33 thoughts on “Ujumbe kutoka kwa Mungu kwenda kwa Rais Kikwete – Askofu Kakobe

 1. Nyie Wakristo mnaofikiri suluhisho la Tanzania ni chama kingine kutawala hembu soma hii hapa chini, uone ambavyo wanasiasa wengi nia yao ni kutaka tu kukubalika kwa watu hata kama wataleta sera au jambo la kuwaangamiza wananchi kiroho hata kimwili:

  Wednesday, February 5, 2014
  CHADEMA kuhalalisha gongo
  Na Pascal Buyaga,MUSOMA
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amesisitiza kwamba kama chama hicho kitashika hatamu za dola, kitahalalisha pombe ya kienyeji aina ya gongo.
  Alirejea kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mukendo manispaa ya Musoma katika operesheni ya M4C pamoja daima.
  Alisema wananchi wamekuwa wakikamatwa kwa kupika pombe aina ya gongo na kuitwa haramu licha ya kuwaingizia kipato wananchi, hivyo CHADEMA inakusudia kuiboresha pombe hiyo kwa kuagiza mitambo ya kisasa.
  “Wasomi,mawaziri na kada nyengine mbalimbali wengi wetu tumesomeshwa kwa fedha za gongo, mama zetu na baba zetu wamekuwa wakipika kwa kificho, kwa nini tuendelee kuiita haramu,” alihoji.
  Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamesema kauli hiyo inaashiria jinsi CHADEMA kinavyojaribu kuchochea unywaji pombe na kudhoofisha nguvu kazi za vijana.

  WAKRISTO AMKENI, silaha yetu ni INJILI YA YESU KRISTO sio siasa za wanasiasa wanaotaka kujaza matumbo yao kwa ulaghai. TUHUBIRI INJILI YA YESU WATU WAFANYWE VIUMBE VIPYA. Wanasiasa wanahitaji kumjua Mungu, watamjuaje Mungu kama sisi wateule tunashindwa kujua suluhisho lipo kwenye Injili ya Yesu tu?
  NIMEUKUMBUKA ULE WIMBO UPO NYIMBO ZA INJILI(TAG/EAGT) USEMAO : “ENEZA HABARI, HUMU DUNIANI ….(ENEZA HABARI – INJILI YA YESU….” TUHUBIRI KWA BIDII MPAKA HAWA VIONGOZI WA SIASA WAOKOKE NDIPO PENYE USALAMA KWA TAIFA HILI!

 2. Mimi ni Mkristo ninayesali katika madhehebu ya Kipentekoste. Ila kwa kweli sikifurahishwa na unabii huu maana haujakaa vizuri Kibiblia. Wapi Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake kuwalaani wale wanaowatendea mabaya? wapi mitume walitufundisha kuwalaani wale wanaotutendea mabaya?
  Mathayo 5:44 – 45
  44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
  45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

  Warumi 12:14
  14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

  Kwanini tunawalaani viongozi wa CCM? Je, kweli ndivyo Neno linavyotufundisha kuwalaani watu badala ya kuwabariki na kudumu kuwaombea?

  Kwani hata chama kingine kikitawala hao watawala wake ni malaika? je, si watu kama hao hao walio CCM ambao pia wanahitaji msaada wa Mungu? unafikiri shida iliyopo ni ya kichama? SHIDA TULIYO NAYO NI WATU/Watumishi wote WABADILIKE NDANI YA MIOYO YAO, WAWE NA HOFU YA MUNGU!
  Sasa watu watapataje hofu ya Mungu kama na sisi wapentekoste tunakuwa kama mataifa kuanza kulaani? Mungu anataka tuhubiri Injili ya Yesu, hiyo ndiyo dawa ya kubadilisha mioyo mibovu na kuleta hofu ya Mungu kwa viongozi wa vyama vyote!

  Mbona basi tunakubali kuunga mkono unabii ambao unaenda kinyume na Neno la Mungu? kwani Yesu Kristo alituagiza tuwaamini watumishi kuliko Neno Lake?

  Mimi nimejifunza na kuamua thabiti kupima kimaandiko kila unabii/ujumbe utakaosema na mtumishi au mtu yeyote. Kama unabii/ujumbe hauko sawasawa Kibiblia siuamini kabisa haijalishi umesemwa na nani!

  Kwani hata chama kingine kikitawala hao watawala wake ni malaika? je, si watu kama hao hao walio CCM ambao pia wanahitaji msaada wa Mungu? unafikiri shida iliyopo ni ya kichama? SHIDA TULIYO NAYO NI WATU/Watumishi wa CCM na vyama vyote na watendaji wote wa serikali katika ngazi zote WABADILIKE NDANI YA MIOYO YAO, WAWE NA HOFU YA MUNGU! Hiyo itawawezesha kutenda haki na kujiepusha na kutenda udhalimu katika maofisi yao/kazi zao kwa ujumla.
  Sasa watu watapataje hofu ya Mungu kama na sisi wapentekoste tunakuwa kama mataifa kuanza kulaani? Mungu anataka tuhubiri Injili ya Yesu, hiyo ndiyo dawa ya kubadilisha mioyo mibovu na kuleta hofu ya Mungu kwa viongozi wa vyama vyote!

  Kwani hata chama kingine kikitawala hao watawala wake ni malaika? je, si watu kama hao hao walio CCM ambao pia wanahitaji msaada wa Mungu? unafikiri shida iliyopo ni ya kichama? SHIDA TULIYO NAYO NI WATU/Watumishi wa CCM na vyama vyote na watendaji wote wa serikali katika ngazi zote WABADILIKE NDANI YA MIOYO YAO, WAWE NA HOFU YA MUNGU! Hiyo itawawezesha kutenda haki na kujiepusha na kutenda udhalimu katika maofisi yao/kazi zao kwa ujumla.
  Sasa watu watapataje hofu ya Mungu kama na sisi wapentekoste tunakuwa kama mataifa kuanza kulaani? Mungu anataka tuhubiri Injili ya Yesu, hiyo ndiyo dawa ya kubadilisha mioyo mibovu na kuleta hofu ya Mungu kwa viongozi wa vyama vyote!

