Nini Tofauti?

utatu

Shaloom

Ninaomba kuelimishwa tofauti iliyopo kati ya Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho mtakatifu, then nitaulilza maswali mengine baada ya kupata majibu haya.

Asanteni

Janeth mari

Advertisements

30 thoughts on “Nini Tofauti?

 1. Dada Janeth,

  Katika kukujibu swali lako, baada ya yale maelezo yangu ya awali, yaliyofuatiwa na fafanuzi nzuri ya mjoli Haule, basi ninaona ni vema nikalimazia jibu langu hilo kwa kadiri ninavyofahamu.

  Kimsingi, jambo uliloliuliza si la ki Maandiko, bali ni la ki Teologia. Ndipo katika mtazamo wa kiteologia, unapotaka kuitazama tofauti iliyopo kati ya Miungu hiyo mitatu ambayo ni Mungu mmoja; inakubidi kwanza uamini kwamba suala zima la hiyo Miungu mitatu kuwa Mungu mmoja, kwamba hilo ni “FUMBO KUU la UTATU” au Fumbo la Imani!

  Nayo maelezo yanayoambatana na “Fumbo” hilo yako hivi:
  Mungu ni mmoja bali ana nafsi tatu dhahiri zinazojitegemea na zenye mamlaka sawa. 1. Nafsi ya Baba, 2. Nafsi ya Mwana na 3. Nafsi ya Roho Mtakatifu.
Basi kuhusu hizi Nafsi ni kwamba, Baba ni Mungu; Mwana ni Mungu, na Roho Mtakatifu ni Mungu; na hawa Watatu si jinsi tatu za Nafsi Moja (yaani mtu mmoja) bali ni Nafsi Tatu dhahiri (yaani watu watatu) zikiwapo hapo katika ushirikiano wa dhati baina yao. Yaani hawa Watatu wakisimama kwa kweli katika uhusiano wa kibinafsi mmoja kwa mwingine!

  Ndipo jambo hilo likiwa ni “Fumbo”, kimamlaka tunaweza kusema hawana tofauti, maana wote wana mamlaka sawa. Hakuna aliye juu ya mwenziwe. Nao ushirikiano wa mamlaka hizo tatu huwafanya kuwa Mungu mmoja!!!

  Lakini, kwa vile jambo hili ni la kiteologia, licha ya kwamba makundi mengi huonekana kukubaliana katika mpangilio huo, bado ziko tofauti ambazo huivuruga setup hii, nadhani huenda ndicho kilichokufanya uliulize swali hili! Kwamba Miungu hao watatu wana mamlaka sawa, juu ya hilo, kati ya makundi hayo ya ki Teologia, kuna ambao hukiri kwamba RM ndiye Nguvu za “Mungu” huyo, jambo ambalo tayari lingezalisha tofauti ktk “ushirikiano” wao, haswa katika mtazamo wa usawa walionao! Maana kwa kusema hivyo, mamlaka aliyo nayo Mungu Baba na hiyo aliyonayo Mungu Mwana zitakuwa na walakini, kwani sidhani kama kuna mamlaka isiyo na Nguvu na ikabakia kuwa mamlaka! Maswali ni mengi sana, lakini majibu ni duni kwavile rejea tunayoweza kuitumia ili kuyapata hayo majibu, wanateologia wameifunga kwa kutuambia kwamba hilo “Fumbo”!

  Basi kwa vile Miungu hii imejificha ktk “Fumbo Kuu la Utatu”, tunapaswa tubaki na maswali yetu mioyoni mwetu mpaka siku Fumbo hilo litakapofumbuliwa, ndipo tutajua kwa uhakika Miungu watatu wanawezaje kuwa Mungu mmoja!!!

  Asante,
  &
  Gbu my sister!

 2. Sungura,
  Nakushukuru na nimeyafurahia sana maelezo uliyonipa! 

  Nimefurahi pia kwamba sasa tunaanza kuelewana vizuri katika tafakari ya Neno la Mungu, yaani maongezi yetu na vitendo vyetu tunapoweza kuvirudisha ktk Biblia na kuzitafuta characters zinazoshabihiana na hayo, zile roho; kama ulivyoniona nilipokuchonganisha na Mungu kwanza, na uliporuka, nikakuchonganisha na dada Janeth; ndipo ukaniona ninavyomtumikia Shetani; Nimeipenda sana hatua hii, inaonesha ukomavu!

  Jingine ulilonifurahisha, ni pale ulipogundua kuwa nilkosa uelewa wa ulichokisema, na kuishia ktk huo uchonganishi, basi niwaombeni radhi wote mliotatizika na niliyoyasema, pia nikushuru tena ndg yangu Sungura kwa nuru uliyoniangazia, maana katika ufinyu wa uelewa niliokuwa nao, siku zote huwa najua kwamba: SUALA NA MWENYE SUALA NI KITU KIMOJA! Yaani sikujua kwamba unaweza kulipotezea suala na hapo hapo mkaendelea na mwenye suala shwaari kabisa, ila bado sijajua mtaendelea ktk nini, haswa mnapokuwa mmekutanishwa kwa suala hilo!!!!

  Yaani jambo hili unalonifundisha ni sawa na kumtenga mtu na neno lake kama tunavyojaribu kumtenga Mungu na Neno lake na kuishia ktk ibada ya miungu!!!

  Hata hivyo, nami naungana nawe, sote tuyafurahie maisha, afterall we only live once in this chaotic world, and if by the Gospel you can walk with your head high, waaaaaa, then heaven must be on earth!!!!!!

  Tukiyaacha mambo haya, basi na tuyaendee hayo yaliyo ya kina, “the deep things of God” – “”NINI TOFAUTI???””

  Karibu Sungura!

 3. Asante

  NI kweli lazima kuangalia vizuri NAFSI na ROHO ….

  Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho “Ebr 4:12”

  Natumai tutafakari zaidi NAFSI…Ngoja niwe na subira wajoli wengine nao wachangia .

  Ubarikiwe

 4. Lwembe,
  Nilikwambia kwamba kama ni aibu mtu mzima kuomba msamaha, basi potezea. Nilijua jinsi ulivyo mtata kwa vitu kama hivi kwa hiyo ungetafuta tu namna ya kukwepakwepa, na ndivyo uefanya.

  Kwanza nilikuonyesha tofauti ya nilichosema na kile ulichosema wewe. Mimi nilisema neno ‘tupotezee’ wewe ukasema ati nimesema neno ‘tumpotezee Mungu’. Sasa hivi umekuja na jingine kwamba ati nimesema ‘tumpotezee Janeth’,wakati sikuwa kabisa nasemea swali la Janeth, bali majibu ya watu kwa swali la Janeth.

  Ngoja tu nikusaidie kuelewa kile nilichosema, maana haitusaidii sana kulumbana kwa ishu ndogo kama hii.

  Nilimaanisha hivi:

  Kama suala la kujua tofauti iliyopo kati ya Baba, Mwana, na Roho ni gumu na linawachanganya wengi, na wengi hawalielewi, basi tusisumbuke nalo saana au tulipotezee. Lakini tu kama kulipotezea kwetu hakutatuzuia kufika mbinguni,ambako tukifika tutajua yote.

  Ilikuwa ni rahisi tu kiasi hicho, wala sikusema tumpotezee Mungu au mtu yeyote,ispokuwa suala!

  Sasa nashangaa Lwembe unalazimisha kunigombanisha na Mungu ati nimemwambia tumpotezee, kisha unanigombanisha tena na Janeth. Kazi ya kugombanisha ni ya shetani, usitake kumsaidia tafadhali!

  Kuna mambo ya msingi ya kujadili katika mada hii Lwembe, ni bora ukaibuka na hayo kuliko kuibuka na suala jepesi kama hili, na kumbe tu ni kwa sababu ya kutokuelewa kwako.

  Furahia maisha!

