Kwa njia gani mtu hujazwa na Roho Mtakatifu?

filled-with-the-spirit

Wapendwa katika Kristo, kuna kitu kinasumbua watu wengi na hata leo bado kinawasumbua. Ni njia gani (process) ambayo mtu hupitia hadi akajazwa na Roho Mtakatifu???

KARIBUNI SANA!!!

–Rev. Damasus F. Mkenda
Advertisements

39 thoughts on “Kwa njia gani mtu hujazwa na Roho Mtakatifu?

 1. SIyi,

  Unajaribu kuJIFANYA huelewi ni nini humu ndani toka mjadala huu uanze??

  Ni kweli una kiu na hamu ya dhati ya kutaka kujazwa RM hii ya kikwetu/KiBiblia/Ki Matendo ya Mitume Church au ni kupoteza muda na kuendeleza mazungumzo tu mara A kisha B halafu Z, kisha rudi A halafu cheza kati hapo C then ambaa mpaka W halafu unateremka kwa J?

  Ngoja niulize a very practical question which will make clear cut tofauti kati yako na sisi

  SWALI: Uliwahi kunijibu swali kua umeshajazwa RM- sasa, ulishawahi sikia RM akiongea ndani yako? Explain kidogo tu

  Press on

 2. Mabinza,
  Shalom mjoli.
  Uliyaelewa hayo aliyoyaleta Ziragora akijbu maswali yako? Mimi sijamwelewa. Kama wewe umemwelewa, nisaidie na mimi kunielewesha in relation to what you asked.
  Au/na kama Ziragora ataona umuhimu wa hili jambo kuwa alijibu bila ya kueleweka kwa wengine kama siyo wote, aweza kurejea kuelewesha watu akiwemo Siyi.
  Bwana awabariki sana

 3. Soma shairi hizi kwa makini, pengine zitakusaidia. Kwani kujazwa RM au la ni mapenzi ya Mungu mwenyewe wala si harakathi za mwanaadamu. Jambo lingine, kujazwa RM si kusema kwa lugha tu, hii ni sehemu ndogo sana. Sijue kabisa kam unataka ujazwe kivipi. Ukitaka ujazwe kam yule mwengine hutapata kwani una karama zako naye ana zake. Tena usijiswali mingi juu ya mwenendo wa mtu ili iwe kigezo cha kujazwa RM. Hatutasahau vile kama kuna wanaoiga, hawo hatuwazungumuzie.

  Warumi 9:

  10 Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu,

  11 (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),

  12 aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.

  13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

  14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

  15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.

  16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.

  17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.

  18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.

  19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?

  20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?

  21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?

  1 Wakorintho 13:
  1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

  2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

  3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

  Waefeso 4:

  11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

  1 Wakorintho 12:

  4.Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

  5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

  6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

  7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

  8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;

  9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;

  10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;

  11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

  12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

  13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

  14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.

  15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?

  16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?

  17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

  18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

  19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

 4. Siyi,
  Punguza kujionesha kuwa unajua kiusahihi mno kitu ambacho usahihi wake hauko nao 100%, bali unajua tu kwa sehemu.

  Kama unadhani neno lugha nyingine na lugha mpya yana muktadha tofauti, basi jua kuwa sisi tuaminio ahadi inasema tutasema kwa lugha mpya (Mark 16:17b -In my name they will drive out demons; they will speak in new tongues;)

  Na kama mitume hawakusema kwa lugha mpya kama unavyodhani, basi yafikirie sana maneno haya:

  Lugha mpya ni ahadi ya Kristo kwa waaminio, wakati Petro alikuwa angali anasema, Roho mt. aliwashukia, na wale waliokuja na Petro (wayahudi) wakashangaa kusikia wale watu (waaminio) wakisema kwa lugha kama wao (mitume na wengine) ilivyowatokea pale gorofani (Acts 10:44-45)

  Walioshukiwa hapa ni wale walio katika ahadi ya Yesu kwenye Mark 16:17 – lugha mpya, kwa hiyo hiyo ahadi ilitimia kwao. Lakini ilitimia kwa mfano wa jinsi ilivyokuwa kwa waliokuwa ghorofani siku ya Pentecoste.Lakini kwa nini hawa wanasema waliwasikia hawa mataifa wakisema kwa lugha kama wao wakati Siyi anasema kwa mitume siku ile ilikuwa ni lugha nyingine,wakati hawa ni wale waaminio ambao ahadi ya kristo inasema watasema kwa lugha mpya?

  Sasa kama wewe ni msomi mwenye hekima hukumu sasa mwenyewe kama kuna tofauti hapo kati ya lugha nyingine (waliyonena mitume), na lugha mpya (ambayo ni ahadi kwa waaminio)

  Nilijua tu pia kwamba kwa mind- set ya wasabato hata mtu anayejifunza/soma lugha fulani akaeielewa, eg Kifaransa, Kichina, Kiingereza, Kisukuma, Kisambaa, n.k
  akisimama na kuanza kuongea hiyo lugha, akisimama kanisani na kuanza kuongea hiyo lugha huko nako ninyi mnaita kunena kwa Lugha.

  Na bila shaka ulitaka kuniambia kuwa Paul aliposema ananena kwa lugha kuliko wao wote, alisema hivyo akimaanisha kunena kwa lugha zile alizokuwa akizifahamu kama Kiebrania, Kirumi, Kigiriki, Kiaramaiki, nk, maana Paul alikuwa ‘multilingual’.

  Pole Siyi, kama ndo hivyo, maana hujui maana ya kunena kwa lugha, na wala hiyo unayonenaga huko usabatoni kama ni lugha uliyojifunza ukaielewa, siyo kunena kwa lugha kunakosemwa kwenye biblia!

  Unaweza ukaamua kuendelea kujifariji!!

 5. Wapendwa,

  Nimeifurahia michango yenu yote . Kusema kweli .ni mizuri na inavutia kuendelea Kuisoma naomba kujua hasa yafuatayo ili kuufikia mkutadha wa swali la muulizaji!

  Nauliza hivi :-

  1. Kujazwa roho mtakatifu ndiyo Kuwa na Roho mtakatifu?

  2. Kama siyo tofauti yake .ni nini?

  Mtu yeyote anaweza kunijibu .

  “Ufahamu .ni chembe ya uhai !”

