Tunawatakia sikukuu njema Wapendwa wote!!

???????????????????????????????

Kuna watu mwaka huu umekuwa ngumu kwao, kwa wakati huu wa sikukuu wana huzuni na wanadhani watamalizaje mwaka huu na kuingia mwaka mwingine, wanahisi kuanguka wanatamani mtu wa kuwanyanyua, kwa desturi kila sehemu ni furaha katika nyakati hizi za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya, kwenye Televisheni na simulizi za kuvutia AMANI DUNIANI, MWOKOZI AMEZALIWA, unachoona ni furaha na tabasamu kwa watu, lakini ukijiangalia mwenyewe unajiona mpweke, mikono mitupu, umekataliwa, umechoka na kuisha kabisa! Umepoteza matumaini, ndoto zako hazijatimia na unasumbuliwa na jambo ambalo ulidhani mwaka huu ingekuwa shwari.

Naongea na wewe ambaye ndoa yako umeiona kama mwiba, wewe ambaye mchumba amekukataa kaoa mwingine pia na wewe ambaye kwa miaka mingi umesubiri kupata mtoto haijawezekana! Umejipa moyo labda mwaka huu, labda mwaka huu mpaka ukachoka kabisa kufikiria! Na wewe uliyepima afya yako ukakutwa na HIV/UKIMWI, KANSA na magonjwa mengine sugu, umeona kama huna pa kwenda unakaribia kufa!

Ninayo habari njema kwako kwamba YESU NI YEYE YULE YULE JANA LEO NA HATA MILELE, HAJABADILIKA, na Neno lake ndio UZIMA WAKO! Linafanya kazi!

Mambo yakuzingatia;

 • Pambana na hali uliyonayo, ikatae kwamba hustahili kuishi hivyo, JIAMINI

 • Kubali kwamba ni kweli imetokea lakini sio mwisho, ondoa kumbukumbu zinazokupa huzuni JIACHIE

 • Usiwachukie waliokuwa hawakuelewi, au ulioona kama hawakujali, kila mtu ana hadithi yake, huwezi kujua wakati huo alikuwa anapita katika wakati gani. SAMEHE

 • Angalia kufanya yale uliyoshindwa kuyafanya mwaka huu. Angalia maisha yako umeharibu? Umepoteza? Umerudi nyuma? Kuna mambo ulipanga siku moja utafanya/utakuwa. Ili ndoto yako itimie! JIPANGE UPYA

 • Jichanganye na marafiki wanaokufaa, wasiokufaa achana nao, tafuta kuwa na amani, hakuna mtu aliye mkamilifu au anayeishi maisha sahihi! Lakini kila mtu anayo nafasi ya kuyatambua mahusiano yake binafsi na Mungu. UWE NA MATUMAINI

 • Hujampokea Yesu? Ulirudi nyuma? Mpokee Yesu sasa kwa imani, kupitia maombi! Kuomba ni kuongea na Mungu kwa urahisi, Yesu anabisha kwako anataka aingie umpe nafasi AZALIWE NDANI YA MOYO WAKO.

Omba maombi haya: Bwana Yesu, nahitaji kukujua zaidi, asante kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, nakukaribisha moyoni mwangu, uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu, uniongoze.Asante kunisamehe na kunipa maisha ya milele, nifinyange kama upendavyo!

Je, maombi hayo yamekufaa? Mkubali Yesu aingie ndani ya moyo wako kama alivyoahidi, “Tazama nasimama mlangoni nabisha, mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango nitaingia kwake nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami (Ufunuo 3:20) Jifunze zaidi kuhusu Yesu na umpende zaidi atakutana na haja ya moyo wako! Atakuponya magonjwa yako yote na atakupa kile unachokistahili.

UJUMBE HUU NI KWA AJILI YA

Kumuandaa aliyekata tamaa na kurudi nyuma, na ambaye hajapokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake, pia unaweza kumfaa yeyote kusahau aliyopitia mwaka wa 2013 na kuanza mwaka mwingine akiwa mpya na mawazo mapya. BILA SHAKA kwa waliookoka kila siku ni inabidi iwe sikukuu bila kujali sherehe au miandano ya mwezi. Mungu awabariki wote

–MD

Advertisements

17 thoughts on “Tunawatakia sikukuu njema Wapendwa wote!!

