Mchungaji mwema yukoje?

mchungajii

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote, 

Katika Kitabu cha Yohana 10, kwenye mistari ya 11 na 14, kuna sentensi ya Yesu imejirudia mara 3 inaitwa, ‘’Mimi ndimi Mchungaji Mwema’’. Akili na Moyo wangu ukavutwa kuangalia kwa macho ya nje na ndani kwa nini Yesu kujisema kwa msisitizo mara zote izo kua Yeye ni Mchungaji Mwema! Huyu Mchungaji wa Kondoo Mwema, yukoje-koje? Tutafakari pamoja baadhi ya mistari ya Yohana. 10 

Imeandikwa, 1.Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. 2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. 7 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. 9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. 11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. 13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. 14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; 16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. 28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. 29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

SIFA ZA MCHUNGAJI MWEMA WA KONDOO NI KAMA IFUATAVYO

 

Toka na Ingia yake ktk huduma, inafahamika/ni  wazi sana

Mistari ya 1-2,7-10 Yesu anasema Mchungaji wa kweli, haingilii  hudumani kwa kukwea kupitia njia nyingine bali hupita waziwazi kuingia zizini kuwatoa wakale malisho mema. Mchungaji Mwema wa Kondoo ana ujasiri kwa kusema waziwazi kuhusu wengine wasiofuata utaratibu huo wa kuingia ktk huduma! anasema ni wezi  na wanyang’anyi.Hasiti wala kumung’unya maneno kuwaelezea wale wote wasio kwenda kwa utaratibu huo  kwamba hawafai kazi iyo. Anajitambua huduma yake na hata kujiita Yeye Mchungaji Mwema ndiye haswaa mlango wenyewe wa Kondoo. Kuingia ktk huduma bila kujulikana umetokea wapi, umepitia wapi lakini ghafla tu uko zizini unawachunga Kondoo, ni hatari sana na Mchungaji wa ivyo hapaswi kujiita yeye ni Mchungaji Mwema wa Kondoo, atakua anachunga mambo yake wala si  ya Uhai na hatima njema ya Kondoo

Anamimina moyo wake ktk kujenga Uhusiano na Mafahamiano  na Kondoo

Mistari ya 3-5, 14, 16, 27 Yesu anasema Kondoo wake wanaisikia sauti yake. Kwa maana nyingine wanajuana sana anasema Mwenyewe ivi, ‘nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi! Mpaka sauti za Mchungaji feki mgeni, hawataifuata bali watamkimbia maanake wanauwezo wa kujua sauti ya mgeni ikoje kwa kufahamu kwa hakika ya Bwana wao inafafanaje.. Mchungaji wa aina hii wa Kondoo kumjua kiasi icho lazima atakua na moyo na muda wa kutosha kukaa na Kondoo hata kujenga urafiki na upenzi kiasi icho. Ni pale tu moyo na maisha yake yanapomiminwa kwa ustawi wa Kondoo ndiposa uhusiano na mafahamiano ya dhati na kina yanajengeka kati yao.

Ameyatoa maisha yake kwa ajili ya afya, ulinzi na uzima wa Kondoo

 

Mistari ya 4, 11-13, 17, 28, 29. Anasema Yesu kua anapowatoa Kondoo kuwapeleka malishoni, Yeye huwatangulia-manake kama kuna hatari nje au njiani, itamdhuri kwanza Mchungaji, Kondoo watakua salama. Kisha anasema Yeye anautoa uhai wake kwa ajili ya Kondoo hata Kondoo wanapovamiwa kuliwa, Yeye husimama kidete kuwapigania na si kama Mchungaji wa mshahara tu ambaye hukimbia mbwa mwitu wakitokea maana maswala ya ustawi na ulinzi wa Kondoo si jambo ya kufa na kupona kwake. 

Mchungaji  wa Kondoo ni mojawapo ya huduma wanayoitiwa na kupewa baadhi yetu hata ivyo ziko huduma nyingi kila mtu kapewa kuanzia zile za jumla yaani za kila aliyemwamini mpaka zile maalum kwa kila mmoja, je tunafanania au tunazo sifa kama izo za Mchungaji Mwema YESU tunapotumika? 

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

3 thoughts on “Mchungaji mwema yukoje?

 1. Milinga Juma Venerando,

  This is an interesting and well thought statement man…’ badala ya wao kuwa wachungaji wema wanataka waumini wema, ha ha ha aisee kumbe, ni funny yet sad indeed.

  Bless u kwa inputs ya nguvu,

  Press on

 2. Mpendwa Seleli,

  Siku hizi kumpata mchungaji mwema ni issue. Ukitembea makanisa mengi sana utakutana na wachungaji kibao ambao wao wanatafuta waumini wema badala ya wao kuwa wachungaji wema wanataka waumini wema.

  Waumini wema ni wale wanaotoa sadaka sana. Kama wewe hutoi sadaka sana hauhesabiwi tena katika kundi. Wachungaji wengi siku hizi wanatazama pochi ikoje kwanza. Hata wakikosa pochi nzito nzito wako tayari kuiacha huduma ya kuchunga.

  Wengine wako kama Mzee Robert Mugabe. Yeye pamoja na kwamba nchi inakabiliwa na uchumi kuporomoka yeye anaendelea kuporomosha sherehe kali za birthday yake zikigharimu mamilioni ya dola za kimarekani huku wananchi wakifa njaa na kushindwa kumudu gharama za afya na shule. Ndivyo wachungaji wengi walivyo nyakati hizi. Wako tayari kuishi maisha ya kifahari na kulala nyumba za kifahari na kuvaa kwa anasa na hata kutapanya bila kujali kondoo wao wako kwenye hali gani. Huyageuza makanisa kuwa himaya zao (their spiritutal empires) na hakuna wa kuwatoa wala kuwapindua kwa sababu wanasema wao ndio waliohenyeka sana kwenye maisha magumu wakati huduma zikiwa changa.

  Hali ndivyo ilivyo leo hii kwa sehemu kubwa. Sijui kama bado kuna wachungaji wema wa kondoo siku hizi. Kama wapo, Mungu awabariki milele.

 3. mimi naomba niwe nje ya mada naomba niulize swali nami kwa leo Biblia inasema katika kitabu cha ezekiel kuwa Baba hata chukua uovu mwana wala mwana kuchukua uovu baba ezekiel 18:20 lakini ukisoma vizuli biblia utaona wako watu wengi wamehukumiwa kwa dhambi za watu wengine kwa mfano wana wa israel wakati wanaenda kupigana na watu mji wa ai watu kalibu 3000 walikufa kwa dhambi ya akani aliye chukua vitu vilivyo wekwa wakifu Yoshua 7:1 wakati wa yona yona ndiye aliye kosa kwa kushidwa kutii agizo la Mungu lakini watu wengine wakaangamia kwa kosa la yona na mengine mengi sasa nauliza biblia inajipinga naomba kujibwa kwa maandiko

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s