Sabato Matengenezo!

matengeezo

Baada ya Sabato Masalia kusikika miaka kadhaa iliyopita sasa kuna kundi jingine linaloingia kwa kasi nchini, likianzia mikoani, linaitwa Sabato Matengenezo, Je kuna anayejua zaidi kuhusu hawa? wanaamini nini?

–AK

Advertisements

41 thoughts on “Sabato Matengenezo!

 1. Kwa sasa hakuna dhehebu lolote ambalo ni kanisa la kweli la Mungu! Hakuna dhehebu lolote ambalo linamtumikia Mungu pekee!

  Yote yameasi kutoka kwa Mungu na kuanguka.

  Lakini kanisa la kweli la Mungu ni watu wanaompenda Mungu na kuzishika amri zake zote na shuhuda (Isa 8:20; Ufu. 12:17) Maana kwa hakika walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina la Yesu, kama ni watiifu kwa amri na shuhuda zake. Yeye u hapo pamoja nao. Hao ndio wanaunda kanisa maana uwepo wake aliye Mkuu (Yesu) u pamoja nao. Kwa maelezo zaidi bofya hapa: http://www.sabbathlight.wordpress.com

 2. Nafikiri wote mna kiasi fulani cha ukweli. kinachotakiwa ni kijifunza ukweli wote

 3. lwembe,

  Kwani,ndugu yangu,wewe unapokosea neno la Mungu siku unapolijua kwa ufasaha unafanyaje? Unaiacha imani au unapiga moyo konde na kusonga mbele?

  Kwa kifupi, kama ilivyo leo,nuru mpya inaponizukia siwezi kata tamaa bali nainuka na kusonga mbele kwa imani.!

  Tambua jambo ili, mama wa makahaba ameendelea kujivunia vitoto vyake na kuvinywesha mvinyo wa ghadhabu yake.heshimuni mamlaka ya Mungu sio mapokeo ya wanadamu ndugu zangu.

  Kejeli zako haziwezi shinda ukweli wa neno la Mungu, kamwe! Hakuna cha santuri wala zomari,uo ndio ukweli! Sabato ya siku ya saba ikikuwepo tangu tarehe 7\1\1 KK. Na itakuwepo ktk mbingu mpya na nchi mpya! Uo ndio ukweli, maoteo mengne, niya kishetani na hayapaswi kukumbukwa na kutukuzwa kamwe!

  Kumbuka, amri za Mungu niza milele,ikiwemo amri ya Nne-sabato,na kwakuivunja iyo moja, itakugharimu umilele km asemavyo yakobo.! Ushahidi kuwa amri ya nne niya milele, ni ..”… Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi.. Na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja KUABUDU mbele zake.”isa66:25. Siku ya ibada ni sabato hata sabato.! Rafiki unataka ushaidi upi zaidi ya huo!

  Acha ukengeufu kumtukuza mnyama! Fuata neno la Mungu rafiki,utaangamia!

  Nasubiri porojo zako za kimapokeo!

 4. Mjema,
  Tatizo lako, unafanya conclusion ya jambo la jana ktk giza la leo ili kulihalalisha leo kwa kisingizio kilicho nje hata ya nuru ya leo unayoangaziwa; unapenda giza enhe?!

  Hivi wewe kwa mawazo yako, ukiwa umekwisha kuuamini huo uongo uliobuniwa kuficha hiyo disappointment ya kufeli kwa unabii huo; unadhani kwamba ungeishi ktk hizo siku za kutengeneza mbawa na kupanda huko mlimani ili mruke muondoke kwenda kumlaki Kristo mawinguni, wewe kweli usingekuwa mmoja wao???

  Kama usingekuwa mmoja wao, hebu nipe vigezo ambavyo vingekufanya usiwe pamoja na hao nduguzo ktk kituko hicho cha karne!

  **Kuhusu sabato, najua hapo ndipo santuri ilipokwamia, vuta subira, tutapapiga msasa pawe safi ili wimbo huo umalizikie ktk Kristo huyo Bwana wa Sabato, uijue na maana hiyo ya kuwa Bwana wa Sabato ktk jambo zima lihusulo kumwabudu yeye aliye Bwana wa hiyo Sabato!!

  Hayo unayotaka nikupatie “aya”, vuta subira nitakupatia vyooote, labda uvikatae mwenyewe tu!

 5. Lwembe,

  Ipo siku utajua ukweli ni upi!Ninachomuomba Mungu, usiwe umechelewa!

  Lwembe, tumeshakwambia, 1.Sabato ilikuwepo tangu mwanzo na mwanzilishi ni Mungu,mwanzo2:1-4.

  2.Mungu alifundisha watoto wake kuikumbuka na kuitakasa sabato na ili kusisitiza ni Amri ya Nne,Kut20:8-11

  3.Yesu alitunza sabato, Luk4:16, na yeye ni Bwana wa Sabato.

  4.wakati wa Yesu wanafunzi walitunza sabato, Luk23:50-54.

  N.B-Siku ya sabato ni Jumamosi-Luk23:50+ na 24:1+

  5.baada ya Yesu kanisa la mitume walitunza,sabato Mdo17:17

  N.B:ni kati ya kipindi cha kanisa la mitume na zama za giza ndipo ibada za jumapili ziliandaliwa na kupewa kibali na wanadamu-dogma-hakuna ushaidi wa maandiko kuwa Mungu ameridhiria amri yake ya Nne kubadilishwa.

  6.mbinguni tutaivnza sabato yaani siku ya saba. isaya66:25.

  7.wakatoliki ktk vitabu vyao e.g kateksimo wanakiri kuwa wao ndio walioibadili amri ya nne na wanajisifu kuwa iyo,iyo,hasa ndio “alama ya mamlaka yao” na wote waifuatao hakuna cha uprotestanti,bali vifaranga vyao.

  Na, kwa taarifa yako, behind the scheme “nyuma ya pazia” ipo mikakati kemkem inayokaribia kupevuka ambapo madhehebu ya dini za jumapili,budha,hindu n.k wameshakubali kuacha tofauti zao na kurudi chini ya bwawa za yule mtawala mkuu,apewaye nguvu na yule joka!! Kazi kwenu!

  Lwembe, uwe Muungwana kuhukumu. ni wapi hapo kwenye izo aya umeona mkono wa katoliki! tatizo lako unapambana na Wasabato bila kujali kuwa unapambana na Amri ya Mungu!!

  Haya, na wewe thibitisha kuwa wasabato ni watoto wa katoliki. Hapo juu nimeonyesha aya zinazopinga uongo wako na walimu wako.!

  Kaka, Mungu ameruhusu magugu na ngano vikuwe pamoja,siku zote ktk umma wake, wapo wanaodhoofisha ukweli,kufanya vihoja,na ivyo huwezi kudai kuwa kwa hao , kundi zima halifai!

  Unapojibu zingatia hasa, iyo sabato mnayoipinga ! Mtaikva mbinguni! Isaya66:25. Km umeikataa hii hapa duniani ambayo ni kivuli ya ile ya mbinguni,kaka utafika kweli.

  Karibu.

  Tafadhali leta aya zinazoonyesha kuwa kuna kuikumbuka kuwa

 6. Mjema,

  Hivi, Uongo wa Kisabato na Uongo wa Kikatoliki kuhusu Ibada kufanywa siku ya Jumapili, una tofauti gani?

  Mimi naona shina lake ni moja, ndio maana nina amini kwamba Usabato ni mtoto wa Katoliki aliyebuniwa ili kuwachanganya Waprotestant!!!

  Mlipowakatia kamba Wakatoliki, mkawa mnaelea bila nanga, mkawageukia na kuanza kuwashambulia mpaka majuzi walipofanikiwa “kuwatia mkononi”; na mkaelekezwa msimamishe machapisho yenye kuitusi Katoliki, na mliyonayo muyaharibu; wenzenu wote wametii bado ninyi tu mnaoendelea na mambo hayo mafichoni!!!

  Mjema, huko hakuna uzima, hata wewe mwenyewe, kwa akili iliyo safi kabisa, umekiri kwamba mko sawa na yule aliyebandika mabango stendi akitangaza mwisho wa dunia!!!!!

