Mchungaji alisha washirika Nyasi!!

Woman eating grass, Rabboni Centre Ministries

Mchungaji Lesego Daniel kutoka Afrika Kusini alilisha washirika wake nyasi!!

Mchungaji huyo kiongozi wa kanisa la Rabboni Centre Ministries amepata ufunuo wa kuponya kwa kulisha watu nyasi, kwa mujibu wake : “Kulikuwa na wafuasi wengi na wengine hamuwajui. Hebu Mungu awaoneshe kwamba kuna miujiza mingine Mungu alitaka mtu aifanye, mambo mapya, Nathanael alikuwa mwanafunzi wa Yesu lakini hakuna kitabu cha Nathanael, Vipi kuhusu miujiza, Ishara na maajabu? Vipi kuhusu hao ambao hawajatajwa kwenye biblia? au kufundisha. Tunajua kuhusu Petro na wengine itachukua nguvu za Mungu kuonekana kwa Bartholomayo, Tomaso aitwaye pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wawili wa Zebedayo na wengine wawili wa wanafunzi wake….” 

“Ulimwengu hauwezi kuona au kusikia na baadhi ya watu wanaishi kama wasiomjua Mungu na kumkosoa Bartholomew kwa sababu hawawezi kumwona. Umekula nini? Mwili na damu na yeye anaishi ndani yangu, siku zote yuko ndani yangu, na yeye anaishi ndani yangu. Njoo na ule ili macho yao yaweze kuona” 

Daniel Lesego

Picha ya Mchungaji mwenyewe

Washirika wakila nyasi!!

Advertisements

12 thoughts on “Mchungaji alisha washirika Nyasi!!

 1. wapendwa mliokula nyasi poleeeeeeeeeeeni, naungana na seleli kweli mnahitajika BAKORA SWAAAFI

 2. Nini matokeo ya hao wapendwa waliotafuna nyasi?Wamepokea miujiza yao?Wapendwa tuwe macho

 3. MATHAYO 7:22
  “WENGI WATANIAMBIA SIKU ILE, BWANA,BWANA, HATUKUFANYA UNABII KWA
  JINA LAKO, NA KWA JINA LAKO KUTOA PEPO, NA KWA JINA LAKO KUFANYA MIUJIZA MINGI. NDIPO NTAAWAAMBIA DHAHIRI, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ONDOKENI KWANGU, NINYI MTENDAO MAOVU.

  2 PETRO 2:2
  “NA WENGI WATAFUATA UFISADI WAO; NA KWA HAO NJIA YA KWELI ITATUKANWA”

 4. Tukiwaambia “Dini si mchezo”, mnatuona wazushi!!
  Ukilikataa Neno la Mungu alilokufunulia, ukachagua kufuata Dini yako ni lazima uishie kama hawa wanaokula majani!!! Tena huenda hawa wana afadhali, wakitoka hapo wanakwenda kupimwa minyoo na kuendelea na maisha yao; hebu wafananishe na wale, kwa maelekezo ya dini yao, wakaenda kupiga kambi airport wakitaka kupanda ndege za watu bure na bila pasi za kusafiria, waende wakahubiri Injili Ulaya, walipotimuliwa wakaenda kukaa kwenye mashamba pori na wengine wakaumwa na nyoka wakafa!!!

  Msicheze na Neno la Mungu, mtajichafua mlivyotakaswa na mjikute mmekuwa najisi mbele zake!!!

 5. aisee ni shida..watu tusome Neno jamani..na pia tuwe tunajifunza kutoka kwa watumishi mbali mbali.,,hilo linajenga ufahamu wako kuhusu MUNGU zaidi

 6. Ukiwaita wagalatia, utaonekana umewahukumu!! Lakini hata mkisema hivyo, Siyi hana maana ya kuwahukumu ila anawaambia tu kuwa TOKENI BABELI.
  Mimi niwatia moyo waachane na kuamini neno lolote la mchungaji au mwalimu yeyote, isipokuwa neno hilo, limethibitika kwenye Biblia kuwa ndivyo lilivyo.
  Kula nyasi ni ishara ya laana!!
  Hosea 4:6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa

 7. Huyu sio mchungaji amepagawa na pepo, wapo wachungaji wengi tu sana ambao wanatudanganya kuwa wanaongozwa na R/M kumbe ni pepo, la muhimu kwa waumini wenyewe kugundua haraka kwamba mtumishi wetu amepotoka na kumrejesha kwa upole, jingine ni authorities zetu kama (CCT,WAMA,TAG, EAGT ) kupewa mamlaka kamili ya kumuonya na ikibidi kumfutia usajili mtumishi anayetumia ukristo vibaya,
  Mungu atusaidie wapendwa.

 8. DINI YETU NI:
  Agano jipya, (MATHAYO 26:28)
  kila atayeingia yuko chini ya mjumbe wetu YESU KRISTO.

  MCHUNGAJI WETU NI:
  Roho mtakatifu(YOHANA 14:26)
  …….atawafundisha yote na kuwakumbusha yote.
  Kama huna Roho Mtakatifu Mungu hakujui.(yohana 3:5, matendo2:4, warumi8:9, yuda 1:19)
  KAMA HUNA ROHO MTAKATIFU UNA ROHO YA DINI YAKO: SIKU YA MWISHO USIMWAMBIE YESU NIPELEKE MBINGUNI IAMBIE DINI YAKO NIPELEKE MAKAO MAKUU YA DINI YETU LABDA KUNA USALAMA. MAANA DHAMBI YA KUMKEJERI ROHO MT HAISAMEHEWI NDUGU (MATHAYO12:31,32,36) USIWE MPUMBAVU. USITAFUTE SIFA KWA KUMKASHIFU ROHO WA MUNGU,POLE SANA.
  KATIBA YETU NI:
  Biblia (YOHANA17:17)
  ……..uwatakase kwa ile kweli neno lako ndiyo kweli.