 5. Mjoli Haule,

  Maana ya kwanza ya “Nafsi” ni hii tunayoikuta hapo Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”

  Kwa kadiri ninavyofahamu kwa sehemu, ndio hivyo. Kwamba kwanza mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Na kulingana na Maandiko, tunafundishwa kwamba “Mungu ni Roho”, Yn 4:24, kwahiyo hilo hulifunua jambo la kwamba Adamu wa Mwa 1:26 alikuwa ni roho. Ndipo mbele akapewa mwili wa nyama, hayo mavumbi kama tulivyoona hapo juu.

  Baada ya hapo akapewa maelekezo ya maisha ambayo huko mbele yalimshinda, ule uwajibikaji, na huo ukawa ndio mwanzo wa kukatiwa mawasiliano na Mungu. Hata hivyo Mungu alitengeneza namna ya kumkomboa kutoka Hukumu Yake mwenyewe. Pia Mungu, kuhusu Nafsi, anasema kwamba zote ni mali yake! Eze 18:4
  “Behold, all souls are mine; as the soul of the father, so also the soul of the son is mine: the soul that sinneth, it shall die.”

  Pia kwa kadiri utakavyolifuatilia jambo hili, yaani Nafsi, utaona sehemu nyingine limekuwa reffered to as spirit, kwahiyo unahitajika umakini ktk kuangalia muktadha wa matamshi hayo katika uaminifu.

  Sijui kama nimekidhi haja ya swali lako, bali ninaamini wapendwa wengine wenye ufahamu zaidi, wanaweza kutusaidia katika hilo, au wewe pia!

  Ubarikiwe!

 6. Pastor Sungura,

  Naona “Bwana Jela” amekushawishi mpaka nawe umekuwa mtu wa kuziwinda samahani hata zisipostahili! Wewe ndiye uliyepaswa kunishukuru kwa kukurejeza, badala yake unanitaka nikuombe samahani!

  Dada Janeth ameuliza swali linalohusiana na “Mungu” katika uhalisi wake, nawe maelezo yako yalikuwa yamejaa kejeli, sijui kwanini dada Lilly alikupotezea, angalia unachosema:
  “Nimecheka mpaka basi, Vitu vilivyojaa ndani ya vichwa vya wapendwa wengi anayevijua ni Mungu mwenyewe, maana inatisha kuona ni jinsi gani watu wanamwabudu Mungu wasiyemfahamu sawasawa!”

  Sasa, hata kama ulitaka tumpotezee huyu dada aliyeuliza swali hilo kwa nia njema ya kuujua ukweli, ukijidhanisha kuwa huyo si kitu, basi unapaswa kunishukuru kama kweli ulikuwa humaanishi tumpotezee Mungu, maana yeye Mungu anasema kwa kadiri utakavyomsaidia huyo aliye mdogo, umemsaidia Yeye! Unaona ! Unaweza kumkuta dada Janeth ndio yuko mlangoni kwenye semina mbinguni, nawe huna kiingilio, basi kama ulimpotezea itakuwaje?

  Vigilance protects hope!

 7. Ndg Amani,

  Ni kweli kwamba maneno matakatifu ktk 1Yohana 5:7-8 yamejitosheleza kama unavyosema, nami ninaamini hivyo, bali jambo hilo halizungumzii UTATU MTAKATIFU katika maana ya Nafsi Tatu zilizo ktk UMOJA, kwa hicho kifungu cha 7, “For there are three that bear record in heaven, the Father, the Word, and the Holy Ghost: and these three are one”, yaani watatu hawa ni MMOJA na si UMOJA kama unavyosema!

  Pia hata hicho unachokisema kwamba, “Hebu jichukulie Umoja wako kati ya roho yako, maji na damu na huo umoja uliopo ndivyo ilivyo kwa Bwana (UTATU ndio mwili wake)”, pia unasema, “Lakini kwa uweza alionao Bwana nafsi hizo tatu (yaani huo mwili), zimekuwa hai na zenye kujiwakilisha. soma tena…
1timotheo 3:16” Haya yote ni maelezo yaliyojikanganya kidogo! Hebu jaribu kutafuta tafsiri ya Utatu Mtakatifu kwanza, ili uwe sawa katika ufahamu, vinginevyo hii tafsiri yako inautengeneza Utatu Mtakatifu mwingine mpya!

  Utatu nilio nao mimi wa hizi components, “roho”, “maji” na “damu” unashabihiana na huo unaozungumziwa ktk kifungu cha 8, “And there are three that bear witness in earth, the Spirit, and the water, and the blood: and these three agree in one”, lakini si katika namna ya Nafsi Tatu za Mungu unavyoelezea bali katika namna ya KUZALIWA MARA YA PILI tunakokupitia!

  Hatuzaliwi mara ya pili mbinguni, bali hapa duniani, ndipo ushuhuda anaouzungumzia Yohana ni wa hapa duniani, tukiwa na huo ushuhuda ndipo tutayaelewa hata hayo ya kifungu cha 7 yanayozungumzia mambo ya mbinguni!

  Katika uzazi wa kawaida, akina mama wanapojifungua, tazama kinachotokea, kitu cha kwanza huwa ni Maji. Mfuko wa uzazi unapopasuka basi maji humwagika. Cha pili ni damu na cha mwisho ni roho, ambayo mtoto huichukua hapo anapofika duniani, wakunga wanalijua hilo, wanapo kapokea hukainua na kukapiga kofi laini mgongoni kisha ungesikia “Ng’a-aa”!!! Ukiingia eneo hilo unaweza kudhania mtu kachinjwa, pametapakaa damu iliyochanganyika na maji, lakini chumba kimejaa furaha, mama haukumbuki tena ule uchungu, amepata mtoto, “IMEKWISHA”; vivyo kuzaliwa mara ya pili!!!!

  Mtazame Kristo, 1Yn 5:6 “… aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu”; pale msalabani akiwa katika ule Uchungu wa Uzazi, akilizaa Kanisa lake. Maji na Damu vilimwagika, na akaitoa roho yake, “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” hizo elements tatu ndizo huleta kuzaliwa upya! Maji, damu na roho ndio hufanya kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo, ndio huko kupatana kwa habari moja. Yaani unaweza ukawa na ushuhuda wa Damu na usiwe na ushuhuda wa Maji, au ukawa na wa Maji usiwe nao wa Damu, au ukawa na wa Damu na Maji na usiwe na wa Roho; bali kuwa na ushuhuda wa Roho ni lazima uwe nao pia wa Maji na Damu!

  Kwahiyo elements haziwezi kuwa Nafsi, yaani Maji hayawezi kuwa Nafsi, wala Damu wala Roho, bali muunganiko huo ndio unaotufanya kuwa Nafsi hai! Hata katika mtazamo wa kawaida tu, Je, kwani mtu anapoongezewa damu ya mtu mwingine mwilini mwake, huwa anaongezewa nafsi??

  Basi unapoipokea Injili kama ilivyohubiriwa na mitume ndipo wewe huipokea Damu ya Yesu iliyomwagwa pale msalabani, hiyo hukuongoza katika ubatizo wa Maji kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili kuziondoa dhambi zako na kuingizwa ktk kuyashika yote yampasayo mkristo, lile Fundisho la Mitume; hapo ndipo unakuwa chombo kisafi, tayari kwa kutumika. Kisha Mungu, baada ya kukigau chombo hicho na kuridhika nacho, ndipo hukijaza Roho wake, akikukamilisha kwa utumishi, ule Ukuhani, Roho wa Mungu mwenye kuzijua Siri za Mungu, yale Mafumbo, hukuongoza katika njia akikuweka ktk kweli yote, pamoja na hiyo 1Yn 5:7!!! Hilo lawezekana tu iwapo utaufikia ukamilifu huo, la sivyo utabaki katika dini iliyojiviringisha katika mafumbo magumu sana kama hili la “Utatu Mtakatifu”, kama unavyomuona Nikodemu, Yn 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Dini yake haikumsaidia kulijua jambo hilo, licha ya utakatifu aliojidhania anao!!!

