Kumtumikia Mungu!

huduma

Tunaweza kujengana kwa Uhakika kabisa Kibiblia, Kiu-Uzoefu wako, Ki-Ushuhuda wako/mwingine, Ki-Ushauri nasaha wa Kiroho na kiuhalisia, Kiufunuo na kwa njia yoyote njema na iliyo sahahi KiMungu kuhusu maswali haya: • Kumtumikia Mungu ni kitu gani? • Ili Mtu aonekane/ajue/aambiewe anamtumkia Mungu , ni mpaka awe anafanya nini? • Unaposema naende Kumtumikia Mungu wakati ulishaokoka mwezi uliyopita, mwaka,miaka, manake nini?

Je kabla ya hapo ulikua hautumiki? • ILI MTU ASEME KWA UHAKIKA KUA MUNGU AMEMUITA KTK UTUMISHI KISHA AFANYE MAAMUZI YA KUANZA/KUONDOKA/KUUENDEA UTUMISHI/MWITO HUO WA UTUMISHI, NI MPAKA IWEJE/KUTOKEE NINI? sauti, msukumo, Mtumishi wa Mungu kukuambia una kitu, kuota ndoto, kukwama kwa mambo fulani yako binafsi, hamu ya kila mara ya kufanya mambo ya Mungu? Ni nini hicho hasa ambacho kwa hakika, UNAJUA KWELI UMEITWA NA UNG’OKE KWENDA SHAMBANI? 

–Seleli

Advertisements

8 thoughts on “Kumtumikia Mungu!

 1. Amina Kaka Edwin. Sifa na utukufu kwa Mungu! Tumtumikie Mungu kwa uaminifu popote pale tulipo huku tukiendelea kujifunza njia zake.

 2. Patrick and all,

  Amazing indeed the way you have replied! Majibu mema, ya kina, yenye mafuta, ya ufahamu wa hali ya juu, hakika nimeshiba na kujengwa in Jesus name, amen. Glory to God and I appreciate sana kwa efforts zenu, fantastic indeed.

  Press on

 3. Edwin my dear brother, uzidi kubarikiwa na Bwana Yesu.

  Unfortunately maswali yako karibu yote ya nyongeza hayana jibu moja tu, yako very subjective. What do I mean? Simply this, nitakavyousikia wito wa Mungu mimi sivyo utakavyousikia wewe.

  Throughout the Bible Mungu aliwaita watu in many different ways, no copying and pasting hapo. Alivyoitwa Musa, sivyo alivyoitwa Samweli na sivyo alivyoitwa Daudi, wala sivyo alivyoitwa Elisha, na Eliya hatuambiwi aliitwaje. Bwana Yesu alivyowaita wanafunzi wake pia tofauti, wengine waliitwa wakiwa wanatengeneza nyavu zao za uvuvi, mwingine mtoza ushuru, Paulo naye aliitwa kitofauti kabisa and in very dramatic fashion if you will.

  Sasa basi utaona kuwa hakuna one size fits all ya kuitwa, hivyo hatuwezi kuweka formula ya kuitwa, as in “utajisikia hivi, utajihisi hivi na hiki na hiki kitatokea”, that won’t work kwani we are all different and God deals with us individually, ila wewe uliyeitwa you will know umeitwa labda ujibaraguze tu na kutafuta “proof” ya kutokuitwa kwako which would be non-existent kama umeitwa, kwani Roho Mt. atahakikisha unamuelewa vizuri tu – God knows how to communicate with you in a way that you will know exactly what He is telling you.

  Watu wengine wakiongozwa na Roho Mtakatifu wanaweza kutumika ku-confirm wito wake but by the same token wengine wakiongozwa na wanachokiona kwa macho yao wanaweza kukukatisha tamaa na kukuambiwa hujaitwa kwa huduma ambayo wewe ndani mwako unajua umeitiwa. It then comes down to a question of boldness, utakuwa na ujasiri wa kumsikiliza na kumtii Roho wa Mungu ndani yako au utanywea na kuwatii wanadamu huku ukisononeka moyoni na kuwalaumu “kimoyomoyo” kwa kukuzuia huduma fulani wakati the real issue was, you let the fear of man stand between you and your call? Only you can tell!

