Je Ungefanyaje?

SAFRICA-POLITICS-HEALTH-MANDELA

Je ungefanyaje kama ungejua kwamba muda huu kuna mtu anapewa nusu ya malipo kwa kazi ya kukutoa uhai wako leo hii?

Je ungefanyaje kama ungejua kuna mtu yupo kwa wachawi akikufanyia uchawi ili kukusambaratisha?

Je ungefanyaje kama ungejua muda huu kuna mtu hapo ofisini kwako anaiba nyaraka zako muhimu ili ufukuzwe kazi?

Je ungefanyaje kama ungejua kuna mtu muda huu anatengeneza ujumbe wa uongo ili kuvuruga ndoa yako?

Je ungefanyaje kama ungejua kwamba muda huu kuna mtu anapanga kumteka mtoto wako ili wakudai pesa?

Je ungefanyaje kama ungejua kwamba rafiki yako wa karibu yupo busy sana kushirikiana na wabaya wako kutaka kukuangamiza?

Je ungefanyaje iwapo ungejua kuwa jirani yako amepanga kuchoma moto nyumba yako usiku wa leo?

Je ungejuaje iwapo ungejua kama kuna mpango unapangwa ili kusababisha ufukuzwe chuoni?

Pamoja na hayo yote, Mungu amesimamisha malaika wake ili wakulinde na kukupigania kwa kila baya litakaloinuka juu yako katika maisha yako. Tusichoke kumuomba na kumshukuru Mungu kwa maana hatujui ni mambo mangapi mabaya anatuepusha nayo kila siku ya maisha yetu.

Siku njema

–Dennis Kwambiana Mponji

 
Advertisements

11 thoughts on “Je Ungefanyaje?

 1. nimefarijika na ujumbe kiukweli yote katika yote ni MUNGU pekee ashikiliaye maisha yetu

 2. Mimi nlishawahi kugundua kuwa rafiki wangu wa karibu kabisa alikuwa akishiriki KUKWAMISHA shughuli yangu fulani. Nilichofanya baada ya kugundua hilo nilijitenga nilijitahidi shughuli yangu hiyo isipitie tena kwenye anga zake. Nikajitenga naye. Huku urafiki ukiendelea. Mwishoni mambo yake yaliharibika. Akja kuniomba msaada wa kipesa. Sikusita. Nilimsaidia kwa kadri nilivyoweza. Nilipokwama nlimwambia Nimekwama.

  Katika hili nilijfunza KUCHUKUA HATUA ninazo weza mimi na ambazo ziwezi NIMUACHIE MUNGU. Pia nikaona kumbe wakati mwingine yawezekana kuruhusu DHAMRI ya mtu IMSHITAKI. Nakama IMEKUFA basi Mungu atashughulika Naye.

  Yako Matizo ambayo TWAWEZA CHUKUA HATUA ZA KIBINADAMU kama vile kuripoti kwenye vyombo vya habari au kumuona muhusika moja kwa moja na pale ambapo HAIWEZEKANI kibinadamu TUNAMWACHIA MUNGU!

 3. Maisha yetu yote yako kwenye maamuzi ya Mungu,anaamua siku zetu,usalama wetu,amani yetu na kila kitu chema kwa ajil yetu.Utukufu na heshima ziko kwake milele

 4. Je ungefanyaje kama ungejua kwamba muda huu kuna mtu anapewa nusu ya malipo kwa kazi ya kukutoa uhai wako leo hii?
  = Kwa hakika kwa kua ninajua huyo Mtu yupo basi sheria za Nchi zipo na kuua au aina yoyote ya attempt kuua ikithibitika, ni hatia kubwa ivyo ningempeleke mahakani haraka sana maana mamlaka za Wanadamu zimewekwa na Mungu kudeal na mambo kama hayo, hakuna haja ya kusumbua wa Mbinguni kuwatia pressure na maombi ya kupanic kugwaya kufa.
  Je ungefanyaje kama ungejua kuna mtu yupo kwa wachawi akikufanyia uchawi ili kukusambaratisha?
  = Ningetamka Neno tu kwa kumaanisha..’Hakuna uchawi juu ya Israel mie na kila silaha inayolengwa kwangu, naimuru kufutika, over and out, kisha am serious nachukua Fanta bariiiiiiidii sana nakunywa kwa amani, furaha na full confidence ktk Bwana, simple yet powerful., wala sitaomba au kufunga unless kuna special Holy Spirit readings kule chumba cha ndani.
  Je ungefanyaje kama ungejua muda huu kuna mtu hapo ofisini kwako anaiba nyaraka zako muhimu ili ufukuzwe kazi?
  = Namwekea mtego ili nimkamate live na ushahidi kisha nashitaki baraza la migogoro na usuluhishi la Kazi kwa hatua kali sana za kinidhamu dhidi yake, wala sitaomba, sheria zinamtia akili na adabu.
  Je ungefanyaje kama ungejua kuna mtu muda huu anatengeneza ujumbe wa uongo ili kuvuruga ndoa yako?
  = Ningemwambia/tonya Mke/Mume wangu in advance hence hata yakija hayo madudu, ni full love to each other, haisumbui na wala hakuna haja ya maomb hapo, simple! Right?
  Je ungefanyaje kama ungejua kwamba muda huu kuna mtu anapanga kumteka mtoto wako ili wakudai pesa?
  = Mawili..ningemtegea na akakamtwa na Polisi and story is over, au asinge toka ndani siku iyo
  Je ungefanyaje kama ungejua kwamba rafiki yako wa karibu yupo busy sana kushirikiana na wabaya wako kutaka kukuangamiza?
  = Najiepusha naye from tha time on nilipojua pia nitamface na kublast niki mwambia aache tabia iyo chafu wala sitambughudhi Mungu ashughulike na minor case kama iyo iliyo saizi yangu kabisa
  Je ungefanyaje iwapo ungejua kuwa jirani yako amepanga kuchoma moto nyumba yako usiku wa leo?
  = Natafuta ushahidi wa bila kuacha shaka kisha naita police na later mahakami-huyo ni muhalifu, hapaswi kuombewa bali ni kuweka chini ya vyombo vya mamlaka za wanadamu wamsulubi na atanyooka tu
  Je ungejuaje iwapo ungejua kama kuna mpango unapangwa ili kusababisha ufukuzwe chuoni

