Vijana msiwape uongozi watu mafisadi – Sitta

sitta

Mgeni rasmi Samuel Sitta (katikati) akiwa na Dr Harrison Mwakyembe na Askofu Godfrey Malase

Dar es Salaam. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amesema vijana watafanya makosa endapo tu wataikabidhi nchi mikononi mwa wahuni ambao wanapenda kutumikia matumbo yao kwa nguvu ya pesa kitu kitakachowacheleweshea maendeleo yao.

Sitta anayetajwa kuwa miongoni mwa wawania urais 2015, aliyasema hayo  kwenye mkesha wa Mwaka Mpya uliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo alikuwa akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete.

“Mtafanya makosa kuwapa nchi watu wa jinsi hii ambao badala ya kuwatumikia wananchi wenye hali ngumu  kila kukicha, wanazidi kuteseka kunakosababishwa na mafisadi wachache.

“Endapo vijana wataendelea kupima viongozi kwa nguvu na uwezo wa pesa, tutaendelea kuchelewesha maendeleo ya nchi,” alisema Sitta.

Mbali na hayo, Waziri Sitta alibainisha kuwa kuna baadhi ya viongozi yeye akiwa mmojawao wanaweza kuibadilisha nchi, kwani maono yao ni kufuata tochi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Mkesha huo ulioandaliwa na Umoja wa Makanisa Tanzania, ulihudhuriwa viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi.

–Mwananchi

Advertisements

2 thoughts on “Vijana msiwape uongozi watu mafisadi – Sitta

  1. >Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amesema vijana watafanya makosa endapo tu wataikabidhi nchi mikononi mwa wahuni ambao wanapenda kutumikia matumbo yao kwa nguvu ya pesa kitu kitakachowacheleweshea maendeleo yao.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s