  Kaka, watu huwa wanakufa, lakini roho hazifi, shetani anaendelea kuwadandia watu wa dini, haswa Cults, ili kuendeleza vituko, kwa nia ya kuifedhehesha Injili; ndio kama hao wa mabango, akina Miller, Sabato Matengenezo, Sabato Masalia, Sabato Hakuna Wokovu, …nk….. mpaka mwisho wa dahari ni vituko tu!!!!

  Amos, usichoke, mahepe ndio yanayokuonesha jinsi Neema ilivyokujifadhi ktk wokovu hata usichezewe na mapepo ya dini!!

  Gbu!

 7. Amos,

  Uanashangaa tukio la Mwaka 1843 kwa Wasabato unajisahaulisha matukio yenu Wajumapili kumpangia Yesu tarehe za kurudi!! Tena wengne walibandika mabango stend ya Ubungo-Dar Es Salaam, mbona iyo hauisemei.

  Aidha,unasema wasabato mafundisho yetu manyonge kwa suala hili la kukosea unabii halafu unajisahaulisha kuwa Wajumapili wanahialifu\vunja kwa makusudi Amri ya Nne kuhusu sabato kwa kufuata Mapokeo ya Kanisa la Roma.ambapo hasa ndio mafundisho manyonge,kuvunja amri za Mungu kwa kufuata maagizo ya wanadamu ambao hadi leo wanajigamba kuwa Jumapili ni alama ya mamlaka yao-waroma!!haya ndio mafundisho manyonge hasa kwani yanaishi hadi leo na mnayaadhimisha! Usijisahaulishe kaka upande hasi wa huko ulipo.!

  Ubarikiwe

 8. wasabato tumechoka na mafundisho yenu manyonge yaliyo jengwa ktk misingi ya uwongo mlitazamishwa na William miller kwamba ifikapo tarehe 21/4/1843 Yesu angelud kwa mara ya pili kuwachukuen

 9. Edwin,

  Nakusubiri ujibu comments zangu za tarehe 15/03/2014 at 10:17 AM part I na tarehe: 15/03/2014 at 1:08 PM na tarehe, 18/03/2014 at 07:46 AM.

  Usisingizie kuwa Sungura hameshajibu. Hajatoa jibu lolote. Kwani wewe huna akili yako mpaka usaidiwe. Jibu tafadhali.

  Nasubiri

 10. sungura,

  Kwa kuwa umekuja kiwokovu zaidi, naomba tujibizane kwny post yake, wokovu halafu matendo. hapa tuache mambo ya sabato matengenezo maana najua hii issue ya wokovu itakuwa ndefu.angalia huko.

  Tafadhali jibu maswali yangu juu ya amri za Mungu za Mungu na hasa ya Nne-sabato mnayotakiwa kufanya matengenezo.

  Twende huko: Wokovu halafu Matendo post

 11. Mjema,

  Hata maamuma anaweza kwa wazi kabisa kukucheka kuwa umetengeneza jibu ambalo linaelea hewani, na la uongo!

  Neno mchakato umelitoa wapi, kama si magumashi ya uongo uliojazwa na walimu wako?

  Mimi wala sijakuuliza mambo ya kusamehewa dhambi na kutolewa mapepo.

  Kinachokutesa ni ujinga juu ya maana ya neno ‘wokovu’ au kuokoka.
  Kama ambavyo Siyi aliamua kukataa maana halisi ya wenye lugha yao ya neno wokovu (Sodzo au Soteria), akaamua kusema kuwa kila mtu abaki kama anavyoamini. Lakini ukweli ni kwamba aliamua kukataa kwa nguvu.

  Mjema hiyo mistari haijasema ‘saa ya mchakato wa wokovu ni sasa’

  Niambie na wewe maana ya kuokoka unayoijua, ili tujue kama kuwepo kwa shetani kunamaanisha kuwa wokovu haupo sasa hivi.

  Halafu umesema habari za kurithi uzima wa milele hapo baadae. Hebu niambie ya uzima wa milele ni nini

  Nangoja!

 12. Sungura,
  Kwanza, kukutajataja rafiki, mara nyingine hutokea tu automatically. Si unajua kwa mtu unayempenda sana. Kumtaja huja tu. Nina imani hata Mjema anakutajeni sana kwa sababu, hataki kwenda mbinguni peke yake. Anataka kwenda na akina Sungura, Lwembe, Seleli na wanaSG wote. Kwa hiyo usipate shida kutajwatajwa na wajoli wa Bwana, maadamu wanakutaja kwa nia njema ya kukutaka kuja kuishi na wewe milele mbinguni. Uwe na amani sana kaka.
  Pili, aya yako ya maandiko, haina maana ya salvation ile ya “eternity” . Ina maana ya kuponywa kwa mtu wakati wa taabu yake. Haina maana ya kuondolewa duniani. Hasha!! Ukilichukulia neno salvation kila mahali lilipotokea kuwa lina maanisha eternity, utakosea kweli rafiki. Mungu anatunusuru na hatari za ibilisi kila siku. Na kwa mantiki hiyo, mtu akisema Mungu amemwokoa na hatari hizo, yuko sahihi kabisa. Lakini ukitumia maana hiyo ya kuokolewa kutoka kwenye hatari ni sawa na ile kuokolewa kuuingia umilele, tutakucheka mpaka asubuhi.
  Kwa sasa, tukisema kuwa tumeokoka kwa maana ile ya eternity, Mungu atatushangaa sana. Tena kama ni kutuhoji, angetuhoji kwa kutuuliza, kuwa, “kama mlishaokoka tayari mkiwa duniani, bado mnamhitaji Mwanangu-Kristo kuja awaokoe tena”? Sijui wewe ungejibuje!!
  Sungura kipenzi, ni rahisi sana kama utatofautisha mambo haya badala ya kung’ang’ana na mambo ambayo kimsingi unayajua ila hutaki kuyasadiki.

  Kuhusu mimi kutoijua kazi ya Kristo pale msalabani, huenda ni kweli sijaijua vizuri ndiyo maana nazidi kujifunza kila siku. Lakini huwezi kukifahamu kile alichokifanya Kristo pale msalabani bila ya kukifahamu kile kilichokuwa kinamwakilisha kabla ya YEYE kudhihirishwa. Ili ufahamu kwa marefu na mapana maana ya kafara ya Kristo msalabani, hauna budi kujua taratibu/sheria za kafara kwa undani zaidi. Hata mimi Siyi bado sijazifahamu zote. Naendelea kujifunza. Na ndizo zinazonionyesha mawanda na mipaka ya kile alichokifanya Kristo pale msalabani. Ndiyo maana sisi -wasabato, hatubahatishi ktk suala zima la imani. Kwa upendo wote, tunakuombea tu.
  Ubarikiwe na Bwana

 13. Sungura,

  Baada ya kufafanua juu ya wokovu km ulivyouliza kuhusu 2Kor6:2. Nimerudi tena kuhusu amri za Mungu unazozipuuza.

  Ukweli ni huu kwenu, wapentekoste, si kwamba hamfuati sheria /amri la hasha. Ninavyojua, Amri za Mungu km zilivyo ktk Kutoka20 mnazisika zote isipokuwa moja ile ya nne tena na yenyewe ni sehem ya pili tu ambayo hamshiki.Na ni kwasababu bahati mbaya sana amri iyo imefanya tofauti kati yetu ndio maana mnasema sisi ni washika sheria.ole wenu!

  Rafiki ujumbe wa Yakobo2:10, unawasonda kidole, ni ujanja wa ibilisi kuwa mshike sheria yote na mpuuzie moja tu ili iwagharimu uzima wa milele.(it will cost you eternally).

  Hapo juu nimetoa mtiririko wa utuzaji sabato-amri ya nne kuanzia, Edeni-waisrael-Yesu-Mitume-Leo-Mbingu mpya na nchi mpya iweje leo muikatae iyo kweli na kuendeleza mamlaka ya RC!

  Ona Sungura, mbinguni watu watatunza sabato Isaya 66:22, iweje leo tuipuuze! wapentekesto mnatakiwa kufanya matengenezo kwa hili. Na nina wapendekezea hivi: sio mpaka muwe Wa adventista Wasabato ndio muitunze amri ya Nne, la hasha, itiini amri ya nne ya sabato ya siku ya saba-jumamosi huku mkiendelea kuwa wapentekoste na mising yenu ya imani.

