Kanisa la Gilgal Mwanza lavamiwa na mtu mmoja kuuawa!!

gilgal2

Taarifa kutoka Mwanza ni ya mtu mmoja kuuawa na wengine watatu wamejeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo ndani ya kanisa la Gilgal Christian Worship Centre Pasiansi, Ilemela Mwanza.

Tukio limetokea saa saba usiku ambapo Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi pia na mwenyekiti wa vijana wa kanisa aliuwawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine ambapo Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu walijeruhiwa na hali zao sio nzuri lakini wako Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kutokana na mapanga waliyokatwa.

Askofu wa kanisa Eliabu Sentoz alisema kama Jeshi la Polisi likiamua kukomesha hivi vitendo inawezekana kuvimaliza kabisa ambapo kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ernest Mangu amethibitisha tukio limetokea lakini mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa kitu ambacho kinaongeza maswali zaidi kuhusu tukio lenyewe.

–Millard Ayo

3 thoughts on “Kanisa la Gilgal Mwanza lavamiwa na mtu mmoja kuuawa!!

 1. Hao majambazi wako njiani kuokoka.

  Maana MUNGU aliwaona mapema pia Aliwaacha Makusudi.

  Imeandikwa mwenye haki wangu ataishi kwa imani YAKE.

  Poleni ndugu zangu wokovu ni Vita isiyo na Mwisho kabisa.

 2. mpendwa ni ,mapema sana kusema polisi wamekaa kimya bila kutoa tamko pia wanaoutaratibu wao wa kufanya kazi naamini wataoa tamko kutokana na tukio hilo poleni katika yote yaliyowapata
  pastor thobiasi TAG mponda

 3. Mungu atulinde na maadui zetu wanaotaka kuharibu kazi yake kwa jina la Yesu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s