 3. Mabinza,

  Unaponiambia nipande basi unamaanisha nini?

  Kuna wakati mtu unaweza ukahangaika na mtu ukidhani akili yake iko sawa, lakini kumbe kesha changanyikiwa. Mabinza nafikiri kuna kitu hakiko sawa kichwani mwako. Kuendelea kukuelewesha ni kupoteza muda, sijaanza na wewe hapa.

  Nilishakwambia kuwa ukiropoka siwezi kukuacha bila kukwambia.

  Nikiamua kwenda nawe katika mwelekeo ako; hebu onesha ushahidi wa nabii aliyewahi kuuawa kiroho baada ya kutabiri uongo, au mahali amabpo biblia imesema hilo fundisho kuwa sasa nabii wa uongo hatauawa kimwili bali kiroho.

  Tuoneshe wa maandiko ni nani huwa anawapiga mawe kiroho wale wanaokosea, angalao mtu mmoja aliyewahi kupigwa mawe kiroho.

  Maana naona huu ni ujuaji tu wa kujifanya kujua kutafsiri biblia, lakini kumbe ni kutengeneza fundisho la kubuni ambalo kimsingi ni fundisho la uongo.

  Ninyi ndio wale watu amabao wanajaribu kuishi maisha ya agano jipya, lakini wakijaribu kumwelewa Mungu kwa mfumo wa agano la kale. Hamwezi kufika mnakodhani mnakwenda, ila ni kuishia kuchanganyikiwa tu na kuanza kufundisha ‘Heresy’

  Unaona unakojaribu kuturudisha, kwenye adhabu ya dhambi ya uzinzi, bila kujiuliza kwa nini Daudi hakuuawa alipolala na mama yake Suleiman (mke wa Uriah), kwa nini Suleimani hakuuawa kwa hiyo idadi ya wanawake aliolala nao, na kwa nini Yesu hakumuua mwanamke aliyekamatwa na mafarisayo anazini.

  Kusema kuwa Kakobe ni mfu na wakati hukuwepo wakati anapigwa hayo mawe unayoyasema ya kiroho, ndio kuhukumu kwenyewe sasa, kama ulikuwa hujui maana ya kuhukumu. Na wala siyo kusema ukweli kama ulivyojaribu kumjibu Anthony. Hakuna ukweli wowote unaousema hapo.

  Mabinza kama wewe ufahamu wako uko hivi, sijui hao wengine ulio nao huko uliko wana hali gani!!

 4. Ndg yangu Anthon,

  kwanza nikushukuru sana kwa kuniambia yale UNAYOYADHANI kuwa mimi niko vile, kwakifupi upo mbali sana na ukweli kuhusu mimi! Mimi sijawahi kutengwa katika kanisa, pili mimi siyo Msabato hata kido na tatu sisumbuliwi na fundisho lolote la kidini.

  Ni hivi, iko tofauti kati ya kusema kweli na kuhukumu, vilevile ipo tofauti kubwa sana katika kutoa maoni yako na kuhukumu. Mimi sijamhukumu Asikofu kakobe wala Sikumhukumu, nilichosema nikwamba, Nabii yeyote akitabili uongo huawa, na kwasasa hawauawi kimwili, bali huawa kiroho.

  Maoni yangu ni kuwa, kama Askofu Kakobe alichukua nafasi ya kuwa Nabii ni sawa sina shida ya kujua kama ni Nabii wa kweli ama la, ila ni KWAMBA NABII AKITABIRIVISTOKEE, HUYO HAKUAMBIWA HAYO ALIYOYATABILI NA MUNGU HIVYO HUPIGWA MAWE NA KUFA, SASA KAMA KAKOBE NAYE ALITABILI NA HAVIKUTOKEA, YEYE HAJAPIGWA MAWE TAYARI? Kwa hiyo, kama Kama Kakobe anakili kuaw ni Nabii, nye aliyoyatabiri hayakuwa, utasemaje kuwa hakupigwa mawe ya kiroho na kufa kiroho kwa kosa la kusema kuwa kaambiwa na Mungu kumbe hakuambiwa? Kwa maana hiyo nikasema Mfu, ki kimwili ila Kiroho! Sasa, kama wewe hukubali mimi sikulazimishi, na wala kusema hivyo si kwamba simpendi Kakobe na wala si kwamba ninauadui na upentekoste, ila kweli yenyewe ya Biblia ndiyo hiyo, kuwa ukitabili jambo lisitimie Mungu anakuua!

  Hoja yako kuwa, hatia atakuwa nayo Mtu akikamatwa, huo ni mtazamo wako, si Neno la Mungu hilo. Biblia inamkuu Yesu ambaye ndiye Mungu mwenyewe kwa kinywa chake akisema, “…..na mtu akimtamani Mwanamke asiye mkewe tayari amekwishazini……” na tunajua adhabu ya wazinzi walipigwa mawe sawasawa na Mabii waongo, je sasa mtu akimtamani mwanamke anakuwa ameonekana nani ili akamatwe, ili apigwe mawe kama sheria isemavyo? Kumbuka Bwana Yesu hakuja kuiondoa Torati!

  Kwa maelezo yako Anthoni, wewe unaona kuwa Kakobe siku alipotabili kuhusu NCCR kuwa itatawala, alisemea sirini na hivyo hawezi wala hakupata kukamatwa kwa adhabu ya watabili waongo?
  Naamini kuwa utarudi kwangu hivi karibuni, karibu sana ukiwa na majibu ya kimaandiko.

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai”

 5. Shida hapa ktk mabishano ni ule ubinafsi wa kidini, sijui hili pepo dini litaisha lini, MSABATO, MARMO, MPENTEKOSTE, MLUTERI, MKATOLIKI, Kilamtu anataka kutoa umaarudu wa mafundisho ya dini yake.