 6. Sungura,
  Ubarikiwe kwa kuniijia tena.
  Nami sina budi kukufuatilia umeniambia nini!
  Ukisema kuwa nilikuwa na mapepo, huenda ni kweli. Maana kila tu tunapoanza kusali, baada ya muda, nilikuwa sielewi kinachoendelea japo mwili wangu ulikuwa kwenye movement na midomo yangu ikiendelea kutamka maneno. Shida ilikuwa ni kujua kuwa nilikuwa naongea nini! Ukisema kuwa nilikuwa na mapepo, kwa kweli siwezi kukubishia. Aidha, hata hayo mapepo niliyokuwa nayo, naona yalikuwepo kwa waumini wenzangu pia na mchungaji wangu. Maana niliwasimulia hali hiyo wakanitia moyo tu kuwa huko ndiko kunena kwa lugha mpya haswaa!! Maana hata wao walinieleza kunena kwao kwa lugha ambako hakukuwa tofauti na hali iliyokuwa inanipata mimi. Kwa hiyo ukisema kuwa Siyi nilikuwa na mapepo kwa wakati huo, siwezi kukubishia kabisa, na nina imani wenzangu niliowaacha huko, bado wako kwenye mapepo hayo!! Kwa hiyo ninakubaliana na wewe kabisa kuwa, madhehebu ya kipentekoste, ni full mapepo tu, japo wanaamini kuwa wananena kwa lugha mpya. Hiyo siyo lugha mpya.
  Ukisema kuwa sijui maana ya lugha mpya, sidhani kama uko sahihi. Maana nina uzoefu wote wa haya ninayoyazungumza. Na kama ingekuwa ni CV, ya kwangu ingekuwa inalipa zaidi kuliko ya kwako wewe unayesema siijui lugha mpya!! Anyway, ngoja tuangalie maana ya lugha mpya ni nini!!
  Kwanza, naomba ukumbuke kuwa, ahadi ya Kristo kwa wanafunzi wake kabla hajaenda mbinguni, haikuwa kunena kwa lugha mpya. Kunena kwa lugha ni matokeo ya hicho walichokipokea – RM (yaani nguvu itokayo juu kwa ajili ya utume). Lengo kuu la RM lilikuwa ni uinjilisti –utume. Utume huo ulijengwa kwenye kitu kinachooitwa upendo. Kwa maneno mengine, huu ulikuwa ni ubatizo wa RM – mdo 2:1-4.
  Jambo la kuzingatia hapa, ni kwamba, mitume hawakuongea LUGHA MPYA baada ya kujazwa na RM! Biblia inasema waliongea lugha nyingine. Ushahidi wa maandiko mdo 2:4;
  KJV; And they were all filled with the Holy Ghost, and began to speak with other tongues, as the Spirit gave them utterance.
  NIV; All of them were filled with the Holy Spirit and began to speak in other tongues as the Spirit enabled them.
  AKJV; And they were all filled with the Holy Ghost, and began to speak with other tongues, as the Spirit gave them utterance.
  RSV; And they were all filled with the Holy Spirit and began to speak in other tongues, as the Spirit gave them utterance.
  SUV; Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka
  Binafsi mimi ni mpenzi sana wa KJV au AKJV kuliko matoleo mengine ya Biblia. Lakini nimekuletea ili usome ujiridhishe kwanza juu ya hili. Kimsingi, mitume waliongea lugha zilizokuwa kieleweka kwa watu-lugha nyingine. Hazikuwa lugha mpya. Walijifunza lini lugha hizo, maana hawakuwa wazawa wa lugha hizo? Hilo linabaki kuwa la kimiujiza tu. Kwa hiyo, siyo sahihi kusema kuwa mitume walinena kwa lugha mpya. Hao walionena kwa lugha nyingine tu. Ni akina nani wanaonena kwa lugha mpya? Tuendelee mbele , tutawaona tu, bt not now.
  Hivyo, kwa mujibu wa aya hii ya mdo 2:4, ninachotaka ukione ni hiki, hakuna ushahidi wowote kuwa walijifunza saa ngapi. Inaonekana walipewa uwezo tu kwa njia ya RM. Walisema kwa lugha nyingine. Biblia haisemi kuwa lugha nyingine walizoongea, hawakuwa wanazifahamu. Ila wale waliosikia, walielewa kilichokuwa kikisemwa. Jambo la kujiuliza, ni kwanamna gani waliongea lugha za kueleweka kama wao hawakuzielewa? Nina imani kama Mungu aliwapa uwezo wa kuongea lugha hizo bila kujifunza, nina imani pia kuwa, aliwapa na uwezo wa kuzielewa, ndiyo maana waliongea kwa kupangilia sentensi hadi mataifa wakawaelewa walikuwa wanasema nini. Nasema hivyo kwa sababu, kwa Mungu hutoka vitu kamili. Kwa maana “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka”- Yakobo 1:17. Kwa hiyo, kusema kuwa mitume hawakuzifahamu lugha hizo nyingine, siyo sahihi. Tuna imani kuwa walizielewa ndiyo maana hata hao mataifa walielewa kilichozungumzwa na mitume. NB: kumbuka kuwa hawakuwa mitume peke yao –yaani 11 tu, bali walikuwepo na waumini wengine wengi amabo idadi yao ilikuwa kubwa sana japo inasemekana ilikuwa ni 120+). Hawa wote kila mmoja aliongea kwa lugha nyingine…

  Halafu, binafsi sijapata hata aya moja ndani ya maandiko ya Biblia, inayosema kuwa, mtu anaweza kunena kwa lugha nyingine yeye mwenyewe ktk kusali, tena anene kwa sauti hadi watu wengine wamsikie, wasimwelewe na hata na yeye mwombaji asielewe akiombacho. Nioneshe hiyo aya kama unayo nami nijifunze kwayo. Katika 1Cor 14: 27 na 1Cor 14:18 -18I-19, ulichokisema hapa kiko tofauti sana na hicho ulichokisema kaka. Wewe umesema habari za kusali kunavyohusiana na kunena kwa lugha. Lakini aya hizi, zinaongelea habari za kujengwa kwa kanisa through speaking in tongues. Ukisoma historia ya Wakoritho na Wagiriki jinsi walivyokuwa wakinena kwa lugha zao – Kigiriki na kilatini, utaelewa Paulo alichokimaanisha hapo. Sasa, hivi naona unababatiza tu.