  Umedai kuwa sisi tunajua sana sheria zaidi ya kumjua Yesu.

  Kwani Sungura, kumjua Yesu au kuwa na uzoefu na Yesu ni kupi kama sio Kumpenda. kwani wewe hujui kumpenda ni kuzishika amri zake. Yoha14:15, na anaesema anamjua Yesu km wewe sungura ila azishiki amri zake ni mwongo. Wewe unataka watu wamjueje Yesu km sio kumpenda kwa kushika amri zake.

  Sungura, unajua ninyi walokole mnasumbuliwa na utapia mlo wa kiroho. uwezi sema mdomo tu ” Nimeokoka Nampenda Yesu” kama ushiki amri zake! Ni ukweli mmoja kuwa tunaokolewa kwa neema ya Yesu ILA pia ni ukweli mwingine pia tutahukumiwa kwa sheria ya uhuru Yak2:12. Haya mawili Neema na Sheria ni pande mbili za shilingi ile ile. Neema ya Yesu inatuwezesha kushika sheria/ yaani inatufundisha kukataa uovu,dhambi, uasi ambayo ndio sheria hiyo.

  Yohana 1 : 17. “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” na Yesu hakuja kutangua torati. yote haya uenda pamoja.

  Wokovu bwerere mnaoudai ninyi ni bandia na msipofanya matengenezo mtaishia hapa hapa.

  Hivi Sungura, utaukataaje ukweli huu wa Neno la Mungu:

  1.Isaya 8:20″ na waenende kwa sheria na ushuhuda, ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili bila shaka kwa hao hapana asubuhi”

  2.Mhu12:13 “hii ndiyo jumla ya maneno yote yamekwisha sikiwa, Mche Mungu , nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu”

  3. Yoh14:15″mkinipenda mtazishika amri zangu”

  4. Yesu aliulizwa, nifanyeje nipate kuurithi uzima wa milele/yaani kuokoka? Akajibu, “Wazijua Amri…”

  5. Yak2:12-” semeni ninyi na kutenda kama watu mtakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru”

  6. 1Yoh5:3″ kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu kwamba tuzishike amri zake”

  7. Wale wanaomshubisi Yesu wanaambiwa hivi,”hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na Imani ya Yesu”Ufunuo14:12.

  Fanya matengenezo rafiki. acha na wokovu bandia unaoipuuza sheria ya kristo.

 14. sungura,

  Wewe na wenzako hao tunao wataja yenu wote mamoja tu.ndo maana twawataja. Mbona hata nyie mwafanyaga ivyo?

  Kuhusu 2kor6:2- kwani ina tatizo gani, umekuwa ukitukumbushia kweli ukidhani kuna la maana kweli.

  Maana yake ni kwamba, kuingia kwenye mchakato: Wokovu= kuhesabiwa haki+kutakaswa+kutukuka kwa mpasa mtu kuanzisha mausiano mapya na yesu mara asikiapo habari za Yesu leo/sasa kwani kuhairisha kuanza mchakato huo ni hatari kwani hatuna uhakika wa kesho as mauti imbele yetu.

  Na mtu huyo anapoanza kuingia ktk mchakato huo yupo vitani hivyo yampasa kuvumilia hata mwisho ktk vita hvyo vya kiroho na kuilinda imani inayojaribiwa ndipo mchakato huo wa wokovu utakamilika!

  Vivyo, hv hata kina zakayo alipoambiwa hakika leo wokovu umefika nyumbani kwake, au jamii ya kanisa la awali iliongezeka kwa wale waliokuwa wanaokolewa kila siku Mdo2:47, ni kwamba waliingia kwenye mchakato, kwanza, kuhesabiwa haki, pili, kuendelea kutakaswa , tatu, kusubiri kutukuka. Kama hauamini soma aya za rejea za matukio hayo utapata maana ya kuokoka.

  Sungura, ihnlihali dhambi na adui shetani wangalipo, tena ananguruma km simba akitafuta mtu ammeze, tena ana hasira na kanisa na uzao wake, hatuwezi kudai kuwa tumeokoka hapa duniani kwa mtazamo wa uzima wa milele, huko ni kujidanganya. Merits/Manufaa ya kuwa pamoja na Yesu na hvyo kutuponya magonjwa sio kuokoka kwani wapo watakatifu wa Mungu watakufa kwa magonjwa na ulemavu ila wataurithi uzima wa milele.

  Pia ,kusamehewa dhambi na kutolewa pepo uo ndio utakaso km tunavyoonyesha kuwa ni hatua ya pili baada ya kuhesabiwa haki!

  Pamoja

 15. Mjema,

  Kwa nini unapojibu hoja ya Lwembe au Seleli unanijumlisha na mimi lakini ndani ya hoja zako hakuna hata neno moja linalonihusu, au unajisikia tu vizuri kukaa unamtaja Seleli, Lwembe na Sungura?

  Hata Siyi pia, nakushangaa kunitaja mimi wakati unajibu hoja za Lwembe na Seleli. Wewe beba furushi lako mwenyewe, usirukeruke.

  Mimi nimewaulizeni tu swali dogo kuhusu wokovu lile la (2 Cor 6: 2 For he says, “In the time of my favor I heard you, and in the day of salvation I helped you.” I tell you, now is the time of God’s favor, now is the day of salvation – NIV)

  Niambieni hiyo mistari inamhusu nani?

  Halafu Syi, unaniambia mimi na Edwin kuwa tutakufa kibudu, this funny indeed, kwamba mfu anawaambia walio na uzima wa milele kuwa watakufa kibudu!!

  Siyi unajua wewe una ufahamu mkubwa wa torati ya Musa kuliko unavyomjua mwokozi Yesu Kristo. Mindset yako iko so deep kwenye torati, na iko very shallow kuhusu kazi ya Kristo!

  Jililieni wenyewe!

 16. William Mjema, waingizaji watakuwepo, lakini nawalioanza vibaya toka mwanzo nao wapo. Yesu alikuja kuleta badiliko la maisha basi. Muigizaji atajitahidi saana hataweza, nasisitiza HATAWEZA na ndio maana hata wasanii huishia majukwaani na baadae huendelea na maisha halisi. Yamesemwa mengi sitaki kuyarudia maamuzi huwa yanabaki kuwa ya mtu, cha muhimu ni kujulishwa ukweli na maisha yanaendelea.

 17. Lwembe,
  Ha ha ha haa!!
  Sasa yaelekea na wewe umeanza kuchoka!! Hivi Ellen G. White alisema nini ambacho akina Siyi na Mjema hatuwezi kukijibu? Hebu kilete hapa tukione na tukiri kuwa kweli hatuwezi!!.
  mimi nataka nikupe changamoto ya kufikiri kidogo. kafara za wanyama katika agano la kale, zilimwakilisha Kristo. Je, sheria na mtukio yanayohusiana na sheria za Maadili (Amri 10), zenyewe ziliwakilisha nini? Jaribu kujibu in refence ya safari ya waizrael jangwani, Sanduku la Agano linpoibiwa, nini kilikuwa kinatokea, Watu wanapotaka hata kuvuka mto, Sanduku liliwekwa wapi na kwa nini nk.
  Halafu jaribu kuangalia kilio cha leo duniani – tz, wanasema maadili yametpotea. Kwa nini hawasema maadili yalipotea/yaliishia pale pindi Yesu alipokufa msalanbani? Kama sheria za maadili hazipo, kwa nini mnalalamika mabinti na vijana wetu wa kiume wanapotembea nusu uchi??

  Seleli naye kama mtoto tu!! Sungura naye walewale!! Mtakufa kibudu marafiki zangu. Msipojibidisha kujifunza kile TU alichokifanya Yesu pale msalabani, mtaendelea vilevile kwenye hilo ombwe na mtapotea hakika. Poleni

 18. Siyi & Mjema,

  Mnasema hamuelewi!
  Yaani kwamba hamuelewi, ndio mmeelewa jinsi ambavyo hakuna linaloeleweka ktk imani yenu!!!
  Mjema, record iliyokwama huwa haifiki mwisho! Na jambo lisilo na mwisho halifai kuanza kujifunza maana utakuwa unapoteza muda wako bure, hapo litakapokuacha njia panda usijue kwa kwenda.