  Hebu ziangalie Fumbo hizi, kisha jaribu kuzirudisha katika Utatu ili uzipambanue Nafsi hizo katika ulinganishi na hayo uliyoyasema:
  1: Yn 3:13 And no man hath ascended up to heaven, but he that came down from heaven, even the Son of man which is in heaven.

  2: Zek 3:2 “BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee”

  3: Kut 34:5-6 “BWANA akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la BWANA. BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma…”

  Kum 4:15
  “Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto; msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke.” Basi juu ya ufahamu huu, ndipo ile 1Tim 3:16 “…Mungu alidhihirishwa katika mwili…” inapaswa itupeleke mbele na kumuona huyo Mungu aliyedhihirishwa katika mwili na kuachana na “fumbo ngumu zisizoeleweka wala elezeka!

  Ndg Amani, ni rahisi sana kuingia ktk ibada ya miungu kwa kupandikiziwa “mafunuo” kutoka ktk Biblia hiyo hiyo unayoisoma na usiwe na uwezo wa kuyashitukia maana Ibilisi naye anayo “mafumbo”, Ufu 2:24 “…wasiozijua fumbo za Shetani…”; ili kuwa salama ni lazima uwe umaezaliwa mara ya pili, kwa Roho uliyenaye basi akufunulie na fumbo hizo maana vyote vi utupu mbele yake!

  Ubarikiwe, ndg yangu ktk Kristo!

 8. Wajoli wa Bwana……..
  Mbarikiwe

  Maana tunajifunza,na nina shauku ya kuwasikia Bro Lwembe na Mabinza ,
  Naomba kuuliza nini maana ya” Nafs”i kibiblia,mkielezea kwa maandiko itakuwa njema zaidi tupate ufahamu,na isiwe maandiko “mingi”

  kwa mabandiko yenu(Lwembe&Mabinza)mliyoandika kuna maswali nitaendelea kuwaliza ili nipate kujifunza nipate/tupate kulinganisha na ule ufahamu wangu ninaoufahamu kwenye maandiko(Neno la Mungu)

  Karibu

 9. Tumaini,

  Unajua kuna shule zingine ni ngumu sana, na zinawezekana tu kwa watu fulani. Hii shule tunayojadili hapa ni ngumu sana kuliko inavyoweza kuonekana. Na ugumu wake unaongezeka pale watu wanapotaka kuyaelewa mambo haya kwa mantiki za brain ya kawaida.

  Kwa mfano, kwa kuangalia kwangu mtu kama Amani itachukua muda mrefu sana kuelewa hili suala, kwa jinsi tu mimi nilivyomwona.

  Mfano wa shule kama hii kwenye biblia huu hapa Yohana 3:

  YESU: 3 “Very truly I tell you, no one can see the kingdom of God unless they are born again.[a]”

  NIKODEMO: 4 “How can someone be born when they are old?” “Surely they cannot enter a second time into their mother’s womb to be born!”

  YESU: 5 Jesus answered, “Very truly I tell you, no one can enter the kingdom of God unless they are born of water and the Spirit.

  6 Flesh gives birth to flesh, but the Spirit[b] gives birth to spirit.

  7 You should not be surprised at my saying, ‘You[c] must be born again.’

  8 The wind blows wherever it pleases. You hear its sound, but you cannot tell where it comes from or where it is going. So it is with everyone born of the Spirit.”[d]

  NIKODEMO: 9 “How can this be?”

  YESU:10 You are Israel’s teacher, and do you not understand these things?

  Tumaini umeona hiyo shule ilivyokuwa ngumu kwa Mwalimu Nikodemo? Maana yeye alitaka kuyatambua mambo kama hayo kwa mantiki (logic) za mwilini. Kwa hiyo alijikuta anapigwa nock-out kali sana, maana ile shule ilikuwa inatambulika kwa logic za rohoni, nazo logic hizo hupatikana kwa mtu wa rohoni tu.

  Nje ya hapo mtakesha, hakuna atakayeweza kuelewa mantiki ya tofauti kati ya Baba, Mwana, na Roho!

  Mtaishia kuwa kama wale ambao huwa haiingii akilini kuwaambia ati Mungu alizaa mwana, tena ati huyo mwana naye ni Mungu!

  Simply huwa wanauliza, ‘je Mungu alimuoa Mariam, na je kuna Mungu wawili mpaka hapo?’

  Tuendeleeni!

 10. Lwembe,

  Kuna wakati nawe huwa unanishangaza si kidogo rafiki yangu. Umenikejeli kifalsafa kuwa ungenipa zawadi, lakini bila kuwa makini katika jambo unalonikejeli nalo.

  Ngoja ninukuu ulichosema kuwa mimi nimesema:

  ”Unasema “TUMPOTEZEE Mungu”!!!!! Yaani baada ya kuhubiriwa Injili miaka yooote hii, mwisho wa siku unasema eti tumpotezee Mungu? Halafu unajiaminisha kuwa eti “tukifika mbinguni tutajua yote”

  Swali; ni wapi mimi nilisema tumpotezee Mungu?

  Ngoja ninukuu nilichosema:
  ”Kama vipi,TUPOTEZEE tu, maana tukifika mbinguni tutajua yote, kama kutokujua kwetu hapa hakusababishi tusifike hata huko mbinguni tusemako tunaenda!!”

  Mheshimiwa Lwembe, je ulichosema wewe na nilichosema mimi vinafanana?

  Ukiwa muungwana utaniomba msamaha, lakini ukiona ni aibu mtu mzima kuomba msamaha, basi potezea tu!

  Asante!

 11. Kaka Lwembe
  Naamini maneno matakatifu katika 1Yohana 5:8 yamejitosheleza sana hasa mtume Yohana anaposema watatu hao wote ni UMOJA. yaani kama ulivyo wewe mwanadamu u roho,maji na damu, ndivyo alivyo Jehova ni BABA, NENO(YESU) NA ROHO MTAKATIFU. Yeye Yohana hakuyasema hayo kwa Ufahamu wake bali alifunuliwa na Roho Mtakatifu 1Yohana 5:7.
  Hebu jichukulie Umoja wako kati ya roho yako, maji na damu na huo umoja uliopo ndivyo ilivyo kwa Bwana (UTATU ndio mwili wake).
  Lakini kwa uweza alionao Bwana nafsi hizo tatu(yaani huo mwili), zimekuwa hai na zenye kujiwakilisha.soma tena…
  1timotheo 3:16.
  Mungu alidhihirishwa katika mwili (Kwa hakika huyo ni Yesu/Emanueli, math 1:23 soma Isaya 9:6, sasa tujiulize mbona alimtaja Baba na alimsema kuwa ndiye Mungu?) Hizi ni nyakati za Mihuri kufunguliwa na mambo magumu kuwekwa hadharani, Ishara ya nyakati za mwisho, zamani maneno haya yalifichwa kwa sababu yangewapoteza tu wakristu wachanga, na ndio maana zikawa siri za kanisa/siri ya utawa..
  Huo mstari unaelezea mpango wa Mungu kuwa atakuja kama Bwana Yesu na atadhihirika kuwa ni kweli/haki kama Roho mt (Yesu alikubalika kuwa haki baada ya kupaa kwake wengi walimkubali hata leo kuwa ni haki kupitia matendo ya Roho wake soma matendo ya mitume)
  Lakini udhihirisho huo wa MUNGU kupitia YESU na ROHO MTAKATIFU haumfanyi asiwe MUNGU na yeye kuwa MUNGU hakumfanyi asidhihirike kama YESU NA ROHO MTAKATIFU.
  Sio watatu katika mmoja bali watatu katika umoja
  Kuhusu malaika kuumba, wote tunajua kuwa malaika hawaumbi! 🙂
  Hebu soma vizuri huo mstari mwanzo 1:26 na tumfanye mtu kwa mfano wetu, sidhani kama malaika ni mfano wetu wao wana mabawa sisi hatuna, ni Mungu tu huko mbinguni ndiye aliyekuwa wa mfano wetu, soma tena Mwanzo 2:7 Ni Mungu pekee, ingekuwa ni malaika angewataja na hapo, lakini kutokana na watatu hao kuwa umoja ilikuwa ni sawa kwa Mungu kusema ni yeye pekee katika mstari mwingine.
  Kuhusu ubatizo ikifanyika kwa mujibu wa maagizo ya Bwana yaani Baba, Mwana na Roho mtakatifu ni sawa kwa kuwa huyo ndiye Mungu.
  Pia kwa Yesu ni sawa pia kwa kuwa huyo ni Mungu katika mwili aliyekufa kwa ajilli ya dhambi zetu.(Mungu kupitia mwili wa damu na maji ndiye mpatanishi mkuu wa wokovu wetu kwa kuwa alijitiisha hata kufa kwa ajili yetu kwa hivyo si mbaya tukitumia nafsi ya Mungu mwana kwa ubatizo pia)
  Hebu jadili haya
  Wagalatia 4:6 ( Roho wa Mwana?)
  1 Wakorintho 7:40 (Roho wa Mungu?)
  Katika lugha tuna viwakilishi vya nafsi (yaani kama kitu ni nafsi hutumia viwakilishi hivi, huwezi kusema “mlango alikwenda” ila “Jane alikwenda”)
  Ukisoma Yohana 16:13, Matendo 21:11 na mistari mingineyo utaona kuwa huyu Roho anatajwa kama nafsi hai kwa mujibu wa lugha iliyotumika. sasa anaposema batizeni kwa Baba, Mwana na Roho Mathayo 28:19 anamaanisha nafsi tatu zilizo hai katika umoja wa Kiungu.
  Not three in one but three as ONE.
  Wagalatia 6:17
  Maranantha!! 🙂