  Hofu ya mwanadamu imepelekea wengine kuishia kuitika wito wa wanadamu na kufanya huduma walizopangiwa na wanadamu. Matokeo yake wanakosa amani katika huduma hizo, wanazifanya kwa shingo upande au kinafiki wakitaka kuonyesha kuwapendeza wale waliowapa hizo huduma lakini ndani kabisa wanajua hawajaitwa kufanya wanachokifanya. What a miserable thing that is…Dada Gladys ameiweka vizuri kuwa ni “option” siyo “major” ambayo Mungu aliyokuitia kuifanya. Labda niseme kuna tofauti kati ya “training” na kupachikiwa huduma. Ukizoea kuandikiwa cha kuhubiri sidhani kama utaweza ku-develop discipline ya kuwa na fellowship na Roho Mtakatifu akuambie yeye cha kusema. Matokeo yake unakuwa extension ya yule anayekuandikia cha kuhubiri, in other words unakuwa kipaza sauti chake, see the problem in the long run there?

  Kwa habari ya kuacha kazi yako ya kukuletea mkate wa kila siku, hilo Mungu akuongoze, usijiachie tu na kukurupuka. Atakuongozaje? Anaweza kukupatia provision ambayo ita-replace kipato chako na kukupa amani ya kuacha hiyo kazi ili ufanye anachokuita kufanya 24/7 kwa kukufungulia milango mfululizo ya huduma na provision kwa ajili ya huduma hizo au pia anaweza kukutaka uchukue hatua ya imani na atakutana nawe utakapofanya hivyo…all in all He will make it clear for you.

  Vilevile, ni vizuri tuanze kwa kufuata mfano wa Mtume Paulo alihudumu na kushona mahema at the same time and look how much he accomplished for Christ and the Gospel? More than all the other apostles put together and he says so himself, hivyo kigezo cha kufanya kazi ya kawaida na kuhudumu siyo kisingizio cha huduma kupwaya…

  Tuendelee kujifunza…

  Patrick

 4. Seleli mpendwa,

  Naomba ni jump in km mpita njia.

  Huu ni ufahamu wangu na wala sibebi ufahamu wa mtu mwingine.
  lakini ndani yake yawezekana kwa hakika ukapata majibu sahihi kwa swali au maswali yako.

  Kwa ujumla wake AMPAYE MTU NEEMA YA WOKOVU NI MUNGU BABA.
  ANAYEOKOA NA KUMPA MTU IDENTITY MPYA NI BWANA YESU.
  NA AMPAYE MTU HUDUMA (ofisi/ajira shambani mwa BWANA), KARAMA, VIPAWA MATUNDA YA ROHO(vitendea kazi shambani) NI ROHO MTAKATIFU.

  kwa kuwa tumekuwa wavivu sana kumtafuta Mungu, ndio sababu tunafanya huduma kwa hisia.

  Wapendwa tusipotaka kukaa chini na kumtafuta Mungu ili RM atupe ajira kwa namna ya qualification ZAKE juu yetu, tutajikuta tumetumika sana lakini mwisho wa siku kwenye kutoa hesabu una ZERO kwa sbb ulifanya OPTION badala ya MAJOR.

  Nilikuwa napita tu,

  Sr Gladys

 5. Patrick my brother,

  Ubarikiwe sana kwa majibu yako,

  Kuna mambo napenda kuendelea kupata na kwa humble signature yako kila mara unayomalizaga nayo ktk posts/inputs zako ya ..’’Tuendelee Kujifunza’’ hence yafuatayo tuendelee kuyaangalia kidogo.