  Kwa taarifa yako, wasabato tunanena sana kwa lugha. Huelewi tu rafiki. Huwezi kuelewa maana huwa mnafundishwa negativities tu towards wasabato. Ndiyo maana kuna mambo mengine ambayo mmemezeshwa nanyi mmeyameza vivyo hivyo bila ya kuyafanyia uchunguzi wa kina. Na bila haya, huwa mnakurupuka kusema kuwa tu ooh, wasabato mko vile, kumbe sivyo. Mara Ellen g. White alitabiri uongo, kumbe sivyo. Cha ajabu zaidi, walimu wenu hao, hawaujui usababto, watawezaje kuwafundisheni habari za usababto nanyi mkasadiki enyi watu wazima na akili zenu nzuri? Nafahamu sana sumu mnazopewaga na walimu kuhusu wasabato. Tena walimu wengine hudiriki kabisa kuwaambia waumini, “msiwasikilize wasabato”. Why ufyate mkia kama mtu unajiamini na hicho unachokiamini/imani? Wasabato tunanena sana tena kwa namna tatu. Ninyi mnayo aina moja ambayo nayo si ya kibiblia. Sijui mliitoa wapi!!

  Huku kunena kifaransa na kiingereza, ni aina mojawapo tu ya kunena kwa lugha. Zipo nyingine mbili zaidi. Nitakuletea kwa kina baadaye hizo aina za kunena kwa lugha. Nitakuelezea na habari za Paulo za kunena kwa lugha zaidi ya wengine, alimaanisha nini!! Wewe kaa mkao mzuri tu. Karibu kwenye usababto upate uzoefu mpya. Hutabaki mkavu kama ulivyo sasa.
  Barikiwa.

 7. Thnx Sungura kwa maswali mazuri kwa Siyi na kwa namna ulivyomtel ukweli!Anywa naendelea kula shule.

 8. Ooh, Asante mjoli Lily,
  Ubarikiwe ndg yangu. Kimsingi ulichokiandika kilikuwa so tangible sana ndiyo maana kwa kila aliyekisoma kwa jicho la rohoni, alipata kitu. Ubarikiwe na Bwana. Songa mbele kusema tu unapovuviwa ili kuimarishana kiimani.

 9. Nashukuru wachangiaji wote waliopita. Kimsingi mimi binafsi napenda tujengane kwa mafundisho na uzoefu wetu na hatimaye mwili wa Kristo uwe imara. Siandikia ujumbe kwa mtu fulani. Mbarikiwe

 10. Asante Siyi.

  Pole kwa yaliyokupata.

  Nilichogundua ni kitu kimoja kuwa, inawezekana kabisa ulikuwa na mapepo ndani yako ambayo hayakukuacha uendelee na imani ya kipentecoste. Kwa hiyo ulikuwa ukienda mahali ambapo kuna moto wa Roho mt. yalikuwa yanapata shida.

  Na ulipoamua kuwa msabato yalitulia kwa sababu yalipelekwa mahali ambapo hayawezi pata shida. Nakunukuu;
  ” Inakuwa ni vigumu sana kusema kusema kuwa nilikuwa nanena kwa lugha mpya kwa maana hata sijui nilichokuwa nakiongea. Ilikuwa ni kama namna fulani ya kuzirai na baadaye kupata fahamu hivi” Hizi ni dalili za mtu mwenye mapepo.

  Siyi unajua hata sasa hujui maana ya kunena kwa lugaha mpya japo wewe unadhani unajua.
  Kwa nini inaitwa lugha mpya? ni kwa sababu wewe unayenena huijui hiyo lugha.
  Lakini wewe ona unachokisema hapa kuhusu lugha unayonena huko kwenye usabato.
  ”Ya pili, nilinena na bado naendelea kunena kwa lugha mpya sana. Naelewa ninachokinena kwa Mungu wangu” Hii si kweli, kama unaielewa hiyo lugha basi si lugha mpya hiyo.

  Hata ile siku ya pentekoste wale waliojazwa walisema kwa lugha ambazo wao walikuwa hawazielewi, ispokuwa wale waliowasikia walishangaa kuwasikia wanaongea lugha zao( yaani zao wale wasikiaji) wakti waliwajua kabisa kuwa hawazijui(wanenaji) hizo lugha (Matendo 2:6-7)

  Halafu suala la kufasiri, si pale mtu anaponena kwa lugha wakati akiwa anasali peke yake, bali ni pale anapokuwa ananena akiwa anasali na wengine (kusanyiko).

  Ona biblia inavyosema -1Cor 14: 27 – If anyone speaks in a tongue, two—or at the most three—should speak, one at a time, and someone must interpret.

  Ona Paul,anavyosema hapa; 1Cor 14:18 -18I thank God, I speak in tongues more than you all; 19however, in the church I desire to speak five words with my mind so that I may instruct others also, rather than ten thousand words in a tongue.…”

  Kwa hiyo Siyi ulipojaribu upentekoste hukuwahi kunena kwa lugha mpya, na hata sasa huneni kwa lugha mpya huko kwenye usabato. Wala usijifariji.

  Tangu lini kwanza wasababto wameanza kuamini katika kunena kwa lugha wakati siku zote wamekuwa wakisema kuwa hiyo ilikomea kwa mitume!!!?

  Au unadhani pale anapokuja mhubiri anaongea kifaransa au kiingereza au kireno na mwingine anatafsiri kiswahili ndio kunena kwa lugha mpya nini?

  NB: Niambie zile aina tatu za kunena kwa lugha, na tofauti ya kunena kwa lugha kwa mitume na kule unakonena wewe tafadhali!

  Asante.

 11. Sungura,
  Nashukuru rafiki kwa vile umebarikiwa/vutiwa na ushuhuda wangu. Kimsingi, nilianza zamani sana kumtafuta Mungu kwa moyo wangu wote. Yaliyonitokea naweza kuandika kitabu kizima cha ushuhuda tu. Namshukuru Mungu kwa leo kwa kunifanya msabato. Na ninaomba nisiwe msabato jina tu. Niwe msabato halisi anayeenenda sawasawa na Biblia. Maana kwa kuwa msabato tu, haitoshi chochote kunifanya niokolewe siku ya mwisho, bali natakiwa kuwa msabato anayeliishi neno. Hili ndilo jukumu zito, lahitaji maombi sana na kujikana nafsi(kubeba msalaba) maana majaribu ni mengi sana na shetani hajalala/fa.
  Naomba nijibu maswali yako kwa ufupi sasa;

