Tuwe Makini na tunayoongea

methali

Tuwe makini na kila tunachoongea kwa sababu:

Mithali 6:2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,

Mithali 12:18 Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya

Waefeso 4:29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Yakobo 3:5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

Mhubiri 5:6 Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?

Mhubiri 5:2 Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.

Ongea mazuri kwa sababu:
Mithali 13:2 Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.

Mithali 16:21 Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu.

Mithali 16:24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.

Mithali 18:4 Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.

Mithali 18:20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.

Mithali 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.

1Petro 3:10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.

Wakolosai 4:6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Unachojaza moyoni ndicho unachokisema:
Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Linda moyo wako:
Mithali 4:23 Mithali 4:23. Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Moyo unalindwaje?
Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Kwa sababu:
Mathayo 12:34b Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.

Mathayo 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

Mathayo 12:37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu(Mwanzo1):
Waebrania 11:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

Kwa neno unaloamini na kulisema waweza badili ulimwengu wako:
Marko 11:23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

Maneno yako yawe machache, ukiwaza mabaya jizuie usiseme:
Mithali 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Mathayo 5:37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Kutoka 4:12 Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.

Mithali 30:32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.

Ayubu 15:6 Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi; Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako.

–Silva Giga

2 thoughts on “Tuwe Makini na tunayoongea

Andika maoni yako