Jaji Ramadhani awa mchungaji Anglikana

Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhani akitoa mkate kwa waumini wa Kanisa la Anglikana baada ya kupewa Daraja la Ukasisi katika Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini mjini Zanziabar jana. Picha na Sahim Shao

Zanzibar. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati  Mzee Abeid Amani Karume.

“Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi,” alisema.

Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.

Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo. Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.

–Mwananchi

Advertisements

One thought on “Jaji Ramadhani awa mchungaji Anglikana

  1. Nimeipenda hii!!

    Mungu ambariki huyu mtumishi wake, kalitumikia taifa letu kwa uadilifu!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s