Dhambi zote ni Sawa mbele za Mungu?

viwango

Bwana Yesu asifiwe, Kuna mahali nilisoma kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo kwa Mungu, ninaomba msaada wana SG, je ni kweli? aliyeua na aliyezini wote wanahesabika ni dhambi moja? naomba mistari ya Biblia

Nashukuru

–PJ

Advertisements

112 thoughts on “Dhambi zote ni Sawa mbele za Mungu?

 1. Mpendwa Lwembe,

  Do not panic Lwembe, my friend! Come down and feel free!
  Hivi Lwembe, kuwa hojaless inakuleta hofu kiwango hiki? Tulia bwana, uko hapa Nyumbani mwa Bwana. Soma kwanza hapa “Mathayo 11:30”, pengine utatiwa nguvu. Hujue kama hiyo ukosefu ndani ya hoja zako ndiyo inakuleta kuelewa Neno la Mungu?
  Hebu tulia na utafakari kama hizo swali zangu hata ikizibandika kwenye barabara, mitaa na popote, kama zinalenga ugomvi!!!!
  Acha tena nipaste hapa:
  “Sasa jibu na wewe hata kwa sehemu : “Wapi katika agano jipya wanaposema kama dhambi ya uzinzi haisamehewi?”, “Wewe unafikiri kwa sababu gani watoto wamoja wa Mungu walipigwa mawe na wengine hapana, wote wakiwa wamefumaniwa wakizini?”, “Wapi katika agano jipya waumini walifundishwa dhambi kupitia agano la kale?”.”
  Lwembe unaweza onyesha ugomvi katika swali hizi? Na kama umekosa jibu si uwe mkweli kaka yangu? Hakuna atakaekucheka. Ile unayobandika kama “jibu” ukiisha kiri udhaifu na kuogopa, unafikiri ina maana?
  Kwa nini uliposwali mara nyingi ukitafuta upewe wapi agano jipya linafundisha dhambi ya uzinzi, mimi sikuiona kama ugomvi? Toka huko uliko ni pabaya, usiendelee tetemeka.

  Kuchelewa kujibu siyo tatizo. Sote ni hivo tu. Pengine utakayoandika utangoja 2 weeks bila jibu!!!

  Tuingie basi katika uchambuzi wa kauli yako.

  Unaimba kufundisha “dhambi ya uzinzi” na bado kufahamu dhambi ni nini. Ndugu yangu, usijifanye kiziwi, sikiliza. Dhambi ni kila ukeukaji wa maagizo/sheria za Mungu. No derogation for sins!!! Dhambi ni dhambi na adhabu yake ni moja kwa wote wanaoitenda. Lakini wewe nakuona ukiiwazia kama crimes aiganst humanity ambapo wanaweka watetezi wa kutetea mwenye makosa, na kuweka derogation kwa wale wanaoshikilia vyeo vikubwa vikubwa.
  Wapi ulitosha sheria kwamba mpakaliwa wa Mungu haadhibiwe kama wengine akitenda dhambi kama ya wengine? Hujue kama dhambi ya mpakaliwa inaambukiza anaowaongoza? Kwa nini unataka wafunika hawo wapakaliwa, na kwa leo utafunika wanani? Ni wale walimu wako unaowataja kila leo?

  Ukifika kwa agano jipya ambalo ni kamilifu kuliko la kale ndipo unabandika hii “””Deut 22:22 ” If a man be found lying with a woman married to an husband, they shall both of them die, …””””
  Swali ni pale pale: Je hii shairi unayoleta inampa mpakaliwa wa Mungu akiwa mwanaume au mwanamke kutenda kinyume ya sheria bila kupata adhabu ambayo ile sheria imetia?

  Unasema ukweli wakati unazungmuzia Daudi:

  -Kwa upande mmoja anakataa kuuwa mpakaliwa wa Mungu. Hii ni uuaji tu lakini si adhabu ya dhambi.
  -Kwa upande mwengine, unamtaja kama alitenda dhambi ya uzinzi wala hakupigwa mawe akiwa mpakaliwa wa Mungu, na unasema kama hakufumaniwa. Kwani unahakikisha hilo alilolitenda halikujulikana ?
  Acha sasa niandike ile shairi ambayo ulijichunga sana kuandika tuone kama alifumaniwa na nani, na kama alisamehewa au la.

  « 2 Samweli 12:13 Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana DHAMBI. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye AMEONDOA DHAMBI YAKO; HUTAKUFA. »

  Ndugu Lwembe, acha mzaa. Hii shairi inaonyesha ukweli wote wa uzinzi wa Daudi. Amefumaniwa na Mungu, ndio maana akamtumia Nabii. Ukisoma zaidi utaona aliepashwa muona kama mtu ni yule mjumbe wake aliyehusika kwenda kuita yule mwanamke, mke wa Uria. Lakini huyu mjumbe hakuwa na madaraka yoyote.
  Hili jambo halingejulikana, kama halikuandikwa cleary ndani ya Biblia : « 2 Samweli 11 : 3 Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
  4 Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; NAYE AKALALA NAYE; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. »

  Tena hii dhambi ni sawa ule uzinzi ulio ndani ya torati , ule wa kufumaniwa kwani Nathani, nabii analenga kama DAUDI ALIKUWA NI WA KUUWAWA.

  Lakini, Daudi akiisha kiri kama ametenda dhambi, adhabu ikabadilika na AKASAMEHEWA kwani imeandikwa « …BWANA NAYE AMEONDOA DHAMBI YAKO, HUTAKUFA »

  Sikiliza vizuri Lwembe, dhambi ya Daudi ilikuwa bila shaka dhambi ya mauti, lakini Bwana akaiondoa/akaisamehe. Lakini ingelikuwa mtu wa chini ambaye anaweza fumaniwa na mtu yeyote hiyo sheria ya torati ingempata na angelikufa kufwatana na sheria.
  Ndio maana tunamshukuru Yesu alietutosha chini ya laana ya sheria. Bwana Yesu asifiwe!

  Pengine unasema ni Daudi tu, lakini ukiulizwa orodha ya waliopigwa mawe kwa adhabu ya uzinzi hutapata cases nyingi tofauti licha ya kuwa hii dhambi imeandikwa ndani ya torati.

  Ndivyo torati ilivyo, haikamiliki, ina woga, haiko defined vizuri. Ndio maana Yesu aka i fullfil akifanya agano jipya. Haleluya!!!

  Hivi ndugu yangu sitarudilia swali zangu kwani hii ninayokupa ndiyo ulipashwa nijibu. Sasa kwa hofu tu, ukakwepa ukileta maneno isiyoambatana na swali.

  Fahamu, tena usisahau, Mungu anabaki Mungu, na anafanya apendavyo. Usije ukaanguka kwa kuiga tu wanaadamu kwa mambo yote. Si kwamba alikuwa mtume au mfalme, au nabii inayompa uwezo wa kupindisha mapenzi ya Mungu .

  Usijitahidi kugeuza kauli isiyo yako. Nikikuambia kama maneno uzinzi na uasherati yapatikana ndani ya dictionaries ni ukweli. Kinyume yake ndiyo uongo mtupu. Hebu taja dictionary ambayo haina hayo maneno. Lakini nikakwambia ukiyaongelea kama dhambi ndipo tu unauliza bible. Sasa unapouliza agano jipya linakueleza. Lisingelikuwa na ile uwezo kama halina superiority juu ya agano la kale. Wale tu wanao moyo mgumu kama hawo mafarisayo waliyouliza Yesu juu ya talaka ndiwo mashabik wa hiyo torati kama wewe.Hiyo ZERO uliyoandika uidake vizuri ni yako, tena si mara yako ya kwanza unatumia style kama ile.

  Acha kupoteza watu ili wafikiri kuna dhambi ambayo mshahara wake si mauti. Tulitoa shairi nyingi. Mshahara wa dhambi yoyote ni mauti, ndio maana katika agano kamilifu wala si hilo la kuchakaa na karibu kutoweka, dhambi ya uzinzi iko katika orodha ya dhambi nyingine zote na utaisoma katika shairi hapa chini. Tatizo ni moja « kukataa kutubu ». Hence, usiendelee na uongo ukidhani hutakufa nayo. Jambo lingine tulilokuzungmuzia ambalo linahusu kifo ni kuua. Katika torati unapoua nawe unauwawa. Jambo lote ulilofanyia mwenzio likiwa baya nawe ulilifanyiwa(Jicho kwa jicho)

  Mda unao, soma bwana :

  “Ufunuo wa Yohana 21;8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”

  “1 Wakorintho 6:9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? MSIDANGANYIKE; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,”

  (LAKINI WEWE Lwembe UNAYETOFAUTISHA DHAMBI MBELE ZA MUNGU HUONI KAMA UNADANGANYIKA?)

  “Ufunuo wa Yohana 22:15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”

  “Ufunuo wa Yohana 22:15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”

  “Waebrania 13:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.”

  “Marko 7: 21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
  22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
  23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. »

  “Mathayo 15: 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
  20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi. »

  « Ufunuo wa Yohana 2 : 21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki KUUTUBIA UZINZI wake. »

  (Je HUONI KAMA MTU ANAWEZA TUBU UZINZI ? NA KAMA ANAWEZA TUBU SI KWAMBA ASAMEHEWE? ASIPOTUBU HAPO NDIPO ANAKUFA!)

  « Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. »

  Mungu wa Mbinguni akubariki.

 2. Ndg Ziragora,

  Nimeyaona majibu yako baadaye sana, halafu sikurudi tena ktk thread hii licha ya kwamba nilikuwa na shauku ya kukujibu, hata hivyo nakushukuru kwa majibu yanayo ufunua uelewa wako wa haya tunayoyaongelea!

  1. Katika wazo lako la na 1, nakuona bado unatatizika na uhalisi wa matukio! Jibu la swali lako kuhusu case ya uzinzi iliyosamehewa, nimekuonesha wazi kuwa HAWAKUSAMEHEWA, ila hawakuuliwa tu! Yawezekana ni kwa kukosa ufahamu mzuri wa tabia za Neno, Mpakwa Mafuta wa Bwana huwa hahukumiwa na yeyote yule zaidi ya Mungu mwenyewe, 2Sam 1:14-16 “Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.” Adhabu hazikuwa zikitolewa kiholela kama unavyodhani, walikuwa na mwongozo, hiyo Torati yao ndiyo iliyowaelekeza nani apigwe mawe; kwahiyo ukimuona Daudi hajapigwa mawe usijidanganye kuwa nawe utapona!!!!

  Pia unasema, “” …torati ilikuwa mkusanyiko wa sheria za KIDINI, KIJAMII na KISIASA kwa ajili ya uongozi wa taifa. Hivi yote tukiikamata kama ni ya kidini tutakuwa tumepoteza lengo.”” Hapa ndipo tunapoachania, maana kauli yako hii inadhihirisha wazi kuwa “umepoteza lengo” kama unavyosema! Hivi kuna SIASA ambazo zinakuleta kwa Kristo?? Fanya utafiti vizuri kabla hujakurupuka na maelezo yasiyoeleweka!! TORATI ni NENO LA MUNGU na si hayo unayotueleza!!!

  2. Kuhusu Agano Jipya kufundisha habari ya Uzinzi na msamaha wake, unahangaika bure kutafuta kitu ambacho hakipo!! Msingi wa habari ya uzinzi umewekwa huko AK, nakupastia tena kama itakusaidia:
  “””Deut 22:22 ” If a man be found lying with a woman married to an husband, they shall both of them die, …””””
  Ukiisha kuyaelewa haya, sasa ndio unaendelea huko ktk Ufu 21 nk ndipo utayajua hayo vizuri sana.

  Uzinzi wa ibada ndg yangu, ndio unaoanza na kisha kudhihirika ktk mwili! Kwa mfano wewe unapowafundisha wakristo kwamba wakizini wanaweza kusamehewa wakiutubia uzinzi wao, jambo la kwanza linalojengeka mioyoni mwao ni huo msamaha ambao hupatikana ktk ibada, yaani umewaelekeza kumsujudia mungu mwingine, huyo “ndama wako wa dhahabu” mwenye kuwasamehe wakristo wazinzi; hapa ndipo uzinzi wa kiroho unapoanzia, baada ya hapo wanaendelea ktk mambo yote mawili, uzinzi na ibada!!

  Pia ukitaka kuijua hasira ya Mungu juu wazinzi wa kiroho, hebu rudi kule pale Kut 32, ukiona kwamba ktk vifungu hivyo kuna fundisho la msamaha kwa wazinzi wa kiroho, basi jua kwamba Injili imekushinda!!! Kwa taarifa yako wote hao waliishia jangwani, kama ambavyo wazinzi wa kiroho wa leo watakavyo ishia!!! Watazame manabii wa Ahabu, hao wenye mfano wa walimu wa leo wanaowafundisha wakristo kwamba watasamehewa uzinzi, waliishia kwenye ncha ya upanga!

  Kuhusu Dictionaries, jitahidi ulitazame jambo hilo ktk ufahamu ulionao, kwamba unajua kuwa kuna Mungu; basi kitikise kidogo kichwa chako, ili ubongo uchangamke, halafu jiulize kati ya waandishi wako wa dictionaries na Mungu, ni yupi aliye na maana kamilifu ya maneno? Ukiona ni hao waandishi, well, utakuwa umepata ZERO; “Hapo mwanzo kulikuwako Neno…”!!!!

  6. Ni kweli umenijibu kuhusu AJ kufundisha uzinzi kwa kadiri unavyofahamu, nimelipokea jibu lako, ingawa halikulijibu swali langu kikamilifu maana umeniletea nukuu zinazoongelea wazinzi, nadhani ni kutokana na kuikosa kabisa maana ya neno “kufundisha” ndio ukaja na nukuu hizo nje ya swali! Bali kama nilivyokuambia, Torati ndiyo inayofundisha Dhambi, Agano Jipya huzirejea Dhambi tu na si kufundisha Dhambi; ukiambiwa kumchukia ndg yako ni kumuua, basi unapaswa ujue kwanza kuua ni nini, ndipo maelezo hayo ya chuki yatakuwa na maana kwako!!! Kwa kudhani kwako kwamba unapoteza muda kuyajua ya Torati, ndiko kutakufanya uishie ktk kesi usizozitegemea, kwa ujinga!!!

  Suala la wazinzi “kufumaniwa” kisha wakaachwa wasipigwe mawe ktk Agano la Kale, hili ni jipya kwangu, sijawahi kukutana na jambo hili, ingawa nafahamu kwamba wazinzi wengi sana hawakupigwa mawe kwa sababu tu hawakufumaniwa ktk uzinzi wao kulingana na matakwa ya Torati; na kama unayemsemea hivyo ni mfalme Daudi, kwa kweli sijawahi kusoma popote pale kwamba alifumaniwa, labda ukinielekeza yalipo haya mambo mawili! Na kuhusu adhabu kwake, hilo nimekwisha kukuonesha kuwa mpakwa Mafuta huwa hapotei, ndio maana hata Sauli hakupotea!!!

  Swali lako lenye vipengele vitatu ni la kigomvi zaidi kuliko kujifunza, lakini wakati mwingine hata ugomvi hutusaidia kujifunza!
  1. “Wapi katika agano jipya wanaposema kama dhambi ya uzinzi haisamehewi?”
  JIBU: Mkristo ni huyo aliye ktk nuru, ambaye Torati imemleta kwa Kristo, basi huyo akianguka ktk Uzinzi Maandiko yanasema hivi: Ebr 6:4-6
  “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.”

  2. “Wewe unafikiri kwa sababu gani watoto wamoja wa Mungu walipigwa mawe na wengine hapana, wote wakiwa wamefumaniwa wakizini?”
  JIBU: Daudi ndiye ninayemfahamu kwamba alizini na hakupigwa mawe, hata hivyo sifahamu kwamba alifumaniwa, na pia nafahamu kwamba Mungu asingeruhusu apigwe mawe kwasababu ni mpakwa Mafuta wake, wapakwa Mafuta huwa HAWAPOTEI, wakipotea kama hawa wengine, basi Mungu atabaki kilema, ndio kisa cha kumleta Kristo kwa ajili ya hao tu awalipie huo uzinzi wao, wa mwili na wa kiroho!!!

  3. “Wapi katika agano jipya waumini walifundishwa dhambi kupitia agano la kale?”.
  JIBU: Gal 3:24 “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.” Basi hata kama uliokokea ktk mkutano wa Injili viwanjani, bado unapaswa ukamilishwe kusanyikoni mwako ambako Mungu ameziweka Huduma Tano kwa ajili hiyo. Kama hizo hazipo, basi endelea huku kwenye blog wapo walimu wengi tu, tena utasaidika vizuri tu!

  Ubarikiwe ndg yangu!

 3. Mpendwa Lwembe,

  Bwana Yesu asifiwe !

  Nashukuru sana Mungu tena nakushukuru pia kwa majibu ulionipa. Ubarikiwe.

  1)Wakati ule wote ulikuwa ukikwepa kujibu « ndio » au « hapana » kiukweli, ulikuwa ukijitahidi kufanya homework niliyokupa inayoambatana na hayo maswali. Sasa nakupigia saluti kwani umejaribu kuufikia ukweli. Hiyo homework ilikuwa utafiti kwa hiyo swali « Je, una uhakika kama katika agano la kuchakaa, hakuna case ya uzinzi iliyowai samehewa ? ». Hiyo swali ulilipewa licha ya kuwa umetumia mda mrefu ukidai kwamba katika agano la kale hiyo dhambi haikusamehewa, na kama yeyote aliyesubutu alipata adhabu ya kuuwawa kwa kupigwa mawe. Kwa hivi umehakikisha kama kuna wana wa Mungu ambao walizini kwa ile wakati bila kuadhibiwa palepale kwa adhabu ya kifo kupitia kupigwa mawe, umepata jibu na ninaamini kama hutaendelea na ile msimamo yako kama agano la kale liliadhibu kila mzinifu kwa kifo hicho.
  Kuweka hitlafu fulani katika jibu lako kama hawo wazinzi wanangoja huko wakiisha kufa kifo cha kawaida(contradiction na kuuwawa pale pale kwa mawe) hainitishe kwani hivyo ndivyo ulivyo. Kwa hiyo sitapoteza mda ya kukupatia shairi wakati wewe mwenyewe umepata. Inakubaki tu kuondoa hila na kusema wazi kama wale watoto wa Mungu unaowasema walisamehewa uzinzi kwani naamini hivyo ndivyo ulisoma. Jina la Bwana libarikiwe !
  Pengine ukiwa na upungufu fulani uombe mwenyewe shairi ya kukusaidia ili uliyogundua uisimamishe vema. Nakuona ukijitahidi pole pole kudaka ukweli.
  Ni vema kuelimishana zaidi. Kama kweli ulipata utaona kama zile cases ni zile ambazo Mungu mwenyewe aliingilia kati. Hio ina fundisho kubwa: kama hakuna mwanaadamu anaeweza samehe kama Mungu. Haleluya!
  Utaelewa pia kama torati ilikuwa mkusanyiko wa sheria za KIDINI, KIJAMII na KISIASA kwa ajili ya uongozi wa taifa. Hivi yote tukiikamata kama ni ya kidini tutakuwa tumepoteza lengo.
  Unapoendelea unasema ilikuwa bado Damu kumwangika. Je ulisahau kama ulisema hakuna dhabihu kwa dhambi ya uzinzi? Je damu haikumwangika katika agano la kale kwa ondoleo la dhambi? Ndipo ufahamu kama ile damu haikuwa na nguvu kama ya Yesu Kristo. Bwana Yesu apewe sifa!
  Sasa hii Damu ya Yesu Kristo inapoingia kati ndipo mwanaadamu hana tena ruhusa ya kupana adhabu kwa dhambi yoyote bali Yesu Kristo mwenyewe ambaye hakutofautisha dhambi akisema zote ni za mauti kwa yeyote asiyetubu. Hii inatupeleka kwa point num 2.

  2)Kuwa agano jipya inafundisha dhambi ya uzinzi na adhabu yake nilikupa shairi, ile ile yote niliyokupa inayofanana na hii “Ufunuo wa Yohana 21;8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” unayoendelea kukataa ukiikubali kwa upande mwengine. Pengine wewe una namna yako ya kusikia kufundisha dhambi. Kwangu mimi, ile neno “kufundisha dhambi” ni kukataza/kukemea dhambi na kuonyesha adhabu yake. Sasa shairi zote nilizokupa zinakataza na kukemea ile dhambi ya uzinzi pamoja na kuarifu kama watakaofanya moyo wao kuwa mgumu, adhabu ni mauti. Kinachofanya agano jipya kamilifu ni kwamba linaonyesha wazi kama dhambi zote mshahara wake ni mauti wakati agano la kuchakaa lilitegemea uzito wa dhambi kufwatana na licho ya mwanaadamu. Ndio maana utakuta torati inasema “anaeondoa jicho naye aondolewe jicho, anaeuwa naye auwawe”, lakini Yesu alifika na Injili inayotuambia “akupigaye shavu la kushoto umgeuzie na la kuume, …”. Ndugu yangu, nafikiri umejibiwa, ukikosa jibu kwa maswali uliyopewa usifanye hii kuwa kisingizio. Utaona pia kama hizo dhambi zisizosamehewa kirahisi katika agano la kale ni zile zilizotendewa zaidi wanaadamu. Ukisoma vizuri Biblia yako utaona kulikuwa ingine aina ya uzinzi ambayo unakwepa kusema: ile ya kuzini na miungu(kuabudu miungu). Hio dhambi ilifanyiziwa tu Mungu na ilisamehewa tu kwa condition moja ya kuwa taifa ya Mungu imgeukie tena Mungu wake, lakini Mungu hakuwapiga mawe hao wazinzi.

  Unaposema kama dictionaries hazina maneno kama “uzinzi”, “uasherati” unataka leta ubishi kwa bure. Hii maneno ni ndani ya lugha, na hizi vocabularies ni ndani ya kitabu cha lugha. Nilikuambia, kama ufafanuzi kama uzinzi ni dhambi ndiyo biblia(teolojia) inaleta, lakini neno linajulikana. Hence, uzinzi kama neno, kila anaejua lugha anaifahamu, lakini kama dhambi unaipata ndani ya biblia na agano jipya inaisema kama dhambi. Hivi kuwatuma watu kujifunza katika agano la kuchakaa neno uzinzi ni kuwapotezea mda.

  3) Neno « zaidi » siyo scientific, usidanganye, ni ya kawaida.Uwe tu muungwana usemeshe ukweli kama uliyoshindwa ni kusema « ndio » au « hapana » kwa kweli ukihofia kutokuwa mkweli. Kupitiya hayo, ufahamu kwamba nilikuwa nikitafuta nijue kama tulipatana au la kwa vipengele fulani kwani mimi napenda nuru. Sasa kama ulinyamaza, mim nadaka kama umeitika na ukileta swali lolote linalolingana na hivyo vipengele usidai jibu kwangu.

  4) Unasema mim nawaita wenzangu « watoto ». Nafikiri ulitaka andika “kama watoto”, si ndio? Nilichokisema si kukukataza kuniita mtoto kama kawaida yako ya kila leo lakini nilikwambia kama hata mtoto anastahili majibu. Mimi sijawai kusema sitaleta jibu kwani mtu amesema au ameswali kama mtoto. Mtoto anapashwa rekebishwa bwana! Unaposema mim ni mtoto nangoja ujibu kirahisi kwa maswali yangu. Lakini wewe unaifanya kisingizio cha kutojibu. Sasa ndio maana badala ya kuwa mkweli unatawaliwa na hila.

  5) Kuwa robot imekufurahisha sana, uwe tu robot ndugu yangu, ujisikie huru, no problem.

  6) Kwa mwisho mimi nimekujibu mara nyingi kwa swali lako linaloomba wapi agano jipya linafundisha uzinzi, hata kama wewe unaona haikamilike lakini umeiona.Na isitoshe homework uliopewa ilikuelekeza kufahamu kuna wasiyowai pigwa mawe kwa dhambi ya uzinzi licha ya kufumaniwa ktk agano la kale. Sasa jibu na wewe hata kwa sehemu : “Wapi katika agano jipya wanaposema kama dhambi ya uzinzi haisamehewi?”, “Wewe unafikiri kwa sababu gani watoto wamoja wa Mungu walipigwa mawe na wengine hapana, wote wakiwa wamefumaniwa wakizini?”, “Wapi katika agano jipya waumini walifundishwa dhambi kupitia agano la kale?”. Nimetia vipengele vitatu lakini swali ni moja.

  Asante Ndugu yangu kwa kujibu kale ka swali kadogo tu wakati wewe ulijibiwa mengi.

  God bless you.

 4. Sungura,

  Unajua ktk majadiliano, kuna wakati yanaweza kukwama kwa kutofautiana, lakini mkidumu ktk spirit ya kujifunza, mara nyingi tofauti huondoka na mkafikia kuliona jambo kama linavyopaswa!

  Mimi ninakushukuru kwa hilo, ni jambo lenye manufaa katika Ufalme wa Mungu!!!

  Kuhusu jambo la Uzinzi, its a bit tricky, ndio maana huko nyuma ktk mjadala huu, kuhusu kumsamehe mzinzi, nilisema tendo la kujamiiana, kimsingi ni kwa ajili ya kupata watoto na si starehe kama tulivyolizoelea baada ya Anguko. Kwahiyo unapoufikiria msamaha kwa labda mke mzinzi, nikasema ujitayarishe na kulea mapacha labda kumi watakaozaliwa kutoka tendo hilo la uzinzi, yaani wale ambao uswahilini wanaitwa “kitanda hakizai Haramu”!!!

  Kwahiyo tunapozungumzia Msamaha ni lazima tumuone Mungu akimsamehe huyo kwanza, vinginevyo msamaha wetu ni kazi bure, ni intellectual tu, bali Hukumu ya Mungu itabaki imesimama kulingana na Neno lake ambalo HALIJAUTANGAZA msamaha huo!

  Jaribu kwenda pole pole na jambo hili, ni tatizo kubwa sana kwa kanisa. Kanisa limejichanganya sana na kulifanya “so light” an issue wakati it is INSTANT Death!!

  Asante,
  &
  Gbu!!

 5. Ndg Ziragora,

  Kwanza nikushukuru kwa maelezo yako, ni baraka kukusikia au kukusoma, maana yote ni ktk kujifunza!

  Basi katika kuyapitia hayo, kwa kadiri ulivyoyaorodhesha, nitasema haya juu yake:
  A: Nakuona uko ktk mapambio ukiusubiri upako wa kulijibu swali langu!

  B: Nilikuambia kuwa maswali yako ni scientific ktk maana ya kwamba ni mambo unayopaswa ujifunze huko shule, kwamba ukiisha liongeza neno “zaidi” ktk jambo lolote lile, halibakii kuwa ni lile la mwanzo tena ktk kiwango! Mambo ya Mungu sio scientific, yanajulikana kwa Imani hapo unapoliamini Neno lake na si hisia za dini na mafundisho yake, kama hizi abracadabra za kuzini mara moja na kuzini mara saba; ukikamatwa hawaangalii ulizini mara ngapi kaka, UNAPIGWA MAWE tu mpaka ufe!!!

  Kuhusu kuandika kwangu kama “robot”, ukiniambia tena kuwa nakurupuka kiakili, basi utakuwa hujui hata “robot” ni nini! “Robot” hana akili yake, anaendeshwa kwa program mahususi za kisomi, ndio maana nilipokupima nikatambua kuwa nawe ni “robot” anayeendeshwa kikamilifu na programu za dini, kwahiyo huna uwezo wa kuyapima mambo kimantiki!

  Kuhusu swali la Uzinzi nililokuuliza, kwamba unioneshe ni wapi A/Jipya LINAPOFUNDISHA uzinzi na adhabu yake? Na wapi linapofundisha MSAMAHA kwa wazinzi? Majibu unayonipa ndiyo yanayonidhihirishia kwamba wewe ni “robot” wa dini na huna uwezo wa kupambanua chochote kile! Dah! Unajua, uliponiambia kuwa Injili inahubiriwa, Torati inafundishwa, niliamini kuwa unajua unachokisema, lakini naona ni tofauti, hukijui, utakuwa una mimic mafundisho yenu ukidhania ndiko kujua!

  Tena kwa kiwango ulichoshuka kiufahamu inasikitisha sana, maana Torati uliyojitutumua kuijua na kwamba utanifundisha, naona sasa umegeuza mwelekeo unanipeleka kwenye dictionaries!!! Hivyo vifungu unavyokazana kuninukulia HAVIFUNDISHI kuhusu Uzinzi kama unavyofikiri, bali vinaelezea yatakayowapata wazinzi! “Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, … na WAZINZI, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI.” Sasa, kwa akili yako kifungu hiki kinafundisha kuhusu Uzinzi? Jamani, msiwe wepesi kuyajibia mambo msiyoyajua kwa kutafuta umaarufu msiokuwa nao! HAKUNA mahali popote ktk Agano Jipya linapofundishwa jambo la Uzinzi! Msingi wa Dhambi uko ktk Agano la Kale, hiyo Sheria, ndiyo inayoifunua Dhambi.

  Ktk Agano la Kale ndiko kuna tafsiri ya Uzinzi na si dictionaries! Mzinzi ni mtu anayelala na mke wa mtu, “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.” (MWA. 20:3 SUV)
  Deut 22:22 ” If a man be found lying with a woman married to an husband, they shall both of them die, …”
  Ulipohubiriwa Injili, baada ya kuipokea, ulipaswa uketishwe chini ufunzwe mambo haya, kama ilivyoamriwa ktk Mathayo 28:19-20 ktk uanafunzi wako!

  C: Nikiyajibu maswali yako:
  -Je, unaweza leta shairi ya agano jipya linalosema kama uzinzi haisamehewi?
  JIBU: Ukiona kwamba UMESHINDWA kupapata mahali ktk A/J ambapo panafundisha MSAMAHA kwa Wazinzi, kama nilivyokuomba mimi kwanza unioneshe, basi jua kwamba kushindwa kwako ndilo jibu la swali lako! Ndio maana nilikuambia kuwa unapaswa uwe umejengwa juu ya Msingi wa Agano la Kale ndipo utaweza kuyajua ya Agano Jipya!

  -Je , una uhakika kama katika agano la kuchakaa, hakuna case ya uzinzi uliyowai kusamehewa?
  JIBU: Wakati wa Agano la Kale Damu ilikuwa bado HAIJAMWAGIKA. Kwahiyo unapoziona instances za watoto wa Mungu wakianguka ktk Uzinzi na kisha kutokuuliwa, isikuchanganye sana ukadhania eti walisamehewa uzinzi wao, walikufa wakiwa na Hatia hiyo, wote waliisubiri “Siku Iliyokubaliwa”, ndipo Damu ilipomwagwa nao wakatoka wakiwa HURU Dhambi yao ikiwa imeondolewa!

  Basi kwa leo baada ya Damu itakasayo kuwa imekwisha kumwagwa, mkristo anapaswa akufikie KUJAZWA RM ili awe huru na Dhambi, kwani asipolifikia jambo hilo hatauona Ufalme wa Mungu, na inawezekana kwamba ameshindwa kuifikia Hatua hiyo kutokana na Uzinzi wa Kiroho anaoendelea nao kulingana na Mafundisho ya Dini yanayomshikilia, baada ya kuwa ameposwa na Kristo!

  Kuhusu kuyajibu maswali yako, nadhani wewe utakuwa umejichanganya, kushindwa kwako kuyapokea majibu, kunakuongoza kulalamika kwamba hujajibiwa, ndipo unakuwa kama mtoto mdogo anayeililia keki yake aliyokula! “Motoni na motoni zaidi…” umejibiwa, hutaki, basi ujibiweje?!! Twende tuzungumzie Injili kaka, achana na hila za kuharibu akili za nduguzo, mara sijui “uko jela” mara sijui “pembe” ya …, sponji enhe? Ukiwaambia wenzio “watoto” sawa, ukiambiwa wewe “acha utoto” unawaka, kama si Hila ni nini hicho?!

  Kama una maswali yanayohusu Injili, hilo ni jema, hata kama mimi nimeshindwa kukupatia jibu, wengine watakujibu!

  Karibu sana ndg yangu, tujifunze!

 6. Lwembe,

  Nimefurahishwa na ulivyoendelea kufafanua kwa usahihi sasa suala la ‘kutimiliza’-‘to fulfill’. Maana umetoa maelezo ambayo ni yakinifu sana juu ya kile alichofanya Yesu katika dhana hiyo nzima ya kuitimiza torati na manabii.
  Maelezo yako yatamfanya hata rafiki yangu Siyi aelewe hilo fungu maana anapenda sana kulitumia kimakosa.

  Kuhusu ufalme wa Mungu kuwa ndani yetu kwamba ndiye Roho mtakatifu. Mimi kifasihi nakuelewa unachomaanisha haswaa. Lakini kuna watu hapa hiyo neema hawana, ni lazima tu jambo hili likae sawasawa ili hata asiyejua fasihi andishi( vizuri aweze kuelewa.

  Maneno ‘ufalme wa Mungu uko ndani yenu’, yalisemwa kabla hata ya Roho mt. kuanza kukaa ndani yetu.
  Ufalme wa Mungu kwa maana ya neno ufalme, ni mfumo wa jinsi Mungu anavyotenda kazi, au anavyo-operate mambo yake.

  Roho mt yeye ndiye anayetuwezesha sisi kufanya mambo/kuenenda kama huu mfumo(ufalme) wa Mungu ulio ndani yetu unavyotaka. Kwamba pasipo yeye hatuwezi kumudu kutenda kama ufalme huo unavyotaka.

  Na ni katika mantiki hiyo sasa inakuja hiyo maana ya kifasihi kwamba Ufalme wa Mungu ni Roho mtakatifu. Ikibeba dhana kwamba, ili ufalme wa Mungu uweze ku-perat-ika ni lazima kuwe na Roho mtakatifu.

  Lakini haina maana kuwa ‘definition’ ya neno ‘ufalme wa Mungu ni Roho mtakatifu, na nimegundua hata wewe hukumaanisha hivyo

  Lwembe mimi si miongoni mwa hao makanisani, ambao huwalazimisha waume wawasamehe wake wazinzi kwani hawaruhusiwi kuwataliki,ispokuwa, sijakubaliana tu na wewe ulivyofikia hitimisho kuwa dhambi ya uzinzi katika agano jipya haina msamaha.

  Asante.

 7. Sungura,

  Hila inakuwa hila hapo unapoweza kuithibitisha kuwa ni hila!; vinginevyo hata kumwambia mtu ana hila ni hila pia!!!

  Unajua, tukisema tutoke katika majadiliano plain, tuingie katika uwanda wa philosophy, tutazeeka tukiwa hatujui chochote kuhusu Mungu! Mimi ninachokifahamu ni kwamba RM ndiye hukaaga ndani ya watu, kwahiyo Maandiko yanaponiambia, “… the kingdom of God is within you” huwa naelewaga kuwa ndio huyo RM, labda unifundishe tofauti!

  Hahahaha…! Nimefurahi kuyasoma maelezo yako kuhusu neno “Kutimiliza”, its a romantic word, no wonder huwa ninalileta katika maana ya “to magnify”, nadhani hata maelezo yangu yanareflect maana hii! Nimeitazama Biblia yangu ya KJV, inasema “to fulfill”, at this stage, ninaipokea pole yako na asante kwa ufafanuzi wenye rejea!

  Kwamba Kristo alikuja kuitimiza Torati na manabii, “to fulfil”, kama nimeelewa vizuri, ni kwamba aliyatimiza yaliyoandikwa kuhusu yeye na si yaliyowashinda wengine! Na akiisha kuyatimiza hayo, hapo ndipo yanapoishia, baada ya hapo wote wanapaswa kumsikiliza yeye aliye Sauti ya Mungu, “Kristo ni mwisho wa sheria”. Kuyatimiza yaliyoandikwa ndiko kunakomtambulisha kwamba huyo atokana na hiki tunachokishikilia, Torati na manabii humo yalimo andikwa kumhusu, na yeye mwenyewe anakiri kwamba hakuja kuitangua Torati ili awaletee kitu kipya, hapana! Ndio maana baada ya wale washtaki wa yule mwanake kushindwa kuitimiza Torati juu ya yule mwanamke mzinzi, yeye hakumpiga mawe yule mwanamke, ingawa angeweza, bali hakufanya hivyo maana HAKUNA palipo andikwa kwamba atalitimiza hilo!

