Kutoka bungeni na Mchungaji Msigwa!

msigwapicha

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), amesema asilimia 40 ya Baraza la Mawaziri limedumaa kwa sababu limeshindwa kutekeleza majukumu yake.asilimia 40 ni sawa na mawaziri 20

Alitoa kauli hiyo bungeni mwanzoni December wakati akichangia mjadala wa taarifa za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.

Alisema kila mwaka wabunge wamekuwa wakizungumza mambo yale yale na serikali imekuwa ikijibu vilevile wakati matatizo yale yale yameendelea kuwepo.

“Bunge la mwaka juzi la Bajeti nilitoa takwimu za Wizara ya Afya, kwamba asilimia 42 ya watoto wanaozaliwa Tanzania wamedumaa, mtu anayedumaa hawezi kufikiri, hawezi kuhoji wala kudadisi, kwa kutumia takwimu hizi hizi Baraza la Mawaziri ambao ni zaidi ya mawaziri 56, asilimia 40 wamedumaa na moja ya sababu ya kudumaa ni changamoto wanazozipata katika Bunge hili.

“Kila mwaka tunazungumza yale yale, tunapata majibu yale, watu hawabadiliki maana yake kuna tatizo kwenye akili zao.

“Matatizo ya wizi wa fedha lazima tuyapatie ufumbuzi, haiwezekani kila siku tuseme yale yale, matatizo yapo pale pale,” alisema.

Mchungaji Msigwa alisema lazima kuwepo kwa nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali na kuitaka serikali kuzikumbusha halmashauri kwamba nchi inaongozwa kwa mfumo wa vyama vingi. Hii ni mental problem haihitaji economical solution, Bali mental solution.

–Bungeni

Advertisements

35 thoughts on “Kutoka bungeni na Mchungaji Msigwa!

 1. Mabinza,

  Kwa nini unakwepa kusema, kama lililo moyoni mwako ni jema si useme wazi hapa kila mtu asikie? Nimekutaka useme huyo unayemwita baba yetu ni nani!

  Kama una akili timamu ulitakiwa kujua kuwa siasa safi lazima iwe imechanganyika na kweli ya Mungu ndani yake.
  Lakini ninavyojaribu kukuona ni kwamba u mjinga hata kwenye kuelewa maana ya siasa. Mtazamo wako juu ya siasa umetiwa giza, na giza hilo limejaza ujinga ndani yako kuhusu siasa.

  Hata hujui kwa nini Yesu alisema haombi ili tutolewe hapa duniani, bali aliomba tuendelee kuwa hapa ila tulindwe dhidi ya mwovu.
  Na sijui kama unaelewa maana ya sisi kuwa chumvi ya dunia(dunia inayosemwa hapa siyo hii sayari). Hatuko hapa duniani ili tujifiche makanisani kwetu kufanya maombi na kusoma biblia tu.

  So far, kama uko hapa duniani elewa siasa inakuhusu utake usitake. Wanasiasa ndio wanaopanga wewe uendesheje gari lako( kama una gari), ndio wanaopanga mtoto wako asome nini shuleni, ndio wanaopanga bei ya maji iwe shilingi ngapi, ndio wanaopanga mkutano wa injili uishe saa ngapi, ndio wanaopanga uhuru wako wa kuabudu, ndio wanaopanga uhuru wako wa kwenda nchi nyingine, ndio wanaopanga kutembea kwako iwe mwisho saa ngapi,n.k!

  Sijui kama kuna mtu yeyote mwenye akili timamu hapa ambaye angependa na kufurahia hayo mambo yote yafanywe na mtu mwovu asiyemcha na kumtumikia Mungu, wakati anajua kabisa kwamba wakishayapanga analazimika kuyafuata.

  Kama unaona mawazo yako yamezidiwa na hauna jipya,ni vema ukakubaliana na ukweli hadharani au kimyakimya, na ukanyamaza kuliko kuendelea kusema maneno-maneno yasiyo faida.

  Fikiri sawasawa!

 2. Sungura na Seleli,

  Jihadhalini!
  Make Mabinza ana hasira kama mbogo aliyejeruhiwa! Amebainisha hilo katika post yake aliyotuma akiwalalamikia sana kwa kitu mlichomfanya.

 3. sungura

  unasema kweli kuwa humjui baba yenu? Biblia katika Yohana inasema, “Mtoto hafanyi jambo isipokuwa kamuona baba yake akifanya” Jiangalie unafanana na nani, katika kuchanganya Neno LA Mungu na Siasa ?!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai”

 4. Ndg. Mabinza,

  Kwa asili binadam tumeumbiwa utu ndani yetu. Huruma hutoka katika huo utu. Watu wengine huuita ubinadam. Ukiona mtu hana huruma, ujue hana huo utu ndani yake. Si kwamba yeye hakuumbiwa huo utu, la hasha; bali ule utu umekufa ndani yake. Nini kimeua utu? The highest point of evil in us kill humanity. In other languange, when the spirit of evil take full control in us, kills humanity. That’s why you get some people acting devilic.

  Mfano mzuri upo kwenye government yetu kwa sasa. A group of evil people in the system is cruching this country bila huruma!!!! They are evil people. The great evil (the devil) has full control in them. God is the Spirit. He cannot act in the physical realm without using the physical body. So, He acts through people who are in the physical body.
  Satan likewise. In this, we perceive God’s works and evil works of the devil.
  Kuna watu kwenye government sasa hivi who are extremely evil. Hawana utu hata kidogo. Watu maskini wa kutupwa kwenye hii nchi kiasi kwamba kama una
  utu ndani yako, inatia huruma sana!!! But no one cares! A selfish greedy evil group in the government system is mercilessly crunching the country to its bones. Shetani hana utu. Kwa hiyo hana
  huruma. Kazi yake ni kuchinja na kuharibu!
  The church is watching from afar. The church takes no concern in the matter in the perspective: “The worldly things”
  Christians out of fear occasionly pray for
  peace. God is asking, “I’ve given you
  peace ever since, what have you done with it?”
  Tumeshuhudia watu wakiteswa na kuuawa kinyama kwa kujaribu kupinga uovu na kutetea haki. Na wengine si kwa
  kupinga uovu na kutetea haki, bali wanaokutwa katika njia ya kupitishia uovu, au katika harakati ya waovu kufunika uovu wao na kubaki katika system, nao wanauawa pia.

  Matthew 5:13;
  13.”You are the salt of the earth. But if the salt loses its taste, it cannot be made salty again. Salt is useless if loses its salty taste. It will be thrown out where
  people just walk on it.”

  We all know the function of the salt. Esp. that of preservation and giving
  flavour. The church is the salt in the evil
  world. It’s preserving the evil world from God’s anger. At the same time the
  church should have its flavour felt in the world. (in nation’s politics, in the governenment etc.)

  Ndg. Mabinza, kama nilivyoanza kuongea mwanzo hapo juu. Nilishikwa na huruma baada ya kusoma post yako iliyojaa lawama juu yetu (Sungura, Kaswahili na Seleli).
  Pole sana kaka!
  Ilikuja picha akilini mwangu nikakuona kama unagugumia kwa maumivu makali chini ya marungu ya kina Sungura. Mbaya zaidi Seleli akaja kuponda kichwa bila huruma!
  Pole kaka!
  Nakutakia upone haraka urudi tuendelee na mada zingine.
  Hawa kina Sungura na Seleli naona wazi kwamba si watu wa kuchezea aisee! Uswahiba wao naufananisha na wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na William Ruto. Make mmoja agonga kwanza, mwingine yupo pembeni anaangalia tu. Unatolewa manundu yakutosha tu, afu mwingine akija anamalizia, afu wanakaa pembeni wanaanza kucheka.
  Lakini mimi pia nadhani ni kwa 7bu umekosa back up. Siku nyingine nakushauri pengine usikubali kupigana pekee yako.
  Lakini nikupongeze tu kaka!
  Mchenzo ndivyo ulivyo. Katika kushindana kuna kushinda au kutolewa manundu.
  Pole sana kaka!

 5. Mabinza,
  Baba yetu nani, unayesema ‘Miyoni mwenu yamejaa hayo, kama alivyo baba yenu?

 6. HAYA TENA KUMEKUCHA KUTOANA AKILI!

  Kwako Sungura, Kaswahili na Seleli.

  Matusi yenu mimi nimeyapotezea, maana mambo kama hayo hutoka vinywani mwa wanasiasa! Mwanasiasa hajari chochote zaidi ya kuangalia watu wengi wanataka nini, wakitaka kuwekewa matuta katika Bahari ataunga mkono, wakitaka maji jangwani ataunga mkono, wakitaka udini ataunga mkono, wakitaka kutandaza mitumba na mboga mboga Barabarani ataunga mkono, yupo tayari kusimama akihutubu kuwa Mungu wa Wakristo ni sawa na mungu wa wahindi, waislamu, wachawi nk, kisa KURA! lakini Mungu husema njia iendayo uzima ni nyebamba (si ya watu wengi wape).

  Miyoni mwenu yamejaa hayo, kama alivyo baba yenu. Mnaishi kwa dhana na mitazamo ya Kimwili zaidi, mnadhani kwa Juhudi za kibinadamu Dunia itakuwa salama! Lakini Neno linasema, “ajizaniaye amesimama aanalie asianguke”, lakini kama tayari mtu amekwisha anguka aangalie asisimame? Shauri yenu, kila mtu hupewa anachoomba! Shetani anasifa nyingi tu, lakini zilizo kuu ni tatu KIBURI, UONGO na UUAJI!

  Seleli anajizungumzisha bila kufikiri akiwaunga mkono ‘ndugu zake wa baba mmoja’ ati akinisema, “..Anapenda kuongea vitu vyepesi kwa mneno mengiii! Mimi naona ufahamu ulio ndani yake una chembe ya maangamizi wala si uhai kama anavyodai kwenye kibwagizo chake”
  Kiburi chenu cha ujuaji na thiolojia, manadhani Mungu yumo humo, Mungu yumo katika URAHISI wa ajabu, katika kile usichotazamia humo ndimo yumo! Wenye Elimu na wenyekujiita wanajua kama ninyi, walipigwa chenga pale Nathareti, hadi mamajusi toka mashariki wanafika kumsujudia ndipo wanang’aa macho, ha! Wanaulizana wasomi, ati, “MAANDIKO YANASEMA ATAZALIWA WAPI?” Golgotha napo, hadi anakufa ndipo wanasitukia “HAKIKA HUYU ALIKUWA MWANA WA MUNGU!”

  Nanyi mtajua mwisho, na mtasema kwa vinywa vyenu wenyewe kuwa, “WACHUNGAJI WA KWELI WA KUNDI LA MUNGU HAWAKUPASWA KUTUMIKA KWA WAKATI MMOJA KATIKA UTUMISHI WA KITUME NA WAKATI HUOHUO KATIKA VYEO VYA KISIASA!” Nabii, moja ya kazi zake ni kumweleza mtawala na Taifa kwa ujumla, kile Mungu anachosema na anachotaka Mungu kifanyike, na mtawala anapotii hayo, huamini Neno la Mungu, na kwakuwa ameamini yasemwayo na Mungu, HUYO NDIYE HUITWA MTAWALA MWENYE HAKI! Biblia inasema, “Kwa kuamini mtu hupata haki” lakini Imani chanzo chake ni kusikia, kusikia Neno la Kristo. Kwa akili zenu (Sungura, Kaswahili na Seleli) Kazi ya kuwasikizisha Watawala na Taifa Neno la Mungu ambalo kwalo watu wawe na Imani ili wafanyike kua Taifa lenye haki ni Wachungaji kuwa wana siasa? Au mnaonaje, mkikutana na Yohana mbatizaji, mkamweleza kuwa manabii inafaa wawe wanasiasa, unadhani atakufanyaje akikumbuka yaliyompata pale Gerezani, apokuwa amewekwa kwa kosa la kumwambia Kiongozi wa kisiasa, atii Neno la Imani ili awe MTAWALA WA HAKI KATIKA TAIFA?

  Kinachoangaliwa hapa na watu ni ile KWELI, si swala la kujua kuchangia, kuandika vizuri, Kuandika kwa kifupi sana, ama kuwa wewe ni mjuzi, mwelevu, msomi na una akili sana. Sungura, utachanganyikiwa sana kama umeona mbwa vile, hadi nakuhurumia, nasema hivyo kwa sababu hujui kama tunajadili NENO LA MUNGU na wala siyo SIASA. Nakushangaa sana uliposema, “Nauchukia sana upumbavu wa watu wapumbavu wenye kusema kuwa siasa haiwahusu” MPUMBAVU MARA ZOTE HUSEMA KUWA MUNGU HAYUPO, Biblia ndivyo inavyosema, wala Biblia HAISEMI KWAMBA, MPUMBAVU HUSEMA SIASA HAIMHUSU MCHUNGAJI! Mtu anayesema Siasa haimhusu mchungaji, SIYO MPUMBAVU kwa mjibu wa Biblia, endeleeni kuweka cha mbele nyuma na cha nyuma mbele. Ila kwakuwa ni maisha yenu kuishi huku na huku, mnajionea sawa tu!

  Mimi naona kama ni hivi, mtafitinika sana, mnaruka hata mliyoyasema wenyewe, ndiyo sifa yenu WAONGO! Wewe Kaswahili hukusema kuwa, “kama mtu alikuwa mtumishi wa Mungu kanisani
  katika nyazifa nyeti kama uchungaji, anapochagua kuingia katika siasa yafaa akaacha kazi ya uchungaji.
  Hata mimi naonelea hivyo bw. Mabinza”HUKUSEMA????! Ati sikukuelewa! Kwani unauza vocha za simu?

  Munasema “naandika maneno mengi, lakini pumba!”jibu ni rahisi tu, ni kwamba, ACHENI KUSOMA WALA MSIYAFANYIE KAZI MPOTEE!

  “UFAHAMU NI CHEMBE YA UHAI!”

