Serikali imewatenga wapentekoste?

Watumishi wakiongoza maombi na watu mbali mbali wakiombea Taifa. Picha kwa hisani ya Gospel Kitaa

Hivi karibuni Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste nchini (PCT) Chini ya Uenyekiti wa Askofu David Batenzi Na uratibu mkuu wa Jopo la Maaskofu likiongozwa Na Askofu Josephat Gwajima, Askofu Zakaria Kakobe Na wengineo wakiongozwa Na Askofu Dkt. Paul Shemsanga walitoa TAMKO Kwa Serikali juu ya Kupuuzwa Kwa wapentekoste nchini katika mchakato wa Uundaji Wa Bunge la KATIBA. Katika TAMKO Hilo lililohudhuriwa kwa wingi na wanahabari, Maaskofu hao waliilaumu Serikali Kwa kutochagua wajumbe Kwenye Bunge Hilo la katiba kutoka Kwenye chombo hicho muhimu katika ukristo nchini.

Katibu Mkuu wa PCT, David Mwasota, alisema waliamua kutoa tamko hilo ili kuonyesha namna ambavyo wamesikitishwa na kitendo hicho.

“Tumewaita ili mtusaidie kufikisha masikitiko yetu kwa viongozi, Watanzania na waamini wa Kipentekoste kutokana na kitendo cha serikali yetu tunayoiheshimu, kuipenda na kuiombea, kwa kutubagua na kututenga katika bunge maalum la Katiba, huku tukiwa ni miongoni mwa taasisi kubwa za kidini na makundi mengine ya kijamii,” alisema na kuongeza:

“Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais aliagiza makundi mbalimbali ya kijamii na taasisi za kidini kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la Katiba na kwa kuzingatia wingi wa wanachama wetu tulipendekeza majina tisa ya watu tulioona wanafaa kutuwakilisha, lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyeteuliwa.”

Wakati hali hiyo ikiendelea Jopo Hilo la maaskofu tarehe 15 February 2014 limeitisha Maombi makubwa Kwenye Ukumbi wa PTA SABASABA. Maelfu ya Waumini kutoka kila dhehebu la kipentecoste walimiminika Na kufurika Kwenye Ukumbi huo.

Kulikuwa mwamko wa nguvu na umoja katika kusanyiko hilo Kwenye Kanisa la Kristo. Maaskofu Na Maelfu ya Wapentekoste wameiombea Kwa Uchungu nchi ya Tanzania huku wakimkumbusha Mungu kuhusu Maziwa,Mito, Madini ya kila aina Na Sasa Gesi Na Mafuta Lakini kwanini Taifa Hili Ni Maskini!!?.  Lazima Kuomba ili kama Kuna Kiongozi anayesabanisha haya Mungu amtupilie Mbali. Hakuna aliye shindana Na Taifa la Mungu akabaki Salama.

Wapentekoste ambao Kwa sensa ya Haraka wanakimbilia Milioni 11. Idadi hii inayozidi kukua siku hata siku inaleta changamoto chanya Kwenye uhai Wa Taifa.  Maaskofu walitanabaisha Kwamba kuna watu wanasema makanisa ya Kilokole Ni Mengi, kimsingi hata haya yaliyopo Ni machache mno, Mpaka yazidi wingi wa baa zote, grocery zote Na vilabu vyote vya starehe.

–Habari kutoka sehemu mbalimbali

Advertisements

16 thoughts on “Serikali imewatenga wapentekoste?

 1. AIDER,

  Unasomaga Biblia wewe hii hii Wapentekoste tunayoiamini au? Ati Mungu hakutuita kwa kazi ya Serikali!!!!!!!!!! Embu angalia hawa Wacha Mungu apa- walikua ni akina nani serikalini kwa King Nebekadreza..Daniel. 2:46-49

  Toa jibu nakungoja Kaka, walikua akina nani uko Ikulu?

