Ikulu haikupokea mapendekezo ya majina kutoka PCT – Dr. Turuka

ikulu picha

OFISI ya Rais, Ikulu, imesema uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, haukuwa na nia ya kulibagua Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania.Imesema kuna kila sababu ya kuamini kuwa mapendekezo ya wajumbe kutoka baraza hilo hayakuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kama sheria ilivyohitaji.

Pia, imesema pamoja na baraza hilo kutowasilisha mapendekezo yao kama ilivyotakiwa, litawakilishwa vyema na wajumbe walioteuliwa ambao wanajumuisha mjumbe aliyeteuliwa kutoka moja ya madhehebu yanayounda baraza hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ikulu mjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Florence Turuka, alisema tamko la Baraza la Maaskofu kuwa linabaguliwa na serikali halina ukweli wowote.

Dk. Turuka alitoa ufafanuzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, na kuongeza kuwa kama mapendekezo ya baraza hilo yengewasilishwa kwa mujibu wa sheria, yasingeachwa.

Alisema uchunguzi uliofanywa na Ikulu, haujathibitisha kuwa baraza hilo liliwasilisha mapendekezo yake na kwamba ni vyema baraza likajiuliza kwanini kama kulikuwa na mapendekezo hayakufikishwa kwa wakati kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar.

Dk. Turuka, alisema iwapo mapendekezo ya baraza hilo yangefikishwa kwa makatibu wakuu hao, Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohammed Sheni, wangechagua mwakilishi kutokana na mapendekezo hayo.

Alisema uchambuzi wa majina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba umebaini kati ya wajumbe 13 kutoka taasisi za kidini wa Tanzania Bara walioteuliwa, Respa Adam, ameteuliwa kutoka Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Patmos Vission, Kigamboni, ni moja ya madhehebu ambayo maaskofu wake wakuu wanaunda baraza hilo.

Kwa mujibu wa Dk. Turuka, Februari 11, mwaka huu, baraza hilo lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa limebaguliwa na serikali wanayoiheshimu, kuiombea na kuipenda katika uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

Alisema anawahakikishia Watanzania hususan waliolengwa na taarifa ya baraza hilo kwamba serikali haikupuuzia kundi lolote lililoanishwa kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba.
Dk. Turuka alisema serikali inaliheshimu baraza na inalishukuru katika juhudi inazozifanya kwa kushirikina na serikali katika kuwaendeleza Watanzania.

Alisema makundi 850 yaliwasilisha mapendekezo ya majina 3,636, ambapo makundi ya kidini yalipendekeza majina 429.

Katibu Mkuu huyo, alisema uchambuzi wa mapendekezo 52 yaliyowasilishwa nje ya muda, haukubaini kuwepo kwa mapendekezo kutoka baraza la maaskofu wa Kipentekoste Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dk. Turuka alisema hana uhakika kuwa wajumbe waliochaguliwa kutoka Chama cha NLD ni mtu na mke wake.

–Magazetini

Advertisements

11 thoughts on “Ikulu haikupokea mapendekezo ya majina kutoka PCT – Dr. Turuka

 1. Ndugu yangu Edwin Seleli, Shalom,

  Nakushukuru sana kwa meseji yako tamu na yenye hisia. Imenihusa sana Kwa kweli wote tuna uchungu huo huo kuona tumeachwa katika uchambuzi wa majina; kwamba hatuna wawak ilishi wetu huko rasmi kutoka PCT.
  Kwa kadri tulivyowasikia au kusoma mitandaoni viongozi wetu wa PCT waliilalamikia Ikulu wakidai kwamba walipeleka majina huko Ikulu lakini yakatupwa nje! Sisi hatujui Kama kweli yalipelekwa yakatupwa nje au! Sasa hatumo Bungeni tufanyeje? Tukae Kimya? HAPANA.

  Ndugu zangu, pamoja na machungu yetu ya moyo kwa uzembe wao viongozi au wa Ikulu kutowachagua wawakilishi wetu tunyamaze? Ndiyo maana nikasema yale yaliyomo katika Rasimu hiyo tuyafuatilie na kuyafanyia mkakati wa maombi, nina ukakika kwa umoja wetu (japo si sana kwa sababu ya udini) na kwa tushirikiana tutaiombea nchi, Rasimu yenyewe kutaka nini toka kwa Mungu ili atutendee, iweje na kwa sababu gani.