  KANISA LETU NI:
  Moyo wako(YOHANA 4:24)
  ……itakuwa nyumba ya sala. ……tutakuja na kufanya makao kwake…….imewapasa kuabudu katika roho na kweli.

  SILAHA YETU NI:
  Maombi (LUKA 22:46)
  Maombi yana nguvu kubwa sana. Mtu anakuwa maarufu mbinguni kwa sababu ya maombi.
  Maombi yanaweza kufanyika hadi mtu akafa. Muombaji hatekwi kirahisirahisi. Muombaji haingii majaribuni yakamuangusha. Mchungaji hawezi kumchanganya mtu muombaji. Labda waombaji wa baraka masaa yote hawana muda wa kuomba nguvu za Mungu na utiisho wa kimungu ili kulinda utakatifu wao.

  KITAMBULISHO CHETU NI:
  Upendo
  Basi watendeeni wengine ambayo mgependa wao wawatendee
  mathayo 7:12 kama huna upendo Mungu hakujui.

  Kwa hiyo basi uponyaji siyo jukumu lako au la mchungaji wako ni jukumu la Yesu.
  Mfano mwanao akipata tatizo utasubiri akuombe ndo umpeleke hospital!?, hautachukua tu jukumu la kumpeleka bila kuambiwa maana unajua ni jukumu lako.
  Sisi tuna jukumu la kutii amri za Mungu halafu Mungu ana jukumu la kulinda uhai wetu. Usipotimiza jukumu lako lazima utaingilia jukumu la Mungu.
  NAOMBA WAZIRI WA MIFUGO AWAONGEZE HAO WAUMINI KWENYE IDADI YA MIFUGO ILIYOKO TANZANIA.

 9. POLENI NDUGU MLIOLISHWA NYASI MUNGU ANGALIPO VITANI ATAWAPIGANIA,MTAFUTENI MUNGU KATIKA MAANDIKO
  (ref.YOHANA 17:17),KAENI MIGUUNI PAKE, HATA SIKU ILE TUKAHESABIWE USHINDI NA KUTUPA TAJI ZETU MIGUUNI PAKE MAANA YEYE NDIYE ASHINDAYE NDANI YETU.MUNGU ANGALIPO ANAENDELEA KUWAVUTA WATU KWAKE.(MKISHINDA HAPO KWENU KUWE SIKU MMOJA USHUHUDA KAMA NDUGU YETU PAULO)

  AYUBU 12:16
  “KWAKE YEYE ZIKO NGUVU, NA MAKUSUDI KUFANIKIWA; HUYO ADANGANYWAYE NA MDANGANYI PIA NI WAKE.”

  AYUBU 12:22
  “HUVUMBUA MAMBO YA SIRI TOKEA GIZANI NA HICHO KILICHO GIZA TUPU HULETA MWANGANI.”

  GIZA LIKIWAPO YASHIKWE HAYA;
  2 PETRO 1:16
  2 PETRO 1:19

 10. mh! kweli shida noma umeona kali ya mwaka! na mshkaji(mchungaji)alikuwa anawacmamia au???

 11. Ha ha ha ha haa!!
  Hebu na wewe umeona kama nilivyoona mimi. Pastor ni mali oriented jamaa!!! Mtaniambia ninyi waolokole kama na hiyo nayo ni kazi ya RM.

 12. Kwa mambo kama haya, ndipo mimi hupenda sana kuhimiza Wapendwa kua, tutumie hata GOD GIVEN AKILI AU COMMON SENSES ZA KAWAIDA ku-rule out mambo! Pastor mwenyewe tu ukiimwangalia tu alivyo, unaona tu hapo ni ‘shekeli strategist; call! yuko yankiiiiiiii, sopu-sopu dizain ivi( Men and women should not be boring and bad in looking ofcoz) nonetheless, wengi wa Mayanki hawa wa leo dot com Ministers, hamna lolote, fix tu za kuishi Majijini na Mijini, well hata mashambani siku izi, I CANT IMMAGINE mtu na akili timamu, reasoning yako iko swafi, IQ iko active mbali na network za ndani, unawezaje kaa/submit kwa ka-yanki Minister kama ako, hunategemea nini kama siyo ma-deal ya town na ya mashambini kununua mashamba na migodi sites! oo yes in this case, watakula mpaka ‘soodast” ya/from mbao.

  Inawezekanaje unaambiwa neno/una hubiriwa bila hata ku-reason? unakula tu kila kitu? kisa kasema so called ”Man/ Women of God’ Mr/Miss ….and the most honorable and dangerously untouchable Apostle and Prophet! Toka lini mwanadamu kufanya manyasi bonge la menyu? wamekua Nebukadreza King? cant use common senses jamani! inatia hasira kweli, wote wanahitaji kutandikwa mboka kuanzia kwa Pastor wao na Kondoo, wote stick tu kwanza then counseling later.

  Press on

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s