 7. Sungura,

  ……Mabinza take note pia………

  wow, wow, wow, yaani toka moyoni, nimekupenda sana kwa hiyo comment ya cementation uliyonijibu hapo juu, great and great indeed na nimeguswa sana na izo data on upuuzi unaofanywa ktk Nchi hii kwa kua na viongozi full uovu, maneno ya Mabinza kua tuko rohoni sana-manake sisi si wa hapa, tuyaacha tu ayo, ni kujifariji tu but joto ya jiwe lake upuuuuuzi huo wa waovu, anauramba na kuunywa barabara kabisa kwa majuto na mifungo ili Mungu abadilishe hali lakini ngoma ndio kwanza inaamka asubuhi, why? Maandiko yameshasema, akitawala muovu tu, wenye haki wanaugua, so what next? atawale mwenye haki, as simple logic as that! Mabinza huelewi nini wewe Kaka na best langu la siku tuko kuleee group-unakujua mpaka hapa wanguuuuu? aaaa bwanaaaa!

  Again, mi unanimaliza sana Sungura na kicheko na pin tena kama izi ha haha ha ha ha opsuuuuuuuu acha nipumuie mie, nacheka mpaka jasho Sungura, yaani ukiamua kua ktk business, u real mean it..inakumbusha mengi mazuri na matembo pori ya wakati wa mada ya Fungu la Ten mie na wewe hahahahahaha, uwiiiiiiii Sungura

  Look/feel/see the reality at these ”Kristapeni..hahahaha

  ”Anapenda kuongea vitu vyepesi kwa mneno mengiii!”

  ”Mimi naona ufahamu ulio ndani yake una chembe ya maangamizi wala si uhai kama anavyodai kwenye kibwagizo chake”

  Press on man..

 8. Seleli,
  Unajua nini ndugu yangu! Huyo mpendwa Mabinza sijui akili yake ikoje. Anakomaa na jambo utadhani ana point ya maana sana ndani yake, kumbe ukifuatilia unakuta ni utoto-utoto tu!

  Huyu naye ni design ya watu wanaosemwa na Mch. Msigwa kuwa ni wenye akili ndogo wanaotaka kutawala akili kubwa.

  Inapendeza sana unapochuana kwa hoja na mtu ambaye hata kama hukubaliani na msimamo wake, lakini hoja zake zina-make sense. Sasa Mabinza yaani anaudhi kweli, anaandika billa co-ordination yoyote ya kimantika. Lakini unakuta kaandika weeee!

  Anapenda kuongea vitu vyepesi kwa maneno mengiii!

  Hebu fikiria kama aliyekuwa anaingia mikataba ya madini yetu angekuwa na akili kama ya Daniel, kweli sisi tungebaki na 3% tu?

  Hebu fikiria kama kwenye halimashauri zetu za miji kungekuwa na watu kama Yusufu, kila mwaka kungekuwa na hati chafu kweli?

  Hebu fikiria wanyama wetu wangekuwa wanasimamiwa na mtu Daniel, kweli leo tungebakiwa na tembo elfu 13 kutoka laki 3?

  Hebu fikiria kama operation tokomeza ujangili ingesimamiwa na mtu kama Yusuf, mama na dada zetu kweli wangebakwa na kudharilishwa kiasi hicho kwa kuingizwa chupa sehemu za siri, ndugu zetu wangelazimishwa kufanya mapenzi na mama zao, kufanya mapenzi na miti, n.k?

  Halafu mtu kama Mabinza kwa akili nyepesi kabisa anasema sisi hayo hayatuhusu,ati ni mambo ya dunia hii!!!

  Mimi naona ufahamu ulio ndani yake una chembe ya maangamizi wala si uhai kama anavyodai kwenye kibwagizo chake.

  Kama hayo hayatuhusu si tungekuwa tunampokea tu Yesu anatuchukua kwenda mbinguni, why are we here then?

  Wenye wito wa kumtumikia Mungu katika siasa na serikali wajipange, sisi tutawapa support.

  Tunataka wenye haki watawale ili watu wote tuwe na furaha!

  Ubarikiwe Edwin!

 9. Sungura,

  Ivi unatowaga wapi hizi pin aisee hahahah…dah””Risasi hufanya kazi yake vizuri pale inapokutana na mfupa, kwenye minofu hata huwa haifanyi kazi kubwa.

  Nimefutilia hu mjadala kimya-kimya toka nimetoa comment yangu , sikutaka tu kuingia… lakini honest brother Mabinza kweli hujaelewa well done joby ya Kaswahili na Sungura? be honest, hujaelewa kweli?

  Ndio maana jamaa yangu unamfanya anachachamaa ivi..”Napata shida sana kusoma makala zako ndefu ambazo ndani yake zimejaa pumba za kutosha. Wala sikudhihaki kwa kusema kwangu hivi. Unapenda sana kuongea vitu vya kitoto kitoto ndani ya kikao cha watu wazima. And to be honest, I hate that behaviour of yours..

  Nadhani watu tujifunze-kua na moyo safi usio na madoa-doa ya kenge ili kuweza appreciate kama umepata kitu kipya na chema toka kwa mwenzio

  Press on and indeed i buy Sungura’s big statement kua si ufahumu ni chembe ya uhai bali ufahamu sahihi

 10. Mabinza,

  Kwanza nampongeza Kaswahili mbele zako kwa ustahimilivu wake na uvumilivu wa kuchukuliana na wewe.

  Risasi hufanya kazi yake vizuri pale inapokutana na mfupa, kwenye minofu hata huwa haifanyi kazi kubwa.

  Napata shida sana kusoma makala zako ndefu ambazo ndani yake zimejaa pumba za kutosha. Wala sikudhihaki kwa kusema kwangu hivi. Unapenda sana kuongea vitu vya kitoto kitoto ndani ya kikao cha watu wazima. And to be honest, I hate that behaviour of yours.

  Si lazima kila mada uchangie rafiki yangu, zingine zipotezee tu. Unaandika maneno mengiiiii, lakini unachomaanisha kukisema ndani yake ni kidogoo, na halafu si cha kweli vilevile.

  Mtu mwenye kusema maneno kama haya sidhani kama ni mtu sahihi wa kuendelea kujadili nae mada kama hii. Maneno yenyewe haya hapa; ” Sasa, kufikilia kuwa ‘akina msigwa’ wataleta ‘NAFUU’ ya maisha kwa watu wa Mungu, ambako kwa sasa wachungaji kama hao hawatambuliki kama Wachungaji wa kondoo wa Kristo, ni Ndoto ya mchana!

  Yakumbuke sana maneno haya kuwa ” Haki huinua taifa, na mwenye haki akitawala watu wote hufurahi” Kama huelewi kajifunze maana na matokeo ya taifa kuinuliwa.

  Nauchukia sana upumbavu wa watu wapumbavu wenye kusema kuwa siasa haiwahusu, lakini waovu wakitawala na kusababisha hali kuwa mbaya katika nchi, watu haohao(yaani wapumbavu) hutuhimiza watu wa Mungu tufunge na kuomba kwa ajili ya hao watawala waovu.

  Anyway, sihitaji hata kuendelea kupoteza muda na wewe hapa.

  Kwa kifupi ni hivi, wewe endelea kukaa hivyohivyo mpaka utakapoyaelewa mambo haya, utatukuta sisi( yaani akina Msigwa) ndio wale watu wenye haki ambao tunatakiwa kutawala ili watu wote wafurahi. Na wewe mwenyewe utafurahi.

  In fact hatutaki kutawala kwenye siasa tu, bali hata serikalini, na kwenye sekta binafsi, tunataka wenye haki watawale.

  Na mbinguni tunaenda pia!

 11. Kaswahili,
  “Is it a Jadgement day?”
  Tubishanie nini tena, iwapo Neno limekufikisha kwenye uelewa kwamba Mchungaji hafai kuwa Kiongozi wa Kisiasa hapa Duniani? Nilikuambia tangu mwanzo kuwa Maandiko hayaruhusu mtu aliye na cheo cha utumishi katika Serikali ya Mungu, kwa wakati huohuo atumike katika Siasa za ufalme wa kidunia. Lakini mkabisha sana wewe na Sungura mkiwanukuu akina Danieli, Daudi, Selemani, Yusufu nk. Kulinda hoja zenu! Namshukuru Mungu kwakuwa leo umekubali (Kaswahili) wazi kuwa haifai Mchungaji kuwa mwanasiasa. Tarehe, 12/01/2014 at 1:26 am. katika kipengele 14 umekubali, ati ukinigeuzia kitako cha bunduki kuwa,

  “14. Kwa hapa umeanza kusogea kwenye ukweli uliposema kwamba, kama mtu
  alikuwa mtumishi wa Mungu kanisani
  katika nyazifa nyeti kama uchungaji,
  anapochagua kuingia katika siasa yafaa akaacha kazi ya uchungaji.
  Hata mimi naonelea hivyo bw. Mabinza. Maana hizi nyazifa zote mbili ni kubwa
  na zinahitaji muda mwingi ku-
  concentrate kiasi kwamba ni vigumu kuzi-handle zote kwa pamoja sawasawa…….”

  Hukumu husimamia hoja iliyokuwa inabishaniwa. Katika hili, hoja ilikuwa ni moja tu ni kwamba, KUONA KAMA NI VEMA MCHUNGAJI KUWA MWANASIASA WA SIASA ZA KIDUNIA NA HAPO HAPO KUWA MCHUNGAJI WA KANISA LA MUNGU. Hiyo ndiyo iliyokuwa hoja, mambo mengi yaliyopitapita hapo ni majumuisho ya hoja ili kupata kipi ni kipi alimladi kila mhusika alinde hoja zake kwa mjibu wa Neno la Mungu. Kwa hiyo basi, hukumu ya kweli lazima imalize shauri kwa kuzingatia hoja iliyofikishwa Mahakamani hapo na Mdai (Plaintiff) chini ya ‘kiapo’ (Afidavit) na si kuzingatia hoja (Startment of defence) mpya zilizoingizwa na mdaiwa (Deffendant) inje ya “Kiapo”Maana KIAPO HAKIREKEBISHWI!

  Kaswahili, Mtu akiacha kazi katika Kampuni “A” na kuajiriwa kampuni “B”, Kampuni A linakuwa halimtambui, hivyo hutakiwa Kurudisha vitendea kaz vya kampu ambako ameacha kazi, kama aliwahi kupewa kikiwemo na KITAMBURISHO kilichokuwa kikimtambulisha kuwa yeye ni mfanya kazi wa Kampuni “A”, vitendea kazi pamoja na kitambulisho husika analazimika kupewa na kutumia vya Kampuni “B”!

  Umesema, “…..katika nyazifa nyeti kama uchungaji,
  anapochagua kuingia katika siasa yafaa akaacha kazi ya uchungaji……..”

  Kwa tamko lako hilo ambalo kwakweli linakubaliana na Neno la Mungu, ni wazi kuwa, Wachungaji kama ‘Akina Msigwa’ hao SI WACHUNGAJI tena! Walishaachishwa kazi ile, walishanyang’anywa kila kitendea kazi hadi kitamburisho! Hawatambuliwi na mmiliki wa awali, wanatumika kwa mwajiri mpya. Na sote tunajua kuwa, KIONGOZI HAWEZI KUWATAFUTIA MASLAHI MAZURI WATU WASIO WA KAMPUNI ANAYOIONGOZA! Sasa, kufikilia kuwa ‘akina msigwa’ wataleta ‘NAFUU’ ya maisha kwa watu wa Mungu, ambako kwa sasa wachungaji kama hao hawatambuliki kama Wachungaji wa kondoo wa Kristo, ni Ndoto ya mchana!

  In Jesus’ time, there were no printing presses, no television and no internet. God’s chosen method of spreading the Good News was person to person to person.

  Jesus Trained His Followers
  Jesus’ followers learned mostly by spending time with Him, watching and listening as He taught others. When they were ready, He gave specific instructions and then sent them on a mission:”The Lord now chose 70 other disciples and sent them to all the towns and places He planned to visit” (Luke 10:1). – GoodLife.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 12. Bw. Mabinza,

  Salaam!
  Kwanza kabisa nakupongeza na nakushukuru kwa kuanza taratibu kudondosha silaha na kuinua mikono juu; si ku-surrender kwa Kaswahili au Sungura. Bali ku-surrender mbele ya
  kweli. Nakunukuu kwa maneno yako mwenyewe hapa chini:

  Kwanza amini kuwa, sipingi kabisa kuongezeka watu kuwa kama ‘akina Msigwa’ (kwakuwa wapo!) na pia sisemi KUSIWEPO KUCHANGANYA NENO LA MUNGU NA SIASA, maana Neno ndilo
  linalosema hivyo. Vile vile niwaweke wazi na muelewe kuwa, DINI NA SIASA HAVICHANGANYWI SASA,
  VILISHACHANGANYWA TANGU ZAMANI, NAWEZA KUSEMA DINI NA SIASA NI
  KITU KIMOJA! Dini ni taasisi kama zilivyo
  taasisi zozote Duniani, Dini husajiriwa
  kwa mjibu wa taratibu za kisheria za Nchi husika, lakini bila Siasa haiwezi kuwepo Tasisi yoyote kwakuwa Siasa
  ndiyo ‘Tool’ inayoendesha Taasisi yoyote ile. Ndiyo maana unasikia kunaserikali
  ama tawala za Kidini, za kijeshi, za
  Kidikteta, za Kidemokrasia nk.”

  Bw. Mbinza, nimekupongeza kwa 7bu kama unakumbuka nilisema simo humu
  na sitoi michango yangu ili kujionesha jinsi nilivyo na akili nyingi na uwezo mkubwa wa ku-reason.

  Yumkini imani yetu ya msingi (kwa Kristo) ni moja. Ila tatizo ni katika
  kuelewa maandiko. Hapo ndipo tofauti inakuja. Na hii inatokana na:
  1. Uwezo wetu binafsi wa kuelewa neno la Mungu.
  2. Jinsi tulivyoambiwa kwenye dini zetu. Kwa 7bu imani ya msingi ni moja lakini
  wanaotufundisha kule kwenye dini zetu wanatofautiana kati ya mtumishi kwenye dini hii na dini ile; ila imani ya msingi yumkini ni moja.

