Maji ya Baraka kibiblia!!

maji

Bwana Yesu asifiwe, naomba kufahamishwa kuhusu Maji ya baraka,nimekuwa nikiona sehemu mbalimbali na baadhi ya makanisa yakitumia huduma hii ya maji ya baraka,,swali langu ni jee ni sahihi kutumia huduma hiyo au inaendana kinyume na maandiko matakatifu?,nitashukuru iwapo nitapatiwa majibu kutoka mistari ya biblia. Amen

–Daniel Geoffrey Pyuza

Advertisements

8 thoughts on “Maji ya Baraka kibiblia!!

 1. Ndg wasoma.Naomba muelewe kuwa Biblia inasehemu kuu 2,(1),Agano la kale (mwanzo-malaki),linahusu wayahudi tu,ni agano la Mungu kwa wayahudi watakavyo toka MISRI kwenda KANAANI,wakati huo wanaongozwa na WINGU,NA NGUZO YA MOTO.Hawa kuongozwa na Roho Mtakatifu.(hakuwepo duniani).(2),Agano Jipya,linahusu watu wa mataifa au (kanisa),ili watoke DUNIANI hadi MBINGUNI.Tuko njia 2 tofauti ,hatuongozwi na wingu,nguzo ya moto,musa,yoshua,wafalme,nk,tunaongozwa na Roho Mtakatifu.Agano jipya hatuna haja ya maji,mafuta,udongo,chumvi,sabuni,nk kila ibada huo ni uongo na udanganyifu.YESU ndo maji ya uzima,acha kudanganywa,na kudanganya.By pst Jackson.

 2. Shalom.Kumbuka biblia ni kitabu kipana sana! pia tutaondoka duniani bila kukimaliza! kwahiyo mtumishi yeyote akiitwa na mungu kumtumikia huwa anatii agizo la Yesu matayo 28:19-20.Inabidi tufanye aliyotuagiza.Siyo tunayotaka sisi.Kutumia maji,mafuta,udongo,chumvi nk,si kosa likitokea kama UFUNUO,wa hapo kwa hapo,siyo endelevu.Eliya,Jacob,Elisha hata Yesu,walitumi miujiza hiyo mara moja,siyoendelevu.Kazi endelevu ni Neno la Mungu,na Maombi tu.By Jackson.

 3. Kuna watu wengi wamekuwa wanauliza maswali mengi sana juu ya kutumia maji yaliyobarikiwa au yanavyojulikana kwa wengi maji ya Baraka katika makanisa yetu kama ni sawa kulingana na maandiko au siyo sawa.Tatizo kubwa la watu wengi wanaangalia sana jambo hili kama watu wa kawaida .Katika maisha ya mtu aliyeokoka kitu kikubwa kinachotenda kazi imani.Neno la Mungu katika waraka wa waebrania 11:6 inasema pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.Ingawa haikuandikwa moja kwa moja katika biblia katika biblia ni sahihi kabisa kwa mtu aliyeokoka au mkristo kutumia maji ya Baraka kwa ajili ya huduma iwapo anaamini kile kilichofanyika katika maji haya.Mara nyingi maji ya Baraka ni maji yaliyobeba maombi ya Baraka.hili lisikushangaze sana jambo hili lilikuja kutokana na watu kupata kufunuliwa ni kama vile Yesu alivyotumia matope katika huduma yake kumponya kipofu,Nabii Elisha alivyotumia chumvi kuponya maji yenye mapooza katika 2 falme 19-22.Pia nikama Yakobo alivyotumia miti yenye mabakamabaka akaweka kwenye mabirika ya kunyweshea mifugo ili wale kondoo,mbuzi na ngombe aliokuwa anawachunga wakija kunywa wazae watoto wenyenye mabaka mbaka baada ya kuwa amekubaliana na Rabani mkwewe kuwa huo ndiyo utakuwa mshahara wake sawa na mwanzo 30:37-42.Yote yanawezekana kwa mtu mwenye imani.

