Swali kwa Mitume na Manabii!

 

swali

Katika kusoma maandiko sijaona kabisa aliyekuwa mtume na nabii, kama alikuwa nabii ni nabii na kama alikuwa mtume ni mtume, sasa hawa wa sasa mtu mmoja huyo huyo ni mtume na nabii inakuwaje?

Naomba kueleweshwa jambo la pili hawa mitume na manabii wa sasa hawaelewani wala kushirikiana wao kwa wao, kila mmoja ana ufunuo tofauti na mwingine, hizi funuo wanazipata wapi? kwani Bwana Yesu kasema wote wawe na umoja kama yeye alivyo na Baba sawasawa na Yoh 17:20-20.

Natamani kufahamu haya wapendwa,

–Alfa Kimaro

Advertisements

14 thoughts on “Swali kwa Mitume na Manabii!

 1. John Bethania hizo nukuu za kunyofoa mstari moja na kunyanyulia bango ndizo watumiazo matapeli kama marehemu Munuo. Kwa ufasaha unaweza tupa tofauti kati ya andiko na neno. Mimi.nawaonea huruma mmejazwa ujinga pasipo kujua. Wengi mnadhani kutamka ndio kuwa. Huwezi kuwa mwana wa Mungu na bado ukawa mchoyo, mwongo, tapeli, mzinzi, mwizi etc. Huo ni ujinga sawa na wanajiita milionea wakati hata elfu tano huna, na hata mkakati wa kuwa milionea huna.

 2. Claus,
  Mungu akisema jambo, hakuna anayeweza kulitangua!

  Dunia imetupiga sindano ya ganzi ya kiroho, suruali haiyasitiri maungo ya mwanamke kwa sababu ni vazi la kiume, isipokuwa kwa ile ganzi ndio unawaona mabinti na wamama watu wazima, hao ambao wanapaswa wawafundishe hao mabinti, lakini wamekuwa ndio mifano ya waliopotea wakiwapoteza na hao mabinti wadogo, na waume ndio kabisaaa walikwisha potea siku nyingi, na nyumba zao zimebaki mikononi mwa hao wake zao!

  Mungu anasema mwanamke anayevaa mavazi ya kiume ni chukizo, basi sala na maombi yako yatafikaje kwa Mungu ilhali u chukizo?

  Dada zangu, ni heri mzivue hizo suruali, mpate nafasi ya kuongea na Baba yenu, kuliko hivyo mnavyoishi ktk udanganyifu, sala na maombi yenu yakiwa yamezuiwa bila ninyi kujua! Misisimko sio uwepo wa Mungu, siku utakayofika uweponi mwake ndio utaijua tofauti, tupa hizo suruali zako halafu utaniambia!!!!

 3. Imeandikwa katika bibilia takatifu kwamba na mwanamke asivae mavazi ya mwanaume je,hii ina maana nyingine zaidi ya hizi suruali?

 4. Katika kusoma maandiko? Soma Yohana 5:39 kama unadhani kwenye maandiko mna uzima!!!!!!!! Katika maandiko mna uzima? Ila katika Neno

 5. Ndg yangu, hebu lands andiko chili litakusaidia, lkn tu, ukilisoma name kulitafakari kwa kiina sana. 1timotheo 2:7, “nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe
  Mhubiri( MWINJILISTI) na
  Mtume, ( nasema kweli, sisemi uongo),
  Mwalimu wa mataifa ktk imani n kweli”.

  Hivyo, yaonekana y kuwa, kwa andiko hili Paulo alikuwa na zaidi y Huduma moja. Bado swali lako la dumu mpaka hapo?

 6. Lwembe,

  Nimekumisi kweli hapa SG. mzima wewe? come on mtumishi.

  Kuna jambo wanaSG napenda kuuliza kwenu ambalo najiuliza juu kuhusu hawa mitume na manabii wa kizazi chetu.