  Mbaya zaidi sisi washirika tunayachukua
  na kuyaamini tuliyoambiwa moja kwa moja bila kuyarudia hayo maandiko na kuyapima baina ya ufafanuzi tuliopewa kwenye ibada.

  Hivyo ukikutana na mtu mwenye uelewa
  na mtazamo tofauti na wa kwako, utambishia si kwa 7bu una uhakika neno la Mungu halisemi au halimaanishi
  hivyo, la; lakini ni kwa 7bu sivyo mchungaji wetu sisi alivyotufundisha.

  Kwa bahati mbaya, kama mtoto anavyo mwamini sana babaye (unquestionably) kupita mtu yeyote, ndivyo
  tunavyowaamini viongozi wetu wa kiroho (unquestionably) katika kila wanachotufundisha. Tunashindindwa kukumbuka kuwa nao ni binadamu tu. Matokeo yake hata wakitufundisha isivyo sawasawa hatuwezi kugundua.
  Tunajikuta tumeshika kitu ambacho si sahihi. Hapo ndipo dhana ya dini huja.

  Sasa tuendelee,

  1. Ndg. Mabinza, hakuna mahali popote
  kwenye michango yangu ambapo nimesema nataka wote tuwe wachungaji na papo hapo wanasiasa. Tafadhali nitake radhi!

  2. Nakubaliana na wewe kabisa kwamba
  ni tatizo kubwa sana kwa mtu kutojitambua kuwa yeye ni nani katika dunia au maisha haya.

  3. Umeswma utumishi uliotokana na uteuzi wa Danieli ulikiwa si kitu kingine
  chochote ila ku7bisha nafuu ipatikane kwa watoto wa Mungu chini ya utawala
  wa kibabeli.

  Swali: kwani lwo kina Msigwa kuwepo kwenye siasa hakuwezi kuwa sa7bu ya nafuu kupatikana kwa wa Mungu (kama
  mimi na wewe; na watanzania kwa ujumla) dhidi ya utawala wa kifisadi na
  kinyama unaomaliza tembo wetu,
  kutafuna kodi za walipa kodi maskini, watu kutekwa na kutesa kwa kung’olewa kucha meno na kope, kufunga mikataba
  ya kifisadi, kupeleka askari kwenda kupiga na kufanyia raia unyama
  usioelezeka ndani ya nchi yao badala ya kukamata majangiri na wanaojihusisha na biashara ya nyara za taifa na
  kuwafunga jela.

  4. Ieleweke wazi kwamba, Danieli wala
  Yusufu hawakuchaguliwa kwa kura ya mtu yeyote katika nchi walizokuwa wanatumika. Mungu aliyekuwemo ndani
  yao ndiye huyo aliyefanya uteuzi huo kupitia kwa wakuu wa nchi hizo.

  Swali: shida yako ni kura au? Umesahau
  kuwa Stefano alipatikana kwa kura? Umesahau kuwa mwanafunzi aliyechukua nafasi ya Yuda Iskariote alipatikana kwa kura?

  5. Yohana uliyorejea kuhusu Yesu
  alipokuwa akiwajibu wanafunzi wake kuwa si kazi yao kuzijua nyakati haina uwiano wowote hapo!

  6. Unaposema Danieli hakuwepo katika
  nafasi hiyo zaidi ya hilo alilotakiwa na
  Mungu kulifanya; kwani kina Msigwa nani kasema wapo zaidi ya lile Mungu analotaka walifanye?

  7. Danieli alikuwapo pamoja na kuinua
  utukufu wa jina la Mungu katika Babeli; kwani kina Msigwa hawapo katika siasa
  kuunua utukufu wa jina la Mungu Tanzania?

  8. Pia umesema kuwa alikuwepo katika
  wadhifa ule ili ku7bisha makusudi ya Mungu ya kuwalinda na kuwaondolea mzigo wa kutawaliwa kwa kamba za chuma watu wake;
  Kwani kina Msigwa hawapo ku7bisha makusudi ya Mungu ya kuwalinda na
  kuwaondolea kamba hizo za chuma
  watanzania?

  9. Sijasema mahali popote kwamba
  Danieli hakuwa mtiifu hata kidogo
  kisiasa. Tafadhali nitake radhi!

  10. Akina Msigwa kutokubaliana na ufisadi au kutokubaliana na matakwa
  yoyote maovu ya watawala waovu hakiwi

  kigezo cha wao kutojihusisha na siasa.
  Bali maovu na uovu wa watawala kinatakiwa kiwe kigezo cha wao kwenda katika siasa kuwatetea watu wa Mungu.

  11. Hakuna mahali ambapo nimesoma
  Danieli anamkatalia Mungu ili kumtii
  Dario.

  12. Mimi nilitaja mifano michache hiyo
  inatosha, mifano ni mingi; lakini kama
  unataka na mfano wa Esta, basi mtaje na
  wewe.

  13. Mimi sijaona mahali ambapo Yusufu anaingia matatizoni na kubidi aachie
  ngazi. Labda nioneshe hiyo sehemu
  kwenye biblia; hapo nitakiri ujinga.

  14. Kwa hapa umeanza kusogea kwenye ukweli uliposema kwamba, kama mtu
  alikuwa mtumishi wa Mungu kanisani
  katika nyazifa nyeti kama uchungaji,
  anapochagua kuingia katika siasa yafaa akaacha kazi ya uchungaji.

  Hata mimi naonelea hivyo bw. Mabinza. Maana hizi nyazifa zote mbili ni kubwa
  na zinahitaji muda mwingi ku-
  concentrate kiasi kwamba ni vigumu kuzi-handle zote kwa pamoja sawasawa.
  Lakini kama anaweza kuzimudu kazi zote mbili kwa pamoja vizuri hakuna shida.

  15. Mabinza, nasoma hoja zako hapa
  mpaka nacheka tu!
  Unaleta hoja za kitoto kweli!
  Umezungumzia upande wa Daudi kuwa yeye alikuwa masihi wa Bwana; kwamba yeye ndiye aliyerejesha heshima Israeli
  kwa kuwashinda wapinzani wao kitaifa.
  Kwani kina Msigwa hawawezi kutumiwa na Mungu kurejesha heshima katika taifa la Tanzania kwa kuwashinda viongozi waovu (mafisadi)?

  16. Israeli lilikuwa taifa la Mungu
  mwenyewe. Liliongozwa kwa sheria za Mungu na wal hakukuwepo katiba ya kidunia. Katiba yao ilikuwa neno la Mungu.
  Mabinza, ndiyo maana kuna sehemu kwenye michango yangu huko nyuma
  nilikwambia bado unahitaji maziwa (kifikra) make hujaota meno bado.
  Hivi unadhani Tanzania itakuwaje taifa la Mungu mwenyewe ikiwa akina Msingwa hawatakuwa tayari kuingia kwenye
  mfumo wa utawala wa nchi na kutekeleza matakwa ya Mungu (haki na upendo)?
  Unategemea mafisadi ndo watengeneza katiba inayoshabihiana na neno la Mungu?
  Au unaelewa nini wewe mwenyewe unaposema sheria za Mungu au neno la Mungu?
  Mungu ni Mungu wa haki. Kila lililo la haki latokana na Mungu. Kwa hiyo kila atendaye haki atumikia kusudi la Mungu.

  Hebu katika makundi haya mawili ya maneno niambie ni kundi lipi linalooana na sheria au neno la Mungu (mapenzi ya Mungu):
  a) Wizi, ufisadi, rushwa, uuaji, hukumu
  isiyo haki, ulafi (greed), ubinafsi, upendeleo, uongo, uonevu n.k.
  b) Upendo, haki, utauwa.

  Kwa hiyo bw.Mabinza, ukitaka Tanzania iongozwe kwa sheria za Mungu, itungwe
  katiba yenye misingi yake katika neno la Mungu (haki na upendo). Lakini katiba hiyo wenye dhamana ya kuisimamia (viongozi) lazima lazima wawe wacha Mungu. Maana hakuna upendo wala haki kwa waovu; kwa maana hakuna upendo wowote ndani ya shetani, hivyo haki haimo ndani yake.

  17. Daudi hakuongoza bila mwonaji. Nabii ndiye alikuwa mshauri mkuu wa serikali.
  Mafisadi hawahitaji huyo mwonaji. wanamwonaji wao Bagamoyo. Ila kina Msigwa wakiingia wao watamtaka huyo mwonaji wa Mungu.

  18. Leo katika serikali za mataifa ni rahisi ukatukana bungeni na ukabaki ukiitwa na wafuasi wako mchungaji mwema wa kondoo.
  Hapa nitakuomba uthibitishe tusi alilowahi kutukana mchungaji yeyote kati ya wachungaji waliokwenye siasa. Tena naomba unukuu na tusi lenyewe.

  Yesu aliwahi kumwita mtu mbweha. Tena alikuwa mtu mwenye mamlaka makubwa, mtawala.
  Yesu aliwahi kuwalamba watu bakola waliokuwa wakofanya biashara hekaluni na kumwaga mwaga vitu vyao. Tatizo la watu wanakuwa watakatifu kumpita hata Bwana Yesu mwenyewe.

  19. Kuhusu CCM au CHADEMA kuwapenda wanaowapigia kura tu, hiyo hakubariki. Ushindani ni kitu cha kawaida lakini mwisho wa siku lazima maslahi ya watanzania wote bila kujali chama, kabila, rangi n.k.
  Rejea maelezo yangu hapo katika kundi b), Upendo, Haki na Utauwa. Naamini kina Msigwa (watauwa) wakishika hatamu upendo utatawala.

  20. Je, upinzani na utawala wanaweza kukaa pamoja na kufanya mambo yote kitaifa?
  Ndiyo. iwapo utawala mwovu utaamua kujivua gamba na kuwa waumini wa haki. Hapo wapinzani hawatakuwa na hoja. Itabidi tu waungane na utawala ili kujenga nchi, kama kweli wanachopigania ni haki na usawa.

  21. Mfalme Sulemami alikuwa tofauti na babake Daudi. Yeye alilenga kiwastarehesha wana wa Israeli.
  Haya kina Msigwa wanatafuta kuwastarehesha watanzania waliosetwa chini ya mkono dhalimu wa mafisadi katika taifa lenye rasilimali za kumwaga.

  Bw.Mabinza, sijui kama unajua maana ya mambo ya kidunia. watu wengi sana wana misperception kuhusu hii concept. Baada ya Mwanadamu kutenda dhambi walipoteza mandate ya kuitawala dunia kisheria. Shetani aliwapokonya mandate hiyo kwa hila sana pale alipowahadaa pale bustanini.

  Mandate hiyo kisheria ilihama kutoka mikononi mwao kwenda mikononi mwa shetani. Mandate hiyo iliendelea kuwa mikononi mwake mpaka Yesu alipokufa msalabani. Yesu alimnyang’anya shetani hiyo mandate na kuirejesha tena mikononi mwa mwanadamu, kwa wale wanaoikubali zawadi ya Mungu kuwarudisha kwenye himaya yake pekee. kwa hiyo hapa duniani kuna falme mbili:
  1. ufame wa (nuru) Mungu
  2. ufalme (giza) shetani

  Kwa hiyo biblia inaposema msifuatishe namna ya dunia hii, biblia inamaanisha mkatengwe na mambo ya ufalme wa giza/mkatengwe na mambo ya ufalme wa shetani/mkatengwe na mambo maovu.

  Hili si taabu kuloelewa bali imekuwa vigumu sana kwa wacha Mungu kuelewa mpaka kati ya ufalme wa nuru na ufalme wa giza. Shetani ametua mwanya huu wa ujinga wa wapendwa wa kutoelewa mipaka kuwapokonya maeneo yao halali. Kuna maeneo mengi sana ambayo ni ya wapendwa lakini hawajui kama ni ya kwao na wamemwachie shetani ameyakalia isivyo halali na wapendwa wanayaogopa sana kiasi kwamba hawawezi kutia mguu. Shetani ni mwongo na anawanyanyasa sana wana wa nuru kwa ujinga wa kutojua haki zao.

  wana wa nuru pia wanasumbuliwa sana na dhana ya jambo la kiroho na jambo lisilo la kiroho.
  Jambo lolote lililo la haki, jambo lolote lililo la kweli/jambo lolote lisilo dhambi ni la kiroho. Kwa maana haki yote na kweli vyakaa na Mungu. Hakuna kweli wala haki ndani ya shetani.
  Pia jambo lote lisilo la kweli na lisilo la haki halitokani na Mungu bali natokana na shetani, hivyo si la kiroho. Hakuna jambo la kati maana falme zipo mbili tu. Aidha black au white.

  Karibu bw.Mabinza tutete kutafuta ukweli. Mitume na wazee walipokaa kule Yerusalem waliteta mpaka wakapata ukweli.

  Duniani ndipo shetani alipotupwa

 13. Ndg. Kaswahili na Sungura,
  Mpo akina braza? Ndiyo nimekuja tena, ili isiwe nimewakimbia, nawajua!

  Kwanza amini kuwa, sipingi kabisa kuongezeka watu kuwa kama ‘akina Msigwa’ (kwakuwa wapo!) na pia sisemi KUSIWEPO KUCHANGANYA NENO LA MUNGU NA SIASA, maana Neno ndilo linalosema hivyo. Vile vile niwaweke wazi na muelewe kuwa, DINI NA SIASA HAVICHANGANYWI SASA, VILISHACHANGANYWA TANGU ZAMANI, NAWEZA KUSEMA DINI NA SIASA NI KITU KIMOJA! Dini ni taasisi kama zilivyo taasisi zozote Duniani, Dini husajiriwa kwa mjibu wa taratibu za kisheria za Nchi husika, lakini bila Siasa haiwezi kuwepo Tasisi yoyote kwakuwa Siasa ndiyo ‘Tool’ inayoendesha Taasisi yoyote ile. Ndiyo maana unasikia kunaserikali ama tawala za Kidini, za kijeshi, za Kidikteta, za Kidemokrasia nk. Lakini kamwe huwezi kukuta hayo katika Utawala wa Mungu, kwa hiyo na watendaji wa serikali hiyo ya Mungu wapo katika nafasi zao na hufanya kazi zao kwa kufuata Neno la Mungu tu na si matakwa ya Kisera kama zilivyo taasisi za kidunia, ambazo sera zao kila kukicha hubadilika! Zaidi sana Wakati Dini zinasajiriwa; Neno la Mungu halisajiriwi popote Duniani, lipo tu na litaendelea kuwepo!