 1. Kazi yenu ni njema. Songeni mbele.
  Mary D, Mwenyezi MUNGU azidi kuyainua Maono yako.
  Happy new year.

 2. Siyi,

  Nimekuona vema sana, una hangaika, unakimbia kigingi hapo…JIBU SWALI….siku ya uhuru Tz, Unai-observe?

  Press on

 3. Seleli,
  tofauti na sherehe ya pumziko la Sabato, mimi sina siku nyingine ya kusherehekea. Hata kama sijaenda kazini haina maana nitakaa bila kazi siku hiyyo. Mimi nafanya kazi siku sita, ya saba kwa Mungu. Nisipofanya kazi miongoni mwa siku hizo 6, nitakuwa nimetenda dhambi mbele za Mungu kwa kuvunja amri ile ya fanya kazi siku 6, ya 7 kwa Mungu.
  Kwa hiyo kwangu au kwetu, hatuna utamaduni wa kupumzika tofauti na sikuya sabato.
  Ubarikiwe

 4. Siyi and Lenda,

  Waga mnasherekea siku Uhuru wa Tanzania-hamuendi job mnakwenda? mnasherehekeaga Ndoa ya Baba zenu kukaa na Mama zenu miaka 50 kwa ndoa?, ulishasherehekea kumaliza Mtoto wako au wewe shule?

  Kama ni ndio, naomba maandiko kama hayo yamo na Mungu Yehova alituambia tuyatende?

  Nangoja majibu, otherwise stop nonsense here!!!!!!!!!! excuse me ala!

  Press on

 5. Mary D,

  Wow! wow, wow! Glory to God indeed, hii kitu ni tamu sana in Jesus name. No questions that this is great msg ya kufungia mwaka

  I am telling you, hii MSG ni yangu pia, kuna pisi hapo, zimepiga/ponya moja kwa moja angle fulani ktk maisha yangu mwaka huu na kusema ivyo, nakwambia kweli kua RM alikukamata kufyatua kitu maridadi kama hiki, safi Mary kuji-tune kwa waves za RM mpaka ukanasa kwakwe na akakupa Mkate huu for us- wa Rohoni wenye RM pia, Wana na si watu tu wa Mungu! tehe! msg sent kwa jamaa zangu!

  Press on

 6. Lenda, Mwogope Mungu! si jambo jema kutumia Injili kama bakora ya kuwaadhibu wavivu wa kusoma maandiko, Marko 7:1-38 imebeba maudhui mazito kuhusu MAFUNDISHO YA VYAKULA NAJISI. Acha kabisa “KUBINUA” na kupotosha mantiki. Mungu ametupa utashi acha tuutumie kuadhimisha maajabu yake ya kuacha utukufu wake nakuja kuzaliwa na bikira ili atukomboe. Ubarikiwe!

 7. MARKO 7:7

  “NAO WANIABUDU BURE WAKIFUNDISHA YALIYO MAPOKEO YA WANADAMU, NINYI MWAIACHA AMRI YA MUNGU, NA KUYASHIKA MAPOKEO YA WANADAMU”

  DITTU HAKUNA MTU ANAYEKUHUKUMU NENO/KRISTO A/LITAHUKUMU

 8. Siyi, Ukristo si imani peke yake bali ni mfumo mzima wa maisha ya aliyempokea kristo. Chochote ufanyacho kinatakiwa kimtangaze Yesu, iwe shuleni, kazini nk. Ikumbukwe kuwa “KUNA NA MAMBO MENGI ALIYOYAFANYA YESU; AMBAYO YAKIANDIKWA MOJA MOJA, NADHANI HATA ULIMWENGU USINGETOSHA KWA VILE VITABU VITAKAVYOANDIKWA”. (Yohana Mtakatifu 21:25). Istoshe Paulo Mtume anawaambia Waroma kuhusu kuadhimisha siku Rum 14:5. Basi u nani wewe unayechukua majukumu ya Mungu kutuhukumu sie kuwa sio wakristo kwa sababu tunaadhimisha kusanyiko la kristo (CHRIST-MASS)? Basi kwa kuwa krismas inaasili ya upagani tuache kumwabudu Mungu kwa sababu kabla wamissionari kuwasili pwani ya Afrika mashariki tuliabudu miungu (upagani) ambao baadae Mungu alipewa nafasi mahala pa miungu??? BWANA YESU UTUHURUMIE! Amen.