  Basi, sasa akishakuwepo uwanjani, ndio anayaleta kama hayo ya kumtazama mwanamke kwa kumtamani kukuingiza ktk Uzinzi. Hapo si kwamba anafundisha Uzinzi ni nini, bali anawazungumzia wazinzi ni wepi, kwamba sasa katika kundi hilo wamejumuishwa na wenye kutamani wanawake, wanaowataliki wake zao nje ya Uasherati, nk. hao anao ongea nao wanajua Uzinzi ni nini na adhabu yake, kama nilivyoyarejea ktk AK, hao si ma mbumbumbu wa jambo hilo kama wengi wetu tulivyo leo hii.

  Umeniambia, “”Na jambo jingine, nilikutaka wewe uoneshe mahali katika agano jipya biblia imesema dhambi ya uzinzi haina msamaha.” Naona hujaelewa vizuri mwenendo wa Biblia, Agano la Kale ndilo Msingi wa Agano Jipya; na Kristo ndiye Utimilifu wa Maagano yote mawili. Mtazame yeye utayaelewa yote, hata hili la Uzinzi linalowasumbua wengi!

  Nawe nadhani ni mmoja wa kama hao makanisani, ambao huwalazimisha waume wawasamehe wake wazinzi kwani hawaruhusiwi kuwataliki kutokana na agizo la Bwana linalotoa ruhusa kuwataliki waasherati tu! Poleni sana!!!!

  Bali hilo latokana na kutokuwa na ufahamu kamili wa huko “kuitimiza”, kwamba alipoitimiza Torati basi na kupigana mawe kumekwisha, mambo ni kusameheana tu, wengine wanafundishana kwamba Kristo alimsamehe yule mwanamke mzinzi na mambo kama hayo, kisha kulazimishana kuishi ktk uzinzi kwa kukosa Maarifa! Basi hata kwa kutumia logic ya kawaida tu, hushangai kwamba anawaambia wanaweza kumtaliki mwanamke muasherati, lakini hamzungumzii mzinzi kabisa, kwanini?! Hakuja kuitangua Torati!!!!

  Na “Aliye safi awe wa kwanza…” inasimama mpaka leo hii!! Nikakuambia kuhusu jambo hilo, kwamba kati yetu hakuna aliyesafi wa kumpiga mwenzie mawe, la sivyo tutauana sana tu, ndio akasema tutatupwa Jehanumu; je, kuna ambaye anaweza kumpeleka mwenzake huko? Hakuna, Yeye ndiye anayewajua wazinzi wote, mpaka wenye kukaa kwenye kona za mitaa kuwapiga chabo wanawake wanaopita, usisahau na wanaonyemelea akina dada makanisani!

  Umeniuliza, “”Lwembe, kwani mtu akitenda dhambi, ili asamehewe anatakiwa kuomba msamaha mwenyewe au anaweza akaombewa msamaha na mtu mwingine pia?””
  Mtenda dhambi si lazima ajiombee mwenyewe, anaweza kuombewa na mtu mwingine iwapo tu dhambi aliyoitenda si ya mauti kama Biblia inavyofundisha!

  Asante,
  Gbu!

 8. Lwembe,

  Ivi unajua kuwa wewe ni mtu mwenye kutuia hila pia ili kujaribu kuonekana kuwa haukosei katika yote unayoandika hapa?

  Mimi nilikwambia kuwa sentensi yako kwamba Roho mtakatifu ndio ufalme wa Mungu haiko sawa, na nikakutaka uifafanue, lakini ukaongea-ongea maneno mengine tu.

  Baadae ili kukusaidia jinsi unavyoweza kuifafanua ili ueleweke ulikuwa unasema nini, nilikupa mfano wa sentensi nyingine kimuundo, ambayo ni ‘wokovu ni matendo’ ikusaidie uweze kufafanua ulichosema.

  Pamoja na kukubali kwako kuwa kimuundo hiyo sentensi kwamba Roho mt. ndiye ufalme waMungu iko sawa na wokovu ni matendo, lakini bado hutaki kukubali kuwa ulikuwa umeandika kitu chenye mapungufu.

  Badala yake unatka kuanza kunifundisha mambo ya ufalme wa Mungu kuwa uko ndani yangu. Kwa kufikiri kwako uliweza kabisa kuthubutu kuwaza kuwa mimi sijui kuwa ufalme wa Mungu uko ndani yangu? Usijaribu kuwa mwalimu kwa somo ambalo mtu halihitaji .

  Lakini pia kuna maelezo yako fulani huko nyuma wakati unajaribu kufafanua kuwa dhambi ya uzinzi haina msamaha ulisema, katika Mt 5:17 kuwa neno kutimiliza ni kule alikosema Yesu kuwa badala tu ya mtu kulala na mwanamke, sasa ni kule kumtazama tu kwa kumtamani tayari mtu ameshazini.

  Nakuona na wewe hauko tofauti na watu wenye ufahamu mdogo au kwa makusudi au kwa kutokujua kwa sababu ya uzembe wa kujifunza, wanaodhani kuwa hiyo ndo maana ya neno ” kutimiliza”. Poleni!

  Lwembe neno timiliza ni Kiswahili cha zamani kabla ya hiyo lugha kusanifishwa. Maana yake kwa KIswahili sanifu ni ‘kutimiza’. Biblia za kiingereza zimesema ”to fulfil”(wewe najua umaelewa vema maana ya ‘fulfil’ siyo huko kutoa kitu mwilini kwenda rohoni, wala siyo kuboresha kitu bali ni kutenda kitu kwa mu-meet reqiurements zote zilizohitajika – Na suala la uzinzi, uuaji, n.k, kutoka kwenye tendo kwenda kwenye wazo siyo huko kunakoitwa kutimiza. Yesu alikuja kuitenda Torati na manabii kama ilivyokuwa inatakiwa,ambako watu wengine wote waliotangulia kuliwashinda.

  Nstari unaofuata(Mt 5:18) anasema mbingu na nchi zitapita, lakini kilichoandikwa kwenye torati na manabii lazima chote kitimizwe( kitendwe kwa ukamilifu kama kilivyotakiwa kutendwa)

  Na jambo jingine, nilikutaka wewe uoneshe mahali katika agano jipya biblia imesema dhambi ya uzinzi haina msamaha.
  Maana uliyoikokotoa toka agano la kale kuwa mzinzi alipigwa mawe kwa hiyo katika agano jipya kwa vile hawapigwi mawi basi mbadala wa kutokupigwa mawe ni kutosamehewa, siyo ya kweli.

  Lwembe, kwani mtu akitenda dhambi, ili asamehewe anatakiwa kuomba msamaha mwenyewe au anaweza akaombewa msamaha na mtu mwingine pia?

  Barikiwa!

 9. Ndugu yangu Ziragora,

  Heri ya mwaka mpya kwako pia.
  Nilikuwa sijatembea hii kona kwa muda sasa.

  Asante sana na Mungu akubariki.

 10. Ndugu yangu Lwembe,

  Asante kwa kunijibu.

  A. Unasema, nakunukuu : “Hata wazo lako kwamba eti umenihubiri nikatubu ni la kitoto sana, mimi nilikuridhisha ili UYAJIBU maswali uliyokuwa unayakimbia kwa kisingizio cha “Uongo” usiokuwepo. ”
  Ina maana ulitubu kwa hila ili niendelee kukufundisha. Hila siyo nzuri ndani ya mijadala. Kama hukutubu uongo kwa kweli licha ya kuwa umesema umetubu, ina maana unasema uongo uliopangilia vizuri.

  Kwa hivi, ndugu yangu, ikikupendeza, baki ndani ya jela iliyotayirishiwa waongo na Ibilisi baba yao hadi utakapopata neema ya kuokoka.
  Ninavyoona ni kwamba kwa uongo unaongeza hila ya hali ya juu. Fahama kama si watu wote wanaotumia hila. Kufundisha viziwi sina ile uweza kaka yangu. Kiziwi wa kiroho ndiye yule mwenye hila na uongo. Yeye anahubiriwa wala hafundishwi. Nitakayofanya baadaye ni ku paste tu uongo wako tena ili pengine kwa kuisoma sana utambuwe kama uko upotevuni. Unatakiwa ufundishwe torati ipasavyo, lakini kabla ya yale uamini, na unapoamini uache dhambi ukianzia kwa hii ya uongo. Unazunguuka sana ukitumia kila neno mbaya kwa kuhofiya kuonyeshwa kama hata katika agano la kale uzinzi ulisamehewa. Ndiyo maana unasema kama hukutubu, unasema eti kusema ndiyo au hapana ni scientific, unasema nikufundishe pale pale ukipinga mafundisho yangu kabla sijayaleta, unakwepa kwa kuweka histories ambazo unafahamu hazina maana katika hii mjadala, nk. Hiyo ni hofu ya kukimbia kukiri upungufu.
  B. Nakufahamisha kama leo sikufundishe ila nakujibu tu kwa maswali yako kwani hata ukiwa upotevuni, nakupenda.
  -Unaposema “tanuru”, kiisha kuongeza kwake mara saba, hii haikulete katika haki kwani umesema wewe mwenyewe kama ni tanuru ile ile iliyoongezwa. Hapa ni kitu kimoja kinachozidishwa. Si kama kulinganisha makaa na furnace. Ni kama mtu aliezini limoja, na yule aliezini mara saba. Unafikiri hiyo dhambi imebadilika?
  -Unaandika kama robot, asante kwa kuikubali ukiigeuza nzuri. Unakurupika kiakili na unaandika kama robot, ok?
  -Uzinzi ni neno lipatikanalo ndani ya dictionaries zote zisizokuwa hata za kiteolojia. Ina maana, kama tendo hata wasioamini wanalijua. Unasema nikupatie mahala ambapo agano jipya inazungumuzia “uzinzi” na adhabu yake! Sasa ninaikupa mara ngapi? Lwembe, ukiwa serious si utaona nimekupa shairi nyingi na ya mwisho ikiwa hii? ” Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na WAZINZI, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI. »
  Ukiona ambayo nimetia kwa herufi kubwa, ya kwanza inataja “uzinzi” kama dhambi umbalimbali na dictionaries za kawaida, na ya pili inasema adhabu yake. Isipokuwa kuonyesha dhambi na adhabu yake, sione mafaa ya mafundisho mengine unayodai. Kama ni mafundisho “scientific” ndipo utaandika novel.
  C. Swali:
  -Je, unaweza leta shairi ya agano jipya linalosema kama uzinzi haisamehewi?
  -Je , una uhakika kama katika agano la kuchakaa, hakuna case ya uzinzi uliyowai kusamehewa?

  Lwembe, usiendelee kusema hujajibiliwa wakati ni wewe usiyejibu ukidai kama maswali ni za kitoto na mengine “scientific”. Isipokuwa hila, unawaza hata mtoto hana haki ya jibu? Na kwa nini ushindwe kujibu swali unaloona ni rahisi kujibu kiwango uliite la kitoto. Ok, kama wewe una akili kubwa sana bila hikima, sema ni la kitoto lakini tia jibu bwana!!!
  Hebu nikuulize, kila mtu akikwepa maswali kama wewe akidai ni maswali ya kitoto, mjadala itaendelea je? Ninachojua ni kwamba UKIWA MUUNGWANA, kama jibu halijakamilika, unaendelea ongeza hadi ukamilifu. Hata ndugu yako anaekusoma atapata nafasi ya kunyoosha ili ueleweke vizuri. Lakini unapokwepa hueleweki!!!!!

  Mungu akuwezeshe kaka yangu.

 11. Shalom ndg Ziragora!
  Yale unayoyasema ni maswali, ukweli si maswali, labda uwe mtoto mdogo unayejifunza maneno! Pia nilikuambia ni scientific kwa sababu ni mambo tunayojifunza huko shule za utotoni, huko ndiko tulikofundishwa kwamba neno “zaidi” hulipeleka jambo ktk kiwango kingine, Dan 3:19 “… basi akatoa amri watie moto ile tanuru MARA SABA kuliko desturi yake ya kutiwa moto.”

  Iwapo hao waliotumwa wangekuwa na akili kama yako, wangekoleza moto wa kawaida tu badala ya huo wa zaidi; kwahiyo si jambo la kujitia kamba shingoni kama unavyofikiri, bali ni jambo la ufahamu tu, kama unajua ndio hivyo na kama hujui ndio hujui!! Mtu asiyelijua jambo, halafu akawa hana uwezo wa kujifunza, njia rahisi ya kukataa kujifunza huwa ni kudai kuwa huyo mwenye kumpa maelekezo ni “muongo”, ndipo hujijengea wigo kuzuia elimu, naye hubakia akiwa cocooned katika ulimwengu wake wa kufikirika, ambako maneno hayana maana zaidi ya anayoiwazia yeye!!!

  Moto wa desturi ya tanuru hilo, kiulinganishi ningekuambia ni sawa na Dhiki Kuu watakayoipitia wakristo walio ktk wokovu hao wanao asi kwa kuikataa sehemu ya Neno, kama kwa kudanganywa kwamba wakizini wanaweza kutubia nk, hawa miili huangamizwa bali roho zao huponywa. Lakini, tanuru inapokolezwa mara saba, shughuli huwa inabadilika, hiyo inawahusu walimu wa uongo, ukitumbukizwa humo, lah, hata sijui itakuwaje maana wale askari waliowatupa wale watoto wa Kiyahudi, Biblia inasema ule moto uliwaramba, unahiyari ya kuyaona hayo kama yako sawa au yana utofauti!!!

  Hahahaha… kumbe hata hujui kwamba unawashawishi watu wafanye “uzinzi”? Hapa ninachofanya ni kuwakumbusha wote walioathirika na ushawishi wako kwamba wakithubutu kujiingiza ktk Uzinzi, basi wajue kuwa kwa uhakika “Wamekufa”!!! Unaweza kuniona kama mtu niliyekurupuka, lakini sijawahi kuona robot anayekurupuka, maana najua kuwa huwa wanakuwa programmed ktk hayo waliyopangiwa, hata akiwa ni robot wa Injili! Na robot wa Injili huwa wanakuwa programmed kuanzia huko kwenye Torati, sasa ukiniambia kuwa eti wewe unahubiri Injili halafu hata Torati hujui inafundisha nini, basi aliye kuprogramu robot wewe ni nani? Dini???

  Hata wazo lako kwamba eti umenihubiri nikatubu ni la kitoto sana, mimi nilikuridhisha ili UYAJIBU maswali uliyokuwa unayakimbia kwa kisingizio cha “Uongo” usiokuwepo. Nilichokifanya ni kumpigia mruzi nyoka aliyejificha shimoni ili atoke, si unaona umeyajibu maswali, na shimo lenyewe nimelifukia, ila nakuona unajitahidi kuchimba shimo jingine!!! Nimefurahi kwamba wewe mwenyewe umejiona jinsi unavyolongofya kwa kukiri kwako, umedanganya kwamba nilikiri kushindwa bila aibu ili tu uukimbie ukweli!!!

  Bado hujalijibu swali langu, umekuja na maelezo meeeengi yasiyo na maana, wewe nipe tu jibu la swali langu na kama huna jibu basi sema hivyo, kwamba hukijui ulichokisimamia, ulikuwa unajiandikia tu na kubandika vifungu visivyo na uhusiano wowote na tunachokijadili!

  Ninakuomba, kwa heshima ya majadiliano, nioneshe ni wapi Agano Jipya linafundisha kuhusu Uzinzi na Adhabu yake; na wapi linafundisha Msamaha wa Wazinzi?

  Asante sana ndg yangu, ninakusubiri mwalimu wa viziwi!!!

 12. Ndugu Lwembe,

  1.Napenda nikushukuru kwa sehemu, pia nikuhimize/nikuonye.
  -Nashukuru kwani uliona kam kusema ndiyo au hapana ni scientific. Umejitambua, na ulipojipima ukakuta wewe si mkweli. Ukaona kusema ndio au hapana utakuwa ukijitia kamba shingoni kufwatana na hili andiko : « Yakobo 5 : 12 Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; BALI NDIYO YENU NA IWE NDIYO, NA SIYO YENU IWE SIYO, MSIJE MKAANGUKIA HUKUMU. ». Umeingiwa hofu ya ajabu ya kuhukumiwa ndipo ukakosa useme nini, halafu ukaamua kusema uongo kama hayo maswali ni scientific. Ila tu ulisahau kama uongo nayo ni dhambi ipelekayo mautini.
  -Nakushawishi kutobaki ndani ya hiyo hali, nikikuhimiza kujifunza kusemesha ukweli ili usiogope unapoambiwa ujibu kwa kweli. Ndiyo maana unaendelea kwepa maswali kwa kushindwa kusemesha ukweli, jambo ambalo sikutakie kuendelea zama ndani. Hebu, fikirini, ni yupi mukristo asiyetambua kilichokweli, asiyejua kusema NDIYO kwa kweli na HAPANA kwa kweli ? Hayo maswali niliyokuuliza ujibu ndiyo au hapana, uliendelea kuyakwepa, mimi nikawaza kama umesahau, sasa nimetambua umeyakwepa kwa kutaka tu. Tena naona unaendelea kwamisha mada ; hizo ni dalili za matukio mabaya.

  2. Lwembe, vaa vizuri kofia yako. Uko muandishi lakini uchambuzi wa maneno huna. Unaandika kama robot. Unajichanganya tu ku neno motoni! Nani asiyefahamu kama ukisema motoni ina maana ni ndani ya moto. Sasa wewe unakimbilia kutofautisha moto wakati ulitakiwa kujua kam moto ni ile ile, lakini kiwango cha kuwa ndani ndicho kinakuwa kawaida ndani au ndani zaidi. Pia hueleweki wakati kila mara unaogopa kujibu kiisha unauliza unayo tayari. Si hiyo shairi inaongea dhambi kubwa na kubwa zaidi ? Kiisha uulize eti imeandikiwa wapi ? Kuna kikubwa zaidi kama hakijawa kikubwa ? Lwembe, try to be honest !!! Pia unapozungmzia moto unalinganisha makaa na furnace, heuh! Utatiwa ndani kiisha hutaungua? Na mwisho ni kufa tu…. Ndio maana dhambi hupimwa kwa final adhabu yake.

  3. Sijue kwa nini unarudilia neno « kufundisha uzinzi » ! Ina maana hapa uko unafundisha watu uzinzi? Wakati unapoandika unachunguza au unakurupuka tu? Nilikuambia Injili inahubiriwa. Torati ndiyo inafundishiwa. Nimekuhubiri ukatubu, sasa kama unataka nikufundishe na hiyo torati, unatakiwa hakikisha wewe ni mkweli kwa kuweza kijibu kwa hiyo maswali kidogo. Kuambia Lwembe aache uongo sitakiwe kuchelewa kuonyesha kama torati inasemaje, kama asemae uongo anauwawa au la. Lakini namuwekea neno kama hili lipatikanalo ndani ya agano jipya:” Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na WAONGO WOTE, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. Hii ndiyo mauti ya pili. »

  4. Yooooo! Lwembe, kumbe hujaelewa kama Injili ni rohoni? Wewe unaitafutia kichwani, kwenye akili. Naona kinachokuleta kushindwa kuwa mkweli. Akili zako za uandishi zinakubomoa bongo, na roho yako unayidharau ukizimisha vilevile Injili ambayo inlitakiwa kubaki ndani.

  5. Unataka niandike ulipokiri kwamba umeshindwa!
  « Ck Lwembe 04/01/2014 at 9:03 PM
  Ndg Ziragora,
  Nimefurahi kukuona tena ktk Mwaka Mpya huu! Ni mategemeo yangu kwamba umeongezeka katika umri na hekima!
  Jambo la kwanza nisilopenda kuingia nalo ktk Mwaka huu Mpya wenye matumaini makubwa ni hali yangu ya “Kuwekwa Jela”; kwahiyo ninakuomba unisamehe “Uongo wangu” na “UJINGA WANGU” WOTE; PIA UKUPOKEE KUSHINDWA KWANGU KUYAJIBU MASWALI YAKO KAMA CHANGAMOTO YA KUZIDI KUNIFUNDISHA HAYO NILIYOYASHINDWA ILI WOKOVU UNAONITAMANIA UNIFIKIE NA NIWEZE KUUFIKIA UFAHAMU KAMA WAKO KTK HAYO UNAYONIFUNDISHA NA MENGINEYO UTAKAYOYALETA!
  Pia, ninatarajia sasa kwa kuacha “Uongo wangu”, wana SG wote wanafuraha kubwa kama ulivyosema au unavyotaraji, kwa uhakika kabisa najua walio na furaha ya kupitiliza watakuwa ni Seleli na Sungura na Mabinza, pamoja na wote, nawaombeni radhi nyote!
  Basi kwa imani nikiwa nimekwisha kutoka “Jela”, ninakusubiri ndg yangu Ziragora, uniweke sawa katika hayo niliyokuuliza pamoja na majibu sahihi ya maswali yako ili tuendelee kujifunza!!!
  Ubarikiwe ndg yangu!!! »

  Hii ninayobandika uliitia katika mada ya kiingilio lakini uliiweka in general kwani munamo mambo mengi ya hii mada. Kama unawezaondoa maneno fulani, sitakuzuiza, uko huru. Mim niliyapokea bila kukusumbua, kukuuliza kwa nini ulichanga yote mbili, kwani hudaiwe kuandika hapa na pale neno unalotakasema at once.

  6.Unasema « Nimekuomba unioneshe ni wapi Agano Jipya linafundisha kuhusu Uzinzi na Adhabu yake; na wapi linafundisha Msaha wa Wazinzi? Punguza kunizungusha kwa maneno na maswali yasiyofundisha! »
  Sasa ukiona ninayoleta haifai kwa kufundisha, pia unaniomba nikufundishe nikileta unayoita «NONDO», wewe unaona una akili timamu kabisa? Lwembe, nenda kwa shule la viziwi au ubaki na kushindwa yako.

  Asante.

 13. Ziragora,

  Umenifurahisha saaaaaaaana!
  Yaani umejiaminisha kabisa kwamba mimi na wewe akili zetu ziko sawa; kwamba nawe kama mimi umepasuka kichwa kwa akili mingi!!! Yaani Injili imekushinda sasa unakuja na maswali “premeditated” eti nijibu NDIO au HAPANA! Hahahahahaha..!

  Maswali uliyoniuliza ni more scientific kuliko unavyodhani!
  Ukisema “Motoni” inaweza kuwa burning temperature yoyote ile, lakini ukiongeza “Motoni Zaidi” hapo unakuwa umeyaingiza mambo mawili katika comparison; motoni inaweza kuwa jiko la mkaa na motoni zaidi inaweza kuwa ndani ya furnace!!!
  Basi ukiyaona hayo kuwa ni sawa, hilo ndilo tunaita “ufahamu wa chini” ktk lugha!

  Halafu unaniambia,
  “Almradi, kila dhambi ni kubwa; sasa wewe unaefahamu zaidi tafuta kam huko jehanum kubwa zaidi itatiwa ndani ya chumba gani.”

  Hivi ni wapi Biblia inasema kuwa “kila dhambi ni kubwa”? Kwamba wenye ‘Dhambi Kubwa Zaidi’ watatiwa chumba gani, hilo kwako sidhani kwamba lina umuhimu, kama umeshindwa kuamini kwamba kuna Dhambi Kubwa Zaidi, hata Mungu akishuka akuoneshe, HUTAAMINI almradi umeshindwa kuliamini hilo dogo alilokuonesha!

  Kuhusu Agano la Kale na Jipya, hebu jaribu kuchunguza nyumba inavyojengwa labda utaelewa! Hakuna Agano Jipya bila la Kale!!! Huwzi ukapaua nyumba bila kujenga Msingi, huo ndio unaoibeba nyumba. Agano Jipya limejengwa juu ya Msingi wa Agano la Kale; nao Msingi wa mafundisho ya Uzinzi uko katika Agano la Kale, huko ndiko mambo hayo yamefundishwa; Uzinzi ni nini!!

  Katika Agano Jipya Uzinzi unarejewa katika msingi wa Agano la Kale, wakirejewa Wazinzi tu, wigo ukipanuliwa. Msingi wa Dhambi uko ktk Sheria. Hizi tambo unazoleta sioni hata maana yake. Naona ni mtu aliyeshindwa kutimiza ahadi yake na sasa anazungusha akili za watu kwa vitu asivyovielewa!

  Nimekuomba unioneshe ni wapi Agano Jipya linafundisha kuhusu Uzinzi na Adhabu yake; na wapi linafundisha Msaha wa Wazinzi? Punguza kunizungusha kwa maneno na maswali yasiyofundisha! Kukubali kwangu au kukataa kunategemea utakayoyafundisha kuhusu hayo unayoyauliza kuhusiana na jambo tunaloliongelea!

  Halafu unaniambia kuwa “-Hili jambo la uzinzi liko katika makala ambayo ulikiri kuwa umeshindwa.” Unaweza kunikopia na kupaste hapa hilo unalosema nilikiri, nitafurahi maana sikumbuki kabisa jambo hilo!

  Asante ndg yangu ninakusubiri katika hayo uliyoyaahidi, LETA NONDO!!!

 14. Sungura,

  Lugha kama lugha haijawahi kuwa tatizo, tatizo mara nyingi huwa ni Ufahamu au Understanding, ambayo huivuka lugha! Ni lazima u blend na spirit ya anayeongea ili umuelewe katika anachokisema sawa sawa; uinase sauti na gestures zake, hata ikiwa ni katika Maandiko!!! Yaani u blend na Spirit ya Mungu!!!! Ujue what is God at, what is He saying? Etc!

  Umeniuliza, kuhusu kauli yangu, “”‘Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu” ‘, kimuundo ni sawa na sentensi inayosema ‘wokovu ni matendo’?””
  Jibu la rahisi ni SAWA! “Faith without works is DEAD” James 2:20 “…O vain man…”!!! Wokovu hauji pasi Imani, nayo Imani hudhihirika katika matendo; basi tusemeje, kwamba matendo ya mwokovu yaweza kuwa nje ya Imani? Mimi ninaamini kwamba matendo ndiyo yanayoutangaza wokovu wako, hayo ndiyo waraka usomwao na si kelele zetu! Yn 14:12 “12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.” Tazama alipokwenda kwa Baba yake nini kilimtokea mwaminio hata aweze kuzifanya kazi hizo!

  Otherwise nimetatizika kidogo kwamba haulewi concept ya kwamba “Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu”! Roho Mt ndiye ALL of IT; yeye ndiye Mfumo mzima wa Ufalme, yeye ndiye kiongozi na mwaminio! Ukimchukua paka ukamuoperate on na kumuwekea roho ya mbwa, definitely atabweka kama mbwa; basi RM akiwa ndani yetu inakuwaje? Msikilize Kristo hapa kama unaweza kudaka kitu, Jn 14:10:
  “Believest thou not that I am in the Father, and the Father in me? the words that I speak unto you I speak not of myself: but the Father that dwelleth in me, he doeth the works.”
  Hivi ndivyo inavyokuwa kwa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili!

  Juu ya hayo ongeza na na hili ktk “your understanding” of the Kingdom issue, Lk 17:21:
  “Neither shall they say, Lo here! or, lo there! for, behold, the kingdom of God is within you.”
  It just can’t be different!!!!

  Gbu!

 15. Ndugu Lwembe,

  Pima tu jibu kwa hizo swali zangu nilizokuuliza kujibu ndio au hapana. Kama hunizuize pale pale nami nitakufundisha SANA kusamehewa kwa dhambi hiyo ya kifo (uzinzi) ktk agano la kale na KIDOGO ktk agano jipya kwani ktk agano jipya hutiye mkazo sana.
  Tuendelee, kiisha tuone ni nani atakaekwamisha mada.

  AMIN, nakwambia ubarikiwe.

 16. Lwembe,

  Hata mimi nitafurahi kama utanionesha katika agano jipya mahali ambapo panasema mkristo ikitokea amezini basi hawezi kuitubia dhambi hiyo!

  Nafikiri kuanzia hapo tutajifunza kitu kizuri zaidi/

  Mimi msimamo wangu katika hii mada ni kwamba, dhambi zote si sawa mbele za Mungu. Na kipimo cha kwamba si sawa ni yale matokeo yake, na namna yake ya msamaha.

  Lakini pia biblia kuna sehemu zingine imesema kuhusu kipimo/viwango. Eg dhambi/ uovu mkubwa, dhambi nyekundu kama bendera!

  Barikiwa.

 17. Lwembe,
  Dah, kweli haya ni maajabu!

  Unajua baada ya kuona umerudia kugusia suala la kwamba ufalme wa Mungu ni Roho mtakatifu, nimepata shauku kusoma nione kuna nini kipya kizuri umesema.

  Nilpokuta ulichosema na maneno mengine mengi, yakiwemo ya kuniponda kuwa niko nyuma kiufahamu labda kwa sababu ya kujichanganya kwangu na Elimu za biblia, nimeishia kupigwa butwaa na kusikitika.

  Pengine ni tatizo la lugha;

  Hebu niambie, hiyo sentensi yako kwamba ‘Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu” ‘, kimuundo ni sawa na sentensi inayosema ‘wokovu ni matendo’?

  Au uliposema Roho mt nduye ufalme wa Mungu, ulikuwa unamaanisha kuwa bila Roho mt. hatuwezi kuifanya kazi ya Mungu, kama ulivyojaribu kufafanua hapo juu?

  Hapa unasema ”Roho Mt. ni Kristo ndani yako! Basi Ufalme wa Mungu ndio jambo hilo, hiyo ndiyo chapa ya Ufalme huo”

  Ni kweli Roho mt. ni Kristo ndani yangu, nakubali, na kwamba Roho mt. ndio chapa ya ufalme , nakubali.

  Lakini kwamba Roho mt. ndiye ufalme, huo ni uongo mkubwa Lwembe.Ufalme wa Mungu maana yake siyo Roho mt. Ufalme wa Mungu ni ufalme wa Mungu (ni mfumo), na Roho mt. ni Roho mt. Yeye ndiye anayetuwezesha kutenda kama ufame wa Mungu unavyotaka tutende.

  Umeniuliza kuhusu Mathayo 28:20, naona ni swali la kitoto sana. Lakini jibu lake ni kwamba walikuwa hawakuwa na nafsi mbili ndani yao!

  Kutokuweza kwetu kifanya kazi ya Kristo bila Roho mt. haimaanishi kuwa Roho mt. ndiye ufalme wa Mungu.

  Ni vema tu Lwembe ukakiri kuwa ulikosea au ukanyamaza tu kimya. Maana hata maelezo yako ya sasa haya-justify kuwa Roho mt. ndiye ufalme wa Mungu, bali yanaoneshe tu jinsi tunavyomwitaji Roho mt. katika ufame wa Mungu.

  Maana ya Roho mt. siyo ufalme wa Mungu!

  Amen!

 18. Ndugu Sungura,

  Nafika kukutakia Happy New Year 2014.
  Pia sitajizuiza kukuambia kam ktk makala yako ya 07/01/2014 umechapa Injili safi. Mungu Akubariki.
  Kumbe zambi zisizosamehewa si lazma ziwe zile ambazo watu wanaona ni nzito nzito. Anania alidhani kwa kudanganya anatenda ile ambayo watu wengine wanaita ndogo kumbe amenaswa na dhambi ya mauti. Alidhani anadanganya mtu kam yeye kumbe anadanganya RM
  Alie na sikio asikie.

  Mungu akuongezee maarifa.

 19. Ndugu Lwembe,

  Asante kwa kunijibu ndugu yangu.

  -Lwembe, heeh! kwa nini mzaa namna huu ?
  Wewe Lwembe ambae umejulikana kuwa mtaalamu wa kuandika lugha !!!!!!!
  Hivi ni kweli, ni kweli, ni kweli na imetoka kichwani mwako utegemee kama tamko « kubwa » na « kubwa zaidi » ni vocabulary gumu? Ikusukume kuijivunia na kunitukana mimi? Hivi uko honest kabisa? Au utaalamu wako umekupasua kichwa, Lwembe!!!

  OK, sasa ongea:
  Je Alie motoni na alie motoni zaidi hawako wote motoni?
  Je Alie na umri wa miaka 20 na 30 wote si vijana?
  Je Alie mpumbavu na aliye mpumbavu zaidi, wote si wapumbavu ?

  Najua tuko tofauti sana kwa points nyingi. Lugha haiwezi kuwa tatizo kwani ninaweza andika ktk lugha nipendayo. Tofauti kubwa iko ktk kutulia na uweza wa kupekua maneno. Mara kwa mara unakurupuka tu kama mtoto anaelota akiruka na mabawa. Unapojibu, huheshimu andiko la mwenzako (kwa mfano mtu anaposema hiki kitu kinafanana kile wewe unageuza eti alisema hiki ni kile). Unageuza kila mara tunayoandika ili uonekane wewe ni sahihi kuliko wote. Unapogeuza sana unafikia kiwango unabandika negative form ya tamko la mwenzako. Ndivyo ulivyo lakini sitafwatilia hiyo mambo wakati hujajadili mingi mara tu unapotubu uongo.
  Sasa usisingizie vocabulary. Unapozungmuzia neno unatakiwa ulitie ndani ya mazingira yake. Hapa tunazungumzia dhambi isiyosamehewa na inayosamehewa, ya mauti na isiyo ya mauti. Mim ndimi nilileta shairi hii ambayo imekuhangaisha siku nyingi. Nimeileta nikiwa na akili timamu. Sasa usijifiche ndani ya vocaburary. Tunayoongea ni mambo ambayo ni opposite. Lakini dhambi kubwa siyo opposite ya dhambi kubwa zaidi. Wewe pengine unataka tupoteze mada!

  Ninairudilia kam nilivyosema: kilicho kikubwa na kilicho kikubwa zaidi vyote ni katika kundi ya vikubwa. Una masikio?

  Almradi, kila dhambi ni kubwa; sasa wewe unaefahamu zaidi tafuta kam huko jehanum kubwa zaidi itatiwa ndani ya chumba gani.

  -Hili jambo la uzinzi liko katika makala ambayo ulikiri kuwa umeshindwa. Siwezi kurudisha nyuma. Tutaiweka pamoja na zile swali, nikikuletea jibu uliloshindwa kupata. Usikate tamaa ungoje tu, ni kwa faida yako, tulia. Tutaongea mingi, wala si katika agano jipya tu, bali ktk biblia yote. Ninayotaka mimi pengine haitakupendeza lakini mim napenda utaratibu. Kuandika kam anaepika nyama na samaki chungu moja ni kuchanganya wasomaji.

  -Ila tu niseme juu ya Agano jipya pasipo neno uzinzi kwanza na majibu yako itaniruhusu kukuletea lile somo linalohusu uzinzi, hapo tukifahamu kam hiyo ni kipengele kimoja tu ktk hii mada.
  Jibu ni ndio au hapana, sikuombe tafsiri, nakuomba kunifahamisha tu. Na kama inaomba andiko la kibiblia ndipo uamue, uniambie. Kwani, kwa kweli ninakushangaa namna unavyoshikilia makala hii.

  -Je niliposema Agano la kale linachakaa ni kweli au la ?
  -Je niliposema Agano la kale liko excellent na lile jipya more excellent, unakubali ?
  -Je niliposema dhambi zote na adhabu ziko defined ktk agano jipya, unakubali ?
  -Je niliposema Yesu ali fulfill agano la kuchakaa akilifanya agano lisilochakaa, unakubali ?
  -Je niliposema kama Yesu si torati bali ni bwana wa torati, unakubali ?

  Lwembe, hii maswali yote na mengine iko katika jibu langu ambalo unadharau. Hebu unipe jibu pasipo tafsiri ili nijue kam ulisoma niliokuandikia au la ! Sidhani kam makala inaweza kuwa empty kama iko na hoja kama zile.

  Asante ndugu yangu

  Jesus bless you.