  Kaswahili na Sungura, nimewaelewa sana kwanza ninyi, mlichokiongea ni cha aina moja, kinafanana kama mpo mapacha vile! Ati kwamba wote mnataka muwe wachungaji na hapohapo muwe wanasiasa wa siasa za falme za dunia! Kwa pamoja, mnajaribu kuitaka Biblia ikubaliane na ninyi ili mpate manono huku na huku, mkioanisha utashi wenu huo na utashi wa Mungu juu ya utendaji wa kama, Danieli, Yusufu, Daudi, Sauli na au nata Selemani, kifupi mnatisha na mpo juu kidunia! Mungu hana tamaa za kiutashi kama hivyo!

  Ndugu zangu, ni shida kubwa kwa mtu kutojielewa, kutokana na kutojitambua kuwa Yeye ni nani, yupo kwa nini na yupo kwa ‘misheni’ gani kwa leo! Biblia inasema, makusudi ya Mungu ni yake mwenyewe, bali makusudi ya wanadamu yanatoka kwa Mungu, pia ni kwamba, kila jambo lipo kwa wakati wake na kwa makusudi ya Mungu. Mungu anajielewa, anatambua makusudi yake, huyaratibu mambo kwa wakati na kwa makusudi yake! Mungu anajijua leo yeye ni nani na kwamba, anafanya nini leo. Kujitambua huku kwa Mungu ndiko kunakofanya kuratibika kwa shughuli na mambo yote kama yanavyofanyika hapa ulimwenguni.

  Kaswahili, umenitaka kuthibitsha juu ya utumishi wa Danieli, Yusufu, Daudi na pia Selemani kuwa walikuwa na makosa, sijajua maana hasa ya makosa unayoyasemea, ila na hisi tu kuwa, huenda unataka uhakika kama watu hao, katika kuwa na nyadhifa zile ni sawa ama ni kosa kwa mjibu wa Neno la Mungu; Kama ndivyo, jibu ni kwamba HAWAKUWA NA NYADHIFA HIZO KIMAKOSA AMA KUWA NAZO NI MAKOSA, HATA TAWALA ZIWE MBAYA NAMNA GANI HAZIKO KIMAKOSA AMA KUWEPO NA WATAWALA KAMA HAO NI MAKOSA LA HASHA, HAKUNA MAMLAKA ILIYOPO HAPA DUNIANI KWA KUJIWEKA YENYEWE, BALI ZIPO KWA KUWEKWA NA MUNGU NA KWA MAKUSUDI YAKE MWENYEWE. KWA HIYO ZIHESHIMIWE KWANI MIPANGO YA MUNGU HAINA MAKOSA!

  Kuhusu watawala hao uliowataja, Biblia inasema, Mungu atawabebea mizigo yao yote na atawatunza watoto wake hapa Duniani. Utumishi uliotokana na uteuzi wa Danieli ilikuwa si kingine chochote ila kusababisha nafuu ipatikane kwa watoto wa Mungu chini ya utawala wa kibabeli, ieleweke wazi kwamba, Danieli wala yusufu hawakuchaguliwa kwa kura ya mtu yoyote katika nchi walizokuwa wakitumika, Mungu aliyekuwemo ndani yao ndiye huyo aliyefanya uteuzi huo, kupitia wakuu wa nchi hizo! Yafaa uelewe pia kwamba, Utawala uwe mbaya sana ama mzuri sana lazima utakuwa umewekwa na Mungu kwa kazi maalumu kwa wakati maalumu, kwanini? Biblia inasema katika Yohana, “si kazi yenu kuzijua nyakati” Kwa hiyo kutaka kujua, kama viongozi hao walikuwepo ki makosa ama walikosa kukubali kutumika katika nyadhifa walizoteuliwa kuzitumikia, ni kupoteza wakati wako bure, kwani unataka kuzijua nyakati!

  Aidha Danieli hakuwepo katika nafasi hiyo zaidi ya hilo alilotakiwa na Mungu kulifanya. Danieli alikuwepo pamoja na kuuinua utukufu na Jina la Mungu katika Babeli, pia alikuwepo katika wadhifa ule ili kusababisha makusudi ya Mungu ya kuwalinda na kuwaondolea mzigo wa kutawaliwa kwa ‘kamba za chuma’ watu wake. Unasema pia kuwa, Danieli alikuwa mwanasiasa na hapo hapo kumtumikia Mungu, na kwambia Danieli hakuwa mtiifu hata kidogo kisiasa! Ndiyo maana hata katika tundu la simba alitupwa alipoambiwa atekeleze sera ya serikali, naye hakuwa tayari maana alijua kwa kuitekeleza sera ile ingembidi aende kinyume na Mungu ambaye hasa ndiye aliyemuweka pale, kabisa hakuwa tayari! Kama mwanasiasa, akawa kinyume na Taasisi yake utamwita mtumishi bora wa taasisi husika?! Ili labda ‘Kubalanzisha ikwesheni’ Je waweza kuniambia ni wapi Danieli alimkatalia Mungu ili kumtii Dario na serikali yake? Sijui kwa nini hukumtaja Esta katika hili.

  Yusufu, ‘Misheni’ yake ilikuwa ni kumpeleka Islaeli utumwani ili kukamilisha Neno la Mungu alilomwambia Ibrahimu kuwa, atakuwa utumwani miaka mianne, si zaidi ya hapo. Na alipojaribu kuwatetea wana Islaeli na wakati huohuo kumtumikia Falao ilishindikana, akalazimika kuingia matatizoni na hivyo hakuwa na jinsi ni kuachia ngazi ili amtii Mungu! Kaswahili, elewa pia kwamba, yapo madaraja katika utumishi, mwana wa Mungu wa kawaida, anaweza kuwa mtumishi wa Serikali au mwanasiasa ama mwanachama wa chama chochote cha Siasa, akatumika kwa mjibu wa Neno la Mungu, mfano; asipokee na kutoa rushwa, asiibe mali ya Umma, asitege kazi na nk. Huyu wala mimi sina tatizo naye endapo anajitambua kuwa yeye kwa vyovyote hana Cheo chochote cha kimbingu ambacho kinatumika hapa Duniani, si nabii, si shemasi, si asikofu, si mchungaji, si mwinjiristi, si mwalimu nk, maana kuwa na vyeo hivyo na ukaingia katika siasa, unakuwa umeacha kimoja bila mjadala; Hivyo, Msigwa ama Lwakatare walishaacha uchungaji tayari, ila waweza kuona hawajaacha maana inategemea Afya ya macho na unatazama kutoka wapi na kwa wakati gani, usiku au mchana, usiku wa mbalamwezi ama usiku wakiza kinene, mchana wa jua kali au jioni ya mawingu na utusitusi wa manyunyu ya mvua nk!

  Nilichokiona hapo ni pengine umeshindwa kuelewa ni nani hasa ambaye hapaswi kuwa katika utumishi wa mambo yote hayo mawili kwa wakati mmoja! Haiwezekani mtu anayejiita Mchungaji wa kondoo wa Bwana, Askofu na nk; na hapohapo kuwa Mbunge, Diwani au hata kuwa Rais wan chi, ni lazima aache kimoja! Kwa sababu mataifa haya ya Dunia ni muungano wa mataifa mawili, limo taifa la Mungu na limo taifa la shetani, na wote wana misingi huru ya kiimani na Itikadi. Lakini, ukiwa kiongozi kama Diwani, Mbunge au Rais Kamwe huwezi, katika mikutano yako ya kisiasa, katika mahakama zako, katika majeshi ya ulinzi wa nchi, katika polisi, katika Mgambo, katika Bandari, katika ofisi za mapato, katika hospitali, katika Biashara mbali mbali mfano, za Baa, Hoteli, Nyumba za kulala wageni, uendeshaji wa Benki ama katika usajiri wa vifo na watoto, usajiri wa dini na vyama mbalimbali, na hata katika serikali zako za vijiji ukatekeleza utendaji wako kwa kutumia Biblia, wakati kuna watu wa Imani na Itikadi tofauti humo! Maana wote hawa wanatakiwa kutendewa sawa kwa mjibu wa mising ya sheria, kanuni, taratibu na haki za Binadamu ki mataifa na kwa mjibu wa katiba ambayo ni huru! Je, iko serikali kama hiyo na haina migogoro Kaswahili?.

  Daudi ni tofauti na watu hao wawili, yeye alikuwa ‘masihi’ wa Bwana, ndiye aliyerejesha Heshima katika Islaeli, Kurejesha heshima ya Islaeli kwa kuwashinda wapinzani wao kitaifa, mpango ama kuwepo na wazo la ujenzi wa Hekalu kuu , kuimalishwa kwa Neno la Mungu, na ujio wa Bwana Yesu Kristo. Kwanza eleweni kwamba, Israeli lilikuwa Taifa la Mungu mwenyewe, liliongozwa kwa seria za Mungu na wala hakukuwepo katiba ya Kidunia, katiba yao ilikuwa ni Neno la Mungu.

  Daudi hakuongoza bila ‘MWONAJI’ – Nabii alikuwa ndiye mshauri mkuu wa Serikali za Wafame kama Daudi na wengine, Nabii hakusema ama kushauri mambo yake mwenyewe, hakunena yaliyo yake, ndiyo maana Nabii muongo aliuuawa! Lakini leo katika Serikali za mataifa, nchi haiongozwi hivyo, ndiyo maana sasa ni rahisi ukatukana Bungeni na ukabaki ukiitwa na wafuasi wako kuwa mchungaji mwema wakondoo ama Shemasi ama Askofu nk, huku mdomoni umejaa matusi! Vilevile si rahisi CCM kuwa na sera ama itikadi moja na CHADEMA, kiongozi toka CCM atawapenda wanaCCM wenzake ambao humpa kura na kwa CHADEMA vivyohivyo hata kwa Duniani kote, wakati Neno linasema UMPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO! Je, upinzani na utawala wanaweza wakakaa pamoja na kufanya mambo yote kitaifa? Nakubali yapo baadhi lakini si yote!

  Selemani kama alivyokuwa Baba yake, alitawala Taifa la Mungu lililokuwa likisimamiwa na Sheria za Mungu, hivyo ni tofauti sana na Daneli, Yusufu, Mussa ama akina Esta. Huduma ya selemani ilikuwa kuwastarehesha Israeli, kutokana na mapito ya nyuma, maelezo ya maisha ya Israeli kabla ya Selemani yameelezwa vizuri katika vitabu vya Wafalme. Kwa hiyo Selemani alikuwa pia tofauti sana kiutawala na au Daudi baba yake, Daudi alikuwa mtu wa vita, na hakutawala katika utulivu, namna alivyotumika Daudi imeelezwa vema katika kitabu cha wafame na hata katika Samweli. Kwa hiyo watawala hao hawawezi kuitwa ni watawala wa Sera za siasa za Kidunia, maana waliongoza Nchi kwa mjibu wa Neno la Mungu kwa kuusikiliza unabii ambayo ndiyo sauti ya Mungu na hiyo ndiyo sheria iliyowapasa kuendeshea nchi ama Serikali zao!

  Sisi ni Makuhani katika Uflme wa Kristo, kama alivyokuwa Daudi ama Sauli, nasi tu wapakwa mafuta ambao tutatawala Pamoja na Kristo, sisi ni makuhani wa Kifalme, ufalme huo ni ule wa Kristo. Mara zote kuhani husimama katika zamu yake kama kuhani, humtumikia Mungu kwa usahihi na kamwe hawezi kuwa pamoja na Siasa za Kilimwengu maana hawezi kwenda nazo kwa usahihi. Kuhani humfanyia kazi Bwana mmoja, maana akiwatumikia wawili atafanya ubaguzi na kuheshimu zaidi upande fulani kwa maslahi fulani. Zaidi ya yote, Mungu ni Mungu mwenye wivu hutaka atawale yeye tu! Kwa hiyo, mtu atatumika kwa kadri ya anavyojitambua, ukiona wewe ni mtoto wa Mungu na hunawadhifa wowote wa Ki mbingu, kafanye siasa, mimi sikulaumu wala kukuhukumu, utajijua na aliyekuumba!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 14. Wapendwa,

  Sungura na Kaswahili, nimewaona nakuja wazee, kuna kitu tu kidogo kilininyima nafasi ya kuwajibu mapema, nakuja kaeni chonjo!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 15. Wana SG heri ya mwaka mpya!!!. Naona mjadala huu umekua mrefu lakini kusema ukweli wengi (wote?) wetu tunaona nchi yetu ilipofikia na inakokwenda. Hivyo tunahitaji watu wa Mungu wenye sifa njema na uwezo kuliongoza taifa la Tanzania. Nadharia kuwa taifa litaendeshwa kwa amani na haki bila watu wenye hofu ya Mungu kuwa katika madaraka si sahihi na ni vigumu ikatimia. Huu ndio ukweli halisi katika neno la Mungu na hali halisi.

 16. Meeeen, bravo Kaswahili!!!!!!

  Huo unaitwa ukweli wenye ithibati kuntu, ambao huwa ukitolewa mahakamani, basi hakimu huwa tayari kutoa hukumu.