  Pepo dini baya sana, mtu analeta ubishi na hukum dhidi ya watumishi wa Mungu ambao binafsi hajawajua bado. Mabinza nilichunguza sana posti zake za nyuma nikajua huyu anamajeraha na wapentekoste. Yamkini aliwahitengwa au mafundisho ya dini (Sabato)yanamsumbua Kiukweli Mungu angehesabu maovu yetu nani angesimama? Ivi unajua sheria unayongangania kwa askof zk unajua kwamba zamani ilikuwa ni apply kwa anayekamatwa tu? Usipokamatwa basi umepona. Pia maana ya Yesu kuwambia asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe unajua maana yake? Au usabato haufuati new testment?

  Kwa kifupi kuna mkanda ambao zk aliomba toba mbele ya wachungaji kwenye kongamano uliona?
  Halafu wewe nani hata useme zk ni mfuu? Au ndio kama mafarisayo ya kunyosha kidole huku kingine kikikurudia?

  Mimi ningekuona grown up ungekija na hoja ya kuthibitisha unabii sio kwa umahili wa kuandika riwaya nonono bali kwa uvuvio wa uweza na nguvu za kiungu.

  Ukweli utabaki palepale, kazi anayofanya kakobe wewe hujafanikiwa hata 0.1% kwani kiushahidi mkubwa unachoandika unaonekana upo mwilini sana na kitheolojia na watumie elimu dunia mithili ya wale uamsho au boko haramu, au hujui kama hata wao wanajua maandiko kwa akili kama wewe.?

  MWISHO NISEME KWAMBA SI MSHIRIKA WA FULL GOSPEL ILA NI MTU NA SIJAWAHI KUHUDHURIA HAPO, ILA HUZIPIMA KAZI ZA WATUMISHI. NA KABLA SIJANYOOSHA KIDOLE LAZIMA NIJIPIME KWA ULINGANO. OLE WANGU MIMI, OLE WAKO WEWE.

  DHARAU SI NZURI.

 6. Sungura,

  sijaona lolote linalokufanya uchukie vile! mjadala uliopo mezani ni unabii wa Askofu Mkuu Kakobe uliotabiliwa kuihusu CCM na Seriali take. Nikatoa maoni yangu kwa kuwa Mimi ni MTU huru. Niliiangalia Biblia kwa kuwa ndiyo dira yangu ili kujiridhisha kuona kama unabii ule umetolewa ipasavyo, nikakuta SIYO! Hivyo nikasema hayo niliyoyasema.

  Nilitegemea atakaye nipinga atakuja na maandiko kuwa, licha ya mtu kuwa nabii akitabiri uongo anaweza kuwa hai tu kiroho hata kuweza tena kutumwa na Mungu kutabiri! Jambo lingine nilitegemea kupata jibu la kibiblia kutoka kwenu akina Sungura kama, Unabii unweza kutolewa hata na ‘Nabii’ aliyejaa chuki kwa kunena haki ya Mungu akiongozwa na Roho mtakatifu!

  Mwisho kabisa, kwa wewe unaye weka mbele ubishi, hasa kubishia kila utakachoona Mabinza LS kakisema. utakufa kwa kiu kwa mtazamo tu kuwa Mabinza LS huwa hachemshi maji!

  Kama kweli unataka kujua wewe si huru jiangalie unavyochachamaa na kutoka povu bila kuleta hoja kwa maandiko kudhibitisha kwa nini tuuamini unabii wa Askofu Kakobe. Vinginevyo nitakuona upo STAND hupandi Gari kwa maelezo kuwa kila gari lijalo kituoni ulipo limejaza sana Abilia, bila kujiuliza kuwa kunawengine hushukia vituo vya kabla ya unakokwenda wewe, panda BUS Sungura, Seat utaipaipata
  humohumo nani ajuaye?

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 7. Dawa ni moja tu wapentekoste ni kukataa kupigia kura CCM kwa ujumla wetu na kupigia upinzani kwa ujumla wetu. Hapo mtarejesha heshima ya kanisa la wacha Mungu.

  Mkiamua moja hakuna litakaloshindikana. Kura milioni kumi si haba.

  Mbarikiwe

 8. wapendwa,

  Sameheni saba mara sabini, wala msiiombee serikali wala vyama vya siasa mabaya kumbukeni kukitokea machafuko watakaoteseka si hao vigogo wa CCM, bali walalahoi ambao wengn wao hawajampokea kristo.

  Naona wengne wanajazba mpaka wanataka kurudisha kadi za vyama.Hapana “Mkubwa hakosei anapitiwa tu” hebu tuacheni malumbano, hebu tuache kupandikiza chuki za kidini vs kisiasa.

  Mimi nina wazo la kuwasaidia, unajua km umenyimwa kuingia kupitia mlangoni kwny jambo ulipendalo utapitia dirishani, wakifunga madirisha utapanda darini, wakiziba huko utachungulia kwenye matobo, kwa kifupi tunasema ‘penye nia pana njia’. Au ‘mtafutaji hachoki”. Nadhani baadhi yenu mnajua habari za mgonjwa mmoja aliyekuwa amepooza ambaye ndugu zake walimpeleka kwa Yesu, ila watu walikuwa weng sana wasingeweza kumfikia Yesu ambaye alikuwa ndani ya nyumba fulani, walipofikiri “nje ya box” walipata wazo nzuri, walipanda juu ya dari, wakatoboa usawa wa pale alipokuwa Yesu kisha wakamshusha mgonjwa wao akapata huduma. Hata nyie ndugu zetu achen kulaumu,acheni manung”uniko,acheni kulumbana, just think outside de box, kama issue sio mafungu bali ni kufikisha maoni yenu bungeni, bado njia ipo.

  Wapendwa km nia yenu hasa ni kutoa maoni yenu kwenye bunge la katiba linaloendelea msikate tamaa, mafungu ni kweli inawezekana mmeyakosa ila penyesheni maoni yenu kwa njia ifuatayo:

  1.watumieni wakristo wenzenu mnaofanana interests kuwasilisha maoni yenu,

  2.Jamani, kati ya wajumbe zaidi ya 600, si wapo wapentekoste walioingia kwa kofia nyingne, wapo wabunge, wapo watu wa asasi na taasisi mbali mbali. Fanyeni haraka, watumieni hao, waorganize wapeni madesa wameze halafu wawawakilishe.

  jamani ni ushauri wangu kama nimeteleza mahali mnisapehe.

