Petro aliwezaje kuwatambua Eliya na Musa?

petro

Bwana Yesu apewe sifa! Napenda kuuliza katika biblia, kuna muda nabii Musa na nabii Eliya walimtokea Yesu, 1 upande wa kushoto na 1 wa kulia, Petro alipoona akamwambia Yesu, mwalimu tujenge vibanda 3, kimoja chako, kimoja cha Eliya na kimoja cha Musa, na kweli manabii hao walikua ni ndio.

Ila Wakati huo walipokuwepo manabii hao hapakuwepo na picha, kamera, video na ni muda mrefu toka manabii hao mpaka Petro. Je Petro aliwezaje kuwatambua kuwa huyu ni Eliya au Musa ikiwa hajawahi kuwaona?

–Patrick Mhina

Advertisements

27 thoughts on “Petro aliwezaje kuwatambua Eliya na Musa?

 1. Nabii Eliya alichukuliwa kwa uweza wa Mungu kwenda mbinguni. Hakuonja mauti. Yeye anawakikisha watakatifu watakaonyakuliwa wakiwa wahai wakati wa marejeo ya Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili.

  Musa alikufa. Akazikwa karibu na nchi ya ahadi.
  Mungu aliahidi kumleta nabii kwa mfano wa Musa. Sote twafahamu kuwa nabii aliyekuja kwa mfano wa Musa ni Yesu Kristo.
  Musa ni kielelezo cha watakatifu ambao watafufuliwa ufufuo wa kwanza katika marejeo ya Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili. soma Yuda 1:9 ambapo shetani alikuwa akigombania mwili wa Musa na Mikaeli

  Ufunuo wa yohana : Mlango 14
  13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

  Hatuwezi kuchunguza mapenzi ya Mungu kwa akili zetu. Bali maandiko Matakatifu yameweka wazi kuwa Musa Yuko mbinguni. Yesu alikuja duniani akaishi kama Musa na akafa kama Musa. Akazikwa kama Musa. Lakini alifufuka.

  Unaposoma fungu kama hili 👉1 Wakoritho : Mlango 15

  54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

  Kuna jambo ambalo twaweza kulifahamu kulingana na 1 Wakoritho : Mlango 15

  52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

  Musa alikuwa chombo kwa Mungu katika kujitambilisha kwa binadamu wa vizazi vyote baada ya uasi. Kwa hiyo kulingana na mafungu hayo ya Paulo, Musa alifufuliwa na Roho wa Mungu naye Yuko mbinguni pamoja na akina Eliya.

  Hatuwezi kuishi kwa mtazamo huo kwani utatuondolea dhana ya kumpenda Mungu kwa roho, na kwa akili na kwa nguvu zetu zote na kuzihamishia kwenye umizimu.

  Bali tuishi kwa ushauri huu Ufunuo wa yohana : Mlango 14

  13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; b kuwa matendo yao yafuatana nao.

  Kwamba tuwe na matendo mema na kujilinda na dunia pasipo mawaa ili mauti ijapotukuta tuwe na matumaini

 2. Biblia kamwe haikutuficha. Mungu aliweka bayana mwanzo kabisa baada ya kuumba dunia. “lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.” (Mwanzo 2:17).
  Lakini shetani aliingilia na kuwadanganya Adamu na Hawa. “lakini Mungu alisema, ‘Msile matunda ya mti ulio katikati ya bustani, wala msiuguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, “Hamtakufa!” (Mwanzo 3:3,4). Na hili ndilo fundisho la umizimu linaloendelea hadi sasa ya kwamba mtu akifa anaenda kuishi mbinguni kama akitenda mema na anaenda kuchomwa moto akiwa kuzimu (zingatia muda anachomwa moto yupo hai) au Purgatory anapotakaswa dhambi., haya ni baadhi ya mafundisho ya umizimu na uongo ambayo alianzisha shetani edeni!

