Kuna haja ya kuogopa Kifo?

woga

Bwana Yesu asifiwe, napenda kuuliza swali. Mtu akifa anaenda wapi? Kuna maisha mengine baada ya kufa? (Rejea Hadithi ya tajiri na maskini)

Je kuna haja ya kuogopa kifo??

Yesu akamwambia, mimi ndiye huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hatab milele. Je Unayasadiki hayo?” – John 11:25-26

Advertisements

16 thoughts on “Kuna haja ya kuogopa Kifo?

 1. Lenda,
  Kwa kadiri ninavyoyasoma maelezo yako, nakuona ni mtu uliyejichanganya sana, inaonesha unataka kwenda Njia mbili kwa wakati mmoja; ya Agano la Kale na ya Agano Jipya, jambo ambalo haliwezekani!!!

  Haya maelezo yako yote uliyoyatiririsha hapa, yanayo majibu yake katika ile thread ya “SIRI YA KIFO NA KABURI”! nenda ukayasome huko yamefafanuliwa zaidi huko. mimi sijui jinsi ya kuweka link, labda Moderator atusaidie ili kurahisisha.

  Hata hivyo, kwa kifupi, kwa kuwa umekiri kwamba Biblia imekosewa ili ulichomeke fundisho lenu kuhusu kifo, maana yake ni kwamba umelikataa hilo Neno halisi lililoandikwa ktk hiyo Luka 23:43, hilo lililohakikiwa mara saba; basi kuna rejea gani tena itakayo kufaa!?

  Mimi siioni rejea ya kuitumia, labda hayo mafundisho yenu, maana ni sawa na kuzungumza na Muisilamu halafu mkawa yeye anatumia Quran na wewe unatumia Biblia, ni wendawazimu!

  Labda kwa faida ya wasomaji wengine, ngoja nilirejee hili fundisho lenu linalochezea Maandiko kwa kuhamisha vituo ili kuyabadili maana iliyokusudiwa; yaani mkilitimiza lile jambo la KUONGEZA na KUPUNGUZA yaliyo andikwa ktk kitabu hiki, Biblia; Ufu 22:18-19 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”

  Duh, nawahurumia saaaana!!!!!!

  Neno linasema hivi:
  “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”

  Lakini kutokana na mafundisho yenu yanayowalaza wafu kaburini miili na roho, mpaka siku ya ufufuo hapo atakaporudi Kristo, ndio mmeyabadili Maandiko hayo ili yakidhi fundisho lenu hilo, ili kwamba huyo mwivi aonekane ataingia ktk ufalme huo huko mbele, basi mkaisogeza “comma” mbele kutoka “nakuambia,” kwenda “leo hivi,”:
  “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi.”

  Hata andiko hilo analo kataa asishikwe, Yn 20:17, mnalitumia nje ya ufahamu maana hakuna mfu aliyekwenda huko kwa Baba anakokuzungumzia Kristo, alikwisha kusema hakuna aliyepaa kwenda mbinguni isipokuwa huyo aliyeshuka… Yn 3:13, jambo hilo lingekuonesha kwamba hao wanaolala ktk Kristo hupelekwa mahali wanaposubiri kukamilika kwa Injili, licha ya wewe kuiweka miili yao makaburini ioze na kuurudia udongo. Yule Adamu wa Mwa 1:26 hakuwa wa udongo hivyo hawezi kukaa kaburini kama mlivyodanganywa!

  Labda nikuulize, Eliya alipaa kwenda wapi? Naye Musa, Maandiko yanatuambia kuwa alikufa, lakini hao wawili tunawaona wakiongea na Kristo, je walikuwa ni mizimu????

  Asante kwa leo!