  Swali
  1. Kwa hiyo kuna Roho mt uliyejazwa wakati ukiwa umeokoka, na mwingine ukajazwa ulipokuwa msabato?
  Jibu
  Ndiyo na baada ya kuwa msabato, nimejazwa RM mwingine pia
  Swali
  2. Tofauti ni nini kati ya hizo jazo mbili Siyi?
  jibu
  Ujazo wa kwanza, nilikuwa nazirai tu na kupoteza network hata sikujua kilichokuwa kikiendelea wakati wa maombi. Nilikuwa sawa na yule aliyepagawa mapepo tu. Hata mtu akiniuliza kuwa nilikuwa naomba nini, nisingeweza kumweleza. Na kwa sababu ya imani hiyo, nilikuwa najisikia burudani tu. Sikuelewa maana ya lugha, sikuelewa maana halisi ya kunena kwa lugha, sikuelewa kutofautisha kunena kwa lugha kulikofanywa na mitume na huku ninakokufanya mimi. Nilikuja kuelewa vizuri baada ya kusoma vizuri Biblia na kisha kulinganisha na alpha course (meditation courses) zilizokuwa zinazofundishwa kwa waumini wakati wa kupokea RM. Hii ni mojawapo ya sababu ilinifanya nichomoke huko.
  Ujazo huu wa pili, nilipata hamasa kubwa sana ya kujifunza neno mimi binafsi na kuwashuhudia wengine. Kila saa nilikuwa na kiu ya kusoma neno japo mara nyingine mazingira hayakuniruhusu kufanya hivyo. Nilielewa maana ya kunena kwa lugha kuwa kumegawanyika katika aina tatu ndani ya Biblia. Na miongoni mwa aina zote hizo, hakuna hata aina mojawapo niliyokuwa naipractise huko mwanzo. Sasa hivi niko huru sana ndani ya Kristo aliye Bwana wa Sabato. Nami nazidi kujitahidi kufanana naye kila kukicha.

  3. Na je katika hizo jazo mbili zote ulinena kwa lugha mpya?
  Jibu
  Ya ya kwanza hata sijui kama nilikuwa nanena kwa lugha mpya, maana sikuwa na ufahamu wakati huo. Mwanzoni nilikuwa naongea maneno yanayoeleweka ya kiswahili kwa kuyarudirudia, lakini baada ya muda fulani, sikuwa naelewa kilichokuwa kikiendelea. Inakuwa ni vigumu sana kusema kusema kuwa nilikuwa nanena kwa lugha mpya kwa maana hata sijui nilichokuwa nakiongea. Ilikuwa ni kama namna fulani ya kuzirai na baadaye kupata fahamu hivi. Hii ilikuwa ikinitokea kwa sababu nilikuwa najiachia sana.
  Ya pili, nilinena na bado naendelea kunena kwa lugha mpya sana. Naelewa ninachokinena kwa Mungu wangu. Hata mtu anaponena kwa lugha nisiyoijua, watu wanaoifahamu lugha lugha hunitafsiria nikaelewa tofauti na ilivyokuwa huko mwanzo. Maana mtu alikuwa akiinuka na kuanza kutafsiri hata lugha asiyoifahamu kwa kisingizio kuwa ana karama ya kutafsiri. Hivyo jamaa alikuwa anatuburuza tu kwa kusema interests zake mwenyewe. Na kwa sababu waumini wanamwamini sana mtu huyo, nao husema amina, amina kumbe ni ulghai mtupu!
  Bwana akubariki sana.

 12. Nzali,
  Ubarikwe na Bwana.
  Sisi tuendelee na mjadala wetu ndg yangu. Ninavyomfahamu Seleli, ana lake jambo. Wewe subiri. Utaona tu. Huwa hariziki na majibu hasa akikujua kuwa wewe uko kinyume naye kiimani. Tena anadai huwa hajifunzi chochote kwa watu kama hao.
  Mara nyingine maswali yake mimi huwa najibu kumwangalia tu anavyotunisha misuli mwanaume yule. YAelekea kwao ni first au last born. Watoto ambao ni mafirst born, hujulikana tu vituko. Ni vizuri kumchukulia alivyo pia. Maana huo ndio ukristo

 13. Ohhhh,
  Kumbe Siyi uliwahi kuokoka halafu ukachepukia upande mwingine!!!!!

  Kwa hiyo kuna Roho mt uliyejazwa wakati ukiwa umeokoka, na mwingine ukajazwa ulipokuwa msabato?

  Tofauti ni nini kati ya hizo jazo mbili Siyi?

  Na je katika hizo jazo mbili zote ulinena kwa lugha mpya?

  Ushuhuda wako umenivutia.

  Thanks!

 14. SORRY Brother Seleli,

  Unajua Nzali na Nzala vinataka kufanana.. Nimepitia kwa haraka Mchango wako Nikadhani maswali yananihusu mimi, kumbe umeyaelekeza SOUTH – WEST kwa Nzala Siyi… Ngoja nimwachie uwanja rafiki yangu..!

  Nzali Daniel.

 15. Kumbe Majina yetu yanashabihiana Sikujua kama N = Nzala, Brother SELELI umenifungua hapo.

  Bwana M.J.Nzala binafsi pia nimefurahishwa na changamoto ya maswali yako ndio maana mpaka sasa nimetulia nikiyavutia kasi ya kuyajibu maswali yako mengine.

  Dada LILY binafsi nimefurahishwa na ushuhuda wako, umeelezea Experience uliyokutana nayo. Kibinafsi sidhani kama umeniandikia mimi Nzali au Nzala kama alivyohoji Rafiki yangu M.J.N Siyi, but najua huo ni ushuhuda wa Maisha yako binafsi ambao mtu yeyoye anaweza kupata kiu ya kukitafuta hicho ulichokipokea baada ya kuupitia ushuhuda huo.

  BROTHER SELELI, Maswali yako huwa naogopa kukurupuka kuyajibu, maana najua yatafuatia mengine ”10” times ya mwanzoni.. Nivutie subira pia.

  Nzali Daniel.