  Je mtu akifa anaenda wapi!? Biblia haikukaa kimya! “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.” (Mhubiri 12:7). Wengi wamekuwa wakijiuliuza roho ni nini, je ndicho kinawafanya watu waone wakifa wanaenda mbinguni! Ayubu ameeleza juu ya roho. Ayubu 27:3 (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,Na roho ya Mungu i katika pua yangu;). Unaweza kujuliza roho inakaa kwenye pua? Jibu ni kuwa roho ni pumzi. Kwa kiingereza muhubiri 12:7 inasomeka “and the dust returns to the earth as it was, and the life’s breath returns to God who gave it.” Eccl 12:7.
  Hivyo mtu akifa haendi popote kwani mwili unarudi mavumbini na pumzi humrudia Mungu kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimpulizia pumzi ili awe kiumbe hai. Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. Hivyo kifo ni Pumzi-Mavumbi = Kifo. Hivyo fundisho la Mungu linabaki kuwa mtu anakufa kwa hakika!
  Je hali ya mtu aliyekufa ipoje?
  (Muhubiri 9:5) kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.Hivyo mtu akifa hajui lolote. Ni sawa na mtu aliyelala hajui kitu kinachoendelea duniani, ni sawa na mtoto ambaye hajazaliwa wala hajui kama atazaliwa wala hajui kama kuna dunia na mambo hake yanayoendelea.
  Muhubiri 9:10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.” Hakuna linaloendelea huko kwa wafu, wala hawajui lolite linaloendelea si dunia wala mbinguni!
  Hivyo ndugu usidanganywe kuwa waliokufa wanaenda kuishi sehemu kwani biblia imeweka wazi kuwa wafu hawajui lolote. Iweje wewe uamini kuwa wafu wapo mbinguni au motoni, Mungu alikwisha sema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,. Hebu tambua hili leo ubadilishe mtazamo.

  KUHUSU MUSA NA ELIYA
  Nabii Eliya alichukuliwa kwa uweza wa Mungu kwenda mbinguni. Hakuonja mauti. Yeye anawakikisha watakatifu watakaonyakuliwa wakiwa wahai wakati wa marejeo ya Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili.

  Musa alikufa. Akazikwa karibu na nchi ya ahadi.
  Mungu aliahidi kumleta nabii kwa mfano wa Musa. Sote twafahamu kuwa nabii aliyekuja kwa mfano wa Musa ni Yesu Kristo.
  Musa ni kielelezo cha watakatifu ambao watafufuliwa ufufuo wa kwanza katika marejeo ya Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili. Soma Yuda 1:9 ambapo shetani alikuwa akipigania mwili wa Musa na Mikaeli.

  Ufunuo wa yohana : Mlango 14
  13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

  Hatuwezi kuchunguza mapenzi ya Mungu kwa akili zetu. Bali maandiko Matakatifu yameweka wazi kuwa Musa Yuko mbinguni. Yesu alikuja duniani akaishi kama Musa na akafa kama Musa. Akazikwa kama Musa. Lakini alifufuka.

  Unaposoma fungu kama hili 1 Wakoritho : Mlango 15

  54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

  Kuna jambo ambalo twaweza kulifahamu kulingana na 1 Wakoritho : Mlango 15

  52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

  Musa alikuwa chombo kwa Mungu katika kujitambilisha kwa binadamu wa vizazi vyote baada ya uasi. Kwa hiyo kulingana na mafungu hayo ya Paulo, Musa alifufuliwa na Roho wa Mungu naye Yuko mbinguni pamoja na akina Eliya.

  Hatuwezi kuishi kwa mtazamo huo kwani utatuondolea dhana ya kumpenda Mungu kwa roho, na kwa akili na kwa nguvu zetu zote na kuzihamishia kwenye umizimu.

  Bali tuishi kwa ushauri huu Ufunuo wa yohana : Mlango 14

  13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; b kuwa matendo yao yafuatana nao.

  Kwamba tuwe na matendo mema na kujilinda na dunia pasipo mawaa ili mauti ijapotukuta tuwe na matumaini

 3. Nabii Eliya alichukuliwa kwa uweza wa Mungu kwenda mbinguni. Hakuonja mauti. Yeye anawakikisha watakatifu watakaonyakuliwa wakiwa wahai wakati wa marejeo ya Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili.

  Musa alikufa. Akazikwa karibu na nchi ya ahadi. 👇👇👇👇👇👇
  Mungu aliahidi kumleta nabii kwa mfano wa Musa. Sote twafahamu kuwa nabii aliyekuja kwa mfano wa Musa ni Yesu Kristo.
  Musa ni kielelezo cha watakatifu ambao watafufuliwa ufufuo wa kwanza katika marejeo ya Bwana wetu Yesu Kristo mara ya pili.

  Ufunuo wa yohana : Mlango 14
  13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

  Hatuwezi kuchunguza mapenzi ya Mungu kwa akili zetu. Bali maandiko Matakatifu yameweka wazi kuwa Musa Yuko mbinguni. Yesu alikuja duniani akaishi kama Musa na akafa kama Musa. Akazikwa kama Musa. Lakini alifufuka.

