Nani anachukua roho na uhai wa Wanadamu?

swali

NENO la Mungu lina Hekima na Maarifa yote hivyo tunaweza kulitumia kupata ufahamu na kueleweshana mambo mengi. Kilichonisukuma kutaka tujifunze jambo hili ni mambo 2, kwanza kuzoeleka kua kila Mwanadamu anapokufa, Wote kama si wengi, tunasema ni kazi/mapenzi ya Mungu au kazi ya Mungu haina makosa, Pili, Matukio ambayo yakitokea Africa, Watu wanakufa lakini yakitokea Nje nyingine za Walioendelea, Uhai wa Wanadamu unaokolewa sana tu, sasa kipi ni kipi Wandugu? Unasemaje juu ya maswali haya? yanafanana-fanana kwakua lengo ni kufafanua zaidi mada.

 • Nani ana miliki roho zote  na uhai wa  Wanadamu? 

 • Je ni kweli kila kifo kinachotokea, ni Mungu au pia shetani na Wanadamu? 

 • Ili pumzi ya uhai imtoke Mwanadamu kisha ahesabiwe kua Maiti/Mfu, ni lazima Mungu tu hausike au pia Shetani na Mwanadamu mwenyewe au  Nani ana mamlaka ya kutoa/kuruhusu roho/uhai wa Kiumbe yoyote kutoka? 

 • Mtu akichukua sumu na kunywa kisha kufa, Kulewa pombe mpaka kufia bar, kufanya uzinzi na kuukwaa ukimwi, kuiba na kugongwa mpini kwa kisogo ukafa, roho au uhai huo uliotoka Mtu akafa, ni Mungu anahusika, Mtu mwenyewe au shetani? 

 • Dereva kuendesha gari vibaya kisha ajali kutokea na Watu kufa, nani kachukua roho na uhai huo, Mwanadamu, shetani au Mungu mwenyewe ? 

 • Mwanamke Mjamzito kafika kujifungua, Nesi anapewa maelekezo ya kumuhudumia kisha anasahau au anatoa taarifa vibaya kwa mwenziwe anayempokea zamu halafu Mama au Mtoto anakufa tumboni, boti inazama, kunakosekana vifaa vya kuokoa, ndege inatua na abiria kisha hitilafu na inawaka moto, Uwanjani hakuna zima moto system njema, Watu wanakufa, nani katoa roho na uhai huo? 

 • Ivi kuna uwezekano roho au uhai wa Mwanadamu ukatoka bila Mungu kua ameamua/panga yaani akawa hana taarifa au ikawa mshituko kwake-surprise? Na kama hakuna ina maana basi  kila kifo kinachotokea lazima amekiridhia Yeye? 

Press on digging the Word and grow mightily in His Wisdom and Knowledge.

–Seleli

Advertisements

7 thoughts on “Nani anachukua roho na uhai wa Wanadamu?

 1. Wapendwa,

  Roho ya mwanadamu hukaa wapi? Hivi Roho ya mtu ikoje? Inatokaje anapokufa? Awapo hai roho inakaa sehemu gani mwilini? Inakaa miguuni, kifuani, kichwani, ubongoni, au kiunoni?

  Seleli naomba majibu. CK Lwembe naomba jibu. Sungura naomba majibu. Wote naomba majibu. Asante.

 2. Mwz 1:26,27 Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu;wakatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na wanyama na nchi yote pia,na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba.
  Kwa mfano wetu maana yake utatu wa binadamu yaani binadamu ana roho, nafsi na mwili kwa maana Mungu naye ana nafsi tatu yaani Mungu baba, Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kwa sura yetu maana yake ni roho ya binadamu.

  Ndugu Milinga nanukuu maelezo yako hapa chini:
  “Roho ya mwanadamu haina tofauti na mwili wa mwanadamu. Ukisema uhai, roho, mwili, nafsi, mtu vyote vina maana moja.
  Uhai, roho, mwili, nafsi vina maana ya mwanadam. Hakuna kitu fulani kinaitwa roho kipo ndani ambacho mtu anapokufa eti kinachomoka na kutoka.”
  Maelezo yako hapo juu si kweli ni upotoshaji tu.
  Mwz 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu akawa nafsi hai.(Utatu wa binadamu yaani roho,nafsi na mwili)
  mavumbi ya ardhi ndo mwili na mwili si sawa na roho(pumzi ya uhai)
  Ndg Milinga najua wewe ni mbishi kama ndg zangu wanaotoka kandokando ya ziwa moja lenye kina kirefu kuliko mengine lakini ukweli ndo huo.Naomba unitafute tupate muda wa kutosha ili niweze kukufafanulia vizuri. Ubarikiwe sana ndg yangu.