 20. Sungura,

  Hapo nyuma, niliposema kuwa “Ufalme wa Mungu ni Roho Mtakatifu” ulinishangaa sana! Ngoja nikunukuu:
  ‘’” Kuna hili hapa nalo nimeshangaa sana jinsi ulivyolisema kwa ujasri kuwa, ”Kwa kukusaidia, Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu”
Kabisa, unataka tuwaamnishe watu wanaofuatilia michango yetu hapa kuwa Ufalme wa Mungu ni Roho mtakatifu?
  Hebu tufikiri hivi:
  Roho mtakatigfu ni nafsi – kwa hiyo ufalme wa Mungu ni nafsi!

  Roho mtakatifu ni msaidizi wetu – kwa hiyo ufalme wa Mungu ni msaidizi wetu
Roho mt. ni mwalimu wetu – kwa hiyo ufalme wa Mungu ni mwalinmu wetu.

  Huyu ni mwalimu Lwembe anatufundisha hivyo!!!

  Ukimuuliza nani kamfundisha hayo, yawezekana akakwambia ni Roho mt. ndo kamfundisha, kwa sababu namjua ni mtu ambaye yuko kinyume kabisa na elimu ya biblia!!!
  Kwa mimi huu ni mzaha mkubwa sana!!!!””

  Maelezo yako haya yanathibitisha kwamba bado uko nyuma kidogo katika ufahamu! Huenda ni kutokana na kujichanganya kwa Elimu za Biblia, maana kwa sehemu kubwa Elimu hizo huwa ni mawazo ya watu kuhusu vifungu vya Biblia, ndipo ukiyameza bila kipimo, basi unaishia katika ufahamu kama huu ulionao!

  Kwa taarifa yako hakuna anayeweza kuifanya kazi ya Mungu bila kwanza kujazwa RM! Hata kuyaelewa Maandiko kunamuhitaji RM! Kristo alikuwa ni Mtume, na ni Nabii, tena ni Mwinjilisti, Mchungaji na Mwalimu kwa kusanyiko lake! Ndipo vipawa hivyo ameviweka katika makusanyiko yake ili kuuendeleza uwepo wake katikati ya watu wake, hajawaacha wakiwa (Efe 4:11)! Huduma Tano hizi ndizo zinazo mdhihirisha Kristo katika kusanyiko!!! Kanisa ambalo HALINA Huduma Tano hizi litakuwa linaongozwa kwa Liturgia au misisimuko ya vipawa, au kwamba ni Cult tu! Roho Mtakatifu alipo ni lazima ajidhihirishe katika Huduma hizo. Kuombea wagonjwa au kunena kwa lugha hakuwakamilishi Watakatifu. Wako wengi sana walioponywa na Kristo na kuyaona Matendo Makuu yaliyoahidiwa kumhusu yakiwatimilia machoni pao, lakini ndio hao hao waliopiga makelele wakimtaka Baraba muuaji!!

  Roho Mt ni Kristo ndani yako! Basi Ufalme wa Mungu ndio jambo hilo, hiyo ndiyo chapa ya Ufalme huo; ukiisha kujazwa RM ndipo unapopewa Mamlaka, kazi alizozifanya Kristo nawe utazifanya, na kubwa zaidi! It is this simple, na si mambo magumu mnayojibebesha mpaka mnakosa ufahamu kwa kulemewa! Tazama unachotaka kutufikirisha ambacho hata wewe mwenyewe kimekushinda:
  “Roho mtakatifu ni nafsi – kwa hiyo ufalme wa Mungu ni nafsi!”
  Basi kama ndio hivyo kwamba RM ni nafsi, hebu nifafanulie Andiko hili ktk Mt 28:20 “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” naye Kristo akiwa ni nafsi, je, ndio kusema wanafunzi wa Yesu walikuwa na nafsi mbili ndani yao, ya Yesu na ya RM?? Mimi nadhani “huu ndio mzaha mkubwa sana!!!!”

  Gbu!

 21. Sungura,

  Kuhusu kulitumia jina lako katika mfano nilioutoa, well, utakuwa umekwenda overboard kwa bitterness! Unisamehe! Sikufikia kuwaza kwa jinsi ulivyoyapeleka mawazo yako, I’m real sorry!!! Lakini pia unapaswa kujua ya kwamba jina “Sungura”, wako watu wengi sana wenye jina hilo, na si lazima sana uwe wewe, ninaamini ukweli huo ungekuondolea bugudha na uchungu uliokupata over a light issue!! Hata hivyo, kindly NOTED!

  Tukirudi ktk mada, unaniambia,
  “Unalazimisha kusema kuwa dhambi ya mauti aliyosema yohana ilikuwa ni dhambi ya uzinzi ati kwa sababu kwenye torati uzinzi adhabu yake ilikuwa ni kifo, ni kutoa uchambuzi wenye upungufu mkubwa.”

  Jaribu kutulia unapotaka kuzungumza jambo! Kifungu hicho cha Yohana nilikirejea ili kukudhihirishia kwamba Dhambi zote si sawa kulingana na Maandiko ambayo ndio Kiongozi tunapojadiliana! Na katika mjadala huu tulifika mahali tukawa tunazungumzia “Uzinzi”, ndipo mimi kulingana na Maandiko, ninaelewa hivyo kwamba Dhambi ya Uzinzi ni ya Mauti kwa mkristo! Na kama Uzinzi unaweza kutubiwa, ndio nimekuomba unioneshe ni wapi lilipo Fundisho hilo. Nilikutegemea sana uje na Maandiko yanayolionesha jambo hilo, lakini badala yake umenijia na Orodha ya Dhambi za Mauti, sijaona mahali popote pale tulipozungumzia “Orodha” ya Dhambi za Mauti, wala kukinukuu kwangu kifungu hicho ktk Yohana, haikuwa ktk kulazimisha Dhambi ya Uzinzi, kuwa ni ya Mauti kama unavyosema, labda wewe ndio unataka kuwadanganya wakristo kwamba wanaweza kuutubia Uzinzi!!

  Usiwe kigeugeu, tena wewe ndiye uliyeikazia mada hii katika Uzinzi hapo ulipoulinganisha na mwizi wa shilingi mia! Tazama swali uliloliuliza huko nyuma,
  “Tujaribu tu kujiuliza, Aliyeiba shilingi mia, na aliyezini ikatungwa mimba usawa na utofauti wa dhambi zao mbele za Mungu unaupimaje?”

  Ulipozungumzia “mbele za Mungu” ndio nikakuletea jinsi ya kiMaandiko kuhusu Dhambi hizo (hiyo Yohana), na Mungu alivyozielezea katika Torati kwani huko ndiko Dhambi inakofunuliwa, ili ujionee mwenyewe kama Dhambi zote ni SAWA? Conclusion ya jambo lililowekwa wazi ni ya mtu binafsi, ukiona Torati haikuhusu, haya, la inakuhusu, basi utajifunza na itakuwa ni akiba yako ktk maisha yako ya wokovu!! Tunayo hiari ya kuupokea UPOFU au EYESALVE!

  Bado nitafurahi iwapo utanionesha Agano Jipya linapofundisha kuhusu Uzinzi na Adhabu yake na Msamaha wake!!!

  Gbu!

 22. Ndg Ziragora,

  Ninakushukuru kwa maelezo yako.

  Kwa kadiri ya uelewa na ufahamu, naona tumetofautiana katika jambo la msingi, LUGHA! Unaponisisitizia kwamba “KUBWA” na “KUBWA ZAIDI” yote ni sawa, hilo linanifanya nishindwe kukuelewa haswa una maanisha nini, kwamba ni kwa makusudi unaivuruga maana ya maneno, au ni kwamba vocabulary yako ni ndogo? ‘Kubwa’ na ‘kubwa zaidi’ hayawezi kuwa sawa, vinginevyo, basi lugha imepoteza maana!

  Pia, kuhusu Agano la Kale na Agano Jipya, maelezo yako kuhusu “Uzinzi” naona ni maelezo ya mtu anayejitetea zaidi badala ya kulifunua hilo unalolijua ili wanaotusoma wawe wametendewa haki. Nimekuuliza swali jepesi sana, ni wapi Agano Jipya linapofundisha juu ya Uzinzi na Adhabu yake, na linapofundisha Msamaha kwa Wazinzi? Nioneshe hayo Maandiko kwanza badala ya maelezo yasiyojengeka katika Msingi wa Neno la Mungu!

  Hebu na tuyatazame maelezo haya yanayohusu Uzinzi ktk A/Jipya, Mt 5:27-30:
  “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.”
  (Jehanamu si mbinguni, na wala si uliko Uzima wa milele!)

  Nayo hukumu ya Mzinzi, huyo aliyeivunja Amri ya Saba, ktk Agano lililochakaa, hii hapa ktk Law 20:10:
  “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.”
  Kuna AHUENI gani kwa mzinzi wa A/Jipya? Labda uwe hujui Dhambi hiyo inaongelewa kutoka wapi na uwe hujakielewa anachokirejea Kristo!!!

  Ninachokiona mimi ktk Agano Jipya ni kupanuliwa kwa wigo wa kuwanasa wazinzi na si wao kupewa ahueni yoyote ile! Kwamba unanitaka nikuoneshe “katika agano linalochakaa mahala waliweka adhabu ya mtu aliyetamani mke wa mwenziwe!” hilo haliwezekani kwasababu ni kinyume na Maandiko. Ukiisoma vizuri hiyo Mt 5:27, utaona kwamba jambo unaloniuliza linahusiana na KUTIMILZWA kwa hiyo Torati, “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini”; hii ndiyo Torati, Yesu anarudi huko nyuma kuyachukua yanayohusu jambo hilo, ambapo Amri ya Saba ndiyo hiyo anayoirejea kwa wanaoijua Sheria na Adhabu yake (Law 20:10), kisha anaupanua wigo, sasa akiitoa Sheria hiyo na Adhabu yake kutoka mwilini na kuiingiza Rohoni, ndio maana anakwambia kuhusu JEHANAMU, hakuna mtu anayeweza kumpeleka yeyote yule huko, ni Mungu pekee! Usitegemee kumuona mtu wa kumpiga mawe mzinzi leo hii!!!

  Agano Jipya linawaingiza Rohoni wenye kuijua Sheria, ndilo linalowakamilisha wakiisha kupelekwa huko na Torati, ndio maana imeandikwa, Gal 3:24, “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo”; basi utaijuaje Neema bila Sheria, utakuwa unaimba tu!

  Sheria ndiyo inayotutambulisha Dhambi, kuikataa Sheria ni sawa na na kumchukua simba aliyekulia zoo na kumtupa porini, huyo ataliwa hata na fisi! Basi Mkristo aliye imara ni yule anayeijua Dhambi kikamilifu, huyu ndiye Torati humfikisha kwa Kristo ili aipokee Neema ya Kuishinda Dhambi, yaani RM, ndipo ile Rum 10:4 humtimilia, “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria”. Nako kuwa Mwisho wa Sheria, maana yake rahisi ni kule KUTOKUTENDA DHAMBI anakokufikia Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, huyo anayeongozwa na RM akimdhihirisha Kristo!

  Ninakushukuru Ziragora, kwa kadiri ya kujifunza!

 23. Lwembe,

  Kuna mambo mengine huwa inabidi tu kuonesha uvumilivu na ukomavu wa kiufahamu, lakini huwa ni ya kipumbavu yanapojitokeza katikati ya watu wastaarabu.

  Naweza nikaona upuuzi uliokuwa katika kichwa chako mpaka ukaamua kunitolea mfano hasi wa kutembea na mchumba wako, tena ukiniita ‘jeuri’. Kwa nini hukumtolea mfano kaka yako au mdogo wako kama ilikuwa ni azima utaje jina la mtu kwenye mfano wako.

  Please, hakikisha adabu haikosi kuwa ndani ya makala zako. Kubishana kwa hoja tubishaneni tu, lakini tusikoseane adabu na staha katika maneno yetu. Ukiona kuwa huwezi kujizuia kuandika maneno ya dhihaka kama hayo, basi tulizana kwanza ili baadae akili ikitulia baadae uweze kuchangia kwa utulivu zaidi.

  Unalazimisha kusema kuwa dhambi ya mauti aliyosema yohana ilikuwa ni dhambi ya uzinzi ati kwa sababu kwenye torati uzinzi adhabu yake ilikuwa ni kifo, ni kutoa uchambuzi wenye upungufu mkubwa.

  Kwani ni dhambi ya uzinzi tu ndo ilikuwa adhabu yake ni kifo kwa mujibu wa torati, kwani aliyeua adhabu yake ilikuwa ni nini, aliyevunja sabato adhabu yake ilikuwa ni nini?

  Lwembe unatakiwa uitazame dhambi ya mauti kwa picha ya mifano michache iliyo kwenye agano jipya.

  E.g;
  Kuna dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu – Matt. 12:31-32

  Kuna dhambi walifanya Anania na Safira – Acts 5:1-3, 5, 7-10

  Kuna aina fulani ya zinaa walifanya wakorintho – 1 Corinthians 5:1-5

  Dhambi za namna hiyo ndo dhambi za mauti. Ukiangalia vizuri unaweza ukaona kuwa dhambi ya mauti inaweza ikawa yoyote ile kulingana tu na namna ilivyotendwa, na hadhi pia ya mtu aliyetenda!

  Thank u!

 24. Ndugu Lwembe,

  Usiwe mtu wa mzaha ktk Neno la Mungu.

  -Nadhani haihitajiki kuwa msomi ili ufahamu kam kilicho kikubwa na kilicho kikubwa zaidi vyote ni katika kundi ya vikubwa. Mwandishi yakushindwa kuandika kale kaneno “ndogo”. Hata asiye wa kiroho anaweza sikia masemi haya kirahisi. Ni kama jinsi mtu angeliambiwa ataingia motoni na mwengine motoni zaidi. Unafikiri kwa upande wako ukiwa motoni utajisifu kwani wewe si ndani zaidi?

  -Hakuna nafasi nilipokushurtisha kunijibu. Kwani ukiwa mtu mzima hulazimishwe kujibu kwa ujinga ili ujibu tu. Nilikuambia wazi hivi : kama huna jibu linalofaa usitafutishe bali ukiri upungufu na tuendelee na mengine pamoja na kukusaidia ulipopungukiwa. Mimi nafikiri hutakuwa umepoza chochote kwa sababu wakati nami nitakapopungukiwa utanisaidia. Lakini usipoweza jitambua itakuwa vigumu uwe na uweza wa kusaidia mtu mwengine. Na kam huna jibu lisilo la ujinga na hupendi msaada yoyote unyamaze kimya, usilete fujo.

  -Nilikuambia kam agano jipya liko very (more) excellent. Linaonyesha adhabu ya uzinzi na dhambi zote kwa namna iliyo more excellent na ya kiroho; nimeirudilia kwa namna hiyo tu mara mingi. Labda ungelisoma tena nilioandika kama umesahau. Mim naona si vema kunipotezea mda ukinishurtisha kurudilia neno ambalo ni rahisi kusikia wakati ninaemuandikia anajifanya kiziwi.

  Lwembe, hapa si uko ukijibu kwa hoja yangu ambapo nilikuonyesha vizuri kama Mkubwa wa agano jipya, Yesu Kristo, ali define kwa jinsi ambayo ni very excellent dhambi ya uzinzi na adhabu yake akileta ufafanuzi juu ya tendo na tamaa, wakati agano la kuchakaa lilishindwa ambatanisha hayo mambo mawili licha ya kuwa yote yanapatikana katika zile amri kumi za Mungu, nikakuonyesha kama kulikuwepo upungufu kwani adhabu ilitegemea licho ya mwanaadamu, nikakuomba kuonyesha katika agano linalochakaa mahala waliweka adhabu ya mtu aliyetamani mke wa mwenziwe! Sasa utaniambia hii unayoandika ndilo jibu? Si ile mtindo wako wa kukwepa hujaipona tu, Lwembe? Huwezi kabisa kujihukumu mwenyewe ili usihukumiwe? Unaposema mimi nina majivuno, acha nijivunie Yesu alietuletea agano lisilochakaa. Au unataka sema kam na wewe unajivunia torati inayochakaa na karibu kutoweka!!! Kama hujitambue utatoweka nayo!!!

  Asante kwa kuacha mzaa, na Mungu akusaidie..

 25. Ziragora,

  Naona unajizungusha kwa maneno mengi mpaka umesahau hata uliyoyafundisha!

  Nimekunukulia Maandiko yanayotufundisha kwamba Dhambi inahusikana na Sheria (Torati), Rum 5:13
“… lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria”
  Basi hebu jiulize, Neema inaitoa wapi Dhambi kama si katika Sheria?

  Usiwe mbishi wa tabia!!!
  Mada inauliza iwapo Dhambi zote ni sawa? Hebu lirejee jibu lako ulilolitoa:
  “”Ukweli kamilifu ni kwamba Biblia haijawai kutuambia kuna dhambi kubwa na dhambi ndogo. Inasema kuna dhambi zilizo kubwa zaidi. “Yohana 19:11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.”
Zote tuseme ni kubwa kwani iwe kubwa au kubwa zaidi, inayoanekana ni kwamba ni kubwa.””

  Sasa kama Biblia inasema “Dhambi Kubwa Zaidi”;
  halafu wewe unatuambia,
  “iwe kubwa au kubwa zaidi, inayoanekana ni kwamba ni kubwa”,
  Je, haujioni kwamba roho anayekuongoza si huyo aliyezitofautisha hizo Dhambi? Hii ni dalili mbaya, kuzichanganya Dhambi!!

  Pia nilikunukulia Torati inachokifundisha kuhusu Uzinzi, naona UMEIKATAA, ukisema kwamba huko ni kuambatana na mauti. Ndipo ninakuomba unioneshe ni wapi Agano Jipya linapofundisha juu ya Uzinzi na adhabu yake, na linapofundisha Msamaha kwa Wazinzi?

  Kuhusu maswali yako nilikwisha kukujibu nawe ukasema ni majibu ya mtu mjinga, basi unapotaka nikupe majibu mengine ya kijinga ndiyo nakushangaa; kwamba yawezekana nawe ukawa ni mjinga mara mbili yangu????

  Ifukuze hiyo roho ya PRIDE, ni hatari tupu!!

  Ubarikiwe tunapouendea Mwaka Mpya!

 26. Ndugu Mabinza,

  Ukweli unasemwa pasipo kigugumizi na tamko hupatikana kirahisi.
  Sione niongeze nini kwa hoja yako isipokuwa kukuambia kam umechapa injili na Mungu akuongezee maarifa.
  Ila pale ulipoandika wa Ebr. 8:26, nadhani ulipenda andika wa Ebr.10:26. Hii ni kusaidiana tu, naitia kwa yule atakaesoma. Wakati atakapokosa huo msatari aupate hapa.

  Happy New Year , my brother.

 27. Ndugu Lwembe,

  Nitapanga hoja yangu kwa vipengele 2 :

  1) Nje ya mada :
  -Lwembe, Lwembe, kwa nini umejifanya kama mtoto labda wa primary school? Uliwai kuniambia niko mwalimu sasa nimegundua mim ni mwalimu wa nani. OK, CAN LWEMBE STAND UP AND REPEAT “JELA”, PLEASE ! Sijawai ona mtu ambae anasikia utamu katika uongo kiwango anapoonywa akionyeshwa mahala alipo na kufunuliwa kwa nini anakurupukia tu ndani, kiisha, badala ya kutubu, anaanza leta sifa kwa lile linalomnasa shingoni. Lwembe, unachekesha sana kabisa, uko mtu wa mzaa kweli !!!
  – Lwembe, kwa nini hujue leta jibu kwa swali?
  -Lwembe kwa nini huwezi zingatia neno la Mungu? Na kwa nini unashindwa acha uongo? Unatafsiri na ujasiri kabisaaa! Hivi anaekusoma unaweza muonyesha wapi nilitetea uzinzi wakati nilisema kama hata zile dhambi mnazoita ndogo, nimekwisha rudilia mara nyingi kam zote “mshahara ni mauti”. Ok, acha niandike tena ili uelewe. “Kila ukeukaji wa sheria za Mungu ni dhambi na mshahara wake ni mauti”.
  -Injili inahubiriwa, torati inafundishwa. Ndio maana unasema kila mara watu ni walimu kwani wewe unafundishwa tu. Sasa na wewe fundisha basi vizuri.

  2) Ndani ya mada:

  -Unadaiwa ujibu ipasavyo, na nilikuambia kam si mim kuhakikisha kam umefaulu au la. Sasa usiingie nje ya mada, baki pale na ujibu kwa zile swali zangu A, B, C, D. Hazijasahaulikana, ndio maana sifanye copy-paste.

  – Kuna jambo lingine linalolingana na mada: agano la kale na agano jipya. Nakupasha kama agano la kale (torati + agano zingine za kale) liko excellent, na agano jipya very excellent. Tena la kale limechakaa. Sasa inategemea una upako upi. Kam unataka tegemea lililo excellent tena linalochakaa, sawa, lakini hilo lilikuwa kwa wayahudi tu. Acha sasa anaetaka ambatana na lililo VERY excellent apite, usimzuize. Ina maana anaetegemea lililo very excellent amepitia lililo excellent na kuvuka kwa namna ya kiroho.
  Soma ukitulia Waebrania 8:13; 7:22; 8:6.

  Lwembe, acha injili ikupenye, ukisikia injili usiwe kama wasp inayochokozwa. Mtu wa kiroho anajua kam agano jipya linajitosheleza; dhambi zote pamoja na adhabu ziko wazi ndani, uponyaji wa dhambi, wokovu, na ahadi zote ziko humo humo. Inaomba tu anaesoma asome akiwa wa kiroho. Agano jipya halina upungufu fulani. Agano jipya ni agano la kale witch is fulfilled by Jesus Christ, making it very excellent. Kitu hakiwezikuwa very excellent wakati kinategemea kilicho excellent. Maandiko ya agano la kale yapo ndani ya Biblia tunayoamini kwa faida inayojulikana, kwa kuonyesha kile ambacho agano jipya lina fulfil, kwani ni lazma ujue kilichokuepo mbele, kusudi ufahamu manufaa ya kile kipya.

  Kwa mfano, tukizungumzia mwanamke na mwanaume wazinzi, katika agano la kale ilitakiwa wafumaniwe ndipo wauwawe, tena zingatia kam siyo dhambi pekee iliyoleta watu kuuwawa. Hence, upungufu ilitokana na jinsi ni wanaadamu walioshikilia maamzi juu ya hili jambo. Wale waliotenda hiyo ndambi bila kufumaniwa wala hakuna aliewawazia maksudi wanaowaziwa kuhusika wapelekwe kwa kuhani, hawo hawakuuwawa.
  Ndani ya agano jipya wazinzi WOTE wa kila aina(wa kitendo na kutamani) wanafumaniwa kiroho. Aneekufa kiroho ni yule asiyependa kutubu ukijumlisha na yule anaetubu kiisha anatenda tena dhambi namna anavyotaka, maana yake anaendelea kudharau Yesu hapo akimpinga RM aliyemshuhuda hapa duniani kam Yesu ni Mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kutukana RM, dhambi isiyosamehewa. Hence, mpendwa, usidhani utahurumiwa kirahisi uongo au kusengenya au kutukana, nk ukivirudilia kila siku pasipo kujali. Hali kadhalika kwa mzinzi. Ndugu Lwembe, kama hupendi ubishi tu, unaweza niambia mahala walipouwa kwa mawe aliyetamani mke wa mwenziwe? Ona jinsi agano jipya inaonyesha ile mbili yote wakati agano linalochakaa lingali linategemea jicho la mwanaadamu.

  Wala hujue kabisa kama mashtaka mengi makuhani, waandishi na wafarisayo wa lile agano la kale waliomshitaki Yesu ni kwamba yeye Yesu hakuheshimu torati? Uwe muungwana bwana, hapa hatuchezi!!!

  -Lwembe, kweli, wewe uliniswali au uliongea tu? Soma vizuri uliyoandika, najua unazoea kurupuka. Umeweka wapi swali? Uliyoongea kam haifai kwa nini niiongelee tena? Au umefahamu huna ruhusa ya kuniswali wakati hujanijibu, si ndio ? Lwembe, jibu tu au uhakikishe umeshindwa upate msaada.

  -Swali: Je unawezajibu kwa swali zangu A, B, C, D au huwezi? Kama unaweza, jibu bwana. Kama unaona inakulemea, tembea polepole, moja kwa moja.

  Happy New Year, my brother Lwembe.

 28. Sungura,

  Punguza “Ngonjera”!
  Katika kuigopa kwako Injili, unajizungusha sana kwa maneno yasiyo na rejea ya Maandiko bali unafiki wa mtaani na vijiwe vya dini; eti, “…huwa nafikiria sana kuhusu mwito wako katika blog kama hii”; watu wengine kwa kujikoki!!!

  Fikiria zaidi juu ya injili unayoihubiri, Je, ikipimwa kama mtume Paulo anavyosema itasimama? Je, hiyo injili unayoihubiri ni ile waliyoihubiri mitume? Kazi zote zitapimwa kwa moto, na mafundisho yaliyotofauti yanakaribisha laana!

  Haya, hebu yaangalie maelezo yako na maswali unayoniuliza,
  “”Hatuko hapa kuhalalisha dhambi, lakini tuko hapa kuusema ukweli kama ulivyo. Lwembe nataka utoe hapa maandiko yenye kuliweka wazi hilo. Acha kuongea maneno ya kutungwa, thibitisha hii kauli yako kuwa ”Uzinzi ni Dhambi ya mauti kwa Mkristo, haina dhabihu”””

  Sijui kama huwa unasoma michango ya nyuma kabla ya kuuliza maswali ama kulibishia jambo, au ndo ule ubishi kwa kwenda mbele! Swali unaloniuliza nilikwisha mjibu ‘Bwana Jela’ siku nyingi sana, ila ni kwavile ninyi ni wagumu wa kujifunza tu, lakini nawe nitakujibu ili mradi umeliuliza, na pia nafahamu kwamba ni uungwana kujibu kuhusu uliyoyasema!

  Kwanza, ni vizuri ukajiweka katika nafasi ya kuielewa Injili kwa kuifuata ktk Mpangilio inayo kuweka. Tunafunzwa kwamba Agano la Kale lilikuwa kivuli, na pia tunafundishwa kwamba hicho Kivuli kazi yake ni kutuleta kwa Kristo. Basi tunapozungumzia Dhambi, iwapo tutajikurupukia tu na kuvidandia vifungu vya Agano Jipya, bila Msingi wa Agano la Kale, tutaishia kuuana!

  Biblia inasema wazi kuwa kuna Dhambi ya Mauti na isiyo ya Mauti; 1Yn5:16
  “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.”

  Dhambi ya Uzinzi katika Torati inabeba Hukumu ya Kifo, Law 20:10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.” Hiki ndicho Biblia inachofundisha. Mkristo anapaswa kufundishwa jambo hili hapo anapoukulia wokovu mpaka alielewe sawasawa. Juu ya uelewa huu sasa anasogezwa mbele Mt 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Unaona! Unapaswa uwe uliisikia Torati kwanza ndipo utaweza kuyajua yanayofuata, adhabu ya Uzinzi haijaondolewa bali wigo wa kuwakamata wazinzi umepanuliwa!

  Hiki ndicho ninachokifahamu kuhusu Uzinzi kwa walio katika Sheria kwanza, na sasa kwa walio katika Wokovu. Kwa walio nje, hao wanaendelea katika mipango yao kuhusu jambo hilo. Ninachokijua kwa sehemu kubwa ni kwamba wazinzi wao, hao wanaume wanaofumaniwa na wake za watu, hushikwa Ugoni na hutozwa fine, aidha ya pesa au wanyama wa kufuga kama ng’ombe nk, na baada ya hapo maisha huendelea kama kawaida. Kwa jinsi ninavyowaona akina Sungura, hii ndiyo hali mnayoigombea iingizwe makanisani!!!

  Kuhusu Uzinzi na Uasherati, ingawa vyote vinahusu tendo moja, lakini maudhui yake ni tofauti.
  UZINZI kwa leo:
  Uzinzi hufanywa pale mwanamke aliyeolewa anapotoka nje ya ndoa yake halali, awe amelishiriki tendo hilo na mwanaume aliyeoa au asiyeoa, wote huhesabiwa Uzinzi. Au mume anapomuacha mke kwa sababu isiyokuwa ya Uasherati, na hivyo kumfanya mwanamke huyo kuchukuliwa na mwanaume mwingine, ndipo mume huyo huhesabika kumsababishia mkewe huyo aliyemuacha kosa la uzinzi, naye mwanaume anayemchukua mwanamke huyo aliyeachwa katika mazingira hayo, huhesabiwa uzinzi. Unaweza kujifua zaidi kwa vifungu hivi:
  Mt 5:32 “…Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
  Mt 19:3,9 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? … 9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.”

  Yasikilize maoni ya wanafunzi wake baada ya kuyasikia maelezo hayo, nao wakiijua Hukumu ya Uzinzi, na sasa ile ‘talaka ovyo’ waliyoizoea, ambayo iliwapa fursa ya kuwachezea watoto wa kike, ikibandikwa Uzinzi, yaani KIFO;
  “10Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.”

  UASHERATI:
  Uasherati hufanywa pale mwanamke asiyeolewa, yaani binti, anapotembea na mwanaume awe ameoa au hajaoa. Hawa huhesabiwa kufanya Uasherati.

  Ndiposa, binti aliyefanya Uasherati sirini huko nyuma, ikafika wakati akaposwa, basi kabla ya ndoa kufungwa anapaswa au confess uasherati wote alioufanya, kwa huyo aliyemposa, na kumpa fursa ya kuamua kuendelea na ndoa au la, juu ya ufahamu huo. Jambo hili huiondoa Dhambi hiyo kwa huyo binti na likiivunja kabisa nguvu yake. Yaani ni sawa na kusema, mchumba wangu akiwa amekwisha kuniambia kuwa alitembea labda na Sungura, nami nikalikubali jambo hilo na kulisamehe, ndipo hata huko mbele akija mnafiki na kuniambia kuwa mkeo alikuwaga mpenzi wa Sungura, halitakuwa na Nguvu, nami nitamwambia kwa wepesi kabisa kwamba hilo aliniambia!!!

  Lakini iwapo mchumba huyo atauficha uasherati alioufanya, akadanganya, na juu ya uongo huo ndoa ikafungwa, Dhambi ya Uasherati itamwandama, maana hakuikiri kwa mchumba wake! Ndipo huko mbele mume akijakugundua kwamba mke alitembea na Sungura, yule mjeuri, basi akiona hawezi kulivumilia hilo, ndipo juu ya Dhambi hiyo atamuacha mke huyo! Na kulingana na Fundisho la Talaka, mke aliyeachwa kwa Uasherati, ninaamini ANAWEZA kuolewa na isiwepo Dhambi ya Uzinzi juu yake na huyo anayemuoa juu ya ufahamu huo, maana ametalikiwa kihalali!

  Kwa leo ngoja niishie hapa kwa haya machache, nikusubiri, kisha tuliendee lile la “Ufalme wa Mungu”

  Asante & Gbu!

 29. Mpendwa lphonse Ziragora,
  Nimekuelewa ndugu yangu, umesema kuwa,

  “Ndugu Mabinza,
  Niliona ukijaribu kusema kitu fulani kinachoambatana na kusamehewa kwa yule mwanamke mzinzi au la. Ninachoona ni kwamba unarudilia tu kukanusha, lakini husemi Yesu alimfalia nini kwa tamko fulani…….Nauliza, Nini Yesu alifalia huyu mwanamke? Kwani ulikuwa kam umekubali mengine matatu kupata ushindi isipokuwa hilo jambo moja.
  Je:
  -Yesu alimuokoa?
  -Yesu alimponya?
  -Yesu alimfufua?
  -Yesu alimficha?
  -Yesu alimhukumu?
  Nitakujibu kwa jumla maulizo yako kwakuwa yote yanamaanisha kitu kimoja kama ifuatavyo:-

  Habari ya Yesu na mwanamke mzinzi imeainishwa kwa uwazi na kwa uzuri katika kile kitabu cha Yh. 8:3-11, Katika mistari hiyo takribani 8, inaonyesha wazi kuwa, Yesu alimuokoa, alimponya, atamfufua, alimficha KWAKUWA HAKUMHUKUMU MWANAMKE MZINZI YULE!! Usipofikiri vema, unaweza ukashangaa sana kusikia ninavyokuambia, kwani utaona kama napingana na niliyoyasema mwanzo, lakini ukitulia na kunifuatilia vizuri utagundua kuwa sipingani hata kidogo. Ninachojaribu kukiweka hapa ni kukuonyesha tu kwamba, Yesu alikuja kwa wenyedhambi walio tayari katika toba ya kweli, kwa hiyo aliwapokea na anaendelea kuwapokea wazinzi wote hadi sasa ambao wapo tayari kuuacha uzinzi wao, na kuokolewa kwa kumwamini Yesu kristo! Ki ukweli, ukisha okolewa na kukakamilishwa kwa mhuri wa Roho mtakatifu, ukizini huna dhabihu ya kuiondoa dhambi yako tena! Hiyo ni kwa mjibu wa Ebr. 8:26.

  Labda katika kuliweka sawa hili, hebu rudi Yuma katika hiyohiyo Yohana, tazama Yh.5:1-10, kuna mtu mmoja aliponywa ugonjwa ambao ulimsumbua kwa miaka 38. Lakini habari inaendelewa vizuri kwa kufundisha juu ya msamaha wa dhambi kwa wanadamu wakubario kuacha dhambi, ukiendelea mbele hata ukiishia hadi mstari wa 29 Hapa ninataka uone, mtiririko mzima wa habari ile, ukioanisha na ile habari ya mwanamke mzinzi katika Yh.8, ili ujue kwa nini nasema kuwa Mwanamke mzinzi alisamehewa na Bwana Yesu kristo na kuokolewa tokana na hukumu ya mauti. Ukiutazama ule mstari wa 14 katika Yh.5 unasema, “14Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya hekaluni na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitenda dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.’’ Sentesi hiyo ya “USITENDE DHAMBI TENA” tunaiona, ikiwa sawa na ile ya katika Yh.8:11, hapana shaka kabisa kwamba wote wawili walikuwa katika hatari ya kufa, ila kwa vifo vyenye vyanzo tofauti, mmoja ni mgonjwa na wapili ni kwa kupigwa mawe tokana na uzinzi, lakini kifo ni kifo tu. Wote tunajua, kifo kililetwa na shetani hivyo wote walikuwa katika kufa, bali uzima uliletwa na Yesu na wote wakawa wazima! Ona, Yh.5:21 inasema, “21Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda.”

  Lakini uwazi zaidi unaendelea kuonekana kuwa, watu wale mwanzoni kabla ya kukutana na Yesu wote wawili walikuwa ni watenda dhambi, na walipoponywa hawakupona kimwili tu, walipona pia kiroho, ndiyo maana Neno, ‘usitende dhambi tena’ likatumika. Lakini kama nilivotangulia kusema kuwa, ukitenda dhambi wakati tayari ulishakwisha kuokolewa na tayari ulisha kwishaonja vipawa vya Roho mtakatifu, hakuna dhabihu tena ya kukuondoa katika hatia ya kifo! Na hilo ndilo jambo kubwa na lililobaya zaidi, yaani mtu kufa kwa dhambi. Jambo hilo Yesu alimwambia mgonjwa katika ile Yh.5:14 ambapo inasema wazi kitu ambacho kitampata mtu ‘ALIYEPONYWA’ akitenda dhambi tena, inasema, “14Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya hekaluni na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitenda dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.”

  Kwa hiyo mwanamke mzinzi aliokolewa kwa kule kuliamini Neno la Yesu, ‘usitende dhambi tena’ kwa imani mtu hupata haki, lakini Yesu analielezea vema hilo katika hiyohiyo Yh.5:24 ambapo anasema, “24‘‘Amin, amin, ninawaambia, ye yote anayesikia maneno Yangu na kumwamini Yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.”

  Watu wote wenye dhambi wapo katika hatari ya mauti, lakini kwakuwa saa ya uzima ndiyo hii, basi, kila atakaye mpokea Kristo hakika atapona. Kwa hiyo, ni makosa kufikiria tu kwamba, watu walioonana na Yesu, waliishia kupokea miujiza tu ya kimwili pekee na kuacha kufikiri kama walipata pia uponyaji wa ki roho! Lakini Yesu mwenyewe anatuambia hilo waziwazi kuwa, aliwaponya pia kiroho, hebu ona hiyohiyo Yh.5:25, Yesu anafundisha kwa kutuhakikishia kuwa, “25Amin, amin, nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai.” Unaona?