  1. Nasikia huwa manabii na mitume walio wengi ni lazima waende Nigeria kupewa upako na/au kusomea unabii au utume.eti kuna vyuo vyao huko.. Huko Nigeria kunani tena. mbona manabii na mitume wa zamani chuo chao kilikuwa kusoma neno na kupokea mafunuo toka kwa RM. na hakuna popote Mungu alipo waambia waende ili kupokea uwezo.daima aliwapa popote na kumtumikia? Wapendwa msininukuu vibaya,nimesema nasiki tu, km maneno haya ni uongo basi tuachie hapa na tuendelee kuzijaribu hzo Roho zao km zinatokana na Mungu.

  2. Miujiza km kigezo cha kuipokea imani fulani.

  Wapenda tuwe macho, miujiza isituvute km kipaumbele ktk kusema iman hii ina RM na hii haina,kumbka hata shetani kama malaika wa nuru anaouwezo wa kutenda miujiza. Vipi kuhusu wale wachawi wa misri na nyoka zao mbele ya Musa, ktk kitabu cha Kutoka.

  Itapendeza sana km mitume na manabii wa kizazi chetu watatangaza sio miujiza na uponyaji tu bali watawaita watu wamfuate Yesu kwa sababu atawapa nguvu ya kushinda dhambi maishani,kujazwa RM,Kupata tunda la Roho kwanza, then miujiza ni kipaumbele cha tatu,nne au hata tano.

  To GOD we belong!

 7. Wapendwa,

  Kulingana na swali lililoulizwa, msingi wa majibu yetu ni lazima uwe juu ya Neno lililofunuliwa, ambalo ndilo hilo tuliloletewa na mitume. Sisi ni Kanisa, basi kwa sehemu, Neno linaloweza kutuongoza katika majibu yetu ni huo Msingi wa jambo hilo ambao kwa sehemu, tunauona ktk Efe 4:11-12
  “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”

  Basi, hizi Huduma Tano ndizo zinazomleta Kristo ktk kusanyiko, hata kulifanya kuwa sawa na lile kusanyiko la kwanza, alipokuwa na mitume wake! Labda tuzitazame kwa uchache jinsi ya Huduma hizo ktk kuujenga Mwili wa Kristo. Kwanza ikumbukwe kwamba anaye watoa hawa kuwa ktk hizo nafasi ni Kristo mwenyewe, kama alivyowachagua wale 12, ndivyo anavyofanya hata kwa hawa ktk kila kusanyiko, hata liwe dogo kiasi gani huko kijijini kwenu, sio mambo ya kusomea chuoni, hapana, bali ni karama au kipawa.

  1: Mtume: ni mwaminio aliyewekwa wakfu kwa ajili ya Utume. Huyu ndiye mjenzi wa makusanyiko. Kristo humpeleka ktk sehemu za jangwa la Injili, huko ktk milki za kipagani, naye akifika hapo huisimamisha Injili na kuwaita wote waliokusudiwa ktk kusdi la Mungu la kumpeleka hapo. Tena huyu hubeba neno la kinabii kwa ajili hiyo, maana ni hilo pekee lenye nguvu ya kuwavuta hao waliokusudiwa kulingana na Mungu alivyolitayarisha kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa na sasa akilitimiza kupitia huyo mtumishi wake.

  Ndani ya mtume kunawezekana kuwamo vipawa vingine, kama cha Uinjilisti, hapo anapowahubiria wapagani, akiwashitaki kwa mienendo yao na kuwaonesha Ukarimu wa Mungu aliowakirimia kupitia uwepo wake yeye, kwa kadiri ya miujiza itakayofanyika ktk sehemu hiyo kwa ajili ya udhihirisho wa Uwepo wa Mungu ktk Kristo. Ndipo unabii wenye kuzifunua siri za mioyo ungeonekana, na pia Ualimu katika kuifundisha Misingi ya Wokovu na hata Uchungaji wa kusanyiko ktk hatua hizo za Ujenzi.