  Kubaki ktk Sheria ni utovu wa adabu unaostahili adhabu. Na pia ni kielelezo cha hali mbaya mliyonayo kiasi kwamba mmekosa ufahamu kabisa wa kazi ya Msalaba, tena ni uhakika wa ninyi kuwa sealed outside the Kingdom upon your own confession mlipo ukataa Wokovu mliokirimiwa kwa kuupeleka huko mbele msikokujua!

  Nimewaambia kuwa ninyi ni sawa na santuri iliyokwama kutokana na kukosa kwenu uwezo wa kuyatafakari hata mambo historical. Hata huko nyuma nimewahi kuwaambia kuwa by all standards ninyi ni chombo cha wakatoliki cha kueneza uongo wao, ila hamjui kuwa mnatumika ktk jinsi hiyo. Mungu kwa kuwajua kimbele ndio akawaorodhesha pamoja ktk ile list ya wenye mafundisho ya kishetani, akianza na Wakatoliki wenye kuzuia watu wasioe na kumaliza na ninyi wenye kuwazuia watu vyakula, hili si bahati mbaya bali ni uhalisi wa hali!

  Kuhusu nabii Ellen White, ninyi wenyewe ni mashahidi wa hali yenu, kwamba hamjui leo hii mumpe cheo gani. Mlikwisha kumuita nabii, lakini maswali yanayojitokeza kuhusu unabii wake ni mengi na hamnayo majibu ya kujitosheleza kuhusu hilo kiasi kwamba inakuwa ni rahisi hata kwa kipofu wa kiroho kutambua kwamba huyo hakuwa nabii aliyesimamishwa na Mungu kama mnavyotaka kuwaaminisha watu; ndipo ili kulificha jambo hilo, ninawasikia mkimwita “Mwana Matengenezo”!

  Wana Matengenezo ni akina Luther, aliyekuja na Kuhesabiwa Haki, na kisha Wesley aliyekuja na Neno la Utakaso juu ya hao waliohesabiwa Haki. Ni katika haya yamefanyika hayo Matengenezo kwa Kanisa, wakisogezwa huko mbele kuisogelea Taji. Ninachoweza kuwaambia kuhusu hayo matengenezo mnayompachika White, huyu alileta Uharibifu kwa Kanisa, akiwatoa ktk kuhesabiwa haki na kutakaswa kwao, akawarudisha matopeni huko kwenye Sheria akiwarudisha ktk laana walimotolewa! Nao mzunguko wa Mauti kundi hilo waliomo ndio haya mambo ya Sabato Masalia, Sabato Matengenezo vikijizaa kutoka humo humo.

  Basi ingawa haya ninayoyaeleza nilikwisha kuyaeleza sana huko nyuma, nitayarudia tena kujibu huo mkwamo wenu wa ufahamu mpaka santuri itoboke!!!

  Vuteni subira kidogo nitayarishe utenzi wa kuyajibu hayo ya uongo wa Katoliki kuhusu huyo kipenzi chenu Constantine, mliyemsoma ktk Katekesimu na kuuamini uongo huo mpaka mko tayari kupotea kwa ujinga huo kuliko kuyaamini Maandiko yanayowaonesha kuwa kanisa ktk kuzaliwa kwake walikuwa wakikutana siku ya kwanza ya juma! Its a pathetic condition!!!

  Bwana na awape subira!

 19. Mjema/Siyi,

  Mjema, Umemjibu Lwembe eti…”’ Nimemuuliza Edwin makusudi kabisa maeneo yote anayo wapondea wasabato ili tuyaweke sawa. Kama kuna rejea yoyote kuwa mliwahi kujibu/kujadili niliyouliza hapa….”’

  Unataka nikujibu na mimi tena? nini sasa wakati Sungura kashamaliza kazi? Yaani wewe bwana unapenda sana kurudia rudia mambo, mada nk, sasa una nondo gani umeuliza so huge Sungura ameshindwa kujibu?

  Unataka nikujibu yapi unadhani Sungura hajayajibu moja kwa moja au kuyagusia remotely yet perfectly? haya yatate hapa nitayashukia mara moja. Karibu

  Siyi na wewe umekuja hapa tulipofika? Una shida gani? sema tatizo au hoja yako kisha tutainywaaaaa haraka kwa serious drinking Water, ayaa karibu na wewe.

  Press on

 20. Edwin/Sungura/Lwembe,

  Naona uo ukweli hapo juu hakuna wa kuupinga kwani ni wiki sasa wewe na akina edwin,lwembe mpo kimyaaa. Inaonekana mmeelewa. Mtakapoongoka waimarishe na wengne. Msiuonee aya ukweli ufuateni

  Ushauri: sio lazima muwe wasabato, cha kufanya ni kumpa Mungu siku yake-Jumamosi ili muwe mmekamilika ktk sheria yote. Endeleeni kuwa wapentekoste mnaosali siku ya sabato_jumamosi mtakuwa mmeitii na amri ya nne.wala sio suala la dini hapa, ni suala la AMRI YA NNE km ilivyoandikwa kwa mkono wa Mungu, Kutoka 20:8-11.

  Pia kumbukeni haya:

  i) kuvunja sheria moja kunatosha kuwanyima uzima wa milele, Yakobo2:9-11

  ii) mbinguni wote tuta kuja mbele za BWANA kuabudu sabato hata sabato. Isaya 66:22-23

  Leo pia nina haya ya kusema,

  Ipo hivi, ni kawaida ya shetani kuigiza vitu halisi katika hali ya ubandia/kudharaulika ili watu wavidharau vitu halisi. Kwa maneno mengne, uleta imani bandia kutoka ktk imani halisi ili watu wadharau imani halisi.

  Mmekuwa mkitupondea juu ya waigizaji wa sabato walioibuka km ifuatavyo:

  1.Wasabato Masalia- kutaka kwenda uarabuni kwa ndege kutangaza injili bila nauli .

  2. Wasabato Matengenezo-wanaokataza kwenda shule na hospitali.

  Hawa wote ni waigizaji. Wasabato halisi wanaitwa:

  -Wa adventista Wasabato-ambao ujumbe wao mkuu ni kutangaza ujumbe wa malaika watatu kama unavyowekwa wazi kwenye, Ufunuo14:6-12.

  Jina lenyewe, Wa adventista Wasabato linamaana:

  Wa adventista- wana marejeo ya kuja kwa Yesu mara pili

  Sabato-Siku ya Saba. Km sehem muhmu kukumbusha Amri ya nne iliyotiwa mikono.

  Edwin/Sungura, hebu nikupe na hivi vionjo vilivyowahi kutokea kwa walokole halafu utajua nina maana gani,

  1.habari gani ya wale walokole waiojifungia ndani ya kanisa wakijifungia wakimshubiri Yesu kisha kanisa/jengo likatiwa moto.!!

  2.vipi kuhusu wale walioripotiwa hapa SG kuwa mchungaji wao aliwalisha majani km ng’ombe!!

  3. Vipi kuhusu yule Mch. huko kenya anayewachaji watu pesa ili awaangalizie km majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima,

  Je, hv sio vituko ktk imani zenu.? Unafikiri wasio wa imani iyo wanaposikia wataichukuliaje hizo imani?

  Hivyo, hakuna haja ya kukosoa imani halisi kwa ujinga na upuuzi wa waigizaji wachache tu. imani halisi zikosolewe kwa mapokeo au mapungufu yake tu yasiyoendana na Neno la Mungu.

  Hebu nikupe home work hii

  1.unafikiri kwa nini wasio wakristo wana kejeli/fanyia mizaha ujio wa Yesu?

  -mfano: utawasikia vijana vijiweni wanasema,” acha uongo wewe, unakuwa muongo kama Yesu, amewadanganya wafuasi wake hadi leo hajasudi” AU utawasikia wengne wanasema, ” yesu harudi, amekula nauli huyo”.

  Hebu tupeane uelewa mtumishi.

