaba tena ktk utumishi nk. Kuna mifano mingi sana Seleli. Jaribu na wewe kufuatilia mambo haya. Najua kwa vile wewe ni Associate Prof. sina shaka ktk hilo. Inakubidi uwe Full Prof. kwa kuwa mtendaji wa neno(msabato halisi) na si muigizaji tu.
  Mungu akubariki.

 9. Siyi,

  Usinichekeshe rafiki yangu wa miaka

  Ati mi kiboko! Mie tena? can a memory card be proud kua iko kiboko ikiwa haijaingizwa kwa kifaa chochote eg sm, saa, laptop nk? ha ha ha amen? JESUS in and via me ndio Kiboko, glory to God..

  Usiogope kunasa, kwa neema ya Bwana tutanasuana, so twende kazi, nakungoja majibu yako niruke na wewe in love au kama vipi, sepa!

  Press on

 10. Ziragora,

  Sema labda hujapata muda wa kusoma yote niliyokuandikia, ungesoma nguekuta asante yangu na kufurahi sana maana kuna kitu umeshangaza kweli kwa uzuri na utamu na upako kabisa, maana paragraph moja nimesema/kukiri iv… nanukuu…

  ‘’’Swali langu tuichukulie kwa uzito upi statement ya Gamalieli- Mdo.5:34-39, ukasema kua hakusema jipya maana alikua Mwl wa Sheria na umemanisha kua BILA SHAKA analijua andiko hili….“Mhubiri 3:14: Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.?,…..nimefurahi sana kama ulivyosema ujibu ili unifurahishe, excellent indeed and lovely good big levelling job

  Si umeona nilivyobarikiwa na kazi yako njema? PLZ READ ALL

  Otherwise, love u man of God and my brother- by the way nakukubali sana, uko na Neno na u can make strong and tangible senses, nakufahamu sana umu SG, mimi kukuchallenge na kukuweka au kuwekana sawa haimaanishi sitambui grace Mungu alikupa, unatisha sana kwa uzuri wa Mungu na ufahamu wa Neno ndani yako, glory to God,amen, una capacity kubwa mno brother, love u, hata normal thinking/reasoning yako ni so huge. Una Neno sana wewe.

  Press on

 11. Ndugu Seleli,

  Nataka nikujibu kwa hoja zako 3 at once na kwa jinsi hutashangaa tena.

  Nashukuru sana. Lengo langu si kujadili. Hata wewe iliona hiyo mapema. Nilipoona ulileta mambo sahihi kabisa kufwatana na tafsiri ya Biblia uliyoitumia, nilifikiri nikuletee mchango wangu kama rafiki ili usipoteze mda, nikikuletea tafsiri inayo leta nuru zaidi kwa zile shairi mbili zilizosisimua hoja yako. Chukueni hili jambo kam jinsi ningelikuwa na namba yako ya simu ningelikupigia tu. Nikajipanga zaidi kwa ile shairi ambayo wewe binafsi uliweka kama msingi wa hoja yako. Baadae nikakuletea maandiko ambayo nilidhani hukuona.

  Kama haikukusaidia, tafadhali NISAMEHE kwani sitapata mengine zaidi ya yale ambayo nilidhani utayachukua kuwa kitu cha faida. Lakini kama ilikusaidia kidogo nakuomba ikiwezekana kwa upande wako, nitolee hata ka asante kadogo rafiki yangu.

  Mambo mengine, tuyaachie basi Mwalimu kwani lengo langu si kisimamisha hoja katika hii mada ya Mawalimu ambayo ni kam « Aladdin’s cave ». I realize that to go on like this is to become more than an Admirable Crichton. Why not let SG’s people continue to glorify God for Mwalimu’s advices!

  Kwa kuwa umeniandikia mingi nakushukuru sana, ni neema kubwa. Kwa hivi kama uliyosoma kutoka kwangu inakuletea utata, samahani. Kiukweli sina ingine msaada niliyobaki nayo kwa hoja yako. Mukristo anasemeshaga ukweli… Hata chakacha sina ! Uliyoniswali yote, endelea pekua toleo langu utapata jibu tu. Alimradhi, huwezi kosa kitu katika nilichokutolea kwa nia njema isiyo ya upinzani. Naamini umenielewa rafiki yangu.

  Asante kwa kunichukulia basi kaka, uwe na amani na usijihukumu kwa jambo lolote.

  Mungu wa Mbinguni akubariki.

 12. Seleli,
  Mmh!! Maswali yako haya!!
  Maana una mashaka na majibu yangu yaliyopita na yajayo pia!! Nitanasa, teh teh teh!! Wewe kiboko bro!! Ngoja niyasome taratibu na kuyajibu taratibu ili nisinase!! Sawa kaka?? Nitayajibu muda si mrefu.

 13. Siyi, Shalom

  May I challenge/advice/encourange you kua Unapojibu au changia kitu hapa SG, just relax, uwe huru tu, hii kusema umejibu kifupi au sijui umenichanganya, plz drop them….always kama unajiamini na una hoja, Neno, kitu or any serious stuff for serious minds/spirits/hearts, just freely flow/share and be ready for any response- namely soft and sweetily juicy AU stony and citric !!!!!!!! Pia am happy kukujulisha confidently kua mi napendaga kuji-dedicate kwa jambo/huduma ivyo ukijibu kwa kirefu kama makala za gazeti la Mawio u Raia Mwema nitasoma kila dot kwa raha na hamu na kijibu kila spot sinaga shida maana nami pia ni mtu wa mambo marefu/mengi, so we leta tu iwe kitabu au kadogo, vyote nitakula na kujibu vema kabisa.Amen

  Mimi NIKUCHANGAMSHE na siyo ‘’KUKUCHANGANYA yako’ kama ifuatavyo:

  Andiko hili la Wakolosai 4:6 ambalo umelinukuu kusemelea swala la kuonya, embu tulitafakari ktk context yake yote kwa kuzingatia mistari michache ya juu yake ya 2-5….

