Umeshakutana na hali hii?

prayers

Naomba kuuliza wana SG wenzangu kama mmeshakutana na situation kama hii hua naingia kwenye maombi na unakuta napata majibu mazuri lakini wakati naanza kushukuru kwa lile nililoomba hali inarudi kama kabla sijaomba mfano niliomba kwa ajili ya uponyaji wa mamangu na kipindi namshirikisha kushukuru alizidiwa na kulazwa hospitali wiki 2.Niliumia sana na hata nikawa na woga wa kutoa ushuhuda kua amepona kwa maombi kwakua ntaonekana natoa shuhuda ya uongo.

Naomba msaada wenu wa mawazo na kibiblia jinsi ya kuepukana na hali hii kama kuna mahali nakosea nipate uelekezi wenu.

–Tina

Advertisements

14 thoughts on “Umeshakutana na hali hii?

 1. Nawashukuru tena kwa mara nyingine jamani sijui nieleze vipi furaha niliyonayo kwa miongozo yenu ninyi mliochangia na ni kweli nimegundua mahali udhaifu ni kwamba hua siombi ulinzi juu ya ninachokiombea nina imani kuanzia sasa nitapata mabadiliko makubwa kwa kulifuata hilo. Mengine yote mliyonishauri nimeyapitia na nilikua nayatimiza nyakati za maombi. Mengi nimefanikiwa kwa njia ya maombi na sala niliumia sana kwa ombi hili kutojibiwa sasa ninayawekea ulinzi yale niliyokwishajibiwa yasije nayo yakaingiliwa na shetani. Pia nashukuru kwakua hata mgonjwa ninayemuombea anaendelea vizuri nahisi jaribu limeona aibu kwani miongozo mliyonipa imezidi kunyima mianya yake nina imani nitakuja kuonekana kweye ushuhuda mda mchache ujao mana itakua hakuna kona itakayoachwa wazi.