  ****Mungu ibariki Tanzania**Mungu liongoze Bunge la Katiba

 9. Aider,
  Ubarikiwe kwa kuwa na macho ya rohoni na hivyo kuujua wito wako ambao ni mkuu kuliko siasa za dunia zinazozunguka kama pia, pamoja na washirika wake!

  Wapentekoste wanagombea kula mezani pa Ahabu, hiki ndicho kinachowavuruga hata kunafikiana wao kwa wao!!!

  Nao unafiki husambaa mpaka kwa makusanyiko, yakitekwa ktk unafiki huo na kuendeleza chuki na husda ambazo hata shina la uchungu walilonalo hawajui wamelitoa wapi!!!

  Ni vigumu kuliamini hili, lakini Aider, hebu angalia wapendwa wanavyo argue strongly, but out of ignorance!!!!

 10. ‘msibishanie Neno langu bali mpingeni shetani.’ busara itumike zaidi, naona wengi mnahama kwenye lengo

 11. Watu wa Mungu nawasalimu nyote katika jina la bwana wetu YESU KRISTO .uku ni kiwauliza mta mwa achia nani ule ubunge wa mbinguni tuliyopewa kwa kifo cha Bwana wetu YESU KRISTO kama maandiko inavyo tuambiya

 12. Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) ndg Zakaria Kakobe (Z K) mzaliwa wa wilaya mpya ya Kakonko mkoani Kigoma, anayefanya kazi ya Mungu sasa hivi katika nchi mbili yaani Tanzania na USA, Mungu akubariki kwa kusema yaliyokuwa ya Moyoni mwako na yale unayosema Mungu amekupa umptaie President wa Bongoland ndg Dr. Jakaya Kikwete na umma wote wa Bongo.

  Baba Askofu tumekusikia sana tangu mwaka 1989 ulipozindua huduma ya kiroho ya FGBF hapo Mwenge Dar. Mungu akubariki sana.

  Kama Chama na viongozi wake watawala hawajui nguvu ya umma wa walokole wapentekoste, na kama wamesahau hilo kuwa lilitaka kuwagharimu mwaka 2010 wakati wa uchaguzi waendelee kupuuza umma huu wa walokole. Wataipata sana.

  Mimi naishauri CCM na wanasiasa wote hapa nchini kwamba pamoja na mapungufu ya wapentekoste wanayoweza kuwa nayo; labda ukiwalinganisha na Wakatoliki, Warutheri na Waanglikana, na labda ni kwa sababu wapentekoste hatuna Vyuo Vikuu, Mashule, na Mahospitali makubwa kama KCMC, BUGANDO MC, NYAKAHANGA, BUNDA DDH, NYERERE DDH, KIGOMA CDH,nk, ni kwamba wasiwadharau wapentekesto kwa kiwango cha kitaifa kama kilivyotokea wakati wa uteuzi wa wajumbe wa kutunga katiba ya nchi hii.

  Kama kuna chama cha siasa kinapanga kuendeleza dharau kama hizo za tangu zamani za ukoloni, basi chama hicho kijiandae kusambaratika hata bila kutegemea unabii wa Askofu Kakobe.

  Hata kama Kakobe unabii wake haungekuwa na ukweli kama baadhi wanavyoutazama, bado kabisa mimi nabaki nikiamini kwamba kama utawadharau walokole kwa wingi wao walionao kwa sasa, hakika wewe kama mwanasiasa au chama cha siasa iwe CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP, nk hautakuwa salama kabisa. Lazima utasambaratika tu.

  Kwa hiyo, kama JK Mrisho Khalfan na wenzake wanafanya maksudi kubagua kundi la walokole wanaowakilishwa na PCT, hakika chama chao CCM hakiwezi kubaki salama kwa kosa hilo. Hata bila unabii wa Kakobe. Huwezi kuwadharau watumishi wa Mungu kama hao halafu ukabakia madarakani milele. Utashushwa tu.

  Kumbuka kwamba wapentekoste wa sasa siyo kama wale wa miaka ya 1990’s. Kwa sasa nao wao wamesoma na wapo wenye shahada za uzamivu (PhD) na shahada za Uzamili (Masters). Wapo wengi tu. Wanafahamu kuchambua mambo kwa upana na kwa uelewa wa hali ya juu. Usiwadharau.

  Siku hizi na wao wameanza kumiliki shule za sekondari nyingi tu. Wapo wameanza kumiliki Vyuo vya elimu ya kati na ya Juu. Wapentekoste nao wameanza kumiliki vyombo vikubwa vya habari kama TV, Redio, Magazeti, Blogs, Website, nk. Wapentekoste sasa wanamiliki makanisa makubwa sana yenye watu wengi sana kuliko hata makanisa ya katoliki na kirutheri siku hizi. Usiwadharau.

  Wapentekoste ndio kundi pekee la kidini lenye uwezo wa kufanya mikutano mikuuuuuubwa ya Neno la Mungu ikakusanya maelfu ya watu kuliko hata makanisa makongwe kama katoliki. Usiwadharau. Washirikishe kwenye maamuzi ya nchi hii, vinginevyo watakuacha solemba siku utakapowahitaji.

  Kama hujui nguvu ya wapentekoste kamuulize Zitto Kabwe yaliyomkuta mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaaguzi za mwaka huo. Kama asingeenda kuwapigia magoti Jimbo lake lilikuwa limeshaenda kwa mgombea wa CCM, lakini Zitto Kabwe alivyowapigia magoti hapo ndipo alishinda. Wakati wa uchaguzi wa 2010 mimi nilikuwa Mwanza, hapo ndipo nilijionea nguvu ya wapentekoste. Maaskofu wote walikuwa hawana time na mtu anayewadharau hata kama alikuwa ana pesa nyingi au yuko chama gani iwe tawala au wapinzani. Acha kabisa.

