Mchungaji David Yonggi Cho ahukumiwa kwa ubadilifu!

yong

Mchungaji David Yonggi Cho, 78, mwanzilishi wa kanisa kubwa duniani la Kipentekoste, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kufuja $ milioni 12 fedha za kanisa.

Cho kutoka Korea ya Kusini, mwanzilishi wa Yoido Full Gospel Church, kanisa lililo chini ya Assemblies of God lenye wanachama zaidi ya milioni 1, na kulifanya liwe kanisa lenye kusanyiko kubwa duniani.

Hivi karibuni amekutwa na hatia ya ubadilifu wa kuruhusu viongozi wa kanisa kununua hisa kutoka kwenye kampuni ya mwanawe mkubwa, Cho Hee-Jun, viongozi hao walinunua hisa 250,000 mara nne ya thamani ya soko, kwa mujibu wa taarifa za habari

Shirika la Habari la Yonhap limetangaza kwamba hakimu anaamini Cho lazima aadhibiwe na iwe fundisho kwa wengine, hasa kwa mtu wa hadhi kama yake katika jamii.

Wakati huo huo watumishi wa Mungu kutoka sehemu mbali mbali wamemtetea Mchungaji Cho, kwamba hakujua yote. Wakati wa ushahidi Cho alisema alimwamini kijana wake mkubwa na hakuweza kuangalia na kusoma maelfu ya kurasa za makaratasi, ambayo yalikuwa tayari mbele yake kutiwa saini. Alisaini karatasi. Yeye hajawahi kupokea fedha yoyote kutokana na hizo karatasi.

Advertisements

6 thoughts on “Mchungaji David Yonggi Cho ahukumiwa kwa ubadilifu!

 1. Mteule Shalom,

  Ni kweli Mchungaji David Yonggi Cho alifanya makosa na anastahili kifungo kwani alisaini mkataba ambao hakuusoma wote na kuwaamini viongozi au familia yake kumponza nakubali!

  Nakubali pia anastahili hukumu hiyo ya kifungo. Concern yangu hapa ipo katika maneno haya nanukuu “MAONI YANGU: Kanisa la Mungu linatakiwa kuwa makini kuwasaidia watumishi wa Mungu katika kufanya kazi za Mungu kuwa urahisi kwani makosa yetu kiutendaji yanaweza kuiponza kazi ya Mungu na watumishi wetu kama vile ilivyotokea kwa Mchungaji David Yonggi Cho

  Na kwa viongozi wa makanisa yetu kitendo cha kusaini mikataba ovyo ovyo mara ya mikopo ya riba, mara viwanja vya makanisa mara… tuwe makini sana!”

  Asante,

  Makunzo C.H.M

 2. naamini sheria ni msumeno. kuwa kiongozi wa dini hakumzuii kuhukumiwa kifungo, mradi tu akutwa na hatia.

 3. Shalom,

  Wapenzi wangu katika Kristo mimi ni mmojawapo wa wasomaji wa wakubwa wa mafundisho ya mtumishi wa Mungu Mchungaji David Yonggi Cho, mwanzilishi wa kanisa kubwa duniani la Kipentekoste, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela ati kwa kosa la kufuja $ milioni 12 fedha za kanisa.

  Kama kweli tu wapenzi wa Yesu Kristo tumwombee na kuiombea kazi kubwa ya kanisa ambayo ameifanya Duniani kama mtumishi mwaminifu wa Mungu. Kazi ya uharibifu huu imefanywa na shetani ili kudhoofisha kazi ya Mungu nchini Korea na duniani lote.

  Inaonekana kwamba kosa lipo zaidi kiutawala siyo kiroho kwa maana ya kukiuka taratibu za kikanisa. Kiongozi wa kanisa kubwa kama hilo duniani anatakiwa kuwa na wasaidizi makini wanaoweza kumsaidia katika maswala ya kisheria au kiutawala

  Mtumishi wa Mungu Mchungaji David Yonggi Cho kaponzwa na mtendaji wake kwani alimwamini kijana wake mkubwa na hakuweza kuangalia na kusoma maelfu ya kurasa za makaratasi, ambazo zilikuwa tayari mbele yake kutiwa saini. Alisaini karatasi kwa kujua mambo yote ni sawa kumbe sivyo lakini yeye hajawahi kupokea fedha yoyote kutokana na hizo karatasi.

  MAONI YANGU: Kanisa la Mungu linatakiwa kuwa makini kuwasaidia watumishi wa Mungu katika kufanya kazi za Mungu kuwa urahisi kwani makosa yetu kiutendaji yanaweza kuiponza kazi ya Mungu na watumishi wetu kama vile ilivyotokea kwa Mchungaji David Yonggi Cho. Na kwa viongozi wa makanisa yetu kitendo cha kusaini mikataba ovyo ovyo mara ya mikopo ya riba, mara viwanja vya makanisa mara… tuwe makini sana!

  Naliomba kanisa lote duniani limwombee na kuiombea kazi ya Mungu nchini Korea na kwingineko duniani.

  Mzee Makunzo C.H.M.

 4. Sijui kwa nini nimesoma hii habari, da! Pastor Y. Cho kabisaa Mtu wa Mungu mzuri na Kaka yetu tunayempenda sana, sana ktk imani na utumishi uliotukuka! Inauma na imenisitua sana, ni kama siamini nilichosoma kwa kweli, oooh my God, such great true man of God kwenda jela!, Historia, impact ya utumishi wake S.Korea na maeneo mengine Nje ya Korea Kusini na heshima alioyonayo-maana Mtu akinitumikia, Baba yangu atamuheshimu- ktk Kingdom of God kwa kufanya interests za Baba kwanza-KUINUA JINA LA YESU na kuchunga Kondoo wa Bwana, huwezi amini kama haya yanamtokea brother huyu in Christ maskini wa Mungu, dah! jamani, hii dunian hii, kweli kuna dhiki ziwe man or devo made, zote dhiki tu.

  Nakuomba Mungu Baba mtie nguvu na ewe RM mnong’oneze Mtumishi wako how to go about or accommodate such time as this, Amen

  Press on

 5. Du hii ni huzuni sana kwa jamii ya waamini. Nimekuwa nikifuatilia mafundisho ya huyu mchungaji kwa muda mrefu na kwa kweli ameitwa na Mungu kuifanya kazi yake. Shuhuda zake na mafundisho yake ni ya kipekee. Hili la kufungwa kwa kweli ni huzuni. Mungu mwenyewe anajua ukweli na way forward

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s