  MBARIKIWE SANA

 2. Bw. Yesu asifiwe! wapendwa, na Pole sana dada Tina. Nimesoma swali lako na ushauri uliotolewa na wapendwa. Ushauri wote ni kweli kabisa! lakini sio kwamba ushauri wote uliotolewa unakuhusu wew na tatitizo linalokupata. Hivyo inabidi upite katika kila sababu na ujichunguze kuanzia hofu, kutokuwa na imani, dhambi, kumjua mungu(elimu ya nguvu ya Mungu), mahusiano yako na Mungu kwa habari ya upendo kwa watu sadaka na Ibada kwa ujumla. ukishaona wapi umenaswa rekebisha. Mimi nakuja na sababu zifuatazo na kutoa ushauri wake. yawezekana kati ya hizi au zote ndizo zinazozuia majibu ya maombi yako.
  Naomba utambue kuwa matatizo yote aliyonayo mwanadamu aliyeokoaka au hajaokoka, yamesababishwa na kwenda kinyume na Mungu(Dhambi) ambayo huzaa laana (tatizo lilipo); iwe ni ugonjwa, umaskini, utasa, ulezi vifo kabla ya wakati, kutopata kazi, na mangine uyajuayo. Yamkini umeona watu waliookoka na wako kwenye wokovu muda mrefu na wanatenda miujiza mingi lakini bado wanasumbuliwa na matatizo niliyoyataja na mengine. Laana haimzuii mtu aliyeokoka kwenda mbinguni, bali maisha ya mtu huyo hapa duniani yanakuwa hayana uhuru. yanaambatana na mateso fulanifulani, na wakati mwingine mpendwa huyu huona kama tatizo/matatizo aliyonayo ni mapenzi ya Mungu kumbe ni minyororo ya shetani. Sisi tuliookoaka tunatakiwa kuishi maisha ya furaha na amani tukimtumikia mungu wetu hapa duniani na mwisho tukafurahie utukufu wa Mungu Baba Mbinguni. Sasa nirudi kwa Dada Tina juu ya tatizo la kuomba lakini baada ya maombi tatizo linarudi na kuwa kubwa zaidi. Hii yawezekana ni kutokana na sababu niliyoiongea hapo mwanzo, kwamba kuna laana ya ugonjwa huo inayomtesa unayemuombea, maana tabia za laana ni kwamba unaombea tatizo haliiishi kwa sababu ya mkataba wa dhambi uliofanywa kati ya binadamu na shetani, sasa kam ule mkataba haukuvunjwa kwa damu ya yesu tatizo halitaisha maana bado kibali cha kukaa kwenye himaya yake haikijabatilishwa. vivyo hivyo kwa matatizo mengine. Dada Tina na wapendwa wengine somo hili la laana ni refu na hatua za kuvunja laana ni ndefu pia nimeona niandike vile ambavyo nina uzoefu navyo na nilivyopitia katika maisha yangu ya kumtafuta Yesu. kwa bahati nzuri ni kwamba wokovu nimeupata kwa sababu ya kuwa na matatizo sugu ambayo nilihangaika nayo sana kwa muda mrefu lakini namshukuru Mungu aliyeniongoza kwanye kanisa linalofundisha KUTUBU DHAMBI na KUVUNJA LAANA kwa UNDANI, na sasa niko huru katika Nyanja zote.
  sababu ya pili ni kwamba yawezekana umeshavunja laana lakini unapata shida hiyo, hii ni kwa sabababu unapooomba unavunja ngome na kuharibu kazi za ibilisi. sasa kama hujafunga kisasi cha ibilisi dhidi ya maombi na kuharibu roho za mashambulizi baada na wakati wa maombi, na pia kufunika kwa damu ya Yesu maombi hayo, ina maana shetani atapata mpenyo wa kukushambulia na ili akumalize nguvu ataleta tatizo palepale ulipoomembea ili akuvunje imani yako.
  Lakini pia unapoona umeomba na kwa macho ya nyama unaona tatizo linashamiri ujue ushindi uko karibu(Usiwe kama petro aliyeangalia maji wakati akimfuata Yesu juu ya bahari) bali angalia uweza wa Mungu na Nguvu zake, unachotakiwa ni kukiri uponyaji au kukiri kile unachoomba. Tafuta maandiko yanayosurpport maombi yako kama vile Kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, au the common one Yoh: 14; 12-14, au Yer: 51:20-21, na mingine uijuayo inayosurpport maombi yako. lakini mwisho wa yote mpe sifa Mungu kwa kuyataja matendo makuu aliyoyafanya ya kwenye biblia na yale ambayo watu walimshuhudia au wewe mweyewe Mungu aliyokufanyia.
  Dada Tina chukua hatua muafaka.
  Mungu akubariki sana

 3. Bwana Yesu asifiwe! maombi yana nguvu,maombi hujibiwa! Majibu ya maombi huyaombayo yanaweza yakachelewa wakati mwingine ili kupima kiwango cha imani ulichonacho.Hivi Tina wewe ni nani mbele za MUNGU? JE,Unajua kuwa una haki ya kupokea kutoka kwa MUNGU? lakini vilevile unajua kuwa unaowajibu wa kufanya kabla haujamwita au kumsogelea MUNGU? Nampenda MUNGU kwa kuwa yeye ni zaidi ya mwanasheria,hutoa HAKI palipo na WAJIBU.Shughulika na IMANI yako na IMANI yako itakuponya.Ahsante.

 4. Halafu pia kumbuka ukiombewa bila kupona usimdharau huyo anayekuombea usije ukaonekana ulienda kumjaribu.
  Ila uendelee kutafuta uso wa Mungu kipitia watumishi wengine bila kumsengenya wa awali.