 12. Janeth,

  Isaya 44:24 “BWANA MKOMBOZI WAKO YEYE ALIYEKUUMBA TUMBONI ASEMA HIVI MIMI NI BWANA NIFANYAYE VITU VYOTE ,NIZITANDAYE MBINGU PEKE YANGU NIENEZAYE NCHI NI NANI ALIYE PAMOJA NAMI ?”

  Ndugu yangu katika Kristo, kutoka katika tamko hilo la Mungu mwenyewe hapo juu, litabaki hivyo hivyo, maana ndiyo kweli yenyewe kuwa, Mungu ni mmoja tu naye yupo katika nafsi hiyohiyo moja!

  Nafsi huwa moja tu katika uhai mmoja, na huwa vilevile moja katika ufu mmoja! Nafsi hai kinyume chake ni nafsi mfu – Mw.2:7 “7BWANA Mungu alimwuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa nafsi hai.”.Mungu ni mmoja, hai, na nafsi moja – Ebr 9:14
  “Basi si zaidi damu yake Kristo ambaye kwamba kwa roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu mpate kumwabudu Mungu aliye hai..” Kama ilivyo nafsi ni moja na uhai ni mmoja tu, Yoh 10: 17 “ Ndiposa Baba anipenda kwa sababu nautoa uhai wangu ili ni utwae tena” Hakuna pahali popote katika Biblia panaposomeka, Mungu mwana au Mungu roho mtakatifu. Ila lipo andiko linalosomeka Mungu Baba, baathi ya maandiko ni katika, Efe 6:23 Gal 1:3Yn 6:27; 1Cor 8:6,nk.

  ASILI YA MAFUNDISHO HAYO YA MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU;

  Asili ya mafundisho hayo ni shetani mwenyewe, kama ambavyo shetani mwenyewe hutangatanga tu hovyo, ndivyo hivyo hivyo na mafundisho yake hayana asili thabiti! Huu ni uthibitisho tosha kuwa suala linalohusu Utatu Mtakatifu wanaouamini baadhi ya “Wakristo” yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu kuwa ni kitu kimoja ,huleta shida ya kufahamu. Kama ambavyo nimekuwa nikisema kila siku katika maada zinazofanana na hii kuwa, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu , si nafsi tatu za Mungu Mmoja, na wala siyo miungu mitatu, liko neno katika Kiebrania,ambayo ni lugha ya asili iliyotumika katika Agano la Kale huitwa “Elohim” ambalo wanazuoni huliona kama linaonesha wingi wa Mungu, wanaofanya kazi kwa pamoja na wakati huo huo kila moja ikiwa peke yake (unity in diversity). Kwa maana hiyo watu hupotoshwa na hata kutoijua ile kweli yenyewe, na kufikia kuuamini uongo kuwa kuna Mungu Mwana na Mungu roho mtakatifu!

  Si kila mwenye kuamini kuwa Mungu mmoja, anajua ki ukweli juu ya Mungu, alivyo na tabia yake. Mashahidi wa Yehova ambao nao huamini kuwa Mungu ni mmoja wao HAWAAMINI kuwa Yesu na Roho mtakatifu ndiye yuleyule Mungu mmoja; si shangi sana maana wao si wakristo na kwakuwa ni kawaida ya shetani kwamba, hajisemei tu, hutumia maandiko hayahaya ya Neno la Mungu, lakini kwa kuyawekea tafsiri zake mwenyewe. Ipo mifano michache ya maandiko wanayosimamia Mashahidi wa Yehova (Jehova’s Witness) ili kuhalalisha hoja yao kuwa Yesu na Roho mtakatifu si yuleyule Mungu mmoja, wao husema kwa mjibu wa, Mt 4: 1 “ Yesu alijaribiwa na Ibilisi” wakati Yak. 1: 13 inasema, “ Mungu hajaribiwi “ pia ile Yh 8: 40 inasema, “Yesu alisema mimi mtu” wakati ile ile Hes. 23:19 inasema “Mungu si mtu” lakini wakasahau kupaona palipoandikwa kuwa Mungu akaumba mmtu kwa mfano wake Mw.1:27 na ile Mw. 3:22; inayosema “huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu” wanaisoma Yoh 17: 3 “ Yesu alisema wakujue wewe mungu wa pekee, pia naile ITim 2: 5 Kwa kuutazama ule mwili wa Kristo na kufeli kukiona kile kilichokuwa ndani ya ule mwili wakafikia katika uamzina uelewa kuwa “ Yesu ni mwanadamu tu (siyo Mungu) nk. Katika Jarida lao liitwalo ‘Je Tuamini Utatu” ule uk 20-23 linaelezea kuwa “Roho Takatifu (Nasiyo Roho Mtakatifu ) humuita ni kani yenye kudhibitiwa ambayo Yehova Mungu hutumia kutimiza makusudi yake tofautitofauti kama apendavyo. Wao humfananisha roho mtakatifu, ambaye humwita roho takatifu kuwa ni kama nguvu za umeme , kani (Energy/force) ambayo yaweza kutumiwa kwa njia tofauti ili iendeshe mambo kwa hiyo Roho mtakatifu ambaye wao humuita Roho takatifu si mtu kwamba awe na nafsi, wala si Mungu.

