Kanisa la T.A.G kuanzisha benki!

mtokambalii

Askofu Mkuu Barnabas Mtokambali wa T.A.G kulia akiwa na Byron D. Klaus

rais wa Assemblies Of God Theological Seminary, Marekani

Na Asha Bani

KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) lipo katika mchakato wa kuzungumza na wasomi ili kuanzisha benki yao.

Hayo yalielezwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Barnabas Mtokambali, wakati akizindua jengo jipya la Kituo cha Uamsho na Umisheni lililopo Msasani.

Mtokambali alisema haiwezekani wakakosa wasomi wenye mioyo ya kusaidia kanisa hilo kuanzisha benki, hospitali na chuo kikuu.

“Sisi tuna uwezo wa kuanzisha chuo kikuu kupita hata kile cha Dodoma na hospitali kupita ile ya KCMC na jambo hili linawezekana kabisa kama kutakuwa na lengo na nia katika hilo,” alisema Mtokambali.

Askofu huyo alisema si vema nyumba za ibada kutumika kwa kufanya biashara na mambo ya siasa.

Mchungaji wa kanisa hilo Mashariki Kaskazini, Samson Swila, alisema jengo hilo limegharimu sh milioni 146 hadi kukamilika kwake, na kuongeza kuwa wamekabiliana na vikwazo vingi lakini Mungu aliwasimamia.

Source : Tanzania Daima.

Advertisements

3 thoughts on “Kanisa la T.A.G kuanzisha benki!

  1. Mungu awabariki viongozi wetu kwa maono makubwa naamini tutaweza na hapo tutakuwa tumeifikia jamii kwa kiwango kikubwa sana.

  2. NI MATARAJIO YETU KUFIKA TULIPOKUSUDIA ILA KILA JAMBO LINAWAKATI WAKE KUEPUSHA DROP OUT YA MAONO KWA MSAADA WA BWANA TUTATENDA MAKUU
    PASTOR THOBIASI MOSHA
    MPONDA TAG CHURCH

  3. Tunamshukuru Mungu kwa hatua kubwa. Songeni mbele kwa kuwekeza kwenye social institutions km mabenk, shule, vyuo nk nk. Hapo tutawahudumia watu kikamilifu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s