 5. BWANA YESU asifiwe.Nilimpigia simu rafiki yangu kumjulia hari akaniambia mke wake anaumwa kuchanganyikiwa amezunguka kwa waganga wakienyeji wengi ila bado hajapona akasema ila leo nimempeleka kwamganga mwingine nimemuacha uko.mimi nikamwambia kwanini hujampeleka kwenye maombezi akanijibu nimeisha mpeleka kwenye maombezi amekaa wiki mzima akuna muhujiza wowote ulio tendeka.mimi ndiyo nikaanza kumshauli hivi;ukiona mtu anamuombea mtu anapona ujue ujue ni msafi mungu akai sehemu ambayo anbayo ni chafu hata ukimuita kwa vuvuzera ndiyo maana kabla ya kuombewa tunatanguliza sala ya toba ili uwe safi ili mungu haanze kukutumia au kufanyia kazi maombi yako.kwahiyo unaweza ukakuta wale walio kuwa wanamuombea wiki nzima walikuwa siyo wasafi sala zao zikawa ni kelele tu.Nikamuelekeza akamtoe kwa mganga ampeleke kwenye mkutano mmoja wainjili ulikuwa arusha,akaniambia sasa kwamganga nitamtoaje na nilimpeleka jana na ela ya kumpeleka arusha sina yote nimemalizia kwa waganga.nikamwanbia ela nitakutumia na yule ni mke wako wewe ndiyo unamamlaka naeusiogope mganga.basi siku iliyo fuatia akasafili kwenda arusha alipofika siku ya kwanza akufunguka siku ya pili akafunguka sasahivi ameisha jifunza kitu fulani.KWAHIYO USIKATE TAMAA MUNGU ANACHELEWESHA MUHUJIZA WAKO ILI UJIFUNZE KITU FULANI KWAKE.UKISA KITAMBUA TUNASHUSHA UPONYAJI.DON’T GV UP

 6. Amina washiriki mliopita kunishauri na Mungu awabariki kwa michango yenu na imenisaidia kuangalia nyendo zangu na hata za mgonjwa ninayeshiriki kumuombea ukweli ni kwamba vingi nimevitekeleza hata kuna wanaoshuhudia kipindi napata shida na wanathubutu kusema nina moyo wa tofauti kupokea hayo mapito na hata nina imani ya ajabu. Kikubwa nilichojifunza toka kwenu ni kusimama na maombi , imani na sadaka, pasipo kuangalia uzito wa tatizo. NIMEFARIJIKA SANA NA USHAURI WENU.Nina mengi ambayo Mungu ameyasimamia na yamedhihirisha ukuu wake ndo mana nimeumia kwa hili moja na lingine nitafunguka nikipata majibu yake. MBARIKIWE SANA NA NINAUNGANA NA WALE WENZANGU WENYE KUHITAJI MSAAADA WA MAOMBI.

 7. Kuna jaribu na kipigo
  unaweza kusema ni jaribu kumbe bado unaudhaifu/dhambi unaopelekea upigwe sawasawa……
  Nimeshuhudia watu wengi wanaombewa lakini wakipona wanarudi kwenye mambo yao ya kidunia biblia inawaita wako uvuguvugu…………
  Hebu jiangalie vizuri juu ya IMANI, UPENDO kwa watu wote na SADAKA kamili kabisa
  halafu fanya toba ya kumaanisha kutorudia tena
  maana MUNGU siyo msanii akisema atakuponya ni AMINA.
  Ni bora kukusaidia kuliko kukutia moyo ukashangaa kuona kipigo kiko palepale
  wanaoponywa na MUNGU ni kwa rehema na matendo yao siyo maombi mengi.
  AYUBU ANASEMA MJUE SANA MUNGU UWE NA AMANI

 8. Dada Tina hakuna jambo lolote linaloweza kumshinda Mungu kikubwa unatakiwa uwe na imani na wala ucwe na shaka yoyote!ujuwe shedani ni mjanja sana so lazima akupige mkwara thn aone je umecmama?Au ndiyo tena unazuga?cku zote hofu,mashaka huwa ndiyo silaha ya shetani anayoitumia kushinda!Just ona Jesus anavyowatel wanafunzi wake Mt 17:20-21 hata Petro alitaka kuzama kwenye maji just bcoz aliona hofu Mt 14:28-33!So Tina amini Mungu anaweza lolote na wala uctie shaka hata tatizo lako liwe kubwa kiasi gani!Na mara nyingi Mungu anaruhusu tupite kwenye dhiki ili kutuonyesha kuwa kwa juhudi zetu hatuwezi bali yeye pekee ndiyo anaweza na hivyo hututaka tumtumainie yeye pekee kwa asilimia zote pasipo kuwa na hata chembe ya hofu!Hivyo dada yangu Tina amini Mungu anaweza kwa kila jambo na ucangalie ukubwa wa tatizo lako bt angalia ukuu na uweza wa Mungu wetu ktk kila jambo.Mungu akubariki na aendelee kukuongezea imani.