  Kama hujui nguvu ya wapentekoste mheshimiwa uwe ndani ya CCM, CHADEMA au wapi, utajionea mwenyewe. Subiri ifike mwaka 2015 utaona. Labda mikoa ile isiyokuwa na waumini wengi wa kipentekoste, hapo sina neno. Lakini waumini wapatao 10,000,000 na zaidi, usiwadharau kabisa.

  Unabii wa ZK kwa JK na umma wa Tanzania, utatimia tu hata kama haukutoka kwa Mungu unayemwamini wewe, lakini yatazame hata mazingira yenyewe tu yanatosha kukwambia kwamba siyo lazima ZK atoe unabii bali mazingira yenyewe yanatoa unabii wa kweli.

  Karibu tena.

 13. Mabinza,

  Kwa akili yako timamu unafikiria kabisa kuwa mimi ninadhani kuwa tunaokolewa kwa sababu ya upentekoste? – Huu nao ni upuuzi wako mwingine.

  Kwani ni nani anayekulazimisha wewe uuamini unabii wa Kakobe? Kuuamini au kutokuuamini kwako hakuwezi kuongeza wala kupunguza lolote juu ya huo unabii.

  Ndio maana nakushangaa sana unapopiga mbiu hapa kuwa watu wasiuamini huo ujumbe. Nani alikwambia unabii hutimia kwa sababu mtu fulani ameuamini au hakuuamini? Wwewe uamini au usiamini kama ni unabii wa kweli utatimia kama si wa kweli hautatimia.

  Usijaribu kusimama hapa na ushawishi wako wa pupa,kama na wewe una unabii uliotofauti na huo utoe tu tuusikie, kuliko kuleta porojo za mambo yaliyopita ambayo huwezi hata ukayathibitisha.

  Ulisema kuwa kuchafuliwa usemi kwa watu wa Babeli hakuhusiani na kuchafuliwa usemi kwa CCM, kwa kusema kuwa Babeli haina ulinganifu wowote na CCM, ati kwa sababu CCM si taifa na Babeli ilikuwa taifa. Mimi nikakwambia kuwa hawakuchafuliwa usemi kwa sababu ya wao kuwa taifa au la, bali ni kwa sababu walichokuwa akikifanya ahkikuwa katika mapenzi ya Mungu.
  Haya hebu thibitisha sasa ni wapi nilipojikanyaga ktika kulifafanua kwangu hilo.

  Wewe ulitaka kuwe na uhusiano wa namna gani kati ya majina yaliyopelekwa na huo unabii ndo ujue kuwa kuna uhusiano?

  Mabinza, kama mimi siko huru basi wewe ni mfu kabisa. Hatuanzii kwenye mada hii wewe na mimi kuvutana. Kuna maada nyingi sana huko nyumma, na zingine ulikimbia bila kulipa madeni.

  Wewe siyo independent thinker, mara nyingi sana mawazo yako huwa yako vague kwa kiasi cha kutosha tu. Binafsi siwezi kukuacha uturopokee chochote kisicho sawa, lazima nitakupinga Mabinza.

  Ukisema kitu tangible nitakupongeza!

 14. Sungura,

  Neno la Mungu kwa wanaopotea ni upuuuzi! kwako unadhani tunaokolewa kwa sababu ya ‘UPENTEKOSTE’ usizungumzie ushabiki wala upenzi, jambo hilo la upenzi limewasumbua wengi, hata kuikataa kweli ya Mungu! Inashangaza kutotaka kuuchunguza na kuukubali ukweli, unashadadia jambo bila ushahidi, ili kuwapoteza watu kwa upenzi wako, wa kuongopa ama kwa kudhani kuwa kwakuwa nataka ukweli, basi mimi siwezi kuwa mpentekoste, hata hivyo, ukiwa mpentekoste wa Mungu wa kakobe asiyetimiza unabii wake ndipo unakuwaje?!

  Kama nimeongea upuuzi au kama siyo Mpentekoste, sikukatazi kusema hivyo, kwani dharau na ushabiki badala ya hoja ni kawaida ya watu wa mlengo mmoja. sijajua unafafanua kitu gani juu ya habari ya kumezwa kwa Yona na Kifo cha Bwana Yesu au Habari ya Babeli na CCM, mimi naona unajikanyaga tu, ama kwa sababu unadhani kuna mtu ana mshambulia Kakobe kama Kakobe, hoja ni kwamba,

  kutokuzingatiwa kwa Mapendekezo ya majina mliyopeleka ili kuingizwa katika Bunge la katiba (KAMA KWELI YAPO!) ni kwa vipi kuna uhusianano wa maana sana na Unabii wa Askofu mkuu kakobe! Hoja ya pili ni kuwa, kwa mjibu wa Biblia, Nabii ‘Muongo’ ni lazima afe, na mfu hajui neno lolote, sasa ni kwa vipi, Askofu mkuu Kakobe, tumuamini kuwa kaambiwa na Mungu, ikiwa Mungu si Mungu wa wafu, maana hadi Mh. Mrema anakihama Chama cha NCCR hajawahi kuwa Rais, kwa hiyo unabii wa Askofu mkuu Kakobe haukutimia!
  Sungura wewe haupo huru, kweli kwako itakuwaje si upuuzi?

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 15. Wapendwa,

  Kwanza nawapeni pole nyote ambao mnaishi ktk ulimwengu wa kufikirika!

  Pili napenda kuwarudisha ktk ulimwengu halisi ambao kila mmoja wetu anapaswa kuwajibika ktk majukumu yanayomhusu, hata akiwa ni mlei, ktk mfumo wa maisha aliojichagulia, haswa Wokovu!

