Vuka Historia Yako

conieee
Bwana YESU Asifiwe, kwanza nataka ujue kuna watu HISTORIA ya Maisha yao imesimama hapo hapo haiendi mbele wala hairudi Nyuma,Wakati Mwingine hali hii imesababisha hata watu wako wa karibu waone hiyo ni historia yako siku zote..Lakini nataka nikuambie HISTORIA HIYO leo inakwenda kubadilika,Watu wa karibu walimuona yule RAHABU kama ni kahaba aliyeshindikana na hata ndugu walikuwa wanamtegemea yeye na kazi ile ya Ukahaba,Ni kweli Rahabu alikuwa na msaada mkubwa sana kwa ndugu zake,lakini msaada ule ulikuwa na dosari (Shetani ndiye alikuwa anahusika) Rahabu alipochukua hatua ya kumsogelea MUNGU,MUNGU akambadilisha (Yoshua 6:25) “Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu,yule kahaba,na watu wa nyumba ya baba yake,na vitu vyote alivyokuwa navyo naye akakaa kati ya Israel hata leo;kwa sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko”..

Ukiusoma huu mstari kwa umakini utaona Kupitia Rahabu nyumba nzima waliokoka, Biblia inatuambia akakaa kati ya Israel hata leo (Maana yake akahesabiwa ni kizazi cha Israel) Hujanielewa? Ebu soma hapa (Waebrani 11:31) “Kwa imani Rahabu,yule kahaba,hakuangamia pamoja na hao walioasi;kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani” Unaweza ukaona Rahabu alifanya kitu kidogo sana lakini kwa MUNGU ni kikubwa sana…MUNGU akaona vema Amuweke Rahabu katika kundi la wazee wa IMANI (Waebrania 11:39) “Na watu wote hao wakiisha kushuudiwa kwa sababu ya imani yao”

Ebu leo Vuka historia yako “Bwana yu pamoja nawe Ee shujaa (Waamuzi 6:12b) Vuka Historia yako leo,yawezekana una ugonjwa ambao waliumwa Babu/Bibi zako au Baba/Mama zako,yawezekana unahistoria ya kujikaata kuwa wewe haufahi au kuna dhambi umetenda unaona ni vigumu kurudi kwa MUNGU….Sikia nikwambie MUNGU anasamehe..Rudi leo….Rahabu aliporudi kwa MUNGU Historia MPYA ilifunguka katika maisha yake.

–Conrad

Advertisements

2 thoughts on “Vuka Historia Yako

  1. Yesu alitubaadilishia historia zetu kabisa,ukielewa neno linasema nin kuhusu kubadilika kwako ukaliamini na kuliishi mabadiliko yatatokea..

  2. Amina! Lakini Ndugu mpendwa tuombeane kwa Mungu maana Kubadili historia zetu tunahitaji mwongozo wa Roho na hivyo maombi ndiyo silaha yetu pekee ili kupokea hiyo nguvu kuushnda uovu! Si kwa kuamua tu kwa nguvu ya akili zetu na uwezo mkubwa wa kufikiria. Basi Mungu Mwenyezi na Atuongoze sana katika maisha haya tuweze kusimama kati ya malimwengu maana Mamlaka na uwezo na Nguvu ni vyake Mungu!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s