 3. Mpendwa,

  Roho ya mwanadamu haina tofauti na mwili wa mwanadamu. Ukisema uhai, roho, mwili, nafsi, mtu vyote vina maana moja.

  Uhai, roho, mwili, nafsi vina maana ya mwanadam. Hakuna kitu fulani kinaitwa roho kipo ndani ambacho mtu anapokufa eti kinachomoka na kutoka.

  Maandiko yanasema mtu akifa amelaa, hakuna kitu tena kinachoendelea. Kuna watu wanadhani kuwa kuna sehemu tatu kwa mwanadamu yaani Mwili Nafsi na Roho. Ukiwauliza wavitenganishe wanashindwa.

  Kwa hiyo inabidi kwanza Mpendwa Seleli tuelewane ni nini maana ya roho, nafsi na mwili. Hapo ndipo tujue kwamba nani anachomoa roho au roho huchomokaje? Inapita wapi? Je, uwapo hai roho hukaa wapi? Wengine husema roho hukaa kifuani. Ukiwauliza wanaonesha kwenye kifua upande wa kushoto eti ndipo roho imekaa. Ukiwauliza tena roho wanasema moyo. Mara Moyo, Mara roho, sasa kipi ni kipi na kipi kinakaa wapi? Roho inakaa moyoni? Kama inakaa ndani ya moyo unaosukuma damu mwilini inakuwa na ukubwa gani?

  Maswali kama hayo ukiyajibu ndipo unakuwa uko kwenye mstari wa kujua ni wapi roho inakaa na inatokaje kwa mtu na nani anaichomoa, Mungu, Mwanadamu au Shetani?

  Mimi ninachojua roho ya mtu ndiyo mtu mwenyewe. Maandiko yanasema roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Sasa je roho inakufa? Maandiko pia yanasema, tutavikwa mwili wa kutoharibika siku ya unyakuo, je tutapewa miili ya vipi?

 4. naona mara nyinyi anayahusika kutoa roho za watu ni shetani . makusudi ya Mungu kumuumaba mtu ni ili aishi milele .kifo na mauti ni laana iliyoingia Duniani baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi .dhambi ilipoingia duniani mauti ikazaliwa

 5. Yusha,

  Barikiwa kwa inputs yako, ila see again this, anayechukua sumu na kuinywa na uhai kuondoka, ingawa Mungu anajua kila kitu but nani kaondoa uhai huo?

  David Msuya,

  NILISHAFAFANUA-UKISOMA TENA POST TARATIBU-nilimaanisha kua, ziko ajali-za meli, ndege, gari-system ya Nchi zilizoendelea uwezesha maisha ya Watu kuokolewa haraka kuliko kwetu, sasa je uku meli ikizama-eg Mv-Bukoba au Zanzibar kule na kukakosekana vifaa na wazamiaji wa haraka, Watu wakafa, ni Mungu kwa kua Mungu ndio ana milki uhai au ni uzembe na umaskini wa Wanadamu? Umenipata? karibu jibu/changia tena ufahamu wa jambo hili

  Press on.

 6. Labda ufafanue kidogo wa hii sentensi
  (Pili, Matukio ambayo yakitokea Africa, Watu wanakufa lakini yakitokea Nje nyingine za Walioendelea, Uhai wa Wanadamu unaokolewa sana tu, sasa kipi ni kipi Wandugu? )
  Mimi nadhani ni mtazamo tu wa kuyatykuza mataifa hayo yaliyoendelea , kufa ni kufa tu , hata huko tonedo, tsunami zinaua watu sio Africa tu

 7. Kwa majibu yangu ya haraka haraka;Mungu huwa anahusika/anajua kila kifo cha mwanadamu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s