  Kamau,

  Nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa ya uliyosema but kusema kua Elimu ndogo ndio inawatesa Wapentekoste, what do u mean? mbona wapo/mpo mliokwenda shule za kutisha ziwe za dini au secular tena baadhi ya Maaskofu wana CV za kutisha sana za shule za kawaida na ya Neno/Dini hata kwa mambo ya Serikali maana wengine waliitwa na Bwana ktk kazi wakitokea job serikalini tena toka job kubwa na office sensitive za Nchi hii? Elimu ndogo una maanisha nini haswa? does that include you? au ni wale wa Uongozini tu?

  Press on

 2. Elimu ndogo itawatesa sana wapentekoste. Hili suala ni la kitaaluma na kisheria. Ilipaswa PCT kutumia wanasheria na wasomi wa mambo ya katiba wa kipentekoste kuchambua katiba iliyopita na rasimu ya katiba mpya na kuona masuala ya manufaa kwetu kama wapentekoste. Ni wakati muafaka kwa wapentekoste kutambua umuhimu wa taaluma na kuendesha shughuli zake kisomi. La sivyo wataendelea kubaguliwa na kudharauliwa na serikali ambayo wanaiita “baba yetu” wakati hata mtazamo huo ni ukengeufu. Baba yetu ni aliye mbinguni peke yake. PCT wanaendesha shughuli zake kwa kujipendekeza kwa serikali ambayo awamu hii ya nne imeleta madhara makubwa kwa kanisa na wakristo kwa ujumla wake kuliko awamu zote zilizopita zikijumuishwa pamoja!

 3. Hata injili ni kazi ya kawaida ya dunia hii.

  Kwani ni wapi tena tunaweza kuihubiri injili kama si hapa duniani, kwenye sayari ya mars au? tehee…

  Watu wanaoponda kitendo cha maaskofu kuilaumu serikali nilitegemea mseme mambo fulani ya msingi ambayo tunaweza kutumia nafasi hii kuwa-challenge nayo maaskofu wetu. Lakini badala yake mnaongea tu vitu ambavyo hata havina msingi.

  Ni hivi, tatizo kubwa la maaskofu wetu ni uoga, au kukosa mindset makini ya kuisadia au kui-challenge serikali.

  Ulishawahi kujiuliza kwa nini maaskofu wetu huwa wanakemea ufisadi/mambo mabaya ya viongozi wa serikali wakiwa kwenye mimbari makanisani, utadhani sisi washirika wao ndo mafisadi?

  Nimesema ni waoga kwa sababu ni mara nyingi tu huwa wanapata nafasi za kwenda Ikulu kuonana na Rais. Lakini wakifika Ikulu huwa wanakomea kunywa tu juice nzito ya Ikulu, bila kusema au kuchallenge kuhusu mambo ya kipuuzi yanayoendelea kwenye hili taifa.(pardon me my dear bishops)

  Na kama maaskofu wetu ni waoga, basi na sisi washirika wao are good as cowards.

  Tunataka mtu anayekwenda pale Ikulu kuongea facts na solutions za matatizo ya hii nchi kwa hekima tukufu ya Mungu. Unawezaje kufurahia kwenda kunywa juice nzito wakati hili taifa liko kwenye shimo kubwa kiasi hiki.

  Sasa kama huwa wanaenda ikulu kwenda tu kunywa juice na kupeleka malalamiko uchwara ya kawaida tu, bila kumwaga wisdom ya Mungu ambayo italeta solution kwa taifa hili kwa nini serikali isiwapuuze katika ishu kama hii.

  Mafisadi wengi walioko serikalini wanajijua kuwa wao ni mafisadi, na wanajua ni nani anayestahili kuwakemea. Sasa anayestahili kuwakemea asipofanya hivyo badala yake akacheka na kunywa nao tu juice, pamoja na kuwaomba misaada, kwa nini wasimpuuze kwenye masuala ya kitaifa kama hili?

