Yesu asema na John Mulinde!

mulindejohn

Bwana asifiwe wapendwa

Nawasalimu nyote kwa Jina la Yesu Kristu.

Naombeni mkipata nafasi msikilize huyu mtumishi wa Mungu kutoka Uganda anaitwa John Mulinde

“After working in the power of the Holy Ghost and seeing signs, wonders and miracles, JOHN MULINDE was an Evangelist fully sure of his Salvation. But when JESUS revealed himself to him, he was shocked of what he was told.”

Mungu alimonyesha maisha yake ya ndani na kwa uhakika alimwambia kuwa kama angerudi wakati ule anauhakika angebaki.

Sikiliza mtu wa Mungu na Bwana atusaidie. tumuombe atupatie Roho ya Toba na tumuangalie yeye katika maisha yetu. tumuombe atufunulie siri za Neno lake ili tumjue yeye aliyetupenda hata akamtoa Mwanae Yesu ili aturudishe kwake

Kama Daudi alisema ‘funua macho yangu nione uzuri wa maneno yako’ 

Utakatifu ndo tunatakiwa kukimbizana nao maana bila huo hatutaweza kumuona Bwana. na hatutaweza kwa nguvu zetu wenyewe ndo maana Yesu akatuahidi Roho wa Mungu ili akae ndani yetu na atuongoze. 

Naomba nisiseme sana, niwaache msikilize halafu basi mtaleta maoni yenu tuweze kujengana.

Kama ukishindwa kufungua hiyo link basi nenda youtube na u-type 

 

shocking message from Jesus to John Mulinde. imepandikwa na Yves YN Nahishakiye

Mubarikiwe wapendwa.

-CM
Advertisements

5 thoughts on “Yesu asema na John Mulinde!

 1. Na nukuu Kitabu cha Yohana 14

  ” MTU AKINIPENDA ATAZISHIKA AMRI ZANGU NAMI NITAKUJA NA KUJIDHIHIRISHA KWAKE ”

  Muogopeni sana Mungu yupo pia atarudi
  ujio wake unaanza kunukia…

 2. oooh God nimesikiliza kwakweli nahitaji kutengeneza tena sana tu. ubarikiwe mtumishi wa Mungu. ahsante kwa aliyeweka clip hii.

 3. Samahani CM nilisahau hata kukushukuru kwa kutuwekea hii clip, Mungu akubariki sana

 4. Nimetazama pia clip yote, nachoweza kusema sijapata kwakweli kukutana na mafundisho yanayogusa ya namna hii. Huyu mtumishi wa Mungu kwakweli namwombea ili Mungu azidi kumtia nguvu ili atakapomaliza safari yake ya hapa duniani basi aingie mbinguni. Kama alivyosema Lily hapo juu hata mimi naombeni jamani tuitazame hii clip, ni ndefu lakini ukimaliza mpaka mwisho ndio utagundua ni wapi umesimama katika kutimiza mapenzi ya Mungu. Binafsi nimejiona kwakweli sifai kabisa mbele za Mungu na nahitaji toba tena ya nguvu, na ukimsikiliza wala huitaji macho ya rohoni (kama ambavyo nasikiaga watu wengi wakisema kuwa tunahitaji macho ya rohoni) kuelewa kile anachoongea na kujua kuwa kweli anamtumikia Mungu wa kweli. sijawahi kupata bahati ya kusikia mtumishi yoyote akijiongelea tena kwa unyenyekevu mkubwa kama ambavyo nimemsikia huyu, huenda wapo lakini kama nilivyosema sijawahi kupata bahati ya kuwasikia. Hebu iangalieni jamani itawabarikini sana

 5. Nimetazama clip nzima kwa kweli nimebarikiwa sana na experience na mafundisho ya ngd John Mulinde. Kiwango cha Mungu cha utakatifu ni cha juu sana, iam deeply humbled and brocken in my heart. I need to repent again and watch my ways. Ukiweza tazama pia clip hii hakika utabarikiwa. Asante CM

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s