 2. “PAMOJA NA HAYO ATACHUKULIWA KABURINI NAO WATALINDA ZAMU JUU YA ZIARA LAKE.”
  AYUBU 21:32

 3. NI MANENO GANI YESU ALITUMIA LAZARO ALIPOKUFA

  “…RAFIKI YETU LAZARO AMELALA, LAKINI NINAKWENDA NIPATE KUMWAMSHA.” YOHANA 11:11

  WANAFUNZI WALISHANGAA KUAMBIWA MTU WALIYEMZIKA KABURINI KUWA AMELALA WAKAULIZA

  “…BWANA IKIWA AMELALA, ATAPONA. LAKINI YESU ALIKUWA AMENENA HABARI YA MAUTI YAKE; NAO WALIDHANIA YA KUWA ANANENA HABARI YA KULALA USINGIZI.”

  “BASI HAPO YESU AKAWAAMBIA WAZIWAZI, LAZARO AMEKUFA.” YOHANA 11:12-14

  “…BWANA, KAMA UNGALIKUWAPO HAPA, NDUGU YANGU HANGALIKUFA.” YOHANA 11:21

  “..NDUGU YAKO ATAFUFUKA.” YOHANA 11:23

  WAFUASI WA YESU PIA WALIAMINI MTU HUFUFUKA SIKU YA MWISHO SI KAMA WAKRISTO WANAOAMINI UMIZIMU SIKU HIZI ANASEMA;

  “NAJUA YA KUWA ATAFUFUKA KATIKA UFUFUO SIKU YA MWISHO.” YOHANA 11:24

  -YESU ALIPOMWITA LAZARO ALITOKEA KABURINI, PALE ALIPOLAZWA SI MAHALI PENGI NA ALIKUWA AMEANZA KUOZA.

  “BWANA, ANANUKA SASA; MAANA AMEKWISHA KUWA MAITI SIKU NNE.” YOHANA 11:39
  KISA CHA MWIZI MSALABANI KIMEWAFANYA WENGI KUTUMBUKIA KWA URAHISI KATIKA IMANI YA UMIZIMU.

  “KWA SABABU WALIO HAI WANAJUA YA KWAMBA WATAKUFA; LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE…” MHUBIRI 9:5
  “KISHA AKASEMA, EE YESU NIKUMBUKE UTAKAPOINGIA KATIKA UFALME WAKO.” LUKA 23:42
  ANGALIA TOFAUTI KATIKA UANDISHI WA BIBLIA KATIKA KARNE TOFAUTI, HAPO AWALI BIBLIA HAZIKUANDIKWA KWA VITUO MPAKA KATIKA KANISA LA ZAMA ZA KATI.NA MABADILIKO HAYO YAMELETA TOFAUTI KATIKA UANDISHI KAMA HIVI;

  “YESU AKAMWAMBIA, AMINI, NAKUAMBIA,LEO HIVI UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI.” LUKA 23:43

  “YESU AKAMWAMBIA AMINI, NAKUAMBIA LEO HIVI, UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI.” LUKA 23:43

  YESU HAKUPAA KWENDA MBINGUNI SIKU HIYO KAMA SENTENSI NAMBA MOJA HAPO JUU INGEFAFANULIWA VILE INAVYOSOMEKA,INGEPISHANA NA HII HAPA CHINI

  “YESU AKAMWAMBIA. USINISHIKE; KWA MAANA SIJAPATA KWENDA KWA BABA. LAKINI ENENDA KWA NDUGU ZANGU UKAWAAMBIE, NINAPAA KWENDA KWA BABA YANGU NAYE NI BABA YENU, KWA MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU.” YOHANA 20:17

  KISA CHA LAZARO NA TAJIRI KINATUAMBIA NINI?
  WAHUSIKA KATIKA KISA CHA LAZARO NA TAJIRI
  1.TAJIRI
  2.LAZARO
  3.MBWA
  4.ABRAHAMU
  MARA NYINGI MANENO YA YESU YALIWACHOMA MAFARISAYO, NA HIVYO MARA NYINGINE ALITUMIA MIFANO KUVUTA WATU KWA MAFUMBO KWA KUANGALIA KITU GANI WATU HUSIKA WALIKIAMINI, NA MARA NYINGINE ALIONGEA NA WATU WALE WALIOKIRIMIWA KUFUNGULIWA SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI.