  Hata kama tukiamua kufunga mwaka mzima kuombea nchi hii ibadilike, bila sisi mindset yetu kubadilika, tutakuwa tunapoteza muda. Sisi ndo nuru ya hii nchi, sisi ndo chumvi ya hii nchi. Lazima nuru itoe soluhisho gizani ili iendelee kuwa na sifa za kuwa nuru, na lazima chunvi otoe soluhisho pale ambapo hapana ladha ili iendelee kuwa na sifa za kuwa chumvi.

  Vinginevyo, chunvi ikipoteza ladha yake haifai kitu, ila kutupwa na kukanyagwa na watu.

  Maaskofu wetu hawakutakiwa kukosa kwenye bunge la katiba

  Think about it u serious thinkers!

 4. Unajua sisi wengine tunafanya kazi serikalini. Tunaifahamu serikali yetu na viongozi wake. Ukweli ni kwamba bado kuna negative perception towards wapentekoste.

  Serikali kupuuza kuchagua mtu hata mmoja kutoka kwenye kundi la wapentekoste halafu wakaenda kumchagua Kingunge Ngombale Mwiru eti kupitia kundi la waganga wa kienyeji ni AIBU sana.

  Unawezaje kuwaacha maaskofu wenye hekima kubwa kama akina Askofu Batenzi, Mwingira, Kakobe, Gamanywa, nk ukaenda kuteua Kingunge?

  Halafu tuache, utani hivi kwenye dini ya kiislamu wameteua watu wangapi? Mbona hawakuwacha wawakilishi wa dini za Kihindi na Kiislam?

  Kama wanasema kwamba eti hakuna majina yaliyowasilishwa mbona hawajakanusha kwamba yule bwana aliyepokea BAHASHA yenye majina 9 ya kutoka PCT siyo mtumishi wa Ikulu? Mbona hawajakanusha kwamba ile saini siyo ya mfanyakazi wa Ikulu?

  Kama wanataka kuipima nguvu ya wapentekoste wataiona ikifika siku ya kupiga kura mwaka 2015 Oktoba. Hivi wanadhani kwamba wapentekoste tukiamua hatuwezi kuamua nani akalie kiti cha Ikulu? TUNAWEZA. Au wamesahau jinsi wapentekoste wanavyosaidia kuombea amani ya nchi hii kwa kufunga na kukesha?

  Wamesahau kwamba watu wapatao milioni 10 wakiamua kwamba safari hii ya uchaguzi wa 2015 watachagua mtu wao, unajua nchi hii haitakalika? Nenda kamuulize Zitto Kabwe mwaka 2010 yaliyotaka kumkuta Kigoma wapentekoste walipokuwa wameamua kumwaacha solemba. Kama asingeenda kuwapigia magoti na kuwabembeleza hangepita kamwe kwenye ubunge wake mwaka 2010. Kamuulize mzee Kikwete pia ilikuwaje mwaka 2010 pale jijini Mwanza alipolazimika kumtuma mzee wa Bunda bwana Steven Wassira. Wapentekoste kote nchini walikuwa wameamua kutoichagua CCM na Kikwete wake kwa sababu tu ilionekana kwamba SERIKALI ya chama tawala ilikuwa inawabagua wapentekoste. Hali ilikuwa mbaya sana jijini Mwanza kwani wapentekoste wote walikuwa wameamua kuzira kabisa wasichague mgombea wa CCM kutokana na tabia kama hizi.

  Kama CCM wanadhani wanaweza kuendelea kutawala huku wakiwabagua wapentekoste, kuna siku wapentekoste wataamua tofauti kama siyo 2015 huenda ikawa mwaka 2020 Oktoba. Wee subiri tu.