  Karibu

 21. Mjema,
  Mimi naona umesema mambo mengi sana mtumishi wa Bwana. Yote ni keys kwa ajili ya wokovu wa mtu. Najua umewakamata ile mbaya akina Seleli na hoja zao za kizushi za kujidai wao wana RM na sisi hatuna. Habari za sabato na historia ya uvunjaji wake uliofanywa na Rumi, umeuweka vyema. Nina imani akina Seleli, Sungura, Lwembe, Yusha, Nelson, Haule, na wengine wote watakuwa wameelewa vyema habari za ukweli wa mafundisho ya wasabato. Lililobaki ni kwao sasa kuamua kusuka ama kunyoa.
  Na kwa habari ya wasabato matengenezo, wasijidai hawajui kitu. Nina imani wanajua sana. Nawatia moyo wasome historia za maisha ya mitume enzi zao wakihubiri injili ya Kristo. Kuna wazushi wengine waliokuwa wanaibuka (kwa majina ya mitume) kwa makusudi kabisa ili kuitia dosari injili ya mitume. Na waliwapakazia mengi sana mitume. Hilo liko wazi sana kwenye historia ya kanisa. Ukisema ukweli tupu, daima tarajia mamluki wa yule adui kukupakizia kwa mabaya, naam zaidi ya mabaya unayofikiri. Lengo lao likiwa ni kukuhafifisha, kuchafua, na kuharibu tu sifa za wasabato. Lakini pamoja na hayo, Mungu alizidi kujiinua kupitia mitume. Hata walipoamua kuwaua mitume, ndipo idadi ya waumini ilipoongezeka zaidi.
  Mateso na mauaji yaliyowapata mitume, yalipanda mbegu njema za watu kuwaleta kwa Yesu. Ukiwa na njia ya kiimani iliyo tambarare tu, jiulize sana. Hauko salama. Njia ya kwenda mbinguni, imejaa vikwazo lukuki naam, vikwazo kutoka nje ya kanisa, na hata ndani ya kanisa. Jitahidini sana wapendwa.
  Bwana awabariki sana

 22. Sungura/Lwembe,

  nyesha wapi tulipokosea, kwani wewe nani amekwambia neno la Mungu alirudiwi.

  Lwembe, ni mara ngapi ulipokwenda kanisani mhubiri alitoa somo ulilowahi kulisikia kabla. je ulitoka nje au uliendelea kusikiliza? Uliliona jipya au lilikuwa vile. Nimwemuliza Edwin makusudi kabisa maeneo yote anayo wapondea wasabato ili tuyaweke sawa. Kama kuna rejea yoyote kuwa mliwahi kujibu/kujadili niliyouliza hapa, si kazi ni rahisi kwenu, unachofanya ni copy-paste tu.

  Kama alivyoshauri siyi, acha kucheka tu. Weka wazi huko kujirudia kwa santuri.

 23. Lwembe,
  Sijaelewa uichoongea hapa kaka. Maana umecheeeka tu na kuzungumzazungumza pasi na kueleweka. tafadhari be brief bro.

 24. Sungura/Mjema,

  Hahahahaha..! Unajua santuri inapokwama inachokifanya? Huwa inajirusha nyuma na kuanza kuimba ikijirudia rudia bila ufahamu, maana haina uwezo wa kuendelea mbele!!!

  Basi hata wimbo ukiwa ni “wokovu”, huwa unaanza vizuri kabisa, “Yesu alikufa msalabani, ili atulipie deni yetu ya dhambi, akatuokoa tupate Uzima wa milele…” ikisogea mbele kidogo tu, hujirusha huko nyuma ya wakati na kuanza kuimba madude yasiyoeleweka: Moral laws, Sabato Matengenezo, Ceremonial laws, Creation Sabbath, Sabato Masalia, Sabato Muhuri wa Mungu, na mwisho inajirusha ktk lile Shimo reeeeeeeefu ikiimba chorus ya “HAKUNA WOKOVU DUNIANI!!!!” Hahahahahahahaha…..!!!

 25. Mjema,

  Kama unataka kujua kuwa kuokoka ni mpaka wakati ukifa jikumbushe tu huu mstari(2 Cor 6: 2 For he says, “In the time of my favor I heard you, and in the day of salvation I helped you.” I tell you, now is the time of God’s favor, now is the day of salvation – NIV)

  Wewe endelea kusubiri mpaka ukifa!

 26. Mjema,

  Zimeisha hoja za kuchangia kuhusu wasabato matengenezo?
  Maana naona umerukia mada nyingine ya wokovu, ambayo kimsingi iko na uwanja wake katika hii blog. Usituchanganye bwana kwa maneno mengiiii yasiyo hata na substance ndani yake. Wewe eleza kuhusu wasbabto wenzako.

  Hamjaanza leo kutuletea mkanganyiko wa mambo ninyi wasabato, kuna maiaka fulani ya tisini mlikesha milimani mkimsubiri Yesu. Sijui nani aliwadanganya. Inaonekana imani yenu ni ya kubahatisha.

  Maswali yenyewe unayouliza kuhusu wokovu ni kindagateni, na tumeyajibu sana wakati tunajadili mada ya wokovu. Kurudia kuuliza maswali yaleyale kwa namna ileile ni uchanga mkubwa sana kiimani.

  Tafadhali, hapa jadili wasababto matengenezo, wala siyo suala kuokoka.

  Ishu ya kuoka nilishawaambia mie, kuwa kama mmeamua kutokutaka kuelewa na kukubali kuwa wokovu ni sasa, subirini siku mnayoingoja halafu mtaona kitakachotokea.

  Usituletee mchanganyo.

 27. Edwin,

  Kabla haujajibu commemts zangu za leo, tafadhali jibu zilizotangulia- naona kimya bila shaka unaandaa jibu lililoshiba!

  Naomba ufafanue tuhuma zifuatazo juu ya ufu unaosema upo kwa wasabato!

  1.umesema wasabato hawana RM? Umetumia vigezo vipi kutujaji? Kwani mtu mwenye RM anajulikanaje/unamtambuaje?

  2.umedai ibada(kuomba na kutafakari neno) zetu ni mfu, ibada hai zikoje?

  3.hivi Yesu alipokuja duniani alikuwa ameokoka kwa kipindi chote cha maisha Yake tangu alipozaliwa au kuna siku ilifika ndio akasema ameokoka, je ni lini?

  4.mnaposema wokovu hapa duniani (yaani kabla mtu ajafa na/hajakwenda mbinguni) kwa maana ya kuponnywa magonjwa au ulemavu, vipi kuhusu wale walio pamoja nanyi ila ikatokea wakafa kwa HIV ,MALARIA au ugonjwa mwingne wowote ule, mfano paulo, Je, watakuwa ?hawajaokoka.

  -katika mjadala wa ndoa zenye migogoro, mmoja wenu(wewe au sungura) aliwahi kutoa mfano mhubiri maarufu Pr.Benn.. Kuwa alikosa hekima hadi ndoa yake ikavunjika, Je, kwa dhana ya kuokoka, Pr.Benn., hajaokoka?uoni kwa pigo ilo inaonyesha sio sahihi kusema umeokoka?

  -vipi kuhusu wale walio nje ambao mnawashabikia kuwa ndoa zao poa tu? Wameokoa au la?

  5.kuhusu kusamehewa dhambi au kutolewa pepo kua ni kuokoka! Vipi wale ambao si walokole-hawajampokea Kristo ila hawana pepo wameokoka?
  5.Ni fundisho lipi la E.G.White ambalo lipo kinyume na Neno la Mungu-Biblia.
  Zingatia: wito wa kuzijaribu hz roho, auhusisi kuangalia jinsia,rangi,utaifa wala mapungufu ya mwili bali hali zao za kiroho kwa mujibu wa Neno la Mungu!

  Zingatia: Sio Wasabato wote wanaosema hakuna wokovu hapa duniani! Wapo baadhi wanamtazamo finyu km nyie kuwa ni sahihi kusema Tumeokoka!

  -Hii ni mada ya kujadili ili kupata uelewa wa pamoja-concesus.

  Nitabarikiwa ukirespondi kila swali hapo juu kwa ushaidi wa maandiko.

  Asante Mtumishi.

 28. …. Inaendelea,

  Edwin,

  Part II,

  Nadhan umepata picha halisi kuwa ili watu wa Mungu waokoke kwa maana ya kwenda mbinguni(sio hapa duniani) ni lazima “wazishike amri” zote, na kwa kupuuzia hata moja itawagharimu eternally.

