Mchungaji Afungwa miaka 3 1/2 Iran

pst

Vruir Avanessian, Mchungaji kiongozi wa kanisa la Assemblies of God mji wa Tehran, Iran, alikamatwa mwezi Januari, na kuwekwa ndani katika gereza la Evin na kuhojiwa kwa siku 15 kabla ya kutolewa wakati akisubiri kesi yake kutajwa. Mwezi Desemba 2013 Mahakama ya Tehran imemhukumu Mchungaji Avanessian miaka 3 1/2 gerezani.

Avanessian, ambaye alikuwa akiongoza maombi nyumbani kwake wakati anakamatwa ameshtakiwa kwa kuhubiri Injili au kuendeleza shughuli zilizo kinyume na heshima ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Avanessian , 61, ni mdhaifu ana matatizo ya figo pamoja na magonjwa ya moyo.

Makanisa mbali mbali pamoja na Msimamizi mkuu wa makanisa ya Assemblies of God amepinga hatua ya mahakama hiyo na kuita ni ukiukwaji wa haki za binadamu pia na kuhimiza watu kutoka sehemu mbali mbali kumuombea Mchungaji ili aweze kuachiwa huru.

Hali hii imekua si ngeni nchini Iran na nchi zingine ambapo wachungaji au watumishi wa madhehebu ya Kikristo kushtakiwa na kufungwa wengine kuteswa.

Tusiache kuwaombea watu hawa, Omba kwa ajili ya Injili ifike kila sehemu lakini pia usiache kuombea watumishi wa Mungu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu.

Advertisements

8 thoughts on “Mchungaji Afungwa miaka 3 1/2 Iran

  1. NEEMA KUBWA YA MUNGU WA ELIYA ILIYOFUNULIWA KWA KANISA NAITUMA IKUTOE KTK GEREZA HILO KTK JINA LA YESU! KANISA TUNAOMBA TOBA KWA AJILI YA KUSABABISHA KUFUNGWA KWA MCHUNGAJI HUYO KWAKUWA HATUKUSIMAMA KWENYE SAFU YETU KWA UAMINIFU. TOBA YA KWELI INAFUTA UOVU,UASI NA DHAMBI NA KUREJESHA MAJIRA YA KUBURUDISHWA NA BWANA – Matendo 3:19. HONGERA KWA USHINDI MCH. MAANA UMETOKA KTK JINA LA YESU!

  2. HAKIKA NI HESHIMA JUU YA MWILI WA KRISTO MAANA BWANA WETU YESU KRISTO ALITABIRI HAYA WANATAWAPPELEKA MAGEREZANI KWA AJILI YA JINA LANGU MUNGU ATAMTETEA NA HETANI ATAAIBIKA

  3. hata Mtumishi Paulo alifungwa, na alipofungwa alizidi kujawa na nguvu mpya na akatumia njia za panya kuhubiri injili. aliandika na kutupa dirishani, huenda itaokotwa na yeyote. alitumia hata damu yake kama wino. kama wamemsalimisha shingo yake basi, mfuatilie utaona makubwa atakayofanya na nguvu mpya itamjia hapo gerezani.

  4. Huu ni mpango wa MUNGU injili kufika pande zote za dunia haijalishi kutakuwa na vikwazo gani!Mungu amtetee mtumishi wake na cc tuendelee kuwaombea watumishi wa MUNGU dunian kote ili kazi ya injili isonge mbele

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s