Malaika Wamuokoa John Komanya kutoka kwenye Ajali!!

john

Mwimbaji anayetamba na wimbo wa “Zawadi gani nitamtolea BWANA” ambaye pia ni mtume akichunga kanisa jijini Dar es Salaam John Komanya amepata ajali mbaya juzi mchana maeneo karibu na daraja la Mto Wami akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kukutana na viongozi wanaohudumu na mwalimu Christopher Mwakasege, kwa ajili ya mkutano wa injili ambao utakuwa na lengo la kuombea taifa kwa siku nne mwezi Disemba.

Akizungumza na GK mtume Komanya amesema lengo lilikuwa ni kupeleka barua kwa viongozi hao ili wamfikishie mwalimu Mwakasege kwaajili ya mkutano huo. Amesema akiwa njiani katikati ya Msata na Wami na wakati huo hakuwa amefunga mkanda wa gari, ndipo akasikia sauti ya Roho Mtakatifu ikimwambia kwa upole afunge mkanda lakini akawa anapuuzia na kuanza kujiuliza kwanini, sauti ikarudia tena kwa upole ikimwambia afunge mkanda akiwa bado anajiuliza ndipo anasema akasikia sauti ya Mungu ikizungumza kwa haraka na ukali “John funga mkanda” ndipo akafunga mkanda.

Mtume Komanya amesema akiwa anateremka kuelekea wami akiwa katika mwendo wa 180 wakati akipita katika kona kulikuwa na malori matatu mbele yake kukawa na lori lingine likifuatiwa na mabasi matatu yakipandisha kutoka Arusha kuja Dar, kwa wakati huo aliona malaika saba ambapo walishuka mithili ya makomandoo washukavyo kutoka kwenye kamba ya helikopta, mmoja akiwa amekaa kwenye boneti mbele, mwingine kulia, kushoto na mwingine nyuma yake ambaye alimwambia Komanya afuate maelekezo yake, anasema akiwa anamwangalia malaika aliyekaa karibu naye katika kiti cha dereva aliambiwa afuate maelekezo anayopewa na malaika wa nyuma yake.

Alipokuwa akiangalia mbele akaona gari linayapita mengine kwa spidi hali iliyomfanya Komanya kutaka kuingia katikati ya magari mengine lakini malaika akamwambia afuate maelekezo yake na kuambiwa aachie uskani jambo ambalo alilipinga kwakuwa aliona kifo mbele yake na kutaka kuingia katikati ili kukwepa, lakini malaika akamwambia ukiingia katikati utakufa, wewe achia usukani kama ninavyokwambia kwakuwa wametumwa kumlinda, akawa bado anatafakari kutokana na kuliona korongo kubwa upande wake huku malaika wakimwambia asiguse kitu chochote ikiwemo kutokanyaga breki lakini bila kusikia akakanyaga na kusababisha gari kuyumba sana, malaika akamwambia tena aachie breki na kuweka mikono yake kifuani. Anasema alipoweka mikono kifuani aliona wakiligonga lori huku malaika akiwa ameshika usukani na kuonyonga sana huku yeye akisema alijikuta akiwekwa kwenye kitu kama chupa ya maji, na yeye kwa wakati huo kuona kama vile yupo ndani ya glasi ya maji, ila anaona kinachoendelea.

Kisha baada ya hapo, upande wake wa usukani ndio uliogongwa, mara baada ya malaika kuchezesha usukani kidogo ili kuepusha madhara zaidi, na kisha ile semi-trailler ikamtupia kwenye korongo na kubinuka mara tatu hewani kabla ya kutua chini kwa mara ya nne, ambapo gari ilikuwa juu chini, yaani matairi yakiwa yanatazama juu.

Baada ya hapo kilichofuata ni kuendelea kusikiliza malaika wasemacho, ambapo hapo alisikia sauti ikisema fungua mkanda utoke, na kwa wakati huo kulikuwa na moshi ullioanza kutoka kwenye gari – na hapo akapewa dakika 12 kuchukua baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwenye gari. Maajabu ya Mungu, hakuna kitu chochote kilichogusa mwili wake, na wala hakuna damu iliyovuja kutokana na gari hilo kupindukia kwenye korongo.

Hakika utukufu ulimrudia Mungu kwa wakati huo kwani baadhi ya mashuhuda walikiri hapohapo ya kwamba hakuna mtu anayeweza kusalimika kwenye ajali hiyo, bali ni lazima tu mkono wa Mungu umehusika hapo kuokoa.