  2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; 3 mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, 4 ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena. 5 Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

  Notice: Anawaambia kua…. Ili wajue jinsi iwapasavyo KUMJIBU kila mtu

  Unaona nini hapo? Je umefanya sawa kulitumia kwa point yako kuhusu kuonya? We waonaje/Wajionaje hapo? uko sawa?

  Nonetheless, kama niki buy point yako ivyo ivyo tu bila kuangalia context ya andiko ilo na nikakubaliana kienyeji na wewe tulitumie kwa maana ya kuonya ilo andiko, soma haya maandiko kwanza kisha jibu swali

  Paul ktk Wagalatia.3:1,3.. anashangaa na kukemea/kuonya kwa maneno/speech ya flavor hii….
  ‘’Enyi Wagalatia msio na akili/wajinga, nani amewaloga? ……………2 Je! Mmekuwa wajinga namna hii? ……………………….. Notice words…Wajinga/kulogwa

  Yohana Mbatizaji naye ktk Mathayo.3:7 anasema
  ‘’Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? Notice: words…Wazao wa nyoka

  Funga kazi ni Yesu mwenyewe maeneo mengi ila mfano ktk Mathyo.16:1-4
  1 Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. 2 Akajibu, akawaambia, [Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. 3 Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?] 4 Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake. Notice mstari 4 words…Kizazi kibaya cha zinaa.

  Yohana.8:44
  Ninyi ni watoto wa baba yenu shetani; kwa hiyo mnapenda kufanya maovu kama yeye. Tangu mwanzo yeye alikuwa muuaji na hana uhusiano wo wote na mambo ya kweli; kwa maana hana asili ya kusema lililo kweli. Shetani anapodanga nya anadhihirisha asili yake kwa kuwa yeye ni mwongo na ni baba wa uongo. Notice: Words Ninyi ni Watoto wa baba yenu ibilisi/shetani

  Swali: Nionyeshe the so called MANENO YALIYOKOLEA MUNYU HAPO KTK KUONYA ulikokumaanisha wewe ukianzia kwa statement ya Paul mwenyewe aliyosema kwa Wagalatia maana ndiye aliyesema kwa Wakolosai kuhusu maneno yaliyokolea munyu

  Umesema/Umekiri kua kuna nyakati Yesu alitumia lugha kali kwa kua alikua na uwezo wa kusoma mioyo yao na kwamba sisi hatuna uwezo huo so tunatakiwa kukemea lugha nzuri!

  Maswali:

  (a) Paul kwa lugha ile kwa Wagalatia naye alikua na uwezo wa kusoma mioyo ya wanadamu?

  (b) Je ni mambo yote mabaya/mis conducts za baadhi ya Watumishi/Huduma, hatupaswi kuzifyatua kisha mpaka tufunuliwe/ kuona mioyo?

  (c) Je Tunaweza hukumu kwa kuliangalia Neno au kila kitu mpaka kufunuliwa? Je Neno lina kazi gani? Halina nafasi? Ni kwa RM tu? je kuna ufunuo zaid ya Neno kweli?

  Naona kwa mchango wako UMEJICHANGANYA mwenyewe kwa kiasi kikubwa wala si kunichnganya mie.Niseme tena kua pengine uliwahi sana kusema kua mchango wangu una majibu yangu!!!!!!!! Be informed kua Niliyouliza yana misisitizo yanayotafuta, njoo taratibu hapa, usikimbie ili mradi tu kujibu, utanasa vibaya kama ulivyonasa, pole but karibu kwa response nyingine ya hiyo niliyokupa sasa then nitakujia tena nikishaisoma yako

  Press on

 14. Ziragora

  Statement yako hii….’’Mwalimu hatarudi tena kwani hakuna hoja inayoshitusha ya kumrudisha hapa’’ IMENISHANGAZA KIDOGO! Well, let me check your inputs kama zimenisaidia mambo/hoja nilizoleta!

  Kuhusu kua umejibu kila nilichouliza kwa ufafanuzi wa Maandiko uliochambua kwa kunukuu AMPB, tafadhari pitia ufafanuzi ktk response yangu kwa hayo, utafahamu mara moja kua uliongea HARDLY connected stuff to the main thing/context ya maandiki hayo

  Swali langu tuichukulie kwa uzito upi statement ya Gamalieli- Mdo.5:34-39, ukasema kua hakusema jipya maana alikua Mwl wa Sheria na umemanisha kua BILA SHAKA analijua andiko hili….“Mhubiri 3:14: Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.?,…..nimefurahi sana kama ulivyosema ujibu ili unifurahishe, excellent indeed and lovely good big levelling job

  Ili la …“Mathayo 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

  Umesema kua Yesu alishajenga Kanisa, kwa hiyo hakuna haja ya kupasua-pasu mambo maana una maanisha..hayapo!

  Sasa, nikuulize kitu kimoja on SERIOUS NOTE utakavyojibu, then next post nitaona kama kuna haja ya kueleza/uliza zaidi.

  Nauliza, UNA UHAKIKA NA UNA MAANISHA BIBLICALLY, SPIRITUALY, pia KIHUDUMA ZILIZOPO, KIHALI-HALISI MAKANISANI, WATUMISHI WA LEO NA KILEO, kua hakuna haja ya kufanya alivyofanya Yesu -pasua-pasu ‘michezo michafu’ ya baadhi ya Wanadamu/Viongozi wa dini/imani/huduma kwa kua tu Yesu ameshajenga Kanisa ivyo hamna shida wala tabu?

  Kuhusu la chuki, nadhani nimeeleza vema ktk response yangu ya pili. Chuki uliyoelezea wewe ni tofauti na niliyomaanisha- I MEANT a natural or side effects baada ya Waaongozwaji na Waongozaji wa mambo ya imani, kujua Kweli ya Mungu, wako wanaoaibishwa uovu wao na wasingefurahi na wako pia wanaojisikia kukasirika kwa nini wanamedanagwa na hao walaghai kwa njia ya madhabau/dini/imani.