 16. Seleli
  Ha ha ha !! Umeanza ukorofi wa kiinjilisti!! Ha ha ha !! Ngoja nijibu maswali yako.
  Majibu ya Siyi kwa Maswali ya Seleli
  (a) Umeshajazwa RM? Lini?
  Jibu
  Ndiyo. Nilijazwa baada ya muda mrefu kupita nikiwa ndani ya Kanisa. Kwa sasa nina muda mrefu tu tangu nijazwe RM.
  (b) Ulijazwa kabla au baada ya kuokoka-tehe?
  Jibu
  Nilijazwa baada ya kumwamini Yesu tena nikakaa ndani ya kanisa kwa muda mrefu tu.
  (c) Ilikuaje ulipojazwa(toa shuhuda fupi tu kama 1 para)
  Jibu
  Nilipojazwa, niligundua utofauti mkubwa sana ktk maisha yangu ya kiroho. Na niligundua tofauti kubwa kati ya kipindi nilipojazwa RM nikiwa kwenye ulokole na hii niliyojazwa RM nikiwa huku niliko sasa (usabato)
  (d) Unapo omba waga unajisikiaje/kunatokea nini?(eleza kidogo tu your experience)
  Jibu
  Mara zote tangu nijazwe RM, wakati wa kuomba huwa najisikia mambo mengi sana. Ngoja nikutajie machache
  i. nguvu ya kuendelea kuomba tu
  ii. sauti ya Mungu ambayo hunena nami rohoni kwa njia ya mafunuo
  iii. Maumivu makali juu ya mabaya niliyoyatenda/waza na hayo yanayotendwa na watu wengine na mara nyingine machozi ya ng’ombe hunitoka.
  iv. Nguvu mpya ambayo huniijia na agh. kupiga hatua ya kiimani.
  v. Daima huwa nasali kwa roho na akili pia. Huwa sipotezi network.
  vi. Nahisi amani sana moyoni baada ya kuomba nk

  (e) Ulishawahi/hua unasikia sauti ya RM? Ikoje? Elezea kidogo tu
  Jibu
  Huwa naisikia sana. Ngoja nikupe mfano ili uniielewe vizuri.
  Kwa mfano, kwa sababu huwa naomba mara nyingi kwa kunukuu mistari ya Biblia, huwa namsikia Mungu kwa njia ya RM akisema ndiyo. i.e.
  Mathalani, ninapodai ahadi za Mungu, huwa namuuliza Mungu maswali juu ya hicho alichokiahidi!! Baada ya kunukuu tu, huwa namsikia Mungu akisema, ‘ndiyo niliahidi’… nk

 17. Lily
  Nashukuru sana mtumishi wa Mungu. Nashawishika kusema kuwa wewe ni msichana/mwanamke. Binafsi nimefurahi kukuona umechomoza kusema kitu kilichojaa ushuhuda kuntu. Bado naendelea kukagua maswali yangu ya huko nyuma ili nijue kama ulikuwa unaniandikia mimi Siyi au rafiki yangu Nzali.
  Barikiwa sana mjoli

 18. Nzali,
  Nimefurahi sana rafiki kwa jibu lako kwa maswali yangu niliyokuuliza siku ile. Nabarikiwa na michango yako mizuri kaka.
  Ninasubiri hayo majibu ya maswali yangu mengine ili nijifunze zaidi kutoka kwako. Bwana akubariki sana ndg yangu.

 19. Nzali D na Nzala Siyi,

  Hongereni kwa debate/lecture na majina yenu matamu kuyaona na kuyatamka. Look/feel this flavor Nzali/Nzala..wow! nice, is it nt?

  Nafuatilia kwa makini flow zenu na naona kitu hiki, Ninyi ni mapacha mshazari, huyu Nzala- Ni wa South-West and huyu Nzali ni wa North-East, asomaye na afahamu

  Maswali kwa Nzala Siyi

  (a) Umeshajazwa RM? Lini?

  (b) Ulijazwa kabla au baada ya kuokoka-tehe?

  (c) Ilikuaje ulipojazwa(toa shuhuda fupi tu kama 1 para)

  (d) Unapo omba waga unajisikiaje/kunatokea nini?(eleza kidogo tu your experience)

  (e) Ulishawahi/hua unasikia sauti ya RM? Ikoje? Elezea kidogo tu

  Nangoja kwa hamu majibu yako Nzala, nitakusaidia kukumbusha ukisahau maana najua uko buzy na huduma za kuwahubiria Watu waokoke haraka kwanza kabla ya kufa hapa duniani , so relax… usijali, nitakukumbusha tu.

  Press on

 20. Sina uhakika km nimelielewaa swali vizuri lakini nitaeleza uzoefu wangu binafsi. Unapoamua kuacha dhambi zote na kumpokea Yesu (Kuokoka) utatu mtakatifu wa Mungu huja moyoni mwako ikiwa na maana RM unaye tayari moyoni mwako (Yoh 14:23). Huo unakua ni mwanzo wa maisha mapya ndani ya Yesu na mwamini hukua ktk Ukristo wake na neema ya Mungu huongezeka ktk maisha ya muamini huyu kupitia kuomba, kusoma neno, fellowship nk nk. Unapokua ukiendelea ktk kufanya mapenzi ya Mungu RM hupenda kujidhirisha na njia moja wapo ni kunena kwa lugha (wengine huita kujazwa RM). Kuna mafundisho mengi lakini nijuavyo mimi ni kwamba kunena kwa lugha ni ishara mojawapo tu ya RM na nimesikia shuhuda nyingi wengine waliwekewa mikono baada ya kutamani huo udhihilisho na wakanena kwa lugha (Mdo 19:1-6). Wengine walijikuta wakinena tu bila hata kuwekewa mikono. Binafsi baada ya kuokoka nilitamani sana kunena kwa lugha (kutokana na faida zake nyingi) nikawa naomba na kufunga sana na ilichukkua muda km 2 yrs hivi, siku moja tukiwa kwenye kikundi cha maombi nikawaeleza naomba mniombee na mimi nipate huu udhihilisho. Nilipoombewa kwa kuwekewa mikono haikuchukua muda nikaanza ongea lugha nyingine kabisa mpaka leo. Mungu hana mipaka na huweza jidhihilisha kwa mtu (ikiwamo udhihilisho wa RM wa kunena kwa lugha mpya) kwa njia apendayo yeye tusipomuwekea mipaka

 21. Ndugu M.J.N,Siyi,

  Mungu akubariki nawe pia kwa lugha nzuri ya Kiinjilisti uliyoitumia.