  Edwin Seleli mpendwa wangu, ninayaheshimu sana mawazo wako mtumwa wa Kristo kama ulivyosema nanukuu, “Hakuna kitu kama icho cha kuchambua Katiba/ rasimu ktk ulimwengu wa roho, tusiwe tunajichosha ktk maombi ambayo yana align na ukweli aliosema Yakobo kua tunaomba hatupati kwa kua tunaomba vibaya.” Mwisho wa kunukuu Mimi naamini kabisa kanisa lina nafasi katika mambo yanayoihusu serikali. Soma maneno haya “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 1 Tim. 2:1-5

  Edwin Seleli, Maombi ni ya LAZIMA huwa hayana tabia ya kuchosha watu kwa kuwa yanalenga kuongea na Mungu Baba yetu kuhusu jambo fulani tutachokaje? Bado ninaitetea hoja yangu kwamba Rasimu hiyo isomwe makanisani ili tuombee vifungu vyote kandamizi kwetu na kiimani. Hayo ni mawazo yangu nionavyo mimi. Hata hivyo kama kuna hoja karibuni.

  Makunzo C.H.M.

 2. Lwembe,

  Suala la kuwa na wapiga kura milioni 11 limetoka wapi ndg yangu?

  Halafu unasema ”Hayo mapendekezo yenyewe, kuna mahali nimesoma kwamba huyo aliyekabidhiwa ayapeleke, aliyatuma kwa sms “kwa jina la Yesu” akitegemea muujiza!!! Hata hivyo kumbe kulikuwa na seti mbili za majina, seti nyingine, huyo aliyekabidhiwa ayapeleke ikulu, naye alimtuma mwanaye!!!! SETI ZOTE MBILI HAZIKUFIKA!!! Na, why 2 sets kutoka kikao kimoja au vikao vingapi????????”

  Haya uliyosema kuwa umesoma mahali fulani, mahali hapo ni wapi? Maana hainipi kuamini kuwa hao watu wazima (maaskofu wa PCT) walituma hayo majina kwa namna hiyo.

  Lakini pia katika kushauri kwako kuhusu suala la kuondokana na ulichokiita ubinafsi, wewe mwenyewe umelaumu zaidi kuliko kutoa ushauri.

  Na unapowaambia maaskofu kuwa wanawezaje kuapa kwa jambo ambalo hawana uhakika nalo, hapo napo nakushangaa ndg yangu. Kwani kati ya wewe na maaskofu, nani ana uhakika na anachokisema kiasi cha kuaminiwa na wasikilizaji?

  Wao wahusika wakuu wanasema majina walipeleka, tena kwa utaratibu unaotakiwa, wewe third party kwa kuamini taarifa uliyosoma mahali fulani unasema hawakupeleka majina kama inavyotakiwa.

  Binafsi naona kufanya hivyo ni kuamua kusimama upande usiopaswa kusimama, tena kwa kusimamia mtazamo ambao siyo thabiti ukilinganisha na ule wa upande wa watumishi wa Mungu maaskofu.

  Mtazamo huo kwa mimi naona ni kuwa so unfair!

 3. Wapendwa,

  Hatuwezi kuform Umoja kutoka ktk machungu yetu kwa serikali!!

  Haya, toka tuwepo tumejenga shule ngapi? Hospitali ngapi? Ni huduma ngapi za kijamii tunazozishughulikia?

  Inawezekana kwamba tuna kelele nyingi kuliko wingi wetu huo tunaowatishia nao serikali, kwamba tuna wapiga kura milioni 11, hii kama si blackmail ni nini???

  Hayo mapendekezo yenyewe, kuna mahali nimesoma kwamba huyo aliyekabidhiwa ayapeleke, aliyatuma kwa sms “kwa jina la Yesu” akitegemea muujiza!!! Hata hivyo kumbe kulikuwa na seti mbili za majina, seti nyingine, huyo aliyekabidhiwa ayapeleke ikulu, naye alimtuma mwanaye!!!! SETI ZOTE MBILI HAZIKUFIKA!!! Na, why 2 sets kutoka kikao kimoja au vikao vingapi????????

  Ubinafsi unatuuwa!!!