  Serikali inapaswa kutenda haki. Haiwezekani kundi kubwa kama hilo la wapentekoste likapuuzwa hivyo tena hadharani anajitokeza msemaji wa Ikulu akikanusha taarifa za maaskofu kwamba hawakuwasilisha majina wakati ushahidi wanao. Eti wamesearch kwa kompyuta na kwa mkono wamekosa jina hata moja la askofu yeyote wa kipentekoste. Jamani badaala ya kuomba radhi maaskofu kisha yaishe wewe unawasha hasira zaidi. Jamani Ikulu yetu vipi tena?

  Wafanyakazi wenzangu mlioko hapo Ikulu ya Magogoni semeni ukweli kwamba majina hayo yalikaliwa tu na yalitupwa pembeni. Mwaogopa nini kusema ukweli mbele ya watumishi wa Mungu.

 5. watu wa Mungu tambueni kwamba yesu kristo hakuwaita kwa kazi hizo za serkali bali kwa shamba lake,yaani kanisa na injili hamjaona kwambwa aliwa acisha mitume kama petro. mathayo na wengine shuguli zao za kawaida ya dunia kwa sababu ya injili. hii ndio kwa maana hakuruhusu mukubaliwe huko bungeni kwa sababu hakuwapa agizo la kwenda uko.

 6. Kaswahili,

  Ndio Kaka, nimekusoma, asante. Unakua ikishafika hata sembe and dona driven logic, reasoning, common senses ktk kuona mambo, zinakua crippled and corrupt, yanayozaliwa toka apo ni mauzi tu na masikitiko kabisa pia magonjwa mabaya ya kukera.

  Tunaongelea Mil 11 ya Watanzania, wamenyimwa special interests zao kusemelewa kwa jamaa kuwapuuza both viongozi wetu na taasisi yetu halafu Watu hawaoni iyo halafu later mambo yamepinda ktk NCHI hii kwa kua Katiba itakua imepitishwa na madude yake, tunanza kufunga na kuomba kavu siku 3, 7 au 40 eti kubadili Nchi, Siasa, sera, moyo wa viongozi ili tupate nafuu ktk maisha! mateso kweli na kujilisha upepo maombi ya kizembe na kung’ang’ana ivyo ili hali tungeingia bungeni na kudebate kwa hoja, madude ambayo yangeingizwa hata kuja kutupelekea kuomba siku moja, yangefutika hapo hapo bungeni.

  Press on

 7. unajua serikari ina sema haina dini ukweli inaonekana ina dini mbili yani C.CT NA BAKWATA kwani kwa mda mrefu nimejalibu kufuatilia mfano sikukuu kama pasaka /krismas utaona vyombo vya habali vya taifa kama radio na TBC hazifatilii ibada za kipendekste kwani hata sisi ni watanzania na tunalipa kodi kwa uaminifu kuliko hao wanaowapendelea kwani sisi tunalipa kodi kwa kumhofu Mungu ninaomba serikari isifanye ubaguzi

 8. Seleli,

  Umenikosha sana kaka, baada ya Lenda kunuchafua na mchango wake mpaka nkasikia kichefuchefu na nkataka kutapika!
  Kwa kweli sina cha kuongezea, make hasira dhidi ya ukakasi wa akina Lenda umeimaliza.
  Tuwasamehe, make Paulo anasema “Wenye imani dhaifu tuchukuliane nao, tusiwahukumu mawazo yao”

 9. Mtu mmoja anasema Mama yake mzazi alimtafsiria fanatism as an extreme act of being a fan where all logic and reason goes on leave.

  Nadhani basing on some inputs hapa, nakubaliana na Mama huyo. It is frustratingly amazing the the manner and the level Watu wanaweza ona mambo na kwa sababu ya kile walichomeza/amini/daka/simamia, wanashindwa kabisa kuona mambo critically important kwa sisi Wapentekoste kuwa nayo.

  Nchi hii kama nikuomba, tumeomba sana yet hakuna mabadiliko MAJOR AND VIVID TUNAYOTAKA SANA, Leo tulipaswa kupata nafasi kwenda kuyatendea kazi maombi kwa vitendo, kumefanyika uhuni TUKAPUUZWA lakini some hapa mnaleta reasoning so cheap and badly suffocating.

