Wahubiri Kulindwa na ulinzi mkali!

Inakuwaje wachungaji kuajiri walinzi wa kuwalinda kila sehemu wanapokwenda? Ni kibiblia? Pichani ni Mchungaji Chris Okotie wa kanisa maarufu nchini Nigeria ambaye yuko kwenye orodha ya wachungaji maarufu wanaolindwa na ulinzi mkali hasa anapokuwa madhabahuni akihubiri.

Wahubiri wengi wanaanza kuonekana sehemu mbali mbali wakiwa na walinzi wao. Je, una maoni gani?

Advertisements

12 thoughts on “Wahubiri Kulindwa na ulinzi mkali!

 1. HEBU TUANGALIE MUNGU ANAVYOLINDA WATU WANAOFANYA KAZI YAKE KATIKA BIBLIA.

  MATENDO 18:9,10
  “BWANA AKAMWAMBIA PAULO KATIKA MAONO USIKU,USIOGOPE, BALI NENA, WALA USINYAMAZE, KWA KUWA MIMI NIPO PAMOJA NAWE, WALA HAPANA MTU ATAKAYEKUSHAMBULIA ILI KUKUDHURU; KWA MAANA MIMI NINA WATU WENGI KATIKA MJI HUU”

  MUNGU HUWAANDALIA WATU MAALUMU WA KUSAIDIA WATU WAKE SI WAO KUJIANDALIA/AU MAADUI WAO KWA WAO KUDHURIANA/KUPISHANA

  YEREMIA 26:24
  “LAKINI MKONO WA AHIKAMU, MWANA WA SHAFANI, ALIKUWA PAMOJA NA YEREMIA, WASIMTIE KATIKA MIKONO YA WATU AUWAWE.”

  DANIEL 6:24
  “MFALME AKAAMURU, NAO WAKAWALETA WALE WATU WALIOMSHTAKI DANIEL,WAKAWATUPA KATIKA TUNDU LA SIMBA”

  MATENDO 23:24
  “AKAWAAMBIA KUWEKA WANYAMA TAYARI WAMPANDISHE PAULO, NA KUWACHUKUWA SALAMA KWA FELIKI LIWALI.”

  MATENDO 9:25
  “WANAFUNZI WAKE WAKAMTWAA USIKU WAKAMSHUSHA UKUTANI, WAKIMTELEMSHA KATIKA KAPU”

  JOSHUA 2:14, 4
  “NDIPO AKAWASHUSHA KWA KAMBA DIRISHANI, MAANA NYUMBA YAKE ILIKUWA KATIKA UKUTA WAMJI; NAYE ALIKAA UKUTANI.”

  YESU ALIPOKUJA HAKUTANGAZA VITA YA UPANGA NA MARUNGU.

  MATHAYO 26:52
  “NDIPO YESU AKAMWAMBIA, RUDISHA UPANGA WAKO MAHALI PAKE, MAANA WOTE WAUSHIKAO UPANGA, WATAANGAMIA KWA UPANGA.

  WATUMISHI WA KWELI WAMEUFISHA MWILI KWA AJILI YA KRISTO.

  MATENDO 20:24
  “MALAKINI SIYAHESABU MAISHA YANGU KUWA KITU CHA THAMANI KWANGU KAMA KUUMALIZA MWENDO WANGU NA HUDUMA ILE NILIYOIPOKEA KWA BWANA YESU, KUISHUHUDIA HABARI NJEMA YA NEEMA YA MUNGU”

  YOHANA 6:63
  “ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA, MWILI HAUFAI KITU;

  WATUMISHI WA KWELI WANATAMBUA UKIHUBIRI INJILI YA KWELI LAZIMA MAADUI WATAKAOKUTIA KATIKA DHIKI WAPO LAKINI ULINZI WA MUNGU TU NI PEKEE.

  MATENDO 20:23
  “ISIPOKUWA ROHO MTAKATIFU MJI KWA MJI HUNISHUHUDIA AKISEMA, YA KWAMBA VIFUNGO NA DHIKI VYANINGOJA”

  MATENDO 14:22
  “WAKIFANYA IMARA ROHO ZA WANAFUNZI NA KUWAONYA WAKAE KATIKA ILE IMANI, NA YA KWAMBA IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA NJIA YA DHIKI NYINGI.”

  NINI WALIFANYA WATUMISHI WALIPOFUKUZWA NA KUTOLEWA NJE YA MIJI

  MATENDO 13:50,51

  “LAKINI WAYAHUDI WALIWAFITINISHA……51..NAO WAKAWAKUN’GUTIA MAVUMBI YA MIGUU, WAKAENDA IKONIO.”