  Mwisho nimalizie tu kwa kusema kwamba, mwenye mamlaka ya kuhukumu ni Bwana Yesu kristo. Kwa vile alimtamkia waziwazi Yule mwanamke mzinzi kuwa’HATA MIMI SIKUHUKUMU’ kauli ile ilimpa mwanamke Yule kuishi akiwa bila hukumu yoyote ya mauti, ile ya mwili na pia ya kiroho, maana Yesu katika hiyohiyo Yh 5:27-28 anasema kuwa, “27Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa Yeye ni Mwana wa Adamu.
  28“Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti Yake.”

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 30. Ziragora,

  Asante kwa ufafanuzi mzuri. Kwa kusimama katika nafasi zetu, wewe ukiwa upande huu wa Agano Jipya unaokupa UHURU juu ya Dhambi, kwamba kwa kifungu hiki ulichoninukulia, Warumi 8:2 “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti” ; kwahiyo kupitia kifungu hiki kwa kukikariri, ndiyo mmepewa Uhuru juu ya Uzinzi; ni dhahiri kuwa tutaendelea kutofautiana sana!

  Hata hivyo napenda kukuhakikishia kuwa, kama ungeijua maana na nguvu ya kifungu hiki, basi kingekuongoza na kuijua Torati ni nini, vinginevyo nakuona ni mtu unayezidi kujitumbukiza katika dimbwi la matope!

  Hebu yajibu maswali niliyokuuliza kwa injili uliyoihubiri, huo ndio uungwana wa vitendo na si kugeuza geuza maneno unakokufanya ukikimbia kuwajibika kwa kauli ulizozitoa!!! Kukimbia kwa hila kujibu maswali ni dalili ya ualimu wa uongo, ambao ni dhambi ya mauti na inawezekana kwamba UKO JELA siku nyingi sana kutokana na jambo hilo, mpaka umekuwa “mnyapara’!!!

  Bwana na akuepushe na Mafundisho ya Uongo!!!

 31. Ndugu Mabinza,

  Niliona ukijaribu kusema kitu fulani kinachoambatana na kusamehewa kwa yule mwanamke mzinzi au la. Ninachoona ni kwamba unarudilia tu kukanusha, lakini husemi Yesu alimfalia nini kwa tamko fulani.
  Tunajua kama huyu mwanamke alikuwa ndani ya mikono ya watu wa kumuua, Kilichomuepusha kifo ni kwamba tu walisubutu kuuliza Yesu wakitaka kumpinga.
  Nauliza, Nini Yesu alifalia huyu mwanamke? Hii ninairudilia kwani mada hapa ndipo inaonyesha uzito. kwani ulikuwa kam umekubali mengine matatu kupata ushindi isipokuwa hilo jambo moja.

  Je:

  -Yesu alimuokoa?
  -Yesu alimponya?
  -Yesu alimfufua?
  -Yesu alimficha?
  -Yesu alimhukumu?
  …….

  Asante.

 32. Ndugu Lwembe,

  Endelea tu pigana na neno la Mungu ukidhani uko sahihi.
  Neno la Mungu halina haja ya kutetewa na mtu yeyote, linajitetea lenyewe:
  “Warumi 8:2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”

  Nadhani umeona mahali ulipo na mahali nilipo. Ni tofauti sana.

  Nimekwisha kukwambia kama hukujibu ipasavyo. Sasa pahali pa kujibu unaendelea hakikisha kam Yesu ni torati. Hebu endelea sikukataze, lakini sikushiriki.

  Matusi yako hayanifanye chochote hata wewe umesamehewa tu. Unachodaiwa ni kutubu uongo ambao unaendelea tangaza. Ndugu yangu siwezi kukudai mengi wakati unashindwa machache.

  Kifupi ni kwamba swali zile A, B,C,D hujapima jibu hata kidogo, unachoongeza ni matusi na utani. Unadaiwa majibu tu jinsi mimi nimekufikishia swali wala si jinsi unayotengeneza mengine ndani ya factory yako ya waongo.

  Na comment ni hiyo tu kwani unapoendelea kuimba jela inaomba ikupenye vizuri na anaekusoma afahamu unaimba nini. Utakapotubu, Mungu atakupa hekima.Nafikiri unafahamu jinsi ulivyojifunga wewe mwenyewe miguu na mikono na kujitumbukiza ndani ya hiyo jela. Yeyote atakaependa afahamu ulifikaje humo atafahamishwa bila kukoroga mada.

  “Kam unaemwita Bwana Jela ni yule Ziragora aliegundua kam wewe ni muongo professional basi umehakikisha umeridhika kuwa ndani ya jela iliyowekewa waongo pamoja na Ibilisi bwana wao. Lwembe, ukitazama jinsi umejitumbukiza mwenyewe ndani ya Jela, huoni kam unaandika bila kufahamu unachoandika? Wewe ambae unapinga kiupofu neno lililo hai ninalokuletea kila leo, iweje tu uwe umetumbukia ndani yangu? Unamaanisha umeguswa na Neno? Uwe muungwana, utuambie basi yaliyo kweli. Kama Injili imekuingia, si usemeshe kweli? Unafikiri kuna atakaekucheka? Pengine utatoka ndani ya jela la waongo, RM akutie ndani ya jela ya wenye haki, ile ambayo Paulo anasema katika Waefeso 3:1.”

  Ubarikiwe kaka yangu.

 33. Mabinza,
  Nina machache tu ya kukuuliza na kukupasha habari:

  Anayetendwa dhambi huwa ni Mungu tu. Kwa mfano: ukiiba ng’ombe wa mtu, au ukizini na mke wa mtu, huyo mtu hujamtenda dhambi, bali umemkosea. Lakini Mungu umemtenda dhambi kwa hayo makosa. Nilikuwa najibu suala lako la kwa nini biblia haisemi ‘utusamehe sisi dhambi zetu kama nasi tunavyowasamehe waliotutenda dhambi’.

  Kwa kuwa mtu aliyekwisha kutubu huwa hatendi dhambi tena bali hufanya makosa tu, kwa hiyo huyo mtu akitukana, hiyo si dhambi mbele a Mungu bali ni kosa tu?

  Asante.

 34. Ziragora,

  Nimefurahi kwamba umeyapokea majibu ya maswali yako, na baada ya kuyatathmini umeyaona ni majibu ya ‘mtu mjinga’. Kinachonisikitisha, ni ukweli kwamba kiwango chako cha ufahamu umekifunga kwa “PRIDE”; inakuzuia kuyaona na kuyaelewa hata yaliyokusudiwa kuwa wazi kwa watu wote, bali kwako wewe yanakupita juu ya kichwa, huyaoni!!!

  Pride inakufanya uwe kituko! Angalia kauli yako hii, “…Kumuita Yesu “torati” ni utani mtupu. Yesu ni bwana wa “Torati”. Sasa, ndugu usitafute chini-juu kupunguza nguvu za Yesu, wala kumtia chini ya miguu ya Musa…”

  Labda ngoja nikujibu hiki kituko chako kipya, kwani hayo mengine uliyoyaandika ni “ngoma ya mashetani” isiyo na mwisho, yaani huna unaloliuliza na wala hulijui hata unaloliuliza bali ni kujibaraguza kwa mtu aliyepoteza mwelekeo na sasa akijaribu kumvuta kila mtu into the irrelevancy pit!

  Kuhusu Yesu kuwa ni Torati, kama hulijui hili, basi inabidi uhubiriwe Injili upya na kuwekwa chini ya wakufunzi wenye Ujuzi wa Neno la Mungu! Kwa kukosa kwako kulijua jambo hili, limekuzalishia kiburi badala ya unyenyekevu, kwani ndivyo ilivyo kwa wote waliochepushwa na kupelekwa ktk njia ya dini!!

  Bwana Yesu Kristo ni NENO la MUNGU lililofanyika Mwili. Nayo Biblia ni NENO la Mungu in Text Form embodying the Spirit of God; Yn 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, TENA NI UZIMA.” Torati ni Neno la Mungu si neno la Musa kama unavyojifahamisha wewe na wengine wasioamini kama inenavyo Biblia, “64 Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini.” Musa hana hata kitabu kimoja alichokiandika yeye kama Musa, ingawa Torati ilitolewa kwa mkono wake! “Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.” Basi hakuna nabii yeyote yule anaye kuja na neno lake isipokuwa wote huja na Neno la Kristo, Mwanzo hadi Ufunuo!!! Basi kuligawa kwako Neno la Mungu ktk mafungu yasiyoeleweka, ni dhambi inayotokana na Pride, yaani Ufarisayo, ambao unabeba gharama ya Presence ktk kiwango cha Mauti hapo unapojing’ang’aniza kuwa uko sahihi na hivyo dhambi yako yako hiyo kubaki!

  Basi kwa imani ya dini iliyojengeka juu ya msingi mbovu kama hii ninayokuona nayo ambayo inakuelekeza kuamini mambo ambayo HAYAPO, ndipo kila unapokutana na Neno Halisi la Mungu lazima likuchanganye!!!

  Mwisho badala ya kuja na maelezo mengi yaliyojaa ulalamishi bila Njia, lete basi uthibitisho wa kiMaandiko kuhusu unayoyatetea, kama ni dhabihu ya Uzinzi kwenye Agano Jipya, tuonesha basi hapo mlipopewa Maelekezo ya kuitoa dhabihu hiyo ili hao wazinzi mnaowafundisha mambo hayo wahakikishiwe zaidi kuhusu msamaha wao kila wanaposhindwa kujizuia, waijue na njia ya kurudia!

  Asante, ‘Bwana Jela’!!

 35. Wapendwa,
  Ninachokiona hapa ni ugumu wa kuelewa kunakoitwa ama kuonekana kuelewa kwa wanaojiona wanaelewa!

  Sina hakika kama watu tunapoizungumzia dhambi tunakuwa tunajua inamaanishwaje kwa mwamini. Labda tu kwa kifupi ‘NICHOKOZE’ tu kwamba, dhambi hutendwa na ASIYEAMINI, mtu ambaye amekwisha kuokolewa ana kuwa tayari keshakuwa mwana wa Mungu, Neno linasema “….yeye alitupa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu, ndiyo waliaminio jina lake…”. Biblia inaendelea kusema, ALIYEZALIWA NA MUNGU HATENDI DHAMBI!

  Ukisoma kwa makini ile Ebrania 10:26 inaeleza kwa uzuri na wazi tu kwamba, “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;”

  Ujuzi unaosemwa hapa ni ile kweli aipatayo mtu baada ya kwisha kuamini na kukamilishwa kwa njia ya roho mtakatifu na kutakasika kwa lile Neno la Mungu. Toka hapo mtu akifanya dhambi, huitwa kafanya dhambi si kwa “bahati” mbaya, kafanya kwa “kukusudia” maana anao tayari ujuzi wa lile Neno, hapo, mtu kama huyo hana dhabihu itakayochinjwa ili kuiondoa dhambi yake hiyo!

  Tunaamini na kutubu na kisha kupata ondoleo la dhambi kwa mara moja tu, kwakuwa dhambi iliingia kupitia mtu mmoja na pia inaondolewa kupitia mtu mmoja tu ndiye Yesu Kristo, kwa kifo chake kilicho fanyika mara moja tu kwa kila atakayeamini. Kwa hiyo ukisha okolewa hakuna tena mchezo wa kuanguka dhambini na kutubishwa tena!

  Tatizo kubwa kwa waamini wengi, wakishakuamini lile neno na hujiona tayari wamekuwa sasa wapo safi. Ndipo sasa huanza kutumia bidii na nguvu zao kuanza kuacha yale waliyokuwa wakiyatenda kabla, kama vile, wizi, uongo, usingiziaji, uzinifu nk; kwa bidii nyingi, huku wakijilazimisha kuukimbia ubaya kwa kutumia akili, maarifa, juhudi na nguvu zao, lakini hubaki wameduwaa kwa mshangao kwani kabla ya tumba kuchanua kuwa ua, huishia kushindwa na kurudia tena dhambi zao za awali, tena safari hii ni kwakiwango cha ukubwa wa kutisha! Biblia inamnukuu Yesu katika Yh. 15:5 akisema, “…bila mimi ninyi hamuwezi neno lolote!” Bila kuujali ukweli huo, washindwaji hao hujiaminisha katika uongo kuwa, ‘WAO BADO WAMESIMAMA KATIKA WOKOVU, ILA WANAANGUKA NA HIVYO WANAYO NAFASI YA KUTUBU TENA!’ wakishindwa kuikubali na kuisoma kwa ujasiri ile Ebr. 18:26, na kwa hali hiyo hiyo, wengine hudiliki pia kusema, wokovu hauwezekani hapa duniani, wala huwezi kuwa mtakatifu hapa ulimwenguni!! hawajijui kama ni waamini wa kweli, wakujifanya ama ni kwamba wao ni wasioamini kabisa!

  Mtu anapopata neema ya kuokolewa, hujiachilia mzimamzima mikononi mwa Mungu, kwa imani huanza kukamilishwa kwa utaratibu hatua kwa hatua. Mungu ndiye mwenye jukumu na uwezo wa kumkamilisha mwamini hadi kuufikia ‘wongofu’ hunahaja ya kujitutumua mwenyewe kuacha mabaya yako, mwachie yeye atawale, Yesu aliseama “…nimekuombea nawe utakapoongoka, uwakamirishe na wenzako” maneno hayo aliyasema Yesu, akimwambia Petro, lakini tunajua Petro alikuwa mtume na aliitwa na Bwana Yesu mwenyewe, lakini hadi wakati huo wote alikuwa bado hajaongoka kama mwamini impasavyo ili kukamilika!

  Yesu alikuja kwa wenye dhambi, si kwa waliokwisha kuokolewa! Mtu akisha okolewa, haondoki duniani hivyo, kinachokuwepo kwake ni kutenda makosa, si kutenda dhambi, ndiyo maana Yesu alipokuwa akioomba, alosema, “tulindwa dhidi ya mwovu, si kwamba tuhamishwe toka duniani”. Biblia inasema, na mkisali, ombeni hivi, “utusamehe makosa yetu kama na sisi tunavyo wasamehe waliotukosea” mtu fulani atasema, mbona kuna pahala fulani katika Biblia panasomeka kuwa, “utusamehe dhambi zetu….”? Ni kweli, panasomeka hivyo, lakini ukiumalizia mstari huo, mwisoni unasomeka, kama na sisi tunavyo wasamehe walio tukosea, hausomeki kuwa, ‘….kama na sisi tunavyowasamehe waliotutetenda dhamdi’, kw hiyo iko tofauti halisi na ya kimantiki kati ya MAKOSA na DHAMBI! Kwa hiyo ukiokoka kabisa hutendi dhambi tena! Mtu akiokoka na bado anaonekana kushindwa, huyo asikate tamaa na asimsikilize shetani, akaze katika kuamini na kujiachilia mikononi mwa Mungu. Kamwe asifanye na kutumia nguvu zake kujikataza ili kujiwezesha kuwa mtakatifu, hizo huwa ni hila za yule mwovu, kukufanya kuwa wewe kama wewe unaweza! Kumbuka Neno linasema, BILA MIMI NINYI HAMUWEZI NENO LOLOTE!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 36. Aise Lwembe,

  Hebu jaribu kuwa na shauku ya kuogopa kusema mambo usiyoyajua uhalisia wake.
  Yaani mimi huwa ikifika kwenye hii tabia yako ya kunena kwa herufi kubwa mambo ambayo ni wazi kabisa huyajui huwa nafikiria sana kuhusu mwito wako katika blog kama hii.

  Lwembe unasimama kabisa kwenye kadamnasi hii unasema dhambi ya uzinzi haina msamaha, just kwa hoja nyepesi kabisa na unayoonekana kuifahamu kwa undani!!!

  Hatuko hapa kuhalalisha dhambi, lakini tuko hapa kuusema ukweli kama ulivyo. Lwembe nataka utoe hapa maandiko yenye kuliweka wazi hilo. Acha kuongea maneno ya kutungwa, thibitisha hii kauli yako kuwa ”Uzinzi ni Dhambi ya mauti kwa Mkristo, haina dhabihu”

  Kwa sababu tukikuacha tu hapa bila kukuambia kuwa unachosema siyo kweli tukasema tu kuwa hayo ni mawazo yako, tujue kabisa tunawakabidhi kwenye upotevu watu ambao tayari walishatumbukia kwenye hili shimo.

  Haya, suala la taraka alilolisema Yesu hebu acha kuliweka kwa ujumla namna hiyo, nataka tufanye uchambuzi mchana kweupe hapa. Kwanza nataka useme hapa tofauti kati ya Uzinzi na uasherati, ndipo tuone kama kweli Yesu aliongelea suala la uasherati tu alipokuwa anaongelea talaka!

  Kwa maana nyingine hapa umejaribu kumaanisha kuwa dhambi ya uasherati yenyewe inasamehewa. Kwa hiyo kujua utofauti ya hayo mambo itatupa kujua hata kwa fikra ya kawaida kuwa, nini huwa kinatokea mtu akizini, amabacho kiko tofauti na kinachotokea kwa mtu aliyefanya uasherati.

  Kuna hili hapa nalo nimeshangaa sana jinsi ulivyolisema kwa ujasri kuwa, ”Kwa kukusaidia, Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu”
  Kabisa, unataka tuwaamnishe watu wanaofuatilia michango yetu hapa kuwa Ufalme wa Mungu ni Roho mtakatifu?

  Hebu tufikiri hivi:

  Roho mtakatigfu ni nafsi – kwa hiyo ufalme wa Mungu ni nafsi!
  Roho mtakatifu ni msaidizi wetu – kwa hiyo ufalme wa Mungu ni msaidizi wetu
  Roho mt. ni mwalimu wetu – kwa hiyo ufamlme wa Mungu ni mwalinmu wetu.

  Huyu ni mwalimu Lwembe anatufundisha hivyo!!!

  Ukimuuliza nani kamfundisha hayo, yawezekana akakwambia ni Roho mt. ndo kamfundisha, kwa sababu namjua ni mtu ambaye yuko kinyume kabisa na elimu ya biblia!!!

  Kwa mimi huu ni mzaha mkubwa sana!!!!

  Kitu kingine, ni kuhusu kusema kuwa Yesu hakuja kuitangua torati. Hii kauli nayo watu wengi ukiwemo Lwembe, hamuilewi kabisa, kiasi kwamba mkibanwa mnaishia kujichanganya tu. Na mbaya zaidi huwa tu mnanukuu robo ya alichosema Yesu – sikuja kuitangua torati- wakati ili ujue ukamilifu wa hiyo kauli lazima usome tungo nzima.

  Ona hapa: Mt 5:17- “Do not think that I came to destroy the Law or the Prophets. I did not come to destroy but to fulfill. 18 For assuredly, I say to you, till heaven and earth pass away, one jot or one tittle will by no means pass from the law till all is fulfilled(KJV).

  Ukiwa msomi uliyejifunza lazima utazingatia sana – til all is fulfilled- maana ndo linaleta maana kilichosemwa mwanzo wa sentensi.

  Ni sawa na anayesema kuwa Yesu kasema mtu akimwacha mkewe na kuoa mwingine azini. Lakini anaruka sentensi inayosema ‘ispokuwa kwa sababu ya uasherati…’

  Swali la kujiuliza ni je yote yaliyoihusu torati Kristo aliyatimiza?

  Kingine ni hivi, waliopigwa kwa mawe katika torati hawakuwa waliofanya zinaa peke yao, kumbuka yule aliyevunja sabato naye alipigwa kwa mawe.

  Mwisho, kilichosemwa kwenye Ebrania 10:28, siyo dhambi ya uzinzi pekee bali ni dhambi zote!

  Kuna umuhimu wa kwenda shule, Mungu hakutumia watu maamuma katika kuiandika biblia!!!

 37. Ndugu Mabinza,

  Asante, tena nashukuru kwa mchango wako.

  Kama unasema mjinga ni yule asiefaa, uko mkweli. Lwembe alijibu kam asiyefaa haswa kwani alisema Yesu=torati. Hafae kwa ile alionijibu wala si kwako au kwangu au kwa mwengine yeyote. Ukiona kama “Bwana Yesu”=”kitu alichokitengeneza” basi wewe usifu Lwembe kwa yale aliyoandika jinsi upendavyo. Tena ndugu yangu acheni ushabik; nafikiri hukusoma vizuri. Niliandika AMENIJIBU(mim) KAMA MJINGA wala sikusema yeye ni mjinga. Sisi tunapima maneno tunayotumia, usipokuwa makini utajichanganya mwenyewe. Ina maana mtu anaweza kuwa si mjinga lakini anayoyafanya yanatetea ujinga na hiyo inajitokeza wakati mtu anatafuta ajifanye kuonekana sahihi kwa njia zote iwemo kuutumia uongo.

  Hiyo hiyo ndio inakusukuma na wewe kumfanya Yesu dhaifu. Unaona vocabulary yake haina maana. Swali yangu mahali pale ni “kwa nini Yesu aambie maiti isitende dhambi tena?”. Hata wewe kwa kumsaidia huna ufahamu wa kulijibu hili swali. Unaposema hakumuhurumia unahakikisha alichomwambia hakina maana.

  Wala sipendi ubishi na wewe kwani ni ktk ubishi usio na maana wengine wanapendelea mada ibadilike makusudi wasikiri kushindwa.

  Ubarikiwe ndugu yangu.

 38. Mpendwa Alphonse,

  Naamini haujambo, nimefurahi sana kuona kuwa hupendi hata kidogo kuwa ‘member’ wa shetani, hili ni jambo jema! Masikitiko yangu tu ni kwamba, unachokikataa ndicho unachokitenda! Neno la Mungu linasema, “…….alichokifanya Mungu usikiite najisi…” kitu chochote kisichofaa iwe kwa Mungu ama kwa wanadamu naweza kusema kuwa kitu hicho ni sawa na Najisi. Mtu mwenyesifa yakuwa ‘MJINGA’ ni yule asiyefaa kwa maarifa, hategemewi kuelemisha, yaani katika kundi la waelemishaji au kwa watu wenye maarifa yeye kwao ni kama ‘NAJISI’ sina hakika kama unauwezo wa kumwita au kumuweka mwalimu mashuhuri kama Lwembe CK katika kundi la wajinga, ati kwa sababu tu hakubaliani katika hoja fulani! Najua ujinga siyo tusi, lakini KATU LWEMBE SIYO MJINGA labda kama humji vizuri ndiyo waweza kumuita hivyo.

  Hata hivyo, hoja ni kuelemishana, swala la kutoana AKILI lingefaa ulifanye ‘ privetly’ labda umuite chemba ama ufuate kwake ama mwaweza kukutana pahala kama vile Karikoo, manzese, Buguruni na kwingineko, ukamtoe akili huko, siyo mbele yangu, umenikwaza Brother!

  Tukiachana na hayo, tuje kwa kifupi juu ya swala la mwanamke mzinzi mbele ya Yesu, kwakifupi Yesu hakumhurumia wala kumsamehe! Isome vizuri Biblia yako, pahala pale katika hiyo Yh. 8:5 na kuendelea, Yesu mwenyewe kwa kinywa chake, anamwambia yule mwanamke mzinzi kuwa ‘…….hakuna aliyekuhukumu kuwa una hatia? Mwanamke akajibu, hakuna, Yesu akasema Nami sikuhukumu, nenda zako na usitende DHAMBI TENA” tamko hilo la Yesu lipo wazi kuwa, yule mwanamke alikuwa tayari alikwisha tenda dhambi, ila asirudie kutenda dhambi kwa mara ingine tena. Hakuna katika maelezo ya Yesu katika mazungumzo yake na yule mwanamke alipomwambia amemsamehe dhambi yoyote pale! Bali alimuonya tu kuwa asitende dhambi tena.

  Pengene mtu atasema, mbona alimwambia “nami sikuhukumu” je, si kwamba akumtaja kuwa anakosa? Jibu ni LA HASHA , Yesu hakuja kuhukumu ulimwengu, na mtenda dhambi yeyoteni wa ulimwengu, hadi anapookolewa.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai”

 39. Lwembe,

  Mpaka pale unajibu kama mjinga.

  A) Mim nimeleta ndani ya hiyo orodha ipatikanayo ndani ya Biblia hoja inayofungana na tukio. Kam wewe huna ufahamu wa kutenga uzinzi, na ulevi, na uasherati, nk…. ukisema kinachovitofautisha ni tukio/hukumu yake, utaendelea pigana na Neno la Mungu kwani limekutangulia na kuweka hizo dhambi zote nafasi moja: wale wote “hawatarithi ufalme wa Mungu”, kwa kiroho hiyo ndio kifo. Hivi huna la kudanganya kwani Neno la Mungu liko wazi.

  B) Anae elimu yeyote anajua kama torati iliingia wakati wa Musa. Lakini kabla Musa awe dhambi zilikuwepo na hukumu ilikuwepo. Wewe una shida ya ufahamu wa maagano Mungu aliyofanya na watu. Ndio maana hushangaze kusomwa kam mwenye kutokuwa ktk agano jipya. Kumuita Yesu “torati” ni utani mtupu. Yesu ni bwana wa “Torati”. Sasa, ndugu usitafute chini-juu kupunguza nguvu za Yesu, wala kumtia chini ya miguu ya Musa.
  Unapomdharau Yesu ukimlinganisha na torati, kweli ni lazma ukose ufahamu wa kujua kam yeye Yesu anayo mamlaka ya kumhurumia anayetaka ikiwemo yule mwanamke mzinzi. Kwani wewe unamtazama Yesu akiwa chini ya sheria. Itakuwa nguvu sana kwako kufahamu kama Yesu ana mamlaka juu ya torati unayofanya kila mara kimbilio lako. Nililokuswali ni hili “Kwa nini Yesu aambie maiti isitende tena dhambi?”, ina maana kuna faida gani kwake, au ana lengo gani? Kwa taarifa yako, anaeambiwa asitende dhambi tena ni yule alieomba masamaha na kusamehewa.

  C) Uwe muungwana na useme kweli kama mim nimekushurtisha kutoenda nje ya mada. Kwani wewe unapenda ongea juu ya “asiyetumika na asile” pamoja na “mtu asiyetaka tumika asile”, hiyo ndio ugeuze mada na uendelee chamsha uongo wako. Ninapokuswali juu ya kiini cha dhambi, niko ndani ya mada. nakuomba tu ujibu ipasavyo. Unaogopa nini wakati hii ni hoja iliyosimama wakati uliposema kama hatuelewi dhambi ni nini? Ina maana unasimamisha hoja usiyofahamu mwenyewe? Mpaka pale hujakosoa. kukosoa ni kutia tamko tofauti. Wewe Lwembe, unataka ufunzwe kila jambo? Jinsi ya kusoma, ufunzwe; jinsi ya kusimamisha hoja,ufunzwe; kutosema uongo, ufunzwe, ….!!! Wewe ni mtu aina gani?

  D) Kwani umekosa mtu anayewajibika kwa leo kumuuwa mzinzi, ukidai kwamba leo jambo hilo ni la kiroho, hebu itika kweli hicho kiroho na ufahamu kam Yesu alifia watu wote, na kwa kupigwa kwake tumepona. Hakuna nafasi hii moja Yesu aliposema alifia wengine wote isipokuwa wazinzi. Nakukumbusha kama mim nilisema mapema siruhusu dhambi yoyote. Unaposema nafundisha watu kutubia kufanya uzinzi, umehakikisha wewe ni muongo. Bakia na picha yako wewe unayetetea dhambi fulani ukiwaza kama tukio lake siyo mauti. Inakupasa kuheshimu neno la Mungu linalosema “mshahara wa dhambi ni mauti”.

  Ninayojibu hapa inahakikisha hujajibu ipasavyo au umeshindwa au una UPUNGUFU, pengine ndio maana hilo swali hukuligusia.
  Kwa hiyo ungali unadaiwa, hujajibu lolote au ungali ndani ya upungufu, njooni ufunzwe. Sivyo huna mamlaka ya kunibeba pabaya ulipo. Ninaendelea kuwekea mara ya 8 swali zangu.
  Kwa matusi, sikushangae, kwani ndivyo ulivyo.
  Unataka maswali mengine wakati hakuna ulilojibu? Nilikuambia kam huna jibu unyamaze kimya. Unajifanya mwenye kujua wakati unachojua ni uongo mtupu!!!

  Other comment:

  Kam unaemwita Bwana Jela ni yule Ziragora aliegundua kam wewe ni muongo professional basi umehakikisha umeridhika kuwa ndani ya jela iliyowekewa waongo pamoja na Ibilisi bwana wao. Lwembe, ukitazama jinsi umejitumbukiza mwenyewe ndani ya Jela, huoni kam unaandika bila kufahamu unachoandika? Wewe ambae unapinga kiupofu neno lililo hai ninalokuletea kila leo, iweje tu uwe umetumbukia ndani yangu? Unamaanisha umeguswa na Neno? Uwe muungwana, utuambie basi yaliyo kweli. Kama Injili imekuingia, si usemeshe kweli? Unafikiri kuna atakaekucheka? Pengine utatoka ndani ya jela la waongo, RM akutie ndani ya jela ya wenye haki, ile ambayo Paulo anasema katika Waefeso 3:1.

  Ubarikiwe.

 40. Ziragora,

  Kwa vile inaonekana kutokana na jazba umeshindwa kuyaona majibu ya maswali yako niliyokuletea, na hivyo unarudia rudia maswali yaliyokwisha kujibiwa, basi ngoja nikujibu upya tena, nawe jaribu kuwa muungwana uyasome majibu kwa utulivu, kisha nawe uyajibu niliyokuuliza huko nyuma, uache kujibaraguza!

  Haya:
  JIBU LA SWALI LAKO “A”:
  Hakuna mahali popote nilipoitoa nje Dhambi ya Uzinzi, bali nimeirejea Hukumu yake baada ya kuwaona mnadanganyana kwamba Mkristo anaweza akazini na akiutubia uzinzi wake atasamehewa, ukaurejea na ule mkasa wa yule mwanamke mzinzi!!! Ndipo nikakuambia kuwa Uzinzi ni Dhambi ya mauti kwa Mkristo, haina dhabihu! Nikakuambia kuwa hata Kristo alipozungumzia Talaka, aliishia kwenye Uasherati tu, hakuzungumzia Uzinzi, na nikasema kwamba asingezungumzia Talaka kwa Mzinzi maana huyo anapaswa kuuawa kwahiyo huwezi kuitaliki maiti! Nikakuona hukuelewa, na hata sasa naona bado HUELEWI!!!

  Vifungu ulivyovinukuu, 1 Wakorintho 6:7-11, mbona viko wazi sana! hao wanaoambiwa mambo hayo ni Kanisa changa, ambalo kiulinganishi linafanana sana nasi. Yaani ni kama tu kanisa analoliongoza “Bwana Jela”, akiwafundisha wakristo kuutubia Uzinzi wanaoufanya ndani ya wito wao wa utakatifu, ndipo mtume Paulo anawaonya kwamba, Mkristo anayeyashiriki mambo hayo hataurithi Ufalme wa Mungu! Basi ulipaswa utafute kujua kwanza Ufalme wa Mungu ni nini (usikalie tu kwenda mbinguni!), ili umuone na huyo aliye nje ya Ufalme huo hali yake ikoje!!! Kwa kukusaidia, Roho Mtakatifu ndiye Ufalme wa Mungu, kwahiyo mkristo aliyeyapokea mafundisho yako ya kuutubia Uzinzi HATAURITHI Ufalme, atabakia kuwa mteja wa kanisa tu maisha yake yote!!

  Mzinzi anayeweza kusamehewa ni huyo Mpagani anayeujia Ukristo. Huyu akiisha kuipokea Injili na Kubatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo, Dhambi zake HUONDOLEWA katika Hesabu ya Mungu kama Mdo 2:38 inavyolitangaza jambo hilo, naye mtume Paulo akilithibitisha Neno hilo ktk hivyo vifungu ulivyovinukuu, “11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  JIBU LA SWALI LAKO “B”:
  Kulingana na uelewa wako uliopindishwa kwa hekima ya dini, ikikuongoza ktk kuamini kwamba Mkristo Mzinzi anaweza kuutubia Uzinzi wake, tukio la huyo mwanamke mzinzi na kupona kwake kipondo, kwako wewe ni lazima uishie kumuona Kristo akimhurumia huyo mwanamke!!

  Bali nilikuambia kuwa Kristo ndiye Torati, na katika kipindi hicho cha huyo mwanamke, Torati ndiyo ilikuwa Kiongozi, naye Kristo hakuja kuitangua, sijui kama unalielewa vizuri hilo! Nikakuambia kuwa Kristo aliipitisha Hukumu juu ya mwanamke huyo kulingana na Torati, HAKUMHURUMIA wala KUMSAMEHE! Nimekusihi mara nyingi upunguze hisia za dini ktk majadiliano ili uyaone na usiyoyafahamu, lakini you are so starchy! “…akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.” Je hii ni Huruma au Hukumu? Kama unang’ang’aniza kwamba hii ni Huruma, na hii hapa ni nini, Lk 7:48, “Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako”???

  Kristo aliipitisha HUKUMU kulingana na Torati, bali kulikuwa HAKUNA anayestahili kuitimiza HUKUMU hiyo. Nikakuambia kuwa Hukumu inaposhindikana haimainishi kuwa huo ni Msamaha! (Usome vizuri mchango wangu wa tarehe 25/11/13) Usiwadanganye watu na mambo yako ya dini dini! Yesu alimtahadharisha asirudie tena uzinzi wake kwani wale wauaji wake walikuwepo na huko mbele waliendelea na shughuli hiyo maana hawakuipokea Injili, na si kwamba alimsamehe au alimhurumia, hizo ni hisia zisizo na faida!

  JIBU LA SWALI LAKO “C”:
  Nilikuambia kuwa HAUIJUI Dhambi kwasababu ulikataa kwamba Sheria ndiyo inayoifunua Dhambi, kwahiyo utaijulia wapi Dhambi, ndio maana unafikiri Mkristo anaweza kuutubia Uzinzi!

  Hata hili unalohangaika nalo, kwamba, “”Mtu akikuambia « kila ukeukaji wa maagizo/sheria ya Mungu ni dhambi », wewe unasema hajue, sasa KOSOA ile sentence, tutakuelewa”; Hebu linganisha na mada uone kama kauli yako hiyo inaendana au umepoteza mwelekeo, “Dhambi zote ni sawa Mbele za Mungu?” Ukiukwaji wa Sheria ya Mungu ni Dhambi, hilo ni kweli kabisa, lakini swali ni je, ukiukwaji huo wote ni sawa mbele za Mungu? Ndipo tukaona huko kwa Mwalimu (Torati), kwamba kuna ukiukwaji unaoweza kutubiwa na usiotubiwa, kama wa Uzinzi, hili ndilo unalolikataa ukisema kwamba unaweza kutubiwa, kwa rejea gani, hiyo ya mwanamke mzinzi aliyemkosa wa kumponda mawe! Unaona ulivyotoka nje!

  JIBU LA SWALI LAKO “D”:
  Hukumu za uovu unaostahili kifo ktk Agano la Kale zilkuwa hivi: Kum 17:5-7
  “… ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe. Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo uovu katikati yako.”
  Huyu hapa mt Paulo akilisisitiza jambo hilo:
  Ebr 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.”

  Naye mwanamke yule Mzinzi ilimpasa adhabu hiyo, bali wote wanaostahili kuitimiza adhabu hiyo, nao pia iliwastahili adhabu hiyo hiyo; ni sawa na mwizi kumpiga mwizi mwenzake!!

  Sasa kwa leo hii ndg yangu mambo yamehamia rohoni, si umeliona hitaji la Hukumu hiyo, linataka mashahidi wawili au watatu, sasa leo hii ni nani shahidi wa mambo ya rohoni? Mungu ndiye Shahidi maana yeye ndiye mwenye kuzijua siri za mioyo! Ukimtamani tu mwanamke, hata wakati unahubiri madhabahuni, TAYARI umekufa!!!! Hebu wewe mwenyewe unganisha hicho kifungu cha Ebr 10:28 na hiki cha 29 “Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
  Unaona? Leo ni adhabu kubwa zaidi ya ile ya kupigwa mawe!!!!

