Naomba kujua majibu ya maswali haya!!

biblia

1) Baada ya Joshua Mungu alimwinua nani?
2) Safina ya Nuhu ilitua mlima upi?
3) Aliye mwongoza  Paulo sala ya toba ni nani?
4) Mwanafunzi yupi alikufa wa kwanza baada ya Yesu kupaa?
5) Mfalme yupi anafananishwa na Yesu?
6) Watu gani ambao hawakuonja umauti?
7) Baba wa Samson anaitwa nani?
8) Baba wa Ibrahim anaitwa nani?
9) Nitajie watoto wa ibrahim.

10) Reuben alifanya kosa gani kwa baba yake?

11)Mwanafunz gani wa Yesu alikuwa msomi kuliko wote?

Tafadhal nijibu kwa kutumia maandiko. asante

–Prisca

Advertisements

49 thoughts on “Naomba kujua majibu ya maswali haya!!

 1. Asante ni sana kwa majibu yenu nimeyapenda na nawapenda kwa Jina la YESU

 2. Nimependezwa sana na forum hii nimefaidika na majibu ya maswali ambayo nilikuwa nimemuuliza ndugu yangu naye akayaleta humu Mungu awababiriki sana

 3. Mimi naitwa Boniface mwamita natokea mkoa wa mbeya nimejifunza vizuri sana endeleen kutu elewesha mungu awa bariki sana ila samahan kuna Leda na neema daniel katika maelezo yao yana ni changanya kidogo kwa mfano kuhusu mfalme moja ana sema melikzedek
  na mwingine ana sema daudi
  sehemu nyingine watoto wa ibrahim moja kataja 2 isaka na ishamael
  mwingine kataja isaka/yokshan/ishbak/medan/midian/sua
  ina maana ibrahimu alio mke wa pili
  hapa mwingine anasema alishindwa kumuokoa mdgo wake yusufu
  mwingine anasema alilala nae ndugua yake! Vp mimi hapo sijajua nani yupo sahih tuwe ken sana

 4. nimependa maswali na majibu naomba nielekezwe namna ya kujoin discussion

 5. jamani- swali ni baada ya yesu kupaa’iskarioti yesu alikuwa hajapaa. lakn pia. Yesu alichagua mitume ila wanafunzi niwote waliotaka kupata kitu kutoka kwake. hata wewe unayejifunza leo mengi kuhusu yesu ni mwanafunzi.
  Swali: Je ni nini maana ya ule ubatizo wa moto yahana alio usema? je upo leo huo ubatizo? na baada ya yesu mbona watu waliendelea kubatizwa kwa kuzamishwa?. nisaidie jaman.

 6. Majibu yenu ni sawa lakini nitajibu la mwisho kwa sababu ni la utata sana.Mwanafunzi msomi alikua Luka.(Wahebrania 4:14-17).
  Nyumbani ni Kenya-Western region.Mbarikiwe.

 7. Bwana Yesu asifiwe Mimi nitajibu machache..mwanafunzi Wa kwanza kukufa baada ya Yesu kupaa si Judas kWa sababu ya alikufa baada ya Yesu ebu soma..mathew27:3-5. Kisha Yuda yule mwenye kumsaliti alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa alijuta,akawarudishia wakuu Wa makuahani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema nalikosa niliposaliti damu isiyo na hatia ..wakasema Basi haya yatupasa sisi? yaangalie haya mwenyewe ..akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu,akaondoka akaenda akajinyonga….
  Nasi si Stefano kWa sababu hakuwa mwanafunzi Wa Yesu Kati ya wale kumi na mbili…ebu soma acts7:59-60..
  Mi naona kama Yakobo ndugu ya Yohana ebu soma acts12:2. ..Akamwua yokobo ndugu ya yohana na upanga..tuenderee kujifunza

 8. Neema Daniel,Umesema Paulo ALIONGOZWA Sala ya toba na Anania!Hebu toa Ufafanuzi.

 9. Nimefurahishwa na maswali na majibu kutoka kwenye Biblia.naomba jinsi kujiunga

 10. Imenifurahisha sana na nimevutiwa kujiunga ili kuchangia na kuulizamaswali pia. naomba maelekezo ya kujiunga

 11. nimefurahi sana kuona jinsi wapendwa mpo active ktk neno la Mungu. barikiweni snaaaaaaaaaa