  Maisha ya ‘Wokovu” hayakuondolei kuwajibika kama wengi wetu tunavyopenda iwe au kulazimishwa kufikiri hivyo. Malalamiko mengi ninayoyasoma hapa, pamoja “thumbs up” anazopewa Askofu Kakobe, ni ishara tosha inayouonesha udhaifu wa kufikiri tulio nao. Yaani tumekosa wajibu wa kuyafikiri mambo ktk uhalisi wake, na hivyo tumeanza kujijengea hulka ya kulazimisha mambo kama ndg zetu wa “siasa kali”!

  Udhaifu wa kujisahihisha au kukubali makosa, huzalisha kujitetea na kuelekeza lawama kwa watu wengine kusiko na wajibu. Yaani hukufanya uishie ktk unafiki, na hivyo kusambaza chuki na masikitiko ktk jamii na mwishowe mifarakano!!

  PCT, ilipoona kwamba majina waliyoyapendekeza hayamo ktk orodha ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, waliilalamikia serikali kwa kuwatenga ktk jambo la kitaifa kama kundi lililopaswa kuwa na uwakilishi. Kimsingi jambo hili ni doa kubwa kwa utendaji wa serikali isiyoendeshwa kwa misingi ya dini, basi kila mmoja wetu alijiuliza, kulikoni? Serikali imefilisika kiutawala mpaka inawabagua wanawe? Tunajiuliza maswali haya na mengine mengi kwasababu tunaiamini kauli ya maaskofu wa PCT; tunaishangaa serikali kulipuuza kundi la watu milioni kumi na moja, yaani karibu robo ya wananchi wake! Kunani mpaka serikali iamue kugombana nao, kwa faida gani??????

  Serikali ilipojibu lawama hizo, ilisema HAIKUIPOKEA orodha hiyo, na kama PCT waliipeleka basi wawakilishe ushahidi wa hilo. PCT ktk kuijibu hoja hiyo ya serikali, wakasema hawawezi “kufunua utupu wa baba yao”, hiyo serikali; bali hapo hapo wakasema wanaikemea dhambi ya uongo, na wakatuthibitishia waumini wao kwamba walipeleka majina!!

  Lakini, jibu hili la maaskofu lina mapungufu makubwa kiuwajibikaji. Walipaswa kuweka hadharani vielelezo vyao vya kuyapeleka majina hayo, km nakala ya barua hiyo iliyo na udhihirisho wa kupokewa kwa majina hayo, ili kauli yao iwe ushahidi mbele ya taifa, na Mungu apate kuheshimiwa hapo anapodhihirishwa kupitia wao kama sehemu ya mwili wa Kristo! Hatujaona lolote kuhusu hilo.

  Badala ya kuliweka sawa jambo hili, ambalo kimsingi, viongozi wetu ni sawa na kuwa wametukusanya pembeni, na kutuambia kuwa serikali imetutenga huku kando kama yatima, ndipo tunamuona Askofu Mkuu Kakobe akikamilisha ukuta wa utengano huo wa watu na serikali yao, kwa kutumia jukwaa la hilo la Kipentekoste, katika maana ya Madhabahu ya Mungu, na sasa akitangaza HUKUMU juu ya serikali, ambayo inakazia ukweli wa PCT kupeleka majina!! Basi ni Hakimu gani huyo anayetoa Hukumu bila vielezo vya ushahidi? Biblia inataka mashahidi wawili au watatu ili jambo lithibitike!!

  Lakini walengwa wa kauli hii ya Hukumu ya Mungu ni sisi waumini na si serikali kama tunavyofikiri!!!! Hii ni hila ya kuzidi kutugawa, ikitukusanya pamoja kuichukia serikali yetu, ikitutia ujinga kwa kutuondolea uwezo wa kuwahoji viongozi wetu waliojikweza na kujiondoa ktk kuwajibika kwa waumini wao, na sasa wakiwageukia waumini wao ili kuwafanya watumwa wa mawazo yao!

  Au Umoja huo umetumbukizwa ktk kampeni za siasa za uchaguzi bila ufahamu au kwa ufahamu kamili? Nani huyo anayetaka kuwapumbaza kundi la watu milioni kumi na moja walioiona Nuru Halisi, na sasa anataka kuwarudisha ktk nuru ya vibali vya siasa, awatumikishe huko, akiisha kuwafanya ni “chumvi” iliyoharibika? Unajua chumvi ni mwokozi, bali ni lazima kuwe na contact, yaani kugusana nayo; sasa hebu niambie ukigusana na mtu mwenye malalamiko utaishia wapi? kwenye dimbwi la malalamiko!!!!

  Tuacheni ushabiki, tafuteni kujua ukweli wa jambo hili kwanza. Jambo la kubaguliwa si dogo. Serikali imesema hadharani kuwa tamko la maaskofu HALINA ukweli, kwa maneno mengine maaskofu hao ni WAONGO hawakupeleka majina; sasa maaskofu wanashindwa nini kutoa vielelezo???

  Basi tukiwa ni watu tusiowajibika kwa kauli zetu, huyo atakaye tuheshimu ni nani? Leo tunautangazia umma kuwa Wapentekoste tuko milioni kumi na moja, hiyo sensa tuliifanya lini hata kupata idadi hiyo???? Katika sensa iliyomalizika, kuna kundi la Waisilamu waliotaka kipengele cha dini kiwekwe ktk madodoso ya sensa lakini serikali ililikataa jambo hilo, hamuoni nanyi kwa kauli kama hizi mnaanza kuwa na mawazo kama ya hao??? Mnataka kuufanyia nini huo wingi wetu? ni wapi ktk Maandiko tunapotakiwa kuuinua wingi wetu???

  Kwanza huu Umoja wenyewe kweli ni Umoja au ni siasa za Umoja? Hivi ni kweli jamani kwamba Wapentekoste wanao Umoja???? Hebu fikirini vizuri, tunao Umoja sisi kweli???? HATUNA Umoja, kama ungekuwepo Umoja solid, na uwajibikaji ungekuwa wazi, no wonder serikali inatuonea aibu kutushushua watu wazima milioni kumi na moja!!!

  Ndg zangu, hebu tufikeni mahali tukomaze kuwaza kwetu, tumejikita sana ktk miujiza mpaka tunakuwa wajinga wa miujiza; tuziinue shingo zetu, tuutazame ulimwengu na kukabiliana nao, tuweni “wajanja kama nyoka”!!!!

