Najivunia kuwa raia wa mbinguni!!

 neno

Ukiwa Mmarekani, Serikali Ya Marekani Itafanya Chochote Kukulinda Ama Kuhakikisha Usalama Wako… Ikitokea Adui Akamgusa Mmarekani Au Kumdhuru, Serikali Ya Marekani Huwa Hailichukulii Kwa Urahisi Jambo Kama Hilo…

Sipati Picha Ukiwa Mkristo, Raia Wa Serikali Ya Mbinguni; Mungu, Rais Wa Serikali Ya Mbinguni Anakuwa Ukuta Wa Moto Kukuzunguka Na Utukufu Ndani Yako, Anakuzunguka Kama Milima Iizungukavyo Yerusalemu, Anakuwa Adui Wa Adui Zako, Anakuwa Ngome, Kimbilio, Msaada Na Nguvu Zako… Huhitaji GPS Kwa Ajili Ya Kuku-locate; Amekuchora Kwenye Kiganja Chake, Kuta Zako Zi Mbele Zake Daima, Jicho Lake Linazungukazunguka Duniani Ili Ajionyeshe Mwenye Nguvu Kwa Ajili Yako, Anakupa Fursa Ya Kuwa Mrithi Pamoja Na Kristo, Anakuhakikishia Kukupatia Hazina Za Gizani Na Kukupa Kabila Za Watu Kwa Ajili Ya Maisha Yako, Anakuhakikishia Kustawi Mjini Na Mashambani, Anakufungulia Mlango Wa Mafanikio Kwa Kila Ulifanyalo Sawa Na Mti Uliopandwa Kando Ya Vijito Vya Maji, Anakupa Uhakika Wa Kuwa Juu Tu Na Wala Sio Chini… Anakupa Access Ya Kufanya Mawasiliano Moja Kwa Moja Na Yeye Kupitia MTANDAO Huitwa JINA LA YESU, Ambao Unakuhakikishia Kushughulikiwa Kwa Hitaji Lako!

Haiishii Hapo, Anakuwekea Majeshi Ya Malaika Ili Wakulinde Na Kukuokoa, Na Anawaagiza Wakuongoze Hadi Mahali Alipokutengenezea, Wanakuwa Pamoja Nawe Muda Wote Maana Hao Ni Watumishi Wako Wewe Utakayeurithi Uzima Wa Milele!

Kubwa Zaidi, Unao UZIMA WA MILELE; Aina Ya Uzima Alionao Mungu, Unaokupa Tiketi Ya Kufanya Vitu Kwa Kiwango Cha Mungu…Kwa Leo Inatosha Mwanafunzi Wangu Mwema!

AM PROUD TO BE A CHRISTIAN; THE CITIZEN OF HEAVEN AND THE AMBASSADOR OF CHRIST ON EARTH! 

–Conrad Conwell
Advertisements

7 thoughts on “Najivunia kuwa raia wa mbinguni!!

 1. Wapendwa,

  Biblia iko wazi……kuanzia Agano la Kale na Jipya, Mungu ana watu aliowaita kwa KUSUDI LAKE…….Mungu kwa kutumia binadamu hao hao aliowaumba…..huita watu wa ajili yake…..unaweza kuanzia NUHU……ABRAHAM……taifa la ISRAEL na hadi kuendelea Agano jipya….na mwisho ni zama zetu hizi……!
  Hivyo basi Mungu anatoa ulinzi, na na kila anchokitaka ( iwe afya…..uponyaji…..uzima…..fedha na kila aina ya Baraka ) kwa aliowaita, aliowachagua ili kutimiza KUSUDI LAKE…..

  Kwa kukubali wito huu wa Mungu, hakuondoi kutembea katika adha na dhiki au tabu…angalia mapito ya watu wote walioitwa na Mungu….kuanzia MWANZONI KABISA…….! Ikumbukwe tunaishi katika ulimwengu ulioanguka…..na Mungu mwenyewe anaandaa Ulimwengu mwingine……ambayo Biblia inasema….”KISHA NIKAONA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA KWA MAANA MBINGU ZA KWA KWANZA NA NCHI YA KWANZA IMEKWISHA KUPITA……NAYE ATAFUTA KILA CHOZI KATIKA MACHO YAO….WALA MAUTI HAITAKUWEPO TENA….WALA MAOMBELEZO…..WALA KILIO……WALA MAUMIVU HAYATAKUWEPO TENA……KWA KUWA MAOMBO YA KWANZA YAMEKWISHA KUPITA…….

  Tatizo ni sisi kutojua nini MUNGU ANAFANYA na anaruhusu tupitie kwa kila wito binafsi binafsi kwa kila aliyekubali kujitiisha katika MAKUSUDI MAKUU YA MUNGU…..! Mateso……dhiki…adha……taabu…….ni mojawapo katika package inayoweza kuruhusiwa na Mungu mwenyewe ili kutukumbusha kuwa sisi ni wapitaji hapa sio kwetu……kutukumbusha pia kuna nguvu za giza…ambazo kwa kutumia adha na dhiki na masumbufu ya maisha ili kututoa katika KUSUDI KUU LA WITO WA MUNGU……! Lakini katika kila adha na dhiki na taabu……MUNGU AMESEMA KUNA MLANGO WA KUTOKEA……ATAKUWA NASI HATA UKAMILIFU WA DAHALI…….NA ADUI WA MWISHO AMBAYE NI KIFO HAWEZI KUTUTENGA NA UPENDO WA KRISTO……..Hivyo Mungu analinda watu wake….UKWELI UKO WAZI NDANI YA NENO LAKE……!