  Mabinza unapotetea hoja, lazima uwe umefanya uchunguzi wako toka kusini, kaskazini, mashariki na magharibi, ili uweze kujiridhisha pasi na shaka yoyote kuwa unachokisema kimejitosheleza.

  Naona wewe bado umekaa kwenye kizazi kilichokuwa kikiambiwa tu maneno kama; usichanganye siasa na dini, basi chenyewe kinaamini kuwa huyo aliyekuwa anatamka hayo si mtu bali ni Mungu. Lakini kumbe kwenye hayo maneno hakuwemo Mungu, bali ni mtu tu, na shetani akikoleza hako kausemi.

  Leo hii sisi ni kizazi chenye mfano wa waberoya, watu wenye kuchunguza maandiko kuona kama yanayosemwa yako hivyo.

  Wewe umekaa kwenye dhana ya usichanganye siasa na dini, na tena unaitafutia na maandiko ya kulazimisha ili kuihalalisha. Halafu nakushangaa hapo juu unajifanya kumpongeza Kaswahili ati kwa kujitambua. Acha unafiki mpendwa, kajitambua nini ambacho alikuwa hajitambui? Zaidi sana alikuwa anatukumbusha tu kwamba msingi wa mijadala yetu iwe ni kujifunza.

  Nani kataka msaada wa SG zaidi ya huu wa kututengenezea uwanja wa kuyasambaratisha mawazo mafu ya dini na kuusimamisha ukweli wa Mungu kama hivi tunavyofanya?

  Au wewe kwa kusema hivyo unataka SG wakusaidie kwa msaada mwingine zaidi ya huo, au unataka nini? Maana naona umelialia tu kwenye hiyo makala yako.

  Anyway, ngoja nikupe nafasi ya kuprove hayo mambo ambayo Kaswahili kayaainisha vizuri hapo juu. Na usilete longolongo, nataka ulete ithibati kuntu kuwa hao watumishi wa Mungu waliotajwa hapo juu walikuwa wrong kushiriki kwenye siasa!

  We need as many people as Msigwa to heal this nation!

 17. Mabinza,

  Aya, jibu hoja sasa.
  Acha umbayuwayu wako humu. Sipendi tabia yako ya kuruka DAMA.
  I’m waiting for you to prove that Daniel
  was wrong.
  I’m waiting for you to prove that Joseph was wrong.
  I’m waiting for you to prove that David was wrong.
  I’m even waiting for you to prove that Solomon was wrong.

  Twende kazi.

 18. Kaswahili na wana SG wote,

  Nimefurahi sana kwa Kaswahili kujitambua, ni kweli sana hatupo kubishana hapa, tupo kujifunza. Tatizo la watu wengi hupenda wasifiwe na kupongezwa na wanadini wenzao. Hata yapo maandiko yanayounga hoja kwa uwazi, atashikilia kukataa, ilimladi kagundua kuwa mwenzie, si labda mpendekosti, mluteri, mwangilikana, m-AICT, Msabato, Mjehova, Mroma, M-Jesus only nk, Utalitambua hilo utakapoona mtu anaacha kutumia Maandiko ambayo ndiyo msingi wa kweli wa mjadala wetu. Na kuanza kushambulia watu kwa maneno ya kukatisha tamaa, kumshusha mwenzake hadhi, dhihaka ama kejeli nk. Na kushikilia alichofundishwa na dini yake, hata kama siyo!

  Mara zote huwa nasema, lete maandiko ili kuunga mkono wa unachokisema. Wanasheria husema, “kama ipo hati Mahakamani dhidi ya jambo linalobishaniwa, na hati yenyewe inakubaliwa na pande zote zinazobishania jambo. Ushahidi wa mdomo hauhitajiki” Kwa hiyo, kulazimisha hoja ikubalike bila kuwa na msingi wa Neno la Mungu (kutokuwa na hata mstari ulionukuliwa toka katika Biblia) ni UBISHI MBAYA!

  Si hivyo tu, kosa kubwa kuliko yote linaloletwa na ubinafsi wa wabishi nikuwa, utaona aitha mtu akiwa hana hoja ataanza kuangalia huku na huko ili awapate watu kutoka ama katika dini yake au kutoka katika mmoja wa marafiki zake, watakaomuunga mkono kwa jambo lake, au utaanza kuingiza habari za kutaka msaada wa SG yenyewe imuonee huruma, yaani kama vipi afanikiwe kusababisha mtu asimamishwe kuchangia, ama afungiwe kabisa, mtu kama huyo huwa hajui athari za upande wa SG yenyewe na kwa watu wa upande wa pili, badala yake anajijali yeye tu! Hayo yote ni ubishi na ubinafsi mbaya sana. Nashauri mwaka huu tubadilike, ili tuifanye SG kuwa kanisa la kweli la Mungu!
  Asante sana Kaswahili kwa kujitambua, haturuhusiwi kuteta, uliyoyasema hapo juu Kaswahili ni wewe mtupu jamaa yangu!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 19. Maibinza,

  Ni rahisi mtu kujiona ana hekima machoni pake mwenyewe.

  Tambua jambo hili kwamba, hatulazimiki kuyakana mapenzi ya Mungu ati kwa sababu tuko utumwani. Hatulazimiki kufanya kitu ambacho ni kinyume na Mungu ati kwa sababu sisi ni watumwa na mfalme kasema tufanye hicho kitu.

  Kama kutumika kwenye siasa ilikuwa ni dhambi, hata kama mfalme angekuwa amesema, Daniel, Shadraka,Meshaki,na Abedinego wasingekubali kufanya hicho kitu. Kumbuka kwa sababu ilikuwa ni dhambi kuanguka chini kuisujudu ile sanamu, hao ndugu walikataa pamoja na kwamba mfalme alitaka wafanye hivyo, na unajua kilichotokea.

  Kumbuka nimekuuliza habari za akina Daudi, na akina Suleimani, ambao walimtumikia Mungu na huku wakitumika kwenye siasa, na hawakuwa utumwani. Mbona unakwepa kujibu kuhusu wao?

  Kwa kifupi bila hata kuendelea kuzebezana hapa, ni hivi, tutamtumikia Mungu kwenye siasa na kwenye nyumba yake tutamtumikia pia. Maana ukiwa mwanasiasa na ukatenda yaliyo haki huko ni kumtumikia Mungu pia.

  Na usitake kutudanganya hapa, kusema kuwa chuma mchanganyiko na udongo ilikuwa ni siasa zenye kuchanganyika na dini. Hayo maneno wapelekee wajinga wasiojua kuisoma biblia. Udongo na chuma zote zilikuwa tawala za kisiasa, wala hakuna moja iliyokuwa ya kidini hapo. Ni kutaka kuleta tu tafsiri mfu za maandiko kwa ajili ya ku-justify wazo la kutungwa.

  Na kuna nini unataka kusema unaposema hapakuwa na ushirika wowote wa utawala wa kiasa wa Babeli ulioshirikiana kwa ufanisi na utawala wa Mungu ndani Danieli na wenzake?

  Ulitaka kuwe na ushirika gani zaidi ya ushirika wa kikazi ambao uliendana na mapenzi ya Mungu? Si unaona Daniel alikataa kukubaliana na suala la kutosali mbele za Mungu lililopitishwa na mfalme, matokeo yake akatupwa kwenye shimo la simba!

  Hayo yanakutosha kwa leo,

  Asante.

 20. Bw. Mabinza, tuendelee,

  Nakubali kunikosoa kuwa nilisema sina la kujibu lakini bado nilikujibu.

  Katika kumjibu bw. Sungura umesema hivi, nakunukuu:
  “Na kuhusu Danieli, umelipuka tu kivyakovyako, kwanza Danieli alikuwa uhamishoni kama mtumwa tu wa kawaida tokana na utawa wa wababeli. Mtawaliwa yeyote ni kama mtumwa tu, hana maamzi. Mfalme wa Babeli ndiye aliyemteua Danieli na kupa wadhifa
  katika Babeli ile ya Kale, Mungu
  aliruhusu lile ili utukufu wake uonekane
  katika wapagani wa Babeli! Hapo wala
  sijui unataka kusemaje, maana hakuna ushirika wowote wa utawala wa kiasa wa Babeli ulioshirikiana kwa ufanisi na
  utawala wa Mungu ndani Danieli na wenzake!”

  Umesema:
  1. Danieli alikuwa uhamishoni kama mtumwa tu wa kawaida tokana na utawala wa Babeli- Kwa hiyo?

  Mtawaliwa yeyote ni kama mtumwa tu, hana maamuzi- Ni kweli mtumwa hana maamuzi ya kwake, lakini si lazima atii kila maamuzi anayoamuliwa kuyatekeleza. Maana umesahau kuwa Danieli alikataa kutii uamuzi/ azimio lililotiwa saini na mfalme la katazo la kumwabudu mungu mwingine yeyote tofauti na mfalme.

  Mfalme wa Babeli ndiye aliyemteua Danieli na kumpa wadhifa katika Babeli- Kwa hiyo kama mfalme alimteua?
  Kwa nini Danieli asingekataa uteuzi? Kwa 7bu yeye (Danieli) ufalme wake haukuwa wa dunia hii?

  Mungu aliruhusu ili utukufu wake uonekane katika wapagani wa Babeli- Kwani leo Mungu anamwogopa nani kuruhusu waamini kuingia katika siasa za Tanzania ili utukufu wake uonekane katika mafisadi na wapagani wa Tanzania?

  Umemuuliza Sungura, “hapo wala sijui unataka kusemaje!?”- Na mimi nakuuliza, “kwani wewe unataka kusemaje!?”

  Umesema hakuna ushirika wowote wa utawala wa siasa wa Babeli ulioshirikiana kwa ufanisi na utawala wa Mungu ndani
  ya Danieli na wenzake. Hebu soma hapa:

  Dan 6:1-4;
  Natumia biblia yangu ya (easy to read
  version)

  1.Darius thought it would be a good idea to choose 120 satraps to rule throughout his kingdom. 2.He chose three men to rule over the 120 satraps. Daniel was one of the three supervisors. The king put these men in his position to keep
  anyone from cheating him. 3.Daniel PROVED HIMSELF TO BE A BETTER SUPERVISOR than any of the others. HE DID THIS BY HIS GOOD CHARACTER AND GREAT ABILITY. THE KING WAS SO IMPRESSED WITH DANIEL THAT HE
  PLANNED TO MAKW HIM RULER OVER THE WHOLE KINGDOM. 4.But when the other supervisors and satraps heard about this, they were very jealous. They tried to find reasons to accuse Daniel. So they watched what Daniel did as he
  went about doing the business of the government. But they could not find anything wrong with him, so they could not accuse him of doing anything wrong. Daniel was a man people could trust. HE DID NOT CHEAT THE KING, and he
  worked very hard.

  Bw. Mabinza pia unasemaje kuhusu Yusufu mwana wa Yakobo aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misiri?

  Gen. 41:1-57;

  39.So Pharaoh said to Joseph, “God showed these things to you, so you must be wisest man. 40.I will put you in charge of my country, and the people
  will obey all your commands. I will be the only one more powerful than you.”

  41.Phaaoh said to Joseph, “I now make you governor over all Egypt.” So Joseph became the governor over the whole country of Egypt.

  Bw. Mabinza, unasemaje pia kuhusu wafalme kama Daudi ambaye alikuwa mfalme na wakati huo huo kuhani wa Mungu?

  Unaelewa lakini Yesu alipomjibu Pilato kuwa ufalme wake haukuwa wa dunia hii?
  Ni kweli ufalme wake haukuwa wa dunia hii. Lakini je, unaelewa ufalme wa Yesu ni wa dunia ipi?
  Kama unaelewa basi unafanya makusudi tu kutafutiliza mistari na kuanza kuzuga nayo ili kuhalalisha ufisadi wako wa maandiko ili doctrine ya dini yako na si doctrine ya Mungu.
  Mabinza, hatubishani hapa ili kulinda na
  kutetea doctrine na misimamo ya dini zetu. Hapa tunarumbana kwa amani. Nia yetu ni kutafuta ukweli wa neno la Mungu ambapo tunadai tumejenga imani yetu kwa Mungu.

  Umedai kuwa mimi bado ningali
  mtumwa. Kweli mimi ni mtumwa. Mtumwa wa Kristo.

  Ufahamu sahihi pekee ndiyo chembe ya uhai.

 21. Bw. Mabinza na wana SG wote,

  Tukirumbana (debate) humu kwa lengo la kutafuta ukweli na kujifunza, kurumbana kwetu kutakuwa kwa manufaa makubwa. Lakini kurumbana kukiwa si kurumbana bali kubishana ili kuonesha ubabe wa maandiko na dini zetu, haitujengi kwa lolote.

  Niwekeze wazi kuwa simo humu ili kubishana kwa dhima ya kuonesha ubabe wangu kimaandiko na dini yangu.

  Mtu mwenye hekima husikiliza mawazo ya watu wengine, huyayafakari na kuyachambua. Akikutana na ukweli humo huuchukua na kukubali kujikosoa. (kwa 7bu dhamiri zetu [kwa msaada wa roho mtakatifu, kama yumo ndani yetu] haziachi kutushuhudia kwa habari ya ukweli unaopita nafsini mwetu).

  Mtu mwenye hekima si mtu mwenye akili sana. Hekima ni hazina kubwa ya
  kweli (truths/facts) ambazo mtu
  amejikusanyia kwa kuuangalia na kuutafakari ulimwengu (observation) [na labda kumtafakari Mungu] kwa njia zifuatazo:
  a) Udadisi (curiosity)
  b) Kusoma (studying)
  c) Kusikia (hearing)
  d) Uzoefu (experience) na
  e) Ufunuo (revelation).

  Yumkini humu tu watu wa madhehebu mbalimbali. Lakini kama madhehebu yetu yamejengwa juu ya imani katika Kristo na katika msingi wa neno la Mungu, basi sote tu mwili mmoja katika Kristo. Na kama ndivyo hivyo, basi tofauti zinakuja katika kuelewa neno la Mungu tu.