 16. Amo 3:7 “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake”

  Kuhusu matukio yanayotokana na Mungu, hapo anapoamua kufanya lolote, hata ikiwa ni kuwasambaratisha CCM na serikali yake, basi hilo halitafanyika isipokuwa kwanza amewajulisha watumishi wake manabii, hao ambao amewainua yeye mwenyewe kwa kazi hiyo, maana manabii wengine ni wa vipawa tu, hivyo visivyo na majuto, kwahiyo huwa hawapewi SIRI za Mungu!

  Basi Neno hilo likiwa liko hivyo, twapaswa tulielewe hivyo na kuliamini ktk kiwango hicho, ili liwe na nguvu iliyokusudiwa juu yetu, hata ikiwa ni kutulinda na udanganyifu wa siku za mwisho, ile “yumkini”!

  Hivyo twaweza kusema kwa UHAKIKA, kulingana na hilo Neno, kwamba huu si Unabii utokao kwa Mungu kutokana na kutolewa kwake kupitia kwa “Askofu Mkuu” badala ya Nabii kulingana na Msingi aliotuwekea Mungu mwenyewe utuongoze ktk mambo haya!!!

  “Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?”

  Mbarikiwe nyooote!

 17. Mungu wa wa Pentekoste ???? Imani ya Kipentekoste ???
  Ningependa kufanya masahihisho kidogo, Mungu aliyehai tunayemwabudu sio wa wapentekoste tu. Imani tuliyonayo ni ya Kikristo sio ya Kipentekoste
  Roho Mtakatifu atufunulie zaidi

 18. Bwana Joshua,

  Hizo harakati za kanisa kuwa pamoja zianzisheni,mbona mnakomea kulaumu tu, mnataka nani aanze?

  Kwa upande mwingine tungepaswa kuwapongeza waimbaji wa injili maana wamelisaidia sana kanisa kuwa pamoja. Warutheli kuimba pamoja na wa-TAG, EAGT, FPCT, wa- Anglikana, n.k. si kazi ndogo. Wanamuziki wamefanya sehemu yao hawapaswi kubezwa.

  Umesema kuhusu kufanya maombi kama katika nyakati za akina Ester. Kumbuka tu maombi ya kufunga ya namna hiyo huwa yanafanyika kunapokuwa kumetokea jambo lenye adha kubwa kwa kanisa. Si rahisi tu ukasema tukusanyike na kufunga siku moja au mbili kwa jambo tu la kawaida.

  Kwa mambo ya kawaida inatosha kukusanyika tu na kuomba maombi kama yale ya juzi yaliyofanyika Sabasaba. Mara nyingi tunarahisisha tu maombi ya kufunga, lakini yanatakiwa kuwa ni kwa ajili ya ishu kubwa kama hiyo ya wayahudi kutangaziwa kuuawa, kama Yohoshafati alipovamiwa na majeshi matatu, kama ninawi walipotangaziwa kuangamizwa, n.k

  Jambo la muhimu tu ninalosisitiza, tuache kulaumu kama na sisi tunayo nafasi ya kulitekeleza jambo tunalolitamani kufanyika. Maaskofu si kila kitu katika kanisa wala wachungaji. Sisi wote tuna nafasi ya kujitokeza mbele za Mungu ili atutumie kutimiza yale ambayo mioyo yetu inayatamani, na yale ambayo mwenyewe anataka yafanyike.

  Tutafuteni wenyewe namna ya kulifanya kanisa liwe pamoja kama tunaona haliko pamoja kama inavyotakiwa. Kuna blogs kama hizi, tuzitumieni kwa ajili ya ktutimiza hayo malengo, kuliko kuendelea tu kuwalaumu maaskofu kwa kila kitu, hata kile ambacho hata sisi wenyewe twaweza kukifanya.

  Barikiwa.

 19. Mabinza,

  Unajua umeendika upuuzi ndio maana umewahi kujitetea kuwa umetupia mzinga mawe. Na mmi hata sikucheleweshi, nakuanzia.

  Kwanza nashukuru leo umenisaidia kujua kuwa wewe si mpentekoste, maana siku zote umekuwa ukikwepa kujitambulisha.

  Uelewa wako mdogo wa kuelewa mambo uko wazi kwenye mfano wa Yesu na Yona na ule wa Babeli na CCM.

  Umesema mfano wa Yesu kwa Yona ulitimia, sasa ngoja tuuchambue tuone kama ulikuwa unafanana na kifo cha Yesu kama unavyodai kuwa ulitimia, maana mfano huo ulikuwa unahusiana na kifo cha Yesu.

  Yesu alifaninisha kitendo cha Yona kukaa tumboni mwa nyangumi siku tatu, ni sawa na yeye kukaa kaburini siku tatu.

  Hebu tuone sababu za Yona kuwa tumboni mwa nyangumi kama zinafanana na sababu za Yesu kuwa kaburini:

  -Yona alimezwa na samaki sababu ikiwa ni kutotii agizo la Mungu la kwenda Ninawi.
  – Lakini Yesu hakuwa kaburini kwa sababu ya kutotii agizo la Mungu, bali ni kwa sababu ya kuleta wokovu kwa wanadamu.

  Yesu alianzia msalabani, lakini Yona alianzia kwenye merikebu

  Hapo hakuna mfanano wowote.

  Unasema CCM si taifa, kwani mnara wa Babeli ulikuwa taifa?
  Kwani Mungu alifarakanisha hao watu kwa sababu walikuwa taifa au ni kwa sababu walilokusudia Mungu hakukubaliana nalo?

  Mungu alifarakanisha usemi wao ili kusudi lao baya lisitimie, si kwa sababu walikuwa ni taifa. Sijui hata kama unaelewa maana ya taifa, au unajisemea tu.

  Na unamaanisha nini unaposema utabiri wa kibinafsi, kwani huwa kuna utabiri wa kiumoja? Kuna sehemu manabii waliwahi kualikana ili wakatabiri pamoja?