  Labda niulize tena kua, So mpaka hapa, una uhakika kweli umejibu KILA NILICHOLETA? Real? Kindly revist your conclusion.

  Press on

 15. Ziragora,

  Naendelea kidogo my responses kwa yako:

  Johana 7:24 – Umeifafamua kua inahusu hata mambo binafsi, kua makini namna tunavyohusiana na Wake/Waume, adhibu watoto, yaani ni evaluation of our acts/ourselves

  Lakini andiko ilo ukisoma toka mistari 14-22-Unaona Yesu anawaambia wale waliokua wanamwinda kumuua na hata waliposikia ana nena, wakishangaa kwa dharau fulani kua awezaje kunena safi vile wakati no shule, ndipo Yesu anawapa shule ya ukweli kua doctrine yake ameipata wapi then anawa-challenge, as a matter of fact, anawa-criticise/hukumu kua Musa aliwapa amri but NONE OF THEM KEPTS IT yaani kwa kua wanatafuta kumua kuko wapi kuzishika amri? Na tea anawapa sababu ya chuki zao za kuua ni kwakua alimponya Mtu siku ya sabato

  NDIPO mstari wetu wa 24…anasema…’’Msihukumu hukumu ya macho tu bali fanyeni hukumu iliyo ya haki’’-simply means, kama Watatafakari vema na kufika level ya kufahamu kua kutenda jema siku ya sabato si shida, then hawana solid ground ya kumhukumu Yesu ovyo/kijuu juu kua Yeye ni mvurugaji wa Amri/taratibu,

  Sasa huo ufafanuzi wako wa hili andiko kuli associate na Mme/Ke home, Parents/Watoto home, wanavyohusiana na kuhukumiana, wapi na wapi Kaka?

  Ndio maana nikasema maandiko yote mawili Mat.7:1 na Yoh.7:24 NIRUDIE KUSEMA KUA hata ukiyatazama ktkt Biblia za aina nyingi-kitu ambacho nami hufanyaga sana kabla ya kujenga hoja au kufundisha jambo au kuleta msg, , HAKUNA MAHALA POPOTE, TUMEKATAZWA KUHUKUMU bali kimantiki/hoja/msisitizo/ the real thing Jesus was pressing on hapo ni WATU KUWA FAIR KAMA SI TRUE TUNAPOHUKUMU/ CRITICISE/CONDEMN….that is simple teaching Jesus meant.

  Kwaiyo kama namuona Mtumishi au mpendwa yuko nje ya Neno kwa matendo na maneno yake na inaku si bahati mbaya bali ni kama approved way of conduct kwakwe, KWA UJASIRI KAMA SIMBA NA WA BWANA, nitamkosoa/kemea/karipia, mwambia kua Yeye ni nabii wa uwongo, Mtume/Mchungaji ovyo/ tapeli na sitamuonea haya wala kumung’unya maneno! Why? BECAUSE NO WHERE IN THE BIBLE TUMEKATWAZWA!!!!!!! AS LONG AS ni true kua yuko nje ya Neno kama order of the day or at least on regular basis, ataambiwa mara moja kua yeye ni muovu tu kama kawaida.

  Ulifafanua kua critics si halali!!!!!! JIBU: zitakua si halai pale tu zitakapofanyika unfairly/ si kihaki.

  Kuhusu Chuki maelezo uliyotoa pia ni tofauti ndugu Ziragora.

  Niliseme kua kama sina chuki na nimeookoka vema, najua Neno( by the way hakuna kuifanya Biblia ni ngumu sana kiasi icho ati mpaka wataalamu waje-labda kwa baadhi ya concepts tena n kwa yale ya kichuo cha Biblia but ya rohoni, mepesi sana kufahamika), nikamkosoa/hukumu ya haki kua fulani si mtumishi bali msanii tu au mjanja wa mjini, wachumia madhabahuni iligeally, ni wazi itakua ivyo kua huyo mtu ni mbofu tu.

  Nikasema pia, wakati unashambulia uovu na wana uovu, chuki kuwepo haikwepeki, wale unaowashambulia watachukia na wale unaowapa kweli kisha wakagundua-WAKAIJUA KWEI kua walitekwa-KWELI ikawaweka huru-lazima watasikia kumkasirikia yule tapeli wa madhabahuni- Wakati unapobomoa misngi ya devo na kusimamisha ya Mungu , chuki itatokea na hatujali- tunachapa kazi tu-Yohana.7:7..Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi bali Wanichukia mimi maana nahushudia kinyume na uovu wake…

  Ndio chuki nilimaanisha kua haikwepeki wala hatuna haja ya kuitetemekea ikitokea wakati tunachapa kazi

  Sasa ilo andiko uliloleta la Waefeso.4:26… Tuwe na hasira ila tusitende dhambi….. wapi na wapi? Hamna connection ya chuki niliyozungumzia…

  Press on(nitamalizia kurespond comment zako za mwisho)

 16. Ziragora

  Nimesoma michango yako, nilidhani nijizuie tu ili Mwl aje, lakini naona unapenda tuongeee kwa kusaidiana au kukosoana kwa nia njema bila shaka, naam, nimeitika sasa na naanza kama ifuatavyo:

  Katika andiko toka Amplified Bible la Matthew. 7.1 “DO NOT judge {and} criticize {and} condemn others, so that you may not be judged {and} criticized {and} condemned your selves.”, Umefafanua kua Tusihukumu/Kuhukumu ya hapo ni associated to condemning someone kwa jehanum

  Sidhani kama AMPB ilivyotumia neno ilo, CONDEMNATION, ilimaanisha condemning ya uliyosema wewe yaani kumuhukumu Mtu kama vile ni wa kwenda jehanum au la. Nadhani ufafanuzi wako wa iyo condemnation umepitiliza iyo ya AMPB maana wazo kuu linaloflow freely and cheaply, ukilisoma toka mistari hii yote Mt.7:1-5 Angalia bold comments zangu ktk brackets)