 12. Nimefurah kujiunga na mtandao huu. Naamini nitajifunza mengi kutoka kwa Mungu kupitia wapendwa.

 13. Mbarikiwe sana… …….wapendwa kwa mimi binafis… ….nimejifunza kitu

 14. Mjadala huu umeoibariki sana. Mbarikiwe wapendwa mimi nilisahau watoto wa ibrahimu wengne nilikuwa namkumbuka mtoto wa sara na hajiri

 15. Baada ya Joshua Mungu alimwinua othiniel ndugu na mdogo wake kalebu soma waamuz 3:9

  safna ya nuhu ilitua mlima wa ararati

  aliyemwongoza paulo sala yatoba ni ANANIA matendo 9:17

  Aliyekufa baada ya Yesu kupaa SIMIONI

 16. John Haule yuko sahihi sana kwa habari ya Othniel kwamba ndie aliyeinuliwa na Mungu baada ya kifo cha Yoshua. Waamuzi 3:9

 17. Hahaaa, Neema!

  Nimefurahishwa na point kwamba mwanafunzi wa kwanza kufa alikuwa Yuda. Ivi ni kweli eh?

  Lakini kwamba Reuben alishindwa kumlinda mdogo wake Yusufu, dah hiyo imenifanya nifikirie sana kwa jinsi gani kushindwa kumlinda dogo kunaweza kusababisha laana.

  Nimependa mawazo yako!

 18. Baada ya Joshua Mungu alimwinua Othniel na wengi wanadhani ni Yuda hapana, Yuda ni Kabila ndilo allkwea kwanza,Mungu anaongea na Kabila/taifa/mji nk kama anaongea na mtu.Baada ya Joshua walikaa kipindi fulanai bila kiongozi ili awaonje/awajaribu kama watasikiliza amri za Bwana nao walianguka kwa miungu mingine ndipo akawainulia waamuzi.kuinuliwa na kukwea ni vitu viwili tofauti

  Waamuzi1.1 -3 Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao?

  1.KUKWEA

  1:2-3Bwana akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake.

  Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika kura yangu,

  Yos8.10 Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli

  Yuda alikwea na Simeoni ndugu yake.

  2.KUINULIWA

  Amuzi2.16 Kisha Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara

  2.18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo,

  Amuzi3.9 -10Kisha wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
  Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli

  3.15 Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto;

  Tunajifunza

  Karibu

  Mjoli Haule

 19. 1. Baada ya Joshua Mungu alimwinua Yuda. (waamuzi1:1-4) 2. Safina ya Nuhu ilitua kwenye milima ya Ararati (mwanzo 8:1-4) 3. Aliyemwongoza Paulo sala ya toba alikuwa ni Anania (matendo 9:3-19) 4. Mwanafunzi wa kwanza kufa alikuwa ni Yuda Iskariote (luka 22:47-48, luka 22:21-, yohana 13:21-27) 5. Mfalme anayefananishwa na Yesu ni mfalme Melikzedeki (waebrania 7:1-3) 6. Watu ambao hawakuonja mauti ni: melksedeki (waebrania 7:1-3), henoko (mwanzo 5:21-22), Eliya (2wafalme 2:11-12)

  7. Baba wa Samsoni anaitwa Manoa (waamuzi 13:2-24) 8. Baba wa Ibrahim aliitwa Tera (mwanzo 11:26) 9. Watoto wa Ibrahim ni Isaka na Ishimael (mwanzo 20:16-,17:16, 21:3 10. Reuben alishindwa kumlinda mdogo wake Yusuph (mwanzo 37:1-36

 20. Ee bwana eh,
  Haule kumbe upo mtu wa Mungu, heri ya mwaka mpya.

  Nilijua kuwa katika maswali yaliyoulizwa lazima kuna machache ambayo yatabeba na kuchagiza mjadala huu, mojawapo ni hili la sala ya toba.

  Lakini kuna kitu Haule umenifurahisha, nacho ni ile maana ya kuongozwa sala ya toba, japo wewe umeiita maombi ya toba. Nakunukuu:
  ”Maombi ya toba ni kuambiwa yakupasayo kutenda.Nawe una amini moyoni na kukiri kwa kinywa, unabatizwa unaupokea Ufalme wa Mungu.(Roho Mtakatifu)”

  Ingawa ulitakiwa kuisema hivi: Kuongozwa maombi ya toba ni kuambiwa yakupasayo kutenda.Nawe una amini moyoni na kukiri kwa kinywa, unabatizwa unaupokea Ufalme wa Mungu.(Roho Mtakatifu).