 9. Brother, Dittu,
  Unamaanisha nini kutuita “Ewe Lenda, Siyi nanyi nyote wazee wa “the great disapointed 1844″?????
  Mwisho napenda nikutie changamoto kuwa, kama kuna kitu cha kiimani unakifanya na huku hakikuandikwa ndani ya Biblia, jua kuwa umekwisha rafiki!!! Huo siyo ukristo na hao wanaofanya hayo, siyo wakristo, japo wao wanaweza kujiita kwa jina hilo. Huwezi kuchanganya mambo ya Mungu (Biblia) na ya dunia!! Huwezi kutumikia mabwana wawili.
  Jitahidi sana rafiki!

 10. 2013 ulikuwa ni mwaka mbaya kwangu, nimefarijika kusoma maneno haya, Mungu amekutumia kwa ajili yangu.

  Alinda

 11. Ubarikiwe MD kwa ujumbe ulio bora. Ewe Lenda, Siyi nanyi nyote wazee wa “the great disapointed 1844” mbona mnakaa chonjo kutibua mission ya kumtangaza kristo? kwani kila kitu tunachofanya wakristo lazima kiwe kimeandikwa ktk biblia? Basi hebu ninyi mtuambie hizi POST mnazotuma hapa SG ni mtume/nabii au kuhani gani katka biblia aliwahi kupost kama ninyi mfanyavyo leo?? au ndo CLOSE MINDED?

 12. YEREMIA 10:3,4

  MAANA DESTURI ZA WATU HAO NI UBATILI, MAANA MTU MMOJA HUKATA MTI MWITUNI,KAZI YA MIKONO YA FUNDI SHOKA. HUUPAMBA KWA FEDHA NA DHAHABU; HUUKAZA KWA MISUMARI NA NYUNDO,USITIKISIKE.

 13. Siyi,

  Wewe ni mnafiki au kitu gani?
  Unamwambia MD abarikiwe kwa lipi hasa, ikiwa alichokiandika umekipinga?
  Hii si ndio maana yenyewe ya unafiki au kuna nyingine?

  Ni sherehe gani ambayo wewe huwa unaisherekea ambayo imeandikwa kwenye biblia kwamba uisherekee?

  Ivi nikiamua kusherekea kwa mfano siku yangu ya kumpokea Kristo nitakuwa nimetenda kosa gani mimi kama mkristo?

  Hata wewe Lenda, ni mnafiki tu. Mnaongea sana vitu vya kukariri ambavyo mmelazimishwa mvifanye kuwa fundisho.
  Kuna dhambi gani kusherekea mwaka mpya nikiamua kusherekea,kwani kila ninachokifanya lazima niwe nimeandikiwa kuwa nikifanye?
  ………………………….
  MD, Mungu akubariki sana kwa ujumbe wako kwa watu ambao mwaka huu umekuwa mgumu kwao,naamini wametiwa moyo.

  Mungu akulinde huko uliko!

 14. Mary Damian – MD au mwingine?
  Umenibariki sana kwa bulletings hizo. Pamoja na ujumbe mzuri dada Mary, mimi umeniacha mdomo wazi kukuona na wewe kabisa, unashabikia sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu – Krismas!! Kwako Mary na wakristo wengine, kwa nini tunasherehekea sikukuu za kipagani kwa kuzibadilishia jina? Ni wapi mnasoma kwenye Biblia kuwa watu walisherehekea au pameandikwa watu washerehekee sikukuu ya Krismas?
  Ubarikiwe sana kwa bulletings zako!!
  siyi

 15. KUMBE WAKRISTO MNA SIKUKUU, SIJUI IMEANDIKWA KWENYE BIBLIA YA KING JAMES AU NIV, AU NSV NIISOME.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s