  JIBU LAKO: Ukiwa umeitwa kufanya huduma fulani utajihisi unavutwa/Msukumo upande huo wa huduma hiyo na Wapendwa watathibitisha kwa kukuambia

  MASWALI NYONGEZA:

  (a) Huko kuvutwa, unasikia nini hasa?

  (b) Kuvutwa uko kunatofautianaje na ile hamu tu ya kawaida ya kupenda kufanya jambo/huduma ya kiroho labda kwa sababu ni kati ya vitu unapenda-spiritual hobbies if you know me?

  (c) Tunatofautishaje kuvutwa na huduma ambako kumetokana na kupangiwa ufanye huduma/shughuli fulani kanisani na nje na kwa kua umeifanya sana, say kuimbisha pambio or P& W au kufundisha kwa kua hakuna wakujitolea, na wewe kwa kujisukuma na kujitia moyo na hata kwa kuandaliwa notes then ukawa unafundisha /imba kila mara kwa muda mpaka
  sasa ukaanza kuvutiwa/ikawa kama sehemu ya zamu/maisha yako?

  JIBU LAKO: Utakuwa na upako wa kuifanya huduma hiyo

  SWALI LA NYONGEZA: Kwa upako, u mean uthihirisho wa nguvu za Mungu mara usimamapo kuifanya iyo huduma au uwezeshwaji wa ajabu unakupa umaridadi/u-smart/ubora na uzuri sana unapofanya icho kitu?

  JIBU LAKO: Wengine wataiona neema iliyoko juu yako kwa ajili ya huduma hiyo

  SWALI LA NYONGEZA: Kwa kuona neema juu yangu, Wataona nini hasa hicho mpaka wajue/wasema huyu Mtu ana hiki kwa kweli?

  JIBU LAKO: Kama Mungu amekuagiza uache kazi yako basi ni heri kumtii Yeye kwani anajua atakutunzaje.

  MASWALI LA NYONGEZA:

  (a) Kwa kua hili limeleta shida kubwa na kusababisha Watumishi kadhaa kujiudhuru Utumishi, wengine wake zao kughairi kuendeea kuwa-join Waume zao maana maisha magumu mno, hakuna pesa za kumtunza na familia,MTU ANAONGOZWAJE KUACHA KABISA KAZI YAKE…hata kwa msukumo tu au in this critical issue, bora strictly asiache mpaka asikie Sauti kabisa ya RM ndani au ya nje?

  (b) Vipi akiacha tu BILA uongozi huo normal-Msukumo au extra-ordinary-Sauti ndani/nje kwa sababu ya nia njema tu ya kuwa na muda wote kwa Bwana na altar maana si rahisi kuwatumikia ma Bwana 2 fully and efficiently, kuna soo?

  (c) Ukishakua na kanisa kubwa/huduma kubwa inayoweza kukutunza kwa kila kitu, kuna haja ya kutafuta uongozi wa Mungu kuacha kazi au ni mara moja wewe kama Mtu kabisa kuamua tu simple namna iyo kuacha?

  JIBU LAKO: Mungu anaweza kuwatumia wengine kukuthibitishia mwito wako lakini LAZIMA yale kutoka kwa Watu yawe yanathibitisha ulichonacho/unachojua

  MASWALI LA NYONGEZA

  (a) Ivi Ni lazima sana kua Watu watakuambia kile UNACHOJUA unacho ukilinganisha na fact hii kua Wafalme/Manabii/Waamuzi walingizwa hudumani, baadhi yao wakiwa hawana hata habari, wakichunga tu
  kondoo-Daudi, wengine Kiurithi-Selemani toka kwa Daudi, Wengine wakiwa wamejaa hasira wakipura nafaka hata na kuongea mbovu-Malalamiko/Manung’uniko wakati Mungu(Malaika) anataka kuwaingiza kwa huduma -Gideon?

