Ulivyo wa thamani mbele za Mungu!!

 thaman

Amani iwe nanyi enyi nyote,         

Ukiwa na Kitu cha thamani husababisha mambo kadhaa mfano:

 • ·   Gharama kubwa na Umakini sana wa kukitunza(Mfano Ikulu, Nyumba kubwa za Dar zina geti zinazo gharimu kiwango cha kujenga nyumba nyingine ndogo, Rais wa Nchi, Bank Kuu ya Nchi, Kambi za Kijeshi) 

 • ·   Tabia ya Mwenye cha thamani hubadilika( Mfano: Kupata fedha kubwa kwa mara ya kwanza na uko ndani ya daladala kumfanya mtu hataki/anashituka-shituka kila mara Mtu akimgusa, pia imeandikwa ‘pale hazina ilipo na moyo upo hapo..Matt.6:21 Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako yaani ingawa hazina hii inazungumzia maisha yajayo lakini pia inatoa picha namna hazina-kitu cha thamani kinavyoweza husiana na moyo-ambako ndani utoka tabia kadhaa zinazoweza mbadilisha Mtu kwakua na kile kitu cha thamani) 

Mipango mizito na mikubwa huwekwa kwa ajili ya kukiendeleza/Kikuza hicho kitu cha thamani-(Mfano mgodi wa dhahabu, Wanyapori, Misitu, Mtoto mwenye bidii Shuleni na nidhamu kwa Wazazi) 

 • ·    Uvumilivu wa kuchukuliana na mharibifu au asiyejali hicho cha thamani ulicho nacho, hua ni mdogo sana, ni rahisi kumchukulia hatua za kinidhamu au kisheria tena haraka bila kuchelewa (Mfano: Kiwanja/Duka/Hotel yako kutumiwa/chezewa na mwingine bila ruska yako, Shamba lako la mazao  kuchungiwa mbuzi) 

Kama ‘’Thamani’’ ni Kitu kinachoweza pelekea mambo mazito hayo, basi ni Kitu cha ajabu sana na kukosa kukifahamu, ni hasara ktk maisha haya na yajayo kama marekebisho hayatafanyika kuuondoa ujinga kwa mtu haraka sana ili atambue thamani yake/Kitu alichonacho.Ni huzuni kubwa, masikitiko na hasara isiyosemekana kwa uchungu, Mtu kutojitambua thamani yake au ya kitu alichonacho. Katika mambo ya Kiroho na Imani, tunatambua thamani ya jinsi tulivyo na yale tuliyonayo kwa kusoma na kutafakari Neno ili kujua KWELI zilizomo kutuhusu sisi..Yohana.8:31-32..  31Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32  tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.( Zingatia hao aliwaambia hilo Neno ni Watu waliokua wamemwamini Tayari-Wameokoka lakini bado anawaambia…Wakikaa NDANI ya –NENO lake ndipo Watajua KWELI halafu WATAWEKWA HURU-Kumbe kuna uhuru zaidi baada ya Kuokoka yaani kua huru toka shetani-kisha kuna uhuru tena kadri tunavyoifahamu KWELI.

Mifano na hasara ya Kutotambua thamani ya kitu

 • ·   Watoto wadogo wa chekechea, shule ya msingi, miaka ya karibuni  wanapomaliza shule, nao huvishwa kofia na majoho kama yale ya Wanaomaliza  Chuo Kikuu matokea yake leo hata kuyavaa ukimaliza Degrees hayana upako wake kama zamani

 • ·  Kabila fulani Afrika lenye ardhi yenye dhahabu nyingi karne za nyuma, walikua wanachezea dhahabu bila kujua, Wazungu walipokuja wakawapa gorori, wao wakatoa  dhahabu

 • ·   Msichana/Mke kujiachia bila kujijali ktk usafi na urembo, anakosa wachumba au upendo wa mume, anamlaumu shetani na Mungu

 • ·    Mrithi wa mali-kitu cha thamani- akiwa mtoto hawezi kujali thamani sasa ili hasi haribu, huwekwa chini ya uangalizi-Wagal.4:1-2.. Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake. 2 Wakati huo wote yuko chini ya walezi na wadhamini mpaka wakati ule uliowekwa na baba yake) 

NAMNA YA KUTAMBUA THAMANI ULIYONAYO MBELE ZA MUNGU

Zifuatazo ni baadhi ya KWELI kutuhusu sisi na zinazoonyesha thamani ya ajabu tuliyonayo.( Yaani kwa thamani tuliyonayo kwake, ‘’Kweli’’ zifuatazo za Neno, zinatuonyesha Mungu alifanya nini Kabla, Wakati na Baada ya Kuokoka) 

 • ·   MPAKA ULIFAHAMU KUA KUNA KUOKOKA NA UKAAMINI, NI MUNGU ALIKUFUNULIA..Matt.11:25-Kulikua hakuna namna ya wewe kufunguka ufahamu wa ndani kujua kuna kumwamini Yesu kwa namna hai hii tuliyonayo tofauti na zamani kwa namna ya kidini/kikavu na mazoea mpaka Mungu mwenyewe alipoamua kukufunulia 