  1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi( Kutohukumu anakokataza/maanisha hapa kuna husiana na concept anayotaka kusema mistari inayofuata)

  2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa( Kama hatutazingatia katazo ilo la kuhukumu kwa kujali icho anachotaka tukielewe tunapotaka kuhukumu LA SIVYO TUACHE KABISA, basi tumo hatarini kupewa/kutendewa/kuhukumiwa nasi ivyo ivyo kirejareja/ovyo ovyo/ illegally/unfairly/inconsiderably, baselessly/bila uangalifu wa kuzingatia icho anachokiweka kama mizani ya kuhukumu)

  3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako(hapa sasa ameweka wazi mizani au kitu cha kuzingatia wakati wa utoji hukumu yaani KUTOA KWANZA BORITI TOKA JICHO LAKO KISHA UTAONA VEMA ILI KUWEZA TOA KIBANZI CHA JICHONI KWA MWENZAKO)

  Look at these arrangements….. Msihukumu….toa boriti kwako kisha toa kibanzi kwa mwenzio which simply means….no prohibition kuhukumu bali IKIFANYIKA…IZINGATIE KIWANGO ICHO! kipi? toa boriti kwanza kwako kisha toa kibanzi kwa mwenzio.

  Pia Kutoa Boriti/Kibanzi ni lugha ya picha kumaanisha vitu visivyotakiwa ktk jicho hence should simply mean Kumtoa mwenzio makosa/kasoro/madhaifu na si swala la kumuhukumu kua fulani ni wa kwenda jehanuma!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwa maneno mengine, Yesu katika maneno hayo ambayo ni mwendelezo wa hotuba yake maarufu inayoitwa Hotuba/Ujumbe wa/ya Mlimani-Mathayo sura zote 5,6,7 ambamo alifundisha mengi na vitu vingi mchanganyiko ktk sura izo/hotuba iyo, alikua anaweka tahadhari/angalizo kirahisi kabisa kua kama tunahukumu au criticise wengine, tuhakikishe hatuna tatizo la wao kutushangaa kua inakuaje tunawakosoa/criticise wakati na siye tuna matatizo- maboriti kibao-ivyo tu! so simple, hakuna jehanum kua ameokoka au la concept hapo!!!!!!!!!!!!!!

  Press on( Nita-respond kwa mchango wako kwa Yohana 7:24 na mwingine)

 17. Ndugu Seleli,

  Pengine Mwalimu hatarudi tena kwani hakuna hoja inayoshitusha ya kumrudisha hapa. Tuache basi watu waendelee kumfwata vizuri.

  Kwanza baadhi ya mambo yako yote nimeyajibu kwa ile vifungo viwili vilivyokuskuma kupanga suali zingine ambavyo ni: ufafanuzi ya shairi ya Mathayo 7:1 na Yohana 7:24, na uhalalishaji wa chuki.

  Kama ulisoma nadhani huna tena chuki na umesikia kwamba usihukumu(condemn) ili nawe usihukumiwe(condemned).

  Kwa kukufurahisha tu kama rafiki yangu, acha niseme juu ya ile unayoita ya Gamalieli ndani ya Mdo.5:34-39 na unayosema juu ya Yesu.

  1. Gamalieli:
  -Huyu mwanaume alikuwa mwalimu wa Torati. Ina maana alijua maneno ya unabii licha ya kwamba hakuwa mukristo.
  -Neno Gamalieli alilosema lilisemwa tangu agano la kale:
  “Mhubiri 3:14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.”

  Hivi Gamalieli aliyoyasema akikataza wayahudi wenzake kudhuru kazi ya Mungu alifunzwa kutoka neno la Mungu la agano la kale. Hence, huyu Gamalieli alitumiwa na Mungu wala hakuleta neno jipya.

  2. Yesu kuwasambua hao mafarisayo alitafuta jenga kanisa lake linalo msingi kefa. Limekwisha jengwa kwa limoja, na neno linasema kam hata nguvu za kuzimu haziwezi libomoa.
  “Mathayo 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

  Sasa wewe rafiki yangu seleli, unataka pasua-pasua ili ujenge kanisa lipi? Utakuwa Yesu mwingine? Naamini huna hiyo mafikara na kam ulipenda tu leta changamoto ili kutoka hii mada elimu izidi.

  Asante basi na uwe na salama.