  Si hao tu ukiwaangalia waislamu japo kwa kifupi wao husema Mungu ni mmoja tu na kwamba hana mshirika, na ukijaribu kulinganisha maandiko kwa mfano ikisoma ile Isaya 44:24 utaona kuwa wapo sawa, lakini ukiwambia habari ya Yesu au Roho mtkatifu kuwa ni huyohuyo Mungu, hawakubali kamwe. Tunapoangalia uislam na waislamu, wao kwao, Roho Mtakatifu ni malaika maarufu katika dini hiyo aitwaye Jibril. Katika Suratul Al- Bagarah (ng’ombe jike) 2:87 “Na hakika tulimpa Musa kitabu na tukawafuatisha mitume (wengine) baada yake na tukampa Issa mwana wa Mariam hoja zilizo wazi wazi na tukamtia nguvu kwa roho takatifu (Jibril)……..“

  `Ukiutazama ule ufafanuzi wa aya hiyo ya 87 katika Quran yao, ufafanuzi ule unasema; Kwa waislam Roho Mtakatifu ni malaika Jibril si yule wanayedai Wakristo kuwa ni yuleyule Mungu au kwa baadhi ya wakristo kuwa ni mmoja wa asili ya Utatu (Trinity).Unaona? Kama nilivyoeleza, kwa ufupi utaona kuwa swala la utatu ni la kidini tu, si la kibiblia. Ndiyo maana wasomi wa kikristo na wasio wakristo kila mmoja wanajua, fundisho la Utatu Mtakatifu kivyake vyake! Fundisho hili la Mungu Mwana na Mungu roho ni la kidini zaidi, maana katika haohao wanaodai kuwa ni wakristo na kwamba wanaiamini Biblia kuwa ni Neno pekee la Mungu, hujikanganya na hata hawajui vizuri ni wapi na lini hasa Fundisho hilo lilitokea! Watu hao ambao si waislamu wala mashahidi wa Yehova inasemwa kuwa, wao pia wanasema:-

  1.Fundisho la Utatu lilianzia katika Mkutano wa Nicea, mwaka 325 B.K uliosimamiwa na mfalme Constantino wa Roma ambao ulihudhuriwa na wajumbe maaskofu wapatao 300 toka kote duniani.

  2. Fundisho la Utatu Mtakatifu lilianzia mwaka wa 381 B.k. katika kikao cha mjini Constanti Nipol – Napol Italy, kwa usimamizi wa mfalme Theodousius.

  3. Wapo wanaosema kuwa utatu ulianzishwa mwaka 362 B.K. mjini Aleksandiria Misri, tokana na mkutano wa viongozi wa kawaida.

  4. Wapo wasemao kuwa, fundisho la Utatu lilianzishwa na kasisi Mkatoliki aitwaye Athanasio aliyekufa mwaka 373.B.K.

  5. Wengine husema Utatu ni fundisho lililotungwa kusini mwa Ufaransa kwenye karne ya 5 B.K.

  6. Wengine wanasema Utatu uliingizwa katika liturgia na baadaye Roma Italy

  7. Na siku hizi waislamu hudai kuwa, Utatu Mtakatifu ni fundisho alililozushwa na Paulo kwa maslahi yake kule Antiokia na kuyaacha mafundisho ya Yesu, kwasababu yeye hakuchaguliwa na Yesu alipokuwepo hapa duniani, hivyo alijitungia mara tu baada ya Yesu kuondoka, nk.

  Zipo theory nyingi nyingi sana tu, lakini ukweli upo pale pale kuwa Mungu ni mmoja, ana nafsi moja na kwamba yeye ni ndiye Baba, Mwana na Roho mtakatifu kama sifa zake za kiutendaji tu, na hakuna mungu mwana wala Mungu Roho kulikoandikwa katika Biblia! Biblia inasema wazi kuwa Baba, Mwana na Roho mtakatifu ni Mungu yuleyule mmoja mwenye nafsi moja tu na kuwa kuitwa Baba, Mwana na Roho mtakatifu ni sifa zake tu za kiutendaji. Ni kwamba, Baba ni Mungu Fil 1:2 “ Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu….”. Huyu Baba, ndiye aliyeumba vyote, Nafsi ya Baba. Mwanzo 1:1 “ Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi”. Na ndiye aliyefanyika Mwokozi akateswa na kuwa yeye ndiye Yule Roho mtakatifu, hebu ona, Isaya 63:7-10 “ Nitautaja wema wa BWANA, Sifa za BWANA…..;….akawa Mwokozi (Yehoshua) wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa…..; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe;..,… Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia ,…”

  lakini Kristo Yesu ambaye ndiye Mwana ni Mungu yuleyule tu, – Yoh 1:1:14 Kol 2:9 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno , naye…..Neno alikuwa Mungu…..”;Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu….” Lakini pia katika ile, Kol 2: 9 tunaona kuwa, “ Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili” Vivyo hivyo na . Roho Mtakatifu ni Mungu, ukiitazama Mdo 5:3-4 “ Petro akasema Anania kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uwongo Roho Mtakatifu….?…..?….?….? Hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu”.

  Kwakuwa Mungu ni nafsi hai ni wazi kuwa, Roho Mtakatifu ni Mungu huyohuyo mwenye nafsi ileile iliyo hai na yenye hisia “emotion”, ndiyo maana huhuzunika (Ef4:30),hunena, (Uf 2:7), anaweza kuzimishwa (1Thes5:19), Hufurahi (Rum 14:17) .Hivyo Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe na wala siyo kitu tu (impersonal) (Yoh 4:24) .

  Mungu ndiye Baba, ndiye mwana na ndiye Roho Mtakatifu, ila si utatu kwa maana ya Mungu Baba, mungu mwana Mungu Roho mtakatifu; ila anakuwa Baba, Mwana na kuwa Roho mtakatifu kutokana na utendaji kazi wake na hizo ndizo sifa kuu zake. Hebu tumuone Mungu kupitia sifa hizo kuu nilizozitaja kama zinashabihiana na sifa za Mungu japo baadhi tu kama zinavyotajwa na Biblia, yaani kama, zikiwa kwa Baba zitakuwa pia kwa Mwana na kwa Roho mtakatifu.

  MUNHGU NI MUUMBAJI;
  BABA:- Mw. 2:7, 7BWANA Mungu alimwuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa nafsi hai”

  MWANA:- Yh. 1:3 “3Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.”

  ROHO MTAKATIFU:- Ayub 33:4 “ Roho ya Mungu imeniumba na pumzi za Mwenyenzi hunipa uhai”

  MUNGU HUFUFUA;
  BABA:- I Thes 1:10 “Na kumngojea mwanawe kutoka mbinguni ambaye alimfufua katika wafu,….”

  MWANA: Yoh 2:19 “Yesu akajibu akawaambia livunjeni Hekelu hili nami katika siku tatu nitalisimamisha….” Yh.6:44 “44Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.” Yoh 10: 17 “ Ndiposa Baba anipenda kwa sababu nautoa uhai wangu ili ni utwae tena. Yoh 5:21
  “ maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha vivyo hivyo na mwana huwahuisha wale awatakao”

  ROHO MTAKATIFU:-
  Rum 8:11 “Lakini ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu , yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anayekaa ndani yenu”

  MUNGU HUKAA NDANI YA WATU;
  BABA:- 2 Kor 6:16 “……, kama Mungu alivyosema ya kwamba nitakaa ndani yao na kati yao nitatembea nami nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu”

  MWANA : Kol 1:27 “ ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa nao ni Kristo ndani yenu tumaini la utukufu”

  ROHO MTAKATIFU:– Yoh 14:17 “Ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea kwa kuwa haumwoni wala haumtambui: bali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu naye atakuwa ndani yenu.”

  MUNGU YUPO MAHALI POTE

  BABA:- 1Fal 8:27
  “Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? tazama mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu ,sembuse nyumba hii niliyojenga?”

  MWANA:- Math 28: 19- 20 “Basi enendeni , mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari “

  ROHO MTAKATIFU – Zaburi 139: 7-10
  “Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni wewe uko, ningefanya kuzimu kitanda changu wewe uko. Ningekuwa na mbawa za asubuhi na kukaa pande za mwisho za bahari huko nako mkono wako utaniongoza na mkono wako wa kuume utanishika”.

  MUNGU HUJUA YOTE
  BABA: – 1Yoh 3:20
  “Ikiwa mioyo yetu inatuhukumu kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote”

  MWANA:- Yoh 16; 30 “Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote wala huna haja ya mtu akuulize, kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu”
  Yoh 21:17 “Akamwambia mara ya tatu Simoni wa Yohana wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu wanipenda? Akamwambia Bwana wewe wajua yote , wewe umetambua ya kuwa nakupenda, Yesu akamwambia lisha kondoo zangu” (Marko 2:8)

  ROHO MTAKATIFU – 1 Kor 2: 10- 11 “ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu .Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu, ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu ,hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu”

  MUNGU HUTAKASA;
  BABA :– I Thes 5: 23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili ,bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”

  MWANA- Mt. 8:3 “Nataka takasika” 1Tim. 4:5,” 5kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu…………”

  ROHO MTAKATIFU – 1 Pet 1:2 “2Ninawaandikia ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo”

  MUNGU NI WA MILELE
  BABA – Zaburi 90: 2
  “ Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia na tangu milele hata milele ndiwe Mungu”

  MWANA- Mika 5: 2 , Math 2: 4-6
  “Bali wewe Bethlehemu Efrata uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele “ (Math 2:4-6)

  ROHO MTAKATIFU – Ebr 9:14
  “Basi si zaidi damu yake Kristo ambaye kwamba kwa roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu mpate kumwabudu Mungu aliye hai?