 4. Nashukuru sana kwa majibu ambayo kwa kiasi kikubwa nimeyaelewa vizuri,nashukuru pia kuwepo kwa blog hii ambayo imeweza kutupatia majibu ya baadhi ya maswali ambayo yanatutatiza. asante sana MJ,N,Siyi, alexander kapinga na NSHIMIRIMANA Emmanuel. Mungu awabariki sana.
  Daniel Geoffrey Pyuza

 5. Maji yana conotations nyingi sana ndani ya Biblia. Kimsing, tangu mwanzo maji yalitumika kwa namna nyingi sana. Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na; Kusafisha, lawi 14:8-9, Hes. 8:7, Ezek. 16:4, Efes. 5:26, Ebr 10:22, Kutakasa, Kutok 29:4, Lawi 11:32, 1Falm 18:33-34, Yoh. 2:6, Ebr 9:19 na Kuponya, 2falm 5:14, Yoh 5:4 n.k
  Baada ya Yesu kwenda mbinguni, huduma ya kutumia maji hufanyika kwenye maeneo kama mawili hivi niyajuayo mimi. Kwanza ni katika hali ya kutawadhana miguu wakati wa kula pasaka kama ukumbusho wa ukombozi wetu. Jambo hili huwa siyo la kimiujiza ni jambo la kawaida. Yanayotumika ni maji ya bomba tu ya kawaida.
  Na pili, maji hutumika kwenye malango ya kikatholiki. Watu/Makasisi walikuwa wakinyunyiza, majia kwenye mapazia wakati wa kuingia ndani. Utaraibu huu ulikuwa ni mbadala wa ule uliokuwa ukifanya kuadhimisha sherehe za mwezi mpya. Hayo ni kwa mujibu wa Canon pg 65, Council of Constantinople (691) na Catholic Encyclopedia, wanaotumia maji kwa sasa, ni mwendelezo wa kile kilichokuwa kikifanya kipindi cha karne 9. Mpaka leo, hakuna sehemu hata punje ambao mitume walitumia maji ya bakuli au chupa kuponya watu tofauti na ubatizo wa maji mengi. Matumizi haya ya maji kwa kanisa katholiki, siyo wa kibiblia. Kuendelea kutumia maji ya kibakuli au chupa, ni kuendeleza upagani wa Roma.
  Damu ya Yesu inatosha kutosha dhambi na udhalimu wetu wote. Ukiona watu wanatumia maji, mafuta , vitambaa au pete jua huo ni uchawi tu kwa vazi la Kristo. Changamka

 6. huduma siyo kibiblia, ni watu wameunda tu kulingana na mawazo yawo tu.
  Biblia inaeleza kwamba maji ni harama ya Roho Mtakatifu, na tunajuwa njia zake za kufanya kazi ndani yetu, biblia iko wazi kabisa ni viziri kuyisoma na kukubari kufundisha ili tufanye huduma sawasawa na neno la Mungu.
  Wapendwa , Mungu wa mbinguni atupe hekima kulingana na neema yake.
  Mubarikiwe wote

 7. kila huduma tunayoifanya ni lazima iwe na mwanzo wake kibiblia. katika biblia maji yametumika tu katika kubatiza napo hutumika kutangaza mauti ya kristo na pia kama ishara ya kuzikwa na kufufuka pamoja na kristo. Na hili ni jambo ambalo ni lazima tulifanye kwani ni mojawapo ya agizo la Yesu kwa kanisa pamoja na lile la meza ya Bwana.
  katika biblia agano la kale Mungu anazundumza habari za baraka katika kitabu cha kumbukumbu la torati sura ya 28. hapo hatuoni hata sehemu moja maji yanapotumika kama kibeba baraka za Mungu. pia agano jipya sioni hata sehemu moja yesu aliposema mkabariki maji alafu zile baraka zilizokwenye maji ndio zitawajia hapana. kutumia maji ya baraka hakupo kwenye biblia na hivyo ni imani potovu sawa na imani za kutumia vitambaa, mafuta, sabuni, udongo na takataka zingine kama hizo. haijalishi anayetumia ni mkubwa kiasi gami lakini hiyo ni imani ya kishetani ambayo ni sawa na anayevaa irizi au anayekwenda kwa mganga wa kienyeji na kupewa mizizi na tunguli akaziweke nyumbani kwake eti zimpe ulinzi huo ni upotovu mkubwa na wafanyao hayo ni wa baba yao ibilisi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s