Baadhi ya mashuhuda ambao walikuwapo kwenye mabasi ya mkoa (hadi mkoa) walimtambua mtumishi wa Mungu ya kwamba ni John Komanya na hatumaye kumshukuru Mungu hapohapo, ambapo baadae Polisi walifika kwa ajili ya kazi yao – lakini hilo halikumzuia Mchungaji Komanya kupiga magoti na kumshukuru Mungu licha ya umati wa watu – na tukio hilo liliambatana na yeye kuisikia sauti ya Mungu ikimwambia “Nimekupa kazi ya kutengeneza kanisa langu,… usiogope nitakulinda, ila kuwa mwaminifu na nitakuweka kwenye uaminifu

Sauti hiyo ilitoka kwa kiumbe ambacho kilikuwa na muonekano wa malaika, Pastor Komanya anaieleza GK na kusema kuwa sauti yake ilikuwa ya tofauti, na mavazi yake yalikuwa ni meupe na kwamba alielezwa dhahiri kuwa hiyo semi trailer ilikuwa imetumwa kummaliza, lakini ndio maana malaika walitumwa kumlinda.

“Zawadi Gani” kama ambavyo alikuwa akiitwa akiwa hospitali ya Muhimbili, alifanyiwa vipimo na kuonekana ya kwamba hana shida yoyote. Na hili linadhihirika hata pale alipotoka kwenye gari lililopiinduka, kwa kuwa alitoa vifaa vyake na kuanza pia kupiga picha, picha ambazo kama mtu akiziona zote, hakika hawezi kuamini kama kuna kusalimika hapo.

Mwisho wa yote Mchungaji Komanya anakiri kuwa amepona kwa rehema ya Mungu, na baada ya hapo amemuahidi kumtumikia kwa kazi aliyompa licha ya kwamba ni ngumu na ina vikwazo vingi. Jumapili hii, Mchungaji Komanya ataimba wimbo mpya kumshukuru Mungu kutokana na kumuepusha na kifo. Kwa wasafiri wote, hapa kuna funzo la kujikabidhi mikononi mwa BWANA kila mara safari inapotokea, katu tusienende kwa mazoea.

–Gospel Kitaa
Advertisements

20 thoughts on “Malaika Wamuokoa John Komanya kutoka kwenye Ajali!!

 1. NImeipenda michango yenu wapendwa na maswali na observation zote , mbarikiwe.

  Mungu hakika ni mwingi wa rehema, kama kweli alikuwa anakwenda 180km’h na bado anabishana na Roho Mtakatifu kama alivyosema mwenyewe hilo ni onyo.

  Kama walivyosema wengine, not every supernatural experience is to be shared, sharing some things simply “cheapen” the experience, labda kama ni kwa ajili ya kuwajenga wengine. Besides, experiences are very subjective, kwanini tusikae kwenye Neno tu jamani? Who are we trying to impress? Beloved, it’s time to check our motives….

  Blessings,

  Patrick

 2. Ninachoamini ni kwamba ukifanya kazi ya Bwana kwa uaminifu na kwa moyo wako wote yeye atakulinda kwa kila jambo. Huu ni mfano tosha wa dhahiri kwa tuliyosoma na kuelewa. sifa na shukrani zimrudie Bwana wa mbinguni.

 3. Mmenifurahisha wachangiaji…..cha msingi……..tunaamini Bwana amemuokoa ndugu Komanya……..kazi ni kwake………atajenga nini katika msingi wa Kristo baada ya tukio hili? Hasa baada ya kupona kifo hicho? Bwana anataka ajengeni nini katika Wito aliomwitia…? Dhahabu……Fedha….au Mawe ya thamani……? La kukumbuka miti, majani….nyasi…zitapimwa kwa moto……! Its opportunity for him to reevaluate his ministry…..Mungu ana kitu chema kwake….

 4. Atukuzwe Mungu ambaye anatufudisha kupitia huu Ushuhuda wa Mtumishi Komanya, kwamba Mungu tukimtii atatulinda na mabaya yote.