  Umeuliza kuwa ninapokuwa kwenye maombi mara nyingi ninakuwa usingizini!!!!!
  Sijawa na maana hiyo Ndugu yangu.. Mimi ni Mkristo na maombi ndio silaha yangu. Muda wowote naweza kuamua kuomba kadri nitakavyosikia msukumo Rohoni.. Nilichokuwa nasema ni kwamba mwanzoni kabisa wa maisha yangu ya Wokovu nilikuwa nikiamini mtu unapozaliwa mara ya pili ni lazima Unene kwa Lugha ili kupata uhakika kuwa umejazwa na Roho Mtakatifu (Rejea Mchango wangu wa kwanza) . Lakini naweza kusema kwa upande wangu nimemuona Roho Mtakatifu akitenda kazi katika maisha yangu,pamoja na kwamba sijawahi ku experience kunena kwa Lugha kama nilivyokuwa nikifikiria awali, nikiwa katika maombi na nimekuwa na amani katika maisha yangu, ila kama nilivyokueleza mwanzo, nimeshawahi kuexperience kama 2 times kujikuta nikiomba kwa Lugha nisiyoielewa wakati nikiwa nimelala (Narudia tena kusema kuwa siwezi nikaelezea hali hiyo). Wakati nikiwa mdogo hali kama hiyo ilikuwa inanitokea na nilikuwa najikuta nikiomba kwa Lugha ya kiswahili pasipo kupenda mwenyewe katika mazingira ambayo siwezi kukuelezea pia. Na ninaamini ni kazi ya Roho Mtakatifu mwenyewe. Na katika mazingira hayo niliyopitia yanawezekana, ninaamini kabisa Roho Mtakatifu anaweza kumsaidia mtu kuombea hitaji fulani ambalo hukujipanga kufanya hivyo kibinafsi.

  Maswali mengine uliyoyauliza nitarudi kuyajibu Ndugu M.J.N Siyi.

  Ubarikiwe!

  Nzali Daniel.

 22. Ninawaomba wanaoweza kutusaidia watuelimishe juu ya swali alilouliza Kaka NZALI hapo chini wengi tunasubiri majibu.

 23. Daniel
  Umenibariki sana kwa majibu yako yenye lugha nzuri ya kiinjilisti. Naomba niendelee kukudodosa kwa lengo la kutaka kujua zaidi.
  Jibu lako la swali la kwanza, umesema kuwa, unapokuwa kwenye maombi, mara nyingi huwa uko usingizini. Huwa unajuaje kuwa unaomba kama hata maneno ambayo huwa unayatamka huyaelewi? Kwa vile umesema kuwa huwa unaloose conscious wakati wa maombi, unajuaje wakati wa kuamka (baada ya kuwa conscious) kuwa ulikuwa kwenye maombi wakati ukiwa usingizin?
  Jibu la swali la pili. Umesema kuwa maneno hayo huwa huyaelewi! Na ukasema kuwa si lazima mimi Siyi ninapoongea na wewe Daniel kilugha cha huko kwetu, mtu mwingine aelewe tunaongea nini kwa vile ni lugha yetu na sisi tunaielewa! Huo nao ni ukweli mtupu. Lakin hoja ya kuangalia ndugu yangu Daniel ni hii, mbali na huyo anayesikia, wewe unaweza kuzungumza lugha ambayo huifahamu? Ukitaka kusema au kuomba kitu, utasemaje ilhali huijui lugha hiyo? Waweza kunipatia na mimi mistari hiyo ya Biblia inayoelezea unenaji wa lugha kama huo wa kwako au mwingine unaofanana na huo?
  Na kwa mujibu wa aya hii, naomba unifahamishe vizuri. “1 Waorintho 14:2 – ‘Maana anenaye kwa Lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu,maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya Siri katika Roho yake”.
  a. Kama mnenaji na Mungu ndio ambao husemezana, wewe unayesemezana na Mungu umesema kuwa lugha (maneno) huwa huielewi, je huwa unawezaje kusemezana na Mungu kwa lugha usiyoifahamu? Na je, Mungu ndio huijua lugha hiyo usiyoifahamu wewe?
  b. Kwa tafsiri ya roho ya mwanadamu, niijuavyo nini ni “pumzi ya uhai” au “akili/ufahamu”. Kwa mujibu wa aya hiyo, Je, ni kipi kati ya hivi viwili mtu huvitumia kuzungumza na Mungu kwa lugha isiyoeleweka?
  c. Kama lugha ya anenaye kwa lugha huwa haisikiki kwa wengine, isipokuwa ni kwa hao wanenaji tu tena rohoni, je, wanachokifanya leo watu kutamka maneno yanayosikika kwa watu japo hayaeleweki, huwa wanakosea namna ya kunena kwa lugha?
  Jibu la tatu, umesema kuwa, huwezi kutofautisha kati ya kunena kwa lugha kuliko halisi na kusiko halisi. Umejibu vyema. Wewe umesema huwa unanena ukiwa usingizini, nina imaani wengine hunena wakiwa kanisani, nyumbani nk na wengine hupata maelekezo ya jinsi ya kunena kwa lugha, je, wewe kwa uelewa wako wa maandiko, ni namna ipi kati ya hizi ziko sanjari na neno la Mungu?
  Nitafurahi kukuona tena.

 24. …Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba akiwaambia watu wamwamini yeye atakaye kuja nyuma yake yani Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.NA PAULO ALIPOKWISHA KUWEKA MIKONO YAKE JUU YAO, RM AKAJA JUU YAO.. Mdo 19.

 25. Mada ni Kujazwa Roho Mtakatifu. Swala la Kunena kwa Lugha limeingilia tu kutokana maswali ya mchangiaji na michango iliyopita.. Ingawa pia kunena kwa Lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu so inawezekana viende sambamba.

 26. Mimi nina swali. Kunena kwa Lugha ndiyo kujaa Roho Mtakatifu? Na kama hapana hapa mada inazungumza kuhusu kunena kwa Lugha ama kujazwa Roho Mtakatifu?

 27. Ndugu MJN,Siyi.

  Nakushukuru kwa kupitia mchango wangu na ninapenda nikujibu maswali yako uliyoniuliza kama ifuatavyo;-
  1.) Umeuliza kuwa kama nilipokuwa niki experience kenena huko kwa Lugha nilikuwa ninakielewa ninachokiongea au kama wanaonizunguka walikuwa wakinielewa.
  JIBU: Kama nilivyosema awali kuwa sijawahi experience hali hiyo nikiwa katika maombi ya kawaida na sielewi kwa nini, But mara chache hali hii imenitokea nikiwa nimelala (Ofcourse siwezi kuielezea vizuri hali hiyo) Lakini nachoweza kusema nikwamba nikiwa katika hali hiyo huwa najikuta nikiomba kwa maneno ambayo siyaelewi na hata inapofikia nimeamka usingizini huwa najikuta bado nikiwa katika hali ya mazingira ya kuwa katika maombi na huwa najisikia amani kubwa Moyoni mwangu.Zaidi ya hapo siwezi kueleza zaidi..