  -pia umejua wasabato kuwa wanasisitiza juu ya kushika Amri zote ikiwemo ya Nne.-sabato ambayo kwa kuwa nyie hamishiki ndio mnatukejeli, ushaidi hapdn juu kuwa amri iyo ya nne imefuatwa na vizazi vyote agano la kale na jipya na pia itakuwa hvyo hata mbinguni wanadamu wote watakwenda kuabudu mbele za Mungu, huu ni ukweli halisi wa biblia usio na shaka na hivyo God-given.

  -sasa nataka nikuonyeshe jinsi inavyokugeukia kuwa nyie wajumapili mafundisho yenu ndio mfu/mapokeo/man-made kma ifuatavyo,

  Historia inaönyesha kuwa, ni mtawala mmoja mpangani kwa interest za kisiasa ndiye aliye timiza unabii wa Dan7:25 na Isa24:5.

  Mwaka 321BK, mtawala huyu kwa jina Constantino, aliazimia kupata umaarufu wa kisiasa ktk himaya yake, lakini utawala wake ulikuwa na changamoto ya kutoelewana kati ya wakristo na wapagani,

  Mtawala uyo akapata wazo, kuwa Wakristo waliabudi siku ya saba- Jumamosi na wapangani waliokuwa na ibada zao siku ya kwanza ya Juma-jumapili jambo lililowafanya wajione tofauti na hvy kujenga uadui kati yao.

  -Lakini pia alijua kuwa wakristo ufurahia kufufuka kwa Bwana na Mwokozi wao Yesu Kristo siku ya kwanza-Jumapili.

  Hivyo, mtawala/mwanasiasa huyu mwenye uchu wa madaraka aliona mwanya wa kuingilia. Akauza wazo lake kwa Wakristo kuwa, kwanini wasiihamishe ibada kutoka Siku ya Saba-Jumamosi,(iliyokuwa kumbukumbu ya uumbaji) kwenda siku ya Kwanza-Jumapili,(inayoonyesha kumbu kumbu ya ukombozi).

  Kwa kushirikiana na viongozi wa kanisa , waliyafanya mabadiliko hayo pole pole, kwa miongo kadhaa ambapo wacha Mungu waliiadhmisha siku1 sambamba na siku7. Kwa kufanya ivyo mwanasiasa uyo alipata umaarufu na kujipanulia sana utawala wake.

  Wapagani akiwemo na yeye mwenyewe, constitantino walijiunga na kanisa lakini wakiwa hawajaongoka kweli kweli. Wapagani hao waliingiza ibada zao kanisani mfano, ibada ya sanamu,wafu, n.k

  Hivyo, hatimaye, mwaka 321BK, tamko rasim lilitolewa huku likiipuuza amri ya nne-sabato ya siku7 na kuamuru wote ibada ya siku1. Na hivyo ili watu wasije kujua ukweli, walipigwa marufuku kusoma biblia ikawa ni kazi ya viongozi tu.

  -hata hvyo wapo wachache waliokataa na kusimama katka neno la Mungu na kuendelea kuitunza sabato.

  Edwin, is that God-given or man-made?

  -na hvyo hadi leo kanisa katoliki linajivunia ndio walioanzisha ibada ya siku1 na hvyo alama ya mamlaka yake. edwin unabisha?

  Edwin, wanamatengenezo akiwemo Dr. M.Luther walichatika kufanya sehemu v ya matengenezo.hakupata kujua kuhusu sabato. Na km kweli nanyi niwa protestant from RC, ni wito kuacha kufuata alama yao Juma2 na mfuate sabato ya Bwana-Jumamosi.

  Hivyo tokeni huko kwny mapokeo ya kibinadam/man made/mfu na mfuate Amri ya Nne km zilivyo Amri nyingne.

  Ikiwa unabisha kuwa imani yenu sio mfu, nipe andiko hata moja linaloonyesha siku1 ni ya kweli na mabadiliko hayo Mungu ameyakubali.

  -Umedai Wasabato wanakataza kumcha Mungu, shutuma ya uongo.ikiwa tunasisitiza Watu wamtii Mungu kwa kufuata sheria zake ndo kusemaje huko?

  Kuhusu E.G.White umetoa points feki kweli. Badala ya kuonyesha udhaifu wa kazi zake alizo zifanya wewe unarusha shutuma zako kwenye mtu kama mtu na mapungufu yake ya kimwili.umesahau mambo yafuatayo:

  1. Mungu amewachagua watu dhaifu kufanya nao kazi 1kor1:26-31. 2kor12:9-10. Siku zote Mungu ufanya kazi na wanyonge kwa sababu wao ni wanyekevu kwake

  2. Ungeisoma historia yake vizuri umjue kwanza kabla ya kumkosoa. inaonekana haujui kuwa E.G.White naye alikuwa wa madhebu ya jumapili kama wewe ila alipoijua kweli aliifuata.

  3.umesema mitume na manabii walishapita wasasa ni matapeli tu.

  -Ni wapi umesoma kuwa nyakati zetu hakuta kuwa na manabii na kuwa kipindi chao kimepita? Mbona biblia inasema yeye RM umpa yeyote km apendavyo 1kor12:4-11. Pia mbona paulo anatutaka tuzidai sana hzo karama ikiwemo unabii na mitume 1kor12:28-31. Wewe unaposema kuwa kipindi chao kilishapita uoni unapotosha.

  -ikiwa E.G.white umwamini kwa kuwa ametokea baada ya hawa mitume wa biblia, vipi kuhusu hawa mitume na manabii wenu wa leo wanaojitangaza mpaka kwny vyombo vya habari nao pia hauwaamini?

  Habari ndo iyo, Wasabato wana iman hai itakayo wapawa uzima wa milele, na nyie mtabakia na mtazamo wenu finyu-wa wokovu hapa duniani na mtaishia hapa hapa duniani. Lakini wapo wengi huko watatoka kama E.G.white kuja huku kwa Bwana kupata Wokovu halisi.

  Tafadhali ukija, njoo kimaandiko acha blaa blaa hapa.

  Barikiwa.

 29. Edwin,

  Part I,

  Asante kuniweka wazi juu ya mtazamo wako juu ya ufu wa imani na mafundisho ya Wasabato. Naona unaweza kuwa msaada kwangu na wengne.

  Hapa naona umetaja baadhi ya imani unazodai zinaifanya iman iwe mfu, ingawa hujatoa andiko kusapoti. Sasa hebu tutumie maandiko kuona ukweli ni upi!?

  Nanukuu sehemu -a- ya jibu lako1 umesema hv: “Ni mfu kwa
  kua haina msisitizo
  ktk mambo ya
  msingi ya Imani ili
  mtu afike mbinguni
  kama KUOKOKA KTK YESU hapa duniani
  na kuanza kuishi
  maisha ya uchaji
  hata kufanyiwa na
  Miungu
  yanayopaswa kufanyiwa
  aliyefanya uamuzi
  wa kumwamini
  Yesu kwa maana ya
  kuokoka, badala
  yake mnasisitiza mambo kama
  kushika siku na
  majira mambo
  ambayo Paul
  aliyanyuka kabisa
  maana alikua akipambana na
  wasabato wa enzi
  zile kama
  tunavyowanyuka
  ninyi wa leo”. Mwisho wa kunukuu,

  Hoja1- umesema wasabato hatusisitizi mambo ya msingi watu kufika mbinguni!!

  Swali la kujiuliza, hayo mambo ya msingi ili mtu afike mbinguni ni yapi? Ndio huko kuokoka hapa duniani au? Biblia inasemaje?

  Hebu tuache maneno makavu tu, tumsikilize Mungu, twende kazi,

  Luka-18 :18 Tena, mtu mkubwa
  mmoja alimwuliza,
  akisema, Mwalimu
  mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?

  Unakumbuka Yesu alijibuje? Msisitizo wa Yesu ili mtu afike mbingu alimwelekeza afanyeje?

  Ingekuwa ni hawa akina edwin angejibu/angesisitiza hv, “ili uende mbinguni okoka kwanza hapa duniani!!!”. na ndivyo kweli mnavyosisitiza.