  Maana ukisema maombi ya toba ni kuambiwa……, hapo utakuwa una-define maombi ya toba, ambayo sasa siyo hicho ulichokisema hapo juu, yaani maana ya maombi ya toba siyo kuambiwa yakupasayo kutenda. (bila shaka unanielewa)

  Baada ya kusema hayo, labda sasa nikuulize swali: Je wewe uliambiwa unachotakiwa kutenda(ambacho kimsingi inatakiwa iwe ni kuambiwa kuwa wewe ni mwenye dhambi hivyo tubu dhambi zako usamehewe), na baada ya hapo ulitubu mwenyewe bila mtu kukuambia ”sema Bwana Yesu, mimi ni mwenye dhambi, natubu leo dhambi zangu, …., futa jina langu katika kitabu cha hukumu, andika jina langu katika kitabu cha uzima, n.k?”

  Na je ilivyofanyika kwenye hiyo mistari uliyoinukuu ndicho kinachofanyika leo kwenye mikutano ya injili na makanisani,au popote anapotubu mwenye dhambi?

  Au ulichokionesha kwenye hiyo mistari kiko sawa na hayo maneno ya ‘futa jina langu latika kitabu cha hukumu.n.k?

  Nakusubiri tujadili!

 21. Sungura, Lenda, Dorothy na wengine wote
  Mimi nimebarikiwa sana na michango yenu. Kimsingi nimefurahi sana kuwasoma hapa. Naendelea kuchimba na mimi ili nione kama kuna lolote la ziada juu ya yale mliyotofautiana.
  Nawapenda sana

 22. Wapendwa……..

  Hivi ni kweli hakuna kuongozwa toba kwenye Biblia!

  Haya hapa Maandiko

  MK1.4 -4 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
  Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, WAKIZIUNGAMA dhambi zao.

  Mdo2.37 -38Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

  Mdo8.12-13Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

  Kwa Habari ya Towahi na Filipo

  Mdo8.29 -31 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.

  Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?

  Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.

  Mdo8:32,33,34……………………..35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.

  Mdo8.36 -38 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

  Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]

  Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.

  Hii ndio kuongozwa toba,waongozaji ni PETRO,YOHANA,FILIPO……..ndio kutimizwa kwa Rumi10:9,10

  Rumi10.14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?

  Kama hakuna muongoza/maombi ya toba,kulikuwa hakuna haja ya Bwana Mungu kumtuma Anania kwenda Nyofu kwa nyumba ya Yuda.
  Mdo9:10-18

  Haya ndio maelekezo anapewa huyo mwovu(mwenye dhambi)

  Mdo9.6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.

  Anania alimwongoza Paul

  Maombi ya toba ni kuambiwa yakupasayo kutenda.Nawe una amini moyoni na kukiri kwa kinywa, unabatizwa unaupokea Ufalme wa Mungu.(Roho Mtakatifu)

  Hata kornelio alikuwa mtauwa na mchaji Mungu lakini alikuwa hajui yampasayo(njia),akaongowa na Petro……kuwa kila amwaminie atapata ondoleo la dhambi…akaamini

  Karibu tutafakari pamoja.

  Mjoli Haule

 23. Prisca:Kwa jinsi maswali ulivyoyauliza inakaa ni mtu unajua majibu yake kabisa.Ila nashukuru imenipa changamoto ya kujifunza zaidi.Sungura ubarikiwe kwa mchango wako.

 24. Prisca,
  Tafadhali na wewe usiwe mvivu wa kusoma biblia.

  Kwa nini unauliza maswali ambayo wewe mwenyewe ukifungua biblia unayakuta majibu yake yako wazi?
  Kwa mfano: kumjua baba wa Ibrahi, baba wa samsoni, kosa la Reuben, watoto wa Ibrahim, unatakiwa tu kusoma biblia mwenyewe, maana hayana utata wowote.

  Maswali yenye utata hapa ni ;Aliye mwongoza Paulo sala ya toba ni nani? Mwanafunzi yupi alikufa wa kwanza baada ya Yesu kupaa?
  Mfalme yupi anafananishwa na Yesu, na
  Mwanafunz gani wa Yesu alikuwa msomi kuliko wote?

  Nakubaliana na Lenda kuwa kwenye biblia hakuna suala la kuongozana sala ya toba. Mistari aliyosema Dorothy ya Mdo 9:17-18, hakuna sehemu imeonesha kuwa Anania alimwongoza Paul sala ya toba.

  Lakini Lenda naye katika kutaja wana wa Ibrahimu, alimsahau Ishmael. Cha ajabu Siyi naye anamfagilia tu Lenda bila kumkumbusha kuwa hata Ishmael alikuwa mtoto wa Ibrahim.