  “UUNONESHE MOYO WA WATU HAWA, UKAYATIE UZITO MASIKIO YAO, UKAYAFUMBUE MACHO YAO; WASIJE WAKIONA KWA MACHO YAO, NA KUSIKIA KWA MASIKIO YAO, NA KUFAHAMU KWA MIOYO YAO, NA KUREJEA NA KUPONYWA.” ISAYA 6:10

  KITABU CHA TALMUD HUFANANISHA WATU WA MATAIFA NA MBWA, WATU AMBAO HAWAMJUI MUNGU. WATU WA MATAIFA WALITENGWA NA MAFARISAYO KWA UJUMBE WA MUNGU.

  “YESU AKAONDOKA HUKO, AKAENDA KANDO PANDE ZA TIRO NA SIDONI.22 NA TAZAMA, MWANAMKE MKANANAYO WA MIPAKA ILE AKATOKEA, AKAMPAZIA SAUTI AKISEMA, UNIREHEMU, BWANA, MWANA WA DAUDI; BINTI YANGU AMEPAGAWA SANA NA PEPO.23 WALA YEYE HAKUMJIBU NENO. NAO WANAFUNZI WAKE WAKAMWENDEA, WAKAMWOMBA, WAKISEMA, MWACHE AENDE ZAKE; KWA MAANA ANAPIGA KELELE NYUMA YETU. 24AKAJIBU, AKASEMA, SIKUTUMWA ILA KWA KONDOO WALIOPOTEA WA NYUMBA YA ISRAELI.25 NAYE AKAJA AKAMSUJUDIA, AKISEMA BWANA UNISAIDIE.26 AKAJIBU AKASEMA, SI VEMA KUKITWAA CHAKULA CHA WATOTO NA KUWATUPIA MBWA.” MATHAYO 15:21-26

  KUMBUKA MWANAMKE HAKUHITAJI CHAKULA CHA KAWAIDA, MAANA HAKUOMBA HIVYO MPAKA AJIBIWE HIVYO NA YESU.

  “27AKASEMA,NDIYO, BWANA LAKINI HATA MBWA HULA MAKOMBO YAANGUKAYO MEZANI PA BWANA ZAO.28NDIPO YESU AKAJIBU, AKAMWAMBIA, MAMA IMANI YAKO NI KUBWA; NA IWE KWAKO KAMA UTAKAVYO. AKAPONA BINTI YAKE TANGU SAA ILE.” MATHAYO 15:28

  WATOTO WETU HUWA TUNAWAWEKA VIFUANI MWETU KUWAFARIJI? LUKA 16:25

  “IKAWA YULE MASKINI ALIKUFA, AKACHUKULIWA NA MALAIKA MPAKA KIFUANI KWA IBRAHIMU.” LUKA 16:22

  “AKALIA AKASEMA. EE BABA IBRAHIMU..”LUKA 16:24
  MTOTO ANAYEITA EE BABA IBRAHIMU HAYUPO KIFUANI MWA IBRAHIM ILA YUPO MTU MWINGINE

  MAFARISAYO WALIMWITA IBRAHIMU BABA YAO. NA IBRAHIMU NI BABA WA IMANI LAKINI WAO HAWAKUWA NA IMANI NA YESU WAKATI. IBRAHIMU ALIMWAMINI MUNGU NA ALIAMINI UJIO MWANA WAKE.