  Ninaamini nimeyajibu tena maswali yako yoote, ingawa umesema yako mengine, basi yalete tu kwa moyo wa furaha ili tuyatazame sote huenda yakatusaidia kukaa sawa!

  God bless u, my beloved ‘Bwana Jela’!

 41. Lwembe,

  Kwa vile wewe huwa huwezi kutofautisha kati ya usichokielewa na unachokielewa, utaendelea sana kuniona kuwa mimi ndo sijui, alhali wewe unaleta vitu ambavyo viko tenge, na kutulazimisha tukubali hivyo ndivyo vilivyo.

  Na hayo yote ni kwa sababu umejidfanya unajua sana kiasi kwamba huhitaji kujifunza elimu ya biblia.

  Ivi unaponiambia kwamba jambo la kuokoka ni hapo unapoamini injili na kubatizwa, yaani Mark 16:16, vipi na mimi nikikuambia kuwa suala la kuokoka si lazima mtu mpaka abatizwe kwanza ndo aokoke, na nikanukuu Rumi 10:9 ambayo haijajumuisha suala la ubatizo ili mtu kuokoka, utasemaje hapo.

  Anyway, hebu nioneshe hiyo mistri inayosema kuwa kuna hatua tatu za kuzaliwa mara ya pili!

  Usijaribu kukwepa kujibu maswali kwa kuponda suala la kutumia mantiki katika uielewa biblia, huo ni umasikini wa akili.

  Kama kuna hekima ya kawaida na kuna hekima ya kiungu, kama macho ya kawaida na macho ya rohoni. n.k, basi ujue kuna logic ya kawaida na kuna logic ya rohoni au ya kiungu.
  Nilishawahi kukwambia kuwa kama unadhani akili aliyotupa Mungu ni useless, basi jaribu kuwa kichaa au chizi uone kama utamwelewa Mungu.

  Narudia tena, usipokubali kujifunza elimu ya biblia/ kwenda chuo, utaendelea kuleta unachokiita ufunuo ambacho ni upotofu tu.

  Onyesha mahali biblia inasema kuwa kubatizwa kwa Roho mt. ni kutukuwa.
  Yesu alisema Roho mt. anatupa nguvu mara anapokuja juu yetu, wala hakusema mtatukuzwa mkishajiliwa na Roho mt. juu yenu.

  Lwembe usilazimishe mawazo yako kuwa fundisho, utaishia kusikojulikana.

  Usikwepe, onyesha hapa kama unazielewa hizo tungo mbili, yaani Kuokoka, na Kuzaliwa mara ya pili, usitulazimishe tu kwa kutumia maandiko kwa nguvu, bali litumie kwa halali!

  Eti unaniambia nifuate biblia inachonifundisha! Wewe na mimi nani anafuata, mbona biblia haijawahi kusema kuwa kuna hatua tatu za kuzaliwa mara ya pili?

  Kumbe unajua kuwa mimi ninawakufunzi, safi sana!
  Sasa wewe wakufunzi wako ni akina nani wanaokufundisha hayo?

 42. Dittu,

  Hahahahahaha! Aliyezini bila kukusudia ni yupi, Lutu au binti zake? Kuzini kunamhusu mwanamke aliyeolewa, hao mabinti wa Lutu walikuwa ni mabikira, kwahiyo jambo la kuzini halipo hapo!

  Halafu, katika nyakati hizo kumbuka kwamba Sheria ilikuwa bado, isipokuwa waliishi kwa Dhamira (Conscience), na pia ile Nguvu ya Utenganisho, ile iliyowatenganisha na Ibrahim, ilikuwa inafanya kazi hata ikamzuia Lutu asiende huko na badala yake akakae mapangoni! Unaona inavyokuwa Mungu akiisha kukutenga? Lutu alikuwa amekwisha kutengwa na Ibrahimu, katika ujumla wa kutengwa, mpaka uzao wao!!!

  Pia uzao wa Lutu na wanawe, unaweza kuwaona humo ktk Maandiko, uzao huo HAUMO ktk WOKOVU, bali HUKUMU! Mwa 19:36-38
  “Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.”

  Asante Dittu, tuendelee kulitafakari hili jambo, Uzinzi wa bila kukusudia!!!

 43. Sungura,

  Wewe kulikataa fundisho unaloliita langu, hakuubadilishi ukweli wa Injili!

  Iwapo huzifahamu hatua hizo tatu, hilo si jambo la ajabu sana, mbona hata lililo wazi zaidi, hili la KUOKOKA, unashindwa kufahamu kwamba ni hapo unapoiamini Injili na kubatizwa ndipo unakuwa umeokoka, kama inavyosema Mk16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”!

  Sote tunafahamu kwamba Petro alikuwa amebatizwa Ubatizo wa Yohana, ishara ya kuupokea huo Ujumbe aliokuja nao Yohana ambao ulimtayarisha kumpokea Kristo. Hii ikiwa ndiyo Hatua yake ya Kwanza katika kuiendea Nchi ya WOKOVU. Jaribu kuwarudia wakufunzi wako ktk chuo ulichosoma, watakuelewesha, maana hata Siyi angalau anajua kuwa kuna hata Hatua za kutembea, wewe sijui ulisomea chuo gani!

  Hatua ya Pili ya UTAKASO, Petro pia aliipitia. Walitakaswa kwa Neno, hilo linalopaswa kujaa kwa wingi ndani yako badala ya mafundisho dhaifu ya kidhehebu yanayolikana Neno la Mungu, Yoh 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Neno la Mungu ndilo linalotakasa. Tazama Kristo anachokuambia, “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.” Hapa ndipo kuna umuhimu wa kukipokea walichokifundisha mitume ndipo nawe Utakaswe, vinginevyo unabaki na uchafu wako, licha ya kuwa UMEOKOKA!

  Kama Hatua hizo alizozipitia Petro kwa ushahidi wa Maandiko zingetosha, basi Kristo alikuwa na haja gani kumwambia, “…lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako”? (Lk 22:32) Kuna Hatua inayomkamilisha Mkristo, na akiifikia hiyo ndipo anaweza kuwasaidia ndg zake, si kumaliza chuo! Unaweza kumaliza chuo cha Biblia na ukawa Hujakamilika! Basi huyo asiyekamilika, bali ana DD yake ya juu kabisa, akikabidhiwa kusanyiko, ni lazima aliangamize!

  Lakini kuna Hatua ya Tatu, ambayo ni KUTUKUZWA, yaani Ubatizo wa Roho Mtakatifu, ambako ndiko kule “kuwekewa Roho wake” kulikotabiriwa ktk Ezekieli! Nikakuambia kuwa huyu ndiye anayezungumziwa kuhusu kutokutenda dhambi. Huyu yuko Kamili, anamdhihirisha Kristo, maana AMETUKUZWA ili aweze kuifanya kazi hiyo, amejaa Ujasiri. Unaweza kuwaangalia mitume ukajifunza jambo!!

  Naona unanitaka nianze kutumia logic, lakini hiyo ukiitumia ktk Neno la Mungu, utaishia huko unakokwenda, nje ya kambi! Angalia unachoisumbulia akili yako kuhusu Kuokoka na Kuzaliwa mara ya pili,
  -Je hiki ni kitu kimoja – how?

  -Ni vitu viwili tofauti, nini kinatangulia-how?

  – Inawezekana mtu akawa ameokoka na akawa hajazaliwa mara ya pili- how?
  
-Inawezekana mtu akawa amezaliwa mara ya pili na akawa hajaokoka – how?

  Maswali yote haya unayojiuliza ni useless garb, labda yanafaa kwa matumizi ya chuo ili ufaulu mitihani yao, otherwise fuata Biblia inachokufundisha! Hebu niambie uta define vipi jambo usilolijua?

  Mungu na atupe kuyafahamu na Maandiko, kwa kadiri tunavyojifunza!

 44. Lwembe,
  Kwa kifupi nimelikataa fundisho lako, maana linachembe nyingi za uongo kuliko zile za ukweli. Shida kubwa huwa siyo kunukuu kile biblia imesema, bali ni kule kuelewa hicho kilichosemwa kina maana gani.

  Unajaribu tu kutatiza mambo pasipo maana yoyote ya msingi, ili kuonekana kuwa umechambua vitu, laikni kumbe ndo umezidi kuvichanganya.
  Hatua tatu ulizozisema zinakwamishwa na ukweli uliotokea kwa Kornelio na wenzake. Lakini badala ya kusema jambo lenye maana, unazidi tu kuleta wazo jepesi kuwa suala la Kornelio siyo mimi nalifanya kuwa jepesi na kumbe ni gumu kama jiwe.

  Najua vizuri kuwa hakuna sehemu biblia imesema ”kuna hatua tatu za mtu kuzaliwa mara ya pili”, bali wazo hilo limetokana na uchambuzi wa mtu wa maandiko( sijui huyo mtu ni wewe au kuna mtu aliyekufundisha hivyo).
  Kama uchambuzi huo ungewiana na maandiko pasipo kuacha shaka, mimi naamini katika uchambuzi wa maandiko ili kuweka wazi kilicho ndani yake, hivyo nisingekukatalia hata kidogo.

  Sijui kama kichwa chako kinaelewa sawasawa hizi tungo mbili: KUZALIWA MARA YA PILI, na KUKOKA, maana wewe ni miongoni mwa watu wasiopenda kujifunza kitu kinaitwa elimu ya biblia.

  Unatakiwa tu ujiulize logically:
  -Je hiki ni kitu kimoja – how?
  -Ni vitu viwili tofauti, nini kinatangulia-how?
  – Inawezekana mtu akawa ameokoka na akawa hajazaliwa mara ya pili- how?
  -Inawezekana mtu akawa amezaliwa mara ya pili na akawa hajaokoka – how?

  Na ili kujua usahihi na ukweli lazima u-define kila kimoja ili kupata maana yake, na ndipo utajua nini ni nini?

  Tofauti na hapo, mimi naona unaongea tu vitu vyepesi kwa lugha ngumu!

  Nakushukuru.

 45. Lwembe,

  Usifikiri sisi ni wasiofahamu kama wewe. Ile maneno unayorudilia kama kitoto kichanga haina msimamo ao haiwezijibu kwa hoja. Mimi sijali nayo. Aliye jela, hata akisema mara elfu neno “jela”, hio haimuweki huru. Au kam akirudilia mazarau haimuweki huru. Unahakikisha tu ulicho. Mim nime copy-paste niliokuswali na nikasema kwa heshima ya wana SG wote kam si mimi tu ninaewezafahamu kama ulijibu ipasavyo. Sasa kusema ulijibu wakati ulijibu kwa hoja tofauti, maana yake hoja unayotengeneza wewe mwenyewe, hiyo ni kutafuta kuleta watu kuzubaa ili ugeuze mada kuwa ingine hapo ukiisha shindwa. Kweli nina mengi ya kufundisha hapa kwa hii mada, lakini kwani wewe ni kipingamizi ninataka ujibu kwanza hata wandugu wengine wathibitishe kam kweli ulijibu ipasavyo. Na kwa uongo wako, tubu. Kupeperusha neno jela katika kila mada siyo garama ya uongo.Uongo wako ukiifanya kama tangazo, utakuwa umehakikisha umeridhika kuwa nani ya jela iliyowekewa waongo pamoja na Ibilisi rafiki yao. Kam wewe ni mukristo, imekupasa kufahamu kama dawa ya uongo ni toba.
  Kwa hiyo nakuwekea tena swali zangu. Ukishindwa, kiri kushindwa kwako kiisha nami uniswali. Mimi ni muungwana bwana, nikikosa jibu nitasema. Nikikuta hoja yako iko strong nitakuambia unifundishe. Kutembea na Mungu ni kuacha Mungu anakuongoza, wala si kujifanya anaefahamu kila jambo hata kwa hila. Lwembe, hiyo mambo ya kinyokanyoka unayoyafanya ni matunda ya Ibilisi.

  Leta Jibu. ikithibitishwa na watu kadhaa kama ni ya kingwaana, swali hiyo itawekwa pembeni.

  A) Naona hapa si lazma tutoe shahiri ingine, nataka nirudishe upya niliyokutolea iwe zamu yako ya KUTOA NJE YA ORODHA DHAMBI YA UZINZI. Unionyeshe umeitia wapi na dhambi nyingine zimebaki wapi. Pia uniambie kama unajitambua kuwa na UPUNGUFU au la.

  “1 Wakorintho 6:7 Basi imekuwa UPUNGUFU kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?
  8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
  9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala WAABUDU SANAMU, wala WAZINZI, wala WAFIRAJI, wala WALAWITI,
  10 wala WEVI, wala WATAMANIO, wala WALEVI, wala WATUKANAJI, wala WANYANG’ANYI.
  11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  B) Kwa nini unakwepa ? Hii andiko ya YOHANA 8, unaisema juujuu kirahisi tu, wala hupendi itika kama kulikuwa huruma. Wewe unakimbilia kwenye hukumu. Nilikuuliza wakati Yesu alimwambia mwanamke aende na asitende dhambi tena, hapo hakumhurumia ? Kwani Yesu angehesabu huyu mwanamke kuwa maiti kwa nini aambie MAITI ISITENDE DHAMBI tena ?

  C) Unaposema hatujue dhambi ni nini, nadhani unadaka picha yako kwa kuibandika wengine. Uwe mwanaume na useme yaliyo kweli. Mtu akikuambia « kila ukeukaji wa maagizo/sheria ya Mungu ni dhambi », wewe unasema hajue, sasa KOSOA ile sentence, tutakuelewa.

  D) Kwani hata waliokuwa wakiua wazinzi(kufwatatana na torati), ilibidi hawo wazinzi wanaswe, na kuwe wanaohusika kuwaua. Kama una ujuzi wa hii mada, nakuomba kwa leo UTAJE WATU WANAORUHUSIWA KUWAUA WAZINZI.

  Ndugu Lwembe, hizi ni swali tu, lakini huko juu kuna hoja nzito nzito ulizokwepa. Zitakurudilia hadi wapendwa wote wanathibitisha kam umejibu ipasavyo. Mim naendelea iweka kwa manufaa ya wote.

  Asante.

 46. Lwembe, Nashukuru sana ndugu yangu kwa kunielewa, kuhusu kuzini bila kukusudia jibu langu ni “NDIYO” Rejea Mwanzo 19:30-38. Ubarikiwe!.

 47. Ziragora,

  Umepatwa na Mfadhaiko wa Injili nini???

  Hata unachong’ang’ana kukielezea, hakieleweki kabisa!!! Hebu tuliza munkari kidogo, hali inaweza kuwa nzuri kisha tukaendelea na Injili, kuliko haya yasiyoeleweka; mara pembe, mara jiwe, mara jela, mara simba anameza watu, mara jela ya wenye haki, mara ukimbie SG, mara Jiwe la Pembe, naona uko karibu kabisa kuirudilia mizimu!!!

  Maswali yako yote nilikwisha yajibu tangia tarehe 25/11 ila naona hukuyaona kwa Mfadhaiko uliokukumba tu!

  Pole pole rafiki yangu, Injili siyo “lele mama”!!!!

  Ubarikiwe!!

 48. Dittu,

  Mimi nimekuelewa vizuri sana katika uliyoyasema, ila hata ulimwengu unayo Hukumu ya mtu aliyeua bila kukusudia. Shauri lake huingizwa katika mfumo wa “manslaughter” na mwendesha mashtaka akijiridhisha kwamba ulipomuua huyo ilikuwa ni jambo la bahati mbaya, basi huyaondoa mashtaka mahakamani, nadhani wanaita “nolle prosequi”

  Je, huyo aliyeiba Tshs 5 na aliyezini, uzito wa dhambi hizo ni sawa? Pia nikuulize, unaweza ukazini kwa bila kukusudia?

  Ubarikiwe!

 49. Naomba kutofautiana na michango yenu. Nionavyo mimi ni kwamba kuna dhambi kubwa na ndogo. 1 DHAMBI KUBWA NI NINI? Hii ni aina ya dhambi ambayo mtu anaifanya kwa kudhamiria hata iwe ni kuiba Tsh 5/=. 2 DHAMBI Ndogo ni ile ambayo mtu anaifanya pasi kukusudia. kwa mfano, mtu akiua kwa bahati mbaya bila kukusudia. Kwahiyo wote watahukumiwa na Mungu “accordingly” kwa sababu hukum zake ni za haki.

 50. Sungura,

  Jambo jingine unalohangaika nalo kulifanyia Fundisho ni la Kornelio. Bali jambo hilo liko wazi sana kama wewe huisoma Biblia yako katika furaha ya kulijua Neno la Mungu, haswa kutaka kuujua Moyo wa Mungu, ilikuwaje kwa Mmataifa yule Najisi!

  Ingawa unapenda kulirahisi jambo hili la Kornelio, lakini hilo ni GUMU kama Jiwe! Mdo 10:1-2:
  “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.” (Kama unao ufahamu utaelewa mtauwa ni mtu wa aina gani, na pia kuwa DAIMA si siku moja!!)
  Jamani, katikati ya wenye kuitwa na Mungu wawe Watakatifu, lakini wakisua sua, mara oh, hakuna Hatua Tatu, mara oh, Hatua ya Tatu tutaifikia mbinguni, nk; lakini alikuwepo Najisi ambaye aliugusa moyo wa Mungu; Haleluyaaaaaa, ninapata Nguvu na kutiwa moyo sana ninapoyarejea haya ya Kornelio!!! “… Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu” hili si jambo dogo ktk namna yoyote ile; kulirahisi ni kukosa Heshima!!!

  Basi kama Sala na sadaka zimepokelewa mbinguni, yeye mwenyewe vipi? HAWEZI kupokelewa!!! Mungu huwa hakiuki Utaratibu wake, hawezi kumpokea Kornelio, ni lazima aipite Njia iliyotayarishwa kwa ajili hiyo, kwa wote walioitwa wamjie Bwana Mungu, ambayo ni kupitia Kristo. Mimi sijui Kornelio alimjua Mungu lini, bali najua kwamba Mungu ilimbidi amlete huyo aliyemkabidhi UFUNGUO ili mtu wake apate KUINGIA! Umeelewa Sungura, hiyo ndio God’s Provided Way ya kuingia katika Ufalme wa Mungu, kama ambavyo Kornelio hakuweza kupokelewa, ndivyo nasi tusivyoweza kupokelewa bila kupita katika Lango hilo alilolifungua Petro ktk siku ya Pentekoste, sala zetu na sadaka zetu hazijalishi!!!

  Kuhusu wewe kujazwa RM, ndio nikakuambia kuwa na hao pia wamejazwa RM halafu wanaamini kwamba Samweli aliyepandishiwa Sauli na yule mwanamke mchawi wa Endori alikuwa ni MZIMU!!!! Kwamba hata huelewi nilikuwa nakuonesha nini, inashangaza zaidi unaponiambia kuwa eti ulimpeleka RM uliyenaye kwenye Neno akakuambia kuwa HAKUNA Hatua Tatu, ila ndiyo yale yale; wewe unapewa “roho mpya” tu, ambaye anaweza akapindishiwa kwenye dini na usielewe!!!

  Ila nimefurahi kukuona katika tafakari ya Neno, pole pole “Tutafanana naye”!

  Asante sana!!!

 51. Sungura,

  Nikijirudisha katika Injili. Nilikuambia kwamba kuna Hatua Tatu anazozipitia Mkristo ndipo afikie kule KUTOKUTENDA DHAMBI. Ingawa umeniita MUONGO kwa jambo hilo, na kwamba halina mashiko, bado ninaamini kwamba umekuwa na mtazamo huo kutokana na kutolielewa vizuri au nusu nusu jambo zima la WOKOVU, au umeridhika na unachokijua, hivyo huna tena nafasi ya kujifunza usiyoyafahamu.

  Hata tukilitazama kwa haraka hilo unalolisema wewe kwamba Mkristo anapoianza Hatua yake ya Kwanza, kule Kuhesabiwa Haki hapo anapoAmini na Kubatizwa na kuwa ALIYE OKOKA, kwamba huyo anakuwa amezaliwa mara ya pili kuanzia hapo; iwapo jambo hilo litakuwa hivyo, basi Biblia itavurugika!

  Kuzaliwa mara ya pili kunakozungumziwa ni huku hapa, Yn 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na KILICHOZALIWA KWA ROHO NI ROHO.” (msisitizo ni wangu) Ndio kusema Mkristo anayezaliwa hapa ni roho, kuhusu Mkristo huyu Biblia inasema, 1 Yoh 3:9,
  “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.”

  Ndipo nikakupa mfano wa akina Anania na Safira, nikakuambia kuwa walikuwa ni sehemu ya kusanyiko la waaminio, kwa uhakika walikuwa WAMEOKOKA, lakini waliishia kutenda dhambi. Je, Andiko hili la 1 Yoh 3:9 tutalioanisha vipi na mkasa huo iwapo tutajiaminisha kwamba walipoHesabiwa Haki ndipo walipozaliwa mara ya pili?!! Nguvu ya kifungu hicho inaondoka, verse hiyo inakuwa fable!!!

  Basi kama Maandiko yanavyojieleza, kuna Kuitwa, kisha hao walioitwa Hutakaswa, na mwisho Hutukuzwa; hizi ndizo Hatua Tatu zinazomkamilisha Mkristo. Pia kwa ajili hiyo Mungu amewaweka watumishi wake ktk makusanyiko yetu, Efe 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; KWA KUSUDI LA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.”
  Unaona, kumbe Mwili wa Kristo unajengwa! Kwa material gani? Neno la Mungu, pekee ndilo linaloweza kuujenga Mwili wa Kristo! Mapokeo yanajenga mwili wa dhehebu!!!

  Pia, kuhusu Wokovu, si kwamba jambo hili limekurupuka tu, ni Programu iliyopangwa katika hizo Hatua katika maana kamili ya kumkamilisha Mkristo. Kuna Kuhesabiwa Haki, halafu Kutakaswa na mwisho Kutukuzwa, ambako ni kuvishwa Utukufu wa Mungu! Tazama anachokisema Mungu hapa ktk Ezekieli 36:26-27
  “Nami nitawapa ninyi MOYO MPYA, nami nitatia ROHO MPYA ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia ROHO YANGU ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” (msisitizo ni wangu)

  Umeziona hizo Hatua? Jambo hili linakamilika katika ujio wa Kristo!
  1. Moyo Mpya wa nyama unaoweza kulipokea Neno la Mungu; “Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo”; ndiko Kuhesabiwa Haki kwa Imani!!

  2: Roho Mpya, Mungu anatuwekea roho mpya ndani yetu, matamanio mapya mwenendo mpya, shauku mpya, hii ndio Hatua ya UTAKASO! Wengi huamini kwamba katika Hatua hii wamejazwa RM, labda ni ile furaha inayoambatana na roho mpya na vipawa vya RM vinavyoanza kujidhihirisha ndani yao, labda walinena au chochote kile, bali hiyo ni roho mpya tu, bado endelea kula Mkate mpaka mbawa ziote!!!!

  Katika Hatua hizi mbili, Mkristo anaweza kutenda dhambi na hata akapotea!!!

  3: ROHO yake! Mungu hukupa Roho yake, naye Mungu hakushukii kipweke bali Hushuka katika Utukufu Wake, Utukufu wa Mungu Humfunika Mkristo katika Hatua hii, hata nawe ungeisikia Sauti ya Mungu ikikuambia ”Wewe ni mwanangu mpendwa”!!! Huyo huwa ni kazi iliyokamilika, UMETIWA MUHURI!!! Ukiisha Funikwa kwa Roho Mtakatifu, shughuli inakuwa imeishia hapo, kazi alizozifanya Kristo na kubwa zaidi utazifanya, utamdhihirisha Kristo ndani yako.

  Hii ndio Hatua ambayo Mkristo anakuwa amekamilika, huyu HATENDI Dhambi! Huyu ndiye ana uwezo wa kulitimiza Neno hili ktk Efe 4:13
  “…hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.”
  Unaona! Hatua hii ya Tatu ndiyo inayoweza kulikusanya Kanisa, hapo litakapofikia kuongozwa na RM ambaye atalileta Kanisa lote ktk “Umoja wa Imani” kama walivyokuwa mitume, bali kwa sasa Kanisa lingali liko Jangwani, huko walikojaa akina Kora nk kila mmoja akijichukulia njia yake; na kila mmoja anasema anaongozwa na RM!!! Bali RM si wa machafuko, Yeye kazi yake ya kwanza ni kukuaminisha Neno, tena hukufanya uliheshimu na kulipenda Neno lake kwani hilo ni Mungu!

  Ubarikiwe!

 52. Sungura,

  Kufundisha jambo kinyume na Mungu alivyolisema ni DHAMBI, ni sawa na KUONGEZA ama KUPUNGUZA katika Neno lake. Kwahiyo changamsha akili, unapofundisha kuwa KIINGILIO ni sawa na CHANGIZO, au kwamba WAZINZI wanasamehewa, au Nabii wa mwisho ni Yohana Mbatizaji, jambo hilo ni DHAMBI, na mada hii inazungumzia DHAMBI, kwahiyo ukinitaka nisizungumzie niliyojifunza na mifano yake, basi faida ya kuwepo hapa ni nini, kulumbana?!!!!!

  Binafsi ninajadili kama mtu mwenye wajibu, na sifanyi unafiki kwasababu ninaipenda Injili, vinginevyo ni rahisi kujiingiza katika Gospel irrelevance kwa malumbano yasiyo na mwelekeo wala faida; basi itatufaa sote iwapo tutajirejesha katika jambo la msingi, INJILI!!!!

  Mijadala itupanue ufahamu!

 53. Lwembe,

  Nimeona ni vema nikurudishie swali zangu ulizoshindwa jibia ili usije ukalete mambo ambayo watu wanaotusoma tu hapa tunapofikia hawataelewa. Unapojaribu ku connect ndugu Sungura na Ziragora, si unapenda danganya watu wawaze kama mmoja ana hoja na mwengine anamfwata tu? Kwa taarifa yako Ziragora ana upako, na Sungura ana upako. Na katika hii mada, Sungura anakudai yake nami nakudai yangu. Usiwaze una hila zinazowezameza upako tunao. Sasa kwa nini hukutaja walio upande wako? Umewakosa? Au kwa nini hukuendelesha orodha ya Sungura, Ziragora, …. ? Umeshindwa kwani ni wengi, si ndio?

  Ninaweka mara ya 5 na ninangoja tu ujibu. Ile ya mwisho ndio nimeweka mara ya 2 lakini hilo swali ulilipewa mapema ukaendelea likwepa. Nitakapoendelea pekua swali zangu ulizoshindwa jibu, nitaziongeza tu. Uko huru, kama huna jibu, unyamaze kimya, usiudhi wana wa Mungu. Au kama wewe unakosa jibu, kiri kwamba umeshindwa, kiisha wewe utuswali, tukufundishe sawa jinsi nimeandika hapa juu. Kwani tangu mwanzo wa mjadala hadi leo, hakuna hata mtu mmoja anaedaiwa jibu kwako, lakini wewe unadaiwa.

  A) Naona hapa si lazma tutoe shahiri ingine, nataka nirudishe upya niliyokutolea iwe zamu yako ya KUTOA NJE YA ORODHA DHAMBI YA UZINZI. Unionyeshe umeitia wapi na dhambi nyingine zimebaki wapi. Pia uniambie kama unajitambua kuwa na UPUNGUFU au la.

  “1 Wakorintho 6:7 Basi imekuwa UPUNGUFU kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?
  8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
  9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala WAABUDU SANAMU, wala WAZINZI, wala WAFIRAJI, wala WALAWITI,
  10 wala WEVI, wala WATAMANIO, wala WALEVI, wala WATUKANAJI, wala WANYANG’ANYI.
  11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  B) Kwa nini unakwepa ? Hii andiko ya YOHANA 8, unaisema juujuu kirahisi tu, wala hupendi itika kama kulikuwa huruma. Wewe unakimbilia kwenye hukumu. Nilikuuliza wakati Yesu alimwambia mwanamke aende na asitende dhambi tena, hapo hakumhurumia ? Kwani Yesu angehesabu huyu mwanamke kuwa maiti kwa nini aambie MAITI ISITENDE DHAMBI tena ?

  C) Unaposema hatujue dhambi ni nini, nadhani unadaka picha yako kwa kuibandika wengine. Uwe mwanaume na useme yaliyo kweli. Mtu akikuambia « kila ukeukaji wa maagizo/sheria ya Mungu ni dhambi », wewe unasema hajue, sasa KOSOA ile sentence, tutakuelewa.

  D) Kwani hata waliokuwa wakiua wazinzi(kufwatatana na torati), ilibidi hawo wazinzi wanaswe, na kuwe wanaohusika kuwaua. Kama una ujuzi wa hii mada, nakuomba kwa leo UTAJE WATU WANAORUHUSIWA KUWAUA WAZINZI.

  Ndugu Lwembe, hizi ni swali tu, lakini huko juu kuna hoja nzito nzito ulizokwepa. Zitakurudilia hadi wapendwa wote wanathibitisha kam umejibu ipasavyo. Mim naendelea iweka kwa manufaa ya wote.

  Asante.

 54. Bwana Yesu Asifiwe,

  Lwembe, na Wapendwa wote wana SG,

  Naona pengine mada imekwisha kwani haiendelee kabisa. Tunachosoma ni mambo mengine.

  Lwembe,
  Unayoyafanya ni kama Ibilisi anaenguruma akitafuta mtu amumeze. Najua umefika na hasira kwani umeona uelewano wa kiroho hapa kwenye SG; kwani wewe katika maandiko yako unajifanya rafiki ya matengano. Ndio maana unachanga mambo mengi ukijichanganya mwenyewe. Kama vile Ndugu Sungura amesema, mijadala ingali open. Unachoogopa kule hapa kingali. Hivi jua kama unachoka bure.

  Kinachonifurahisha ni kwamba naona harakati zote za kuangusha wakombolelewa wa Yesu hazifanikiwe. Hii ni ushindi wa Yesu juu ya mamlaka yote ya ulimwengu wa giza.

  Utaendelea kumpinga Yesu hadi lini? Kwani yeyote anaekuletea Neno la Yesu wewe unamletea torati unayosoma namna upendavyo, wala si namna Yesu apendavyo. Unafika kiwango unacheza na Roho Mtakatifu ukitaka mkamata kama kitu cha mchezo. Yesu ni Bwana wa torati, wala torati haimtawale. Nilikwambia ukiendelea kukwaa kwa Lile Jiwe la Pembe, utajimaliza mwenyewe, Lakini unaendelea kuwa kama kiziwi.

  Anyway, sisi hatuna chuki na mtu yeyote, kama wana SG wananikubalia na kama kweli una hoja kwa ajili ya hii mada kwa namna isiyowai ongelewa katika hoja zilizopita, hebu build that hoja cleary & shortly, tuijadili tena kwa utaratibu yote bila wewe kuingiza hila, iwe kwa manufaa ya wote.

  Hence, tupime tena , tuone kama unaweza okoka. Na kama umesahau, mada ni hii “Dhambi zote ni sawa mbele za Mungu?”. Please, kamata mda, usikurupuke, upime andika maneno inayothibitisha kama wewe ni muungwana makusudi usitulazimishe kukujibu tukifanya simple copy-paste.

  Mbarikiwe.

 55. Lwembe
  Unapoambiwa ukweli usiuite ni manung’uniko.
  Sijakwambia suala la kurejea misimamo yetu katika mijadala iliyopita, bali nimekwambia suala la kuchukua mawazo ya mtu aliyoyachangia kwenye mada nyingine na kuyaleta kwenye mada isiyohusika nayo.

  Hapa tunaongelea mada ya dhambi zote ni sawa, wewe unachukua comment ya mtu kutoka kwenye mada ya Viingilio kwenye semina. Huo ni uandishi uchwara hata kama hutakubali huo ukweli.

  Kama unaona uko na kitu cha kuendelea kusema juu ya mada ya viingilio kwa nini usiende kwenye uwanja wa hiyo mada ukachangia, si ipo wazi hiyo mada kama unataka kuchangia uchangie huko, kwani SG. wameifuta hiyo mada?

  Kama wewe unaona viingilio kwenye semina hiyo ni dhambi, hakuna anayekukataza kuamini hivyo, na mimi ninaona kuwa kiingilio kwenye semina si dhambi, hakuna wa kunikataza kuamini hivyo. Wewe ulitoa maelezo yako ya kwa nini unaamini viingilio si sawa, na mimi nilitoa maelezo yangu kwa nini naamini viingilio ni sawa. Wewe hukusema tu sentensi moja kuwa ‘ viingilio si sawa’ na mimi sikusema tu sentensi moja kuwa ‘viingilio ni sawa’.

  Kama unataka tuendelee kujadili viingilio tufanye hivyo kwenye uwanja wa mada hiyo siyo hapa kwenye mada nyingine. Huo ndio uandishi wa kiungwana.

  Lwembe nazijua vizuri sana hila zako za kutumia maneno katika uandishi wako.

  Unaponiambia vitabu 66 vya biblia vinalifanya neno, una hoja gani hapo, unajaribu kunifanya nione kuwa 66 ya vitabu vya biblia ina uhusiano na kauli yako ya …x666 katika kujazwa Roho mt.? Acha hizo gilba za kawaida. Najua nafsi yako inakushuhudia ukweli wa ulichokuwa nacho moyoni mwako kuhusu hiyo kauli ya ..x666.

  Kuna swali umeniuliza hapa ”Wewe una jambo gani ulilowahi kulifanya hata Mungu akalazimika kukuHesabia Haki?”

  Ulicholenga kujua hapa ni nini, halafu ukishakijua ufanyeje? Nianze kusema hapa kumwambia Lwembe kwamba niliwahi kufanya hivi na hivi kwa misingi gani sasa?

  Hata hivyo, kwani Kornelio alihesabiwa haki, au ni sadaka zake na maombi zilifanyika ukubusho mbele za Mungu? Hakujazwa Roho mt. kwa sababu ya hizo sadaka na maombi yake, bali alijazwa Roho mt. kwa sababu alimpokea kristo kama mimi ambavyo nilimpokea kristo.

  Hapa Lwembe umejiongelea tu chochote kwa sababu hoja yako ya kwamba kuna hatua tatu za mtu kuzaliwa mara ya pili imejikuta haina mashiko, kwa sababu kilichofanyika kwa akina Kornelio kimethibitisha kuwa hizo hatua ulizosema ni za uongo, ni mawazo tu ya kutungwa.

  Mimi hata sikujazwa kwa kusema asante Yesu. Lakini hata kama ingekuwa ni hivyo ubaya wake ni nini, kwa Paul aliweka kanuni gani ya kujazwa Roho mt.?

  ” Pia ni vizuri ukaelewa kwamba mimi si mkaguzi wa watu waliojazwa RM, kwa taarifa yako Siyi, Lenda, Vai, Bezaleli, Seleli, nao wote wamejazwa RM, halafu wanaamini kwamba Samweli aliyepandishiwa Sauli na yule mwanamke mchawi wa Endori alikuwa ni MZIMU!!!!”( nimekunukuu)

  Hapo na penyewe kuna point gani ya maana uliyokuwa unasema, si ndiyo hayo makorokoro ninayokwambia. Badala tu ya kuongea kitu cha maana unachotaka kusema unapoteza muda kusemasema watu kwa mambo yasiyokuwa na maana yoyote hapa .Haya, kama wao wanaamini hivyo unaniambia mimi hapa ili nifanye nini sasa?

  Unaniambia kama ninataka kujua kama nina Roho wa kweli nimpeleke kwenye neno.
  Ok, bila shaka umeona vizuri nilipompeleka kwenye neno nimekuthibitishia kuwa hatua tatu za mtu kuzaliwa mara ya pili ulizotuambia wewe ni za uongo.
  Maana kama zingekuwa za kweli hata akina Kornelio wangezipitia.

  Kwenye suala la dhmbi ya uzinzi kutosamehewa umekimbia kazi Lwembe!

  Lwembe ngoja nirudie kitu niliwahi kukwambia, kwamba kama kuna kitu ninakukubali wewe, ni uwezo wako wa lugha, hasa Kizungu. Hicho rafiki yangu uko vizuri mno, hongera.