  Pia nakubaliana na Orbi kuwa Stefano hakuwa miongoni mwa wale thenashara( yaani wale kumi na wawili), lakini hiyo haimaanishi kuwa hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Kwa sababu neno wanafunzi wa Yesu haimaanishi tu wale 12 (thenashara), bali kuna wengine mbali na hao 12, ambao walikuwa wafuasi wa Yesu nao waliitwa wanafunzi wa Yesu.

  Inawezekana Stefano naye alikuwepo miongoni mwa wale 120 waliopokea Roho mt.siku ya pentekoste (Mdo 1:15, 2:1-2). Maana dalili zinaonesha hivyo, kwa sababu alikuwa mtu aliyejaa Roho mt.miongoni mwa wanafunzi ( mbali ya thenashara) Mdo 6:3-5.

  Kwa kusema hivyo nakaubaliana na Lenda Pamoja na Dorothy kuwa Stefano ndo mwanafunzi wa kwanza kufa baada ya Yesu.

  Tena naungana na Orbi kuwa Luka hakuwa miongoni mwa wanafunzi wa Yesu, na hakuna mahali bibli imeonesha nani alikuwa msomi zaidi kati ya wanafunzi wa Yesu(thenashara na wasio thenashara.

  Sikubaliani na Lenda kwa habari za mfalme aliefananishwa na Yesu, ila nakubaliana na Dorothy kuwa mfalme huyo ni Melkizedeki mfalme wa Salem. Japokuwa andiko alilotumia Dorothy la Mwanzo 14:18-20 halioneshi huo ukweli. Andiko sahihi ni Ebrania 6:20

  Mengine yamejibiwa sawasawa.

  Ila Prisca acha uvivu wa kusoma biblia!!

 25. Shuma:

  Tabibu Luka hakua miongoni mwa wanafunzi alowachagua Yesu mwenyewe, yaani kati ya wale kumi na mbili na jina lake halimo kabisa katika Injili licha ya yeye mwenyewe kuandika kitabu cha Luka na Matendo ya Mitume…….Kwangu mimi labda Mathayo ndio alikuwa Mwanafunzi angala msomi, kwa sababu alikuwa ni mtoza Ushuru….usingelitegea Mamlaka ya Roma kumjua mtu asiye angalau na elimu kuwa mkusanya kodi

  Lenda:

  Inabidi kuwa na tahadahari unaposema hakua sala ya toba ndani ya Biblia….kumbuka mahubiri ya kwanza ya Yesu….”TUBUNI NA KUIAMINI INJILI”

 26. Naomba kumjibu Ndugu PRISCA maswali yake kama ifuatavyo.
  1.Baada ya Joshua Mungu alimwinua Yuda,Wamuzi 1:1-2
  2.Safina ya NUHU ilitua juu ya mlima Ararati Mwanzo 8:4
  3.Aliyemwongoza Paulo sala ya toba ni Anania,Matendo 9:17-18
  4.Aliyekufa baada ya Yesu kupaa ni Stefano,,Matendo 7:54-60
  5.Mfalme aliyefananishwa na Yesu ni Melkizedeki MWANZO 14:18-20
  6.Watu ambao hawakuonja mauti ni Eliya,Waebrania 11:5 na Eliya 2 wafalme 2:11-12
  7.Baba waamson anaitwa Manoa Wamuzi 13:2-24
  8.Baba wa Ibrahim anaitwa Tera Mwanzo 11:26
  9.Watoto wa Ibrahim ni Isaka Mwanzo 21:1-2,na Ishmaeli Mwanzo 16:15
  10.Reuben alizini na mke wa baba yake Mwanzo 49:3-4
  11.Mwanafunzi wa Yesu aliyekuwa msomi ni Luka.Wakolosai 4:14

 27. 1.BAADA YA YOSHUA MUNGU ALIMWINUA YUDA
  WAAMUZI 1:1,2
  1“IKAWA BAADA YA KUFA KWAKE YOUSHUA…..”
  2“BWANA AKASEMA YUDA ATAKWEA…”

  2. SAFINA YA NUHU ILITUA MLIMA ARARAT
  MWANZO 8:4
  “….SAFINA IKATUA JUU YA MILIMA YA ARARAT”

  3. HAKUNA KITU SALA YA TOBA KATIKA BIBLIA KATIKA TUKIO LA SAULI LABDA KAMA UMEIONA NDUGU. SAULI ANAPOONGOKA ILA ALIKUTANA NA MTU ALIYEITWA ANANIA,.
  MATENDO 9:17
  “ANANIA AKAENDA ZAKE, AKAINGIA MLE NYUMBANI; AKAMWEKEA MIKONO SAULI….MARA VIKAANGUKA MACHONI ..”