  Ni heri kurumbana kwa nia ya kutaka kupata au kuelewa ukweli wa neno la Mungu kuliko kubishana na kubisha ili kutetea mapokeo na mafundisho ya dini zetu na jamii zetu kwa ujumla.

  Mtu mwenye busara hutafuta ukweli na akiisha kuupata huuchukua bila kujali alipoupata; alimradi ni ukweli.

  Mtu mwenye busara hujikosoa na hukubali kukosolewa. Kila jambo ambalo mtu yeyote, wakati wowote analofanya, hutanguliwa na huongozwa na nia (intention). Kama mtu ameingia humu kwa nia ya kubishana na kutetea mafundisho (doctrine) ya dini yake, atatetea mafundisho ya dini yake tu, vinginevyo. Katika kufanya hivyo, hata ukweli ukikatiza mbele yake hatauona na hataki kuuona. Kwa 7bu nia yake si kutafuta ukweli na kujifunza, bali kutetea mafundisho ya dini yake.

 22. Sungura,

  Hasira za nini? Usitoke povu Bro, Neno hili wala siyo langu, mwenye nalo ndiye anayewakata nalo! Yale yote uliyoyabambika bambika siyajibu, kunitaka kujibu swali ambalo nilisha kuuliza, ni kunipotezea wakati. Labda ukili wazi kuwa hujui jibu la swali hilo, harafu mimi nione kama unauelewa wa kutosha ili nikikujibu nisijute kwa kupoteza muda. Nitakujibu baadhi tu kama ifuaatavyo:-

  Umeuliza hivi, “Mabinza, Kwamba shetani ndiye mtawala wa dunia hii! Kwa hiyo nawe kwa kuwa unaishi katika hii dunia, shetani anakutawala? – Nijibu tafadhali.

  Jibu:- Ukiwa marekani si lazima uwe huko kwakuwa wewe ni raia wa marekani, mtu asiye raia hawezi kumuuita raisi ama mtawala wa nchi ile ni mtawala wake, maana hakumchagua, ila anachotakiwa kufanya ni kuwa chini ya sheria za nchi ile hadi atakapoondoka mle! Kwakawaida, kiongozi wako, toka katika nchi yako uliyemchagua kikatiba, ndiye mwenye wajibu wa kukuombea ulinzi na haki zingine za kiraia ili uweze kuishi kwa kiasi kwa sheria za kimataifa, ili uepushwe na seria ambazo wewe hukuwakilishwa katika kuzitunga, ndiyo maana kuna makosa meengine mhusika hurudishwa kwao. Kwa kulielewa hilo kwa uzuri, angalia hati yako ya kusafiria ilivyoandikwa (kama unayo).

  Vivyo hivyo, kwa kulijua hilo, Yesu Mfalme wetu sisi akina Mabinza, alituombea jinsi ambavyo inapaswa tuishi, bila mwenye utawala wake kuona kama anafanyiwa udikteta Fulani. Ukitaka kujua vizuri hilo, soma sura yote ya Yoh. 17 yote. Lakini, ili uelewe ninachokisema kwakifupi, mimi nakusomea, Yoh. 17:14 -, inasema, 14Nimewapa Neno Lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama Mimi nisivyo wa ulimwengu huu. 15Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu. 16Wao si wa ulimwengu huu, kama vile Mimi nisivyo wa ulimwengu. 17Uwatakase kwa ile kweli, Neno Lako ndilo kweli. 18Kama vile ulivyonituma Mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. 19Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli20“Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea pia wale wote watakaoniamini kupitia neno lao…………. 24“Baba, shauku Yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu Wangu,yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. 25“Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, Mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma. 26Nimekufanya Jina Lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili kwamba upendo ule unaonipenda Mimi uwe ndani yao na Mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.’’

  Sisi japo tunaishi hapa ulimwenguni, tunalindwa, na upendo wa Mungu ndiyo unaotuzunguka, nasi twaishi tu kwa furaha, hatufanyi juhudi yoyote kuishi kama tunavyopaswa kuishi, hatutawaliwi na utawala ambao hatukuuchagua, japo htunaishi katika utawala ambao hatukuuchagua, kwa sababu TULIKWISHAOMBEWA NA TULIYEMCHAGUA KUTUTAWALA! UPO?

  Kuhusu mchanganyiko wa udongo na chuma, soma vizuri michango yangu, mimi nimesema kuwa udongo na chuma ndiyo utawala wa Siasa za kidunia uliochanganyika na Dini! Sasa dini ndiyo Neno la Mungu?

  Na kuhusu Danieli, umelipuka tu kivyakovyako, kwanza Danieli alikuwa uhamishoni kama mtumwa tu wa kawaida tokana na utawa wa wababeli. Mtawaliwa yeyote ni kama mtumwa tu, hana maamzi. Mfalme wa Babeli ndiye aliyemteua Danieli na kupa wadhifa katika Babeli ile ya Kale, Mungu aliruhusu lile ili utukufu wake uonekane katika wapagani wa Babeli! Hapo wala sijui unataka kusemaje, maana hakuna ushirika wowote wa utawala wa kiasa wa Babeli ulioshirikiana kwa ufanisi na utawala wa Mungu ndani Danieli na wenzake!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 23. Kaswahili,

  Kama hukuwa na cha kujibu ulichokisema hapo juu ni nini? Unapaswa kukaa kimya tena umesimama nyuma kwa unyonge, maana haupo huru hata kidogo! Mtu asipoijua ile kweli hawi huru, wewe kaswali matamshi yako tu yanatosha kukuelezea kiwango cha utumwa ulionao, umechagua vema kushika huku na huku, tangu lini mtumwa akawa na maamzi yake mwenyewe?! Huwezi kuiharalisha tamaa yako ikubaliane na maandiko.

  Ati umeniuliza, “Mabinza, unakubaliana nami kuwa Mungu ni mfalme wa mbingu na nchi?” Aaaah, Kaswahili, hilo nikuulize wewe unayeishi kidunia! Yesu alimwambia Pilato kuwa, ufalme wangu si wa duniani, unataka kusemaje, Yesu hakujijua kama yeye ndiye muumba mbingu na nchi? (Yoh.1:1 na kuendelea)

  Yesu, kunawakati anawafundisha wanafunzi kusali, alisema pamoja na mambo mengine kuwa, “Unaposali, saline hivi,…..ufalme wako uje hapa Duniani kama huko mbinguni…” Kama ufalme wake ni wa duniani, alijisahau, na kujikuta kaja duniani bila huo ufalme?! Umesema, Mungu ni mfalme wa mbingu na nchi, ni kweli kabisa! Nyie akina Kaswahili, hata jografia tu ile ya kawaida hukuisoma? Unavyoelewa wewe, Nchi ndiyo Dunia? Hivi, katika kile kitabu cha Ayubu, Mungu alipotaka kujua shetani anakotoka saa hiyo, Shetani alijibuje, unatoka kuzunguka huku na huko katika nchi? Dunia siyo nchi bro! Hebu toa andiko linaloonyesha kuwa Mungu ufalme wake ni wa Duniani, usisemeseme tu kijuajijuaji.

  Ulinukuu niliposema hivi,“Mara ngapi tumeshuhudia wanasiasa kama Msigwa na wenzake wakiwatumia watoto wetu na vijana wetu wa kike na kiume, wakikimbizwa majiani kwa kile
  kilichokuwa kinaitwa kudai haki kwa nguvu ya umma.” Ukanishangaa, kuwa sina meno mimi ni wa maziwa tu, ukasema,
  “Mabinza kila kitu kizuri kinachohitajika kina gharama. Waingereza wasema, “No sweat no sweet.” ni kanuni ya kimungu.
  Ulishawahi kujiuliza kulikuwa na haja gani Mungu imgharimu kiasi hicho
  kutuokoa, wakati angeweza tu kuchukua kile kitabu cha hukumu na kutufutia hatia biashara ikaisha wala hakuna wa kumhoji?
  Wewe leo unadunda kwa 7bu ilimgharimu Mungu (damu ilimwagika)…..”

  Umesema kweli, ila hujui! Kama unakubali kuwa Mungu alimtuma mwanae wa pekee ili sisi tuokolewe, kumbe kwanini, kama akina msigwa na wenzake wanatafuta kuwaokoa kimaisha, labda kama alivyofanya Mungu kutuokoa na dhambi (kwa mjibu wa mfano wako) mbona nao hawawatoi watoto wao wavunjwe miguu kwa lisasi. Kama ambavyo Mungu alimtoa mwanae akafa kwa ajili yetu, badala yake, watoto wa nyie mnaookolewa ndiyo wanaovunjwa miguu?!! Hujaona tu kuwa huo ndiyo ufalme wa dunia ambao, kanuni zake huwa zipo kinyume na za Mungu? Ipo haja mlikubalie Neno, eleweni kwamba sasa hukumu inatembea!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 24. Mabinza,

  Kwamba shetani ndiye mtawala wa dunia hii! Kwa hiyo nawe kwa kuwa unaishi katika hii dunia, shetani anakutawala? – Nijibu tafadhali.

  Kuna swali niliite la kilimbukeni umeniuliza, nakunukuu:

  ”Sungura, mbona, unatoa zaka na matoleo mengine kanisani kwako kwa pesa, wakati pesa ile ina picha au Nembo ya serikali au Raisi; wakati Yesu alipoulizwa juu ya kodi, alijibu kuwa cha Kaisari wampe Kaisari, baada ya kuiona pesa ile ikiwa na picha ama Nembo ya Kaisari, kwa nini, au hilo hujiulizi, kama unapatia ama unakosea?”

  Majibu: Naona hukujua kuwa hilo swali ulitakiwa kulijibu wewe. Mimi nilishakwisha kukwambia zaka wakati huu siyo, na mimi si mtoa zaka, na tena zaka haikuwa kuwa pesa wala dhahabu, wala fedha. Na wewe ndo uling’ang’ana kuwa zaka ni lazima tutoe.

  Sasa mwenye kuulizwa hilo swali ni nani kama siyo wewe unayetoa zaka za pesa, wakati hata mafarisayo unajua walitoa mnanaa, bizari, n.k ( yaani mazao)?

  Na ndio ujue sasa kwa nini Yesu alisema cha Kaisari mpeni Kaisari, na cha Mungu mpeni Mungu. Umenena vema kuwa alikuwa anaongelea zaka na kodi. Kwamba kodi kwa ilitakiwa iwe ile dinari yenye picha ya Kaisari, na zaka ilitakiwa iwe mazao na mifugo ambavyo mwenye kuvitengeneza ni Mungu. Kamwe dinari haikutakiwa kuwa zaka, maana hiyo haikuwa ya Mungu.

  Then, nikuulize wewe, kwa nini unatoa shilingi, dola, faranga n.k kama zaka kwa Mungu?
  ————

  Halafu umeng’ang’ania sana ule mfano wa utawala wa chuma mchanganyiko na udongo, lakini nikikuangalia hata huelewi unachokisema katika hilo.

  Wewe ile miguu ya ile sanamu ambayo ni chuma mchanganyiko na udongo, unasema ni sawa na siasa na neno la Mungu, kitu ambacho si kweli. Maana neno la Mungu ambalo ni Yesu Kristo ndiye aliyekuja akazipiga ule utawala ambao ulikuwa na mgawanyiko ndani yake, na yeye ndiye akatawala. Ile chuma ilikuwa utawala usio wa Mungu, na ule udongo ulikuwa utawala usio wa Mungu. Kwa hiyo hapo ulikuwa mchanganyiko wa tawala mbili ambazo zote siyo za Mungu.

  Lakini wewe kutoka katika kukosa kwako uelewa juu ya hilo unang’ang’ana kusema ulikuwa ni utawala wa ki- Mungu + utawala wa kidunia, kwa maana ya siasa na Neno la Mungu – Ujinga mtupu. Na huko ndiko kulazimisha kunena mambo usiyoyajua.

  Nakujibu swali lako la kwanza hapa chini!

  Naanza kwa kukuuliza swali ambalo si lazima unijibu, ila jijibu kichwani mwako.
  Swali ni hili: Danieli alikuwa ni nani katika utumishi wa Mungu?

  Kisha sasa ona maandiko yanayonifanya niwe na uhakika kuwa kiongozi wa kisiasa anaweza kuwa kiongozi wa kanisa kwa wakati mmoja:

  Daniel 2: 48 -Then the king placed Daniel in a high position and lavished many gifts on him. He made him ruler over the entire province of Babylon and placed him in charge of all its wise men. 49 Moreover, at Daniel’s request the king appointed Shadrach, Meshach and Abednego administrators over the province of Babylon, while Daniel himself remained at the royal court.-NIV

  -Kama haitoshi, Daniel aliwapigia chapuo watenda haki wenzake ili waingie na wao kwenye mfumo ili nchi ipate maendeleo.

  Swali lako la pili halinihusu mimi, labda nikuulize wewe kama unaombeaga Tanzania nzima au Tanzania nusu!

  Mwisho, nijibu kuhusu wafalme wengine mbali na Saul, kwamba nao hawakuyatenda mapenzi ya Mungu kama Saul?

  Kuna mengi tu uliyobugi humo ndani, bt nayaacha ili tusipoteze muda.

  Karibu!

 25. Ndg. Mabinza,

  Heri ya mwaka mpya!
  Sitaongea mengi kwa 7bu katika kujibu hoja zangu sijaona lolote la maana uliloongea lenye kunishughulisha kujibu.

  Nilitarajia utatulia na kujikita kuitetea hoja yako kuwa wakristo hawana sehemu katika mambo ya siasa na
  uongozi hapa duniani kwa kuwa
  wamewekewa ufalme wao mbinguni.

  (Ni upuuzi ulioje kuamini hivi!!
  Siamini kama bado unahitaji maziwa kiasi hiki! Au meno haimo kwa mdomo?)
  Matokeo yake umeacha utetezi ukaanza kuponda shughuli za kisiasa za chama fulani.