 • ·     MPAKA ULIKUJA KWA YESU, MUNGU ALIKUJAALIAYohana.6: 65 Kisha akasema, “Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakuna awezaye kuja kwangu asipowezeshwa/jaaliwa na Baba yangu.”-Wewe kuamini kisha kumjia Yesu kwa toba na kumpokea, ni Mungu alikujaalia/ruzukia hilo la sivyo ungekufa na Dini yako. Ni ngumu sana kumng’oa Mtu toka mfumo wa Imani/dini/kuabudu Mungu aliouzoea, kuurithi au kuukuta ktk jamii/koo maana hua anajua kwa moyo wake wote kua mfumo anaotumia kumwabudia huyo Mungu ni wa ukweli kabisa na anachoamini ni hakika  kumbe ni giza kweli kweli ivyo anahitajika Mungu mwenyewe kung’o ilo giza ktk akili, moyo, nafsi na roho ya Mtu 

 • ·  MPAKA WEWE UMWAMINI YESU, MUNGU MKUU ALIKUVUTA NA KUKUPELEKA/KABIDHISHA KWA YESU… Yohana. 6: 44: ‘’Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta kwangu; nami nitamfufua mtu huyo Siku ya mwisho’’… Embu Fikiria ni Mungu wa mbingu na Nchi, aliyekuwepo milele iliyopita, sasa na ijayo, aliyeumba kila kitu Nchini na Juu, huyo ajishughulishe na wewe mpaka kuja kukuvuta na kukukabidhi kwa Mwanae!!!!!!!! Ni ajabu  sana Mungu alivyotupenda, inatoa machozi kujua UKWELI huu 

 • ·KWA NJIA YOYOTE ILE HUTATUPWA NA YESU LABDA UJITUPE MWENYEWE.Yohana.6:37-38…Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu, 38 kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwa ya yule aliyenituma.-Kwa upande wa Yesu, hana agenda wala nia ya kukutupa ndio maana amesema wazi, hatafanya hivyo ila maamuzi ya kubaki kwakwe au la, yako kwa Kondoo, haingilii uhuru au utashi wa Mtu. 

 • ·  HUTAPOTEA KAMWE LABDA UJIPOTEZE MWENYEWE NA MPANGO WALIONAO BABA NA BWANA WETU NIKUKUFUFU SIKU YA MWISHOYohana. 6: 39-40… 39 Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote Siku ya mwisho. 40 Maana anachotaka Baba yangu ndicho hiki: kila amwonaye Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele; nami nitamfufua Siku ya mwisho.”-Kwa kua hana mpango wa kukutupa vivyo hivyo hana mpango wa kukupoteza. 

 • ·  HUTACHUKULIWA/NYANGANYWA/NYAKULIWA TOKA KWA MKONO WA BABA YAKE YESU..Yohana.10:29-30.. 29 Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wale hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba. 30 Mimi na Baba, tu mmoja. 

 • ·  ULICHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA DUNIA-Waruni.8:29-39 na Waefeso.1:1-6..Wakati hata dunia haijawepo, alishakuchagua, ulikua ktk agenda yake na ikakamilika kabisa 

 • ·  TUKIWA BADO TUNAMUUDHI NA KUMKERA KWA DHAMBI ZETU, YEYE ALITUPENDA HIVYO HIVYO-Warumi.5:8..Upendo wake haukuthihirishwa tulivyokua wasafi baada ya kuokoka bali wakati ndio kwanza wachafu sana, huko huko  na ktk hali hiyo, ndiko alitupenda kwanza kisha kutusaidia kutoka huko! Ni ajabu sana upendo wake Mkuu huu 

 • ·   ALITOA UHAI WAKE KWA AJILI YAKO..Yohana.15:13..Mfano wa Mke aliyelia sana wakati Mumewe amekufa na akang’ang’ania hakubali Mumewe afe na kuzikwa peke yake akasema anafukiwa naye akajitupa kaburini, waombelezaji wakaamua wawazike wote tu sasa, walipotuma koleo la kwanza tu,  Mke akasema, nivuteni jamani nitoke Kaburini 

 • ·    ANAKUITA WEWE RAFIKI YAKE..Yohana.15:15..Fikiria iliyvo tamu kuitwa na Yesu siyo Obama, kuwa wewe yake Rafiki 

 • ·   ALIJIVUA HADHI YAKE KUBWA SANA ILI KUJA CHINI KUKUTAFUTA NA HATIMAYE KUKUPATA-Wafilipi.2:4-11-Fikiri Obama atoke Ikulu ya Marekani halafu aje kuishi Manzese ili mpango wake wa kufahamiana na Wananchi Waafrika wenzake kisha awasaidie, ukamilike! 