  Lakini kwa habari ya uelewa wa mambo hapana!!

  Nakushukuru pia!

 56. … … …
  Sungura,

  Kuhusu kuandika “roho mtakatifu” kwa herufi ndogo, naona hilo umelielewa vizuri! Iwapo unaniona nafanya mzaha, basi ungenionesha ni wapi umeona jambo hilo likifanyika hivyo ktk Biblia, otherwise utakuwa ni mtu aliye confuse issues, akijidhanisha kuwa “doctrines” za kusanyiko lao ndiyo Standard!! Kuhusu gharama, nimeyapima yote kabla sijayaandika, HAKUNA mahali mtume Paulo alifundisha ujazwaji wa RM kama huo, na kwa sababu Mungu atatuhukumu kwa Injili aliyoihubiri Paulo, nadhani wewe ndiwe unayepaswa kujitayarisha kulipia gharama ya jambo unaolisimamia na kulitangaza, ambalo Paulo hakulifundisha!

  Halafu unaniuliza, “Kwani wewe ndiye unayejua sana kati ya wachangiaji wote hapa kiasi kwamba unachokisema wewe tu ndo kiko sahihi?” maswali kama haya ni dalili ya kupoteza mwelekeo! Kabla hujaniuliza jambo hilo, ulipaswa unioneshe mtu wa tatu, yaani ukiacha wewe na Ziragora, ambaye hujitokeza hapa kuchangia vitu wasivyovielewa, otherwise wengine wote huja katika spirit ya kuchangia wanachokijua, na kama kina makosa hujifunza kulingana na KWELI inavyojifunua, na si kulazimishana kushare UJINGA!

  Jambo la kwamba nakuwa nimekosa Hoja ninapoirejea misimamo yenu katika mijadala iliyopita, na sasa nikiioanisha ktk mjadala mpya, unaweza kuliona hivyo kwa sababu utakuwa HAUJUI hata MAANA na FAIDA za kujadiliana! Tunapojadiliana huwa ni FURSA ya kujifunza. Kuna mambo mengi sana niliyojifunza nilipokuwa darasa la kwanza ambayo ninayatumia mpaka leo, hata huku kuandika na kusoma!!! Kwahiyo kama ulifundisha kwamba “KIINGILIO kwenye Semina ni SAWA na CHANGIZO alizoziamuru mtume Paulo”, kama hilo uliliona kuwa ni JEMA, sasa unalia nini? Mimi nilitegemea ulifurahie sana hilo linaporejewa!!

  Halafu, ULALAMISHI, au roho ya KUNUNG’UNIKA NUNG’UNIKA, huufunga uelewa! Mimi nimechukua mlilolitamatisha kuhusu “KIINGILIO kwamba ni sawa na CHANGIZO” kwamba hili ni POTOFU, na umbali tuliojadili ndio ulionihakikishia kwamba ninyi mme cross ile line of understanding, kwahiyo kila ninapowaona ninawaona ni watu mnaotoza watu viingilio kwenye semina zenu kama mlivyo confess wenyewe, si kwamba mimi nawazulia jambo, au nina chuki nanyi, si kweli I am simply lauding your confession!!

  Hiyo mipaka ya mawazo katika mijadala unayojaribu kuiweka, shows that you are an amateur! Sina haja ya kukunukulia, chochote, bali wewe mwenyewe rudi katika mijadala halafu uone interlacing ya issues inavyokwenda! Vitabu 66 vya Biblia vinalifanya Neno, kama utaelewa!

  Kuhusu kujazwa RM, inategemea uelewa wako kuhusu jambo hilo kuwa ni nini! Unapomzungumzia Kornelio, ukijifananisha naye, utakuwa ni wale watu wenye “kujisikia” kwa tabia, kwahiyo ni wagumu wa kujifunza au kusikiliza jambo na kulielewa lilivyo. Wewe una jambo gani ulilowahi kulifanya hata Mungu akalazimika kukuHesabia Haki? Acha mizaha ya dini kaka!!! Kasome vizuri kuhusu Kornelio halafu uje utuambie unachofanana naye wewe ni nini?!!!

  Nawe unaniambia kuwa, “”Mimi nilijazwa Roho mt. siku chache tu baada ya kuokoka, na wala sikuwa nimejua sana neno la Mungu.” Malizia basi ulizirudia “Asante Yesu” mara ngapi? Pia ni vizuri ukaelewa kwamba mimi si mkaguzi wa watu waliojazwa RM, kwa taarifa yako Siyi, Lenda, Vai, Bezaleli, Seleli, nao wote wamejazwa RM, halafu wanaamini kwamba Samweli aliyepandishiwa Sauli na yule mwanamke mchawi wa Endori alikuwa ni MZIMU!!!!

  Ila ukitaka kujua kama uliyenaye ni RM au roho wa dini, mpeleke kwenye Neno, utajua tu, hicho ndicho kipimo pekee kilicho halisi cha kuzipimia roho!!!!

  Mwisho, unaniambia, “Lwembe nithibitishie kwamba dhambi ya uzinzi haisamehewi!” Unanitaka nikuthibitishie jambo ambalo halipo, nitalithibitisha vipi? Labda wewe ungenithibitishia WAZINZI wanaposamehewa, mbona dunia nzima itakushangilia kwa Injili hiyo, utakuwa tajiri kuliko atakayevumbua dawa ya UKIMWI!!!

  Nimejaribu kupunguza “makorokoro” kama unavyonishauri!

  Asante sana kwa ushirikiano mzuri!!!

 57. Sungura,

  Siyashangai sana maelezo yako, kwani nayo yanawakilisha aina ya uandishi ya mwenye kuukimbia wajibu ktk anayoyaandika, yaani mtu asiye na conviction katika anayoyasema, “a mobile personality”; leo kasema hiki, kesho kile, na keshokutwa ukimuuliza alichosema juzi, anang’aka, oh, hilo si la siku nyingi!!

  Sikiliza, jizoeze kutokuropoka mambo usiyo na uhakika nayo, hata ikiwa ni Injili! Elewa kwamba kila unaloliandika linaacha impression katika mioyo ya watu, usijiandikie tu kama magazeti ya Udaku! Unajua, unashangaza sana; utaniambiaje mimi kuwa maneno ninayoyaandika nitayatolea Hesabu, halafu wewe unakimbia kuyatolea Hesabu maneno uliyoyaandika; tunapoyarejea unalalamika; kama ulikosea, si rekebisha basi kuliko kuficha kichwa kichakani ukimuachia fisi kiwiliwili chote!!!??

  Kumbuka hapa tunazungumzia kuhusu KUFA na KUPONA, so I’m dead sincere abt what I say, hata ukiniuliza baada ya miaka kumi, kwa furaha nitakujibu kama inavyopaswa na si michezo ya kuigiza. Na pia hatufungwi katika wakati kuyarejea uliyoyaandika as long as record yake imebakia humu, na pia elewa kwamba unakuwa identified na ulichokiandika, hiyo ndiyo standard!!!!

  Kama umelielewa hili ni vizuri na kama hujalielewa, basi kadiri tunanavyoyarejea uliyoyasimamia UTAJIFUNZA!!!

  Ni kushukuru kwa hilo, na kwa sababu kuna mambo mengi uliyoyagusia ktk uliyoyaandika, basi juu ya msingi huu nitajaribu kuyajibu.

  …. …. ….

 58. Lwembe,

  Unayo shida moja,na hukufanya uonekane mtu asiyekuwa na lengo zuri na michango yake katika kujifunza kwetu hapa.

  Na ndio maana mimi hukwambia mara kwa mara kuwa kuna aina fulani ya mizaha ya kijuha huwa hata siwezi kuchukuliana nayo. Maana kuchanganya hiyo mizaha na kweli ya Mungu na kujaribu kumsaidia mtu unayedhani kuwa ana shida, hata hakuwezi kumsaidia zaidi sana atakuona ni mtu tu mwenye kusemasema maneno ya vivi hivi. Na ndicho unachokifanya hapa Lwembe.

  Kuna sehemu umeandika Roho mtakatifu kwa herufi ndogo kujaribu kuonyesha kuwa huyo ambao waliompokea waliamini ni Roho mt. kumbe ni roho nyingine, huo ni mzaha Lwembe, na nilishawahi kukwambia tena kuwa acha kufanyia mzaha mambo hayo kwa kudhani tu kwamba wewe unachokielewa ndo kiko sahihi. Believe me, kuna siku utagundua kuwa hakiko sahihi, itakugharimu sana katika nafsi yako.

  Kwani kuna shida gani ikitokea mtu amejazwa Roho mtakatifu kwa kusema asante Yesu- asante Yesu? Kwani kuna kanuni maalumu ya kujazwa Roho mt?
  Siku utakapojua kuwa aliyejazwa kwa kusema hivyo alijazwa na Roho wa kweli, ambaye wewe umemhusisha na namba 666 utaiambia nini nafsi yako?

  Kwa nini tu usiongee kitu unachotaka kuongea bila kuweka vitu vya kipuuzi pamoja nacho? Hiyo kitu inakufanya uonekane mtu asiyemaanisha katika michango yako mingi Lwembe.

  Kwani wewe ndiye unayejua sana kati ya wachangiaji wote hapa kiasi kwamba unachokisema wewe tu ndo kiko sahihi?

  Nafikiri kwa sababu ya kukosa kwako hoja za maana katika mada husika, umeanza mtindo wa kuchukua mawazo ya mtu kutoka kwenye mada nyingine na kuyaleta kwenye mada isiyohusika. Msomi ambaye hakuisoma mada ambayo umahamisha umechukua comments zake, hata hawezi kukuelewa unaongea nini katika mada ambayo umeihamishia hiyo comment.

  Ni mfumo wa uandishi usio wa kiungwana hata kidogo. Ni kama unabeba uchungu wa kubishiwa na mtu kwenye mada moja na kutaka kumlipiza kisasi kwenye mada nyingine. Huo ni uandishi mnyonge sana hata haukusaidii chochote rafiki.

  Masuala ya viingilio kwenye semina si yana mada yake inayojitegemea, kwa nini kama hukuridhika na majibu yetu usiendeleze mjadala wake huko kwenye uwanja wake, kwa nini unayahamishia huku? Vipi wote tukiwa na akili kama ya kwako tukamua kuyajibia hapa, si tutakuwa tumetoka nje ya mada? Huo ni uandishi uchwara Lwembe.

  Lakini mbaya zaidi mara nyingi tu pia unakosa umakini katika mawazo yako na kujikuta umeandika uongo.
  Ulichokiita hatua ya tatu ambayo umesema mtu anakuwa PEFERCTED, ni uongo siyo kweli. Nakunukuu;
  ” Bali Ukilishwa Chakula Safi lile Neno kamili, likakaa kwa wingi ndani yako, ndipo Mungu hukuingiza katika Hatua ya Tatu,yaani unakuwa PERFECTED, anakujaza Roho wake, wewe na Neno mnakuwa kitu kimoja! Hapa ndipo unakuwa UMEZALIWA mara ya pili kwa Roho wa Mungu”

  Kornelio na wenzake walihubiriwa tu siku hiyo walipoamini wakajazwa na Roho mt.pia. Na wewe hapa unatuambia Roho mt unajazwa katika hiyo hatua ya tatu. Kwa hiyo hawa jamaa tayari ndani ya siku moja neno la Mungu lilikaa kwa wingi ndani yao?
  Huwezi kuniambia kuwa mtu aliyempokea kristo siku hiyohiyo neno la Mungu linajaa ndani yake ili aweze kujazwa Roho mt; kama kweli kujazwa Roho mt. ni mpaka mtu ajae neno la Mungu. Huu ni uongo Lwembe.

  Mimi nilijazwa Roho mt. siku chache tu baada ya kuokoka, na wala sikuwa nimejua sana neno la Mungu.

  Na kitu kingine ulikisema lakini sikutaka kukikomalia, lakini nao;

  Lwembe nithibitishie kwamba dhambi ya uzinzi haisamehewi!

  Ndg. punguza makorokoro kwenye michango yako!

 59. Lwembe,

  Kam unaemwita Bwana Jela ni yule Ziragora aliegundua kam wewe ni muongo professional basi umehakikisha umeridhika kuwa ndani ya jela iliyowekewa waongo. Ukitazama jinsi umejitumbukiza mwenyewe ndani ya Jela, huone kama unaandika bila kufahamu unachoandika? Wewe ambae unapinga kwa upofu neno lililo hai ninalokutolea kila leo, iweje tu uwe umetumbukia ndani yangu? Unamaanisha umeguswa na Neno? Uwe muungwana, utuambie basi yaliyo kweli. Kama Injili imekuingia kabla Ndugu Seleli hajafika kukuhubiri, si usemeshe kweli? Unafikiri kuna atakaekucheka? Pengine utatoka ndani ya jela la waongo, RM akutie ndani ya jela ya wenye haki. Alie na sikio anasikia neno wakombolewa wa Yesu wanaambiwa(Waefeso 3:1).

  Hushangaze mtu yeyote kwani umejulikana. Utaendelea nasiku hadi uikimbie SG, au utaendelea jikwaa kwa lile Jiwe la Pembe hadi umalizike.

  Una haki ya kuendelea lalamika kwani wewe ni kipofu, wala huone dawa ya uongo, ndipo unakimbilia kwenye majina usioyafahamu.

  Umeambiwa wewe kama muongo hudaiwe jambo lingine lolote la kujadili ukiwa ndani, ndio maana unaona siweke tena hadharani uongo wako mwengine ambao tayari nimerikodi. Lakini usihofu, Yesu alie ndani yangu aliniambukizia huruma, tubu uwe huru kaka. Usidhani mimi niko chini ya sheria kama wewe. Hiyo torati unaisoma vibaya na huna nguvu ya kuiconnect na Injili kwani unampinga Yesu. Na kwa sababu Yesu ni juu ya sheria ndio maana unanasika kirahisi, unabaki ukishangaa tu. Kwa nini huna ufahamu wa kujiswali mwenyewe kinachokusukuma kuwa slave ya uongo?
  Njooni ufunzwe hekima, usiangamie ndugu yangu!!! Na kam bado kusikia wakati itakapohitajika nita copy-paste niliyokuandikia, pengine kwa kuyarudilia utapenywa.

  Namuacha Ndugu Sungura akujibu kwa hila zako, kwani hoja zimekuishia kabisaaa!!!

  Bwana Yesu Kristo akusaidie.

 60. Sungura,

  Kumbe kuna kiporo nilikichokisahau!

  Kuhusu Mpagani aliyeipokea Injili na kuingizwa kundini, sasa akiwa ni Mkristo huyo aliyeHesabiwa Haki, unasema:
  “”Nafikiri huyo mkristo anakuwa amezaliwa mara ya pili ndio maana anaendelea kuukulia wokovu.
Mkristo ni mfuasi wa Kristo, kwa hiyo ili mtu awe mfuasi wa kristo lazima awe amezaliwa. Mimba haiwezi kuwa mfuasi wa kristo. “”

  Habari ya “mimba kuwa mfuasi wa Kristo”, utakuwa umejichanganya katika uelewa, kwani Biblia au yeyote yule anapozungumzia KUZALIWA, halafu akawa HAJUI kwamba inaanzaga mimba kwanza, basi hiyo ni ishara mbaya, huyo atakuwa anaongelea jambo asilolijua; HAKUNA kinachozaliwa bila kutungwa mimba kwanza! Basi Biblia inapozungumzia Kuzaliwa Mara ya Pili, elewe pia kuwa kutakuwa na Hatua ya Kutungwa Mimba, ndiko huko Kuhesabiwa Haki, na baada ya hapo mimba hiyo huingia katika Hatua ya Kutunzwa, mama mjamzito akipewa vyakula vyenye kuitunza afya yake na ya mtoto aliye tumboni, ndiko KUTAKASWA! Hizi Hatua zote mbili, ni Hatua za MATEGEMEO!

  Mama anapokuwa mjamzito, POTENTIALLY huwa tunahesabu kupata “mtoto”. Lakini mimba inaweza ikaharibika!!! Naye Mkristo aliyeHesabiwa Haki na Kutakaswa, bado anaweza KUPOTEA!! Yuda Iskariote alizifikia Hatua zote mbili, na alipotea. Akina Anania na Safira, walikuwa katika lile kundi la watu walioamini, lakini waliishia huko nje! Shetani alipowajia wakawa hawana namna ya kumkabili, walipouitikia wito wa Injili, walijibakizia nafasi ya mawazo yao katika mioyo yao, huenda ni kule kuyasikiliza na mashauri ya dini yao ya zamani huko ktk Ufarisayo, kwahiyo dhoruba ilipowafika, wakasombwa na tamaa zao, WAKAPOTEA!!!

  Basi, kimsingi tunaweza kusema kwamba wakristo wooote WAMEOKOKA kulingana na Maandiko kama tunayaamini; Mk 16:15-16
  “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa.”
  Hata kama ulibatizwa Ubatizo feki, bado Mungu anakuhesabia Haki kwa sababu hicho ndicho kiwango cha Nuru ulichoangaziwa na ukaamini. Hii ni Hatua ya Uvumilivu ya Mungu, yeye hutupokea kama watoto wadogo, akatuhesabia Haki pale tulipomwamini kwamba YEYE YUPO!

  Hatua ya pili, ile ya kukuzwa kwa mimba, kumbuka tunamzungumzia Sungura yule ‘roho’. Chakula cha “Sungura” huyu ni Neno la Mungu pekee, hilo ndilo lilojaa virutubisho viwezavyo kumkuza na kumpa afya kamili. Ndio maana nilisema kwamba Hatua hii ndiyo Hatua ya Hatari, kwani hapa ndipo wakristo wengi hulishwa chakula cha nguruwe na huishia kufa kiroho wakabakia kuwa watu wa dini!

  Hebu wazia kwamba umekabidhiwa kwa “Bwana Jela” Ziragora na mkufunzi mwenza Seleli, kisha wanakulisha kwamba “Nabii wa mwisho ni Yohana Mbatizaji, hakuna tena Nabii baada ya huyo”; au wanakufundisha kwamba “Ukizini unaweza kutubu na Mungu atakusamehe, yeye anahuruma sana, si unaona alimsamehe yule mwanamke mzinzi”; wanakuambia uwe UNATOZA KIINGILIO kwenye semina zako, hiyo ni sawa na CHANGIZO alizoamuru mtume Paulo!!! Ukiisha kuyashika vizuri mapando hayo uliyopandikizwa moyoni mwako, ndipo wanakuzawadia na “roho mtakatifu” wao, unafundishwa kurudia kwa upesi upesi, ““Asante Yesu, Asante Yesu, …” x 666”” ndipo unalipukia ktk kushandarize; basi unafia hapo katika Uongo wa dini mpaka utakapo fufuliwa kwa Hukumu!!!

  Bali Ukilishwa Chakula Safi lile Neno kamili, likakaa kwa wingi ndani yako, ndipo Mungu hukuingiza katika Hatua ya Tatu, yaani unakuwa PERFECTED, anakujaza Roho wake, wewe na Neno mnakuwa kitu kimoja! Hapa ndipo unakuwa UMEZALIWA mara ya pili kwa Roho wa Mungu! Unakuwa mwana mwenye Mamlaka, Unakuwa ni Neno lililofanyika Mwili kwa siku ya leo! Kama Biblia ilisema “Mzinzi na auawe” nawe unasema hivyo, sio kuanzisha siasa za dini! Kama Mungu alisema “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.”; hauanzi kujitangazia vitu usivyovijua, eti oh hakuna nabii tena!!!

  Basi kama haya yaliyo mepesi yamewashinda, na wala uwezo wa kujifunza hamnao, dhambi mtaijulia wapi? Ndio maana baada ya kugundua kuwa mnatembea kwa hisia ya fimbo, kumbe macho mlishapofiliwa zamani na dini zenu, nimewaacha muongozane mpaka “mbinguni”!!!!!

  Mbarikiwe!!!!

 61. Ndugu Seleli,

  Tunachofanya ni kuhurumia tu ndugu yetu Lwembe. Ndio maana tunaweka jiwe badala ya mawe mengi kusudi asijivunje mwenyewe mifupa ya kichwa na kutoweka pasipo kutubu. Hivi tungali tunacheka sana kwani tunaamini ataokoka. Kwanza angalia jinsi alivyoendesha maandishi yake hapo zamani. Haaah! jamani!!! huyu kijana ni muandishi kabisaaa!!! Akiendelea hivyo umaarufu wake utapita ule wa waliomweka Yesu msalabani.
  Tunachofanya ni kumbembeleza akamate break ili asiangamie haraka. Huyu Lwembe ana neema kubwa kwani sote twampenda, sivyo tungelimuachilia aangamie tu… Yesu usaidie Lwembe!!! Hivi ataanza sema nimetaja Jina la Mungu kwa bure. Ninamuita Yesu wangu, na ninamuomba sana kabla nijadili. Haleluya!!!

  Seleli, tusimbebe kyenyeji-enyeji kam anavyopenda yeye, hapo hataokoka. Angalia vuzuri jinsi ninamuongoza: kwa mwanzo ninakamata style yake, baadaye ninapunguza some sentences, kiisha ninaweka neno ambalo hawezivuka. Ndipo anaanzasema uongo na hapo ananasika kirahisi.
  Tunamleta poleeepole; unajua alimeza sumu nyingi bwana…., ni kutembea polepole asije akakosa wokovu.

  Huone kama amekwisha punguza uandishi wake? Inayobaki ni kutubu uongo na kudaka neno lililo hai. Tutamuongoza wala hatatuongoza, kwani iko always hojaless. Furaha yetu ni kuona Lwembe anakua mtu mzima.

  Seleli, katika andiko hili tu ninaloweka hapa chini, unafikiri hata yeye akijiswali atapata jibu? Bwana asifiwe!!!!
  Simba wa Yuda anasema mwenyewe:
  “Marko 7:21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
  22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
  23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.”

  Kila mara mtu atakapompinga Simba wa Yuda atakwaa tu.

  Jambo lingine, Yesu ni wa ajabu. Angalia anavyosema:”Marko 2:17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”
  Kwa kweli haikumpasa Lwembe kupoteza chance yake.Ndugu yangu, ukimuona mapema umpashe hii injili.

  Ubarikiwe.

 62. Ziragora,

  Umenichekesha sana na hii para yako chini.. hahahahaha ni tamu sana hii apa….”’Utaendelea kukwaa kwenye Jiwe la pembe, utaishia kupoteza mifupa yako yote!

  Yup, yup mpe sure Lwembe maana most of the time does confuse minor things. Ukitaka deal naye, nenda naye kienyeji-enyeji tu, He is not the guy to engage with on serious note maana hua haeleweki, mambo ya kawaida kabisa, so simple msg/statements ktk Bible, yeye hutaka zi sound so huge au sijui kuna ufunuo mkuuuubwaaa sijui au sijui anajua kweli sana yeye halafu kichekesho ni ukishasoma aliyoaandika, yaani unachoka…hana tofauti na Siyi, yaani naonaga sijui wanafafana au sijui nani zaidi ya mwenziwe ktk kuongea mambo ya kwenda Ilala Dar but kwa kucheeeka na kuona raha sana na kutangazia watu, anaanzia Kishasha ya Mobutu then Kgm ya Nyerere then Dar ndipo Ilala!!!!!!!!!!!!!!!!!! mshosho mwanzo mwisho!

  Aisee naku support Ziragora, weka hayo mawe mengine na makubwa-kuba-siyo kubwa ya pembe ili apoteze si tu mifupa but na boni marooooo!

  Twende kazi Zira, weka jiwe pembe Kaka, tummalize huyu msumbufu na mpotezaji muda humu kwa mambo yale ya kiroho na simple ya Bible.

  Press on

 63. Mpendwa Clement,

  Nataka nifahamu umeandikia mtumishi gani na ukijibu kwa hoja gani.

  Asante

 64. Mtumishi kwanza tuanze kujua maana ya dhambi.Dhambi ni uhasi yaani ni kwenda kinyume na maagizo uliyopewa na Mungu,Mungu ni mtakatifu ashirikiani na dhambi yoyote. soma waefeso 5:5,sasa basi kuua ni uhasi na kuzini ni uhasi fahamu hata kutokusamehe ni uhasi kwa maana hiyo dhambi yoyote ile inampeleka mtu kuzimu yaani motoni
  Ni hayo tu mtumishi kwa leo

 65. Lwembe,

  Una tatizo kubwa sana. Kila mara unashindwa jibu. Wengine wetu wanafikia hatua ya kujibu wenyewe kwa swali ulilopewa, nawe unakosa ufahamu wa kuwaambia “asante”!!!

  Unatakiwa uchunguze unayoandika, sivyo kila mara utajipeleka pabaya. Na kama huna la kusema nyamaza kimya, ukae ufundishwe, tunao walimu wengi hapa wanao upako, lengo ikiwa na wakina Lwembe waokoke.

  Utaendelea kukwaa kwenye Jiwe la pembe, utaishia kupoteza mifupa yako yote! Ukiona mtu alieokoka anakuswali, usiwaze ni mchezo wa kitoto. Uwe muungwana, uanze hesabu swali ngapi ulizoshindwa kujibu. Umeanza arifiwa mapema, usije onyesha tena umaarufu wako wa kujishangaa mwenyewe.

  Ndugu yangu, sitakubeba mbali katika matusi yako, ubishi juu ya taratibu ya Yesu, nk. Fahamu kam mim siwezi zama ndani ya hila zako. Hebu soma tena ulioandika ujihukumu mwenyewe.
  Mimi nitaweka tu lile Jiwe la pembe, neno lililo hai, hadi utakapojibu. Sikukuomba kuandika A na B kiisha ubandike unayotaka. Ukikosa jibu unyamaze pahali pa kuendelea kujiangamiza.

  A) Naona hapa si lazma tutoe shahiri ingine, nataka nirudishe upya niliyokutolea iwe zamu yako ya KUTOA NJE YA ORODHA DHAMBI YA UZINZI. Unionyeshe umeitia wapi na dhambi nyingine zimebaki wapi. Pia uniambie kama unajitambua kuwa na UPUNGUFU au la.

  “1 Wakorintho 6:7 Basi imekuwa UPUNGUFU kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?
  8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
  9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala WAABUDU SANAMU, wala WAZINZI, wala WAFIRAJI, wala WALAWITI,
  10 wala WEVI, wala WATAMANIO, wala WALEVI, wala WATUKANAJI, wala WANYANG’ANYI.
  11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  B) Kwa nini unakwepa ? Hii andiko ya YOHANA 8, unaisema juujuu kirahisi tu, wala hupendi itika kama kulikuwa huruma. Wewe unakimbilia kwenye hukumu. Nilikuuliza wakati Yesu alimwambia mwanamke aende na asitende dhambi tena, hapo hakumhurumia ? Kwani Yesu angehesabu huyu mwanamke kuwa maiti kwa nini aambie maiti isitende dhambi tena ?

  C) Unaposema hatujue dhambi ni nini, nadhani unadaka picha yako kwa kuibandika wengine. Uwe mwanaume na useme yaliyo kweli. Mtu akikuambia « kila ukeukaji wa maagizo/sheria ya Mungu ni dhambi », wewe unasema hajue, sasa kosoa ile sentence, tutakuelewa.

  Asante

 66. Lwembe,

  Nafikiri huyo mkristo anakuwa amezaliwa mara ya pili ndio maana anaendelea kuukulia wokovu.
  Mkristo ni mfuasi wa Kristo, kwa hiyo ili mtu awe mfuasi wa kristo lazima awe amezaliwa. Mimba haiwezi kuwa mfuasi wa kristo.

  Halafu ile dhana ya kuchaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu,nilikwambia kule mwanzoni kuwa si shule rahisi kama unavyoirahisiha.

  Ni vizuri na muhimu kutafuta kujua kwanza hiyo lugha ya biblia ”kuchaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” ina maudhui gani hasa, kabla ya kufikia hitimisho kwamba kuna watu ambao wamepangiwa kuokoka na wengine hawajapangiwa kuokoka.

  Kumbuka maneno haya kuwa ”enyi uzao wa nyoka, ni nani ”amewatonya” kuikimbia hukumu…..” (a paraphrase)

  Thank u sir!!

 67. Ndg Ziragora,

  Unajua kuna mambo ambayo yako wazi sana, kwamba unayakosa inashangaza!

  Hivi haujui kwmba kuna Wapagani wengi sana ktk Ukristo? Kwa taarifa yako wako wengi sana, tena wanasoma Biblia, wanaimba kwaya na wengine wanahubiri nk; bali hawajui chochote kuhusu Mungu!

  Mtu wa kwanza duniani kuhubiriwa kuhusu Dhambi ni Kaini, na HAKUELEWA! Hata nawe pia unashangaza, hivi Biblia inapokuambia kuwa kuna Dhambi ya Mauti na ISIYO ya Mauti, unadhani inadanganya? Kama Biblia inazitofautisha Dhambi, wewe kwanini uzifanye kuwa zote ziko sawa? Na mamlaka ya kuzichanganya Dhambi unaitoa wapi? Ondoka katika maisha ya Gizani, ichukue Nuru ya Maandiko ikuongoze!!!

  Maswali uliyoniuliza, mengi hayana majibu kwa sababu ni maswali ya mtu anayejiongelesha ili aendelee kuuamini uongo aliouzoelea kwa kuiogopa Kweli! Lakini ngoja nikujibu

  A: Dhambi ya Uzinzi katika Torati inabeba Hukumu ya Kifo, Law 20:10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.” Hiki ndicho Biblia inachofundisha. Mkristo anapaswa kufundishwa jambo hili hapo anapoukulia wokovu mpaka alielewe sawasawa. Juu ya uelewa huu sasa anasogezwa mbele Mt 5:27-28 “27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Unaona! Unapaswa uwe uliisikia Torati kwanza ndipo utaweza kuyajua yanayofuata vinginevyo utaishia kama hivi unavyojidanganya na hilo kundi linalokufuata:
  “”Mengineo, kwa tendo au kwa mafikiri, anaezini na aneeiba wote inategemea mahala wapo. Wakiwa katika kundi ya wanao haki ya masamaha watasamehewa wakati wanapotubu…””

  Haya ndiyo “Mafundisho ya Uongo” mnayoyaeneza kwa wajinga; ni wapi Biblia ilisema mktisto anaweza kuutubia UZINZI? Wapagani wazinzi wanaweza kusamehewa uzinzi wao hapo wanapoujia Ukristo, ndio maana kuna kutubu kwanza kabla hujabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili uondolewe Dhambi zako hizo zinazojumuisha na huo Uzinzi uliokuwa ni jambo la kawaida tu huko kwenye upagani wako; ukiisha kuondolewa hilo pepo la uzinzi, halafu mbele huko ukalirudia, unayastahili mawe, kama si leo basi yasubiri yaja, “Brimstone and Fire”, maana Kanisa linaagizwa kukutoa nje kwa ajili hiyo, 1Kor 5:13 “Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.”!!!

  B: Kuhusu yule mwanamke mzinzi, naona bado huelewi dhana nzima ya jambo hilo! Hukumu inaposhindikana haimainishi kuwa huo ni Msamaha! Unapojaribu kulifanya jambo hilo kuwa lilikuwa ni MSAMAHA kwa wazinzi, ni upotoshsji mkubwa wa Maandiko, na wote watakao kusikiliza, utakuwa umewaingiza ktk Dhambi ya Mauti!!!

  Katika siku hizo za yule mwanamke mzinzi, licha ya kwamba Kristo alikuwepo, bado wote walikuwa chini ya Torati. Nikakuambia kuwa Kristo ndiye Torati, naona hukunielewa! Yeye ndiye aliyempa Musa hiyo Torati na Programu yake yote anayo yeye, je, wategemea aivunje? Nikakuambia kuwa Kristo aliipitisha HUKUMU kulingana na Torati, bali kulikuwa HAKUNA anaeyestahili kuitimiza HUKUMU hiyo, maana mwenye kuzijua siri za mioyo ndiye huyo hapo utajificha wapi! Rum 2:3 “Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?”

  Hiyo unayosema alimhurumia, ni wapi imeandikwa kuwa Kristo alimhurumia yule mwanamke? Usipende kuchomeka mambo yanayotengeneza kifo! Alimruhusu aende zake baada ya washitaki kukimbia na akamtahadharisha kutokurudia tena uzinzi wake, au wewe unafikiri yule mwanamke akirudia uzinzi na kisha akakamatwa tena, unadhani wangempeleka tena kwa Kristo? Wangemalizana naye huko huko tu!!

  Pia ni vizuri ukafahamu kwamba mambo ya Mungu huenda kwa Utaratibu na si Hisia. Ujio wa Kristo ulikuwa katika Programu kamili ya Mungu. Kristo hakujijia tu aje atafute cha kufanya akiisha fika duniani; Programu yake ilikwisha kuwekwa ktk Maandiko, Mungu alimpa nabii Isaya aiandike (61:1-2)! Tazama hapa Kristo anapoirejea akiwatangazia kanisa, Lk 4:16-21 “…Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, “””Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.””” Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU.” (msisitizo ni wangu)

  Umeyaona yaliyotimia? Asingeweza kufanya tofauti na Programu hiyo, kama ambavyo hisia zako zinavyokutuma! Yule mwanamke kama huko mbele alimpokea Kristo, na akazaliwa mara ya pili, atakuwemo katika unyakuo, na kama hakuwahi kumpokea Kristo, lakini aliwahi kutoa sadaka ya dhambi au hakuwahi, atakuwepo ktk ufufuo wa pili na atasimama ktk Hukumu pamoja na wanaofundisha uongo; huko mbele katika ile Siku ambayo alipokisoma chuo cha Isaya, hakuumalizia ule mstari wa 2, akaishia katikati maana siku ya kisasi ilikuwa bado, hiyo ambayo wewe Ziragora kwa kulazimisha mambo unadhani angeweza kumpiga mawe yule mwanamke na kuivuruga Programu nzima! Hii hapa nusu ya kifungu alichokiacha kukisoma kutokana siku ya unabii huo kuwa bado, “…na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao”!!!

  Tena kwa taarifa yako, ktk siku zetu hizi ndio Dhambi ya Kumkufuru RM inatendwa saaana, yaani unapofundisha tofauti na walichofundisha mitume, ni kufuru ya moja kwa moja!!!

  Jihadhari sana na unayoyafundisha!!!!

  Asante kaka!

 68. Sungura, Seleli,
  Maelezo niliyoyatoa, katika ujumla wake yanahusika na hatua ya kwanza anayoipitia Mpagani anayeujia Ukristo. Hii ndio ile Hatua inayoitwa Kuhesabiwa Haki kwa Imani. Nikasema Mpagani huyu alipoisikia Injili, ikamkamata, akaipokea na ikamuumbia Imani ndani ya nafsi yake, nayo imani ni kipawa anachokupa Mungu.

  Pia ni vizuri tukafahamu kwamba Kristo anasema mtu hawezi kwenda kwake asipovutwa na Babaye, tena tumeshuhudia akimwambia Babaye kwamba “wote ulionipa…”, basi, Injili huwatafuta watu specific, hao walio chaguliwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa na si kila mtu!!! Bali ili Mungu abaki kuwa ni Mwenye Haki, ndipo huwapelekea Injili hata ambao hawataipokea kwa ajili ya ushuhuda wa ile Hukumu, kama alivyohubiriwa Kaini na uzao wake mnao uona ukikemewa kwa kuyapotosha Maagizo ya Mungu!

  Kama utakumbuka nilisema Hatua hii ndio kule kutungwa kwa mimba ya Kiroho katika nafsi zetu, ndipo ktk hatua hii tunakuwa TUMEOKOKA kama Maandiko yanavyosema (Mk 16:16). Bali mimba si mtoto ingawa potentially ni mtoto, ndipo ni mpaka atakapozaliwa hai, hilo hulikamilisha jambo hilo; maana twafahamu pia kuwa huyo mtoto anaweza kuwa “si riziki”!

  Kwahiyo mkristo aliye katika Hatua hii anakuwa BADO HAJAZALIWA mara ya pili bali anakuendea KUUKULIA Wokovu!

 69. Mabinza,
  Nashukuru kwa majibu yako kuhusu mkristo aliyezaliwa/asiyezaliwa mara ya pili. Niliamua kumuuliza Lwembe hilo swali badala ya kumpinga kwa jibu langu moja kwa moja, ambalo ndilo hilo kabisa ulilolisema kuwa, hakuna mtu ambaye hajazaliwa mara ya pili ambaye ni mkristo.