  Hebu tuone Yesu alisisitiza nini na Je kati ya Wasabato na Wapentekoste km Edwin ni akina nani wanasisitiza iliyo kweli,

  Yesu alijibu hivi: Luka18:20 ” wazijua amri, usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako. 21.akasema, hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu..”.

  Umeona edwin, Yesu hapa anasisitiza kushika amri wakati nyie mnasisitiza kuokoka hapa duniani na ni kawaida yenu kuzikataa amri za Mungu ikiwemo Amri ya Nne kukusu Sabato.

  Sisi hatusisitizi juu ya siku bali juu ya Amri ya Nne na ukweli huu umejengeka juu ya neno la Mungu kama ifuatavyo:

  1.Unabii umetabiri kuwa ipo mamlaka itakayobadili Amri za Mungu Daniel7:25-“naye atanena kinyume chake aliye juu…. Naye ATAAZIMU KUBADILI MAJIRA NA SHERIA…” Pia soma,

  Isaya24:5-“tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa, kwa maana wameziasi sheria, WAMEIBADILI AMRI, wamelivunja agano la milele.
  -umeuona unabii uo.-

  Pia, Yesu alipomjibu yule aliyemuliza kuwa afanye nini apate kuingia mbinguni, yule mv alijibu kuwa ayo yote aliyashika tangu utoto. ila Yesu alimwambia amepungukiwa na jambo moja Luka18:22.Ambalö ni ubinafsi.

  Wanafunzi wakajiuliza, Luk18:26-“nao waliposikia
  Walisema, ni nani basi awezaye KUOKOKA? Ivyo nao walielewa wøkovu sio lelemama km nyie mnavyourahisisha. Wokovu na sheria yote havitengani.

  2.biblia inasema ukikosa kwa sheria moja umekosa juu ya yote . Yak2:10-12. Kwa iyo nyie, wapentekoste pia hamjaokoka mmepungukiwa jambo moja, Amri ya Nne. Twende uone jinsi ilivyo kweli,
  Edwin, Jambo mnalokosea ni kusema kuwa wasabato wanasisitiza juu ya siku, uongo mtupu. wasabato hawasisitizi juu ya siku, bali juu ya amri ya nne na sio siku kinachotokea ni kwa sababu tu amri yenyewe inahusu siku na inayoweka tofauti kati ya man-made na God-Given.utaelewa tu ninamaana gani punde!.

  Umeöna Edwin ni akina nani wanamafundisho mfu kati ya Wasabato vs Wajumapili? Km bado twende.

  Nakupongeza kukubali ukweli kuwa mafundisho mfu ni yale yasiyoendana na Neno la Mungu au kwa maneno mengne ni mapokeo tu ya Wanadamu.

  Sasa hebu tuone kati ya Wasabato na Nyie ni akina nani wanafuata maneno ya Mungu vs mapokeo ya wanadamu ( God given vs Man made doctrines).

  Amri ya Nne-kufanya kazi siku6 za juma na kumpa Mungu siku moja ya Saba-Jumamosi.

  Ushahidi:

  1.Sabato / siku ya saba ilitengwa maalum na Mungu hata kabla ya mwanadamu kuasi pale Eden- Mwanzo2:1-3.

  2.Mungu alilipa Taifa la teule Amri ikiwemo ya siku ya saba km siku ya mapumziko. Kutoka 20:8-11.

  3. Yesu aliitunza Sabato ya siku ya Saba na ilikuwa ni desturi yake kufanya hivyo alipoishi nasi ktk Mwili Luka4:16.

  -pia Yesu ni Bwana wasabato. math12:8 na sabato ilifanyika kwa ajili ya wanadamu, Mark2:27-28.

  4.Baada ya kifo cha Yesu siku ya sita(leo mnaiita ijumaa kuu)-ambayo biblia inasema siku iyo ni maandalio ya sabato, wanafunzi wa Yesu walimaliza mambo yote na siku ya saba-Jumamosi walistarehe kama ILIVYOAMRIWA, Luka23:50-56. Na siku ya kwanza-Jumapili Yesu alifufuka, Luka24:1+.

  5.Baada ya Yesu kwenda mbinguni Wanafunzi waliendelea kuitunza Sabato akiwemo na Paulo unaesema amewanyuka wasabato. Uongo Edwin, Paulo aliitunza Sabato, na Biblia inasema ilikuwa ni Desturi yake, Matendo17:2.sijui hoja ya paulo kutoitunza sabato wewe umeitoa wapi!? Mapokeo ayo wapendwa.

  Na cha ajabu zaidi hata watakaokwenda mbinguni wataitunza sabato,

  Isaya66:23- ” Na itakuwa mwezi Mpya hata mwezi mpya, na SABATO HATA SABATO, WANADAMU WOTE WATAKUJA KUABUDU MBELE ZANGU ASEMA BWANA”.
  Edwin, umeona neno la Mungu lilivyojieleza, iyo ni God-given.

  Nitarudi nikuonye yenu ilivyo historically paganic man-made from constantinopole halafu hapo mtajaji ni nani ambao mafundisho yao mfu/man made kati ya wasabato Vs kina Edwin.

  ……inaendelea…

 30. Mjema,

  Ni kweli umeona vema kua ninatakaa sana kukosoa na kuvunja imani potofu si tu ya sabato na nyingine nyingi mfu. Usijitwalie credit kua ni kwa kua unasema/sabato inasema kweli ndio maana mnapingwa na kukusolewa, si kweli, hamna KWELI bali kusambaza dini ya kuzimu-isiyo na uhai

  Umeniomba/uliza haya….

  1. Kwa nini wewe na wenzako mnadai wasabato wani imani na mafundisho mfu? Onyesha hapa SG ufu uo ?! Zingatia: Imani Mfu au Mafundisho mafu ni yale yasioenda sambamba na neno la Mungu.

  JIBU: Ni mfu kwa kua haina msisitizo ktk mambo ya msingi ya Imani ili mtu afike mbinguni kama KUOKOKA KTK YESU hapa duniani na kuanza kuishi maisha ya uchaji hata kufanyiwa na Miungu yanayopaswa kufanyiwa aliyefanya uamuzi wa kumwamini Yesu kwa maana ya kuokoka, badala yake mnasisitiza mambo kama kushika siku na majira mambo ambayo Paul aliyanyuka kabisa maana alikua akipambana na wasabato wa enzi zile kama tunavyowanyuka ninyi wa leo.

  Ni ukweli mmoja kua mafundisho/imani mfu ni ile iliyo kinyume na Neno but ni ukweli wa pili mzito zaidi kua ufu unakuja pale ambapo Neno la Mungu halikai au linakaa but linatumika bila hekima yote..Col.3:16 au isivyo halali. 2Timo.2:15-swala si tu kujua maandiko na kuyakariri maana andiko huua bali ni kuyajua na kuyatumia ktk uongozi wa Roho-hekima yote na kihalali-quality ya kujua maandiko na kuyatumia ktk hekima yote na kihalali haipatikani nje ya Roho Mtakatufu ambaye huja na kumjaza Mtu akiyemwamini Yesu tu-ALIYEOKOKA kwa ivyo sitashanga kukuona unavyopwaya ktk kuyatumia au hata kuyaelewa ya Mungu kupitia Neno lake na namna tunavyo appy.

  2. Kwa nini uwa mnamkejeli, kumtania, kumfanyia mizaha mtumishi wa Mungu E.G.White na mafundisho au mafunuo aliyoyapata ?

  JIBU! Kwa kua Neno limesema tumejengwa juu ya Mitume na Manabii na hao wanafahamika, wanaongezeka baada ya hapo ni wezi na wanyang’anyi ivyo waliyosema, ota, ona, funuliwa, jifunulia ni batili na upuuuuzi maana wengine possibly kabisa ni magonjwa tu ya degedege kama si kifafa au kupagawa tu na evil spirits kuliko wakumba kisha wakatoa maneno wakiwa ktk comma izo za demons na bahati mbaya sana sasa yanatukuzwa waliyosema hata kuzidi yaliyosemwa na kutendwa na Mitume na Manabii originali wenyewe, huo ni uhuni na wafanyayo hayo ni matapeli wa imani tu an wafu indeed.