 9. kilichokuwa kinawagharimu wana wa israeli katika vita vyao na wafilisti hakuwa nguvu ya wafilisti wenyewe bali ni sauti iliyotolewa na jemadaria wao goliath naomba usiogope ngurumo ya kile unachofikiri hakiwezi kuondoka. when fearful, anxious thought come, remind yourself of Jesus words. “let not your heart be troubled neither nor be afraid”. Even if things appear to be worse say Lord I refuse to worry about it. I have seen the finished work on cross of Calvary. Tina asikudanganye shetani kwa kukutia hofu. naomba ukiona hali hiyo usiitazame hiyo hali bali tazama nguvu ya msalaba. kumbuka taji ya uzima umefunikwa na taji ya miiba. lakini hatuwezi kuwa na hofu juu ya miiba hata kama inachoma ushindi lazima kwa damu ya Yesu.

 10. Tatizo una hofu
  jaribu kutumia maneno machache uombapo
  halafu utumie muda mrefu kusoma biblia.
  Halafu ujichunguze mwenendo wako juu ya udhaifu.

 11. Nashukuru kwa wachangiaji mliopita, hadi nimetaka ushauri wenu ni kwamba hali imekua sio nzuri na tegemeo langu ni Mungu ninapokuta sioni njia na nimeomba ninayemuamini naumia zaidi. Imajin mwaka 2008 tukatoa na sadaka ya shukrani amani haikupita siku 3 akaumwa hadi akalazwa tena.Kiukweli nae ana imani vinginevyo angeweza kuyumba.Hali hiyo imekua ikijirudia karibu kila mwaka. Yani kama shetani ametuamulia basi kajipanga tunaomba neema ya Mungu tu ampatie uponyaji situmai kama aliumbwa kuja kuteseka.

 12. Mimi pia imenitokea hiyo natumaini hapa nitapata pia ufahamu zaidi. Nilikuwa na tatizo la muda mrefu ambalo nimeliombea sana, lakini pia nikaamua kuomba na kufunga siku 3, baada ya kumaliza tu kufunga kesho yake ndio kabisa tatizo likajidhihirisha kuliko kawaida, sikukata tamaa nikaamua tena kufunga na kuomba wiki nzima iliyofuata, siku namaliza kufunga ndio tena kabisa tatizo nililokuwa naliombea likawa baya hakuna mfano mpaka nikachanganyikiwa, na bado tatizo hilo halijaisha lakini bado naendelea kuomba kwani naamini ni nguvu za shetani tu zinajaribu kutukatisha tamaa.

  Mbarikiwe

 13. Mashaka mara nyingi huchangia hali hii, na shetani analijua hilo na kwa sababu hiyo hutumia nafasi hiyo kukuzuia kutoa uahuhuda. Vitu  vingine si vya kuomba bali ni vya kutamka tu na vinakuwa. Soma. Yohana. 14:12-14; 15:4,7. 1Yohana 5:13-14. Mpendwa, mistari hii na nyingine nyingi zinajaribu kuonesha mamlaka tuliyo nayo, tatizo la waombaji wengi hawana;1. Maarifa ya kutosha juu ya Mungu, juu ya uweza wake, juu ya haki zao wenyewe na hata juu ya uhakika wa mahusiano yao na Mungu. Hos. 4:6, Yohana. 8:312. Utii wa neno la Mungu ndani yao. Kutokuwa mtii hukutenga na Mungu na kukufanya kukosa haki mbe

 14. Mpendwa katika MUNGU hilo huwa ni jaribu tu shetani anakujaribu kukupima je unashukuru kwa dhati au laa kazana katika maombi usikate tamaa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s