  KAZI WALIYOTAKIWA KUIFANYA NI KUPELEKA NURU ULIMWENGUNI,KWA MASIKINI/ WENYE NJAA YA HAKI

  “NAAM, ASEMA, HIVI, NI NENO DOGO SANA WEWE KUWA MTUMISHI, WANGU ILI KUZIINULIA KABILA ZA YAKOBO, NA KUWAREJEZA WATU WA ISRAELI WALIOHIFADHIWA; ZAIDI YA HAYO NITAKUTOA UWE NURU YA MATAIFA, UPATE KUWA WOKOVU WANGU HATA MIISHO YA DUNIA.” ISAYA 49:6

  “IBRAHIMU, BABA YENU, ALISHANGILIA KWA VILE ATAKAVYOIONA SIKU YANGU; NAYE AKAIONA, AKAFURAHI.” YOHANA 8:56

  “WAKAJIBU, WAKAMWAMBIA, BABA YETU NDIYE IBRAHIMU! YESU AKAWAAMBIA, KAMA MNGEKUWA WATOTO WA IBRAHIMU MNGEZITENDA KAZI ZAKE IBRAHIMU.” YOHANA 8:36

  “AKASEMA ,LA, BABA IBRAHIMU, LAKINI KAMA AKIWAENDEA MTU ATOKAYE KWA WAFU, WATATUBU.” LUKA 16:30

  IBARAHIM ALIJIBU: “AKAMWAMBIA, WASIPOWASIKIA MUSA NA MANABII, HAWATASHAWISHIWA HATA MTU AKIFUFUKA KATIKA WAFU” LUKA 16:31

  YESU ALITOA UNABII JUU YA KUFUFUKA LAZARO KUTOKA WAFU AMBAYE HATA HIVYO BADO HAWAKUAMINI WAKATAKA WAMUUE KAMA WALIVYOWAFANYA MANABII NA LAZARO MWENYEWE ALITOKEA KABURINI SI KIFUANI PA IBRAHIMU HIVYO YESU ALITUMIA HUU KAMA MFANO.

  “NA WAKUU WA MAKUHANI WAKAFANYA SHAURI LA KUMWUA LAZARO NAYE;” YOHANA 12:10

  UTAJIRI WA WAYAHUDI NI KURIDHIKA NA ELIMU YA MUNGU WALIYOKUWA NAYO NA KUPUMBAZIKA
  NENO LA MUNGU NDIO HUWAKILISHA CHAKULA ALICHOKULA TAJIRI (MAFARISAYO)

  LAZARO HUWAKILISHA WATU WA MATAIFA NA MAJIRANI WA ISRAELI, KUMBUKA MWANAMKE ALIYEJIITA MBWA.WATU AMBAO KWAO HAKUKUWA NA NENO WALA WAYAHUDI HAWAKUWAHUBIRIA.

  WATU WA MATAIFA NA WALE WALIOIPOKEA INJILI WAMEFANANISHWA NA WATOTO,MAANA WATOTO HUMWAMINI BABA YAO.

  “KWA KUWA MAMBO HAYA UMEWAFICHA WENYE HEKIMA NA AKILI; UMEWAFUNULIA WATOTO WACHANGA; NAAM BABA, KWA KUWA NDIVYO ILIVYOKUPENDEZA” LUKA 10:21

  WATU WANAODHANI WAMESOMA SANA NA KUIJUA ELIMU YA DINI WAKIJIFUNZA MAPOKEO, BADALA YA BIBLIA HUJIONA WANAUFAHAMU MNO NA KUTUPIA MBALI KWELI ZA BIBLIA WAKISHIKILIA TEOLOJIA ZAO KAMA MAFARISAYO HUJIFANYA MATAJIRI WA IMANI WAKADHARAU WATU WALIODHARAULIKA AMBAO KWAO NENO HALIKUWAPO BALI WAO WALIKUMBATIA BIBLIA (CHAKULA CHA TAJIRI) WAKIWANYIMA WATU KUSOMA KWA MUDA MREFU.
  YESU ANASEMA KUWA;

  “OLE WENU NINYI AMBAO MMESHIBA SASA, KWA KUWA MTAONA NJAA” LUKA 6:25
  MAFARISAYO WALIWANYIMA WATU KUINGIA KATIKA UFALME

  “OLE WENU WAANDISHI,WANAFIKI! KWA KUWA MNAWAFUNGIA WATU UFALME WA MBINGUNI; NINYI WENYEWE HAMWINGII, WALA WANAOINGIA HAMWAACHI WAINGIE.” MATHAYO 23:13

