Mkristo asiyefuata Sheria! – 1

sheria

Ni Jumapili asubuhi kanisani kwenu – kama saa tano na dakika arobaini hivi. Kipindi cha sifa kimekwisha, sadaka zimeshakusanywa, na sasa wakati umefika wa kusikia Maandiko yakisomwa na mahubiri kutolewa. Mchungaji wako anapanda mimbarani, anafungua kitabu kikubwa cheusi, anavuta pumzi yake kisha anapaza sauti yake huku akiwa ameinua mikono juu na kusema kwa mamlaka: “Mtu anahesabiwa haki kwa matendo,si kwa imani tu!”

Je, walio wengi kanisani kwenu wangeitikiaje maneno hayo? Je, wangeshangazwa na kupotoka kwa mchungaji? Au je, wangekasirishwa kwamba anapingana na maandiko yote ya Paulo kuhusu wokovu, ambayo yanataja kweli zenye thamani kubwa sana, zilizogunduliwa tena wakati wa Matengenezo ya Kanisa? Au je, wangemwita mkazia kushika sheria? Au, wangetambua kwamba amesoma maneno ya Yakobo 2:24?

Wale ambao wangeitikia vibaya wanawakilisha makundi ya watu wanaojiita Wakristo, waliokosea vibaya sana. Pasipo kuelewa asili ya imani yenye kuokoa, wao hudhani kwamba matendo yanapingana na imani, wakati ambapo kihalisi ni kwamba matendo yameunganika na imani ya kweli. Kama alivyoandika Martin Luther: “Haiwezekani kutenganisha kamwe matendo na imani, kama ambavyo haiwezekani kutenganisha joto na nuru kutoka kwenye moto.”

Luther aliwakatia jina wale walioamini kwamba kwa kuwa wokovu ni zawadi itolewayo bure kwa neema ya Mungu, kuzitii sheria za Mungu si muhimu. Aliwaita “wapingao kushika sheria” – antinomians – kutokana na maneno ya Kilatini mawili: anti – kinyume cha; na nomos – sheria au torati.

Leo hii makanisa ya KiProtestanti yamejaa watu wanaopinga kushika sheria, na kama Luther angekuwa hai, angepinga sana upotovu huo na kudai watu wafanye upya imani zao. Wala asingekosa kuungwa mkono na Maandiko mengi kuhusu jambo hilo, kwa sababu Bwana Yesu Mwenyewe, na Paulo, na Petro, na Yakobo, na Yohana, na Yuda pia walionya juu ya jambo hilo. Ukweli ni kwamba Luther angepata maandiko mengi sana ya kuunga mkono hoja yake kuliko aliyokuwa nayo ili kuunga mkono kweli za Matengenezo wakati alipoyafanya. Maonyo yatolewayo na Agano Jipya juu ya kosa la kupuuza sheria ni mengi sana kuliko maonyo yatolewayo kinyume cha kushika sheria.

Makosa Hatari Mawili

Katika siku za Luther, kanisa lilikuwa limezama katika kushika sheria. Wengi katika watu waliokwenda makanisani walijua kwamba wokovu unapatikana kwa kufanya kitu. Mtu angeweza kujipatia alama ambazo zingepunguza mamia na hata maelfu ya miaka ya adhabu yake ya baadaye huko Toharani (au purgatori) kama angenunua cheti cha msamaha, kama angekwenda kutazama mabaki ya miili ya watakatifu au vitu vilivyoitwa vitakatifu, kama angefanya kitubio na kadhalika. Injili ilikuwa imepotea.

Lakini, wakati Luther aliposoma kitabu cha Warumi aligundua kwamba wokovu ni zawadi itolewayo bure, inayopokelewa kwa imani tu. Akazaliwa mara ya pili, na mara moja akaanza kuwabana wenzake akitumia zile kweli zilizomweka huru. (Yaani, imani yake ilianza kufanya kazi!) Ukazuka ubishi mkali, lakini mwishowe, kupitia kwa Luther mwenyewe na watenda kazi wengine waliohusika na Matengenezo ya Kanisa, wengi walikuja kuamini Injili ya neema ya Mungu.