  MATENDO 18:10
  “WALA HAPANA MTU ATAKAYEKUSHAMBULIA ILI KUKUDHURU; KWA MAANA MIMI NINA WATU WENGI KATIKA MJI HUU”

 2. ndiyo hivo kaka yaani Mungu anakuwa na jaribiwa na angalieni tusije tukafikia pabaya kweli na huu ndiyo mwisho wa mambo yote.

 3. Ukweli halisi ni kwamba Dhambi ni uasi utokao moyoni. Swala ambalo limezuiliwa kwenye biblia ni ibada za sanamu. Haya mengine ni udhaifu ndani ya wokovu yaletayo mitazamo ya kibinadamu.
  Lakini imani yako ndiyo inakuendesha katika kumjua Mungu na nguvu zake.
  8-)JAMANI MUNGU KAMA MUNGU ANAJITOSHELEZA MAANA YEYE NI ZAIDI YA VITA VYA DUNIA
  AU NYUKILIA8-)
  Mungu hatumjui kwa mazoea bali kwa uvuvio wa roho mtakati.

 4. Kaka hao ni wasanii tu,kufanya miujiza ndo faninyao.
  Yesu alishatahadharisha yote hayo kabla hayajatokea.kuhubili wanahubili ila wanajua wanaemtumikia wenyewe maana kumtaja Yesu so tatizo,tatizo ni agizo kuu alilotuagiza Baba

  Kama Yesu ndo MLINZI ,hao wengine ni akina nani kama sio mbadala wake,hawajiamini tatizo

 5. It is amaizing,ukiona hivyo ujue kuna mambo wanayafanya ambayo ni kinyume na matakwa ya utumishi wa Mungu.

 6. Nakubaliana na majibu ya Mabinza LS, ni mara ngapi kwenye neno la Mungu tumeona Mungu akiwaokoa watumishi wake na maadui zao? Kwani Mungu anabadilika? Yesu Kristo ni yeye yule jana leo na milele Waebrania 13:8

  Walio upande wetu ni wengi kuliko wao(maadui) 2Wafalme 6:16, na hata mitume Paulo, Petro wakiwa gerezani tena kwenye ulinzi mkali Mungu hakushindwa kuwaokoa. Ikitokea mtumishi wa Mungu ambaye anamtumikia Mungu kwa roho na kweli amekutwa na jambo la kutishia maisha , mimi naamini hakuna kitakachoweza kumuondoa labda Mungu mwenyewe aruhusu kama kwa Stefano. Mungu anazo njia nyingi za kumuokoa mtumishi wake na adui, wa kimwili au kiroho.

  Naomba tuangalie neno la Mungu kwa undani kabla ya kutoa majibu, maana ni kweli vita vyetu si juu ya damu na nyama.

 7. Hamjambo wapendwa?

  Mtumishi anayejua kuwa anamtumikia Bwana wetu Yesu kristo, ni lazima ayajue masharti na maelekezo ya kiutendaji kama yanavyoelekezwa na Yesu mwenyewe. Kusema kwamba lazima tuzitizame factor fulani zingine zidi ya Biblia ni uongo ambao hauwezi kamwe kupita bila kupingwa!

  Nakubari kabisa kwamba, kutafuta walinzi ili kujilinda ni vema, kwa sababu mtu anayefanya hivyo yupo kimwili, na Biblia inasema, “kilichozaliwa na mwili ni mwili …..” Lakini si busara na si vema jambo la kiroho kulifanya kimwili! Mtu anapomwendea Mungu lazima ajue kuwa yeye yuko, na kujuakuwa Mungu yupo au yuko ni lazima umjue, uwe unamfahamu na uwe ulishamuona na pia huwa mnaonana!

  Mtu anayemjua Mungu anazijua na nguvu zake, na mtu anayemfahamu Mungu ni lazima awe anazifahamu sheria, taratibu na kanuni zake. Biblia inasema “Vita vyetu si vya mwili….” kwa maana hiyo, vita vyetu ni vya kiroho. Mtu anapojilinda kimwili wakati anatumika kiroho anakuwa hajafikia kwenye uelewa halisi, hajui na hazitambui nguvu za Yesu kristo ambaye ni Mungu anayedai kuwa anamtumikia.

  Yesu alimwambia Petro “rudisha upanga wako katika ara yake, atakayeua kwa upanga atauawa kwa upanga…..”. Unapojilinda kwa kimwili kwa kazi ya kiroho tena kwa siraha, adui wa mwili akitokea utamtofautishaje na yule wa kiroho? Na inawezekanaje mwenyekazi yake aliyekupa, huku akijua kuwa ni ya hatari naye asikupe ulinzi? Ikiwa vile, basi wewe unajifanyia tu kazi ile kwa njaa zako lakini hayapo makubariano wala mkataba wa kazi hiyo unayodai kuwa wewe ni mtumishi wayo! Umeajiriwa, vitendea kazi unajitafutia mwenyewe uliona wapi, na ni kifungu kipi cha sheria za kazi ya Mungu?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 8. Kwa upande wangu mtumishi kuwa na walinzi wanaomlinda si kibiblia, ni namna ya hekima za kibinadamu, ni kama unamsaidia Mungu. BWANA MUNGU asipoulinda mji wakeshao, wanakesha bure.