  Unaposoma fungu kama hili 👉

 4. Je unajua? Je umewahi kujiuliza?
  Mtu akifa anaenda wapi? Je anaenda mbinguni? je anaenda motoni? Je anaenda Purgatory?
  Biblia kamwe haikutuficha. Mungu aliweka bayana mwanzo kabisa baada ya kuumba dunia. “lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.” (Mwanzo 2:17).
  Lakini shetani aliingilia na kuwadanganya Adamu na Hawa. “lakini Mungu alisema, ‘Msile matunda ya mti ulio katikati ya bustani, wala msiuguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, “Hamtakufa!” (Mwanzo 3:3,4). Na hili ndilo funfisho la umizimu linaloendelea hadi sasa ya kwamba mtu akifa anaenda kuishi mbinguni kama akitenda mema na anaenda kuchomwa moto akiwa kuzimi (zingatia muda anachonwa moto yupo hai) au Purgatory anapotakaswa dhambi., haya ni baadhi ya mafundisho ya umizimu na uongo ambao alianzisha shetani edeni!
  Je mtu akifa anaenda wapi!? Biblia haikukaa kimya! “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.” (Mhubiri 12:7). Wengi wamekuwa wakijiuliuza roho ni nini, je ndicho kinawafanya watu waone wakifa wanaenda mbinguni! Ayubu ameeleza juu ya roho. Ayubu 27:3 (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,Na roho ya Mungu i katika pua yangu;). Unaweza kujuliza roho inakaa kwenye pua? Jibu ni kuwa roho ni pumzi. Kwa kiingereza Ayubu 12:7 inasomeka “and the dust returns to the earth as it was, and the life’s breath returns to God who gave it.” Eccl 12:7.
  Hivyo mtu akifa haendi popote kwani mwili unarudi mavumbini na pumzi humrudia Mungu kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimpulizia pumzi ili awe kiumbe hai. Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. Hivyo kifo ni Pumzi-Mavumbi = Kifo. Hivyo fundisho la Mungu linabaki kuwa mtu anakufa kwa hakika!
  Je hali ya mtu aliyekufa ipoje?
  (Muhubiri 9:5) kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.Hivyo mtu akifa hajui lolote. Ni sawa na mtu aliyelala hajui kitu kinachoendelea duniani, ni sawa na mtoto ambaye hajazaliwa wala hajui kama atazaliwa wala hajui kama kuna dunka na mambo hake yanayoendelea.
  Muhubiri 9:10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.” Hakuna linaloendelea huko kwa wafu, wala hawajui lolite linaloendelea si dunia wala mbinguni!
  Hivyo ndugu usidanganywe kuwa waliokufa wanaenda kuishi sehemu kwani biblia imeweka wazi kuwa wafu hawajui lolote. Iweje wewe uamini kuwa wafu wapo mbinguni motoni, Mungu alikwisha sema watu wangu wanakufa kwa kukosa maarifa,. Hebu tambua hili leo ubadilishe mtazamo.
  Je una swali lolote, nini mawazo yako hapa.
  Share ujumbe huu tuwafungue na imani ya umizimu.

 5. Hivyo roho ni nini na inarudi wapi? Je mtu akifa anaendelea kuishi? Hiyo yote ni imani ya umizimu .
  Je unajua? Je umewahi kujiuliza?

 6. Mungu ni roho hvyo basi hafi milele mwanadam tumeumbwa kwa roho ya Mungu na udongo tunapokufa roho zinaenda zilikotoka na mwili unarudi ulikotoka

 7. Nashindwa kuelewa mpaka dakika hii, hiyo yohana 3:13 haimaanishi ufufuo kuhusu musa Bali kutokana ukuu wa mbinguni hakuna Mtu aliyepaa mbinguni kwenda kufanya ukombozi maana kule hakuna mwenye dhambi Bali yesu pekee ndiye aliyeshuka huku duniani kwa sababu kulikuwa na uhitaji mkubwa wa ukombozi. Hivyo tunapaswa kumwaamini yeye! Ole wa yule MTU asiyeamini kuwa walio na Imani katika kristo na waliotenda mema hata wakifa wanakuwa wamelala maana atawapotosha watu wake. Tusitumia tu elimu ya kidunia kufafanua maandiko Bali tumshirikishe roho mtakatifu

 8. Siyi, rafiki yangu,

  Unajua, wewe una mambo mengi saaana ambayo unapaswa uwe unayafanyia kazi kama kweli unatamani kuwa sawa, yaani to be right with God. Usijadili tu bila kuwa na Ono la kukuongoza, nalo Ono lililo bora ni KUJIFUNZA!