Lakini, kulikuwepo na hatari iliyojificha ya Injili kama hiyo, na hata hao watengenezaji walifahamu. Iliwezekana kwamba neema ya Mungu ingeweza kutumiwa kama kibali cha kutenda dhambi. Umuhimu wa matendo mema ungeweza kupuuzwa, na uzushi mpya ungechukua nafasi pa ule wa zamani, ambao ungekuwa mbaya tu na wa kupotosha kabisa. Hivyo, watengenezaji wa Kanisa walitangaza kwa uangalifu sana ujumbe huu: “Ni imani tu inayookoa; lakini imani yenye kuokoa haiko peke yake.”

Leo hii, miaka mia nyingi baadaye, kile walichohofu kimetujia sisi. Waenda kanisani leo hawana haja ya kuambiwa kwamba matendo yao mafu hayawezi kuwaokoa, kama ilivyokuwa kwa washika sheria wa siku za Martin Luther. Badala yake, wanachohitaji kuambiwa ni kwamba imani yao iliyokufa haiwezi kuwaokoa. Wengi wamenunua hisa katika injili ya uongo inayoahidi kwamba kuna mbingu pasipo utakatifu. Neema wanayoitumaini inapelekea kwenye ruhusa ya kutenda dhambi badala ya kumtii Kristo. Lakini Yesu Kristo – ambaye ni yeye yule jana na leo na hata milele – bado anawaonya wanaopinga kushika sheria kila mahali kwa maneno haya: “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa minguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21 – Maandiko mepesi kwa ajili ya kutilia mkazo).

Kushika Sheria Maana Yake Nini?

Fuatilia sehemu ya pili mwendelezo huu….barikiwa

David Servant

Advertisements

7 thoughts on “Mkristo asiyefuata Sheria! – 1

 1. Ujumbe “Imani bila Matendo imekufa” Matendo ni dhihirisho la imani na wala pasipo imani hakuna tendo lolote atakalofanya mwanadamu litakalomsaidia kupata haki mbele za Mungu. Kwa matendo yetu tunadhihirisha imani yetu kwa kristo. kwa hiyo basi hatujivunii imani tuliyonayo kwa kristo bali uwezo wa hiyo imani kutufanya tuishi kama kristo. […….tu barua watu wanatusoma]

 2. Nimefupisha mtazamo wa David, utagawanyika sehemu tatu ili iwe rahisi kwa wasomaji, asanteni kwa kufuatilia.

  Barikiwa

 3. Du hii kali!! next time jaribu kuandika kwa ufupi ndg yetu ili kurahisisha usomaji

 4. Dhuh! kweli mtumishi kama alivyo sema Siyi, una kurasi nyingi kweli ndugu yetu. yabidi nitafute muda niendele. ila ubarikiwe sana kutuletea mambo mazuri..

 5. Pamoja na maandiko mengi aliyoonesha mtumishi wa Mungu David Servant, ila ukweli ni kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki kwa matendo wala kuokolewa kwa matendo yake, hivyo ndivyo neno la Mungu linavyotufundisha. La! Kristo asingekuja basi maana tungeweza kuokoka kwa matendo yetu au kuhesabiwa haki kwa matendo yetu. 

  Au ngoja tuulizane maswali haya, je kwa ufahamu wako wewe na historia iliyoandikwa kwennye biblia je ni nani au mtu yupi aliyeishi maisha ya utakatifu wala hakukosa neno lolote wala kumtenda Mungu dhambi?? mtu ambaye kwa matendo yake yeye mwenyewe alihesabiwa haki? nani??

 6. David,
  Inaelekea una somo nzuri hapa. Lakini unaandika sana mpendwa. Hata hatujamaliza kusoma. Binafsi, nikimaliza kuisoma yote na kuirudia tena, ndipo nitacomment. But, maudhui ya maneno haya, ni kukwambia kama siyo kuishi kwa neema ya Kristo, uwe unaandika kwa ufupi. Yaelekea wewe ni mch. na Bwana akubariki kwa kipaji hiki cha kueleza mareefu!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s