  Nikinukuu kuna mahali umeandika, “… Si
  hivyo tu, biblia inaendelea kusema kuwa,
  watoto wa Mungu wamewekewa ufalme
  wao mbinguni, ambako ndiko penye ufalme wa Yesu mwenyewe”
  Swali ni je, hapa duniani wanaishije kabla ya kwenda mbinguni?
  Mabinza, unakubaliana nami kuwa Mungu ni mfalme wa mbingu na nchi?

  Kuna mahali pengine umesema, “Mara ngapi tumeshuhudia wanasiasa kama Msigwa na wenzake wakiwatumia watoto wetu na vijana wetu wa kike na kiume, wakikimbizwa majiani kwa kile
  kilichokuwa kinaitwa kudai haki kwa nguvu ya umma.”

  Mabinza kila kitu kizuri kinachohitajika kina gharama. Waingereza wasema, “No sweat no sweet.” ni kanuni ya kimungu.
  Ulishawahi kujiuliza kulikuwa na haja gani Mungu imgharimu kiasi hicho
  kutuokoa, wakati angeweza tu kuchukua kile kitabu cha hukumu na kutufutia hatia biashara ikaisha wala hakuna wa kumhoji?
  Wewe leo unadunda kwa 7bu ilimgharimu Mungu (damu ilimwagika).

  Kizazi kilicho zaliwa baada ya ubaguzi wa rangi Africa ya kusini leo kinadunda kwa 7bu mandela alilipa.

  Nakushauri uungalie vizuri huo ufahamu wako na chembe yake kama ipo hai.

 26. Sungura,

  Ha,ha,haaaaa, tehe, tehe,tehe, kha! Masikini mbavu zangu….,!Umesemaje eti? Kwamba?……umenichekesha sana bro! Kwani mwaka mpya, ulikunywa sana mvinyo?! Hebu ona ulivyosema, ati, “Unaongea mambo usiyoyajua sawasawa brother, wewe kama unaona kuwa mkristo kuwa kiongozi wa kisiasa ni vibaya, ni vema ukaendelea kuwafundisha huo msimamo watoto wako, na wife wako. Lakini watu wenye haki wa Mungu wenye charisma za kuwa viongozi waache wawatumikie watanzania.
  Heri ya mwaka mpya Mabinza!”

  Sasa, wewe utakuwa hujajua vema; Kumbe watoto na mke wangu, unategemea wamsikilize nani kwanza kama si mimi ‘Askofu’ wao? Tuachane na hilo, hebu turudi kwenye somo. Sungura, hatuongelei urafiki ama ushabiki ama hatufanyi mzaha tunapozungumzia Neno la Mungu, ukweli ndiyo humuweka mtu huru, taja mstari uliomo katika Biblia, unaokuongoza wewe kuwaeleza watoto na shemeji yangu hapo Nyumbani kwako kuwa, wanaweza kuwa wabunge na wakati huo huo wakawa wachungaji katika kanisa la Mungu!!!

  Ukimenya muwa, ukaukatakata vipande vidogovidogo na kuvimimina juu ya wali, si semi huwezi kula pamoja na wali ule, ila nakuuliza hivi, mwenye kuujua wali atakuona upo sawa katika kombinesheni hiyo?

  Yesu aliposema cha Kaisari mpe kaisari na cha Mungu mpe Mungu, hapo alikuwa akizungumzia Kodi na Zaka, tofauti ya Kodi na Zaka ni kwamba, Zaka hutolewa kwa kumshimu Mungu bali Kodi hutolewa kwa kuendesha tawala za dunia kama apangavyo mtawala! Kwa kawaida Zaka na Kodi zote hutozwa kwa uwiano wa kipato cha mtoaji. sawa na Neno katika 1Sam. 18:17 ambayo inasema, ” 17Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake.” Akioanisha na ile Kumb.14:22-23 ambayo nayo inasema, “22Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka. 23Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo na mbuzi mbele za BWANA Mungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimu BWANA Mungu wenu daima.”

  Kwakweli asingeyaweka sawasawa mambo hayo mawili, ingetokea mkanganyiko mkubwa sana kati ya viongozi wa Dini na viongozi wa kisiasa kuhusu HELA! Ambapo kwa wakati huo ndiyo warumi walikuwa wakiitawala Dunia na ndiyo utawala ulioelezewa na Danieli katika ile ndoto juu ya ile sanamu kuwa, utawala ule ndiyo utakao kuwa sehemu za nyayo za sanamu ile ambazo zilifanywa kwa udongo na chuma. Jambo ambalo ki uwazi tunaliona sasa kuwa akina Sungura wanalitimiliza, kwa kufundisha kwamba, siasa na Neno la Mungu vinaweza kutawala utawala mmoja kwa pamoja. Ambapo Neno linasema katika Danieli kuwa, utawala kama huo hautashikamana! Yesu aliposema cha Kaisari mpe Kaisari na cha Mungu mpe Mungu, hakumaanisha kwamba uwe mtumishi wa Kaisari na wakati huo huo uwe mtumishi wa Mungu, kumpa mtu haki yake si kumtumikia, unampa tu kwakuwa hicho umpacho kinamwangukia huyo umpaye! Biblia inasema, ‘mtu hawezi kuwatumikia mabwana wawili’, ila mtu anaweza kulipa kodi na zaka pia!

  Sungura, mbona, unatoa zaka na matoleo mengine kanisani kwako kwa pesa, wakati pesa ile ina picha au Nembo ya serikali au Raisi; wakati Yesu alipoulizwa juu ya kodi, alijibu kuwa cha Kaisari wampe Kaisari, baada ya kuiona pesa ile ikiwa na picha ama Nembo ya Kaisari, kwa nini, au hilo hujiulizi, kama unapatia ama unakosea?

  Sungura, Duniani kote kuna mataifa ya aina mbili, lipo Taifa la Mungu na lipo Taifa la shetani, lakini mataifa yote hayo mawili yamekuwepo kwa idhini ya Mungu mwenyewe! Taifa la Mungu, huongozwa na Viongozi wanaotokana na Mungu. Na hii dunia na ulimwengu wote upo chini ya utawala wa shetani, kama hujui, Biblia inasema, shetani ndiye mtawala wa ulimwengu huu! Ila Mungu ndiye aliyeviumba vyote na kwamba ndiye anayeviratibu! Yesu, alipojaribiwa kule Jangwani, shetani alimuonyesha Yesu, miliki zote za ulimwenguni na hata Yesu alipoambiwa kuwa niabudu nikupe, Yesu hajambishia ama kumkatalia shetani kuwa hana uwezo huo wa kumliki ulimwengu na mali zake zote, bali alimjibu tu kuwa, anayestahili heshima hiyo ni Mungu, na hiyo aliisena kwa mjibu wa Neno! Mungu ataweka Dunia mpya! Yapo mandiko mengi kudhibitisha hilo. Sioni sababu ya kunukuu kila andiko kwa leo! Ila labda nikuulize hivi,

  -NI ANDIKO GANI KATIKA BIBLIA LINALOKUFANYA UWE NA UHAKIKA KUWA, VIONGOZI WA KISIASA, WAWEZA KUWA VIONGOZI WA KANISA KWA WAKATI MMOJA NA

  -LA PILI, PALE JANGWANI MNAPO KWENDA KUOMBEA TAIFA MNALIOMBEA TAIFA GANI. NI TANZANI NZIMA AU?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 27. Ufahamu sahihi ndio chembe ya uhai!

  Mabinza, ni kweli Sauli alikuwa mfalme/ mwanasiasa mbaya. Vipi aliyemfuatia yaani Daudi, naye alikuwaje? Aliyatenda mapenzi ya Mungu au la?

  Vipi kuhusu Suleiman mwana wa Daudi, naye aliyatenda mapenzi ya Mungu au la?

  Ukijaza kichwa chako na ufahamu usio sahihi, hakutakuwa na chembe ya uhai ndani yako, bali chembe ya maangamizi.

  Unaposema ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu, ulishawahi kufikiria vizuri huo msemo na ukagundua maana yake, au na wewe unatembea tu kwenye ile maana ya kusika wengine wakiisema?

  Nani mwenye wajibu wa kumpa Kaisari ya kwake, na ni nani mwenye wajibu wa kumpa Mungu ya kwake?

  Nakupa jibu:

  Maana yake ni kwamba; mtumikieni Kaisari kwa yale anayotakiwa kutumikiwa nayo Kaisari, na mtumikieni Mungu kwa yale anayotakiwa kutumikiwa nayo Mungu

  Anayetakiwa kumpa Kaisari ya Kaisari ni yuleyule anayetakiwa kumpa Mungu yaliyo ya Mungu.

  Anayetakiwa kutenda haki katika kuyafanya yaliyo ya Kaisari ndiyo huyohuyo anatakiwa kutenda haki katika kuyafanya ya Mungu.

  Kwa hiyo kimsingi mkristo mwenye kumtumikia Mungu ndiye anayetakiwa kuliongoza pia taifa, na hapo ndipo haki itatendeka kwa watu, na hapo ndipo watu watafurahi maana mwenye haki ametawala na kuwapa haki zao. Na hapo ndipo hutimia lile andiko kuwa haki huinua taifa.

  Mimi hata sijui nani kawalisha huo ujinga kuwa wacha Mungu hawapaswi kuwa viongozi wa taifa, halafu bado mtu unasema huo nao ni ufahamu wenye chembe ya uhai!!

  Ni nini hasa unachotaka kutumbia hapa Mabinza, kuwa watumishi wa Mungu hawatakiwi kuwa viongozi wa siasa au ni kitu gani?

  Na ni nani kwakwambia kuwa hii planet- dunia inatawaliwa na shetani na Yesu anatawala Mbinguni tu, tangu lini shetani alikabidhiwa hii dunia ili aitawale, na ni tangu lini shetani alimshinda Yesu mpaka yeye ( devil) akawa mtawala wa hii dunia?
  Unaongea mambo usiyoyajua sawasawa brother, wewe kama unaona kuwa mkristo kuwa kiongozi wa kisiasa ni vibaya, ni vema ukaendelea kuwafundisha huo msimamo watoto wako, na wife wako. Lakini watu wenye haki wa Mungu wenye charisma za kuwa viongozi waache wawatumikie watanzania.

  Heri ya mwaka mpya Mabinza!

 28. Kaswahili,
  Mimi kuwa mjinga ama labda nimepotoka si jambo la ajabu, maana mambo yote hayo mawili hupimwa kwa ufahamu, na ufahamu ulio mkuu, huu huletwa na Neno la Mungu, basi, hebu tulitazame Neno ili lituonyeshe nani hasa ni mjinga ama kwa hakika ni nani hasa kapotoshwa na hivyo kupotoka!

  AKINA Kaswali, “MTAPASUKA MISAMBA” bure kwa kutaka kwenda kwa njia mbilimbili, Wataalamu wa saiklojia ya binadamu husema kuwa, ”Watu wasio na maandalizi, humaliza siku yao wakiwa taabani kwa uchovu tokana na kazi nyingi, huku wakishindwa kuandika taarifa ya kile walichokifanya kwa siku ile, maana walicho anzia kufanya hadi kile walichoishia kufanya hakuna!”

  Biblia inasema, au labda tuanzie hapa, soma 1sam. 8:4 -18 na kuenbelea.
  4Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. 5Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuwekee mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.’’
  6Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,’’ hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba BWANA. 7Naye BWANA akamwambia “Sikiliza yale yote watu wanayokuambia, si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao.…….. 9Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.’’…….11Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake.

  Kaswahili, hiyo nayo ni sifa ya Serikali ya siasa za dunia, ambayo Mungu HAKUIPENDA wala kushauri iwaongoze wana wa Mungu kamwe! Mara ngapi tumeshuhudia Wanasiasa kama Msigwa na wenzake wakiwatumia watoto wetu na vijana wetu wakike na wa kiume, wakikimbizwa majiani kwa kile kilichokuwa kikiitwa kudai haki kwa nguvu ya umma, kumbe lengo la hayo yote ni kuwainua wanasiasa, wapate umaarufu kwa mgongo wa watoto na vijana wetu bila ya hata huruma kwa madhara waliyoyapata! Mwisho wake watoto na vijana hao wkiishia kuvunjwa miguu kwa risasi za polisi wakati watoto wa akina Msigwa na wenzake wakipeta kwa raha zao ndani ya mageti ya nyumbani mwao huku wanetu wakiathirika kwa maandamano hayo! Au hulioni jambo hili ni mojapo ya sifa za siasa za Dunia alizokuwa akiambiwa Samweli na Mungu katika 1Sam.8:11?

  Mara ngapi tunatumikishwa kwa kazi zinazoitwa za maendeleo, huku miradi ile ikibaki bila tija kwa walala hoi, au unadhani hali kama hiyo nitaondolewa na waliookoka wakipewa kura na wananchi, ili watawale, japo kanuni na katiba ni ileile ya kutungwa na watu? Nafarijika sana maana Mungu anazidi kuliweka Neno lake vizuri na kulihakikisha, ona hapa ali vyosema, “16Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike na ng’ombe wenu walio wazuri sana na punda zenu atawachukua kwa matumizi yake mwenyewe. 17Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake.”

  Ukisema siasa ni ya Mungu mimi sikatai, maana hata Bwana Yesu alipoulizwa kama naye ni “mwanasiasa” hakukataa, ila akajibu tu kuwa, “….si wa Dunia hii…!” Swala hapa ni Je, wanaojiita “wachungaji wa kondoo” INAFAA kuwa viongozi katika Serikali ya Dunia hii na wakati huo huo wakabaki wachunga kondoo wa kweli, huku vya kaisari wakipewa wao na vya Mungu wakitaka wapewe pia?!