  Tazama, Mijadala huzifunua roho zinazotuhudumia, ndipo ktk mijadala sisi huipata hiyo fursa ya kuzipima hizo roho kama zinatokana na Mungu au la, hayo mafundisho, hiki ndicho hayo “Matunda yao” kwa leo hii! Yaani kimsingi, Roho wa Mungu yumo ktk Maandiko yake, hiyo Biblia yako, nje ya Maandiko ni roho za dini zenye mfano wa utauwa, kwani hulichanganya Neno la Mungu na mambo yao!

  Neno la Mungu ni infinite, halina mwisho wala kikomo, hutanukia umilele, yaani eternity, tena ni perfect! Hili ndilo tunalopaswa tulijue, kwamba Mungu ni infinite, yeye ni Mkamilifu. Ktk ukamilifu wake aliyajua yote kabla hata hajaiumba dunia, hata kwamba leo hii mimi nitakua ninakuandikia mambo haya Siyi! Kama hakulijua jambo hili, basi si infinite, kwahiyo hawezi kuwa Mungu! Basi yote aliyoyanena Mungu ni makamilifu, hana la kuboresha wala kurejesha kwamba alikosea, ndipo, twapaswa kudumu ktk imani hii, kwamba Mungu na Maneno yake ni makamilifu, na Ahadi zake zote ni kamilifu! Yaani Biblia yako ni kamilifu, it is PERFECT!!!

  Basi unapomleta mtu, ile roho, mpaka kwenye kifungu chochote cha Maandiko, labda kinasema, kuhusu vyakula, “Nimewapeni Vyote” kisha yeye akaanza kukuambia kuwa hiyo “vyote” haiwezi kumaanisha na mijusi, au Biblia yake inapomuambia, “Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu”, yeye akakuambia huyo hawezi kuwa ni Samweli maana huyo alikwisha kufa, nao wafu wanangoja kufufuliwa hapo Kristo atakaporudi mara ya pili, kwahiyo huyo ni pepo! Jambo la jinsi hii linauondoa Ukamilifu wa Mungu na kuifanya Biblia si kitabu cha kuaminika, na hivyo kuiondoa Imani ndani yako. Lakini Biblia ilichokisema kiko hivyo hivyo, kama ilisema “nimewapeni vyote” inabakia hivyo inavyojitafsiri, kama ilisema “yule mwanamke alipomwona Samweli”, hakuna linaloweza kulitafsiri jambo hili zaidi ya maelezo unayoyaona hapo, ukiona linaongezewa lolote lile juu ya vifungu hivyo, basi jua kwa uhakika kuwa yanatoka kwa yule muovu, ndiyo hayo unayoambiwa mafundisho ya mashetani!!!

  Roho za dini zina tabia ya kujiwakilisha kama Roho Mtakatifu, bali zinahudumu kifo, zikiwapofua macho ya kiroho ili kuhakikisha hamzitoroki! Tena kwa taarifa yenu, mapepo ya dini si ya kuchezea, ni majeuri kuliko mnavyodhani. Tazama, mapepo ya kifafa, na ya jinsi yake yalivyokuwa yanatetemeka yakikutana na Kristo, lakini mapepo ya dini, hayana hata wasiwasi, yalikuwa yakimdhihaki, mara Belizebubu, mara yanamrushia mawe, na mwishowe yakamtoa asulubiwe!

  Ni maroho yale yale ya akina Jannes and Jambres, masquerading as the Holy Spirit, kama zilivyojiinua kumpinga Musa, ndio hizi hapa tena zikiifanya kazi ile ile albeit ndani wa watoto wa uasi hao wenye kubuni mafundisho hayo yenye sumu na kuyalisha makusanyiko yao!

  Basi, kwa mafundisho hayo, nasi twakusanywa pamoja kama walivyokusanywa Israeli, pale ktk ukumbi wa mashauri wa Pilato, tukifikishwa ktk hali yao kwa ukiri wetu wa imani, kulingana na Hukumu ya Haki ya Mungu kwa kadiri ya Neno lake, Biblia.

  Mbele yetu limesimamishwa Neno la Mungu kizimbani, akishitakiwa kukiuka Mapenzi ya Mungu; na huko rumande yuko Baraba, muuaji, yale Mafundisho ya Dini ; ndipo tunaambiwa na Pilato kwamba Mshitakiwa huyu hana hatia ya kukiuka Mapenzi ya Mungu, maana yeye ndiye hayo Mapenzi ya Mungu, kwahiyo ninawapeni huyu aliyesafi mwenye mapenzi nanyi, muende naye majumbani kwenu mkasherehekee kuachiwa kwake huru miongoni mwenu akiwa ni Baraka kubwa kwenu!!! Israeli walimkataa, wewe Siyi unasemaje?!!

