Majaribu hutoka kwa Mungu na Shetani?

majaribuu

Amani ya Bwana iwe pamoja enyi nyote.

Majadiliano na fafanuzi ktk mada hii bila shaka yatatusaidia na kutupa ufahamu tuepuke kuwanung’unikia na kuwalalamikia Mungu na Wanadamu. Neno ‘’Majaribu’’ linaeleweka na kutumiwa na wengi hata limetungiwa nyimbo za Injli lakini nilipotafakari kwa uangalifu mambo ya Mungu na  tunavyolitumia neno ilo ktk maisha haya, nimelileta kama mada ili tupate ufahamu hasa kwenye swala la kufafanua ili kuweka utofauti wa wazi  kipi  ni hiki na  wala si kile, kwa maana iyo kupitia ninyi vyombo vya kazi vya Bwana, tunaweza pata akili, uelewa, ufunuo, Neno, Maandiko, fundisho, uzoefu, ushuhuda nk kwa ajili ya kusaidiana na kujengana Kikanisa/Kiroho na Kiimani.

Ili kuuingia Mjadala vema, unaweza tafakari  yasemwayo ktk Maandiko haya:

Kwa upande mmoja, Imeandikwa, furahini mnapoingia majaribuni-Yak.1:2, Wanafunzi walitishwa kutohubiri-Mdo.4:21,29,Stephano akapigwa mawe na kufa-Mdo.7:57-60, Mitume wanawekwa jela, wanapigwa na kuachiwa Mdo.5:16-42,Paul na Sila wakapigwa na kutupwa gerezani-Mdo.16:19-26,Petro anangojea kesho yake kuuawa baada ya mwenzake Yakobo kuchinjwa –Mdo.12:1-17, Ayubu anapoteza Watoto, Mali na Afya-Ayubu.1:14-19, 2:7, Mfalme Hezekia anaugua na Mungu anamwambia atakufa kisha akaomba, kifo kinafutwa-Isaya.38:1-4/ na 2Wafalme.20:1-4, Mtu ni kipofu toka kuzaliwa na ulemavu huo upo  kwa ajili kazi za Mungu kudhihirishwa ndani yake-Yoh.9:1-5, Ainea ameugua na amepooza miaka 8 pia  Dorcas mpendwa amekufa Petro anaomba, Ainea anapona na Dorcas anafufuka-Mdo.9:32-42, Mama Mkwe wa Petro amelala anaumwa homa, Yesu ana mgusa, anapona-Matt.8:14-15 

Kwa upande mwingine, imeandikwa kuwa duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu-Yoh.16:33, Je  tupate mema mkononi mwa Mungu nasi tusipate mabaya-Ayubu.2:10, jaribu halikuwapata ninyi isipokua lililo kawaida ya wanadamu-1Wakor.10:13. 

Kutokana na kichwa cha mada, nakigawa kupata Maswali makuu 4 ili kutoa mwelekeo mzuri unapojadili/changia, nayo ni haya:

Moja: Tukio/jambo gani  likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hili ni jaribu(test and trial, temptation)?

Mbili: Tukio/jambo gani  likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hiki ni kitu cha kawaida tu kwa wanadamu kwakua wanaishi duniani na kwamba tukiomba au tusiombe, tuko kiroho sana au kidogo, tumeokoka au bado, lazima yatatokea/tupata tu bila shaka? 

Tatu: Tukio/jambo gani  likitupata/tokea, tunaweza sema kwa UJASIRI NA UHAKIKA kua hili ni jaribu(test and trial) toka kwa Mungu lenye nia ya kutuimarisha au hili ni jaribu(temptation) la shetani kututoa kwa Mungu?

Nne: Au kuweka katika uhalisia, Mfano Ukifiwa na Mke, Mme, Mtoto, gari ikiibiwa, pinduka, ukavunjika mguu, ukiibiwa mali dukani, ukavamiwa na majambazi, ukipigwa sokoni wakati una hubiri au umekaa tu bila kuhubiri, ukakabwa na vibaka, ukiugua ugonjwa, kanisa-jengo likiunguzwa, ukikosa kazi muda mrefu, ukipata kazi lakini bosi akawa mnyanyasaji, Kanisa  kutokukua, huduma kudumaa, kutopandishwa cheo,kukosa pesa,kutoweza kujikimu kwa utele mahitaji ya maisha, kuchelewa kuoa/kuolewa, kutopata mtoto, kua tasa nk, yapi kati ya hayo ni majaribu toka kwa Mungu, Shetani  au ni  mambo ya  asili au kawaida tu ktk maisha duniani hapa?

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

4 thoughts on “Majaribu hutoka kwa Mungu na Shetani?

 1. Nashukuru sana kwa mtoa mada kwani nimejifunza maana ya mapito, jaribu na jaribio na kufahamu kuwa Mungu huwa hatujaribu bali hutupa mtihani/jaribio ila shetani ndiye huwa anatujaribu ili tuone kwake kuna urahisi! Asanteni na Mungu awabariki!

 2. Test – jaribio- eg Ibrahim kumtoa Isaka
  Trial – pito- eg Paul kupatwa misukosuko baharini, kuchapwa bakora
  Temptation – jaribu- eg Ayubu na majipu yake

  Kwa bahati mbaya sana haya matatu yote waswahili hupenda kuyaita majaribu bila kujua ni mambo matatu tofauti.

