Sielewi hili tamko la Bwana Yesu!

kujifunza

Nawasalimu ktk Jina zuri la Bwana,

Yako maneno ya Mungu(Yesu) Katika Biblia ni mepesi sana kuelewa na moja kwa moja unapata mantiki/ujumbe aliokusudia LAKINI yako maneno mengine ni magumu kudaka mara moja Yesu alimaanisha nini hasa ukizingatia ukweli halisia ambao unaweza kuongea tofauti na aliyosema Bwana. Najua kua Neno la Bwana siku zote litakua juu ya uhalisia na tunapaswa kuliamini ilo tu maana Yeye Mungu si Mtu hata aseme ulongo au kuzidiwa na nguvu ya ukweli halisia(fact), siku zote ‘Ukweli wa Neno’ lake utakua juu kuzidi ‘ukweli halisia’. Ila pia najua Mungu anapenda sisi Wanae tuwe na ujuzi mkubwa wa Neno na mambo yake maana anasema Watu wangu WanaangaMIZWA kwa kukosa maarifa ivyo kulisoma Neno na kulitafakari kwa kina, yafaa sana na ni baraka.

Karibuni tusaidiane kuumega Mkate huu wa uzima ambao kwangu ni mgumu kweli kweli, Tunaumegaje ktk andiko hili..Marko.9:1 yaliyosemwa hapo pia unaweza yapata Injili nyingine kama Mattayo.16:28 na Luka.9:27

Marko.9:1 Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu. Mark 9:1 NIV –New International VersionAnd he said to them, “I tell you the truth, some who are standing here will not taste death before they see the kingdom of God come with power.”

 Au King James VersionAnd he said unto them, Verily I say unto you, That there be some of them that stand here, which shall not taste of death, till they have seen the kingdom of God come with power.

Dondoo za Kuzingatia unapojibu Maswali yanayofuta chini:

·        Ni maneno ya Yesu mwenyewe si Wanafunzi wake

·        Yesu ni Mkweli tupu lakini bado anaanza/atumia maneno ya msisitizo mkubwa kusema kweli tupu yaani..AMIN…. kisha hawata onja mauti KABISA

·        Ambao hawatakufa ni KATI ya Wale waliokua pale wanamsikiliza

MAELEZO: Ni ukweli tupu kua toka Yesu aseme hayo siku iyo mpaka leo, Ufalme wa Mungu                 (alivyosema Marko na Luka) au Kumuona mwana wa Adamu akija ktk Ufalme wake-( alivyoiweka Mathayo), huo Ufalme  haujaja wala Mwana wa Adam hajatokea.

MASWALI:

(a)    Hiyo Mauti aliyosema Bwana kua baadhi yao pale wasingeionja mpaka wauone Ufalme, ni aina nyingine ile ya mauti yaani ya kiroho au hii hii ya live(Kimwili) tusikuze maneno au kumuwekea maneno mdomoni Yesu ambayo hakusema?

(b)     A u kwa kua Biblia kadhaa za Kiingereza zinatumia neno ‘Kifo’ na Kiswahili inatumia ‘Mauti’ ivyo iko tofauti ya maneno hayo na bila shaka mojawapo ndio hilo hasa Yesu alimanisha ambalo tukilielewa maana yake , mstari huu hautakua mgumu( at least kwangu tu, wengine labda ni simple kabisa)

(c)    Je kati ya Wale aliosema Yesu hawatakufa/onja mauti na kama mauti/kifo icho ni hiki cha live(mwili), je Wanaishi  hata Leo? Wako wapi? Si ingekua ni kivutio cha utalii-kila mtu duniani angejua maana media ingefanya kazi kubwa  na hao wangeingia kua mojawapo ya maajabu ya dunia  au siyo?

(d)    Kama  Kati ya Wale au wote kabisa walikufa/onja mauti maana ni miaka zaidi ya 2000 leo na Yesu alisema, HAWATAONJA MAUTI KABISA, which is which now? Tunawekaje sawa hili tunapohubiri/fundisha/tukiulizwa na washirika wa zamani au wapya ktk imani wakati wa Bible studies au Sunday schools sessions? Tuwakemee wa shut up kwakua wamevuka mipaka ya kudadisi na wanatakiwa kuamini tu ivyo ivyo kama Vitoto vizuri vidogo alivyosema Yesu au tuwape jibu?

Press on.

Edwin Seleli

 

Advertisements

9 thoughts on “Sielewi hili tamko la Bwana Yesu!