  Nikikujibia Siyi, nitakuwa sijakutendea Haki, jipime mwenyewe, kipi ni rahisi kwako kuamini, kwamba huyo alikuwa Samweli au alikuwa ni pepo???

  Ikiwa utaungana na hao wanaosema huyo alikuwa pepo, yaani ukimchagua Baraba, utakuwa unashabihiana na yule mwanamke wa Endor, yeye aliiona miungu ikipanda, basi hana tofauti na wewe uliyemuona pepo akipanda, kwasababu nyote mko ktk roho mmoja! Mtazame mfalme Nebkadneza alichokiona ndani ya akina Daniel, au kule kisiwani waliko ishia akina Paulo baada ya merikebu yao kuharibika baharini; walipokuwa wakiota moto na wale wenyeji wapagani, baada ya yule nyoka mwenye sumu kali kumgonga Paulo, nao walipomuona hafi, wakasema Paulo ni mungu!!!

  Kristo anasema, Yn 3:13 “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.” Sasa tumuamini nani, wewe unayesema Mungu alimfufua Musa na kumpeleka mbinguni au Kristo anayesema hakuna aliyepaa mbinguni?? Au huko kupelekwa mbinguni kwa Musa kulikuwaje mpaka Kristo akawa hajui?

  Umemsikia Petro anachokisema? Anataka wajenge vibanda vitatu, kimoja cha Musa, ile Torati, cha pili cha Eliya, hao manabii, na cha tatu cha Kristo, ile Neema; haya ndiyo mawazo ya Wasabato! Wamejijengea vibanda vitatu wakiikaidi Sauti ya Mungu iliyowakataza ktk hilo, wakipingana na ile kweli, dalili ya watu walioharibika akili zao, waliokataliwa kwa mambo ya imani!!!

  Ubarikiwe!!

 9. Siyi,

  Hahahahaha………! Kusali na mtu dhehebu moja kunaweza kuyabadili Maandiko? Wewe utakuwa unaogopa ukweli kwamba, Nyoka anao Uzao, ambao hauujui uko wapi leo hii; you wish iwe ni “hadithi” tu ya Biblia, enhe? Bali Biblia inasema hivyo na hakuna namna ya kuyakwepa hayo, jitahidi uyajue badala ya kuyakimbia, kama ambavyo Uzao wa mwanamke ni Yesu, nao Uzao wa nyoka ni halisi pia!!

  Haya maelezo mengine yamenitia huzuni sana, siamini kwamba wewe unaweza ukayasema haya against your very belief! Nafahamu kwamba wafu wenu huwa wanalala makaburini mpaka siku atakapokuja Kristo mara ya pili. Nafahamu pia kutoka Fundisho hili, ndio mnaamini kwamba yule HAKUWA Samweli hata kama Biblia ilisema ni Samweli! Pia nilikutegemea ubaki ktk Fundisho lenu la wafu kuhusu Musa, bali naona Musa amewachanganya kidogo, walimsahau walipokuwa wanatengeneza Fundisho!!!

  Hata hivyo nisiwe mwepesi wa ku conclude mambo, ngoja nikufuatilie zaidi, tunaweza kujifunza jambo.

  Biblia inasema Musa alikufa huko juu mlimani, kimsingi nilikutegemea uikatae kauli ya Biblia kuwa yule alikuwa Musa, bali jibu ulilolitoa nami limenivuruga kiasi fulani, ngoja nikunukuu maelezo yako:
  “”Mungu alipokuwa akibishana na ibilisi kuhusu mwili wa Musa pale kaburini (japo halikujulikana lilipo), Biblia na vitabu vilivyovuviwa huniambia kuwa, Mungu alimfufua Musa na kumhamishia mbinguni moja kwa moja. So Musa yuko mbinguni maana alifufuliwa na Kristo.””

  Basi kwa vile ninyi ni “watu wa Maandiko”, tafadhali hebu nioneshe yalipo mambo haya uliyoyaandika:
  a. Mungu alipokuwa akibishana na ibilisi kuhusu mwili wa Musa pale kaburini
  b. Biblia inapokuambia kuwa, Mungu alimfufua Musa na kumhamishia mbinguni moja kwa moja.
  c. Kwamba, Musa yuko mbinguni maana alifufuliwa na Kristo, sijakuelewa vizuri kuhusu hili, kwanza umesema Mungu alimfufua na kumhamishia mbinguni, naye Kristo amekuja ya zaidi ya miaka 1000 baada ya tukio la kifo cha Musa, Je, Musa alifufuliwa mara mbili?