  Tengenezeni Umoja wenye Vision ya “Umoja wa Roho” ili unafiki na majungu, vyenyewe vitafute kwa kwenda; A strong Unity based upon the Teaching of Christ! Lakini huu umoja wetu, naona kila siku wanatafutwa wachawi na kubaguana tu, mara oh, hawa sio Wapentekoste … huyu hivi, yule vile nk, hakuna order kabisa, “umoja” full of ridicule, no wonder serikali inatushangaa kwa kauli zetu; HOW can you swear kwa jambo usilo na uhakika nalo? Kule kusema kwamba “tunaogopa kufunua utupu wa baba, na serikali ni baba yetu” ni sawa na kuapa kwamba mlipeleka majina!!!!

  Na mwisho wa siku, it proves that we don’t have a Unity, but think we have one!

 4. Makunzo C.H.M,

  Hakuna kitu kama icho cha kuchambua Katiba/rasimu ktk ulimwengu wa roho, tusiwe tunajichosha ktk maombi ambayo yana align na ukweli aliosema Yakobo kua tunaomba hatupati kwa kua tunaomba vibaya

  Mungu ni Mungu wa utaratibu na ameweka Serikali kufanya mapenzi yake na anatutaka tuheshimu taratibu na kuzifuata za Watawala, kama haumo ktk bunge, hakuna namna utajadili na kuunda Katiba kwa njia ya invisible/remote control, hakuna! hatumo bungeni kama PCT hatumo, basi

  I can guarantee, funga na kuomba sana yet kama hakuna wengi mule Wapendwa na kwa kuzingatia maamuzi yanapita kwa kura, basi madude mabovu aganist Kanisa, yatapita tu, kama unabisha, funga na omba kavu kisha nitakuuliza baada ya Mchakato kuisha.

  Kwa muda mrefu wapendwa tumedhani kufunga na kuomba ndio final mwarobaini na kuacha kabisa kanuni nyingine eg Wapendwa kuinga ktk Siasa na vyombo vya maamuzi ili kui-influence maamuzi na mabadikiko kwa faida ya imani yetu, well hata miasha ya jamii, matokeo yake tumeomba weee miaka, tumefunga weee mara kibao yet mambo yale yale, wafilisti wale wale, hakuna mabadiliko, why? Mungu ni wa utaratibu, hamtaki kuingia ktk Siasa na vyombo vingine ili mpige kura za maamuzi, endeleeni kuomba na kufunga, mtachoka tu na kulala tena bila kuwa makini na kujichunga moyoni/nafsini, mtamkasirikia Mungu na kuwaza moyoni vibaya maana hakuna maudhi, makwazo first class na majazba kama kuomba na kufunga sana kisha mambo yanaharibika zaidi kama si kubaki kama yalivyo, mbovu sana iyo na inamuma sana, ndio maana siku za leo mie huchagua sana nimbeje na hufanya maamuzi makini kweli nombee nini, si bora liende tu kua eti nimefunga na kuomba! No man. It has not worked that way and tukiwa honest kama nilivyo, utakubali tu kua, hakuna kitu MAJOR NA TANGIBLE One toka tumekomaa na kufunga na kuomba. I believe Mungu amekua anatufundisha/situa kua, ”’hey guys, wake up, open your eyes, go into the enemy’s camp live and lively, that is, do the prayers after praying the prayers!!!!!!!!

  Press on

 5. Salam zangu za upendo kwenu kupitia Jina la Bwana Yesu,

  Nadhani Viongozi wetu walipendekeza majina kutoka upande wetu (Wapentekoste) wa PCT. Kama ndivyo hivyo wasingeliilalamikia serikali – wamezimwa tu tuamini hivyo. Kwa hali hiyo tusiwalaumu, tumekatazwa na Bwana. (Wapakwa mafuta hao)

  Naamini, Kanisa lina NGUVU katika ulimwengu wa Roho kuichambua kwa undani kabisa Rasimu hiyo kwa njia ya Maombi, tukitamka yale ambayo tunayapenda na yepi hatuyapendi; serikali iendeshweje, sheria za nchi ziweje nk. Jamani si tunazijua nguvu za Baba yetu kupitia Jina la Mwokozi wetu? Mambo haya hayawezekani pasipo kupitia maombi na kufunga.

  Makunzo C.H.M
  Songea.