  SOMA VISA VYA LUGHA YA PICHA KAMA WAAMUZI 9:8-15

  JAMBO ALILOTAKA KUWASILISHA YESU KWA WATU NI IMANI YA WATOTO WA WA KWELI WA IBRAHIMU

  JIULIZE MASWALI HAYA

  1. TUKIFIKA MBINGUNI WATAKATIFU WOTE TUTAKUWA KIFUANI MWA IBRAHIMU?
  2. WATAKATIFU WA MBINGUNI WANAWEZA KUFURAHIA MBINGU WAKIWA KARIBU NA MAKELELE YA WATU WALIO KATIKA MOTO UMBALI WA IBRAHIMU KUNYOSHA MKONO?
  3. WATAKUWA WAKIWAONA WATU WA MBINGUNI WAKATI WAKILA NA KUNYWA? JE MUNGU NI MKATILI?
  3. JE TONE LA MAJI ALILOOMBA TAJIRI LINGEWEZA KUKATISHA KIU?

  “ENENDA KWA WATU HAWA, UKAWAAMBIE, KUSIKIA, MTASIKIA WALA HAMTAFAHAMU; NA KUONA, MTAONA WALA HAMTATAMBUA; KWA MAANA MIOYO YA WATU HAWA IMEPUMBAA NA MASIKIO YAO NI MAZITO YA KUSIKIA NA MACHO YAO WAMEFUMBA WASIJE WAKIONA KWA MACHO YAO NA KUSIKIA KWA MASIKIO YAO, NA KUFAHAMU KWA MIOYO YAO, NA KUBADILI NIA ZAO NIKAWAPONYA.” MATENDO 28:26-27

  KWA NINI YESU ATUMIE MFANO KAMA HUU WA LAZARO NA TAJIRI

  “KWA SABABU HII NASEMA NAO KWA MIFANO; KWA KUWA WAKITAZAMA HAWAONI, NA WAKISIKIA HAWASIKII, WALA KUELEWA.” MATHAYO 13:13

  MEZA YA TAJIRI NA UTAJIRI
  “NAYE ALIKUWA AKITAMANI KUSHIBISHWA KWA MAKOMBO YALIYOANGUKA KATIKA MEZA YA YULE TAJIRI;” LUKA 16:21
  “NA DAUDI ASEMA, MEZA YAO NA IWE TANZI NA MTEGO, NA KITU CHA KUWAKWAZA, NA MALIPO KWAO;” WARUMI 11:9
  “BASI NASEMA, JE! WAMEJIKWAA HATA WAANGUKE KABISA? HASHA! LAKINI KWA KOSA LAO WOKOVU UMEWAFIKILIA MATAIFA, ILI WAO WENYEWE WATIWE WIVU.” WARUMI 11:11
  “BASI, IKIWA KOSA LAO LIMEKUWA UTAJIRI WA ULIMWENGU, NA UPUNGUFU WAO UMEKUWA UTAJIRI WA MATAIFA, JE! SI ZAIDI SANA UTIMILIFU WAO? WARUMI 11:12

  “TUKIMWACHA HIVI, WATU WOTE WATAMWAMINI; NA WARUMI WATAKUJA, WATATUONDOLEA MAHALI PETU NA TAIFA LETU.” YOHANA 11:48

  BASI TUSIFANYE NENO LA MUNGU KAMA NJIA YA KUTUNZA MAMLAKA YETU/UTAWALA, NA KUWANYIMA KWELI MASKINI NA WENYE NJAA YA INJILI.