 5. John Paul (somo wa John K. aliyesave), nimependa you’re tip picking and placing it uku ikitoa mianga miwili..mtu atafakari mwenyewe na kujipa jibu….what a wisdom….safi bro

  Lily….Ooo Yesu, bless u for getting it right…kuna mbwembwe kweli kwenye shuhuda za kweli sometimes

  Kaka… Nadhani nilikosa ujasiri, nilipaswa niseme hiki ulichosema moja kwa moja kua.. ‘’unaweza kuwa tunapamba sana mambo yetu ili tuonekane tupo karibu zaidi na Mungu kuliko wengine’’…….Sawa kabisa ndio nilimaanisha ktk lugha niliyotumia ya shuhuda zinatoka kwa NIA mbalimbali’’.

  Pia SERIOUSLY nimeipenda hii balance sana, sana kabisa…..’’ si lazima kila experience ya kiroho unayokutana nayo ukaishirikisha kwa wengine’’…..Aisee NI KWELI! kwani lazima kiiiiiiila naniii useme? Ukiacha je na HASA izo za kuongezea kachumbali kwani tutakosa nini critically ktk maisha yetu Kiroho na Kitumishi?

  Press on.

 6. Namshangaa sana Mungu kwa utukufu wake wa ajabu kwa kumuepusha huyu mpendwa katika ajali mbaya kama hiyo.Bwana Yesu apewe sifa.

 7. Nimestushwa sana na huu ushuhuda. Na kwa kweli ninaweza kusema neno moja tu kwamba Mungu atusaidie sana kuwa waKWELI! Tunaweza kuwa tunapamba sana mambo yetu ili tuonekane tupo karibu zaidi na Mungu kuliko wengine na mwishowe tukaishia kutenda dhambi ya uongo. Na si lazima kila experience ya kiroho unayokutana nayo ukaishirikisha kwa wengine.

  Mungu atusaidie!

 8. Mimi tu na hiyo 180 Km/Hr halafu kuelekea Wami? Lakini kwa Yooote Jina la Bwana Libarikiwe!

 9. Ni kweli twaweza dadisi na kuwa na maswali juu ya ushuhuda mzima wa Komanya ila naona anayeweza kujibu ni yeye mwenyewe. Ukweli hata mimi nilisoma ila nina maswali ambayo sikuyauliza maana aliyeandika most likely nae amesikia tu. Pia Seleli ni kweli kuna uchanganyaji siku hizi ktk shuhuda za wapendwa hivyo tusome/tusikie ila tuwe wadadisi for sure.

 10. Sungura,

  Your comments basically Noted, nevertheless, Kwa HALI YA HEWA YA LEO KIROHO/KIKANISA-kizazi chetu kinachoinukia ktk huduma, yamepita na yanajitokeza mengi kwa NIA mbalimbali

  Bila kumung’unyanya maneno wala kuoneana haya, UKO UMUHIMU MKUBWA SANA wa kujaribu kusaidiana kuhakikisha UKWELI HALISI WA KILE AMEFANYA MUNGU-(ambao hata huo unatosha sana kumpa Mungu utukufu ), UNA DOMINATE kisha kuzuia/ANGALIA KWA JICHO LA MOJA KWA MOJA….‘’UKWELI’’ nyongeza kuusaidia UKWELI original.

  Yes nimekupata tunaweza ignore na kua watajuana na Mungu lakini kufanya ivyo, TUTAPOKEA MENGI YA KWELI NA HOLELA…Si unakumbuka Makanisani kulizuka shuhuda fulani kumbe hasa kile alichofanya Bwana au Mtu alichotendewa, sicho au ndicho ila kimeongezewa swaga kibao. Ya nini yote hayo! Honestly Maswali hayo niliyouliza yamesumbua kile nilichopata toka ushuhuda/Ukweli kua KWELI Brother amesave Kifo. Nimetukuza na kumpa Mungu credit toka comment yangu ya kwanza yet vitu vingine ivyo ndio badala ya mimi kubaki na kile hasa cha MUNGU, hayo yamekidisturb, unaona problem iyo?

  Anyway, thanks Mnamala and Nkoi Sungura

  Press on

 11. Napenda watu wadadisi, kwa sababu napenda kuchangamotishana.

  Seleli alichofanya hapa ni kudadisi neno kwa neno katika yale yaliyoandikwa, ni kitu kizuri.

  Katika huo udadisi wake kwa upande wangu naona cha msingi alichokiibua ni hayo maneno ya kujikabidhi mikononi mwa Mungu kila mara safari inapotokea, na mambo ya ‘matitle'(mtume, nabii, n.k). Hizo ni swaga tu za mazoea za wapendwa,ambavyo wengi huvisema bila hata wazo la pili la kufikiria walichokiongea kina maana gani.