  (b) Vipi ukiingizwa huduma kwa Mchungaji wako kwa kukupaka Mafuta kwa ajili ya huduma na kukuambia kuanzia leo, Utafanya hiki na kile na wewe ukatii na kuchukua hatua ya kwenda porini uko au kuanza huduma iyo kanisani au pembeni ya Jiji kama tawi la kanisa lake/lenu/la Yesu, kuna tatizo mbele uko au peace tu na ni tuendelee kuchapa kazi?

  (c) Na je ukiingizwa hudumani kwa maamuzi/maono/anavyokufahamu Mchungaji wako, itahesabika kwa Mungu ni sawa, na Ni Mungu amekuingiza na una haki/full confidence ya kujiita mimi ni Mtumishi wa Mungu au kuna hatari wa kuchapa mzigo kwa miaka 20 only later to realize uliingizwa na Pastor wako si Mungu?

  JIBU LAKO: Wapendwa waliokuzunguka wanakupa shuhuda za jinsi wanavyobarikiwa kila unapohudumu ukawa bado ujiamini/haukubali/unasita, baadaye ukakutana na watu wa Mungu ambao wala hamfahamiani na kila mmoja wao akakuambia maneno ya kukuambia icho ulichonacho/walichosema wanaokufahamu

  SWALI LA NYONGEZA:

  (a) Hakuna uwezekano Wapendwa wanaokufahamu kusema maneno hayo mema kwa kua tu basi wanabarikiwa na si kwamba Wanatumiwa na Bwana kukuambia mwito/huduma yaani Mpendwa amefurahia tu kile unachotoa kitamu na cha ukweli?

  (b) Au kuondoa risk iyo ni bora kama ulivyosema, ithibitike na wengine hata wasiokufahamu, wakafunuliwa pia?

  (c) Na hii ya Wapendwa wanaokujua na wasiokujua kusema icho icho,inaweza tosha Mhusika kufanya maamuzi na kuanza/kuingia hudumani bila sauti specific ya RM?

  Press on Tuendelee Kujifunza,

  Edwin Seleli

 6. Edwin ndugu yangu,

  Kumtumikia Mungu kwa kifupi kabisa ni kumtii kwa kufanya kile ambacho anakuagiza ukifanye kwa ajili yake.

  Ili isemekane kuwa unamtumkia Mungu inabidi kuwepo na mambo mawili, kwanza wewe mwenyewe uwe na uhakika kuwa Mungu amekuita na kukuagiza kufanya huduma fulani na la pili watakatifu wengine waliokuzunguka wathibitishe wito huo. Mfano: Ukiwa umeitwa kufanya huduma fulani utajihisi unavutwa upande huo wa huduma hiyo na utakuwa na upako wa kuifanya huduma hiyo na wengine wataiona neema iliyoko juu yako kwa ajili ya huduma hiyo na kuthibitisha ya kuwa kweli Mungu amekuita kufanya huduma hiyo unayoifanya.

  Kama unavyofahamu, the general idea tuliyonayo wengi ni hii: Kumtumikia Mungu kunamaanisha kuacha whatever secular job you are doing na kuingia kwenye tunachokiita “full time” ministry. Mfano, unajisikia wito wa kuwa mchungaji au mwinjilisti halafu unaacha kazi yako ya kukuletea mkate wako wa kila siku na kwenda kuanzisha Kanisa au huduma. Kwa maoni yangu huu ni mtazamo finyu wa maana halisi ya kumtumikia Mungu. Kama Mungu hajakuongoza kuacha kazi yako ya kawaida ili uende kumtumikia unajitafutia adha isiyo na sababu ila kama Mungu amekuagiza uache kazi yako basi ni heri kumtii Yeye kwani anajua atakutunzaje.