  = Nimekosa nini kwani mpaka nifukuzwe? Kama kosa ni langu, nastahili na hakuna kuitisha maombi, nitimuliwe tu si niliyataka mwenyewe but kama ni uonevu tu, nina shitak ktk baraza la Chuo na sitafukuwa kamwe kwa hatua izo tu hata bila maombi as long as nina haki.

  PLZ NOTICE: Majibu yangu yangekua tofauti kama NINGEKUA SIJUI KUA WAKO HAO/HAYO kwa hakika, but kama najua kabisa, ashukuriwe Mungu maana, si wakati wa maombi huo bali niwakuwakabili kilive au Serikali/Mamlaka za Wanadamu zilizowekwa na Mungu kutusaidia sisi Wanadamu

  Press on

 5. Hakuna zaidi ya kusamehe na kuendelea kumpenda na kutenda mema siku zote!cku zote ibilisi hutafuta kamwanya kadogo tu ili atuangushe!Ucpo msamehe adui yako,utakapomchunia yaani ucongee nae!au wengine utackia nimekusamehe ila cjakusahau!Ujuwe tayari ibilisi kakupata.So hakuna zaidi ya kusamehe hata iweje coz Mungu ametufundisha kusamehe kwanza!Utawezaje kuomba rehema kwa God wakati wewe huwasamehi wanaokuudhi?No janja zaidi ya kusamehe na kusahau kabisaaaa!

 6. Swali zuri,na katika majibu yake, naanza kwa kurudia kipande kidogo cha swali, kwamba (UTAFANYAJE IWAPO UTAGUNDUA,UTAFAHAMU KAMA)nk.Kwa kua sasa umegundua kua kuna muuaji,mchawi,mwizi au muhalibifu wa maisha yako nk ,kumbuka si kwa nguvu zako bali MUNGU yu upande wako,warum 8:31 Azma za wabaya wako zilivyoshindwa ndipo ulipopata nafasi ya kutambua au kujua yale yaliyopangwa kutekelezwa juu yako,kama azma zao zingetekelezeka basi hata usingejua,kikubwa ni kusamehe na kumpenda adui wako kama unavyo jipenda ww tena samehe 7×70 maandiko yana usihukum ukaja kuhukumiwa ndio maana Yesu akasema “akikupiga shavu la kushoto mpe na jingine. zaidi muombee adui yako.

 7. Picha ya kwanza, inaonekana jamaa anakimbia kwa masihara sana kana kwamba hayuko hatarini!! Nimeitafakari sana na kuona jinsi sisi binadamu tunavyocheza na shetani kwenye anga zake za hatari.
  Kimsingi yuko kazi kutudhuru kwa sekunde hata moja tu endapo ulinzi wa Mungu utapungua kwetu. Unapojiona uko salama kwa wakati huo, jua kuwa, Mungu hajakuacha. HAtupaswi kusubiri tusikie mbinu za ibilisi za kutuangamiza ndipo tupige simu kwa Mungu. Kuna mbinu nyingi sana za ibilisi ambazo hata hatujazisikia, lakini ni za hatari zaidi. Mungu anatulinda sana kwa hizo tusidhurike.
  Ni wakati wa kumtafuta Mungu saa zote. “Yet the operations of the Spirit are always in harmony with the written word. As in the natural, so in the spiritual world. Human life is preserved, moment by moment, by divine power; yet it is not sustained by a direct miracle, but through the use of blessings placed within our reach. So the life of the Christian is sustained by the use of those means which Providence has supplied. He must eat of the bread of life, and drink of the waters of salvation. He must watch, he must pray, he must work, in all things giving heed to the instructions of the word of God, if he would “grow up to the full measure of the stature of a man in Christ Jesus.” {3SP 418.3}
  Blessed all

 8. kwa kweli sio jambo la kufikiria harakaharaka bali, mimi ningepeleka kilio changu katika mahakama ya rufaa ya mbinguni. kama hujapeleka uwe na ushahidi wa kutosha usije ukapeleka mashitaka ya kusingizia kwa hakimu mkuu. vita vyetu ni vya kiroho sio vya mwili na damu. Mungu na cabinet yake atafanya awezavyo. Mungu wetu hapendi kisasi anasema niachieni mimi namjua kuliko wewe. umsogezapo na faili lake usikose kulitaja jina lake kinaganaga.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s