  4. MWANAFUNZI WA KWANZA KUFA BAADA YA YESU NI STEFANO
  MATENDO 7:59
  “..WAKAMPIGA KWA MAWE STEFANO”

  5. MFALME AMBAYE HUFANANISHWA NA YESU NI DAUDI

  MFANANO WA DAUDI NA YESU NI KAMA IFUATAVYO;

  1.WALISAMEHE ADUI ZAO
  DAUDI 1 SAMWELI 26 :22 YESU LUKA 23:34

  2.WOTE WAPAKWA MAFUTA. NA ROHO WA MUNGU
  ALIWAINGIA MARA BAADA YA KUPAKWA MAFUTA
  DAUDI 1 SAMWELI 16:13 YESU LUKA 3:22

  3.WOTE WALITUMWA NA BABA ZAO KUWAPELEKEA CHAKULA.
  DAUDI MKATE NA YESU NENO(MKATE WA UZIMA)
  DAUDI SAMWELI 17:8-9 YESU 1 YOHANA 4:14

  4.WOTE WALIKATALIWA NA KAKA ZAO
  DAUDI 1 SAMWELI 17:28 YESU YOHANA 7:5

  5. USHINDI WAO (DAUDI NA YESU) NI USHINDI WA ISRAELI WOTE
  DAUDI 1 SAMWELI 17:51-53 YESU WARUMI 5:19

  6.JAPO WAFALME HAWA KUWA MAHAMISHONI NA KUTENGWA
  WATU WATASIMAMA UPANDE WAO KUPIGANA NA ADUI.
  DAUDI 1 SAMWELI 22:1-2 YESU WAKOLOSAI 2:15

  7. WENYE MADENI WALIMBILIA KWAO
  DAUDI 1 SAMWELI 22:2 YESU (MADENI YA DHAMBI)
  MATHAYO 4:23-25

  8. WOTE WALISHINDA KUPITIA UZOEFU WA CHANGAMOTO
  WALIZOPITIA MASIHANI.
  DAUDI 1 SAMWELI 17:33-37 YESU WAEBRANIA 5:8

  9. WALISIMAMA PEKE YAO KAMA WAWAKILISHI KUTETEA TAIFA.
  DHIDI YA ADUI

  DAUDI SAMWELI 17:8-11 YESU WARUMI 5:18-19

  6. WATU WALIONYAKULIWA NI HENOKO, ELIYA
  MWANZO 5:24
  “HENOKO AKAENDA PAMOJA NA MUNGU, NAYE AKATOWEKA, MAANA MUNGU ALIMTWAA.”
  2 WAFALME 2:1,11
  1“IKAWA, HAPO BWANA ALIPOPENDA KUMPANDISHA ELIYA MBINGUNI KWA UPEPO WA KISULISULI”
  11“NAYE ELIYA AKAPANDA MBINGUNI KWA UPEPO WA KISULISULI”

  7. BABA WA SAMSONI NI MANOA
  WAAMUZI 13:2,12,22-24
  2“….JINA LAKE AKIITWA MANOA”

  8. BABA WA IBRAHIMU NI TERAH
  MWANZO 11:26,31
  26“TERA AKAISHI MIAKA SABINI,AKAMZAA ABRAM,”
  31“TERA AKAMTWAA ABRAMU MWANAE”

  9. WATOTO WA IBRAHIMU NI ISAKA,ZIMRANI,YOKSHANI, MEDANI,MIDIANI, ISHBAKI NA SUA.
  MWANZO 21: 2-4
  3“…IBRAHIMU AKAMWITA JINA LAKE ISAKA”
  MWANZO 25:1-2
  “IBRAHIMU ALIOA MKE MWINGINE JINA LAKE AKIITWA KETURA. AKAMZALIA ZIMRANI, NA YOKSHANI, NA MEDANI, NA MIDIANI, NA ISHBAKI, NA SUA.”

  10. REUBEN ALILALA NA SURIA WA BABAYE YAKOBO AITWAYE BILHA
  MWANZO 35:22
  “…REUBENI AKAENDA AKALALA NA BILHA, SURIA WA BABAYE; ISRAELI AKASIKIA HABARI.”
  MWANZO 49:4
  “…KWA SABABU ULIKIPANDA KITANDA CHA BABA YAKO..”

  “Naam;naja upesi.” Amina;na uje, Bwana Yesu. Ufunuo22:20

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s