  Nadhani kitendo cha kusema unakwenda kumtumikia Mungu wakati ulishaokoka muda mrefu tu uliopita hakimaanishi kuwa ulikuwa humtumikii, nionavyo mimi ni lugha iliyozoeleka kuelezea “level au involvement ” ya mtu katika huduma. Mfano mtu anaweza kuwa na taaluma fulani let’s say Mhandisi na wakati huo huo ana huduma ya Uinjilisti, sasa akiongozwa na Mungu kuacha kazi yake ya taaluma aliyosomea na badala yake kujikita katika kuihubiri Injili hapo wengi tunasema amekwenda “kumtumikia Mungu”. Lakini ukweli ni kwamba amekuwa akimtumikia Mungu all along, ni kwamba tu ameendelea mbele na kuzidi kumtumikia Mungu, yaani involvement yake katika huduma imekuwa kubwa zaidi kuliko hapo awali kwani ametoa muda wake wote ambao angeweza kuwa anafanya kazi au biashara ya kumletea kipato ili aweze kuitikia wito wa kuhudumu.

  Ili uweze kusema kwa uhakika kabisa ya kuwa umeitwa kwenye huduma, kama nilivyotangulia kusema, Mungu atakuonyesha wewe mwenyewe anataka umtumikie vipi na wapi halafu watakatifu wengine watatumika kuthibitisha huduma ilyomo ndani yako.Kila jambo litasimama kwa ushuhuda wa wawili au watatu. Vilevile Roho Mt. anaweza kuwafunulia wengine wakaja kukupa confirmation kuhusu huduma uliyoitwa kwa njia ya neno la kinabii, notice unabii wa kweli always utathibitisha kile ambacho tayari unakifahamu rohoni mwako kwa habari ya huduma uliyoitiwa, usipothibitisha hilo basi unabii huo uweke pembeni, halafu msikilize vizuri Roho Mtakatifu,

  Roho Mtakatifu anajua namna ya kuongea na kila mmoja wetu ili tumwelewe vizuri, wengine kwa ndoto, wengine maono, wengine msukumo tu unatosha, ila akitumia watu wengine mara nyingi ni kwa ajili ya kututhibitishia kuwa kweli tumemsikia yeye. Mfano unaweza kumsikia Roho Mt. akikuambia ndani mwako kuwa amekuita kwa huduma fulani specific let’s say ya Ualimu, wewe ukaona ahh hii haiwezekani, ni mawazo yangu tu au ni mimi mwenyewe tu naipenda hii huduma ndio maana nahisi hivyo ukapuuzia hilo halafu muda si mrefu wapendwa waliokuzunguka wanakupa shuhuda za jinsi wanavyobarikiwa kila unapofundisha bado ukawa hujatilia maanani baadaye ukakutana na watu wa Mungu ambao wala hamfahamiani na kila mmoja wao akakuambia maneno kamai: “Una huduma ya ualimu ndani yako” au “Mungu amekuita kufundisha Neno lake” au “nimeona maono umeshika chaki unafundisha darasani” n.k. Hiyo sasa inakuwa ni uthibitisho kwako kuwa umeitwa kumtumikia Mungu katika huduma ya Ualimu.

  Tuendelee kujifunza

  Blessings,

  Ndimi nduguyo,

  Patrick.

 7. kwanza ni vema ndugu yangu kujua kati ya Mungu na mwanadamu nani anamtumikia mwingine. ukipata jibu hilo unaweza pia kupata jibu la nini maana ya kuwa mtumishi wa Mungu na nani mtumishi. kwa ujumla madai hayo yana maana kubwa yaani kuwa na wito maalumu kwa huduma maalum. hii ina maana hasa ya kutengwa kwa ajili ya kazi fulani maalum. bila shaka waliotengwa hivyo twaweza kusema kuwa ni watumishi wa Mungu na hapa istafsiriwe kuwa wengine siyo ila wito wao maalumu una madai maalumu pia kwa njia hiyo tuna haki yayaa kuwaita hivyo

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s