  Kwa majibu hayo ni wazi kuwa alichokisema Lwembe kwamba kuna mkristo aliyezaliwa mara ya pili na asiyezaliwa mara ya pili tunamkatalia kuwa si kweli.

  Kama mtu anajiita mkristo halafu hajazaliwa mara ya pili huyo si mkristo ila anajiita tu.

  Kwa hiyo hilo swali nililiuliza makusudi ili nijue alichonacho Lwembe kuhusiana na hilo, lakini tayari nilikuwa na pingamizi langu moyoni kwa hiyo kauli yake. Nakupongeza na wewe kuwa unaujua huo ukweli sawasawa.

  Maelezo yako mengine kama haya kuwa akina Sungura hawawezi kujua tofauti ya aliyezaliwa mara ya pili na asiyezaliwa ni mawazo yako tu mfu ya kufikirika. Mabinza tangu tukutane hapa SG bila aibu kabisa umeona kuwa ni sawa kudhani kuwa Sungura hajui maana ya kuzaliwa mara ya pili? Get serious sir!!!

  Na wala usijaribu kumpetipeti Lwembe kana kwamba unaungana naye katika kile alichosema wakati wewe umesema kinyume kabisa na yeye.

  Yeye kasema kuna mristo asiyezaliwa mara ya pili, na wewe umesema hakuna mkristo ambaye hajazaliwa mara ya pili. Halafu ati unajaribu kumwambia ”CK Lwembe usishangae ama kusikitika kuwa unafanyiwa dhihaka! Wenzio hawajaona, watashuhudiaje?” Acha kumzuga Lwembe kwa mgongo wa chupa!!!

  Halafu suala la uwezekano wa mtu aliyezaliwa mara ya pili kutenda dhambi,si mara ya kwanza wewe na mimi kubishana hapa SG. Nilishawahi kukuuliza swali hujawahi kunijibu mpaka leo, kwamba wewe tangu ulipozaliwa mara ya pili hujawahi kukosea kitu chochote ukatubu!

  Hebu sema hapa Mabinza wewe tangu uzaliwe mara ya pili hujawahi kukosea kitu chochote tena?

  Hii kauli yako ” WALIOZALIWA KATIKA MWILI MATENDO YAO NI YA KIMWILI NA WALIOZALIWA KATIKA ROHO MATENDO YAO NIYA KIROHO” unaweza ukadhani umesema kitu sahihi, lakini si kweli.

  Wewe hapo ulipo huna matendo ya kimwili kwani, au wewe hapo ulipo hujui kuwa uko katika namna zote mbili, yaani kiroho na kimwili?
  Ilichosema biblia ni ‘kilichozaliwa na mwili ni mwili na kilichozaliwa na roho ni roho’.

  Si kila tendo la kimwili ni dhambi na si kila tendo la kiroho si dhambi. Unatakiwa kujua lugha ya biblia,kuwa inamaanisha nini inapoziita dhambi kuwa ni matendo ya mwili.
  Lakini ukikariri tu kwamba kila tendo la mwili ni dhambi, basi utasema hata kujamiana na mke wako ni dhambi, maana ni tendo la mwili pia!

  Asante!

 70. Ndugu Mabinza,

  Nimekusoma vema. Nimeona nikwambie kam you’ve been right hapo mwanzo.
  Umejibu swali hili “Mkristo aliezaliwa mara ya pili ni yupi, na asiyezaliwa mara ya pili ni yupi?”
  Kam nimekupata vizuri umesema kam “kila mukristo amezaliwa mara ya pili” Hii ina maana kam walioleta swali hili “hawakuhangaika” kwani walikuwa wameshangaa kusikia kam kuna mukristo aliezaliwa mara ya pili na yule asiezaliwa mara ya pili. Hivi kama wote tumekubaliana tatizo halipo tena.

  Kisichonipenya ni kwani ulisema hiyo mapema, kiisha ukaendelea mafasirio yako weee…ukipoteza utamu wa jibu lako.
  Ulitamatisha ukionyesha utofauti wa mtu aliezaliwa mara ya pili (mukristo), na yule asiezaliwa mara ya pili(asieamini). Hence unaendelea andika kama mwenye kujibu kwa swali lingine. Unatakiwa kusema neno, unaleta mwangaza bila kuchomeka giza ndani.
  Jambo kama hili ndilo linanenepesha mjadala na kuleta watu kupoteza lengo.

  Anyway, asante kwa mchango wako.

  Mungu akubariki.

 71. Ndugu Lwembe,

  Huna mamlaka ya kunifundisha jinsi nisome Biblia. Kwani wakati utakapotembea kichwa chini utapenda nami nifanye vile ndipo ufurahi. Sasa hiyo matakwa yako uitumie nafasi nyingine.
  Mshahara wa dhambi ni mauti haiambiwe maiti (wasioamini) inaambiwa wanao uwezo wa kusikia. Hata ktk agano la kale utaona amri hazikupewa wapagani(makabila mengine), zilipewa wana wa Israeli, kabila teule la Mungu. Ukitaka danganya uangalie kwanza unataka danganya nani bwana!!! Mungu hawape amri wasiyo wake.
  Nakungoja ujibu kwa swali zangu ndipo unikaribishe tena, sivyo itakuwa tu mzaa. Kuna zinazokurudilia mara 3 na mara 2. Nina copy-paste tu:

  A) Naona hapa si lazma tutoe shahiri ingine, nataka nirudishe upya niliyokutolea iwe zamu yako ya KUTOA NJE YA ORODHA DHAMBI YA UZINZI. Unionyeshe umeitia wapi na dhambi nyingine zimebaki wapi. Pia uniambie kama unajitambua kuwa na UPUNGUFU au la.

  “1 Wakorintho 6:7 Basi imekuwa UPUNGUFU kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?
  8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
  9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala WAABUDU SANAMU, wala WAZINZI, wala WAFIRAJI, wala WALAWITI,
  10 wala WEVI, wala WATAMANIO, wala WALEVI, wala WATUKANAJI, wala WANYANG’ANYI.
  11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  B) Kwa nini unakwepa ? Hii andiko ya YOHANA 8, unaisema juujuu kirahisi tu, wala hupendi itika kama kulikuwa huruma. Wewe unakimbilia kwenye hukumu. Nilikuuliza wakati Yesu alimwambia mwanamke aende na asitende dhambi tena, hapo hakumhurumia ? Kwani Yesu angehesabu huyu mwanamke kuwa maiti kwa nini aambie maiti isitende dhambi tena ?

  C) Unaposema hatujue dhambi ni nini, nadhani unadaka picha yako kwa kuibandika wengine. Uwe mwanaume na useme yaliyo kweli. Mtu akikuambia « kila ukeukaji wa maagizo/sheria ya Mungu ni dhambi », wewe unasema hajue, sasa kosoa ile sentence, tutakuelewa.

  Ahsante.

 72. Wapendwa Sungura , Seleli na wote wengine!

  Nimelazimika kujibu swali ambalo kimsingi halikulengwa kwangu, pamoja na sababu zingine, hasa ni kwa ‘uchokozi alionichokoza Seleli. Sasa ni kwamba, Kuzaliwa mara ya pili kunakonenwa na Biblia, ni tendo halisi kabisa. Na nikweli pia aliyezaliwa mara ya pili hatendi dhambi! Najua mtashangaa kama kawaida, lakini hebu tuwe pamoja kwa mda huu kwanza, ikiwa kuzaliwa kupo na kutozaliwa pia kupo, kuzaliwa mara ya pili kinyume chake ni kutokuzaliwamara ya pili!

  Kwa mjibu wa ulizo la Sungura kwa Lwembe la 21/11/2013 at 11:30 AM akimuuliza Lwembe CK kusema, “Lwembe, Mkristo aliyezaliwa mara ya pili ni yupi na asiyezaliwa mara ya pili ni yupi?”
  Na kurudiwa tena 23/11/2013 at 11:29 AM kwamba “…mimi bado sijaelewa tofauti ya mkristo aliyezaliwa mara ya pili na mkristo asiyezaliwa mara ya pili….”nikijumlisha na mahangaiko aliyonayo Seleli, yakutaka sana kutenda na kutubu dhambi huku akisema kaokoka, kama alivyosema mwenyewe 22/11/2013 at 12:52 AM kwamba,
  “Lwembe,
  nangojea na mimi mlangoni kwa usongo ujibu swali la Sungura kuhusu Mkristo aliyezaliwa mara ya pili na asiyezaliwa maana umeongea mambo yenu yaleyale na Siyi na Mabinza yaani mambo makubwa-makubwa kumbe bwana mmmh! Kazi!!!…..Umesema, aliyezaliwa mara ya pili HATENDI DHAMBI…..”

  Kwanza niseme hivi Mkristo ni mfuasi wa kweli wa Kristo, na ili ujiite mkristo hakikisha kwanza umezaliwa mara ya pili, huwezi kuwa MKRISTO KAMA HUJAZALIWA MARA YA PILI, NA TENA UKISHA KUZALIWA MARA YA PILI HUTENDI TENA DHAMBI! Kuzaliwa mara ya pili ni moja ya mchakato mhimu wa kumkamirisha mwamini kuufikia wongofu; Sungura, HAYUPO MKRISTO WA KWELI AMBAYE HAJAZALIWA MARA YA PILI! Yesu anasema katika Yohana Sura ya 3 kuwa, “Hunabudi (NI LAZIMA AU INAKUPASA) kuzaliwa mara ya pili.” Kwa sababu mkristo ni mwamini aliyendani ya ufalme wa Mungu na kwamba anamtumikia Kristo, Bwana Yesu, Yohana na Paulo ndiyo waliyosema hivyo, siyo mimi. Yesu akizungumza na Mwalimu Nikodemo katika Yh. 3:3, Nikodemo alianza hivi, “Rabi, tunajua kuwa Wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo Wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.’’
  Lakini Yesu akamjibu Nikodemu kwamba, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.’’ Naye Yohana kwa wakati mwinginekatika1Yh.3:9 anasema hivi, 9Ye yote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. Lakini Paulo mtume wa Yesu kristo, katika kuelezea maana ya Ufalme wa Mungu na maana ya mtu mkristo ni yupi, katika Rum.14:17 Paulo alinasema hivi, “17Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18Kwa sababu mtu ye yote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.” Kwa ushahidi huu, hakuna mtu akawa Mkristo kama hajazaliwa mara ya pili, na vilevile hawezi mtu kuzaliwa mara ya pili kisha akawa mtenda dhambi na mwenye kutubishwa kila siku na wachungaji!

  Kama nilivyotangulia kusema ikiwa kupo kuzaliwa na kutozaliwa kupo pia, lakini kuna maana mbili kuu za mtu kuzaliwa kwa mjibu wa Biblia, kuna kuzaliwa “KI MWILI” na kuna kuzaliwa “NA MUNGU” mtu akizaliwa na Mungu HAWEZI tena kutenda Dhambi 1Yh.3:9 inasema, 9Ye yote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. (nadhani ni hiki hasa alichokuwa anakisema Lwembe CK, hakuna tena damu ya kuchezeachezea kuwa mwokovu mmoja leo katenda dhambi na sasa yupo hapa mbele kutubu dhambi ‘mpya’ wakati tayari mtu huyo alishakwisha okolewa!)

  Kuzaliwa na Mungu ndiko hasa kuzaliwa kwa Maji na Roho, na huko ndiko Kuzaliwa kwa Mara ya pili! Ukimsikiliza kwa uzuri Yesu wakati akimfundisha Mwalimu Nikodemo, utagundua kuwa Sungura na wengine wanaweza kweli wasijue tofauti ya Mtu aliyezaliwa mara ya pili na Yule asiyezaliwa kwa mara ya pili, kwasababu, MTU HAWEZI KUSHUHUDIA JAMBO ASILOWAHI KULIONA! Seleli, kama mtu kapigwa chenga na jambo dogo la duniani, vipi jambo la mbinguni? Kwa hiyo, CK Lwembe usishangae ama kusikitika kuwa unafanyiwa dhihaka! Wenzio hawajaona, watashuhudiaje? Hebu msikilize Nikodemo hapa, “4Nikodemo akauliza, “Awezeje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee?” ‘‘Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” Unaona? Nikodemo yeye ana hakika kuwa Mtu hawezi kurudi tumboni mwa mamaye na kuzaliwa tena! Lakini Yesu huku akijua kuwa YOTE YAWEZEKANA KWA KILA AAMINIYE aliendelea kumjibu swali lile kuwa,
  5….. ‘‘Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. 6Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. 7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna bud”

  Kwa hiyo tofauti ya mtu aliyezaliwa mara ya pili na yule ambaye hakuzaliwa mara ya pili, ni kuwa, “MWILI HUZAA MWILI, LAKINI ROHO HUZAA ROHO.” (Yh 3:6) Lakini ukiendelea kutojua using’ang’anize kujua, maana mambo ya Roho hufahamika kwa waliozaliwa na Roho! Yesu aliendelea kumwambia Mwalimu mzoefu wa miaka mingi katika Torati ndani ya Islaeli kuwa, “10…. ‘‘Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya? 11Amin, amin, ninakwambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. 12 Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni?”

  “KWA HIYO TOFAUTI YA MTU ALIYEZALIWA MARA YA PILI NA YULE AMBAYE HAKUZALIWA MARA YA PILI, NI KUWA, “MWILI HUZAA MWILI, LAKINI ROHO HUZAA ROHO.” WALIOZALIWA KATIKA MWILI MATENDO YAO NI YA KIMWILI NA WALIOZALIWA KATIKA ROHO MATENDO YAO NIYA KIROHO, maana kila mtoto hutenda kama baba yake atendavyo! J, WEWE UNATENDAJE?!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 73. Lwembe,

  Mpaka hapo kwa maelezo yako mazuri, mimi bado sijaelewa tofauti ya mkristo aliyezaliwa mara ya pili na mkristo asiyezaliwa mara ya pili. Labda jaribu kuwa maalumu zaidi katika fafanuzi yako ili iwe nyeupe na nyeusi zaidi.

  Asante!

 74. Ndg yangu Ziragora,

  Ninavyokuona, ni kwamba unasoma Biblia yako kama gazeti!

  Jaribu kwenda nayo pole pole, usiwe na haraka utaishia kujichanganya kama ninavyokuona! Biblia iliposema “Mshahara wa Dhambi ni Mauti”, haikuwa inawahukumu watoto wa Mungu, bali inawatamkia wote ambao wamelikataa Neno la Mungu, hao wasioamini! Kwahiyo kama wewe unaona linakufaa Neno hilo, huo ni uchaguzi wako, na matokeo yake ndiyo haya yanayojionesha, unajitahidi kupinga kila lililo jema la Mungu kwa kung’ang’aniza mambo yasiyo na faida!

  Nimekuonesha dhahiri kwa Maandiko kwamba HUWEZI kuijua Dhambi bila Sheria, sasa sijui lipi lililo gumu; Dambi inajulikana huko Agano la Kale, ndiko ilikoanzia na si katika Agano Jipya. Huku ktk AJ kuna Dawa ya Dhambi tu ndg yangu, Kuponywa au Kuangamizwa; ndipo kama umeponywa elewa hivyo na kama umejipoteza pia elewa hivyo. Ndio maana nikakukumbusha ukiangalie hiki kifungu ndipo ujue kuwa wana wa Mungu hao wachanga wanaweza kutenda dhambi, na akiwepo aliye mtakatifu akaliona hilo ndipo Mungu anamwambia hivi, 1Yn 5:16-17
:
  “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.”
  Sasa kuna gumu gani hapo la kueleweka? Kama hukufundishwa Torati, ndio utajilazimisha kubaki katika ufahamu wa dhambi ya Mauti kuwa ni ile ya kumkufuru RM tu wakati Dhambi hiyo iko tangu AK!!
  Au ukisoma hapa huwa unaelewa nini? 1Yn 2:1 “1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki” Nenda pole pole kaka!!

  Kuhusu yule mwanamke mzinzi, naona unataka ulilazimishe lisilo kuwepo! Hebu soma tena tukio hilo ili upate ufahamu, Yn 8:7 “Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, YEYE ASIYE NA DHAMBI MIONGONI MWENU NA AWE WA KWANZA WA KUMTUPIA JIWE.” Kama huo ni msamaha, basi huu hapa ni nini? Mk 2:5 “…Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.”!!!!!!

  Karibu Ziragora!!

 75. Sungura, Seleli & all,

  Mnataka kujua, “Mkristo aliyezaliwa mara ya pili ni yupi, na asiyezaliwa mara ya pili ni yupi?”

  Kimsingi, tunapofika ktk kuzungumzia “Kuzaliwa mara ya pili”, msingi wake ni lazima uwe umejengeka katika Wokovu, maana ni ktk Wokovu ndiko kuna Kuzaliwa mara ya pili au Kubadilishwa au to be Converted.

  Kuzaliwa mara ya pili au Kubadilishwa au to be Converted, ni kule kubadilishwa Jinsi; kutoka Jinsi moja na kuwa Jinsi nyingine, kitabia, yaani “characteristics”. A change in form, character, or function.

  Basi ili uweze “Kuzaliwa mara ya pili”, ni lazima kuwe na wakati ilipotungwa mimba, hii ndiyo Sheria ya maumbile kuhusu kuzaa. Ndiposa, mimba ya kiroho inatungwa siku ulipoisikia Injili!! Maana Imani ndiyo Mbegu inayopandwa katika nafsi zetu kupitia Injili, Rum 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Nalo Neno hilo la Kristo ndilo hili hapa likiamriwa tuletewe kwa ajili hiyo, Mk 16:15-16 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”

  Kwahiyo kama tunavyoyaona Maandiko hapo, yanasema “Aaminiye na kubatizwa ataokoka”, hivyo ndivyo lililvyo jambo la Kuokoka, kama ile Injili uliyohubiriwa ilifanikiwa kuipanda Mbegu ya Imani! Pia tunapaswa kufahamu kwamba Injili ndani yake inayo thamani kamili ya Damu ya Kristo, kwahiyo si jambo la bure, thamani hiyo ndiyo iliyolipwa kutununulia UHURU katika Kristo!

  Hatua hii ndio ya kwanza katika Mchakato wa WOKOVU. Pia tunaposema KUOKOKA, ni vizuri tukaijua na tofauti ya kimantiki na neno WOKOVU licha ya kwamba yanazungumzia jambo moja, bali WOKOVU ni compound, ndani yake ndimo kumo KUOKOKA; yaani WOKOVU unaanza na KUOKOKA!!!

  Basi katika hili tuseme kwamba mpagani anapohubiriwa Injili (kule kuitwa), akiisikia humjengea Imani, nayo imani hiyo humuongoza katika Ubatizo, huo wa Jina la Bwana Yesu Kristo ili aondolewe Dhambi zake, akiikamilisha Hatua hiyo ya Kwanza ambayo ndiyo Kuhesabiwa Haki kwa Imani! Hii ndiyo ile Hatua ya Kutungwa kwa Mimba ya Kiroho!!!

  Alipohubiriwa Injili, ilimshitaki moyoni mwake, akaiamini kwa kuyaona makosa yake, nayo Injili ikamtangazia Neema ya kusamehewa Dhambi zake, na kumuongoza katika kuukamilisha Msamaha huo, ndiko huko Kuondolewa Dhambi zake zilizomtenga na Mungu ili sasa aweze kumkaribia. Katika Hatua hii, huyu aliyeujia ukristo, ndipo anapoanza safari yake ya kumfanania Kristo. Mafanikio yake yatategemea kwa ukubwa walimu wake, maana wako walimu wa kweli na wa uongo; lakini zaidi umakini wake wa kuyaoanisha mafundisho anayopewa na Maandiko, Mungu huwapenda watu wenye jitihada ya kweli.

  Ndio kusema mkristo huyo mchanga, anaweza akapotea asipokuwa makini. Maana tunaposajiliwa katika Wokovu, huwa tunasajiliwa kuvipiga vita vya Imani! Nao ushindi wetu ulikwisha kamilika katika Kristo, yeye aliye Ngao yetu, kuizuia mishale ya Adui. Basi ukichanganyiwa mafundisho yasiyotokana na Neno, hayo hayana uwezo wa kuizuia mishale hiyo, unatunguliwa kama bao la kulengea shabaha!!

  Kwa leo ngoja nikomee hapa, ili kama kuna jambo la kulitazama, basi twende sote katika hatua ili tusahihishane palipo na mapungufu ndipo tuendelee!

  Karibuni, Sungura, Seleli na wote,

  Mbarikiwe!!!

 76. Lwembe,

  Ndugu yangu, kam wewe ndiwe unafundisha watu wafanye uzinzi, hebu tuambie tukujue. Kwani sijawai sikia mwalimu mukristo, na hili tamko « mukristo » nikalirudilia, akifundisha watu kutenda dhambi yoyote. Kama umewai kuwaona hawo si wakristo. Ina maana pengine unaenda shiriki mkanisa ya kishetani pasipo kutambua.

  Kwa upande mwengine, anaetetea kam kuna dhambi ambayo mshahara wake siyo mauti huyu ndie ahimizae waumini kutenda dhambi hizo, hio ndio hatari.

  Unaposema hatujue dhambi ni nini, nadhani unadaka picha yako kwa kuibandika wengine. Uwe mwanaume na useme yaliyo kweli. Mtu akikuambia « kila ukeukaji wa maagizo/sheria ya Mungu ni dhambi », wewe unasema hajue, sasa kosoa ile sentence, tutakuelewa.

  Kusudi ufafanue dhambi vizuri unatakiwa kufahamu matukio yake mwilini, nafsini na rohoni. Sasa, hivi vyote ukiviweka nafasi moja kama wakati wa torati utajipoteza wewe mwenyewe kama mafarisayo.
  Kwani hata waliokuwa wakiua wazinzi, ilibidi hawo wazinzi wanaswe, na kuwe wanaohusika kuwaua. Kama una ujuzi wa hii mada, nakuomba kwa leo utaje watu wanaoruhusiwa kuuwa wazinzi.

  Kwa nini unakwepa ? Hii andiko ya YOHANA 8, unaisema juujuu kirahisi tu, wala hupendi itika kama kulikuwa huruma. Wewe unakimbilia kwenye hukumu. Nilikuuliza wakati Yesu alimwambia mwanamke aende na asitende dhambi tena, hapo hakumhurumia ? Kwani Yesu angehesabu huyu mwanamke kuwa maiti kwa nini aambie maiti isitende dhambi tena ?

  Wakati unaongea sentiments, sijue kwa kweli unaongea na nani! Au unajiambia mwenyewe. Kwani palipo sentiments kuna upendeleo. Sisi wakombolewa wa Yesu hatuna sentiments. Hizo zilipatikana kwa mafarisayo. Kwanza msimamo ni mmoja : « kila ukeukaji wa maagizo ya Mungu ni dhambi », na haturuhusu mtu kutenda dhambi yoyote. Sasa wewe unayeona kama uzinzi ndio dhambi pekee ipelekao mautini wewe una sentiments zako mwenyewe.

  Naona hapa si lazma tutoe shahiri ingine, nataka nirudishe upya niliyokutolea iwe zamu yako ya KUTOA NJE YA ORODHA DHAMBI YA UZINZI. Unionyeshe umeitia wapi na dhambi nyingine zimebaki wapi. Pia uniambie kama unajitambua kuwa na upungufu au la.

  “1 Wakorintho 6:7 Basi imekuwa UPUNGUFU kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?
  8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
  9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala WAABUDU SANAMU, wala WAZINZI, wala WAFIRAJI, wala WALAWITI,
  10 wala WEVI, wala WATAMANIO, wala WALEVI, wala WATUKANAJI, wala WANYANG’ANYI.
  11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  Tuendelee saidiana.

  Asante

 77. Lwembe,

  Nangoja na mimi mlangoni kwa usongo ujibu swali zito la Sungura kuhusu Mkristo aliyezaliwa Mara ya pili na asiye zaliwa maana umeongea mambo yenu yale yale na Siyi na Mabinza yaani mambo makubwa-kubwa kumbe bwana mmmh! kazi!!!…. Umesema, aliyezaliwa mara ya pili HATENDI DHAMBI.

  Aya mjibu Sungura kisha we move on.

  Press on

 78. CK Lwembe,

  Nimekuelewa vizuri na sina objection katika kusema kwako kuwa,
  “Kwanza unapozungumzia Dhambi, ni lazima uwe katika ufahamu wa Torati ndipo unaweza kuijua Dhambi, maana hiyo ndiyo iliyotufundisha jambo hilo. Kwahiyo hauwezi ukazungumzia Dhambi nje ya Torati, utakuwa ni muongo, Rum 5:13”

  Lakini hoja ambayo umeisema na hujaiweka wazi ni hii, “Basi kama unajidanganya kuwa Dhambi zote ni sawa, ndio kusema kusanyiko lako halikuwa na mwalimu ambaye angekufafanulia zaidi kuhusu mambo haya, maana sasa, ili Haki yako izidi, Torati imekuwa magnified kwako wewe.”

  Haki izidiyo ya mafarisayo ni ile haki itokanayo na IMANI tu basi, Biblia inasema, “Kwa imani mtu hupata haki”kwa sababu mafarisayo walitegemea haki itokanayo na ushahidi wa macho (jambo likubalike kwa ushahidi wa watu wawili ama watatu nk.) Lakini haki inapaswa kuzidi hapo kwa maana ya kwamba, Roho ndiye awe shahidi wa mambo yote! (hata mnaposali ingieni chumba cha ndani na Baba yenu aliye sirini atawajazi) , vile vile inaendelea kufundishwa na Biblia kuwa, hata katika kufunga kujulikane na Mungu pekee, ndiyo maana hata Yule mtu na mkewe, walipouza shamba na kupatana kwa uongo, walikufa kwa ushahidi waroho mtakatifu tu! Torati ya kimwili ni kivuri cha Torati ya kiroho!

  kwakuwa torati haijapata kubatirika wakati wowote maana ya dhambi inabakia vilevile, na mshahara wake ni uleule mmoja –KIFO! Lakini itabaki haileweki kwa makosa yenye uzito ulitofautiana kuwa na adhabu au hukumu moja! Biblia hailezi kuwa kuna utofauti katika dhambi, maandiko yanakazia kuwa, dhambi ni kutoamini Neno la Mungu. Kuja kwa Bwana Yesu na kufa msalabani ilikuwa ni kwa ajili ya sadaka kwa ondoleo la dhambi na si kwa maondoleo ya dhambi. Na inaeleweka na kukubaliwa na Neno la Mungu kuwa dhambi huondolewa mara moja tu, hiyo inathibitisha kuwa, dhambi ni tabia na si tendo, kutokana na tabia hiyo ya dhambi ndipo hutokeza matendo yenyekuendana na tabia hiyo ya dhambi!

  Tumejifunza na kuelewa kuwa, Yesu alikuja na kuwachagua Mitume kumi na wawili kwa lengo la kwamba, wawahubiri watu wote ili “WAAMINI”‘atakaye amini ataokolewa na asiyeamini atahukumiwa’ kuamini nini? Kuamini Neno la Mungu! Kwa maana nyingine Yesu alikuja kuondoa kule kutoamini na kuweka kuamini ndani ya atakayeikubali injili. Huko ndiko kunakoifafanua maana ya dambi. Yapo matendo ya dhambi, yaani matendo yatokanayo na dhambi, haya ndiyo huwa mengi, yapo tofauti na yanatofautiana kwa majina na kwa uzito wake. Watu huyaita nayo kuwa ni dhambi, lakini kiukweli yale si ile dhambi yenyewe, maana kutoamini diko kunakotokeza hayo matendo. Paulo alipata kufundisha juu ya dhambi na matendo ya dhambi aliposema kama hivi.“NIKITAKA KUFANYA JEMA, NAJIKUTA NIKITENDA YALE MABAYA, HII NI KWA SABABU YA ILE DHAMBI ILIYOMO NDANI YANGU”

  Hakuna kutoamini kudogo ama kukubwa, vile vile hakuna kuamini au kutoamini kwa uzito tofauti tofauti, kama mtu haamini, haamini tu; na akiwa katika kuamini ama kutoamini, mtu huyu huwa yupo katika “SHAKA”na mtu akiwa katika shaka (KUSITA SITA) MUNGU anasema, atamtapika!

  Bado nahitaji kujifunza zaidi, nahitaji kuonyeshwa maandiko ama andiko linaloonyesha ama kusema kuwa, dhambi zipo nyingi, za aina tofauti tofauti na kama zipo dhambi kubwa na ndogo zikipimwa kwa kulinganishwa na nini!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 79. Ndg Ziragora,

  Mwalimu anayemfundisha mwanafunzi wake kuwa anaweza kutubia “uzinzi”, huyo ni “mwalimu wa uongo”, na wako wengi tu! Tena jambo hilo laonesha kuwa hata Dhambi hawaijui ni nini na ni lini imekuwa Dhambi!

  Kuigopa Dhambi bila Maarifa hakuwezi kumsaidia yeyote yule zaidi ya kuishia upotevuni; bali kuijua Dhambi ndiko humsaidia mkristo kujilinda! Pia ni muhimu kujifunza Neno lililofunuliwa, kuliko kutembea katika assumptions zetu; maana Maarifa hutokana na KUYAFUATA Maandiko ktk yanachokifundisha, Isa 28:9 “Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii?…”

  Mshahara wa Dhambi kuwa ni mauti, haimaanishi kwamba usijifunze Dhambi ni nini. Mchango wa Seleli hapo juu ulilizungumzia jambo hili ambalo wewe unataka watu walikanyage, kumbe limewekwa hapo ili kuwapa Maarifa! Maandiko yanasema kuna Dhambi ya Mauti na isiyo ya Mauti. Na yanaendelea kutufundisha kuhusu lipi linawezekana ili kuiokoa au kuikatia tamaa nafsi iliyoanguka katika dhambi hiyo, 1Yn 5:16-17
  “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.”

  Sasa Andiko hili haliwezi kukusaidia chochote iwapo hata Dhambi zenyewe hauzijui! Hebu niambie itakufaidia nini kujipumbaza kuwa Dhambi zote ni sawa, na kisha ukamkuta mwanao mmoja ameiba na mwingine amezini, ndipo ukawanukulia hiyo 1Kor 6:9-10 na kisha ukawaacha hapo ukaenda zako, au ukajiingiza katika kuwaombea wote na kujiridhisha kuwa wamesamehewa? Hapa ndipo pana umuhimu wa Maarifa!!!

  Kristo hakuja kuitangua Torati bali kuitimiliza. “Uzinzi” ni kati ya zile Dhambi za Mauti. Huko nyuma ilikuwa na lazima ukamatwe ktk tendo hilo, lakini sasa hivi hata kwa kumuangalia mwanamke na kumtamani, unaingia ktk Dhambi hiyo ya Mauti!!! Nilikuambia Kristo alipozungumzia talaka, aliishia kwenye Uasherati, hakuzungumzia “Uzinzi” kwa sababu Yeye ndiye Torati, anajua mzinzi anapaswa auawe, kwahiyo huwezi kuipa talaka maiti! Na hilo tukio ktk Yn 8, halina uhusiano wowote na Dhambi ya Uzinzi bali linatoa mwanga ktk jinsi ya Hukumu. Hakuna mchafu anayestahili kutoa Hukumu, hata kwa dunia tu unaweza kujifunza hilo, kwamba hakimu anayepatikana na kosa la jinai haruhusiwi kuendelea na kazi hiyo!

  Pia unapaswa ujue kwamba watu wa Mataifa hawakuwa na Sheria, hiyo ambayo kwayo Uzima ulipaswa kupewa. Walipoitwa katika Wokovu, hatua ya kwanza ni Sheria, ndio maana imeandikwa kuwa kazi ya Sheria ilikuwa ni kutuleta kwa Kristo. Basi hauwezi ukauzungumzia Wokovu bila Sheria, hiyo iliyokufunza kuhusu Dhambi. Utatubu nini kama hata Dhambi yenyewe huijui?

  Tuacheni sentiments, tusiyategemee mafunuo yetu, Mungu hana shirika na mafunuo binafsi wala tafsiri zetu. Tuseme kile Mungu alichosema, pia tuwe wanyenyekevu ili tupate kupewa ufahamu wa Maandiko, maana bila ya huo hatutaelewa wala kukipata kilichokusudiwa. Kama kila mtenda dhambi ataishia kwenye Ziwa la Moto, basi haya Maandiko yana kazi gani?:
  Ebr 12:6 “Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.”

  Pole pole ndg yangu!!!

 80. Br Lwembe .
  Safi…..kwa mpendwa ambaye amepitia hizo hatua 5 zilizoko katika hiyo Ebr6:4,6 hana udhuru…..Ebr10:26-29 inasema kama tukifanya dhambi kwa KUSUDI kwa kumfanyia jeuri Roho wa Neema hakuna dhabihu…nakubaliana nawe hakuna kuchezachea na wokovu.

  Swali

  kwani hizo dhambi zinginine zinzosamehewa kama wizi kama ulvyoesema awali haziusiki na Ebr 6:4.6,10:26-29

  Hapa Bwana Yesu alimaanisha nini…
  ” Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu”.LK15:7

  Mabinza na wengineo wanasema dhambi zote sawa kwa maana ya zote zinakuelekeza shimo la moto…….sawa…….. Tukiacha dhambi ya kumkufuru RM sasa hawa waliosebiwa haki…. LK15:7 wanatakiwa kutubu dhambi zipi ambazo Ebr6:4.6 na 10:26-27.Azikuwashika hao wenye haki.

  tuendelee kujifunza

  Mbarikiwe

 81. Lwembe,

  Right, kuepuka zinaa , kabisa, huu ni UKWELI. Lakini siyo zinaa tu bali DHAMBI ZOTE.

  Nafikiri inabidi uchunguze unayoandika. Hivi umekwishaona walimu wakristo, tena nasema wakristo wangapi wanaofunza waumini wao kutenda dhambi?
  Wanaokuwa kwa upande wa Yesu wote wajua kam mshahara wa dhambi ni mauti. Sasa sijue kam wewe ni upande upi ili utetee dhambi fulani kam ya wizi iwezekane mshahara yake isiwe ya mauti. Ukichunguza vizuri uliyoandika utaona ni mda tu ulimleta kunusurika mwizi katika torati.
  Wanaosema kam dhambi zote zina hasara moja rohoni wao hawafundishe watu kutenda dhambi. Wanaopima kutofautisha dhambi kwa vikundi vikundi ndiwo wanafunza watu kutenda dhambi fulani pasiko kujali hapo wakidhani ni dhambi nyepesi. Yoooo… hawa wote makao yao ni katika ziwa la moto.

  Toleo hili latosha kuhakikisha kam wevi, na wazinzi, nk ni sehemu moja:

  “1 Wakorintho 6:7 Basi imekuwa UPUNGUFU kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu?
  8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
  9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa Mungu, wala WAABUDU SANAMU, wala WAZINZI, wala WAFIRAJI, wala WALAWITI,
  10 wala WEVI, wala WATAMANIO, wala WALEVI, wala WATUKANAJI, wala WANYANG’ANYI.
  11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

  Sasa hila za kutofautisha dhambi kiwango kile ina lengo ya kujaribu kuhalalisha wizi ili watu waendelee iba. Ndio maana mtu utamuona akirafikiana na uongo akidhani hiyo si dhambi, anapoiba anadhani ni rizki, anaponyang’anya anadhani amebarikiwa, …

  Yesu!!! wengi hawajaokoka kweli!

  Sijue kwa nini husome Kitabu cha mwanzo ili pale tu pakufundishe dhambi ilianzaje na adhabu ilikuaje. Kila ukeukaji wa maagizo/Sheria ya Mungu ni dhambi na adhabu ni kali. Adam na Hawa walipokula tunda, hii ilitosha wapate adhabu ya Kifo kutoka Mungu, na hiyo adhabu inaendelea kwa vizazi na vizazi. Hutasoma pale kama Mungu alipanga sawasawa dhambi akisema:mmezini ,au mmeiba, au mmeua, nk. Kinacho kasirikisha Mungu ni kuona Mwanaadamu anatenda kinyume ya maagizo yake. Full stop. Pia kinachompendeza Mungu ni kumuona mwanaadamu akiacha njia zake mbaya.