  Halafu hapa ndio umenimaliza kabisa:
  “”So kaka Mabinza, Petro aliona watu halisi. Na Mungu asingemwambia lolote kinyume na alivyokuwa Petro ameona.””
  Unakiri kwamba “Mungu asingemwambia lolote kinyume…”, sasa hebu niambie, hizi nukuu ulizozitiririsha hapa kuhusu Sauli, ni nani anayekusimulia tukio hilo? Ni nani huyu anayesema, “Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu”? Ukiyatazama maelezo hayo, unaweza kuniambia yana tofauti gani na haya hapa, “Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.”???
  Tena ulipaswa uone ambavyo vyote huwa utupu mbele Neno, hilo lililojiwakilisha ktk Samweli, kwamba alipotokea tu, yule mwanamke akamtambua na Sauli licha ya kujificha kwake, umeambiwa ktk Siku hiyo utayatafuta majabali yakufunike!!!!

  Nakushukuru kwa kutufunulia chungu tuone ndani mna nini!

 10. Mabinza,
  Hivi kaka Mabinza, Lwembe huwa mnasali naye dhehebu moja? Nakuuliza hivyo baada ya kuona kile ambacho Lwembe huwa amekishikilia kuwa ni ukweli wa Biblia, na wewe unacho!!! Sina uhakika huenda na wewe unaamini kuwa, “kula tunda kwa Hawa bustanini Edeni, kilikuwa ni kitendo cha ngono kati ya nyoka na Hawa” Yachunguzeni maandiko marafiki zangu. Angalia aya hizi 1 Samueli 28
  1 Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako.
  2 Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima.
  3 Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi.
  4 Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa.
  5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana.
  6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
  7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.
  8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.
  9 Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?
  10 Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili.
  11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
  12 Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli.
  13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
  14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
  15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
  16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?
  17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.
  18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.
  19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.
  Mabinza,
  Hebu angalia mstari wa 5 na 6, Sauli anaamua kumwacha Mungu na kugeukia miungu wengine ili wampatie msaada wa shida yake. Msatri wa 8, Sauli anaamua kubadili hadi mavazi. Anatambua kabisa kuwa huko anakoenda kukoje. Mavazi aliyokuwa akiyavaa na kukutana na Mungu, hayafai kuvaliwa kwa mashetani.
  Mstari wa 13 ndiyo unaokuambia kabisa kuwa huyo hakuwa Samuel bali ni pepo. Mwangalie huyu mungu aliyepandishwa kutoka ktk nchi…14, Sauli anakiri kabisa, mzee anazuka…Samweli kwa macho alionekana kama yeye.
  Kinachoniumiza zaidi kuwa kwa nini hata wewe Mabinza huoni umizimu huu? Hebu soma mstari wa 16 Samweli mwenyewe anamjibu Sauli..” Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?” Bado tu ndg yangu Mabinza huoni kitu hapo? Mambo mengine nikuachie uyatafakari mwenyewe kaka.
  Uovu mwingi, ulimtenga Sauli na Mungu wake. Ndiyo maana Sauli akaamua kugeukia miungu wengine. Lakini hata hivyo, hata hao miungu na wao, wanamshangaa Sauli kwenda kwao. Why? Walitambua kuwa, Mungu muumbaji ana nguvu kuliko wao.
  Musa kuonekana pale mlimani, haukuwa ni mzimu wala pepo. Alikuwa ni Musa kabisa. Mwanadamu halisi. Mimi niijuavyo, Biblia, inaniambia kuwa, baada ya Musa kufa, shetani alikuja kutaka kutia muhuri wake kwenye kaburi la Musa. Na kwa sababu Musa alikuwa ameshatubu dhambi yake aliyoifanya pale mwambani, Mungu alimsamehe na hivyo kumpatia tiketi ya moja kwa moja kuwa miongoni mwa wateule. Mungu alipokuwa akibishana na ibilisi kuhusu mwili wa Musa pale kaburini(japo halikujulikana lilipo), Biblia na vitabu vilivyovuviwa huniambia kuwa, Mungu alimfufua Musa na kumhamishia mbinguni moja kwa moja. So Musa yuko mbinguni maana alifufuliwa na Kristo.
  Kuhusu Lazaro, Yesu hakumfufua Lazaro peke yake. Alifufua watu wengi waliokuwa wamekufa. Hivyo wanadamu wanakufa. Hata walio katika Kristo, nao wanakufa tu, japo kifo chao, Yesu alikiita usingizi. Lakini haina maana kuwa hawafi. Wanakufa, na kuwa unconcisious kabisa hadi siku ya ufufuo. Habari njema kwa hawa wanaokufa ktk Kristo, ni kwamba, wao wanalo tumaini la kuishi milele baada ya mauti usingizi hii ya hapa duniani.
  So kaka Mabinza, Petro aliona watu halisi. Na Mungu asingemwambia lolote kinyume na alivyokuwa Petro ameona. Watu wanakufa. Na Biblia inalitambua hilo la watu kufa. Tofauti ni kifo cha muumini na asiye muumini. Muumini ana tumaini la kuishi milele. Asiye muumini hana hilo tumaini.
  Hebu yaangalie hayo kwa jicho lingine.
  Jitahidi…