  2.) Umeuliza kama huwa naelewa maana ya Maneno hayo yanayotoka wakati nikiomba, jibu ni HAPANA,huwa sielewewi.. Na sijafuatilia zaidi because huwa inanitokea kwa nadra sana. Kuhusu Maana halisi ya Lugha,nakubaliana na wewe kuwa ni sharti ilete maana ili iweze kuitwa Lugha.Lakini kwa upande mwingine mimi nionavyo ili maana ya Lugha iwepo si lazima Mlengwa wa ujumbe uliyopo katika lugha hiyo awepo na aielewe Lugha hiyo? Ikitokea kwa mfano Ndugu MJN Siyi umenikuta nipo na ndugu yangu tunaongea Lugha yetu na wewe huielewi,utanilazimisha kukuelewesha ili uitambue kuwa ni Lugha? Na hata kama hutailewa ninachokiongea si itabakia kuwa ni Lugha tu? Pamoja na kwamba kwa upande wangu sina experience kubwa ya kunena kwa Lugha lakini ninaamini mtu anaweza kunena kwa Lugha hata kama haielewi Lugha hiyo kutokana na baadhi ya vifungu vilivyopo katika Biblia..

  1 Waorintho 14:2 – ‘Maana anenaye kwa Lugha hasemi na watu,bali husema na Mungu,maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya Siri katika Roho yake.

  Ninaamini kazi mojawapo ya Roho mtakatifu ni kutuombea, kwa hiyo hata kama mtu atanena kwa Lugha asiyoielewa lakini nina uhakika Matunda ya maombi hayo yataonekana tu katika uhalisia.. Lakini pia ninaamini hili somo la Roho mtakatifu ni pana, na pia kuna kunena kwa lugha kwa namna nyingi. Lugha nyingine zinakuja zikiwa na ujumbe kwa ajili ya kuwafikishia watu wengine,hapo sasa inahitajika karama ya kufasiri..

  3.) Kwamba ninajuaje kama kunena kwangu kwa Lugha ni halisi wakati sijajua kutofautisha kunena kwa lugha kuliko halisi na ambako si halisi?

  Nafikiri swali hili limetokana na swali ambalo nimeuliza mwishoni wa mchango wangu..Labda tu nirudie tena ya kuwa sijawa na experience kubwa sana ya kunena kwa Lugha zaidi ya mara chache niliyo experience hapo juu labda nafikiri ndio maana nimejikuta nauliza swali la namna hii. Swali hilo limenijia kutokana na uzoefu ambao nimekuwa nikiuona Makanisani.. Maana najua kabisa kunena kwa Lugha ni kitu kinakuja bila kukitegemea kwa kuongozwa na Roho wa Mungu mwenyewe.. Sasa inakuwaje watu wengi pale anapojisikia tu kunena kwa Lugha basi utakuta ameanza kunena kana kwamba mtu huyo ndiye controller wa hiyo experience..Na mara nyingine unakuta Mtumishi anahamasisha kabisa watu waanze kunena kwa Lugha,inakuwaje hapo? Na ndio maana nikauliza pia Mienendo mingine ya watu mbona haiendani na Utakatifu wa huyo Roho ambaye akikujaa ndio Anafurika na kuanza kunena kwa Lugha?

  Ubarikiwe na Bwana MJN Siyi.

  – Nzali Daniel –

 28. John Rwezaura,

  Ukweli ni kwamba ulichokionesha hapo ndio mchakato (process) wenyewe.
  Kwa hiyo unaposema kuwa hakuna mchakato na huku umeshataja hizo hatua, inatuchanganya kujua msimamo wako.
  Asante!

 29. Rev. Mkenda, asante sana kwa umakini katika kusoma taarifa. PROCESS ni mechanism ambayo inafuata mfumo wa kiakili ambao mtu yeyote akiufuata anapata majibu au anafikia conclusion au solution ya jambo fulani. Kama ni hivyo basi watu wote tunaowaona makanisani kwa kufuata mambo hayo kiakili wangekuwa wamejazwa ROHO MTAKATIFU. Wala siyo suala la matumizi ya lugha kama ulivyopendekeza. La hasha.

  Kama unajua Sheria ya PROCESS, ni mfumo unaolazimisha kuanza na kitu fulani siku zote na kuishia na cha mwisho ili kupata matokeo sahihi. Endapo utakosea na kuanza na cha mwisho au cha kati, ni vugumu kufikia suluhisho au solution ya tatizo hilo. Kumbuka nilidokeza kuwa ni suala lililo ndani ya mamlaka ya Yesu Kristo peke yake na ndiye anayejaza watu wake Roho Mtakatifu.
  Kuna ushahidi wa watu wengi katika maagano yote mawili ya Biblia (ukitaka nitakupa maandiko), yanayoonesha kuwa kuna watu waliojiliwa na Roho wa Mungu kabla ya kuwa na ufahamu.

  Point ya kuelewa hapo ni hivi, vyovyote iwavyo, hayo niliyoyataja katika ushauri wangu wa mwanzo, ni package ya muhimu kuwa ndani ya mtu katika suala zima la kukaliwa na ROHO MTAKATIFU. Ama amejazwa Roho mapema, au amechelewa, lazima ajue inampasa kutubu na kumpokea Yesu kuwa mwokozi wake kisha kuamini katika kujazwa katika Roho Mtakatifu kunakoambatana na ishara ya kusema kwa lugha nyingine ya kiungu. Akipuuza ufahamu huu na kukataa mambo ya Mungu, ROHO wa Mungu anaondoka katika maisha yake.

  Please, suala la ROHO MTAKATIFU lisichukuliwe kirahisi kiivyo, la sivyo tutawapotosha watu kwa kuleta mkanganyo wa akili, na kulifanya kuwa ni juhudi za kibinadamu zinazopelekea kujazwa na Roho badala ya kuwa suala linalohusika na IMANI KWA MUNGU. Kila anayechambua afanye utafiti kwanza wa kina na kujua kwa mapana na awe na ushuhuda binafsi katika ROHO huyo huyo.

 30. Ndugu yangu unaposema kuwa hakuna process halafu ukataja hatua nne maana yake ni nini?? Hizi si ni hatua za kujazwa na roho mtakatifu au tuweke steps. Hapa nadhani ni kiswahili/kiingereza tu si shida kubwa.
  Asante sana!!