  Mimi niko very sensitive na vitu ambavyo naweza kuviita ni ‘christian jargons and religious myths’. Viko vingi sana katika maongezi na maandishi ya kila siku ya wapendwa.

  Sasa rafiki yangu Seleli kuna hayo maswali mengine uliyoyaibua yenye kututaka tuuhoji huu ushuhuda kama ni wa kweli kwa kiasi ambacho umesemwa, mimi naona kwenda huko ni kutaka kufanya kazi isiyotuhusu.

  Hiyo si kazi yetu sisi kujua. Kama Komanya na wengine waliohusika kutufikishia huu ushuhuda waliutunga, au wameongea baadhi ya vitu ambavyo havikufanyika kama walivyotuambia, basi watajuana wao na Mungu.

  Lakini ninachojua ni kwamba hayo yote waliyotuambia kuwa yalifanyika ni kweli Mungu anaweza kuyafanya na kuzidi mbali saaaana, na mazingira yanaonyesha kuwa yangeweza kufanyika.
  Na lengo la kutuambia ni ili tumpe Mungu utukufu.

  E.g, Malaika kumpa dakika 12; kama malaika hakutoa sababu ya kufanya hivyo sihitaji hata kujisumbua kujua ni kwa nini. Maana si lazima kupewa dakika fulani kwa sababu ya gari kulipuka tu, si lazima gari likipinduka lilipuke,kuna mengi tu ya kutokea hata hatuyajui.

  Seleli, mimi naona tumpe tu Mungu utukufu, na kujifunza ya kujifunza kutokana na huu ushuhuda. Kama wameuchakachua basi wao ndo watajiju na Mungu wao.

  Thank u sir!

 12. Anitha,

  H a ha ha ha ha au nasema ulongo mie?

  We niambie tu Malaika wengine 3 wako wapi au wakati gari inakula sambasoti mara 3 hewani kabla ya kutua, nani aliona iyo na why Malaika kutoa 12dk tu? jamani!!!!!!! We need to balance our feelings and mapenzi yetu na kile halisi tunasema/report.

  Press on

 13. Hahahaha Seleli umenichekesha sana. Katika yote ahimidiwe Mungu wetu kwa kumuweka hai Mtumishi wake Komanya. Ingekua hadithi nyingine

 14. Kwamba this friend is alive toka ajali ya kutisha kama hii kwa maelezo na picha izo, inatosha kusema, Jina la Bwana libarikiwe maana tunaongelea Mwenyekurehemiwa badala ya Marehemu John Komanya. Jesus I love again and more for this and my brother, Amen.

  By the ways, niliposoma taarifa hii, ndani yangu, Nilikua a mixed feelings, ya furaha kwa kua Ndugu kapona na ya maswali.Napenda ku-share haya maana nilishajifunza tokana na makosa namna tunavyoshare vitu hata kama nia zetu ni NJEMA mno mbele za Baba, tukichanganya na aims zetu tunazotaka kuachive, tuna-dilute kile original cha Mungu tunachotakiwa kudaka/kupata/kushare/peleka mwa mioyo ya Watu.

  I have some observations out of this info na kidogo niko inquisitive na haya namely:

  Akasikia sauti ya Roho Mtakatifu ikimwambia kwa upole afunge mkanda lakini akawa anapuuzia na kuanza kujiuliza kwanini, akasikia sauti ya Mungu ikizungumza kwa haraka na ukali “John funga mkanda” ndipo akafunga mkanda.

  Observation: Kwanini RM kabisa ASEME kitu(si hisia za kiroho-roho au kuhisi-hisi but anasema RM alisema na unajua ni RM kisha upuuze!!!!!!!!! HAININGII AKILINI NA ROHONI. Nadhani Mtu wa Mungu ukisha SIKIA RM amesema, HII NI VERY SERIOUS THING TO BE HAPPY FOR( Ni raha na ishara nzuri sana ya uhusiano wetu naye Mungu kuongea nasi) AND TAKE IT GRAVELY VERY SERIOUS!

  Kwamba anaitwa ‘Mtume’ Komanya!
  Observation: Kulingana na hali ya hewa ya kiroho iliyokoa leo, kwa nini tusimuite simply tu na yenye kicho tena isiyoleta maswali mengi leo, majina kama Kaka Komanya, Mpendwa, Mwimbaji au basi hata Pastor Komanya? Why do we keep things humble and simple yet anointed?