  Baada ya kazi hiyo, ndipo yeye kwa kile kipawa cha unabii, kwa kulibeba Neno la kinabii, Mungu angemuonesha kati ya hao kusanyiko atakaye muinua kwa kazi ya Uchungaji. Ndipo angefanya utaratibu wa kumsimika mchungaji kulingana na uongozi wa RM, na angeendelea kulilea kusanyiko hilo akiwasaidia ktk hili na lile ktk kuukulia wokovu hata vipawa vilivyobaki vijengeke ndani ya kusanyiko hilo kwa kusudi lililokusudiwa, kuwakamilisha watakatifu. Pia huwa hawajitangulizii nafasi zao walizopewa, kujitambulisha kwazo, sijui Baba Mtakatifu Siyi, au Mtume Mjema nk wao ni wapole kama huwa, ni wanyenyekevu wasiojikweza bali humkweza Kristo ktk maisha yao yote!

  Anapoimaliza kazi hiyo, hungojea maelekezo mapya kutoka kwa aliyemuweka ktk kazi hiyo, aende wapi. Huwa hawayang’ang’aniagi makusanyiko kama luba! Ukitumwa kujenga nyumba, unaijenga kisha unamwita aliyekutuma unamkabidhi, na unapumzika kungojea ngwe nyingine! Ukiona wanang’ang’ania ndani ya nyumba walizozijenga, basi jua kuwa hizo ni nyumba zao, hawakutumwa na yeyote yule, licha ya kauli zao za kutumwa, ni waongo tu!

  Mtume Paulo ni kielelezo kizuri sana kwetu, maana huyo ndiye aliyetumwa kwetu!!

  2. Manabii:

  itaendelea…….

 8. Kwanza nina furahi sana kuwasoma juhu yana nifanya nihelewe zahidi mafundisho ya neno la Mungu
  Swali nilo huliziwa na ndugu moja pendwa kiroho
  Swali: Kati ya mitume kumi na mbili
  Yupi Mtume aliye kuwa na anaye kuwa na ushuhuda mzuri wa kuhigwa? Ambaye Imani yake yafaha kwa mafundisho mazuri na ya kweli ya leta aho yatakayo leta uzima wa milele?

 9. Alfa,
  Kwani manabii wa zamani walikuwa na umoja gani, ambao manabii wa leo hawana?

  Kipengele cha kwanza Mnjema kwa sehemu kubwa amekijibu vema, nampongeza!

 10. A.Kimaro, (1kor14:32)

  Ubarikiwe kwa kuwa mungwana kama waberoya kutaka kujua kuwa kama mbambo hayo ndivyo yalivyo,Mdo17:11. Nimeyapata maswali yako nami kwa uelewa wangu napendekeza majibu yafuatayo kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

  Utangulizi:
  Nadhani unajua maana ya Neno:
  1.Mtume-mtu aliyeagizwa/aliyetumwa kwenda kutekeleza jambo/jukumu fulani. Mfano:Yesu atuma wanafunzi wake kwenda kumshuhudia kwa watu wote (Math28:19-20), ndiyo maana leo wote tunajua habari za mitume 12. akiwemo Yohana (nimemtaja yohana kwa makusudi,utanielewa punde)

  2.Nabii-Mtu anayetabiri jambo kabla halijatokea akiongozwa na RM na likatokea
  kama alivyotabiri (2petro1:20-21).

  Pia nakushauri Soma 1Wakorintho12:4–31-Katika aya hizo utapata majibu kwa maswlali yako yote mawili.

  ukisoma vizuri aya nilizokupa hapo juu Majibu kwa Maswali uliyouliza ni kama ifuatavyo;

  1.Swali lako: Je, mtu aweza kuwa mtume na wakati huo huo akwawa nabii?

  Jibu: NDIYO
  kumbuka hizo ni karama za RM naye uwapa watu kama apendavyo; 1kor12:4. RM akuna popote katika maandiko ambapo karama hizi zimewekewa mipaka kuwa mtu mmoja hawezi kuwa nazo. kumbuka kwa mujibu wa 1kor12 niliyokuelekeza kusoma hapo juu, lengo za karama zote ni ili kukamilisha kazi na kulijenga mwili wa kristo/kanisa.
  Mifano:

  1.Agano la Kale: Nabii Yona- Soma yona 1-4-maandiko yanaonyesha kuwa Yona ALIPOTUMWA (ALIKUWA MTUME) kwenda Ninawi alifanya kazi kama 1.Mtume na 2.Nabii.

