Kwa watu wa Mungu!

mwilii

Watu wa Mungu, ashukuriwe Mungu atupaye uzima na ya kwamba tu hai tena kwa neema yake.

Tunalo la kujivunia lakini si katika miili hii tuliyo nayo bali kwa kuwa tumeipata neema ya Jehova.

Ndugu wapendwa imetupasa kuwa na juhudi sana kuzidi sana katika kulijua Neno la Mungu ili tuwe na hakika na ushindi katika hatari nyingi za dunia.

Maana ”dunia” inasema inayo mazuri, lakini si mbele za Mungu, maana ifahamike hivi; yaliyo yote mazuri duniani ni yaliyo mabaya mbele za Mungu na yaliyo mabaya mbele za Mungu ni yaliyo mazuri kwa duniani, basi kila mtu na asema na akili yake mwenyewe.

Kwa hali hiyo basi; sisi tulio kwa Mungu sawa sawa twajua hivi, kheri uongo wa Mungu kuliko ukweli wa dunia, maana ikiwa kwa uongo huo wa Mungu sisi tu hai rohoni tukiiponya miili hii, basi una faida gani ukweli wa dunia ambao kwa huo tumehitirafiana sisi kwa sisi?

Nasema tena ikiwa kwa uongo huo wa Mungu hatukuwa wazinifu, naam hatujawa walawiti, hatujawa waasherati, hatujawa wafiraji, je si zaidi basi ya huo ukweli wa dunia ambao katika huo tu wanafiki?

Mwaonaje ninyi,
Maana si kwamba hatuoni ama hatusomi alama za kuenenda kwetu na kuishi kwetu maana kila mmoja wetu yu barozi na shahidi wa nyendo zake mwenyewe, jifunzeni katika hili.

Sikia yupo mmoja aweza sema amemaliza kwa sababu ya huu tuuitao wokovu lakini asijue ya kwamba yu apaswa kutambua wokovu ni mbegu iishiyo katika tunda bovu ambalo ni mwili wake mwenyewe.

Maana miili ni kikwazo sana katika maisha ya kuuishia haki, maana tumeokoka ndiyo lakini hatujaihama miili hii.

–Mwamfupe Anyisile

Advertisements

3 thoughts on “Kwa watu wa Mungu!

  1. Asifiwe Mungu kwa kuniongoza nifikiye kwenye malengo haya ambayo mme yataja hapo, na Mungu anisamehe kwa kutotimiza malengo yake kwangu, mimi ninauweka mwili wangu kuwa mchovu sana hata kanisani ninashindwa hata kwenda mara utasikiya nimechoka ila naomba Mungu anisaidiye na anisamehe sababu ninakuja kujikuta ninakuwa mtu wa matatizo chungu nzima ,aksante kwa yote umetenda kwangu.

  2. Na Kubaliana na mtumishi Kwani milli yetu ndiyo adui namba moja wa mtu wa Mungu. Wala si shetani aliye adui namba moja. Shetani ukimkemea atakukimbia. Lakini mwili wako hauwezi kukuacha. Lazima kila mtu ajue namna ya kuushinda mwili wake (1Thes 4:1-4-7).

    Mtume paul alilalamika “jambo Zuri ninalotaka kulifanya najikuta siwezi. Lakini jambo baya nisilotaka kulifanya, ndilo najikuta nimelifanya. Ole wangu Mimi. Nani ataniokoa na MWILI huu wa mauti. (Rum 7:15-25). Anaelekeza wazi kwamba adui wa kwanza ni mwili jamani.

    Ndiyo maana anatuonyesha kwamba, yeye mwenyewe, “… kila siku ninautesa (ninaushughulikia) mwili wangu; nisije wahubiri wengine halafu Mimi mwenyewe nikawa mtu wa kukataliwa.” (1Kor 9:27).

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s