  Aliona malaika SABA, 1- akiwa amekaa kwenye boneti mbele, 2- kulia, 3-kushoto, 4-nyuma yake ambaye alimwambia Komanya afuate maelekezo yake, akiwa anamwangalia malaika aliyekaa karibu naye katika kiti cha dereva-(huyu atakua ni aidha yule yule kati ya wa No. 3 or 4) aliambiwa afuate maelekezo anayopewa na malaika wa nyuma yake- alioyeongea ni wale wale aidha wa no.3 or 4.
  Observation: Malaika wengine 3 walikua wamekaa wapi, maana so far tuna 4 tu yet aliowaona ni 7?

  Komanya akaona gari linayapita mengine kwa spidi hali iliyomfanya Komanya kutaka kuingia katikati ya magari mengine
  Observation: Kuona Gari inapita mengine kwa spidi, inahusiano gani na kuingiza gari katikati ya mengine? Na kati kati ni wapi au barabara ni three ways? maana kama alihama kwake, alikua upande wa pili wa magari mengine na hakuna katikati.

  Malaika akamwambia aachie uskani!
  Observation: Inawezekana kweli Malaika kumwambia aachie usukani ILA SIAMINI—labda kama ingesemwa..Malaika akamwambia shika usukani kwa imara, usiteteleke wala kuogopa! Lakini katika hali ya kawaida, uko spidi kifo live unakiona, kisha unaambiwa achia usukani!!!!!!!!!!!!!!

  Malaika wakimwambia asiguse kitu chochote ikiwemo kutokanyaga breki
  Observations:
  Kwanza Alisema-malaika mmoja- aachie usukukani, kisha WAKAsema-zaidi ya mmoja-wanaongea kua… asiguse chochote na hakuna kukanyaga break, na yote hayo yanafanyika gari iko spidi, mbele gari, pembeeni korongo, SIAMINI hii kitu ya Malaika kufanya mambo ya kurisk kiasi icho! Unless Malaika angeshika naye pamoja au akashika kwanza ndo kumwambia aachie yake! Pia Malaika wawili kuongea at per-si kuimba, nayo ni ajabu isiyo ya kawaida!

  Gari Kubinuka mara tatu hewani kabla ya kutua chini
  Observation: Nani alikuwepo/kasema/aliona kua ilichumpa hewani mara 3?

  Alipewa dakika 12 kuchukua baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwenye gari.
  Observation: Kwa nini apewe dk 12 tu na si 6 au 2, 30? Kulikua na uharaka gani-gari kulipuka? Je lililipuka baada ya muda huo? If no, why hurry or time limit? Any Rationale?

  Komanya kupiga magoti na kumshukuru Mungu na akaisikia sauti ya Mungu ikimwambia “Nimekupa kazi ya kutengeneza kanisa langu,… usiogope nitakulinda, ila kuwa mwaminifu na nitakuweka kwenye uaminifu“
  Observation: Tunaweza amini vipi hicho KITU/MWITO/ASSIGNMENT KUBWA SANA MUNGU ALISEMA KWELI ? Simply tu kwa kua Mpendwa kasema yeye au tuangalie/tusubiri vigezo vingine kama muda, maisha ya usafi, uchaji, uaminifu, ushuhuda, mausiano na Watu na Watumishi wengine, taarifa/ushuuda za Mtu kwa wale tunao na tuliowahi wahudumia nk?

  Mchungaji Komanya ataimba wimbo mpya kumshukuru Mungu kutokana na kumuepusha na kifo.
  Observation: Jina/cheo cha huduma nemely ‘Mchungaji’ ni salama sana leo hasa kwa kijana kama Komanya kuliko kutumia ‘Mtume! Inaharibu mapema wasikilizaji hasa wasiookoka siku izi majina/ma-vyeo hayo, yamechukuliwa kama ujanja wa mjini tu wa kutisha/tiisha Wanadamu ili watoe noti zao au channel ya kusaka pesa. Hamna haja ya kujiingiza ktk question marks unnecessarily, we better keep things simple yet sweet and strictly for His own glory and not our own troublesome ego

  Kwa wasafiri wote, hapa kuna funzo la kujikabidhi mikononi mwa BWANA kila mara safari inapotokea, katu tusienende kwa mazoea.