 11. Dada, Magreth
  Duuu, ya kwako hii mpendwa nilikuwa sijaona. Maelezo yako yake yana kitu hivi. Ubarikiwe kwa jitihada kubwa za namna hii. Ngoja tuendelee kutumbua macho kwenye links

 12. Siyi,

  Ndg yangu, Jiulize kama huwa wanakufa, kwanini Sauli atake kuongea na Samweli, wakati Sauli huyohuyo alikuwa akijua fika kuwa, Samweli Alisha kufa? Au ilikuwejekuweje Yesu akubali kuongea na Musa, wakati Yesu alikuwa akijua fika kuwa, Musa alikwishakufa zamani tu hata kabla ya Israeli kufika katika Nchi ya Ahadi? Je, tusemeje basi, Mungu ni wawafu?

  Au kwanini Yesu awaambie Mitume kuwa Lazaro alikuwa kalala na alipaswa kuamshwa, ikiwa inasemwa wazi kuwa Lazaro tayari alishaanza kunuka, kwakuwa alikuwapo kaburini siku zaidi ya tatu akiwa mfu? Au ni wapi Biblia inasema hiyo ilikuwa Mizimu na si watu husika? Ikiwa kweli hufa kwa maana tuijuayo, mbona Mungu hakumbishia Petro, aliposhauri kujenga vibanda pale mlimani? Tunaona badala yake Mungu, akaelekeza tu kwamba kwa lolote asikilizwe Yesu na katika hilo Mungu hakusema kuwa, Petro acha hizo, hiyo uionayo hapo ni mizimu tu na mizimu haihitaji nyumba!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai”

 13. Mabinza,
  Hii kali brother,
  Hebu tondoa kidogo maana ya hii, “Walio katika Kristo hawafagi Braza.”
  Nisadie tafadhari

 14. Ni kweli wafu hawajui neno lolote, lakini waliolala hujua! Walio katika Kristo hawafagi Braza.

  ” Ufahamu ni chembe ya Uhai”

 15. Lwembe,

  Tehe tehe! yaa nilijaribu kumchomoa maana marisasi unayo yaandaa ni kama nayaona.

  Press on

 16. Lwembe,
  Nashukuru unachokiuliza, umekijibu mwenyewe. Maana najua unajua kuwa Mungu/Yesu hana umoja/ushosti na mizimu. Nimefurahi kwa vile umenukuu hadi Biblia. Ubarikiwe na Bwana. Mimi sioni cha kujibu hapa.
  Labda kama kuna lingine.
  Ubarikiwe na Bwana

 17. majibu yote yako kwennye biblia tusome sana biblia majibu yote yako ndani yake kwanza ujue wakati huo wa akina petro walikuwa wanatembea na yesu live uwepo wa mungu ukiwa juu yao wakati wote kumbuka wakati wanasafiri ziwani chombo chao kilipokuwa kinanachukuliwa na tufani ghafla wanaona kitu kama kivuli cha mzimu lakini Biblia inasema Yesu akawambia wasihofu kisha petro akasema kama ni wewe akaomba kwenda kwa Yesu Biblia inasema petro alitembea kwenye maji hofu ikamfanya aanze kuzama jibu alifunuliwa na Roho mtakatifu kwa sabababu alikuwa katika uwepo wa Mungu balikiwa by ngullo

 18. Seleli,

  Hahahahahaha…..! We taka chomoa yeye!!?

  Subiri kidogo, “rafiki yake kipenzi” mpa jibu sasa hivi!!!
  Hahahahaha…..!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Enjoy the fellowship!

 19. Lwembe,

  Teacher au siyo! aya Mwalimu Shikamoo

  Kwa iyo unadhani ni mzimu siyo? ili Mtu akikuambia NENO limesema ni Musa, wewe unadhani ni mzimu nani aaminiwe kisha ukiambiwa ivyo tu, nshakuona unakwenda wapi, kuleeeeee kwa mwaka juuuuuziiii kwa mzimu samweli! we si ugomvi wako waga hauishi wewe! yaani kila zikikutana, zinanyukwa kuanzia pale ziliponyamazia! we Ticha unahitaji msaada!!!!!!