  HUSIANISHA MAKUHANI KUTAKA KUMUUA LAZARO BAADA YA KUFUFUKA ILI WATU WASIIPOKEE IMANI YOHANA 12:10 NA IBRAHIMU KATIKA KISA KUSEMA HATA WATU WAKITOKA KATIKA WAFU HAWATAAMINI. LUKA 16:31

 4. WAFU WAMELALA MAKABURINI

  MATENDO 13 :36

  “KWA MAANA DAUDI, AKIISHA KULITUMIKIA SHAURI LA MUNGU KATIKA KIZAZI CHAKE, ALILALA,AKAWEKWA PAMOJA NA BABA ZAKE,AKAONA UHARIBIFU”

  MATENDO 2:29

  “…DAUDI, YA KUWA ALIFARIKI AKAZIKWA, NA KABURI LAKE LIKO KWETU HATA LEO”

  MATENDO 2:34
  “MAANA DAUDI HAKUPANDA MBINGUNI; BALI YEYE MWENYEWE ANASEMA..”

 5. Lenda ,

  Yote uliyoyanukuu yapo hivyohivyo , .ni Sawa na yanasomeka hivyohivyo! Lakini mtu akifa anakwenda wapi? Na je , kuna maisha tena baada ya kifo ?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai “

 6. Siyi rafiki yangu,

  Kwa hiyo hakuna maisha baada ya kifo? kulingana na majibu yako kwa Anna?

 7. AYUBU 16:22
  “KWANI IKIISHAPITA MIAKA MICHACHE,NITAKWENDA NJIA AMBAYO SITARUDI TENA.”

  AYUBU 27:3
  “KWA KUWA UHAI WANGU UKALI MZIMA NDANI YANGU, NA ROHO YA MUNGU I KATIKA PUA YANGU”

  MHUBIRI 12:7
  “NAYO MAVUMBI KUIRUDIA NCHI KAMA YALIVYOKUWA, NAYO ROHO KUMRUDIA MUNGU ALIYEITOA.”

  ZABURI 146: 4
  “PUMZI YAKE HUTOKA,HUURUDIA UDONGO WAKE SIKU HIYO MAWAZO YAKE YAPOTEA.”

  MHUBIRI 9:5
  “KWA KUWA SABABU WALIO HAI WANAJUA YA KWAMBA WATAKUFA; LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LO LOTE,..”

  ZABURI 115:17
  “SIO WAFU WAMSIFUO BWANA…”

  MHUBIRI 9:5
  “KWA SABABU WALIO HAI WANAJUA YA KWAMBA WATAKUFA; LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE, WALA HAWANA IJARA TENA; MAANA KUMBUKUMBU LAO LIMESAHAULIKA.”

  SHETANI SI KILANJA WA HUKO HATA YEYE MOTO UTAMLA.
  MATHAYO 25: 41
  “…..ONDOKENI KWANGU MLIOLAANIWA, MWENDE KATIKA MOTO WA MILELE ALIOWEKEWA TAYARI IBILISI NA MALAIKA ZAKE;”
  TUMAINI KUU LIKO HAPA
  1 WATHESALONIKE 4:16,17
  “KWA SABABU BWANA MWENYEWE ATASHUKA KUTOKA MBINGUNI, PAMOJA NA MWALIKO, NA SAUTI YA MALAIKA MKUU NA PARAPANDA YA MUNGU; NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA. KISHA SISI TULIO HAI, TULIOSALIA, TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO KATIKA MAWINGU, ILI TUMLAKI BWANA HEWANI; NA HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.

  UNAPOSOMA KISA CHA LAZARO AMBACHO WANAOAMINI IMANI ZA MIZIMU WAMEKITUMIA KAMA NYENZO YA KUMPINGA UFUFUO WA SIKU AJAPO YESU. JIULIZE MASWALI HAYA?

  1. ABRAHAMU ANAKIFUA CHA KUWABEBA WENYE HAKI WOTE DUNIANI WAFAPO?

  2. WATU WA MBINGUNI SIKU MOJA WATAKUWA WAKIZUNGUMZA NA WATU WALIO ZIWA LA MOTO? JE MUNGU AWEZA KUJITENGENEZEA ZOO YA WATU WAKE WAKIANGAMIA.