  MUNGU NI UPENDO
  BABA – Yoh 3:16
  “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”

  MWANA- Efeso 5:25
  “Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili yake.”

  ROHO MTAKATIFU – Rum 15:30
  “Ndugu zangu nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu” nk, kwani ipo mifano na zipo tabia nyingi nyingi sana ambazo zinathibitisha wazi kuwa Mungu ni mmoja.

  Hizo ni baadhi tu ya sifa za Mungu zinazoambatana na sifa zake kuu, yaani Baba, Mwana na Roho mtakatifu ambazo kwa pamoja ufanya kitu kinachojulikana kuwa “PENDO”! Labda nihitimishe tu kwa kusema kuwa, tunapaswa kuishi na kulitazama Neno, na tuwe katika kuhitaji sana kukaa humo. Tumtegemee Kristo ili yeye atuwezeshe kumjua ili kile tunchokiabudu tuwe na ufahamu nacho, kwani si kipindi cha kupapasa tena bali yote yatupasayo kuyajua yamewekwa na yanaendelea kuwekwa wazi. Lakini kwa wasio wake, wao hawana nafasi hata kidogo ya kumjua, kwa sababu, “WATAMJUAJE YEYE WASIYEMJUA?” Itabaki hivyo hivyo bila Roho mtakatifu wasio wake ni lazima wapite kapa. Maana kanisa limewekwa mikononi mwa Roho mtakatifu, lakini tunajua wazi kuwa Kristo ndiye aliyekufa kwa ajili ya Kanisa na kwa maana hiyo, matazamio ya watu wa dini ni kuwa kanisa ni lazima litajwe kuwa lipo mikononi mwa Yesu, ndipo wangeelewa, lakini kule kutajwa kuwa liko mikononi mwa Roho mtakatifu (Mdo20:28) wanaona kuwa aliyemwaga damu pale msalabani siye Roho mtakatifu wala si Baba ila ni Yesu, kwani hawajui kuwa, Baba,Mwana,na Roho Mtakatifu ni mmoja ndiye Mungu (1 Yoh 5:6-7).

  KWA HIYO HUTOPATA HIYO TOFAUTI YA MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU KWA KUPITIA BIBLIA ILA LABDA KUPITIA VITABU VYA DINI; MAANA KATIKA BIBLIA YUMO MUNGU BABA PEKE YAKE NA NDIYE ANAYEJULIKANA KAMA LIVYOKUELEZEA HAPO JUU! Mimi nasema,
  Golikipa wa timu yako akipigwa chenga, kaa chini maana hilo tayari ni bao!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 13. Mpendwa Sungura hakuna kupotezea just weka mambo wazi yale ya kweli biblical unayoyafahamu ili tuendelee kujifunza maana tupo kuchambua mchele yaani tuweke chuya,mawe na takataka zingine pembeni tubaki na mchele safi unaolika so lete shule kaka watu tupone.Lwembe nakusoma bt kama vile umeegemea upande flan hivi so nakuwa nakusoma nusunusu!weka mambo wazi Biblical bila kuegemea upande flani hivi!Nitabarikiwa zaidi itakaposemwa kweli tupu maana hi
  yo ndiyo itakayotuweka huru.

 14. Zephania,

  Umenichekesha saaana!
  Umejieleza kwa ufasaha mkubwa sana, lakini mwisho umeshindwa kuyakwepa mapokeo! Tazama Mapokeo yanayokushikilia:
  “”mm kwa ufahamu wangu najuwa nakuamini kuwa MUNGU ni mmoja, ila mwenye nafsi tatu, yaani Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu. Hawa si mungu watatu, bali ni Mungu mmoja…””

  Sasa tuyarejee maelezo yako:
  “”Nafsi ni kitu kilicho ndani mtu, mnyama na kila kitu kiendacho kwa nafsi hai. kwa mfano; mimi naitwa Zephania ndio jina langu linalo nitambulisha kuwa mimi ni mtu,nikiwa kwa wazazi wangu naitwa mwana,lakini bado mimi ni zephania! nikiwa kwa watoto wangu naitwa Baba nayo hainiongezei wingi wa mimi bado nitakuwa mm huyuhuyu zephania, na nikiwa kwa mke naitwa mume, zephania mm huyuhuyu wala hatujawa wa zephania watatu bali ni mm huyohuyo ila kwa nafsi tatu, yaani baba kwa wanangu, mwana kwa wazazi na mme kwa mke.kwa hiyo kwa nafsi ya Mungu kila nafsi ina kazi yake ktka kuukamilisha Uungu wake””

  Ukweli wa maelezo yako ni huu hapa:

  Kwanza, wanyama hawana Nafsi wao ni hayawani tu, kwahiyo hawawajibiki kwa Mungu maana hawatendi dhambi, bali sisi ndio tu Nafsi hai (Mwa 2:7)!
  Nafsi katika mfano wako, ni wewe Zephania, ambaye unaweza kuwa na vyeo vyote ulivyovitaja kukuhusu, ndipo maelezo yako yatakuwa hivi:

  “”mimi naitwa Zephania ndio jina langu linalo nitambulisha kuwa mimi ni mtu (ile Nafsi hai), nikiwa kwa wazazi wangu naitwa mwana, lakini bado mimi ni Zephania (ile Nafsi hai)! nikiwa kwa watoto wangu naitwa Baba nayo hainiongezei wingi wa mimi bado nitakuwa mm huyuhuyu Zephania (ile Nafsi hai), na nikiwa kwa mke naitwa mume, Zephania mm huyuhuyu wala hatujawa wa Zephania watatu bali ni mm huyohuyo ila kwa nafasi tatu (vyeo vitatu), yaani baba kwa wanangu, mwana kwa wazazi na mme kwa mke. kwa hiyo kwa Nafsi ya Mungu kila nafasi (cheo) ina kazi yake ktka kuukamilisha Uungu wake””

  Hahahahaha….! umeona how close you were to the TRUTH, and yet so far away from IT!!!

  Ubarikiwe ndg yangu!

 15. Ndg Amani,

  Maelezo yako ni mazuri, lakini yanahitaji ufafanuzi zaidi ili anayekufuatilia ktk kujifunza apate kuelewa vizuri zaidi.

  Kwanza unawataka wanaokataa Utatu, wathibitishe kiMaandiko ni wapi iliponenwa kwamba HAKUNA Utatu! Jibu lake ni kwamba hawatafanikiwa kukuletea Maandiko ya jambo ambalo Biblia haijalisema na wala hailijui!

  Mwa 1:26 unasema “Mungu ametumia wingi katika uumbaji, ina maana malaika nao waliumba?” Hapa ndipo nilikutegemea uje na uthibitisho wa kiMaandiko kutueleza ukweli wa hilo lililofanyika.

  Pia unasema:
  “”Kristu aliwaambia mitume huyo roho hawezi kuja mpaka mimi nitakapokwenda kwa baba ina maana kuwa yeye huyohuyo ndiye Roho matakatifu kwa hiyo alikuwa nao kwa nafsi ya Mwana akishawaacha ndipo ataweza kuja tena kwa nafsi ya Roho Mtakatifu. kumbuka alisema nitakuwa nanyi mpaka mwisho wa Dahari.””