 18. Shalom Seleli,
  Nimeona tu nigusie kidogo japo sikupenda sana kujikita kwenye mjadala huu ambao uko wazi wala hauna changamoto nyingi na tete za kiimani. Maelezo yako, ndg Seleli, yana majibu ya maswali yako. Mtu akisoma mchango wako kwa kutulia, halafu akasoma na maswali yako vivyo hivyo, ataelewa haya niyasemayo. Nigusie sehemu moja kidogo sana.
  Kujengeka kwa chuki ndani ya watu dhidi ya viongozi wao au dhidi yako wewe unayeonya, hakukwepeki. Tena usipoangalia, wanaweza kukuponda mawe. Kukuita mnafiki na mtu wa kujiona. Mhukumu wa wengine!! Jambo hili huwezi kulizuia. Kumbuka, popote mtu asemapo ukweli wenyewe tu, atachukiwa tu, haijalishi ni kanisani au wapi. Hata wewe Seleli, akitokea mtu akakwambia udhaifu wako tu wa kimwili(maumbile) au kitabia kwa maneno yasiyofunikwa nguo, lazima utakasirika tu, vinginevyo uwe umefikia uongofu/ukamilifu – kiwango cha Kristo jambo ambalo linahitaji neema ya hali ya juu mno. Kwa kuliepuka hili la kukwaza watu, waonyaji wengi hutumia kaulimbiu ya Kristo kupitia mtume Paulo, “MANENO YENU, YAJAE MUNYU NA UPENDO” – Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu. Wakolosai 4:6.
  Waonyaji wanapaswa kujawa hekima ya hali ya juu mno. Sharti kujenga urafiki kwanza na hao wote (mwalimu na wanafunzi) waliopotoka ili ukaribu wenu huo, uwaruhusu katika kulijadili kirafiki neno la Mungu. Uonyaji upo lakini ufanywe kwa akili tu. Hakuna haja ya kutumia panga, kama kisu tu kinatosha!!
  Yesu mara nyingine(siyo mara zote) alikuwa akitumia lugha kali kwa kweli ktk kushughulika na walimu wazushi. Ikumbukwe kwamba, YEYE alikuwa na uwezo wa kusoma mioyo ya watu. Alivyokuwa akiwasoma mioyoni mwao, na jinsi wanavyofanya, vilikuwa ni vitu viwili tofauti. Ndiyo maana Yesu aliwakemea kwa namna ile. Sisi hatuna uwezo wa kusoma mioyo ya watu. Na kwa vile tunaweza tusijue akiwazo mtu, tunapaswa kutumia lugha nzuri tu kumwelimisha maana siyo sisi tuongoao bali ni kazi ya Mungu mwenyewe. Kazi yetu sisi ni kusema tu, anayeongoza watu kwenye uamuzi, ni Mungu mwenyewe.
  Na kuhusu mambo ya ibilisi kudumu kuwepo, ikumbukwe kwamba, shetani hajachomwa moto bado. Bado anaendelea na kazi yake, akijua muda wake ni mchache sana. Kila siku anabuni mbinu na njia mbali2 za namna ya kuwadaka watu ili akapotee nao jehanamu. Kazi yake hii anaiendesha kwa kutumia mamluki wake. Na itakoma pale atakapochomwa moto na mamluki zake. Ya Mungu haitakoma kwa sababu, yale (ya Mungu) yatendekayo duniani, yataendelea hadi kwenye nchi mpya. Ni ya milele yale.
  Nimesema kwa kifupi tu, sijui kama sijakuchanganya kaka. Karibu tena.

 19. Siyi,

  Kwamba majibu ya maswali yangu yapo ktk mchango wangu!!!!!!!!!!!!!!!!! Interesting indeed, please go ahead and let me see LIVE na uwe huru, pengine Mwl atakuja kujibu au atakua na mengine mengi ya huduma na binafsi na hasije kabisa, ndio maana Mungu amekuweka/leta na wewe, yule na wengine wengiiiii mpo humu Kanisa SG. Karibu kwa icho ulichonacho/kiona

  Press on

 20. Ndugu Seleli,

  Nashukuru sana kwa jinsi ulivyoanza ukileta asante kwa Mwl D.C K. Tunatakiwa kuhimiza anaesaidia wengine akiwa mkweli.

  Lakini hapo chini ukaleta rejea nzito sana ambayo inahusu utafiti. Hii itasaidia wachache kabisa. Nataka sema kwamba si wote watafahamu kinachoendelea. Ndio maana ninaleta mafikiri yangu kwa ufupi kulingana na maneno mawili: Shairi uliyoleta ,na neno chuki.

  Tukisemesha ukweli, kuiingilia kindani maandiko, kuna tafsiri za lugha za Biblia ambazo hazina maneno inayowezaturahisisha licha ya kuwa yana lengo nzuri.

  1. Ukiwa na Amplified Bible utasoma yafwatayo:
  Matthew 7.1 “DO NOT judge {and} criticize {and} condemn others, so that you may not be judged {and} criticized {and} condemned your selves.”
  John 7:24 “Be honnest in your judgment {and} do not decide at a glance (superficially and by appearances); but judge fairly {and} righteously.”

  Unaona kam Mathayo 7.1 anasema usihukumu kwa tafsiri ya DO NOT CONDEMN na DO NOT CRITICIZE. Ina maana usihakikishe kam yule mtu yeye hana “wokovu” au hatakuwa nayo. Inayo maana usiwe kama una jukumu ya kumweka jehanum.Pia hizo critics si halali.
  Lakini Johana 7:24 anasema usihukumu kwa tafsiri DO NOT DECIDE…. Ina maana usichukuwe msimamo haraka. Usiamue haraka. Hii inahusu mtu binafsi wakati anapopanga mambo yake yanayoweza pengine kuwa na tukio juu ya mtu mwengine. Hii shairi inatuomba tuwe makini ktk mafikara yetu, msimamo wetu. Hii inawezahusu hata uamzi wetu kwa namna tunavyo adhibu watoto wetu, au namna tunavyoongea na wake au waume wetu, namna tunavyopangilia tunaowaongoza, namna tunavyo ongeaongea kuhusu wachungaji wetu, nk. Ni uchunguzi wa kila jambo tunalolifanya. This is a judgment of our selves, an evaluation of our acts.

  Ukisoma BBE Bible utaona imeandikwa hivi:
  John 7:24 Let not your decisions be based on what you see, but on righteousness.
  Matthew 7:1 Be not judges of others, and you will not be judged.

  Hivi hii shairi mbili haina lengo moja.

  2. Chuki.
  Ni katazo kuwa na chuki. Neno la Bwana linasema tukasirike lakini tusitende dhambi. Ina maana kasirani yetu isizae chuki.
  “Waefeso 4:26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;”

  Unaona ndugu yangu, ukiwa na chuki kwani kwa maoni yako mchungiji aliviringisha injili, hujawa na haki yoyote. Kwanza huna uhakika kamili kwani umesoma Biblia na umeisikia kwa mtazamo wako labda ukidhani RM ni pamoja nawe. Pengine na wewe ulisoma lakini ukaelewa vibaya. Mpaka pale dhambi bado. Pengine utahuzunishwa, utakasirika kwa mda kidogo, bado dhambi. Lakini ukianzazusha critics, chuki na condemnation ndipo dhambi zinakuzuunguka pande zote.

  Kwa hivi, naona kwa jambo hili Mwl D.C.K iko right kabisa.

  Anyway, nakushukuru kwa hii changamoto.

  Mungu wa Mbinguni akubariki.