  Umesema ivi..”Nitafurahi kaka ukinifungua kwenye hatari iyo km ipo na kufuata, kilicho chema zaidi”….Kwa hakika sasa UMEFUNGUKA, fungukaaaaa in JESUS name, ng’ooka uko ktk ufu mkali na makaburi ya imani za kale-Mafarisayo zilizopinga Wokovu wa Yesu toka past to date, na wewe shamefully, sadly, gravely and frustratingly, ni mmoja wa leo.

  Press on

 31. John Haule,

  Tunashukuru kutupa iyo link. nimeisoma iyo habari. nilifikiri ni chokochoko kwa kanisa la Mungu la Wa adventista Wasabato-Seventh Day Adventist Church kwa kile kinachoendelea kuhusu Uhamsho na Matengenezo-Revival & Reformation kumbe la. ni vijiwatu 6 vilivyojichokea kiimani huko kigoma eti wanakataza watu kwenda shule na hospitali wanapo ugua. Lo, imani za ajabu kweli. safi sana serikali tia ndani wote, chapa viboko hadi waonyeshe iyo iman ya kijinga wametoa wapi kwenye Biblia?!

  -Pia nashukuru mwandishi amewekabayana kuwa wameona wajitenge na kanisa lao la awali Wa adventista wasabato-SDA, baada ya kuona njozi zao zipo nje ya Imani za 28 za msingi ya Wa adventista Wasabato.

  -pia napenda kuwakumbusha hao watu wa sabato matengenezo yafuatayo kinyume na imani waliyoianzisha Biblia inasema,

  1. “Mkamate sana Elimu,usimwache aende zake, mshike maana yeye ni uzima wako” Mith4:11

  -ndugu zangu 6, mliotiwa ndani huko kigoma, hamjaongoza na RM kuleta imani ya ajabu km iyo inayopingana na neno lake. Nyie mmesahau kuwa hata nguo nzuri mnazovaa,nyumba mnazokaa,chakula mlacho,usafiri mtumiao, mawasiliana mfanyayo n.k yote hayo ni matunda ya elimu. Pia mmesahau Mungu anataka tuwe na afya njema ili tumtumikie? Ona sasa ujinga wenu umepelekea kupoteza watoto2. Kwa hili mjue kabisa ninyi niwauaji na mnapaswa kufanya toba kwa kuua.

  2.1Tim4:1″Roho anena wazi wazi ya kwamba, nyakati za mwisho wemgne watajitenga na imani.,” 1Tim4:1 mbona unabii unatimia kwenu. Ole wake yule mtu atimizaye unabii.Tubuni na mrejee ili dhambi zenu zifutwe.

  3. Kama ni uchache wa Waumini wa Kanisa la Mungu huko kigoma ndio umewafanya mmeguke,acheni hofu , kwani wewe hujui, njia ya kwenda uzimani ni nyembamba na wawezaokuipita ni wachache? math7:14 au mumesahau kuwa hata ukiwa wawili au watatu mkikusanyika kwa jina lake yeye yupo kati yenu? math18:20

  4. Ikiwa ni imani kuwa kuja kwa Yesu kumekaribia sana, ni kweli, ila maandalizi kwetu sio kuacha shughuli zetu za kila siku bali 1.tuache dhambi Uf14:6-7 2. Siku ya kuja kwake inaarakishwa kwa kuhubiri Neno kwa watu wote math24:14

  -WanaSG nawasihi msije kulidharau kanisa la wa adventista wasabato kwa matukio km vile, sabato masalia au hawa sabato matengenezo.nawahaidi nitawajia tena mujue kinachoendelea katka kanisa la Wa adventisa wasabato ulimwenguni kuhusu matengenezo vs uongo/ubandia/uigizaji wake unaopelekea kanisa la Mungu kudharaulika kwa njia moja au nyingne. -Tuombeane

  Barikiwa.

 32. Edwin,

  Pamoja na hamu uliyonayo kuhusu Wasabato Vs Matengenezo. Ninachokiana kwako ni kutaka kukosoa tu imani ya wasabato.sijui wamekukoseni wapi? ila hata sishangai ukisema ukweli, ukiutetea na kusimama ktk huo uwezi kupendwa. Yesu pia alitabiri ilo.

  Edwin,kabla hatujaendelea sana, Nikuombe Jambo moja, kupitia post hii naomba uweke bayana mambo yafuatayo,

  1. Kwa nini wewe na wenzako mnadai wasabato wani imani na mafundisho mfu? Onyesha hapa SG ufu uo ?! Zingatia: Imani Mfu au Mafundisho mafu ni yale yasioenda sambamba na neno la Mungu.

  2. Kwa nini uwa mnamkejeli, kumtania, kumfanyia mizaha mtumishi wa Mungu E.G.White na mafundisho au mafunuo aliyoyapata ?

  Nitafurahi kaka ukinifungua kwenye hatari iyo km ipo na kufuata, kilicho chema zaidi.

  Nakusubiri.

 33. WE JE,HUJUI KAMA HIZI NI SIKU ZA MWISHO NA NI KIPINDI CHA MANABII WA UONGO?.MUNGU NA AKUFUNULIE ILI UWEZE KUYATAMBUA HAYA!!!!!!!!!!!!
  SOMA HII MISTARI ILI UWEZE KUFAHAMU!!!!!.
  Matthew 7:15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

  Matthew 24:11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.

  Matthew 24:24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

  Mark 13:22 kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.

  2Petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.

  1yohana 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

 34. Mjema,

  Na mimi ni hamu kuona na kusoma utakayomwagiga hapa kuhusu matatizo aya ya dini mfu zisizo na uhai wa Mungu ktk mambo yao yote iwe ibada, kutafakari Neno, kicho, uwepo na udhihirisho wa nguvu za Mungu, ishara na maajabu na Kujazwa RM na na Yeye kuongea nao ktk maisha yao kuwaongoza ktk mambo kadhaa/mbalimbali.

  Kama kundi hili litakua na rutuba hizo za kiroho, nitabarikiwa sana na kama ni mambo mafu, maono na mafunuo kisha mafuniko ya akina dada kama Ellen waliokua wagonjwa kama si kupagawa na some certain spirits kisha kutoa maono as if ni toka kwa Mungu na watu kuyakubali/kumeza mazimamazima kwa kua tu bahati mbaya ground yao pia haikua na uhai wa Mungu na Roho wake kuwawezesha kupambanua, nitasikitika sana na ofcoz kuyanyuka mbaya maelezo yoyote ya kuhalalisha ufu huo wa kundi hili jipya kama litakua na mambo mafu ayo.

  Aya Karibu, usimbane unprofitably AK, we toa nondo zako ujuayo kuhusu Kundi hili kisha source atakupa later kama ni deal ya maaaanaaa anyway.

  Press on

 35. Mjema c uweke mambo hadharani kwa kile unachokifahamu?maana 2naweza kaa muda kumsubiri AK wakati wewe unafahamu ukweli wake?jiachie 2 mjoli wa Bwana.

 36. AK,

  Habari unayoieleza inaweza kuwa ya kweli kwa namna moja ila jinsi ulivyoileta hapa SG naona inawezekana imepotoshwa AU imetiwa munyu!?! Hasa pale unaposema “wanatokea mikoani” pia ukiwahusianisha na wasabato masalia wa miaka ya miaka michache iliopita.

  Labda kabla sijawapa ukweli ninaoufahamu mimi kuhusu Matengenezo Vs Wasabato,tumuulize AK,amepata wapi hii habari?,toka chanzo gani,gazeti,redio,tv ,au mtandao gani? Wanatokea mikoa gani? Au umesikia sikia tu vijiweni?

  AK, nakusubiri, naona kina Yusha na Lwembe, wana hamu kujua. Fanya hima. tupo kwa ajili yenu.

  Ubarikiwe unapokuja fasta

 37. Bwana asifiwe

  Ndugu katika Bwana niko na swali juu ya Mahana ya jina iyi POST TENEBRAS LUX inamahanisha nini ?

 38. Ndugu zangu Siyi , Lenda, Nashon, Mjema na wengineo wapendwa,

  Njooni basi na maelezo mazuri ya kundi hili la wapendwa, tuna hamu sana ya kuyajua hayo waliyonayo, maana huwezi kujua, inawezekana wakawa na ufunuo wa mwisho wa kutuingiza nanihii!!!

  Mbarikiwe!!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s