  Rev. Damasus F. Mkenda

 31. Kitu pokee cha kukupa Fulsa na kufika hapo unapotaka kuwa, ni kujiachia mbele za Mungu na kusahau matatizo yanayokuzunguka na uhakikishe hauna neno na Mtu ni rahisi mno pindi utakapo unamwabudu Mungu katika Roho na Kweli,
  Tatizo la waumini wa siku hizi hawaendi kumuabudu Mungu, wanakwenda kanisani ili waonekane hawakushinda nyumbani.

 32. Wapendwa katika Bwana, suala zima la kupokea/kujazwa/kubatizwa katika Roho Mtakatifu halina kitu kinaitwa ‘PROCESS’ hasa baada ya mtu kumwamini na kumpoke Yesu Kristo moyoni n akilini. Hiyo ni kazi ya Kristo kwa wale ambao amejipatia hakika kwamba wanampenda na siyo kitu cha kutegemea akili ya kibinadamu, ila kuna vigezo vya msingi ambavyo aliviweka Yesu Kristo mwenyewe.

  1. Mtu Kutambua hatari ya maisha yasiyompendeza Mungu na Kuchoshwa na dhambi na kuwa tayari kuziacha. Hatua hii muhimu inamsukuma mtu kutafuta msaada wa Mungu unaopatikana kwa Yesu mwenyewe kama mwokozi.

  2. Hatua hiyo muhimu inapelekea mtu kutubia dhambi zake na hasa baada ya kutambua kwamba msamaha wa kweli wa Mungu unapatikana ndani ya Yesu Kristo. Hivyo mtu anakubali Yesu amsaidie kuishinda dhambi inayotutenga na Mungu.

  3. Kukubali uwepo wa ROHO MTAKATIFU na kuwa na kiu ya kujazwa au kumpokea ukijua hili ni tukio la kipekee kabisa baada ya mtu kuokoka.

  4. Kukubali na kutambua ambano la kupewa lugha mpya ambayo Biblia imetambulisha kuwa ni kusema lugha mpya. Hii ndiyo ishara ya msingi kabisa inayokuhakikishia kwamba Roho wa Kristo yumo ndani yako.

  Mambo hayo mnne yanakuandaa kumpokea Roho Mtakatifu na kujazwa naye.

  NB. UKIWA KATIKA KUSANYIKO LINALODISCOURAGE KUJAZWA NA KUNENA KWA LUGHA MPYA, HIYO TU NI KIKWAZO KIKUBWA KWAKO.

 33. Mada nzuri saaana tena na hamu sana ya kujifunza somo!Pastor lete unalofahamu kidogo.

 34. Daniel,
  Nimependa mchango wako wa kiushuhuda. Naomba nikuulize sswali kama siyo maswali (mtu mwingine yeyote aweza jibu);
  1. Wakati unanena kwa lugha, lugha hiyo huwa unaielewa wewe na hao wanaokusikia?
  2. Kama ni ndiyo, ni kwa namna gani? Mf. waweza kujirekodi wakati wa maombi halafu baada ya maombi ukajisikiliza na ukaelewa? Na kama ni hapana, kwa nini unaiita lugha? Maana fasili/maana ya lugha, sharti ibebe maana.
  3. Kama hujaweza kutofautisha kunena kwa lugha kuliko halisi na kusiko halisi, unaaminije kuwa wewe unanena kwa lugha kuliko halisi?
  Nitafurahi kukuona!

 35. BWANA ASIFIWE WAPENDWA! TUNAPOSEMA ROHO MTAKATIFU NI MTAKATIFU KWELI, HIVO ANAKAA AU ANAINGIA MAHALI PATAKATIFU AMBAPO HAKUNA DHAMBI,INABIDI KUMTAFUTA MUNGU KWA BIDII NA KUJITAKASA,NA ROHO ATAKUJA MWENYEWE!
  MUNGU AWABARIKI.

  from mpwapwa dodoma

 36. Rev. Mkenda,

  Hili swali umelileta kwetu kwa maana ya kwamba na wewe hujui njia ya mtu kupitia ii ajazwe na Roho mt. au umetuuliza swali ambalo wewe unalo jibu lake?

  Ningeomba wewe mwenyewe pia uchangie vile unavyojua.

  Asante!

 37. Ujazo wa Roho Mtakatifu ni moja ya mambo yaliyokuwa yananipa shida sana toka nilipoamua kumpa Yesu rasmi Maisha yangu miaka 10 na ushee iliyopita.. Mara nyingi niliamua hata kuhudhuria mikutano ya hapa na pale ili tu nipate nafasi ya kukiri sala ya Toba tena na tena na tena nikijidanganya nafsini kwangu kuwa may be sijaokoka vizuri na ndio maana sijazwi Roho Mtakatifu na kunena kwa Lugha mpya… Ilifika kipindi nikawa napata shida sana kuhudhuria Kanisani,maana ikifika wakati wa Maombi kila mmoja unakuta amezama katika maombi akinena kwa Lugha, wakati huo mimi najikuta nimeishiwa maneno ya kuomba.. Jambo lililokuwa likinishangaza, mara nyingine nikawa najikuta nikinena kwa Lugha wakati nikiwa usingizini, lakini hali hiyo sijawahi kukutana nayo nikiwa nafanya maombi nikiwa na akili zangu.

  But all in all, nimekuwa nikimfurahia Bwana katika Maisha yangu.. Maana kwa upande wangu nimejua ya kuwa Roho Mtakatifu ni zaidi ya kunena kwa Lugha.. Na sijapata shida tena toka nilipoanza kumwangalia Roho Mtakatifu kwa jicho la tofauti..

  Lakini Swali ambalo huwa najiuliza sana, na ninaomba wenye uelewa wa jambo hili wanijuze, Nijuavyo mimi Roho Mtakatifu hawezi kukaa mahali penye uchafu. Ni msafi mno.. Inakuwaje leo tunakutana na watu makanisani mwetu, kabla hata maombi ya kujitakasa hayajafanyika, na unakuta mtu huyo njia zake hazina ushuhuda kabisa lakini ghafla bin Vuu ameanza kunena kwa Lugha…Je, anakuwa Roho Mtakatifu kweli? na kama sio Roho Mtakatifu hiyo Lugha mtu anakuwa anaigiza au kunakuwa Roho nyingine imemuingia ndani yake huyo mtu?

  – Daniel-

 38. Pastor,
  Mungu akubariki kwa kuleta hoja nzuri. Nasubiri kujifunza sana pia kwa hili!!

 39. Ni kwa njia ya kumuamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi,na kubatizwa kwa majingi,kisha ukaendelea kuishi kutokana na Neno;ndipo utajazwa kwa Roho mt.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s