Tunaikemea dhambi ya Uongo – PCT

Baada ya Ikulu kutoa tamko kwamba haijapokea majina kutoka PCT, Maaskofu nao wamejibu barua ifuatayo,

maaskofuu

Advertisements

7 thoughts on “Tunaikemea dhambi ya Uongo – PCT

 1. Sungura,
  Unaifahamu serikali ya kwanza hapa duniani? Ina tofauti gani na serikali zilizopo?? Mimi nakuona umekaririshwa warumi 13 vibaya. Jitahidi uisome tena.

 2. Siyi,

  Nahisi unataka kutudanganya.

  Unaposema serikali fedhuli Mungu hajihusishi nazo, ni kujihusisha nazo kwa namna ipi unayoiongelea hapa?

  Hebu na wewe thibitisha kibiblia kuwa kuwa si kibiblia kudai haki kwa serikali.

  Tena thibitisha kibiblia kuwa duniani hakuna haki, na useme kama duniani haki haipo, hiyo haki iko wapi basi.

  Na ni wapi kama si duniani mahali ambapo watu wanatakiwa kutenda haki?

  Halafu unapotutaka tusishikamane na serikali zetu, unataka tuwe na uadui nazo au? Labda jikumbushe tena kichwani mwako maana ya serikali.

  Labda kama ungesema kuwa mtu asijishikamanishe na mtawala mwovu ningekuelewa, lakaini ukisema tusishikamane na serikali bila shaka hukijui vema unachokisema.

  Ndani ya serikali kuna watu waovu na wema kwa pamoja, kwa hiyo ni wajibu wa wale wema kuhakikisha nuru ya kristo inawaangazia wale waovu, ni wajibu wa wema kutenda haki kwa watu wote.

  Mwisho, kushikamana na mtu haina maana kuwa akitenda maovu au akikosea usimwambie uovu wake au kumkosoa makosa yake. Anayejua kutenda haki hutoa hukumu bila upendeleo.

  Tufanyeni uchmbuzi mahususi tunapoamua kujadili mada zinazoletwa hapa, tusiseme mambo bila kuwa na uthibati thibitivu.

 3. Seleli,
  Samahani kwa mara nyingine tena kaka kama nitakuwa nimekukwaza/nimewakwaza. Nina imani unafahamu kuwa, kuna falme ambazo Mungu hakujihusisha nazo kabisa. Falme fedhuli. Falme ambazo hazikutaka kumsikiliza Mungu kwa njia ya watumishi wake manabii. Mara nyingi, falme za namna hiyo zilikuwa na ufedhuli fulanifulani ndani yake. Sitaki kwenda zaidi….lakini ngoja nikupe mfano current.

  Hivi unafahamu kabisa kuwa kuna serikali zilizoruhusu ushoga hapa duniani. Je, unafikiri Mungu anajihusisha nazo? No, Mungu hachangamani na uovu. Na kama Mungu hajihusishi nazo, je, sisi watu (Wakristo) ndiyo tujihusishe na serikali kama hizo kisa warumi 13 imesema?

  PCT walifanya vyema kutuma majina yao. Lakini kama serikali iliyatupilia mbali, hakuna haja ya kulalamika. Mungu huwa ana njia nyingi sana za kutetea watu wake. Ukishafanya sehemu yako, lililobaki, unakaa kimya kumwangalia huyo Mungu unayemwamini.

  Aidha, sidhani kama kuna biblical evidences zilizowahi kuwepo kwa watu wa Mungu wakidai haki zao. Binafsi sijaona. Kama wewe unazo, zilete tujifunze sote. Nijuacho mimi, hakuna na si kibiblia kuandamana kudai haki kwa serikali. Haki inapatikana kwa Mungu peke yake. Duniani hakuna haki. Siku zote, duniani kuna hali ya kukubaliana kutokukubaliana. Ndiyo maana sisi leo waumini wa Kristo, tuna taraja la kuiona haki ya Mungu. Tunamsubiri Yesu ili siku moja aje atupeleke kwenye hiyo haki. Mbinu yetu kubwa ya kudai haki, ni kulihubiri neno la Mungu na kuishi maisha ya utauwa kama vielelezo halisi vya maisha ya Kikristo. Zaidi ya hapo, tunatanga mbali sana na misingi ya Kibiblia.