  Hebu nifafanulie zaidi kuhusu hili: kwamba Kristu ndiye RM, na kwamba RM ni Nafsi ambayo kwa maelezo yako ndiye Kristu, kwahiyo kuna tena Nafsi ya Mwana ambayo Kristu aliitumia, hebu nifafanulie zaidi kuhusu Kristu na RM na Mwana, na Baba, uhusiano wao ukoje kulingana na maelezo yako hayo?

  Pia ktk maelezo yako unasema RM ana umbo/mwili yaani Nafsi kama binadamu na si Upako, pia RM ni Nafsi ya Mungu ambayo huingia ndani yetu baada ya kumkubali Yesu…
  Swali langu ni hili, Nini tofauti kati ya Nafsi ya Mwana na Nafsi ya RM na Nafsi ya Mungu na Nafsi ya Baba? Je, kwamba Kristu ndiye RM, Mwana ni nani?

  Kuhusu ubatizo unasema:
  “”Hata ubatizo kuna sehemu umelenga nafsi tatu mathayo 28:19, na sehemu nyingine umelenga Yesu pekee, matendo 2:38 hii inamaanisha kuwa watatu hao wote ni sawa na umoja.””
  Je, kwa kauli yako hii, ndio unatuambia kuwa huo ubatizo ktk Mdo 2:38, uliomlenga “Yesu pekee” (nitafurahi ukiniambia ni Nafsi ipi) unajitosheleza katika kuitimiza Mt 28:19?

  Pia kuhusu maelezo yako ya UMOJA WA WATATU (waraka wa kwanza wa Yohana 5:8), hebu jaribu kulitazama jambo hilo kwamba hao WATATU ni MMOJA na si UMOJA, uone kama maelezo yako yatabakia hivyo au itabidi uyaboreshe utakapoyaunga ktk hiyo 1Tim 3:16!

  Ni haya machache ambayo ninaamini yatanileta ktk ufahamu zaidi.

  Ubarikiwe!

 16. Sungura,
  Katika michango niliyowahi kuisoma katika blog hii ya Kikristo, mchango wako Sungura ni outstanding kwa vipimo vyote, yaani kama wanatoaga zawadi basi unastahili iliyobora kabisa!

  Unasema “Tumpotezee Mungu”!!!!! Yaani baada ya kuhubiriwa Injili miaka yooote hii, mwisho wa siku unasema eti tumpotezee Mungu? Halafu unajiaminisha kuwa eti “tukifika mbinguni tutajua yote”!!! Mungu mwenyewe naye alisema ukimpotezea naye anakupotezea vilevile, sasa utafika mbingu ya nani? Kama hata Mungu mwenyewe hatumjui ni dalili ya kwamba tuko Jangwani, na tusipokuwa wasikivu tutafia huko!

  Bless you my brother!

 17. Mbarikiwe wapendwa wenye kuitafuta kweli, Injili ya Kristu ndio msingi wa imani ya Kristu, Hivyo tukisema hakuna utatu mtakatifu basi na ithibitishwe ni wapi wamesema hivyo katika bibiia.
  Naamini ni kwa neema ya Mungu ndiyo twafunuliwa haya, hata Petro aliposema kuwa Yesu ni Masiha (yaani MUNGU) Bwana akamwambia wazi kuwa si yeye aliyelijua hilo ila Baba amemfunulia. Ukiwa na roho wa kweli atakuongoza katika kweli yote Yohana 16:13
  Hebu tujiulize mbona Yesu ni Mungu na bado anaita na anamuomba Baba, hapa ndipo ambapo wakristu tunakataa utatu, tunajikoroga kwa maelezo mengi yasiyo na msaada wa Roho mtakatifu kwa sababu hatuombi masaada wake na kuhisi kuwa akili zetu pekee zinatosha.
  Mtu anasema Mungu ni Nafsi moja pekee imekuaje akazaliwa duniani? Isaya 9:6
  Mwanzo 1:26 Mungu ametumia wingi katika uumbaji, ina maana malaika nao waliumba?
  Kristu aliwaambia mitume huyo roho hawezi kuja mpaka mimi nitakapokwenda kwa baba ina maana kuwa yeye huyohuyo ndiye Roho matakatifu kwa hiyo alikuwa nao kwa nafsi ya Mwana akishawaacha ndipo ataweza kuja tena kwa nafsi ya Roho Mtakatifu. kumbuka alisema nitakuwa nanyi mpaka mwisho wa Dahari.
  Roho mtakatifu ni ana umbo/mwili
  Ukisoma matendo 15:28, Yohana 15:26 Roho mtakatifu anaelezwa kama nafsi, binadamu na msaidizi si upako.
  Roho mtakatifu si upako,
  Upako ni nomino ya kitenzi paka; Hapo mwanzo manabii wlikuwa wakiwateua wafalme kwa kuwapaka mafuta,wakifanya hivyo, Roho mtakatifu alikuwa akiwashukia wafalme na walikuwa wakitabiri na kuonyesha nguvu nyingine za kiungu,Samweli 9:6, 10:10 (Roho mtakatifu ni roho wa Mungu)
  Kwa hiyo neno Upako likawa likitumika kumaanisha nguvu za Mungu
  Roho mtakatifu ni nafsi ya Mungu ambayo huingia ndani mwetu baada ya kumkubali YESU na kutufanya kuwa wana wa Mungu, akiisha kuwa ndani yetu ndio nguvu za Mungu hujidhihirisha japo katika viwango tofauti.
  Hata ubatizo kuna sehemu umelenga nafsi tatu mathayo 28:19, na sehemu nyingine umelenga Yesu pekee, matendo 2:38 hii inamaanisha kuwa watatu hao wote ni sawa na umoja.
  UMOJA WA WATATU (waraka wa kwanza wa Yohana 5:8)
  Ni kwa jinsi gani wamekuws umoja (1timotheo 3:16)
  Hiyo ni siri ya utawa kwa maana si kila nafsi iko tayari kuamini Uweza wa Mungu.(Akili ya kidunia haikubaliani na falsafa ya nafsi tatu 1wakorintho 19,20,21)

 18. Nimecheka mpaka basi,

  Vitu vilivyojaa ndani ya vichwa vya wapendwa wengi anayevijua ni Mungu mwenyewe, maana inatisha kuona ni jinsi gani watu wanamwabudu Mungu wasiyemfahamu sawasawa!

  Kwamba Mungu Baba ndiye muumbaji wa kila kitu chema ( sijui kibaya kiliumbwa na nani), na Mungu Roho mtakatifu yeye ni upako! Duh hii kali sana.

  Na nimegundua kweli msemo wa wasukuma walioendelea kwamba, ukitaka kumficha mswahili kitu, kiweke kwenye maandishi/kitabu.
  Biblia ingekuwa kama gazeti la udaku, watu wangeijua sana!

  Ninaona ni jinsi gani watu biblia huwa hawaisomi, lakini huwa wanadhani wanaielewa, kumbe wanachodhani wanakielewa hawakukisoma kwenye biblia, bali walimsikia mwinjilisti wao anakisema kwenye mimbari, bahati mbaya nae hakukisema sahihi.

  Lakini pia hata kwenye blog kama hii tunapoandika mambo wengine wanadhani huwa tunabishana tu akina Lwembe, Sungura, Siyi na kina Seleli, huwa hawaoni kuwa katika kubishana kwetu kuna mambo ya msingi huwa tunasema, hata kama huwa hatufikii kukubaliana.

  Kwa hiyo hata hayo ya msingi ambayo huwa tunayasema katika huko kubishana kwetu huwa hawayafuatilii. Kama mtu angefuatilia kuhusu suala la utatu angekuwa amejifunza kitu fulani maana tumeliongea huko nyuma.

  Kama hili suala la Mungu ni nani au Mungu yukoje bado ni tatitizo kubwa kiasi hiki, sasa inabidi kujiuliza swali kwamba watu wanapomwamini Yesu wanafundishwa nini kuhusu uungu wa Mungu? Na hao walimu wanaowafundisha wanayatoa wapi hayo wanayowafundisha?