 21. Seleli,
  Mbona kama majibu ya maswali yako yana yanapatikana kwenye mchango wako?? Anyway, ngoja nisubiri majibu ya D.C.K mwalimu.

 22. Mwl D.C.K,

  Maswali ni haya…..Karibu kwa ufafanuzi tujengane wote! Mwingine yoyote SG anakaribishwa kusaidiana kujibu pia. Twajifunza wote

  Umekemea kuwashawishi Kondoo Walio chini ya huyu Mtumishi mashaka kutoka uko kwa kua unajenga chuki

  Maswali:

  (a) Unawezaje kusema kweli/kupinga/kutoa hukumu ya haki dhidi ya Mafundisho potofu na Mtumishi wake BILA CHUKI KUIBUKA kati ya Kondoo hao ambao sasa wanakwenda kujua kweli kinyume na ukandamizaji/ulaghai waliofanyiwa miaka? kwakua nia yako ni safi lakini chuki/kumkasirikia/kuhuzunishwa naye kunatokea sasa kama side-effect ya nia yako safi ya kusema kweli na kushambulia uchafuzi huo wa Injili na maisha ya kiroho ya Watu, unauzuia vipi? Kindly be practical and show/teach it/us/me here!

  (b) Wakati Yesu ana-attack ulaghai wa imani, dini na taratibu za Mafarisayo, Masadukayo, Waandishi, Wakuu wa dini na dola tena hadharani, akiwapa pasu-pasu na wengine kuwaabisha na kushusha hadhi zao maana hata aliwaita wanafiki, kizazi cha uzinzi, nyoka, wana wa ibilisi, viongozi vipofu, wameoza ndani ngaa nje wamepambwa na maneno makali mengine, unadhani chuki ilitokea kati ya Waamini na Viongozi wao au haikutokea?

  (c) Kama chuki ilitokea, Je Yesu alijali sana kutengeneza na kua na presha ati Watu wanawachukia Viongozi wao kwa sababu ya Yeye kupasua ukweli hadharani tena akiwawashambulia bila haya wala kumung’unya maneno?

  (d) Je mimi leo nikishambulia baadhi ya Watumishi wapotoshaji, walaghai, wala pesa tu, wakimbilia mijini na majijini tu, wanaojipachika vyeo na majina makubwa ili kuvutia watu si Mungu na Je nikiwashitua Kondoo zao kua wamenaswa uko kubaya, watoke tena haraka, nitakua nafanya kazi ya Mungu barabara kabisa na niko sawa Biblically au niko out Kibiblia?

  (e) Kwa kungalia Matunda tu, baadhi ya Watumishi wa ivyo, hutawatoa makosa wala kuona hatari waliyonayo maana yale yote uliyosema ya kumtambua Mtumishi wa kweli, leo ujanja ume-advance mno, wengi wanatimiza. Kwa uovu ulivyoshamiri kizazi cha leo na hila za ndani na siri za Wanadamu, tufanyeje kuwatambua?

  (f) Kama kisicho cha MUNGU hakiendelei, mbona dini/madhehebu yote yanayopinga Bible na kuokoka duniani, Yesu kua mwana wa Mungu na only Way kwa Baba na hata wale Wanaoiheshimu Bible ila wameongeza na yao mfano kuwainua sana na kuwaabudu Wanadamu na kuwafanya/tangaza Wanadamu watakatifu, why hao/dini izo/dhehebu izo mbovu/ovu/za kidevo/kuzimu/ kibinadamu, za kinyume na Mungu na Yesu mwenyewe, Neno, RM, zimekuwepo karne mpaka leo?

  (g) By the way, aliyesema maneno/comments zile kua kinachotoka kwa Mungu kinasimama na kisichotoka kwa Mungu hakisimami ktk Mdo.5:34-39 ni Gamalieli-mmoja wa members ktk baraza lile la wa Wasomi wa sheria na Watawala wa daily affairs za Wayahudi, JE TULICHUKULIE KAMA NENO LA MUNGU kwa vizazi vyote AU COMMENTS TU ZA KAWAIDA ZA MWANADAMU SUBJECTED TO CHANGES/FAULTS? Meaning, can prove to be true sometimes or wrong the other time?

  (h) Kwamba nikiomba na hawang’olewi Watumishi nisio waamini au nao tilia shaka, na kwamba ndio kwanza wanastawi basi mimi ndio niko wrong na kua nilikua napingana na Mungu! Tunabalansi vipi na ukweli mwingine wa Neno maana twapaswa kujaa na Neno kwa wingi ktk hekima yote- kua Watu wakikataa kua na Mungu wa kweli, Mungu huwaacha, wazifuate akili zao zisizofaa tena imeandikwa Mungu mwenyewe-si pepo, huwaletea nguvu ya upotevu ili waumini uwongo kisha waangamizwe vizuri sana? Je kwa ukweli huo wa Neno, huoni uwezekano kua imani potofu, Watumishi wasioaminika/ wanaotiliwa shaka nyingi, kwamba Bwana amewaacha wafuate nafsi zao na kuziamini ili waangamizwe vema na wafuasi wao kwa kua hawataki kupata hekima, wameaminishwa kiasi kwaba wakikosolewa wao na watumishi wao, wanasema wanaonewa wivu, basi Bwana ameacha ili wote wakae upotevuni na wapoteee vema sana?

  Press on.

 23. My brother Mwl D.C K and Wachangiaji Wote SG,

  Ninaiona nia yako safi ya ndani kuhusu msisitizo wa somo lako hili, umetoa fundisho kwa kuonya ili angalau kusiwepo kabisa au kama zitakuwepo basi izo critics/corrections juu ya huduma/ Mtumishi fulani zifanyike kwa umakini wa rohoni, kwa hilo nimebarikiwa, nice efforts and glory to God for such intent of the msg yako brother.