  Kuhusu kuchangia kila mada. Sidhani kama ninafanya hivyo. Nachangia mada chache sana. Nyingi nasoma. Nafikiri shida haikuwa kuchangia mada hii, shida ni kwamba, wewe hujaukubali mchango wako/mawazo yangu. Na mimi sikulazimishi ukubaliane nami. Wito wangu kwa wakristo wote, saa imefika ya kutojishikamanisha sana na serikali. Siku zinakuja serikali zetu hizi, zitaruhusu mambo ambayo ni unbiblical na sisi tulishajenga misingi ya umoja na serikali. Tutahubirije hizo sera za sserikali kwa waumini wenzetu in relation to the bible?
  Ubarikiwe

 4. Siyi,

  Acha pumba bwanaa…

  unasemaje ivi,..”’ mara nyingine Mungu huwa hahusiki kabisa na mambo ya serikali hasa serikali husika inapoonekana kutanga mbali na matakwa yake” …mmmm!. Mungu hausiki na serikali! we vipi! umeitoa wapi iyo! hata ikiwa inatenda dhambi au haifanyi matakwa yake, atahusika nayo tu hata kuinyuka/kuitandika ije kwa line! Warumi.13: 1-5 inasemaje? Mkuu wa Watu ni God’s minister, sasa why Mungu hasiusike, je si imeandikwa pia Yeye huinua Wafalme na kuwashusha! we vepe wewe! Ndio maana umeomba radhi kama umekwanza ktk comments zako, ni kweli si tu umekwanza but also umevuruga maana ata hayo ya kugusia kua wapendwa wanatoa msaada kisha wanaita media, wapi na wapi kwa mada hii! yaani wewe bwanaa unakurupukaga tu na kunyuka lolote linalokuijia eti eee, sometimes kauka, soma tu comments kisha barikiwa best, dah!

  Kuhusu kuandamana Wakristo kudai haki za kiraia si za kiroho, dhambi iko wapi, wapi tunalivurga Neno? hivi huyu vipi!

  Press on

 5. Sasa je, si mnaona! nilitaka kushangaa kua Watu wameokoka, wana akili za rohoni na kichwani, wamesoma pia, wana hekima na uzoefu wa Uongozi, Utaratibu, Malezi, Utawala ktk nyanja za ndani na nje ya Nchi, halafu wawe hawajapeleka majina tena kwa utaratibu!Ndio maana nilisema toka mwanzo ktk mada hii/izi, ni dharaui tu hawa, wanatuchukuliaga poa tuliookoka na pia kuna usaliti kwa taarifa nilizo nazo za chini ya kapeti.

  Kuhusu dharau ndio maana nikasema na bado natamani siku za Eliya au za akina Paul kidogo tu, unashusha fire na kuchoma-choma mashavu yao kwanza au unatandika mtu upofu dharau zikiisha ndio tunaongea kosa! Wametupuuza sana kwa hili kwakweli, yaani KATIBA kabisa ya Wote, unapuuza portion ya kutosha ya Wananchi wako, ala! mbovu sana Wanadamu hawa.

  Press on

 6. This is what I have been waiting to hear!

  Ukiwa mtanzania mtu mzima na unaewafahamu hawa watu wote wawili (Maaskofu na Serikali), na ukayaangalia mazingira ya jambo hili, utajua tu nani kasema ukweli na nani kadanganya.

  Serikali yetu tunawajua, na maaskofu wetu tunawajua, mpaka hapo naweza kuelewa nani kafanya nini.

  Haki huinua taifa!

 7. Binafsi,
  Sidhani kama kuna haja ya kuendelea kulalamikia sana Serikali. Ingependeza makanisa mengi ya Kikristo leo, yaache kujishikamanisha na kujipendekeza kwa serikali. Nasema hivyo kwa sababu, mara nyingine Mungu huwa hahusiki kabisa na mambo ya serikali hasa serikali husika inapoonekana kutanga mbali na matakwa yake. Sisemi kuwa serikali ya Tz imetanga mbali na Mungu, hasha. Lakini viongozi wetu wa dini inabidi wakae chini kutafakari mstakabali wa kuendesha mambo yao ya dini pasi kuingilia mambo ya serikali na vice versa.
  Siku hizi utaona wakristo nao wanaandamana kulaani jambo fulani. Hivi hakuna njia sahihi za watu wa Mungu kushughulikia changamoto ktk jamii zetu? Watu wanaomjua Mungu kabisa, wanakuwa mstari wa mbele hadi mabomu ya machozi yawagonge? Wakristo hao??!! Hivi kweli tuna tofauti gani kati ya Wakristo na watoto wa mama mdogo?
  Siku hizi utawasikia wakristo, ooh, kuna tukio la kutoa msaada fulani kwa jamii au kundi fulani la watu. Wakristo wanahangaika sana kuita vyombo vya habari ili waonekane wanafnya nini kwa umma/serikali. Kama si kujipendekeza huko ni nini? Je, hili ndilo fundisho la Biblia? Nachelea kusema hivyo maana Biblia inasema, ” Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguniā€- Mathayo 6:1. Sasa kama hatupati chochote mbele za Mungu, kwa nini tuendelee ktk hayo? Kuna haja ya kurudi kwenye Biblia badala ya kwenda huku tunakoelekea sasa.
  Huu ndio mtazamo wangu wapendwa. Samahanini kama nitakuwa nimewakwaza baadhi yenu. Binafsi huwa naumia sana ninapoona haya yanaendelea kutokea. Wakristo wote, kila iitwapo leo, tunazidi kupoteza mwelekeo. Kila siku tunazidi kushikamana na kufungamana na dunia. Mungu atusaidie sana.
  Tujitahidini…

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s