  Observation: Ivi tulishawahi jiuliza kua ni wapagani wangapi, wanaruka na madenge, wana safari kila leo na mabasi, treni, magari binafsi, wakiendesha magari binafsi kwenda kwa maovu na bado hawana presha wala hata idea kua kunaweza tokea ajali, wana relax na wengine tunawasikia wakisemaga kabisa kua Mungu yupo bwanaa. Kama Mungu anaweza jali watu wa ina iyo, vipi WANA WA PENZI LA MWANA WAKE sisi?

  Nadhani wakati mwingine, we need to relax in the Lord, maombi mengine si maombi bali ni madhihirisho ya Hofu tulizokubali zituhubirie akili na nafsi.

  Kufanya maombi kila siku, kwa kila kitu na kila mara, inaweza kua jambo jema Kiroho lakini wakati mwingine tusipojiangalia kule ndani mwetu ni ni hasa icho kinatupelekea kuombea eg safari, usiku tunapolala inaweza kua ni hofu tu na Biblia inasema, HATUKUPEWA ROHO YA HOFU, na ina Neno USIOGOPE kutosha kila siku Jan-Dec

  Kwakua yu hai ndugu huyu, hakuna shaka upo ushuhuda wa alivyookolewa ila namna ulivyowekwa, unazua baadhi ya maswali badala ya kuleta kile hasa Mungu alichotaka tupate kwa muujiza huu. Sijui imetokea ivi kwa sababu ya Mwandishi mwenyewe na ufundi wake au masimulizi as per Komanya, Bwana anajua KWELI NA NIA YA NDANI.

  Press on.

 15. Kama alivyosema Lwembe,
  Lazima kulikuwa na kitu cha adui kisicho cha kawaida hapo. Simply haiwezekani ukawa katika hali ya kawaida ukaendesha hiyo speed kwa barabara zetu hizi, bila kufunga mkanda, tena eneo la mto wami, halafu kwa aina hiyo ya gari. Hiyo lazima tu ilikuwa mission kabambe ya adui, ndio maana malaika ilibidi watie team!

  Nafikiri hila aliyotumia shetani ni kumfanya Komanya adhani kuwa bado yuko USA kwenye high ways, ambako angalao hiyo speed unaweza thubutu, japo si bila kufunga mkanda jamani.

  Kweli Mungu kamwokoa aise!

 16. Ni vema wapendwa tukawa waangalifu zaidi. Ni kweli Mungu kamlinda lakini ajifunze na sisi wote tujifunze kufuata sheria za barabarani. Tupunguze ajali nchini kwetu Tanzania. Imagine 180 pale wami, that’s wrongly serious!!!! Ni neema tu he would have gone!!!

 17. Naungana na wanaomshukuru Mungu kwa kuokoa maisha kwa mtumishi huyu wa Bwana….labda ni ni somo kwake na kwa wengine jinsi ya kumsikiliza Roho Mtakatifu….Lakini pia watu wa Mungu tuwe waangalifu, unaendesha gari 180 Km kwa saa, mahali penyewe Wami…. halafu Hujafunga Mkanda….na umevuka kabisa kiwango cha Speed iliyoweka na sharia …..Je huku sio kumruhusu Shetani….? Au Kukaribisha majaribu…? Nadhani ni somo kwa mtumishi huyu….unapojiweka mikononi mwa Bwana kumbuka pia kufanya unayotakiwa kufanya….Kwangu mimi huu sio muujiza tu kwa mtumishi huyu, bali ni Onyo kwake na kwangu na kwa sisi sote…!!! Siwezi kuendesha gari usiku pasipo kuwasha taa za barabarani kwa makusudi na kupata ajali halafu kusema ni shetani…….!!!!
  Mtu wa Mungu umetuachia somo…..Bwana na apewe sifa kwa hili….! Mbarikiwe

 18. 180 kph, kuelekea daraja la wami yaani ukiliteremkia daraja, mimi nadhani aliyetumwa kummaliza mtume alikuwa naye ndani ya gari, ni Mungu tu aliingilia kati kuyaokoa maisha ya mtume, ashukuriwe Bwana aliye mwingi wa Rehema!!!

 19. Amen kujikabidhi mkononi mwa Bwana ni muhimu, Mungu anatuepusha na Mengi tusiach ekumshukuru sikuzote, Mungu atusaidie pia kuzifuata sheria za barabarani kwa wanaoendesha magari.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s