  Biblia inasema Serikali za kidunia zitaongozwa kwa mapato yatokanayo na tozo lisilo la hiari, hebu ona mstari huu, “15Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake” Ni nani asiyejua kuwa serikali zote Duniani huendeshwa kwa kodi za Raia, huku pia wakilipia matumizi mengi tu ya uongo ya maofisa wa serikali? – juzi kati hapa tumesikia, kuna wabunge walichukua Masurufu kwa ziara ya kiserikali, ikasemwa kuwa baadhi ya watunga sheria wale, kwa namna isivyofaa wakayatumia mapesa ya walala hoi Raia wan chi hii, kwa ngono na starehe mjini Dubai bila hata ya Aibu, JE AKINA MSIGWA WALILIKEMEA HILO?!

  Sasa sikiliza ule mstari wa 18 Watu wanasema wao ni KANISA huku wanashabikia kuwa wanasiasa wa utawala wa dunia, chini ya zile kanuni zilizokataliwa na Mungu, halafu ati wanafunga na kuomba, ili Mungu awaondoe katika matatizo yanayotokana na utawla ule, kwa ama ajaze walokole serikalini ama apindue serikali iwe ya dini Fulani! Kwa huzuni wanabaki kuishangaa Mbingu inavyozidi kuwa kimyaaaaaaaa, wanawaza, labda saa ya jibu bado! Kumbe Mungu Alisha jibu hata kabla ya kuombwa.

  Na akawaelekeza watoto wake kuwa serikali za duniani ni za utawala wa Dunia, ila wao walio watoto wake ambao nao wanaishi humo, wasiwe na wasiwasiati kwa nini watu wa dini wanaona hakuna jibu, kwa furaha wao waendelee kulitazama jibu jema la tangu zamani katika ile 1Sam. 8:18 ambayo inasema, “18Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye BWANA hatawajibu.”

  Kaswahili, tarehe 27/12/2014 saa 8 na robo, umesema ati “UPOTOFU + UPOFU = MAANGAMIZI (doom). Lakini kwa neema ya Mungu inawezekana.
  Mimi sitaki kuamini kuwa ndg Mabinza ni mjinga juu ya utangamano uliopo kati ya siasa na dini. Maana biblia yote iko wazi kabisa juu ya uhusiano wa haya mawili.”

  Ndugu yangu, wewe kutotofautisha siasa ya utawala wa Mbinguni na Siasa ya utawala wa Duniani si wa kwanza, wapo huko nyuma, walimgomea Nabii wa Mungu Mzee Samweli, wakambishia, kama wewe unavyomgomea Mungu katika Neno lake, huku mkifunga na kuomba pale labda Jangwani ama Taifa ama Sabasaba graundi mkishinikiza, Mungu abadili mpango wake kwani si mzuri sana, ila alipaswa kufanya ‘Wakristo wawe wengi serikalini!’ na watumie kanuni kama za kimataifa ili tuwe na umoja na mataifa mengine! Biblia inasema katika Sam.8:19-20 kuwa, “19Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. 20Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.’’

  Ni kweli Yesu ni Mwanasiasa, lakini ni mwanasiasa wa siasa za mbinguni, mwenyewa alipotakiwa kusemea hilo, alisema katika Yoh, 18:33 hadi 37 wazi hivi, “33Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akamwita Yesu, akamwuliza, ‘‘Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?’’
  34Yesu akamjibu, ‘‘Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe au uliambiwa na watu kunihusu Mimi?’’
  35Pilato akamjibu, ‘‘Mimi si Myahudi, ama sivyo? Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?’’
  36Yesu akajibu, ‘‘Ufalme Wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme Wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wafuasi Wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo Ufalme Wangu hautoki hapa ulimwenguni.’’
  37Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo Wewe ni mfalme?’’ Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.’’

  Labda nisichoshe sana, niishie tu kwa kusema kwamba, SIASA ni moja ya ‘Tool’ inayotumiwa na watala ili kutawala, kwakuwa Yesu ni mtawala wa mbinguni naye hutumia siasa yake ya mbinguni na shetani kwakuwa ni mtawala wa Dunia, anayo siasa yake ya kidunia. Na kwa sheria za kimataifa utawala hutambuliwa, pamoja mambo mengine kama miliki ile inajeshi, na hata Yesu mwenyewe alilisema lile, akiainisha mojawapo ya aina ya siasa za tawala hizi mbili, kuwa ule wa Dunia ni tofauti na utawala wa Mbinguni, kwa sababu, siasa ya mbinguni hailindwi na jeshi la kimwili, ona Yoh. 18:36 inasema, “36Yesu akajibu, ‘‘Ufalme Wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme Wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wafuasi Wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo UfalmeWangu hautoki hapa ulimwenguni.’’
  ” Si hivyo tu, Biblia inaendelea kusema kuwa, watoto wa Mungu wamewekewa ufalme wao mbinguni,ambako ndiko kwenye ufalme wa Yesu mwenyewe. Utaliona hilo vema katika Lk.22:29-30.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 29. Salaam,

  Asante sana ndg yangu Edwin. Namshukuru Mungu anayezidi kutupa uzima tumekutana tena humu.

  Ndg yangu Mabinza, kuna vitu viwili hasa vinavyoingiza watu katika maangamizi:
  (1) Ujinga
  (2) Upotofu

  Kati ya hivi viwili kilichokibaya zaidi ni upotofu.
  UJINGA-ni hali ya kutokuwa na taarifa/ufahamu kuhusu ukweli/jambo fulani.
  UPOTOFU-ni hali ya kuwa na taarifa zisizo za kweli/sahihi juu ya jambo fulani bila mhusika kugundua. Kupotoka ni kupotea. Ni kufuata njia isiyo sahihi. Na
  mara nyingi huwa ni ngumu kwa
  mhusika kuokoka kutoka katika upotevu
  wake kwa 7bu mara nyingi upotofu
  huambatana na kiburi.
  Kiburi hupofusha. Yaani huyaziba madirisha yote yanayopitisha mwanga wa ufahamu katika akili. Hivyo ufahamu hunyimwa nafasi ndani ya mtu mwenye kiburi kwa kujikinai kuwa hakuna ufahamu zaidi ya alionao yeye.
  Kwa hiyo: UPOTOFU + UPOFU = MAANGAMIZI (doom). Lakini kwa neema ya Mungu inawezekana.

  Mimi sitaki kuamini kuwa ndg Mabinza ni mjinga juu ya utangamano uliopo kati ya siasa na dini. Maana biblia yote iko wazi kabisa juu ya uhusiano wa haya mawili.

 30. Imeandikwa, Mwovu akitawala, wenye Haki wanaugua(pain na maumivu makubwa)..na tutaugua na kuumia kweli!

  Tunakalia upande mmoja tu wa kiroho sana kilichopitiliza hata akina deal namely Kuomba na kufunga tu kuwafunga Waovu na maovu, yet mkiambiwa upande wa pili kua Tutendee kazi maombi na imani yetu eg kujiunga na Vyama, gombeeni posts kuanzia serikali za Mtaa mpaka juu-..ili tuongeze wigo wetu, mnasema pepo au ni kufa kiroho kupolitic-ayaaa.

  Imagine tungekua na namba 100 kama Mchungaji Msingwa, vipi? mmoja tu huyo kwa neema na ujasiri wa Bwana. anapiga maelfu, je 100?

  By the way, hee! Kaswahili upo kumbe duniani humu SG? safi, karibu sana, si zaka hapa take note eeehee! hahaha

  Press on

 31. Wapendwa,

  Mnasemaje sasa? Kwani nyie mnatakaje?Mbona hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe?Mnasema Kanisa linahitaji lisimame, lijiangalie kwanza kabla ya kuinyoshea serikali kidole?! Mmesahau au hamjui kitu kabisa? Nanyi mgali vipofu mnaotembea katika giza tororo, hamjui kinachoendelea au mnajifanya?Mnadhani Biblia imeongopa, sasa mnataka kuikosoa?

  Mlalapo huwa mnaota nini? Angalieni upya ndoto ya Danieli juu ya ile sanamu iliyotengenezwa kwa madini mbalimbali, kama hamtaielewa, basi itazameni miguu yake, nayo kama hamtaielewa basi jueni kuwa, madini yaliyoifanyizwa sanamu ile ndiyo yaleyale yaliyomfanyiza Mchungaji Msigwa. Mkielewa hilo mtafurahi na kushangilia kwakuwa unabii wa Biblia ni wa kweli, kweli tupu, maana umekwisha kutimia, kwamba udongo na chuma havitashikamana-Dini, siasa!Wanadini na wanasiasa wamo katika zamu yao, ni wakati wao sasa, acha wazurumu, waue, wachinje na kuharibu kama alivyo baba yao!

  Ndugu yangu Kaswahili, kanisa halitahusika katika kuikosoa au kuirekebisha hali hii, ukiona kunamtu anashughulika katika kuikosoa hali hiyo na kujaribu kutafuta kinga ya kiroho ili kuifanya hali hiyo iishe, huyo siyo kanisa, bali ni mmoja wa ule ufalme wenye kufitinika! Kanisa linatazamia matokeo kama hayo, ili Biblila iendelee kuonekana na kutumainiwa na kuaminiwa kuwa NDILO PEKEE NENO LA MUNGU,Biblia imetaja kuwa mwanzo wa utungu ni hayo myaonayo sasa, migogoro na maafa yaletwayo na wanadini na wanasiasa, maana kamwe hawatashikamana kama usivyoshikamana udongo na chuma! Kabisa Biblia ni Neno la Mungu, kwani yaliyosemwa humo yanatimia kila siku! Msiutweze unabii!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 32. Wasalaam Sungura, Tumaini na Lwembe.
  Mmenikosha kweli kweli!
  Lwembe kwa maoni yangu umehiti ze pointi!
  Before we erect a finger toward corrupt rulers (they aint leaders), a finger to the church first.
  Shetani amekalia kiti cha enzi cha taifa hili. Kanisa lipo na wachungaji ndo wanafurahia kwenda kunywa chai kila wanapopata chance kukaribishwa ikulu.
  Ukichunguza vizuri utakubaliana na mimi
  kuwa utendaji wa mamlaka ya nchi hili is completely devilish! Not mannish. Kazi ya shetani ni kuchinja na kuharibu. Kuna mambo mengi ya kusikitisha na kutisha ambayo hayafahamu ambayo
  yanafanyika kwenye system ya mamlaka ya nchi.
  Kanisa limekalia kufanya matangazo ya miujiza na utajiri tu redioni, kwenye runinga na mabango. Hata waganga wa kienyeji nao wanafanya hivyo. Angalia matangazo ya uganga wa kienyeji yalivyotapakaa hadi katikati ya miji nchi nzima. Ni alama kuwa giza limetamalaki.

 33. Sungura,

  Hahahahaha! Umemuelewa vizuri mbunge? Amesema asilimia 42 ya watoto wanaozaliwa Tanzania wamedumaa! Hiyo asilimia 40 ya mawaziri ni katika uwiano tu na si kwamba eti katika hiyo asilimia 42 asilimia 40 ndio hao wabunge, na asilimia 2 ndio wako mahospitalini, hapana!

  Katika kila secta wako asilimia 40 waliodumaa, yaani asilimia 40 ya wachungaji wamedumaa! Asilimia 40 ya wakristo tumedumaa!!! Tena ni kudumaa kunakoambukiza na ni kizuizi kikubwa cha kusonga mbele!!!

  Basi wakristo tutakapofikia “Umoja wa Imani” kudumaa kwetu kukitoweshwa, ndipo nchi itaponywa; viumbe vipya, nchi mpya iliyojaa matumaini tena kimbilio la wengi na mfano ulio hai!!!

  Sungura, anza na Siyi na Lenda wazaliwe mara ya pili, wale waliodumaa wa vanish!!! Hahahahaha!!!

  Merry Xmas!!!

 34. There ur Sungura!isue hii ya viongozi inahitaji kanisa tucmame kama ulivyosema!kinyume na hapo ni usanii mtupu!cku zote wanapiga kelele swala la rushwa na ufisadi bt wenyewe ndiyo wahucka wakubwa!Unakuta hata haya makampuni yanayochukua zabuni yanamikono ya haohao wanaopiga kelele!hata kazi wanazofanya zinapokuwa hazina viwango hakuna wa kupiga kelele!mikataba feki mingi wanaoingia ni haohao wanaoipiga kelele bungeni!ndiyo maana cku zote anapoonekana mmoja wao anaonyesha uzalendo anakutana na vikwazo vingi hata kuhatarisha maisha kabisa coz hao wanaopiga kelele wanaona kama mirija yao ya kunyonya maziwa na asali inataka ikatwe so watafanya kila hila wamwondoshe au wamdhohofishe kicasa!tazama jina la nchi yetu inaitwa Bongo Land yaani kila kitu usanii!viongozi wasanii mpaka wananchi wake tumekuwa tunaishi kisanii!just imagine viongozi waliowengi hawaongozi bila kwenda kwa waganga!unategemea nini zaidi ya mauzauza tu!kunahaja ya kanisa kusmama kwenye nafac yake ili God atupe viongozi wanaotoka kwakwe.Gbu

 35. Kama hatutafanya jitihada za kimwili na kiroho kuhakikisha kuwa wenye haki ndo wanatawala, hii inchi haitakuja ibadilike.

  Mawaziri watabadilishwa mno na hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea,kwa sababu waliolitengeneza tatizo ndio wanaojidai kulitatua,lakini ni unafiki tu.

  Ni sawa na mchawi aliyemuua marehemu lakini ndo anajifanya kulia kuliko hata wazazi wa marehemu.

  Hawezi kuondoa rushwa mtu ambaye ndo anafaidika nayo, hawezi kukomeza ujingili mtu ambaye ndo anafaidika nao,hawezi kukomesha madawa ya kulevya mtu ambaye ndo mwenye kumiliki hiyo biashara.
  Mtu ambaye majambazi wakiiba na yeye wanampa share hawezi kuwaua na kuwakomesha majambazi.

  Wakristo wenzangu, suala la mateso yanayoendelea katika hii nchi katika nyanja mbalimbali hayataisha mpaka kanisa litakaposimama mahali pake, na kuacha kupuuza suala la mambo ya kisiasa.

  Hali ni mbaya kuliko tunavyoiona kwa nje!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s