Maelfu wapoteza Maisha kwa Kimbunga Ufilipino

yolanda1

Inadhaniwa zaidi ya watu elfu kumi wamepoteza maisha na wengine kupotea kutokana na kimbunga kilichotokea Philippines,

Kimbunga Yolanda, pia kinajulikana kama Haiyan, kinakadiriwa ni kibaya zaidi kushuhudiwa, kiliandamana na upepo mkali unaovuma kwa kazi ya karibu kilomita 300 kwa saa na kusababisha mawimbi ya bahari kwenda juu urefu wa mita 15 katika maeneo ya pwani.

Kimbunga kilipotokea wakristo mbali mbali na wakazi wa nchi walimuomba Mungu awaepushe, Naye afisa wa ICRM Unit King Reginaldo, ambaye ni mfuatiliaji wa Kimbunga hicho aliweka bandiko la maombi kwenye kurasa wake wa facebook

Tafadhali tusamehe dhambi zetu zote na mapungufu yetu. Tunajua Wewe ni Mungu mwenye upendo. Watoto wako hapa duniani , hasa katika Philippines, wanakulilia wewe Bwana, tuokoe na dharuba hii, tuma malaika wako watakatifu watulinde ee Bwana

Wewe mwenye kudhibiti ulimwengu na kila kitu ndani yake. Tafadhali ondoa kimbunga hiki kwenye ramani ee Mungu” aliandika ujumbe mwingine. “Tunaomba hayo kwa jina la Mwana wako , Yesu Kristo. Amina.”

Na wananchi wengine waliendelea kuandika maombi mbali mbali kumuomba Mungu awanusuru na kimbunga hicho kilicholeta maafa makubwa kwenye nchi hiyo.

Tuendelee kuwaombea ndugu hawa, Mungu awafariji, wakapate malazi, chakula na maisha yao yakaendelee vema. Amen

Advertisements

2 thoughts on “Maelfu wapoteza Maisha kwa Kimbunga Ufilipino

 1. Mungu awaepushe wenzetu wa Ufilipino na Asia kwa ujumla dhidi ya majanga ya mara kwa mara kama Sunami,Haiyan n.k ——————————

 2. Wapenzi,
  Ni mtazamo tu.
  Mabaya haya yote yanayotokea kwa nchi za wenzetu, ni matokeo ya uasi wa sheria ya Mungu. Mataifa yanayoathirika kwa matukio makubwa kama vile matetemeko ya ardhi, sunami, vimbunga, nk vinavyoua watu, kwa mtazamo wangu mimi nafikiri kuwa ni matokeo ya uasi. Roho wa Mungu alishahama kwa mataifa hayo. Mataifa ambayo matukio kama haya hayajaanza kutokea, inaonekana kama uovu wa mataifa hayo ikiwemo na Tz, haujafikia kiwango cha mataifa yanayoathirika. Malaika wa kuzuia ghasia na pepo, walishaziachia pepo hizo ili ziidhuru nchi…Ufunuo 7:1…
  1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.
  2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
  3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
  4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
  5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
  6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
  7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.
  8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.
  9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
  10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.
  11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
  12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.
  13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
  14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
  15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
  16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.
  17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

  Kuwakumbuka kwa maombi ni jambo jema sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s