 2. Siyi,

  Naona Conrad hakulijibu swali lako la kwanza ambalo halihitaji Maarifa, na hivyo akayaendea hayo yenye kuhitaji Maarifa ambayo naona majibu yake ni yenye kutosheleza, sawa, bali hili swali jepesi uliloliuliza, hilo la kupewa Hazina za Gizani, hilo limeinua shauku ndani yangu ya kuzipokea Hazina hizo ambazo ulimwengu hauzijui!!!

  Siyi, hebu vuta subira kidogo, ninaziendea hizo Hazina, maana Ahadi hiyo ni yangu, punde nikiisha kuzipokea nitakuonesha nawe uzijue angalau kwa kuziona bali si kwa kuzishika, maana hamkawiyagi kuvuruga!!!

  Jipime mwenyewe kwa Ahadi hii:
  “Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.”
  (ISA. 45:3)
  Kama kifungu hiki hakimo ndani ya Biblia yako, basi usiwe na shaka, utaletewa mpya, ulisema unapenda KJV!!!

  Ubarikiwe!

 3. Edwin Seleli

  Ubarikiwe Mno MUNGU akupe Hekima na Maarifa mapya kila siku inayoitwa leo….Sisi ni Raia wa Mbinguni ambao tunamwakilisha MUNGU duniani kwa lugha nyingine ni MABALOZI,balozi ipo siku anaondoka anarudi katika nchi yake Original..nasi tutatudi siku moja katika Nchi yetu Ubarikiwe….Conrad Conwell

 4. Conrad Conwell

  Second para last statement yako hii…””Kwa Leo Inatosha Mwanafunzi Wangu Mwema”… hakika kwa this simple, short and lovable msg, nimekua Mwanafunzi wako maridadi kabisa kumeza hii mana. I am telling you Mwalimu wangu, nimependa na nimebarikiwa sana, tamu kabisa hii kitu.

  Ooh Yes, these facts are true kabisa from these scriptures kuhusu subject yako…Kufurahia/Kujivunia Uraia wetu wa au Makaazi yetu ya JUU, si waTZ, KENYA, SCANDINAVIA au kwa Mzee Madiba chini uko.

  Waf.2:19…..sisi si wageni au wakimbizi bali ni fellow WENYEJI na Watakatifu wengine nyumbani mwake

  1Petro.2:9. Sisi ni uzao MTEULE, UKUHANI mtakatifu, TAIFA takatifu, WATU PEKEE wa Mungu tulioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyetuita kutoka gizani na kutuingiza katika nuru yake ya ajabu

  Yohana.14:1-3..Sisi Makao yetu si hapa bali yanaandaliwa JUU uko

  Ufunuo.21:3…Yeye Mwenyewe ana-enjoy Maskani yake kua na sisi, anapenda uwepo na kampani/fellowship yetu naye kama Baba na Watoto wake wanavyopendana

  KWA NINI YOTE HAYO? ni kwakua……

  Matt.1:23….Originally Yeye ni Emmanuel..Mungu Pamoja nasi hapa na hasa zaidi kue JUU

  Therefore kwa kua tuko na uraia huo, tuna hadhi iyo, Yeye ana interest nasi kiasi icho, lazima atupe mengi, ajishughulishe nasi sana na kutugawia uliyosema kuzidi raia huyu wa Nchi maridadi kabisa ya dunia hii yaani USA. Ni kweli naungana nawe kusema..niko proud kua raia wa real MAJUU nikiwakilisha sana hapa Chini kama Balozi matata sana wa Serikali yangu kuuu mno ya JUU.

  Press on,

 5. CHANGAMOTO ZOTE WANAZOKUTANA NAZO WATU WA MUNGU [ZISIZOONDOA AMANI NA FURAHA YAO] NI MITIHANI TOKA KWA MUNGU KUPIMA UPENDO NA IMANI YAO KWAKE, NA LENGO LAKE NI ILI KUWAPANDISHA HATUA NYINGINE YA UTUKUFU… LAKINI YALE YANAYOLETA MAUMIVU NA MATESO, NA KUONDOA AMANI NA FURAHA YETU YANATOKA KWA ADUI, NA KAMA TUKIMPINGA ANATUKIMBIA (Yakobo 4:6-7)

  MATATIZO MENGINE YANATOKANA NA KUKOSA MAARIFA SAHIHI YA NENO LA MUNGU NA HAKI ZAO (Hosea 4:6)

 6. Conradi,
  Mimi nimefurahishwa sana na fundisho lako mjoli. Bwana akubariki sana. Naomba nikuulize kidogo;
  1. Hazina za gizani atakazokupa Bwana ni zipi hizo?
  2. Umesema kuwa ukiwa raia wa mbinguni, Bwana atakuinua juu daima kwa maisha ya hapa duniani – popote mjini au shambani. Je, matatizo yanayowapata watu wa Mungu, kwa yanawatokea? Au huwatokea kwa sababu hawajawa raia wakamilifu wa mbinguni?
  Tuko pamoja ktk kujifunza

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s