  Press on

 20. @ Yusha,
  Hahahahaha…!
  Mwalimu yuko mmoja tu, Roho Mtakatifu!
  Hawa akina Sungura, Lwembe, na wengine wengi ni “wabishi” tu wa Injili, to keep the Fire Burning!

  Bless your soul, brother!

  @ Haule,
  Nimefurahishwa sana na jinsi ya jibu lako, swali la ki Biblia na jibu la ki Biblia!!!
  Yaani it is that simple!!!

  Gbu, my brother!

  @ Siyi,
  Hahahaha…!
  Hoja very touching indeed!!
  Maandiko hapo yanasema Musa na Eliya walikuwa wanaongea na Yesu na Petro akawatambua, kwa UFUNUO kama alivyosema ndg Haule; sasa ndg yangu Siyi hebu nisaidie hapo kidogo, unieleze inakuwaje mambo hayo ilhali tunafahamu fika kuwa Musa ALIKUFA:-
  Joshua 1:1 ” 1 Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA…”
  Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa…”
  Nao wafu tunafahamu kwa Maandiko, hubaki makaburini na hawajui lolote na hawana ijara, na tunafahamu watafufuliwa atakapokuja Kristo mara ya pili; Je, huyo Musa aliyetambulikana na Petro si MZIMU huo kweli????

  Tusaidane ndg yangu!!!

 21. Haule,
  Ha ha ha haa!!
  Nimefurahishwa sana na hoja yako nzuri. Very touching!!
  Blessed indeed brother.

 22. Nami naungana na ndg Haule. Neno linasema, Roho hugawa karama kwakadri apendavyo.

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai”

 23. So, in the persons of Moses and Elijah, readers are reminded of their great history, as well as their future when God’s promise will be fulfilled. Maybe their presence was interpreted as a sign that the final “Day of the Lord” was about to occur – but it didn’t.

  Scholars have no trouble with the fact that both of them appeared. In a sense, scholars might say that Jesus brought the work of Moses and Elijah to completion. Together, they function as witnesses from the OT on Jesus’ behalf. Both Moses and Elijah met God on Mount Sinai (Horeb). The Transfiguration occurred on a mountain. It certainly gives credence to Jesus’ ministry and mission.

  Lastly, readers should consider the simple explanation that if God caused Moses and Elijah to appear, he also caused the disciples to know who they were. No introductions were needed!

  http://clearbibleanswers.org/questionsanswers/123-how-did-peter-recognize-moses-and-elijah-on-the-mount-of-transfiguration-.html

  http://www.evidenceforchristianity.org/in-the-transfiguration-how-did-peter-know-it-was-moses-and-elijah-if-he-had-never-seen-them-or-a-picture-of-them/

  So, in the persons of Moses and Elijah, readers are reminded of their great history, as well as their future when God’s promise will be fulfilled. Maybe their presence was interpreted as a sign that the final “Day of the Lord” was about to occur – but it didn’t.

  Scholars have no trouble with the fact that both of them appeared. In a sense, scholars might say that Jesus brought the work of Moses and Elijah to completion. Together, they function as witnesses from the OT on Jesus’ behalf. Both Moses and Elijah met God on Mount Sinai (Horeb). The Transfiguration occurred on a mountain. It certainly gives credence to Jesus’ ministry and mission.

  Lastly, readers should consider the simple explanation that if God caused Moses and Elijah to appear, he also caused the disciples to know who they were. No introductions were needed!

  http://clearbibleanswers.org/questionsanswers/123-how-did-peter-recognize-moses-and-elijah-on-the-mount-of-transfiguration-.html

  http://www.evidenceforchristianity.org/in-the-transfiguration-how-did-peter-know-it-was-moses-and-elijah-if-he-had-never-seen-them-or-a-picture-of-them/

  http://evidenceoftruth.org/moses_and_elijah_and_the_transfi.htm

 24. Wapendwa naomba kujibu kwa sehemu….

  Mt16.15 -17Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
  Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
  Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

  My Take:

  Kwa maandiko haya yanatupa mwanga kuwa Peter alifunuliwa na Baba wa Mbinguni kwasasa tunasema alikuwa na karama .

  Barikiwa

 25. Ubarikiwe kwa swali lako ndugu nami nategemea kufaidika kupitia maoni ya walimu wetu wa hapa,kama akina Sungura,Lwembe na wengine wengi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s