 • ·    UKARIBU NA UPENDO WAKE KWAKO UNATISHA SANAIsaya.49:15-16..Kama anaweza kukuchora kwa kiganja chake-lugha ya picha ya Biblia kuonyesha Ukaribu  na mahusiano yake kwetu na  na kama Mama anayejua uchungu wa mwana tena ni ‘’ Mtoto/Kitoto anayenyonya’’ si mwana mkubwa, anaweza msahau Mmanae wa umri huo  lakini Mungu anajisema kua Yeye hawezi, basi  ukaribu na upendo wake kwako ni zaidi ya akili maneno ya kibinadamu kuelezea 

 • ·  ANAKULINDA KULIKO KAWAIDA..Zakaria.2:8-9..Kama Mtu huwezi gusa mboni ya jicho lako mwenyewe au ya mwenzio, basi Mungu anatulinda hakuna mfano maana anayetugusa, anagusa mboni yake 

 • · BABA NA YESU WAMEKUFANYA WEWE NI NYUMBANI KWAO/UMEBEBA SERIKALI YA MBINGUNI…Yohana.14:23, 2 Wakorinto.5:20-sisi ni Mabalozi wa Serikali iyo.Fikiria Kazi za Balozi wa Nchi nyingine ktk Nchi aliyopo Kikazi anakuaje? 

 • ·  UMEFANYWA KUA MTU WAKE MUNGU MAALUMU (SPECIAL)-1Petro.2:9-Ukishakua spesheli wa Mungu, unataka nini tena Duniani? 

 • ·  UMEFANYWA RAIA NA MWENYEJI MBINGUNI, WEWE SI MKIMBIZI HUKO JUU – Waefeso. 2:19-Ukishakua Raia si wa Marekani, New-Zealand au Africa Kusini bali Mbinguni, unataka hadhi gani tena? 

 • ·    MUNGU KUKAA MWENYEWE MBINGUNI BILA WEWE, HAJISIKII RAHA…Ufunuo.21:3-Maskani yake ni pamoja Wanadamu,Matt.1:32-anaitwa Emmanuel- Mungu pamoja nasi, Yohana.14:1-3-Mahali panaandalia kwa ajili yako- Mungu mwenye uweza wote anayejitosheleza kwa kila kitu toka hata hatujaumbwa lakini anaoona hakuna raha kamili bila kuzungukwa na Wanadamu ambao wanakua kwakwe kama Wana, upewe urithi/zawadi gani kubwa na ya kudumu kama huo? 

 • ·  TUMETIWA MHURI KUA WAKE NA ROHO MTAKATIFU NI DHAMANA KWA YALE YOTE ALIYOTUPA.2Wakorinto.1:21-22-..21 Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na ninyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu; 22 ndiye aliyetutia mhuri wa kuwa mali yake yeye na kutujalia Roho mioyoni mwetu kama dhamana ya mambo yote ambayo ametuwekea na  Waefeso. 1: 13-1413 Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia. 14 Huyu Roho ni dhamana ya kurithi yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake! Wagal.4:1-7: . 3 Hali kadhalika na sisi tulipokuwa bado watoto, tulikuwa watumwa wa pepo watawala wa ulimwengu. 4 Lakini wakati ule maalumu ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe aliyezaliwa na mwanamke, akaishi chini ya Sheria 5 apate kuwakomboa wale waliokuwa chini ya Sheria ili sisi tufanywe wana wa Mungu. 6 Kwa vile sasa ninyi ni wana, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwenu, Roho ambaye hulia “Aba,” yaani “Baba.” 7 Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi, wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.). 

Fikiria neno/kifaa kinaitwa ‘’Mhuri’’ hua unakazi gani ktk maisha ya kawaida ofisini, kwa balozi wa nyumba Kumi, Serikali za Mtaa, kwa Mkuu wa Nchi, Mkoa, Wilaya, Kanisa, Shirika, Kampuni? na unapigwa kwa karatasi au barua, kunatokea au inasababisha uzito, hadhi na matokeo gani kwa aliyepewa iyo barua? Ndivyo Mungu ametufanyia sie Wake. Kama haitoshi, ili kutuondolea wasiwasi pamoja na uthibitisho mzito wa kutupiga Mhuri, ametupa ‘’Dhamana’’ yaani Roho Mtakatifu kutuhakikishia pasipo kuacha shaka kua ana maanisha anachofanya na kwa dhamana iyo, iwe dhahiri shairi kua ametupa na atatupa yote na kwamba kweli sisi ni wake haswaa. 

Kuzijua KWELI hizo kuhusu Wewe alizosema Mungu, ni silaha ya hatari ambayo Shetani asingependa uikamate. Ni kweli THAMANI YAKO mbele za Mungu ilimuangaisha na kumgharimu  sana Baba yako wa Mbinguni Kabla, Wakati na Baada ya Kuokoka. Fahamu na ishi ktk KWELI IZI ili uwe huru zaidi na kuwa imara sana ktk Imani, ukifurahia yale Mungu alikufanyia kwa kua alikupenda, anakupenda na atakupenda mpaka mwisho. 

Press on, 

Edwin Seleli

Advertisements

4 thoughts on “Ulivyo wa thamani mbele za Mungu!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s