 6. Jamani,

  Ivi ni kweli maaskofu wetu hawakupeleka majina kabisa, halafu ati wakalalamika?

  Namasubiri katibu wa PCT nae asema ndipo binafsi nipate habari tengemavu. Maana siamini kama maaskofu walifanya hilo kosa halafu tena wakalaumu kutoteuliwa.

  Na kama iko kama alivyosema naibu katibu mkuu-ikulu, kweli nitawamind maaskofu wetu kwa hilo!

 7. Wachungaji na maaskofu wetu waangalie namna ya kuwashirikisha washirika/waumini ambao ni wataalamu katka mambo ya siasa ili wao ndio wawe front line wanaaandaa protokal za siasa kulingana na hitaji, kanuni, masharti husika ya tukio. najua watumishi hawa wanawezakuwa ”busy” kiasi cha kushindwa kufanya kulingana na kukidhi masharti yaliyo wekwa au standards zinazo hitajika.

  sijasema hawawezi, wanaweza sana ila kuna vitu wanahitaji kuwa na watu/wapendwa/waumini waliowataalam kwa taaluma husika ambao wataambatana nao kuwashauri. KAMA WEWE NI DIRECTOR WA KAMPUNI SIO RAHISI UKAWA HR AU UKAWA ACCOUNTANT AU UKAWA MWANASHERIA WA KAMPUNI.

  mbarikiwe wote
  Anthony M.

 8. All in All, ni dharau tu na kukosa hekima ktk maongozi, common senses ya Kiongozi asiyeteswa na dini yake moyoni ingawa nje anaweza onekana balanaced, ingemsukuma tu kuuliza, why sioni uwakilishi toka jumuiya fulani kubwa na nzito. To make my argument more clear, assume kua jumuiya za kiislamu aidha ziSIngepeleka majina au zikapeleka late, am telling you, angeuliza tu why such big jumuiya ya dini, haionekani mezani pake yaani hata kama walichelewa kupeleka, wangeitiswa tu majina yao, hakuna cha deadline wala lainooo maana kwanza wakiwaacha tu, wanaujua mziki wao mnene, hayo maandamano yatakayofumulumuka Nchini, weeeee mpaka watashaaa

  Sasa kwa nini same sensitive isiwe active alipomiss moja ya taasisi kubwa kabisa ya kipentekoste na wakaendelea tu na kuhitimisha uteuzi. Uongozi ni pamoja na hekima ya kufanya mambo si mamlaka uliyopewa na katiba ndio unalala nayo na kunywa nayo chai Nimechukia sana kuachwa sisi. Sasa huyo mmoja wa EAGT ndio atakua na brain yote ya Wapentekoste TZ? Mbona wengine wana brain nyingi uko toka same taasisi/imani! bila haya Turuka anasema eti Baraza letu lote na wanadamu wake, tutawakilishwa vema na mpendwa huyo mmoja tu! matusi makubwa na dharau ya pili kavu kavu. Natamani siku za Eliya, ningeshusha fire kwanza, kunyamazisha dharau hii kisha watu wakishatia akili na adabu ndio tukadili. Wanatuchukuliaga poa sana sisi wana wa MUNGU ndio maana.

  Press on

 9. Wapendwa Maaskofu!

  Tunaomba muache kulalamika. Changamkieni fursa. Tatizo la wapendwa wengi huwa siyo wepesi kuchangamkia fursa nzito za kitaifa na kimataifa.

  Rekebisheni kasoro hizo

 10. Tunashukuru Ikulu imetoa ufafanuzi leo kuhusu huu mkanganyiko hatimaye. Binafsi nimefurahi sana kuelewa tatizo lilikuwa wapi na pia maaskofu hawa nadhani watakuwa macho siku zijazo. Kwa kifupi ikulu imesema haikupokea majina yoyote kutoka Baraza la Wapentekoste Tanzania (PCT) na hii inajustify kwa kweli wao kutokuwemo ktk majina aliyoyachagua na mh raisi. Ni muhimu kushiriki mambo kama haya kitaifa na bila kuchangamka fulsa hizi watazisikia kwenye bomba tu. Hakuna atakayewatafuta au kuwakumbuka eti mpo bila nyie wenyewe kuwa mbele/upfront. Maaskofu wetu hope mtaliona hilo

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s