  Kama sina hila moyoni au chuki binafsi, nimeokoka vema, nalijua Neno, nimejazwa na RM, nina kicho cha dhati cha Mungu wangu, nina mzigo na kazi ya Mungu na moyo wangu umejaa mapigo ya moyo wa Yesu wa kile kilichomfanya aache mbingu aje chini-KUOKOA NA KUTUNZA KONDOO WAKE MPAKA WAFIKE JUU maana alisema Mwenyewe kua ni MAPENZI YA BABA YAKE KUA KILA KONDOO ALIYEMPA, ASIMPOTEZE HATA MMOJA, basi ni wazi mpaka niwe na mashaka au nisiamini huduma ya Mtu fulani, kutakua na walakini kabisa kabisa wa MSINGI. Kwa mantiki iyo, nina observations izi, Unaweza nifuatia polepole napojenga msingi wa hoja zangu tafadhari kisha nitauliza na maswali kadhaa ili upate nafasi ya kufafanua/kufundisha zaidi.

  Kwanza, ni muhimu sana kulijua na kulitumia Neno la Mungu KWA HALALI-2Tim.2:15c na katika HEKIMA YOTE likishajaa kwa wingi ndani yetu-Wakol.3:16a, ni kwa njia ndio tunaweza ona mambo na kuyasema kwa ujasiri na SAHIHI kwa kua tunakua tumezingatia kona nyingi kama si zote za Neno

  Pili, Watu wengi hua tumekariri na kupenda sana kutumia andiko la Msihukumu-Mathayo. 7:1 lakini tunasahanu kabisa pia kuna andiko la toeni hukumu za haki- Yohana.7:24. Kwa iyo, Biblically KAMWE HATUJAKATAZWA KUHUKUMU BALI BALI TUNAHUKUMU KWA HAKI/KWELI! Hata mantiki ya ilo la Mt.7 ukisoma mpaka mstari wa 6…kinachosemwa hapo, ni kutoa KWANZA….kisha PILI utaona sawasawa ili utoe kile kilicho kwa ndugu yako maaana yake ni ruksa ku deal na kosa/kasoro ya mwenzio ikiwa uko ktk misingi sahihi, ni sawa kuhukumu ikiwa tu uko kwa msingi/ukweli/hukumu ya haki.

  Tatu, Tunatoaje hukumu ya haki? Ni kwa kusema KWELI, KUKOSOA BILA WOGA WALA KUMUNG’UNYA MANENO, KUKATAA BILA HAYA, KUPINGA WAZI WAZI MTU NA FUNDISHO/HUDUMA NA IMANI YAKE kinyumen na mambo ya msingi ya Imani ya kweli, IKIBIDI USO KWA USO AU KWA USHAWISHI WA WAZI KUWATOA WATU UPOTEVUNI. NI KWA KUMWAMBIA WAZI KUA UNAKOSEA, WEWE NI NABII/MWALIMU/MTUME WA ULONGO, MWOVU, MNAFIKI nk. Huduma ya Yesu na Paul na jinsi walivyofanya na kupambana na Viongozi wa dini wapotofu ni ushahidi mzito wa Neno.

  Nne, Kwa mantiki iyo, kuonya, kusema kweli, kukemea, kukaripia, mabaya ya Watu na jinsi wafanyavyo huduma zao, NI SAWA KABISA NA KATIKA KIZAZI CHA LEO AMBAPO KUNA UJANJA MWINGI NA WATU WENGI WANAOCHUKULIA MADHABAHU KAMA CHENNEL YA MAISHA, LAZIMA KUHUKUMU KWA HAKI TEA USIKU NA MCHANA ILI YUMKINI WENGINE WAOKOLEWE KAMA KWA MOTO

  Tano, Kizazi cha leo, Huduma na Watumishi kadhaa si kwamba hatuna uhakika na huduma zao, nyingine zina asilimia nyingi za Utauwa lakini misingi nyeti ya imani imevurugwa mfano. Anahubir mtume na nabii mmoja ktk runinga na kusema…’’mwamini Yeye aliyetumwa na Yeye kisha anatafsiri andiko hilo kua huyo Yeye aliyetumwa na Yeye ni huyu Mtume/Nabii!!!!!!!!!! Na ajabu wote wapendwa wanasema aimeeeen kwa raha na wanacheeka! Au siku moja anasema, Mimi niko hapa kama mtumishi wa Mungu kwa kua Bwana aliniona bora kuliko ninyi ili nisimame kuwahudumia! Na ajabu kabisa, wanasema aaiiiiiimeeeeeeeeee na makofi kwaa kwaaaa! Kwa uchungu mkubwa wa uzazi na huruma ya kiroho na kiutumishi kama Paul, LAZIMA kuwaokoa watu hawa kwa kuhukumu kwa halali, kutenga kati ya kweli na wa kweli na waongo. Paul alikwenda mbali na kusema, ikiwa mtu ataleta gospel nyingine tena akasema hata malaika mbinguni akijichanganya naye akahubiri madude, alaaaniwe! Alitangaza LAANA kwa wa JUU na CHINI hapa ikiwa wataleta mchezo ya kuwalaghai watu innocent wa Mungu.

  Sita, hatuwezi kua na hekima, huruma, upole sana uliopitiliza kwa Watu ambao kwao, hata wanadamu wakiangamizwa kwa kuwalisha madude unbiblical, watu wanakandamizwa na kutishiwa kua watakufa wakiwapinga, wakiwanyoshea vidole waovu hao, wanawafanya members kua wanafunzi wao watumishi badala ya Yesu, kama hawana huruma kwa Wanadamu hao, kamwe hawastahili kutendewa kwa hekima na kuvumiliwa ndio maana unaweza elewa kwa nini Paul alikua mbogo hata kusema walaaaniwe kabisa! na hata watoto wake walipopotoka( Wagalatia.3:1-3, aliwafyatukia kuwaambia wajinga/wamelogwa na nani? Hakuna mchezo na simile inapokuja swala la kupoteza Watu kwa mambo ya msingi ya rohoni, upole wetu uzidi kiasi.