  On serious note, SOME Maaskofu hao-waliotoa tamko, tunawafahamu sana, wana akili timamu, wamejaa Roho kama siye, wanamtumikia Mungu, wana hekima, wamekwenda shule, wanajua walichosema na wako sawa kudai haki maana sisi nasi tu wananchi.

  Kulalamika/kudai haki ya kiraia/kitaasisi si dhambi, na kutokudai wakati umedhulumiwa ndio iyo fanatism-in which common logic and reasoning ya any healthy person, gone on leave!

  Swala la sijui kulaani, limetoka wapi hapa! so annoying reasoining indeed. Kama ni kulalamika, sisi si wa kwanza, Bwana YESU alichukizwa na failure to perform ya Wanafunzi wake na akasema, nitachukuliana nanyi hata lini enyi kizazi kisicho na imani, so kipi cha ajabu kulalamika! Mambo mengine Watu huongea tu kwa sababu ya kukosa wide range ya ufahamu wa mambo tu kisha kujenga hoja mfu inayolazimishiwa uhai

  Nadhani tuwapongeze Viongozi kwa kuthubutu kusema/kumwambia Mkuu kua amekosea sana na kweli hakufanya vema kwetu na laiti angejua nini maana ya kuwepo WANA WA MUNGU ktk kila uso wa Nchi, angetubu tena haraka kwa kosa kubwa la kupuuza umma wa waliochanguliwa na mbingu kuwakilisha SERIKALI ya mbinguni hapa DUNIANI.

  Press on

 10. Wapendwa……..
  Mimi binafsi sikubaliani nao hawa maaskofu…….Kuachwa kwao kwangu naona kama ni mpango wa Mungu……..hakuna mwangaza mbele ni kutaka kuchafuka na siasa maji taka za Tanzania.

 11. Mimi nadhani kuna haja ya kufahamu nini kinapelekea viongozi hao kubaguliwa,sambamba na hilo cdhani kama kuna tatizo kwa wao kuhoji kwani nchi hii inawahusu wao pia na wanahitaji kushiriki kwenye mambo ya msingi kabisa ya kuweza kuisaidia nchi yetu.Pamoja na maombi ambayo huwa 2namwomba Mungu kwa ajili ya mambo mengi ktk nchi yetu Mungu anafahamu uhitaji wetu lakini c kizuizi cha cc 2naomwomba Mungu kutekeleza mambo yaliyo ndani ya uwezo we2.Mfano kama hili la hawa viongozi kubaguliwa ni wajibu wao kuzungumza waziwazi kwa serkali kwa namna serkali inavyowatreat!cdhani kama ni kosa!lazima serkali itambue kuwa hawaridhishwi na namna ya ubaguzi unaofanywa.Lakini kama nilivyosema hapo juu kuna sababu ambazo zinafanywa wacwekwe kwenye hiyo list!na ni lazima waseme ili serkali ifunguke na iseme kanini hawawashirikishi nafikiri kuja jambo lililojificha nyuma ya pazia.

 12. Humphrey,
  Kama nchi hii haitambui dini, kwa nini waliagiza taasisi za kidini nazo zipeleke majina, waliwezaje kutambua kuwa kuna hizo taasisi kama kweli serikali haitambui dini?

  Au ni ule uongeaji wa kuongea tu kwa mazoea bila kujua ukweli na uhalisi wa unachokiongea!!

  Kama hawatambui dini, kwa nini huwa wanaapisha viongozi kwa mujibu wa imani/dini za hao wanaoapishwa?

  Usikariri maneno, kariri ukweli uliomo ktk hayo maneno!!!

 13. Lenda,

  Nini maana ya kulaumu?

  Na ni kwa nini kulaumu unakuhusisha na kulaani?

