Mchungaji KENYA apata ufunuo kuangalia jina lako kama liko kwenye kitabu cha Uzima!!

Bishop-Thomas-Wahome

Mchungaji kutoka nchini Kenya, Askofu Thomas Wahome kutoka huduma ya Helicopter of Christ Ministries, hivi karibuni amezua gumzo ndani na nje ya Bara la Afrika baada ya kuibuka na ufunuo aliouita “Check whether your name is in the book of life” ufunuo huu mpya unaambatana na kutoa kiasi cha pesa taslimu za Kenya Shilingi1500, ili aweze kuhakiki jina lako kama limeandikwa kwenye kitabu cha uzima wa milele.

Amedai kuwa kama mtu akilipa kiasi hicho cha pesa basi yeye anao uwezo wa kufanya maombi kumuuliza Mungu kama jina lako limeandikwa kwenye kitabu cha uzima cha watakatifu mbinguni ama la pia kubaini kama wewe ni miongoni mwa watu watakao kwenda mbinguni ama hapana.

Awali mchungaji huyo mnamo mwaka 2012 aliwahi kuibuka na ufunuo wa kudai kiasi cha pesa za Kenya Sh 1,200 kwa mtu ambaye angetaka kugusa pindo la vazi lake kupokea uponyaji kama ilivyotokea wakati wa Yesu miaka elfu mbili iliyopita na kunukuliwa katika kitabu cha Marko 5:21-34

Wahome alidai kuwa mtu yoyote ambaye angetoa kiasi hicho cha pesa kisha kugusa pindo la vazi lake basi angepokea uponyaji sekunde hiyo hiyo.

–Magazetini

Advertisements

9 thoughts on “Mchungaji KENYA apata ufunuo kuangalia jina lako kama liko kwenye kitabu cha Uzima!!

 1. Ni MATHAYO 24:24 Inatimia.Wapo wengi wa namna hii hata Tanzania wamejaa wahubiri wa uongo wa madhehebu mbalimbali ambao mungu wao ni tumbo (1Kor 6:13).Hili andiko(Mathayo 10:8) hawalioni kwa sababu MUNGU awamepofusha macho.(Marko 4:12)

 2. Mhm, aya Bwana mambo ya chapaa ayo. Chezea fweza wewe,

  Kweli pesa imekuwa ngumu. Naona ujasiriamali hadi kwny mambo ya kiroho. Aya wapendwa hao ndio wale tangu enzi za Yesu wanaogeuza nyumba yake kuwa genge la biashara.

  Yesu aliguswa pindo hakuchaji pesa na hilo la kujua endapo jina lipo kitabuni nalo jipya.
  Wajinga ndio waliwao. Asomae na afahamu.

 3. Shalom
  Hivi ni wapi bwana wetu Yesu alitoza pesa ili akufunulie siri ya uzima wa milele!!! Watumishi tunawapeleka wapi kondoo wa bwana??? umepewa bure toa bure,pesa zitakuja tu maana mungu anajua atakavyo kutunza mtumishi!!
  tuwafundishe watu jinsi ya kuisikia sauti ya mungu si kuchukua hela zao,mungu hujifunua kwa yeyote amtafutae kwa bidii atamuona,
  barikiwa!!
  Stella.

 4. Sungura,

  Duh, wapendwa wanaruka vibaya sana kutoa mshiko ili kuijua hatma yao!

  Unaonaje, mchungaji huyo akikodi ukumbi kisha akawatoza hizo pesa kama KIINGILIO kwenye Semina ya kujua kama jina lako limeandikwa ktk kitabu cha uzima ama la; ukumbi bila shaka utafurika!!! Haahahaha…….

 5. NDUGU WAPENDWA MSIDANGANYIKE HIZO NI ZA MAKUTI, MANYASI NA MAJANI AMBAZO SASAHIVI ZIMECHOMWA MOTO. ATUPE KWANZA AGIZO ALILOPEWA NA MUNGU NDIPO TUTAMUELEWA! HUYO MCHUNGAJI ANATAKIWA KUJUA KWAMBA SASAHIVI WANA WA MUNGU/KANISA TUMEPATA UFAHAMU WA NENO KUPITIA UFUNUO WA ELIYA NABII HATUDANGANYIKI TENA NA DINI NA MADHEHEBU YA MAREHEMU SHETANI. KAMA ANAHITAJI FEDHA ACHUKUE UFUNUO WA KILIMO NA UFUGAJI AENDE SHAMBA AKALITENDEE NENO KAZI NA SIO KUDANGANYA DANGANYA TU. KANISA TUNAYE NABII WA KWELI ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI,ALIYEPEWA AGIZO NA MUNGU MWENYEWE

 6. Huo unaitwa, uchawi mweupe. To hell with him, and the devolish helicopter. Bastard!!!.

 7. Kama ndo hivyo je masikini hatapata wapi namna ya kupata huduma Hii.

  wokovu wetu tunapata bure tena kwa Neema tu name si kwa wingi wa Mali zetu.
  Kikubwa hakuna anayejua jambo hili kuhusu kitabu cha uzima Bali Baba pekee (Mungu).

 8. Bwana asifiwe

  Poleni apa sasa dunia inafika kweli mwisho . Inakuwa tena kulipa pesa juu ya kujuwa kama njina lako imeandikwa Mbinguni ? Apa sasa sio tafauti na wafumu. Mwaminifi wa Bwana wetu YESU KRISTU yeye mwenyewe anajijuwa kama iko na NETWORK na MUNGU wake kufatana na mwenendo lake mbele la MUNGU aliye umba mbingu na dunia .
  NB. Biblia inasema tusikatale roho ya unabii lakini tuchunguze. akuna ndani ya Biblia fasi inasema tulipe pesa juu ya kutazama kama jina letu iko ndani ya kitabu cha Uzima ama tulipe pesa juu ya kupata uponyaji ya kimwili . sio tafauti na BABU wa LOLIONDO Tanzania tuombea wandugu juu ya safari yetu ya kwenda Mbinguni
  Kama nimekosa kusema naomba munisamehe

  ROVA MONGA

 9. mimi niliambiwa bure, na malaika alinipasha habari siku moja akaniambia, waoooooooooooooooooooooooo?” you are among them” watakaokwenda na Bwana. niliamka nikatetemeka dakika tano, nikamshukuru Mungu nikasema asante, na inamaana safari imeiva? hili neno kila wakati lipo kwenye akili linanisumbua sana, nikifikiria kuwa safari imeiva ni dereva tu anasubiriwa.
  ndugu yangu katika kristo unyakuo uu karibu sana kwa jinsi usivyozania. wanaojua kupiga mahesabu wamepiga wanasema tangu Yesu atamke neno la kurudi tena , mahesabu hayo yametimia. lingine ni kuwa yeye ni Mungu kamwe hatakaa aseme uongo kama wanadamu ila ni sisi tu tuyaamini maneno yake na yeye mwenyewe tumwamini.

  lingine nililoona nimeona makaburini watu wakiibukia juu kama uyoga. yaani wakifufuka. hili nalo linanitia woga kuwa yuu karibu kadiri tusivyozania.
  asanteni kuwa mjanja ujiandae uhakikishe tiketi yako itakuja naye.
  mbarikiwe sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s