  3. WATAKATIFU MBINGUNI WATAWEZAJE KUFURAHIA MBINGU HUKU WAKISIKIA KILIO CHA WAOVU? UMBALI WA KUWEZA KUSIKIA SAUTI ZAO?

  4. TONE LA MAJI LINGEWEZA KUONDOA KIU YA TAJIRI?

  LUKA 8:10
  “Wanafunzi wake wakamwuliza maana yake nini mfano huo? Akasema, ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.

 8. Anna
  Hao ni waongo kabisa. Usiwaamini watu kama hao. Wewe soma Biblia. Ikikuambia kuwa kuna maisha baada ya kifo (huko kuzimu), basi amini hiyo. Lakini kama imekataa, acha kuamini hayo. Kuamini kuwa kuna maisha baada ya kido, ni spiritualism. Utaishia pabaya ndg yangu. It is unbiblical kabisa.

 9. nimeona shuhuda nying za waliokufa na kurudi tena kisha wanasema waliyoyaona huko. Hii inaniaminisha ni kweli kuna maisha mengine baada ya kufa, ila sijui unaenda wapi kama ni mbinguni au jehanam

 10. Majinge
  Mimi nakwambia kuna haja kwa ya kuogopa kwa upande mwingine, hasa ukiwa na maisha yasiyo na uhakika wa kuiona mbingu Yesu kama angekuja sasa hivi. Maana ungetamani upate muda wa kutengenza mambo yako kwanza.
  Lakini kama mambo yako yako vizuri kiroho, huna haja ya kuogopa kulala rafiki. Hakikisha tu kuwa unapumzika kwenye uzima wa milele-ktk Kristo na siyo ktk Ibilisi.
  Ubarikiwe na Bwana Majige

 11. Hakuna haja ya kuogopa kifo.
  Yesu kashinda kifo na mauti, ndiposa tulio wake hatufi ila tunalala.

  So, why fear?!!

 12. Jesus said to her, “I am the resurrection and the life. The one who believes in me will live, even though they die; and whoever lives by believing in me will never die. Do you believe this?”
  – John 11:25-26 (NIV)

  Today’s commentary
  by Dave Whitehead, Senior Pastor, GraceNYC.org

  Jesus has promised that death is not the final statement to those who believe in Him. There is a resurrection life promised to anyone who calls upon the name of Jesus. Death will claim all of us, but Jesus says that something even greater than this life is waiting for his servants. Do you believe this?

  http://www.biblestudytools.com/commentaries/peoples-new-testament/john/11.html
  25. I am the resurrection, and the life. Christ makes the grand, striking declaration that he is the RESURRECTION AND THE LIFE, words that never could have fallen from the lips of a sane mortal. They mean that he is the power which opens every grave, gives life to the sleepers, and calls them forth to a new existence; that the life that endows men with eternal being is in him and proceeds from him. In the light of his own resurrection they mean that when he burst open the tomb he did it for humanity and in him humanity has won the victory over death.

  26. Whosoever liveth and believeth in me shall never die. Those dead, who believed in him, shall be raised and live, and those living who believe, shall never perish. Death will only be a change to a better existence

 13. “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake, Nao watatoka, wale WALIOFANYA MEMA KWA ufufuo wa uzima,na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.” Yohana 5:28,29

  fungu hili linatuonyesha hata wema na wabaya wamelala kaburini wakimsubiri Yesu kwa ufufuo wa uzima na wabaya ufufuo wa hukumu.

 14. Ubarikiwe mtumishi usiye na jina.
  Kimsingi, binafsi ningependa kusikia unazungumzia kifo cha aina gani? Maana kuna vifo vya aina mbili. 1. Kifo cha Kimwili(usingizi wa muda) na 2. Kifo cha kimwili na Roho (cha milele). Hebu tanabaisha kwanza, wazungumzia kifo kipi kati ya hivi?
  Siyi anakungoja!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s