 9. Kwa mtazamo wangu sio dhambi kuwa na ulinzi binafsi, mfano mlinzi wa nyumbani lakini hii ya kuwa na mabounsa uwapo ibadani tena mimbarani ukihubiri ,inaonyesha kwamba umejijengea maadui wengi kuliko marafiki,
  Yawezekana kwamba unabiashara nyingine ambazo unazifanya kwa dhuluma ndio maana unawindwa na wale uliowadhulumu,Lakini kama wewe ni mchungaji tu ambaye main business yako ni kuitangaza injili ya Yesu Kristo aliye hai then huna haja ya kutembea na mabounsa.

 10. Ingawa ni Mungu analinda Uhai na Maisha ya Wanadamu in general terms, pia katupa utashi wa kufanya mema pia kwa ajili yetu, hence tunakua na Walinzi wa Mtu-Mhubiri, Mwenye Nyumba Home, Rais, Super star nk…Wanalinda MAISHA/UHAI wa mhusika usiharibiwe au kutolewa kirahisi au kienyeji labda mpaka Mungu aamue kuuondoa Yeye na siyo mhuni tu au mvuta bange au mwenye wivu na mhusika au mpinzani tu wa Rais au Mhubiri.

  Timu ya Yesu ile ya 12 ilikua si tu kwa ajili ya injili na kufunza, it also served the purpose ya kum-protect Bwana Kimwili maana alikua mwili na mwanadamu pia-angalia attempt ya Peter kutaka kuramba shingo ya mvamizi yule, akaepa, kisu kikatua kwa sikio na ikawa kwaheri-Ingawa Yesu alimrekebisha na kusema-(akaingia ktk Uungu tena) –kua kuna convoy ya kutisha ya Malaika-angeweza ibonyeza na ikafanya mambo ya hatari pale-yet ni ushahidi kua walikua pia na Ulinzi role maana unapokua na Bwana Mkubwa na wewe ni bwana mdogo, hata usipoambiwa, utafanya kazi ya ulinzi fulani ivi au u-body guard.

  Kama Wahubiri wamejikuta wanafanya kazi ktk mazingira hatarishi kwa maisha yao, hata mie ningetaka ulinzi wa kumzidi Obama-wee! Nani afe hapa! Life sweet kabisa bwanaa! Tusidanganye! Nani afe kienyeji tu kisa mkorofi mmoja amefyumu napopiga injili nagusa angle zake halafu anajaa upepo kuja kunichapa au analipa vijana wa kihuni kunivurugia Mkutano au mimi mwenyewe nashushwa toka kwa jukwaa wakati nachapa fire-fire Neno. Katika hali kaka iyo, Kwakweli hapo natengeneza kikosi hatari cha kimwili- Kikosi cha maombi wakae kanisani kuniombea na kuwaombea hao jamaa wa kazi-kikosi cha kimwili hatari( full makaratee, pistol, kunfuu huu—haa, sarakasi nk)

  Lakini kama nahubiri maeneo shwari tu-ndani ya Kanisa, Nchi ya Amani, vijiji vya ushwari, hakuna fujo wala kitisho cha kuindoa roho yangu niaache family na mke wangu maskini akiwa mjane buree, kama nahubiri kwa watu si watata, basi Kutumia walinzi ni ubishoo tu, kiburi cha uzima, ulevi wa mafanikio ktk huduma. Mtumishi Mnyenyekevu atakua makini na roho iyo ya kiburi, majivuno na kuji-show off.

  Kwahiyo, kuhukumu haraka-haraka kua haifai Wahubiri kua na Walinzi-ni kutoangalia factors zingine na kusema tu inafaaa Wawe nao Walinzi pia itakua umeacha kuzingatia mengine.

  Press on

 11. Nionavyo mimi haipendezi kwa sababu Mungu peke yake kupitia Malaika wake ndio hutulinda sisi tumwaminiye. Hiyo ni kwa upande mmoja, upande wa pili ni kwamba kwani kila kitu tufanyacho Wakristo lazima kiwe KIBIBLIA? Kwani ww umeleta mjadala huu kupitia kifungu gani cha biblia kilichokuambia kuanzisha mjadala hapa SG?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s