  2. Agano Jipya:
  a)Yesu alitumwa na Baba kuja kutuokoa kutoka dhambini (Mtume) -Yoha3:16
  – pia kumbuka alifanya kazi kama Nabii mfano;- aliwahi kutabiri mara nyingi kuhusu matukio yaliokuwa mbele yao, na yalipotokea wanafunzi walistaajabu.

  b) Kumbuka kuhusu Mtume Yohana aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu, ni yeye huyo huyo aliyeandika kitabu cha Unabii cha (Ufunuo wa Yohana).

  -Hii ni baadhi ya mifano tu. Hivyo ondoka shaka juu ya kuwa na vipawa vyote viwili kwa pamoja. kwani ni sawa na mtu kuwa na karama ya Uchungaji na wakati huo huo akawa Mwimbaji. zote hizo ni karama kaka.

  Swali lako 2: Mbona hawa manabii na mitume wa siku hizi hawana umoja kama alivyofundisha Yesu?

  Jibu: Ni kweli Yesu anataka Manabii na mitume wawe na Umoja.kama isemavyo 1Kor12.

  -Hapa ndipo tunapogundua kuwa hawa waloi wengi ni mitume na manabii wa uongo. na Yesu ana sema ” Wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu, kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”.

  Jinsi gani/vigezo gani utumika kuwapima mitume na/au manabii ili kujua kuwa ni wa uongo au wakweli?

  1.Waenende kwa sheria na ushuhuda/Neno lote Mungu kinyume na hapo ni wa uongo. Na sisitiza NENO LOTE, ikiwa kuna kweli za biblia ambazo mtume au nabii anazipuuzia huyo niwauongo. Nabii wa kweli uihinua KWELI YOTE juu. kumbuka yakobo2:10 anasisitiza juu ya kuzisha sheria zote. Kujua sheria soma kama zilivyoandikwa na Mungu mwenyewe. katika Kutoka20:1-17.

  2.Hudumisha Umoja wa kanisa . 1Kor12. Nabii au mtume anayelifuruga kanisa huyo niwa uongo.

  3.Anayetii manabii/mitume wengine. Neno la Mungu linasema “na Roho za Manabii uwatii Manabii”. 1Kor14:32. kwa kuwa uongozwa na roho yule yule hivyo hawawezi kufarakana.

  4.Ufanya yote kwa utukufu wa Mungu. 1Kor10:31-sio kwa kujisifu kuwa wao ndio wanaofanya bali Yeye aliyewatuma.

  5. Utangaza INJILI YA MILELE na sio INJILI tu, Ufunuo14:6-7- Nabii/mtume wa kweli ni yule anayefundisha watu waache dhambi kwa kuzitaja kwa jina. Wanaojiita manabii na mitume wa sikuizi kazi yao ni kuubiri tu miujiza/uponyaji na utajiri huku wakifumbia macho dhambi za washiriki wao. ukiona nabii/mtume wa aina hiyo, ni wauongo.

  Rafiki, miujiza ni matokea-effects za kumfuata Yesu na SIO sababu-causes ya kumpokea Yesu. Yaani Ukimpoea Yesu (ukiacha dhambi) matendo ya muujiza ni matokeo tu. kwani hata shetani ana uwezo wa kutenda miujiza. ukiona mtume/nabii anawafuta watu kwa miujiza mtazame mara mbi mbili

  Rafiki hivi ni baadhi tu ya vigezo ambavyo kama ukivitumia kwa uaminifu ni hakina walio wengi leo wanaojitangaza kuwa manabii na/au mitume hakuna anayebaki kuwa wa kweli.

  UBARIKIWE

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s