Hatua kwa Hatua na Bwana

hatua

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,   Baraka nyingi za Kiroho na Kimwili tayari tunazo na zinajidhirisha ktk macho ya nyama na rohoni lakini pia zile zinazofahamika kama kubwa-kubwa tunazotakaga sana,  ni zetu ila kama hazijajidhihirisha, usipate shida ya kunyong’onyea moyo maana Mungu wetu huenda nasi hatua kwa hatua ktk kutupatia mema   Kumbukumbu la Torati. 7:1,6,7,8,20,22,23…1Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang’oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 6  Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi. 7Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; 8  bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. 20  Tena Bwana, Mungu wakoatampeleka mavu kati yao, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako. 22  Naye Bwana, Mungu wako, atayatupia nje mataifa yale mbele yako kidogo kidogohaikupasi kuwaangamiza kwa mara mojawasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu..   Kutoka.23:29-3029.Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmojanchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. 30Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.   Mistari ya 22 na 30(Kumbu na Kutoka) kuna neno KIDOGO-KIDOGO, in English Biblia nyingi zimetumia adverb – little by little maana yake ‘a little bit at a time, ‘by small degrees or increments’, ‘gradually, ‘by small degrees or amounts,  ‘piece by piece, ‘progressively, ‘slowly. Kwaiyo ni sawa sawa na kusema kwa hakika kua Mungu alisema  kua atayatoa mataifa nje kidogo-kidogo au kidogo kidogo kwa muda fulani halafu tena kidogo-kidogo kwa muda tena mwingine au pole-pole au hatua kwa hatua au kipande kwa kipande au kwa kiasi kichache-chache  ili hatimaye Israeli kurithi nchi yote wakati wakiwa nao wana Israel wanaongezeka  Kinyume cha neno Kidogo-kidogo(little by little) ni kikubwa-kikubwa-kwa Kiswahili kisichofasaha au maana  ghafla, kushitukiza, haraka-haraka,  ya kasi nk. kwa ivyo tunaweza sema kwa hakika kua Mungu alisema  kua HATAyatoa/fukuza mataifa yale haraka-haraka,Ki-ghafla, kwa mshitukizo,kwa kasi nk. Kwa nini Hatayatoa haraka-haraka katika mwaka mmoja bali kidogo-kidogo- little by little? AU… SWALI KUU: Unadhani Kibiblia na kiuzoefu wako na Bwana ktk kutembea na kumtumikia, kwa nini Mungu ameonekana kua ni Mungu wa hatua kwa hatua, hana presha na time? Kuna mambo gani katikati hapo tunapata/Mungu anakusudia tupate before His full visible manifestations on us?. Maandiko ya Msingi kwa soma hili yamesema sababu 2 nazo ni:  

  • · Nchi itakuwa ukiwa,wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu/bara wakakusumbua. Yaani NCHI/BARAKA NILISHAWAPA SIKU NYINGI NILIPOKUJA KUWAOKOA Kutoka.3:8,16-17 na kwa kua Mungu   hutangaza mwisho tokea mwanzo-Isaya 46:10, ivyo baraka alishaindaa na kuitamka kua ni yao ila KUIDHIHIRISHA/KABITHI ni kidogo-kidogo/hatua kwa hatua, maana atakua anawatimua Mataifa upande mmoja wa Nchi kisha watamalaki LAKINI upande wa mwingine wa Nchi, Mataifa mengine yanakuwepo yakingoja kufukuzwa ila yanasaidia kutuza Nchi, uwepo wao huko usababishe wasizaliwe wanyama mwitu ikawapa tabu Wana wa Mungu  ktk kutamalaki , ivyo hapa anawatimua, wanatwaa, kule wanabaki kwa faida yao 

  • Wao Wana wa Israel pia Waongezeke ktk Nchi…Kutwaa baraka kunaambatana na kuongezeka = KUKUA( Imani, utakatifu, maombi, utumishi, kicho, Utii, Unyenyekevu, mahusiano,Uvumilivu, Heshima kwa Mungu, Kujua kuisikia Sauti yake,Tabia kubadilika…jumla ya yote ni KUUKULIA WOKOVU

Kwa hiyo, Baraka zile kubwa-kubwa tunazotakaga sana, ziwe za Kiroho or Kimwili, zipo, ni zetu ila ni hatua kwa hatua na Bwana, kidogo-kidogo na Bwana, tuvumilie kwa furaha tuki- Kumbe kuna baraka nyingine zinakua delayed but not denied…zinatimia polepole(kutowatoa Mataifa yale kwa mwaka mmoja) uku jaribu lile lile (mataifa yale) yanayoonekana kuleta tishio kwa baraka yenyewe(nchi kurithiwa), linafanyika baraka tena yaani Mataifa yale kuachwa ili kuzuia wanyama wasiongezeke wasijekuwasumbua kwa kua nchi itakua ukiwa/tupu. Kwa hiyo uwepo wa jaribu/tatizo ni udhirisho dhahiri wa kuja/kuwepo kwa baraka Dondoo za Kukazia kuhusu Hatua kwa Hatua na Mungu yaani ‘’kidogo-kidogo’’ na si ‘’Kikubwa-Kikubwa’’/’’Kiharaka-haraka’’   Unakumbuka ilimchukua MUSA miaka mingapi toka kukua ndani ya jumba la kifalme kuja kua mchunga mifugo kisha kua Mkombozi wa Wana-Israel? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilimchukua Mungu siku ngapi kuumba uilimwengu? Kwani si ana nguvu zote, si nikusema/kutamka tu mara moja na vyote kwa sekunde au chini ya sekunde vinatokea kwa ukamilifu wote kwa kua ana uweza WOTE kabisa, kwanini siku 6? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu na kwa utaratibu wake   Unakumbuka ilimchukua Mungu mapigo mangapi ili hatimaye Pharao kuachilia wapendwa? Si angemtandika tu ‘’kik moja’’ maridadi kabisa ikawa movie THE END?Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilimchukua Daudi muda gani toka machungani kuja kumiminiwa mafuta mpaka kukalia kiti kwa hakika? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu taratibu   Unakumbuka Daudi  alivyo muombea maombi ya aina gani mwanae Selemani wakati anakua mfalme na kua alihitaji kupata  uzoefu kwanza ,so he needed people close to him for guidance? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilichukua muda gani toka kua Petro wa leo kiroho kesho kukana mpaka kua Petro kiongozi na mtumishi imara? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilimchukua Yesu miaka mingapi kabla hajajitokeza rasmi kuanza kazi wazi wazi? Why would He have to live 30 yrs ndipo atokeze kikwelii? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu.

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

3 thoughts on “Hatua kwa Hatua na Bwana

  1. Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,   Baraka nyingi za Kiroho na Kimwili tayari tunazo na zinajidhirisha ktk macho ya nyama na rohoni lakini pia zile zinazofahamika kama kubwa-kubwa tunazotakaga sana,  ni zetu ila kama hazijajidhihirisha, usipate shida”

  2. Kaka Selelii, Ubarikiwe sana. Hakika Mungu kanipa ufunuo mpya katika somo hili! Na uzuri wa Bwana uwe juu yako na utumishi wako uliotukuka! Daniel.

    Sent from my HTC

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s