  Ni wapi wapentekoste wamelipiza kisasi ?

  Yes, hayo ni ya Kaisari, inaposema mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari maana yake ni kuwajibika au kuyatenda yale yanavyotakiwa kutendwa. Hiyo ni pamoja na kumwambia ukweli anaposhindwa kutenda haki!

 14. Sikubaliani na wachangiaji waliotangulia. Ni kweli kuwa hawa wenzetu wamekua wakibaguliwa katika mambo mbalimbali na kama ni vigezo wanavyo sana huenda kuzidi hata hao wanaokumbukwa siku zote. Hii nayo ni taasisi kama zingine zilizopeleka majina (e.g. TEC, CCT, Bakwata) km serikali ilivyoagiza so iweje taasisi moja ya dini imepewa majina 10 (jina lipo) nyingine hata 1 hakuna ??, nafikiri ni haki yao kulalamika if we are to be fair!!!!. Kwa wale wasiojua kulikuwa na makundi mbalimbali yaliyopeleka majina na kama ni sifa nadhani hawa jamaa wanazo za kutosha. Ninachokiona ni ile kasumba maana hata huko nyuma ktk matukio ya kitaifa huwa hili kundi halishirikishwi na hilo limejitokeza hata ktk mchakato wa katiba. Ni vema PCT mkaungana na kuwa na sauti moja yenye nguvu Tanzania kama mnataka kuondoa huu unyonge. Kufunga na maombi tuu havitoshi lazima kujitokeza wazi na kusema ukweli na kupigania haki yenu kama taasisi kamili yenye majukumu ktk jamii na taifa. Ukiangalia mna washirika wengi nchini karibu 11 mil na mnajulikana mpo lakini cha kushangaza ktk mambo muhimu mengi ya taifa hamkumbukwi!! tujiulize kunani hapa?????

  Ninapendekeza sana sana ndg zangu kama mnataka kuwa na sauti moja inayotambulika kitaifa muwe na umoja na uongozi imara. Bila kuwa na umoja wenu wenye nguvu mtaendelea kubaguliwa siku zote na serikali hii. Ni vema mkaunganisha nguvu wote na kuwa na viongozi wenye nguvu, elimu, uelewa na influence, other wise mtaendelea kulalamika tu. Wakati ni huu, mshikamano daima utawatoa!!!

 15. tutambue kwamba katika nchi haitambui dini,ila wananchi wake wanadini zao,uteuzi unapofanywa hawaangalii dini yako ila vigezo vyao walivyojiwekea,wapagani nao watasemaje,waisilamu nao wanamisimamo mbalimbali,je tuzidi kuangalia dini?no!!!!!!!

 16. NILIDHANI KWA KUWA WAPENTEKOSTE WANA MAOMBI NA MFUNGO WAO, WATAIBARIKI SERIKALI HAWATAILAUMU,ILI WAFANYE KAZI VILE WALIVYOONA BILA PENTEKOSTE WANGEWEZA KUFANYA MAANA HAYO NI YA KAISARIA . ITAKUWA NI AJABU WATU WANAFUNGA HALAFU WANALAANI.

  WARUMI 12:14
  “WABARIKINI WANAOWAUDHI; BARIKINI WALA MSILAANI”

  WARUMI 12:2
  “WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII;”
  WARUMI 13:2
  “HIVYO AMWASIYE MWENYE MAMLAKA HUSHINDANA NA AGIZO LA MUNGU; NAO WASHINDANAO WATAJIPATIA HUKUMU”
  (ACHENI SIASA)

  1 WAKORINTHO 4:12,13
  “TUKITUKANWA TWABARIKI, TUKIUDHIWA TWASTAHIMILI; TUKISINGIZIWA TWASIHI; TUMEFANYWA KAMA TAKATAKA ZA DUNIA”