 1. Mpendwa Patric nimeipenda shule yako jinc ulivyoikata!Nimebarikiwa.Mpendwa Selel swali zuri saana!Ngoja nikupige kashule kidoogo!Ujuwe yeyote asiyeikubali kazi ya msalaba na asiyeshika neno la Yesu huyo atakufa kimwili na kiroho coz hata kwenye chance ya uzima wa milele hayupo!Jesus ametutel yeye ndiye njia ya uzima wa milele so tukimfuata yeye na kushika neno lake hatufi bali tutaishi milele!soma Yoh 8:51.So cyo wale wa kipindi Kile tu bt hata cc waleo tukimfuata Yeye na kulishika neno lake hatutaona mauti milele.GBU.

 2. Mungu awabariki wachangiaji wote hasa kwa mleta mada,
  Comments zote nimezisoma kwa umakini na kujifunza kitu hapa ingawa bado kuna shida naipata katika hili. hebu Ndugu Patrick na wengineo wana SG nifumbueni katika hili, Je kati ya watu hao aliokuwa akiwambia maneno hayo Bwana Yesu hakuna hata mmoja ambae hakuonja mauti?

 3. Mungu awabariki maana nimejifunza kitu kikubwa sana katika maisha haya ya kujifunza Biblia.

 4. Seleli,
  Kwa uelewa wangu wa neno, Yesu allimaanisha mauti ya pili. Mauti ya kwanza, kwa Yesu ilikuwa ni usingizi tu. Ndiyo maana Yesu anasema ….hawataonja mauti hadi ajapo mwana wa Adamu. Yesu aliwalenga mitume (wale 11, japo sidhani kama kulikuwa na wengine kwenye kundi hilo) ambao aliwaona (kwa baadaye), wakipoteza wakilala (wakipoteza maisha yao) kwa sababu ya kulitetea jina lake. Kulala kwao kwa sababu hiyo, kuliwafanya wajipatie tiketi ya kutoonja mauti ya milele kabisa.
  Kwa maelezo zaidi, jifunze habari za ufufuo wa kwanza na ule wa pili, kwamba ukoje na unawahusu akina nani? Nnayo guke!

 5. Kwa uelevu wangu mdogo,ninaona hapa Yesu alikua anazungumzia kifo cha kiroho na si cha kimwili.

 6. ,,,Patrick,,, umenifurahisha sana leo kwa majibu yako mazuri, naamini Roho mtakatifu kakutumia, Selel swali zuri sana . * tuendelee kujifunza*

 7. Edwin,

  Katika kuendelea kujifunza Bwana Yesu alichomaanisha aliposema kuwa baadhi ya watu pale hawatonja mauti hata wauone ufalme wa Mungu, hebu linganisha na maneno aliyomwambia Nikodemo.

  Yohana 3:3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

  Hivyo basi ndio maana nilidokezea kuwa kuuona Ufalme wa Mungu ilikuwa mpaka watu waokoke na hilo lilikuwa bado kuwezekana wakati ule kwani alikuwa bado hajakamilisha kazi ya ukombozi wetu. Aliikamilisha baada ya kufa msalabani, kuzikwa na kufufuka na hapo ndipo baadhi ya wale waliosimama pale waliweza “kuuona ufalme wa Mungu” baada ya kumwamini na kuzaliwa mara ya pili.

  Tuendelee kujifunza

  Nduguyo,

  Patrick

 8. alaa!!!!! ivi maana yake ilo andiko kumbe ni ivyo ulivyoeleza? kua ni kwa maana ya alikua hajaenda msalabani na kweli alipofika, kweli walikuwepo walioendea kuishi mpaka time iyo?Aisee! so bado niko kwa mashangao mpaka sasa!

  Ngoja nitumie sign yako ya ”Naendelea kujifunza

  Press on,

 9. Edwin,
  Hayo maneno ya Bwana Yesu ni kweli kabisa na yalitimia lama alivyosema.
  Kumbuka mafarisayo walipomwuliza ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu vipi? Alisema: Luke 17:20 (KJV) – And when he was demanded of the Pharisees, when the kingdom of God should come, he answered them and said, The kingdom of God cometh not with observation:
  Luke 17:21 (KJV) Neither shall they say, Lo here! or, lo there! for, behold, the kingdom of God is within you.

  Kwa maana hiyo basi Bwana Yesu alimaanisha kuwa kuna watu pale ambao wangeu-experience ufalme wa Mungu kazi yake ya ukombozi itakapokamilika kwani alikuwa hajasulubiwa ili wokovu uweze kuwa available kwa wote.
  Ndio maana Mtume Paulo alisema tumehamishwa toka ufalme wa Giza na ku.gizwa katika Ufalme wa Mwana wa pendo LAKE, yaani ufalme wa Mungu.
  Tuendelee kujifunza…
  Patrick

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s