  Torati iliadhibu watu walioonekana kwa macho ya wanaadamu. Ndio maana hata leo kwa macho ya wanaadamu, dhambi zina uzito tofauti. Wanaoendelea kuwaua wazinzi kwa panga wana macho ya kimwili tu. Torati inaruhusu taraka,lakini Yesu alifafanua kam ilikuwa kwa sababu ya ugumu wa moyo wa wahusika. Hence, ukiwa mgumu wa moyo kwa kufwata torati wewe si wa Yesu.

  Halafu Yule mwanamke!!!
  “YOHANA 8:10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
  11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; WALA USITENDE DHAMBI TENA.”

  Yesu anapomwambia “Enenda zako, wala usitende dhambi tena”, unafikiri hakumuhurumia? Kama hio dhambi haiwezi hurumiwa kwa nini huyu mwanamke asiendelee katika dhambi yake? Kwani kutorudilia dhambi ndio kutubu ya kweli na kupata msamaha kamili.

  Lwembe, wakati moja Biblia haiseme herufi kwa herufi kila jambo, lakini alie na sikio anasikia!

  Ahsante.

 82. Lwembe,

  Mkristo aliyezaliwa mara ya pili ni yupi, na asiyezaliwa mara ya pili ni yupi?

 83. Mjoli Haule/Tumaini na wapendwa wote,

  Ni kweli kwamba yawezekana nikaonekana ninahukumu kwa matendo ya Sheria, lakini iwapo mtalitazama jambo hili vizuri, ndivyo lilivyo!

  Kwanza unapozungumzia Dhambi, ni lazima uwe katika ufahamu wa Torati ndipo unaweza kuijua Dhambi, maana hiyo ndiyo iliyotufundisha jambo hilo. Kwahiyo hauwezi ukazungumzia Dhambi nje ya Torati, utakuwa ni muongo, Rum 5:13
  “… lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria”

  Tangu mkristo anapompokea Kristo, katika kule Kuhesabiwa Haki, hapo ndipo mafunzo huanza, akipitishwa ktk Torati kukiona kile kivuli chake, hata kuiona Dhambi na hasara zake. kwa kadiri anavyodumu ktk mafundisho hayo, ndipo huiona Neema aliyokirimiwa kwa jinsi anavyoendelea kubadilika kwa Injili. Mabadiliko hayo humfikisha hata kwenye “vipawa vya RM” km Kunena kwa Lugha, kuombea wagonjwa nk, kwa kadiri anavyotakasika kwa hilo Neno, yaani UTAKASO.

  Katika hatua hizi mbili mkristo anaweza kutenda Dhambi na hata AKAPOTEA! Ebr 6:4-6
  “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri”
  Huu ndio ukweli wa Maandiko! Hakuna mpagani anayevionja vipawa vya RM!!

  Kwa hiyo ni vizuri kulisikiliza Neno linachokifundisha, ili tupate ufahamu sahihi wa namna na mwenendo unaotupasa, maana Haki yetu inapasa iizidi ya Mafarisayo. Basi kama unajidanganya kuwa Dhambi zote ni sawa, ndio kusema kusanyiko lako halikuwa na mwalimu ambaye angekufafanulia zaidi kuhusu mambo haya, maana sasa, ili Haki yako izidi, Torati imekuwa magnified kwako wewe. Si kwamba ukamatwe nayo, la hasha, wewe umepewa kitu cha ziada, RM kukuongoza, ambaye katika hatua zako za awali, zile mbili, hujidhihirisha katika zile Huduma Tano ulizowekewa ambazo hukijaza kiriba kwa “mvinyo mpya”, ile Injili pole pole ikikutoa ktk kifungo cha Sheria!

  Sasa, kama ulikabididhiwa kwa walimu wa mshahara, ndio watakuambia kuwa unaweza kutubia hata “Uzinzi”! ukiwauliza ni wapi mnalipata jambo hilo, wanakuambia “mbona Yesu alimsamehe yule mwanamke.” Kristo hakumuhukumu yule mwanamke, si kwamba alimsamehe, maana wenye kuitimiza hiyo Hukumu ya mzinzi ndio hao ambao nao wanapaswa kupigwa mawe, ndio maana wakaondoka! Hata leo hii Hukumu ya mzinzi ni ile ile, vinginevyo ungeliona jambo hilo katika talaka! Mzinzi wa leo anakufa kiroho pamoja na uzao wake, huo utakaozaliwa sirini, wale watoto “kitanda hakizai haramu”! Ikimbieni zinaa!!!! Watakudanganya sijui toa “Sadaka ya Upatanisho” tuiunge na maombezi; hakuna kitu kama hicho, umekwisha kutupwa huko nje, hakuna tena Damu kwa ajili yako, yaani hakuna Dhabihu ya jambo hilo kama inenavyo Torati!!!

  Mkristo ambaye hajazaliwa mara ya pili anaweza kuyatenda yote hayo, haswa anapokuwa amelishwa chakula kisichofaa, Nguvu ya lile Neno mchanganyiko ni ndogo, hivyo huvutika haraka, naye akiwa bado hajatukuzwa, Torati huendelea kumshikilia! Lakini kwa yule aliyefikia Kuzaliwa mara ya pili, huyu ni tofauti, huyu humdhihirisha Kristo, ndio maana Maandiko yanaliweka wazi jambo hili kuwa huyu HATENDI DHAMBI. Au kuna kati yetu aliye wahi kusoma popote pale kwamba Kristo alipiga fiksi? Hakuna jambo kama hilo, nao wanaomdhihirisha wanafanana naye!!!!

  Mbarikiwe!

 84. JP,

  Sielewi ki uhalisi ulipouliza swali hili ulimaanisha nini! Swali lako halina jibu rahisi kama ambavyo watu wengi wanaweza kufikiria. Kwa sababu, kuna dhambi na matendo ya dhambi, kwa maana hiyo, dhambi ni kitu kingine na matendo ya dhambi ni kitu kingine! Kitendo cha dhambi kipo kikubwa na kidogo, vipo pia vitendo vya dhambi vingi na vichache, kwa hiyo Vitendo si ile dhambi yenyewe, bali ni matokeo ya dhambi liyomo ndani ya mtu mwenyewe. Kutokana na kutopambanua vizuri jambo hilo, watu wayaonapo matendo, ndipo huyaita dhambi kama ni mabaya na huyaita utakatifu kama ni mazuri. Kwa kifupi, matendo hupimika, lakini dhambi kama dhambi, yenewe haipimiki!

  Unaposema kitu Fulani ni kikubwa lazima kiwepo pia na kidogo, na ili kujua kitu hiki ni kikubwa ama kidogo ni lazima kiwepo KIPIMO (SI unit) na ili kipimo kikubalike ni lazima kiwepo KIPIMIO (Standard of unt).

  Kwa upande wa dhambi, hakuna kipimo, ila kipo kipimio pekee (Standard of unt), hapo ndipo “vurugu” inapoanzia! Kusema dhambi Fulani ni ndogo na dhambi Fulani ni kubwa ni kutojua kazi ya NENO katika mwamini, dhambi ni kutokuamini, ni kutokuamini Neno la Mungu – Sam nakubaliana naye. Kwakuwa hivyo ndivyo, basi hakuna kutoamini kudogo ama kutoamini kukubwa, ila ipo Imani Kubwa na Imani ndogo! Maandiko yanasema “Dhambi zote zinaweza kusamehewa isipokuwa atakaye mkufuru Roho mtakatifu hatasamehewa” msemo huo haumaanishi kuwa kumkufuru RM ni dhambi kubwa sana, la! Bali mtu amkufuruye RM ni kama kusema kwa mfano kuwa ‘mtu huyo analazimisha Kipimio cha kipimo cha kimiminika kiwe kipimio cha kipimo cha kitu yabisi au gesi!’. Jambo ambalo ni usumbufu usiokubalika kitaalamu, hivyo mhusika hutimuliwa aende nje, maana haeleweki sayansi anayoiamini na pia anachezea hatari!

  Neno ndicho KIPIMIO cha dhambi (Standard of Unit). Kwa hiyo katika dhambi hatuna kipimo cha kupimia, kiasi, uzito, kiwango ama ukubwa wa dhambi, kwa nini? Kwa saababu DHAMBI NDIYO KIPIMO CHENYEWE, kama ambavyo ‘tunavihukumu’ vitu kuwa, hiki ni kidogo, kikubwa kizito kirefu, kimejaa ama kimepungua kwa kutumia kipimo, vivyo hivyo kinacho fanya hukumu ni dhami; Hivyo kuwa nayo ni kifo na kutokuwa nayo ni uzima. Lakini kinachofanya kipimo hicho kuwa sahihi kwa namna ya ajabu vile ni NENO! Biblia husema, “Neno ni uzima tena ni Roho” lakini jua pia kuwa, Neno ni upanga nasi sote tunajua kazi ya upanga!

  Ninachokiona kwa watu wengi, ni pale wanapoyaona matunda wanadhani kwamba ndiyo mti wenyewe! Matendo ya mtu ndiyo matunda yamuonyeshaye kuwa yeye ni tawi la mti gani. Dhambi ni mti wa mauti, ndiyo maana Neno linasema dhambi ina mzizi, na mzizi wake ni shetani. Na kutokana na Mzizi huo hutokeza mti mbaya (dhambi) na kutokana na mti huo, tunayaona matunda (matendo) ambayo ni kama vile, wizi, uongo, tamaa mbaya, uzinzi, husuda, wivu, kiburi, uchoyo, ubinafsi, ubishi, nk. Na yote hayo ni kifo!

  Kwa hiyo, hakuna Dhambi kubwa wala ndogo, kama ambavyo mizani isivyo na ukubwa ama udogo isipokuwa sifa ya mzani ni uwezo wake. “Yesu akasema yeye asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe” na si kwamba “yeye asiye na dhambi kubwa, na awe wa kwanza kurusha jiwe” Kigezo, alihitajika mtu ASIYE na dhambi, ndiye awe wa kwanza kurusha jiwe, na kwa kipindi hicho alikuwa mmoja tu mwenye nafasi ya kufanya hivyo, ni YESU peke yake, ila hakufanya hivyo, kwakuwa alikuja kwa ajili ya watu wenye dhambi “Sikuja kuuhukumu ulimwengu”!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 85. Mpendwa Lwembe uko crus kweli na majibu yako au unatania?So kaz ya Jesus pale msalabani iwapi kama kuna mambo ya kulipishana mijing’ombe na kupigana mimawe mpaka kuuwana?B crus ma Br!Au hatambua ujio wa Mwana na kazi aliyopiga na maneno aliyotutel?Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha.Na kama haya Amini,amini nawaambia,Yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele;wala haingii hukumuni,bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani {Yoh 5:24}.Amini,amini nawaambia mtu akilishika neno langu hataona mauti milele(yoh 8:51).Mimi ndimi njia ya kweli na uzima mtu haji kwa Baba kwa njia ya mimi(Yoh 14:6).So Br Lwembe hata uwe na mijidhambi gunia 5000 ukimkubali huyu kamanda na kumbwagia yeye basi kilaiini unakula Fiesta milele!No kupigwa mawe no kulipishwa mijicow no blaablaa!ni Full bata tu!Gbu Br!

 86. Wapendwa,

  Biblia inasema hivi:
  “Waebrania 10:1 Basi torati, kwa kuwa ni KIVULI cha mema yatakayokuwa, WALA SI SURA YENYEWE ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.”

  Hii ni mwangaza kamili Biblia inatutolea sisi walio ndani ya Kristo. (Kwani mambo ya torati siyo njia bali ni kuvuli.)

  Yesu anasema:
  “Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

  Mtu hawezi mkimbilia Yesu kiisha ajihesabu kukwezana na mauti, haijalishi ni dhambi ipi alitenda. Anaemkimbilia Yesu anapata uzima.

  Unaposoma 1 Yohana 5: 9, utaona kam anaeshuhudia hapa duniani kama Yesu ni Mwana wa Mungu ni RM.

  Hence, asiyekubali kam Yesu ni Mwana wa Mungu ndiye amepindisha ushuda wa RM/ amekufuru RM. Huyu ndiye hana uzima hapo akiwa ametenda dhambi ya mauti.

  Ukweli kamilifu ni kwamba Biblia haijawai kutuambia kuna dhambi kubwa na dhambi ndogo. Inasema kuna dhambi zilizo kubwa zaidi. “Yohana 19:11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.”
  Zote tuseme ni kubwa kwani iwe kubwa au kubwa zaidi, inayoanekana ni kwamba ni kubwa.

  Isiyosamehewa, ni jambo tofauti, yeye asiyemwamini Yesu hana uzima. Sasa atasamehewa wakati hasadiki anaeshika funguo ya masamaha?

  Mengineo, kwa tendo au kwa mafikiri, anaezini na aneeiba wote inategemea mahala wapo. Wakiwa katika kundi ya wanao haki ya masamaha watasamehewa wakati wanapotubu, wakiwa ndani ya kikundi cha wasio na haki ya masamaha kam Ibilisi, hawatasamehewa.

  Mbarikiwe.

 87. Sungura,

  Unauliza, unazipimaje, dhambi ya wizi na dhambi ya uzinzi?

  Kwanza ni muhimu kuzitambua dhambi kulingana na jicho la Mungu. Dhambi zote si sawa, kulingana na Maandiko. Ukizingatia na hali ya kiroho ya mtenda dhambi hiyo; je, ni mpagani, au ni mkristo asiyezaliwa mara ya pili yaani huyo aliye ktk Torati? Maana kama ni mpagani basi huyo ni dhahiri atakuwa katika Dhamira. Na kama ni mkristo ambaye hajazaliwa mara ya pili basi huyo atakuwa bado anashikiliwa na Torati na hukumu zake, kwani hii ndiyo inayompeleka kwa Kristo ili azaliwe mara ya pili na hivyo huyo kuwa hatendi dhambi tena, maana amezaliwa kwa Roho wa Mungu! Mzizi wa Dhambi ni kutokuamini Neno la Mungu, iwe kwa sehemu au Neno lote, nayo matunda ya kutokuamini huko ndio huo wizi, uzinzi nk kama unavyoshuhudiwa ktk makusanyiko yetu na huko nje!

  Wizi ni mojawapo ya dhambi ambazo zinaweza kutubiwa, dhabihu hutolewa kwa ajili ya nafsi ambayo imetenda dhambi hiyo, Mungu humsamehe huyo na malipizo yake huwa kama hivi:

  1: Mtu akiiba ng’ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng’ombe watano badala ya ng’ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.

  2: Mwivi akipatikana akiwa yu hali ya kuvunja mahali, naye akapigwa hata akafa, hapatakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake.

  3: Lakini kama jua limekucha juu yake, ndipo patakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake; ingempasa kutoa malipo kamili; akiwa hana kitu, na auzwe kwa ajili ya wivi wake.

  4: Kama hicho kitu kilichoibwa chapatikana hai mkononi mwake, kama ni ng’ombe, au punda, au kondoo; atalipa thamani yake mara mbili. (KUT. 22:1-4 SUV)

  UZINZI ni mojawapo ya zile dhambi zisizo na dhabihu, hii ina hukumu moja tu ambayo ni kifo!

  “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.”

  “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.” (MWA. 20:3 SUV)

  Mtoto aliyezaliwa ktk uzinzi ni ‘mwana wa haramu’; huyo issue yake mbele za Mungu iko hivi:

  “Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.” (KUM. 23:2 SUV)
  Yaani mwana haramu haruhusiwi kuingia uweponi mwa Bwana maisha yake yote, na kizazi chake ni mpaka cha kumi, yaani kizazi chake kitaingia uweponi baada ya miaka 400, usiniulize hao wengine wanaishia wapi!

  Ubarikiwe!

 88. ndg zangu japo kwa uelewa wangu mdogo wa neno la Mungu napenda kuheshimu weledi hekima na wingi wa siku kama michango yao hapo juu ilivyotolewa. lakini japo kwa mda mfupi fuatana nami katika maelezo yangu mafupi

  kama dhambi ni kutotiii na kupindisha kweli ya Mungu nachelea kusema hakuna mwenye mwili atakaeziona mbingu pasipo neeema ya Mungu maishani mwetu! haitaji kufanya utafiti mkubwa kwa kuwachunguza ndg zako, rafiki zako wala waumini wenzanko just jitafiti wewe mwenyewe kwa jinsi gani hautii na kupindisha kweli ya Mungu nadhani jibu unalo ndg!

  nachojua mimi hoja ya dhambi ndogo na kubwa haina msaada sana kwa mkristo kwa justfication iliyotolewa na wachangiaji hapo juu ila the consequence of sin inabeba maaana kubwa na inahitaji tafakuri yenye maaana ktk maisha ya mkristo ya kila sku.

  alichonifunza Mungu njia zetu wanadamu ziko mbali sana na njia zake bwana pengine anasema kama magharibi ilivyo mbali na mashariki ndivyo njia zetu zilivyo mbali na njia za bwana hivyo kudhani magnitude of sin kwa vigezo vyetu wanadamu bila kujua magnitude za bwana tunapoteza mda tu

  maoni yangu ndg tuombe daima neeema ya wokovu wa Mungu kwa njia ya Kristo isitupite daima maishani mwetu na kutaka sana utakatifu tuupatao si kwa matendo ya sheria bali imani kwa Kristo Yesu mwokozi wetu

  MUNGU WANGU NAOMBA UNIKUMBUKE KWENYE UFALME WAKO.

 89. Sungura,

  Swali lako Aliyeiba shilingi mia, na aliyezini ikatungwa mimba usawa na utofauti wa dhambi zao mbele za Mungu unaupimaje?

  Jibu:

  Upimaji wa USAWA WA DHAMBI IZO mbele za Mungu ni kuangalia Mungu anazionaje dhambi zote izo ivyo Kuimba na Kuzini zote zina usawa mmoja machoni pake = zote ni dhambi na zisipotubiwa, malipo yake sawa na sehemu ya mwisho ya kila mhusika- mzinzi huyu na mwizi yule ni sawa maana wote ni kwenye fire na wakiwa uko kwa fire, hakuna mageto ya waiba shilling-fire yao lovely na wazinzi mpaka mimba inatungwa-fire yao catastrophic!!!!! Wote one unfriendly and endless fire.

  Upimaji wa UTOFAUTI WA DHAMBI IZO mbele za Mungu ni …consequences ya dhambi kuzini na mimba kutungwa yaani kulinganisha negative impacts kati ya kuchapa(Kuiba) chapaa na kuzini na bebi akatokea, kwa Mtoto mwenyewe in case akizaliwa, ndoa husika ya Wanandoa 2 sasa-aliyetoka kwa wife wake kwenda nje na wife aliyetolewa nje toka kwa mumewe na hiriii njemba jizi , jamii, family, Taifa na kanisa, ni mbali kama vile Magharibu na Mashariki.

  Press on.

 90. PJ na Wachangiaji wote,

  Najua nina takiwa kujibu moja wa moja swali la mada.. ‘Je dhambi zote ni sawa mbele za Mungu’’ na pia kugusia lile ulilosoma mahala kua ‘’’Hakuna dhambi kubwa wala Ndogo kwa Mungu’’ lakini naona nichangie kwanza kwa nini tumejikuta tuna msemo/dhana/mawazo hayo ya ‘’’Dhambi KUBWA au NDOGO.

  Wanadamu kushikilia mambo kadhaa hutokana na sababu, haitokei tu from nowhere, ukakuta misemo fulani ipo na imekamata minds/daily life za watu bila chanzo, sasa kama chanzo hicho ni cha kweli, kimetumiwa vema au la, ilo ni jambo jingine.

  Nini kililetelezea Watu-Hasa Waamini/Wanaofahamu Biblia-wawe wameokoka au wana dini, wawe na dhana ya dhambi kubwa na ndogo?

  JIBU: I CAN TELL YOU FOR SURE CHANZO KIMOJA WAPO NI BIBLIA YENYEWE wala si gazeti la MAWIO AU WASHINGTON NEW POST! Sasa Kama walisoma na kuelewa/kutafsri vibaya icho walichosoma hilo tena ni jambo/tatizo jingine!

  Maandiko haya 3 ni maarufu sana Wanadamu wanayatumia kudhani lazima kuna dhambi kubwa na ndogo( Mengine Ziragora na baadhi mneyatamka au kuyanukuu kabisa-well done job kwa hilo bretheren)

  KWANZA, 1 Yohan.5:16-17= Inasema kuna dhambi iliyo na isiyo ya mauti. Labda nikiiweka ktk Kiingereza itarahisisha uelewa, inasema ivi NKJV…SIN LEADING TO DEATH and SIN WHICH DOES NOT LEAD TO DEATH..Kwa iyo nikitafsri toka hapo, inafungua kiasi tena msamiati huo wa Kiswahili wa-dhambi iliyo/isiyo ya Mauti yaani..

  DHAMBI INAYOPELEKEA/ MPELEKEA/ SABABISHIA/ SABABISHA/ LETEA/ LETELEZEA KIFO

  Au kinyume chake ni kweli…

  DHAMBI ISIYOPELEKEA/ MPELEKEA/SABABISHIA/SABABISHA/LETEA/LETELEZEA KIFO.

  PILI, Mathayo.12:24-33/Marco.3:22-30 = Inasema Kumkufuru/Kuongea/kutamka kinyume na Roho Mtakatifu, hakuna msamaha hapa na baadaye milele

  TATU, 1 NYAKATI.22:7-9= Mfalme Daudi anasema alizuiliwa kumjengea Bwana nyumba kwa kua alimwaga damu nyingi( aliua sana Watu maana alipigana vita nyingi)

  Kwa hiyo kutoka kweli izo za Neno namely…MOJA: Mtu anazuiliwa kufanya huduma ya Mungu kwa kua AMEUA SANA, MBILI, Dhambi nyingine zote Wanadamu watasamehewa lakini si ya KUKUFURU RM, TATU, Kuwepo kwa dhambi ZINAZOPELEKEA na ZISIZOPELEKEA MAUTI/KIFO, basi Ndio maana haraka-haraka wazo linaumbika/akili zina tafsiri kua kuna dhambi kubwa na ndogo.

  Sasa Mtu akitafsiri UKUBWA AU UDOGO wa dhambi kwa mantiki izo, anakosea au la? Mi sijui, aamueni wenyewe, mi hapo nagwaya kusema ila maneno ya Mungu hayo yanaashilia

  Kuna WINGI WA DHAMBI-kuua sana/kumwaga damu nyingi,

  Kuna UBAYA MKALI WA DHAMBI-kukufuru RM

  Kuna MATOKEO MABAYA SANA YA DHAMBI-dhambi zinazopelekea mauti/Kifo

  Press on

 91. Shalom PJ,

  Niliposoma post yako, mawili haya nimeyamulika ili kwayo nichangie chochote kitu hapa!

  Kwanza umesema..’’Kuna mahali nilisoma kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo kwa Mungu

  My response: I hope hapo mahali uliposoma si toka Bible! Na kama ni toka Bible, which chapter na Sura? Na kama si Bible, kwa hiyo ni andiko la Mwanadamu, ok? Na kama ni ivyo, tukilipima ilo andishi/statement ya Mtu na Kweli ya Neno, litasimama? Jibu tunalo wote.

  Ukauliza ivi..’’Je ni kweli? aliyeua na aliyezini wote wanahesabika ni dhambi moja?

  Jibu: Ni dhambi 2 tofauti ingawa zote ni dhambi tu. Sasa kama ulikusudia kusema ipi ni kubwa na ndogo kati ya izo kulingana na mada yako, HUKUSEMA hapo ivyo kukuwekea maneno mdomoni ambayo hukusema mwenyewe, haipendezi kwa mchangiaji kufanya ivyo, ni kukurupuka au kudhani kua ulisema kumbe hukusema, ivyo mtu ktk akili yake, anajibu kwa kudhani ndicho kimesemwa. Labda useme sasa kama ulikusudia kusema kati ya izo ipi kubwa!

  Kuhusu mada sasa, dhambi kubwa na ndogo, nitachangia pia chochote kitu tena ivi punde.

  Press on.

 92. Tujaribu tu kujiuliza,

  Aliyeiba shilingi mia, na aliyezini ikatungwa mimba usawa na utofauti wa dhambi zao mbele za Mungu unaupimaje?

 93. kweli wapendwa hakuna dhambi kubwa na ndogo zote za toshana, satani hutumia binadamu vibaya sana: hasha kwetu nyumbani familia yetu ilikuwa ya kufaana sana. Lakini kati ya wale mandugu wa babangu mmoja aliinamia mashaita mbaka saa hii, wao wote waliisha kabisa. cha ajabu Mungu halali jameni, mimi na mandugu wangu tuku uhai bado kwa jina mwenyezi Mungu muumba bingu na ulimwengu. naomba mniombe uwepo wake Mungu Aniongoze salama katia maisha. Amen

 94. Said,

  Leta tu mchango wako, wala usihofu.

  Wengi wetu tunasema:
  -Dhambi inaonekana kwa MATUKIO yake mbele za Mungu. Yote humzuia mwanaadamu kuingia MBINGUNI. Ni hii inayomaanisha kwamba mbele za Mungu dhambi ni sawasawa.
  -Mtu anapotubu anaweza samehewa na palepale hahesabiwe tena dhambi.
  -Biblia inatuambia kuna dhambi isiyosamehewa: ile ya kumkufuru RM. Hapa siingie kindandi kwani imeongelewa.
  -Angalau waliosema walitumia style na msisitizo tofauti lakini nadhani kifupi ni hayo.

  Sasa wewe wasemaje?

  Ahsante.

 95. Dhambi ni dhambi kwa sababu humtenga mtu na Mungu, na roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa!

 96. MATHAYO 5:27-37 na YOHANA 8:2-11 YESU ANAONGEA NA KUTOA AGIZO. hii inaonyesha, DHAMBI ni KUKOSA UTII. naungana na Sam, kwa kusema, ni KUUPOTOSHA UKWELI. ndiyo maana hata wale washitaki wa yule mwanamke, kila mmoja alijikuta ametenda dhambi, lakini ambayo ni tofauti na hiyo ya uzinzi. kwa MUNGU, na kwa mujibu wa maneno ya YESU (ASIYE NA DHAMBI) YOHANA 8:6, basi naamini, hakuna dhambi kubwa wala ndogo. zote ni kutokutii, kuupotosha ukweli.

 97. Ndugu Yusha,

  Hii swali lako ni la maana tena jibu si rahisi sana!!!!!

  TUjaribu soma hapa kwa makini:

  “1Yohana 5: 1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
  2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
  3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
  4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
  5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
  6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.
  7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
  8 Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.
  9 Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
  10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
  11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
  12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
  13 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.
  14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
  15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
  16 Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
  17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
  18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
  19 Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.
  20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.”

  NA
  “Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;”

  NA

  “Kumbukumbu la Torati 30:19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;”

  Pengine tutapekuwa zaidi, lakini inayokuwa dhambi ya mauti inatokana na uamzi wa mtu kutoamini Kam Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwani hii ndio ufunuo halisi ya RM. Asiyeamini ni yeye anaetenda dhambi kwa kumkufuru RM; yaani dhambi ya mauti. Hii inamaanisha kam yeye asiyeamini, Mungu hamhesabie makosa mengine kwani yeye tayari ni maiti.
  Anaeamini, anayofanya ni dhambi inayoitwa vilevile kosa. Yeye anasamehewa kwa kuomba binafsi au kuombewa.

  Mbarikiwe kwa michango yenu.

  Ahsante.

 98. Huu msemo wa hakuna dhambi kubwa na ndogo au dhambi zote ni sawa mbele za Mungu, unafanana kimatumizi na msemo wa jisaidie na Mungu atakusaidia.

  Ni misemo ambayo haiko kwenye biblia, ila imebuniwa tu kwa logic na busara za watu na kuonekana kuwa inafanana na kweli ya Mungu.

  Unaposema hakuna dhambi kubwa na ndogo unapima against what?

  Je dhambi zote ni sawa mbele za Mungu against kwenda mbinguni?

  Au dhambi zote ni sawa mbele za Mungu against kusamehewa?

  Au dhambi zote ni sawa mbele za Mungu consequence ya hiyo dhambi?

  Dhambi zote ni sawa mbele za Mungu just against kuingia mbingun.
  Lakini si sawa against kusamehewa, na against consequence ya hiyo dhambi.

  Bless!

 99. Kidogo naomba kutofautiana na wengi wenu. Lakini kabla sijatoa maoni yangu kwa undani, Ningependa kusema dhambi yoyote ile ni mbaya na inachukiza.

  Kuna dhambi zinazosameheka na dhambi zisizosameheka. Kuna dhambi za mauti ambazo zinadhuru mwili na roho na hakuna msamaha. Yesu alisema kuwa ukitenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu hutosamehewa hapa duniani na ahera.

  Kunazo dhambi ambazo si za mauti na waweza kusamehewa, yani hazikuweki katika hatari ya mauti na ukiomba msamaha utasamehewa,

 100. Mjoli Haule
  Uzinzi ni tendo la haki lillilopindishwa ( perverted) Mke anapo toka nje ya ndoa.

 101. Bwana Yesu asifiwe,

  Pengine alieleta mada akaona shairi zinazofanana hizi:
  “Yohana 19:11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.”
  “Luka 12:10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.”

  Nataka nimueleze kam iwe imeitwa kubwa zaidi, ni dhambi kama nyingine. Lakini asieamini hana uweza wa kutubu. Inaomba aamini ndipo aweze tubu. Hata hivi kwa mwisho kama toba haiko tukio ni moja tu.

  Asante.

 102. Dhambi ni moja tu!! Dhambi ni kuto amini, kuto amini nini? Kuto amini Neno la Mungu. Dhambi ni ukweli ulipindishwa, mfano uongo ni ukweli uliopindishwa, uzinzi ni tendo la haki ambalo Mungu kalipitisha ila linafanyika sivyo. Kwa hiyo uzinzi, wizi, kusema uongo na mambo yote yanayohusiana na hayo ni viambatanishi vya kuto amini Neno la Mungu.

  Bwana awabariki

 103. Bwana Yesu asifiwe,

  Ndugu yangu, nakosa niandikeje jina lako. Naona PJ si jina, pengine ni shortcut tu. Lakini hii si tatizo.

  Kwa mwanzo nitakujibu tu kwa swali lako bila kuingiza MPENYEZO INGINE:
  Kipimo cha dhambi ni mshahara wake. Kuua na kuzini yote ni dhambi. Na mshahara ni moja tu. Ina maana ni tendo tofauti lakini matukio ni moja, ndio maana yote ni sawasawa. Wala hakuna awezae kujifariji eti mim nimezini halafu niko mwema kuliko alieua, kwani wote watajikuta nafasi moja. Kwa macho ya wanaadamu pengine wataona uzito ni tofauti lakini mbele za Mungu wote ni wakaidi na wanapata tukio moja.

  “Kutoka 20: …..13 Usiue.14 Usizini……” Amri ya Mungu.
  “Warumi 6:23 KWA MAANA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”

  Unaona Ndugu yangu kama, mshahara wa dhambi ni mauti. Biblia haituambie kam kwa dhambi fulani mshahara ni fulani na kwa dhambi ingine mshahara ni ingine.

  Ubarikiwe.

 104. Ah! nimesahau kuandika kitabu na sura ya mstari unaosema

  bali waoga,na wasioamini, na wachukizao,na wauaji, na wazinzi,na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote sehemu yao ni ktk lile ziwa liwakalo moto na kiberiti na hii ndiyo mauti ya pili

  ni ufunuo 21:8

  ubarikiwe.

 105. AMEN

  Ni kweli kabisa dhambi zote ni sawa mbele za MUNGU hakuna dhambi kubwa wala ndogo alimradi ameshakataza jambo na ww ukalifanya unahesabika ya kuwa ni muasi 1Yoh 3:3-10 ss wanadamu tunazitenganisha dhambi lkn si hivyo kwa Mungu bali waoga,na wasioamini na wachukizao na wauaji na wazinzi na wachawi na hao waabuduo sanamu na waongo wote sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti hii ndiyo mauti ya pili. nafikiri umeona mwenyewe hasa kile kipande cha mwsho anasema waongo wote haijalishi unaongopa kwenye cm au ofisini yaani waongo wote na ktk dhambi tuliyotokea wanadamu kuidharau basi ni hii ya uongo ila mshahara ni m1 na muuaji warumi 6:23 kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti ndugu yangu PJ take care shetani asikurubuni

  shalom
  shalom.

 106. Kwa vile ni mitazamo na uelewa, tu, ngoja tutoe mitazamo yetu.
  Ili kujibu swali lako ndg, ni vizuri kuelewa dhambi ni nini. Biblia imeeleza dhambi ni nini. Mbali na wanaeliungu(wanateolojia), ukiisoma Biblia wewe mwenyewe, utagundua kuwa, Biblia ina neno dhambi 399 katika agano la kale, na 217 katika agano jipya, yanayofanya jumla ya maneno – dhambi kuwa 616. Kimsingi ukiyaangalia vizuri, utagundua kuwa, yote yana maana ileile moja ya kuwa kinyume na SHERIA YA UUNGU.
  Fasili ya dhambi
  a. Tendo lolote lililokinyume na sheria ya Mungu.- 1 Yohana 3:4
  b. Tamanio au wazo la kiakili-kimwili linalopingana na roho(spiritual mind), na ambalo agh. humfanya mtu kuwa kwenye majaribu au kutenda dhambi kabisa.- Rum. 7:7,8. -7, Mathayo 5:27-28, Yakobo 1:14, Mithali 24:9
  c. Kutouamini au kuukataa kabisa kwa nguvu ukweli/kweli ya Biblia. yoh 3;18, yoh 16:8,9.
  d. Uzembe wa kutofanya kazi ambayo ni wajibu wako kabisa. Yoh 4:17, Yok. 2:14, Mathayo. 23:23, Mathayo 25:43-46.

  e. Kufanya jambo baya kwa kukusudia. -Lawi 5:17-19. Luka 12:48; 1 Tim. 1:13.

  f. Hali yetu ya asili tuliyoirithi kutoka kwa Adamu- Zabur 51:5; 58:3, Rum. 5:19,20; Efes. 2:3b; Filip. 3:20,21

  g. Hali iliyopo ndani yetu iliyokinyume na mapenzi ya Mungu (uovu-dhambi inayoishi ndani ya mwili) inayotufanya kuwa watumwa wa dhambi, kiasi cha sisi kutoweza kuishi maisha matakatifu isipokuwa kwa nguvu itokayo juu. Rum. 7:14, 20-23, Luka 11:39; Jyoh. 8:31-34.
  Kwa hiyo ndg, dhambi ni dhambi tu maana, hatima ya dhambi ni mauti. Kosa au dhambi ni dhambi tu mbele za Mungu.
  Note: The first four definitions of sin (Aspect a-e) involve guilt because we choose to commit these sins (guilt involves responsibility or volition). But the last two definitions of sin (aspect f. and g.), which we all inherit at birth because of the Fall, do not involve guilt (i.e., responsibility) but only condemnation (see Rom. 5:18). While these last two definitions of sin do not involve guilt, they nonetheless make us sinners by nature and, therefore, disqualify us from heaven (see Rom. 5:19; Eph. 2:3b; 1 Cor. 15:50).

 107. Dhambi zote ni sawa sababu zinamtenga mtu na Mungu na kumfanya mtu kwenda motoni

 108. Kwa nn kumekuwepo na hii tendency ya with kuuliza maswali ya kawaida sana then mwisho mnamalizia na kuomba mistari ya bible? Binafsi najua Mkristo hutakiwi kujadili ukubwa au udogo wa kitu kinaitwa dhambi,unatakiwa kuzichukia zote na kuomba sana Mungu akujaalie kuziepuka zote.Hui mjadadala wa kubwa na ndogo unasaidia nini zaidi ya kuchochea uzembe?
  Zaburi ya kwanza ni funzo kubwa sana,tuondokane na mizaha tunapoyatafakari matendo makuu ya Bwana Mungu wetu.
  Neema ya Bwana wetu Yesu Kristi na upendo wa Mungu Baba na ushirika wa Roho Mtakatifu utushukie na kukaa nasi daima.

  Oneness Brethren,

  Reggie.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s