  WAEBRANIA 13:13
  “BASI NA TUTOKE TUMWENDEE NJE YA KAMBI, TUKICHUKUA SHUTUMU LAKE. MAANA HAPA HATUNA MJI UDUMUO,BALI TWAUTAFUTA ULE UJAO”

  YOHANA 18:36
  “YESU AKAJIBU, UFALME WANGU SIO WA ULIMWENGU HUU. NA KAMA UFALME WANGU UNGEKUWA WA ULIMWENGU HUU, WATUMISHI WANGU WANGENIPIGANIA, NISIJE NIKATIWA MIKONONI MWA WAYAHUDI”

  WARUMI 13:13
  “KAMA ILIVYOHUSIKA NA MCHANA NA TUENENDE KWA ADABU;SI KWA ULAFI NA ULEVI, SI KWA UFISADI NA UASHERATI,SI KWA UGOMVI NA WIVU”

  MATENDO 10:36
  “AKITENDA KAZI NJEMA NA KUPONYA WOTE WALIOONEWA NA IBILISI”
  MAKANISA YAMEPOTEZA UJUMBE WA UMILELE NA KUKUBALI UJUMBE WA UFALME KATIKA DUNIA HII UNAOLETA SERA ZA.
  1. MAISHA BORA YA KIUCHUMI NA JAMII
  2. KUSHIKILIA MALI ASILI ZA DUNIA
  3. MAENDELEO YA KISIASA NA SOCIALISM (MGAO SAWA WA MALI)

  4. KUPIGANIA HAKI ZA BINADAMU,MAZINGIRA,USAWA KIJINSIA,KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUTENGENEZA UFALME WA UKRISTO WENYE MAISHA BORA YA DUNIANI.

  UJUMBE HUU WA KUOMBEA UCHUMI WA NCHI NA SIASA BORA UMELETWA NA ONE WORLD, ONE RELIGION, NA ZIONISM UKIHUBIRI YERUSALEMU YA SASA NA SI ULE UTAKAOSHUKA.

  WAKRISTO WA KWELI HAWALIPIZI, HAWATISHII

  WARUMI 12:16
  “MSINIE YALIYO MAKUU, LAKINI MKUBALI KUSHUGHULISHWA NA MAMBO MANYONGE”

  WARUMI 12:19
  “WAPENZI, MSIJILIPIZE KISAS….”
  RUDINI KWENYE MKUTANO WA MTAGUZO WA (VATICAN COUNCIL II) MKAUTWAE UJUMBE MLIOHUBIRI AWALI JUU YA KRISTO. HAKUNA ATAKAEWAPA HAKI DUNIA HII.

  UJUMBE MBAYA DUNIA INAYOTAKA MFANYE NI HUU:

  “BRING HERE YOUR BIBLES AND GO TO PREACH PEACE AND JUSTICE, HOW TO GET RICHNESS, PROTECTING THE ENVIRONMENT IN THIS WORLD. WE WANT THIS PLACE TO BE PEACEFUL, WE DON’T NEED THE NEW JESUSALEM HERE”

  KAMA MNATAKA KUTETEA KILIO CHA WATANZANIA, MUNGU AMESIKIA MWENYEWE HATA KABLA HAMJAOMBA NA NINYI WENYEWE MSIWE WATU MLIOJILIMBIKIZIA MALI NA MAJUMBA,NA FEDHA NA DHAHABU.

  YAKOBO 5:3
  “DHAHABU YENU NA FEDHA YENU ZIMEINGIA KUTU, NA KUTU YAKE ITAWASHUHUDIA, NAYO ITAKULA MIILI YENU KAMA MOTO”

  YAKOBO 5:4
  “ANGALIENI UJIRA WA WAKULIMA WALIOVUNA MASHAMBA YENU, NINYI MLIOUZUIA KWA ILA, UNAPIGA,KELELE, NA VILIO VYAO WALIOVUNA VIMEINGIA MASIKIONI MWA BWANA WA MAJESHI”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s