  Pito na jaribu yote hutoka kwa adui, lakini jaribio hutoka kwa Mungu.

  Pito ni changamoto tu za maisha ya kila siku ya mkristo, eg kukosa chakula, kukosa mavazi, kusemwa vibaya na watu wa karibu, kukatishwa tamaa, kukataliwa na mchumba n.k
  Ni changamoto ambazo azina lengo la kumtoa mjaribiwa/mkristo kwa Mungu au kumfanya aikane imani. Lakini pito linaweza geuka likawa jaribu.

  Jaribu ni kipimo ambacho humpata mkristo kwa lengo la kumfanya amwache Mungu au aikane imani. Humfikisha mahali ambapo mtu anatakiwa aamue kuendelea kumpenda Mungu au kumkana. Kwa mfano mateso aliyopata Yohana mwandishi wa ufunuo hadi kutupwa kisiwa cha Patimo.

  Jaribu haliwezi kuwa pito, lakini pito linaweza kufikia kuwa jaribu.

  But, don’t use the three interchangeably!

  Nilikuwa napita tu nikona nitupiemo kidogo.

  Ni somo zuri kujifunza ili kujua nini ndo nini, maana hata kwenye majaribio tu amabyo yenyewe hutoka kwa Mungu watu huwa tunakemea shetani mpaka basi!

  Fikiria kama Ibrahim angeanza kuikemea ile sauti iliyokuwa inamnong’oneza ndani yake amtoe Isaka!!!

  Kwa herini!

 3. Question: “Why does God test us?”

  Answer: When we ask why God tests us, or allows us to be tested, we are admitting that testing does indeed come from Him, as clearly taught in Scripture. Although we are forbidden to test Him (Deuteronomy 6:16; Matthew 4:7), when God tests His children, He does a valuable thing. David sought God’s testing, asking Him to examine his heart and mind and see that they were true to Him (Psalm 26:2; 139:23). In both the Old and New Testaments, the words translated “test” mean to prove by trial. Therefore, when God tests His children, the purpose is to prove that our faith is real. Not that God needs to prove it to Himself since He knows all things; rather, He is proving to us that our faith is real, that we are truly His children, and that no trial or test will overcome that faith.

  In His Parable of the Sower, Jesus identifies the ones who fall away as those who receive the seed of God’s Word with joy, but as soon as a time of testing comes along, they fall away. James clearly explains that the testing of our faith develops perseverance, which leads to maturity in our walk with God. Perseverance in times of trial and testing will result in our spiritual maturity, our completeness (James 1:3-4). James goes on to say that testing is a blessing, because when the testing is over and we have “stood the test,” we will “receive the crown of life, which God has promised to those who love him” (James 1:12). Testing and trying come from our heavenly Father who works all things together for good for those who love Him and who are called to be the children of God (Romans 8:28).

  The testing or trials we undergo come in various ways. Becoming a Christian will often require us to move out of our comfort zones and into areas we have never encountered before. We’ve perhaps heard the saying ‘No pain – no gain’ when exercising our physical bodies. The same applies to exercising our faith in God. This is why James wrote ‘Consider it pure joy, my brothers, whenever you face trials of many kinds’ (James 1:2). Testing our faith can be in small things like daily irritations; they may also be severe afflictions (Isaiah 48:10). Whatever the source of the testing from God, it is to our benefit to undergo the trials.

  The account of Job is a perfect example of God allowing one of His saints to be tested by the devil. Job bore all his trials patiently and “did not sin by charging God with wrongdoing” (Job 1:22). However, the account of Job’s testing is proof that Satan’s ability to tempt us is limited by God’s sovereign control. No demon can test or afflict us with beyond what God has ordained for His perfect purpose and our benefit.

  There are many examples that can be used to illustrate the positive results from our being tested. The Psalmist likens our testing to that of being refined like silver (Psalm 66:10). Elsewhere in Scripture we can read of our trials as that of gold being refined in order to remove all its impurities (1 Peter 1:7). By the testing of our faith, God causes us to grow and mature into strong disciples who truly live by faith in Him, not by what we see (2 Corinthians 5:7).

  When testing and trials come our way, we should receive them with joy, because we know that it is God who allows them to strengthen our faith. When we are knocked about in the storms of life, like the tree that digs its roots ever deeper for a greater grip, we must dig our roots deeper into God’s Word so we can withstand whatever comes against us.

  Most comforting of all, we know that God will never allow us to be tested beyond what we are able to handle and in all things will provide a way out of the test (1 Corinthians 10:13). This does not mean He will remove the trial from us. Why would He when He says trials are for our benefit? Rather, the “way out” is the way through. the trial, with Him ever faithful by our side, until we come out on the other side of it by His grace and power, stronger and more mature Christians.

  http://www.gotquestions.org/why-does-God-test-us.html

 4. Seleli,
  Hii umeileta vizuri sana kaka. Nikupatie kongole za pekee kutoka moyoni mwangu. Nina imani tutabadilishana uzoefu katika hasa ukizingatia kuwa kuna baadhi ya mafundisho ya kimadhehebu, huwa yanapotosha sana juu ya jambo hili. Mungu atuongoze katika kujifunza mada kwa kutumia Biblia na Biblia pekee.
  Nitakuja kwa mchango hapo baadaye kidogo.
  In love
  siyi

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s