  Saba, Ifahamike kua Mungu anatumia watu kujitetea au kutetea watu wake, hatuwezi kaa kutengemea kua malaika atakuja ingawa anaweza tumwa pia kuchinja Watumishi Wataabishaji na watu na Taifa na waaibishaji madhabahu na imani ya wokovu kuonekana wote sisi wajanja-jana za mjini tu nakutafuta pesa. Ni sisi wenyewe kutoa woga wala kusita na kusema kweli moja kwa moja kama Yesu au Paul tena kuwaambia uso kwa uso au kwa njia nyingine ili mradi ujumbe ufike wa kumwambia kua, anakosea, aache mara moja, akitubu na kucha tumempata ndugu yetu, akikaidi kwa kua yeye yuko madhabahuni na ana watu wengi, heshimika, basi lazima tutamwandama kumwambia ache na kwa MAKUSUDI KABISA YA MBINGUNI, kuwaambia na komodo wake walionaswa kwa kujua au la kua uko ni kwa wevi na wanyang’anyi , watoke haraka na kwenda ktk zizi la kweli na malisho ya uhakika

  Press on, ( Maswali yanafuata)

 24. Mwl D.C.K, asante kwa maneno ya hekima, lakini unapomwona mtu anatumbukia shimoni na kwa uhakika na uthibitisho wa kimaandiko usimwambie akifa kabla huduma hiyo haijafa atakwenda motoni na wewe ulijua kuwa kunaudanganyifu ndani ya huduma hiyo na hukuchukua hatua ya kwamwambia ndugu yako. Mbele za Bwana utakuwa umefanya vyema?

 25. Mwl D.C.K.
  Umeongea mambo ya maana sana rafiki. Binafsi nimeyapenda sana. Ni kweli kabisa kuna mapandikizi ya yule adui ndani ya kanisa la Mungu. Kwa matunda yao unawatambua kabisa. Pale Biblia iliposema usifanye hivi, wao wanakuja na tafsiri zao potofu za kupindisha ukweli wa Biblia. Na wewe unauona kabisa kuwa ukweli umepindishwa hapo. Utafanyeje? Utamwacha tu kumshughulikia kisa ati anajiita ni mtumishi wa Mungu? Hasha, haitawezekana!!!
  Kwa uelewa wangu, watu kama hao, tunapaswa kuwapenda sana sana lakini tukichukia na kuumia sana kwa hayo wanayoyatenda(yaliyo kinyume na neno la Mungu). “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki” -matt 5:43-45. Zaidi ya hapo, ni sharti tuchukue hatua ya kuwasaidia kwa upendo sana maana hata wao, Biblia iko kwa ajili yao; kuwajenga na kuwaimarisha kiroho ili waje wakutane na Mungu. Pamoja na mamlaka waliyo nayo, bado na wao wanaukulia wokovu. Ni wanadamu tu wenye madhaifu kama walivyo wengine. Mungu hutenda kupitia watumishi wake pia ambao ni wewe, mimi na huyu anayesoma mchango huu. Ukiwaacha eti mpaka Mungu mwenyewe awashughulikie, utakuja uhesabiwe dhambi na wewe kwa maana uliona hukusema, umekuwa mbwa asiyebweka wa nyumba wa Israel. Na ukiwa mbwa asiyebweka, utakuwa mdhambi sawa na wao. “Na mtu awaye yote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe” Walawi 5:1
  “Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako”. Ezekiel 3:18-19

  Kama tunawapenda kweli hao watu, sharti tutawaonesha upendo kwa kuwaonya na kuwaelekeza ni wapi wanakosea na wanapaswa waenende kwa namna gani vile inavyompendeza Mungu. Maana kama mtu humpendi, huwezi kumkanya kwa baya alitendalo. Lakini kama wampenda kweli, ni lazima utamsaidia ili asipotee yeye mwenyewe na asipoteze na wengine pia.

  NB: Huwezi kuwaonya ama kuwakanya wanaokosea bila ya kuwa mwanafunzi mzuri wa Biblia chini ya uongozi wa RM. Ni sharti ujifunze Biblia kwa bidii, uombe na kushuhudia sana.

  Bwana akubariki D.C.K na wengine wote.

 26. Mtumishi, Mwl. D.C.K, kweli umenena. Mungu akubariiki. Miaka ya early 2000, haswa 2004 niliwahii kuwa na domokaya ama domo chonga sana juu ya watumishi, lkn, km unampeenda Kristo, utamsikiliza na kumpa nafasi kubwa sana R/mtakatifu, atakusaidia kwa kukuonya sana juu ya mambo hayo. Nikiwa kwenye kutokujifanya siieelewi sauti hiyo, hk nikizidi kuwasulubu kwa kinywa changu, Bwn alinikaripia nikiwa njiani ninakwenda kukaa na mtumishi mmoja kwa ajii ya kimuhemuhe changu cha umbeya wkt huo kikiniendesha nataka nimssimulie kila mtu ajaye mbele yangu, nddiposa nilipokaripiwa na Bwn mwenyewe juu ya tabia hiyo. Ww unayenisona hp, ziingatia hayo, mm niliponywa toka hapo kinywa changu. Na Mungu alianza kunifundisha upya juu nanamna watu wooote hao, mfano, dsm hii, jinsi walivyo watumishi wk, isipokuwa, weengi wao, wamejawa na roho ya kiburi, na akanambia, chukua nafasi yko, waombee, na si kuwafanyia crusades za kuwachafua. Mubarikiwe. OGUDA J.E.

 27. Bwana Yesu asifiwe,

  Nashukuru Mungu kwa maelezo ya Mwl D.C.K. Ni mazuri kabisa.

 28. lakini pia wapendwa msome vizuri habari ya kora na wenzake katika Hesabu 16. Utaona ilivyo vibaya kushindana na mtumishi wa Mungu. Muulize Mungu,muombee na zidi kumpenda.Kwani biblia inasema wapendeni wanaowaudhi

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s