  Kama vipi,tupotezee tu, maana tukifika mbinguni tutajua yote, kama kutokujua kwetu hapa hakusababishi tusifike hata huko mbinguni tusemako tunaenda!!

  Haya!!

 19. The grace of the Lord Jesus Christ, and the love of God, and the communion of the Holy Ghost, be with you all. Amen. -2 Corinthians 13:14 (KJV)

 20. Oh!! dada Jane umeuliza swali zuri sana,mm kwa ufahamu wangu najuwa nakuamini kuwa MUNGU ni mmoja, ila mwenye nafsi tatu, yaani Mungu Baba,Mwana na Rohomtakatifu.Hawa si mungu watatu,bali ni Mungu mmoja…Nafsi ni kitu kilicho ndani mtu,mnyama na kila kitu kiendacho kwa nafsi hai. kwa mfano; mimi naitwa Zephania ndio jina langu linalo nitambulisha kuwa mimi ni mtu,nikiwa kwa wazazi wangu naitwa mwana,lakini bado mimi ni zephania! nikiwa kwa watoto wangu naitwa Baba nayo hainiongezei wingi wa mimi bado nitakuwa mm huyuhuyu zephania, na nikiwa kwa mke naitwa mume,zephania mm huyuhuyu wala hatujawa wa zephania watatu bali ni mm huyohuyo ila kwa nafsi tatu,yaani baba kwa wanangu,mwana kwa wazazi na mme kwa mke.kwa hiyo kwa nafsi ya Mungu kila nafsi ina kazi yake ktka kuukamilisha Uungu wake, .

 21. Asante Mjoli Haule, umeliweka wazi zaidi jambo hili, ninaamini umemsaidia zaidi Vai, kwamba sasa anaweza kujikagua zaidi na kujua kwamba anahitaji kujifunza Neno la Mungu katika UHURU, ili limbadilishe, azaliwe mara ya pili, aionje na furaha yake!

  Gbu!

 22. Dada Lily,
  Naona unanilaumu bure tu, hata ikibidi lawama zako ziwe na uhalali, basi nawe ulipaswa unioneshe angalau Maandiko yaliyokutambulisha kuwepo kwa mambo hayo, vinginevyo tutakuwa tunazungumzia assumptions zetu, ambavyo unaposema niwe serious, Je, tunaweza kum asume Mungu na tukabakia kuwa salama?

  Biblia ndiyo iliyotutambulisha kuwa kuna Mungu, kwahiyo tukitaka kumzungumzia Mungu ni LAZIMA turudi na tu comply na maelezo yake. Mimi nimerudi katika Biblia ili niyatazame hayo aliyoyauliza dada Janeth, niliyoyaona kwa uchache ni kuhusu “Mungu Baba” tu:
  Yn 6:27; 1Cor 8:6; Gal 1:3; Efe 6:23; 2Pet 1:17… na 2Yn 1:3 inayosema, “Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.”

  Sijakiona kifungu chochote kile kinachosema “Mungu Mwana” wala “Mungu Roho Mtakatifu”! Lakini nimeiona Amri inayosema “Usiwe na miungu mingine…”, kutoka maelezo ya Amri hii, na kwa jinsi mleta mada alivyoweka wazi akitaka kujua tofauti zao, ndipo nikajua kuwa hiyo itakuwa ni ile “miungu”, ambayo iko mingi sana, na inajipachikaga jina lolote tu, ambayo kimsingi ni mizimu, maana Mungu yuko mmoja tu, JEHOVA Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo!

  Unaposema ningewapa changamoto ya wao kutupa Maandiko yanayothibitisha kuweko kwa Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu, hilo ni kweli, na ninakushukuru kwa kuileta changamoto hiyo ambayo ninaamini wapendwa waliochangia wameiona, na wachangiaji wengine pia wataliona hili, kama ambavyo nami kwa ushauri wako nimelifanya hilo!

  Ubarikiwe dada yangu!

 23. Dada Lily
  Shalom…

  kama alivyofafanua Lwembe
  kwenye Biblia hakuna maandiko yaneandikwa Mungu baba,Mungu mwana,Mungu Roho Mtakatifu,hii inamaanisha kuna Mungu watatu.Lakini kuna maandiko yameandikwa Mungu Baba Mwana na Roho Mtakatifu kuna thread tumejadili kwa kirefu hapa https://strictlygospel.wordpress.com/2012/02/09/utatu-mtakatifu/.

  Kama bandiko la Br Siyi alivyoandika tuko na waamini wanaomini Mungu ana nafsi tatu na wanaoamini Mungu ana nafsi moja.

  Mimi ni mmoja wanao amini utatu ktk Mungu mmoja,unaweza fatilia hapo juu bandiko langu,baadaye nitaandika maandiko mengine yanayopambanua hizo nafsi na zinzvyotenda kazi kwetu sisi ktk njia hii kuu ya wokovu.
  kama una maswali unaweza kuuliza.

  Karibu

  Mjoli Haule

 24. Du, tafadhari sana ndg CK Lwembe, uwe serious angalau kidogo. Pamoja na kwamba hawakutoa maandiko wachangiaji huwezi andika ulichoandika hapa. Ungewapa changamoto kuweka maandiko kusapot maelezo yao.

 25. Dada Janeth,

  Umenifurahisha sana kwa quiz ya Injili uliyoileta!!

  Umemuumbua mpaka Vai, kumbe hana cha “Shika Neno wala Tenda Neno”, si unaona jinsi alivyo score ZERO! Kumbe kashikilia mizimu na hajui, hahahaha!!!

  Kwa kukujibu quiz yako, “…tofauti iliyopo kati ya Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho mtakatifu”, hili hapa jibu lako:

  1: Mungu Baba ni Jehova

  2: Mungu Mwana ni mzimu

  3: Mungu Roho Mtakatifu pia ni mzimu

  Wapendwa wametiririka na hisia zao tu, maana kwa sehemu hakuna Maandiko kwa hayo uliyoyauliza. Hakuna Andiko linalotuambia uwepo wa Mungu Mwana wala Mungu Roho Mtakatifu, hiyo ni mizimu ya dini tu!!!

  Ubarikiwe!

 26. Naungana na VAI kuhusu ufafanuzi wake Mungu baba ni ndiye muumbaji wa kila kitu. Mungu Mwana ni Yesu Kristo aliezaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mungu Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu Baba tunayoishi nayo hata sisi tukizaliwa upya. ambayo ibilisi anapambana kutuweka mbali nayo

 27. Hongera Janet kwa kutafuta ufahamu!
  Mungu baba ndiye Muuumbaji wa kila kitu chema, Mungu mwana ni Yesu au NENO na Mungu Roho Mtakatifu ni Ule upako au nguvu ya Mungu iliyomo ndani yake inayotenda kazi ndani ya wana wa Mungu

 28. Sr Janeth mari…….tafakari haya maandiko…..RM akupe hekima ya kuelewa,Baadaya nitakongezea maandiko mengine.

  Amen

  Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.

  1.4-8 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, ZITOKAZO kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na ZITOKAZO kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;

  tena ZITOKAZO kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,

  na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.

  Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

  Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

 29. Hii ni mada tete sana ndg yangu. Kuna watu wanaamini umoja (unitarianism) na wale wa utatu (tritarianism). Mimi nikutie moyo usome vizuri Biblia yako. Utaelewa tu. Maana Mungu ni Roho. Mungu ndiye Neno aliyefanya vyote! Halafu kuna another Confoter!!! Jitahidi ufahamu mambo haya vizuri.

 30. Swali zuri hapa ni kuuliza umoja uliopo katika utatu mtakatifu, Wote watatu ni Mungu mmoja, kazi zao ndizo zinazowabainisha. Mimi nitakueleza hivi kwa ufupi, Mungu Baba ndiye anayeshughulika moja kwa moja na wanaisraeli na ulimwengu kwa jumla. lnjili ni ya Mungu mwana anayejitambulisha kwa wakati wake. Kuanzia mitume ni enzi ya Mungu Roho Mtakatifu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s