  Mbona kwenye kwenye biblia mabii wote kila mmoja alitabiri peke yake kama ambavyo Mungu alimpa ujumbe!!

  Na kama wewe umeona shaka kwa nini usingekaa kimya tu? Maana mtu mwenye mashaka hana sehemu yoyote katika ufalme wa Mungu.

  Unapotuambia hapa kuwa umeona shaka, unataka na sisi tuone shaka kama wewe au?

  Na ulitaka Kakobe awe rafiki kwanza wa CCM ndipo ungeona kuwa alichokisema ni cha kweli? Kwani zamani manabii walikuwa wanatabiri tu kwa watu ambao/ au falme ambazo ni rafiki zao? Hebu tupe mifano wa hilo.

  Suala la Kakobe na uchaguzi wa mwaka 1995, tulishaliongea sana hapa, kama vipi nenda kwenye hiyo mada utaikuta michango yetu huko.
  Ufahamu wako ni mdogo.

 20. Wapentekoste,
  Mmewakilishwa na kakobe ambaye anasema ametumwa na Mungu kwa Mh. Kikwete na Chama chake cha C.C.M, ili kumuonya na kumshauri atubu yeye kama Rais na CCM kama chama tawala, kwa kile kinachosemwa “KUTOKUSHIRIKISHWA KWA WAPENTEKOSTE KATIKA BUNGE LA KATIBA” Mungu huyo wa Kakobe na ambaye pia ndiye mungu wa wapentekoste kwa mjibu wa Kakobe mwenyewe, amesema atachafua “ndimi” kwa CCM na kwamba wataanza kutoelewana na kufarakana kila mwana CCM na njia yake, hali hiyo itadhilika waziwazi kunako 2015!.

  Kwanza simpingi Askofu mkuu Kakobe kuwa hakuambiwa yale aliyoyasema na huyo Mungu wake kama alivyosema. Lakini nikirudi nyuma mimi Binafsi, nakuta kuwa, Askofu kakobe si RAFIKI wa CCM tangu Enzi za NCCR ya Mrema! Kakobe amekuwa na chuki ya wazi na CCM kwa mda mrefu na sijui ni kwa sababu gani. Ushahidi mmojawapo wa chuki hiyo ni kule kuzuia Miundombinu ya nishati ya Umeme isipite karibu au upande wa Kanisa lake lilipo, akihoji kwanini isipitishwe upande ule wapili mkabala na eneo la Chuo kikuu cha Dar es salaam, sababu alizotoa akidai ni zakisayansi na kwamba zinautafti wa kutosha, hadi sasa ni miaka kadhaa imepita hatujasikia “Kesi” ya ugonjwa ama madhara ya kiafya kwa Binadamu ndani ya Kanisa lake ama nje ya Kanisa lake, yaliyopata kuripotiwa kuwa wametokea kwa sababu za wazi kama ilivyokuwa imeainishwa na Askofu Mkuu Zachary Kakobe.

  Haikuwa hivyo tu, mapema miaka ya nyuma, aliitabiri kushindwa kwa CCM na kwamba Chama cha NCCR ndicho kingetwaa dora na kuiongoza Tanzani, jambo hilo halikutokea hadi leo hii anapokuja na hii mpya ya kumlaani Rais Jakaya Kikwete na Chama chake cha CCM!

  Kwa Mjibu wa Neno la Mungu ambalo ni Biblia, linasema, NABII AKITABIRI JAMBO NA LISITIMIE, ATAUAWA!

  Sasa kama Wapendekoste wanaamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu, Je, Askofu mkuu Zachary Kakobe bado hajafa kweli? Na kama kafa Biblia inasema, Mungu si Mungu wa wafu, sasa Askofu Kakobe atwezaje kupewa Taarifa na Mungu ali hali yeye tayari hayupo Duniani kiroho?, Ninyi wapendekoste mnaomtakia ‘kubarikiwa’ Askofu Kakobe, hamfuatilii mambo ya jamaa yenu, ama ushabiki na ubaguzi wa kidini tu umewajaa? Sasa Askofu mkuu Kakobe anathibitishaje, kuwa hili analoli “TABIRI” la kufaraka kwa CCM ifikapo 2015, litatimia iwapo hautatimia unabii huu kama ule utabiri wake wa mwanzo kwa CCM, mtawaambiaje watu kuwa, MNA MUNGU? Na kama ni kweli kuwa Mungu wa Kakobe ndiye Mungu wa wapentekoste, Kumpa ‘BIGUP’ Kakobe ambaye kwa mjibu wa Biblia ni tayari ni Nabii aliyekufa, wanataka kuniambia nini mimi binafsi na wengine wenye kujiuliza kama mimi?!

  Kwa hayo machache mimi Binafsi inanipa shaka kama Mungu ndiye Mungu wa ‘Type’ ya Mungu wa Askofu Kakobe, mwenye “kuinunia CCM”, kwa kiasi kile kuwa ni Mungu Mkuu wa kweli!

  Mwisho kabisa, sijaona pahala popote katika Biblia, kunakosema kuwa, Mungu alichafua ndimi ama semi za watu hao wa kale katika Babeli ya kale kulitokana na uongozi wa babeli kutowashirikisha wacha Mungu katika kuitunga katiba ya kuongozea Babeli. Nasema hivyo kwa sababu, mifano katika Neno lazima isimame na kweli ya Neno la Mungu, kwamfano yesu alipotoa mfano wa Yona kuwa katika tumbo la Samaki siku tatu, ilikuwa kweli na hata maana ya mfano ule ilikuwa dhahili, na mingine mingi tu. Sasa huo wa Askofu kakobe kuwa, “Tukio la Babeli ya kale” litakuwa kwa CCM, haifanani hata kidogo, kwanza, CCM ni chama na si Taifa, na hata kama ingekuwa ni Taifa, bado si Taifa analomaanisha Mungu, Maana Biblia haizungumzii walionje ya Biblia yenyewe. Nijuavyo mimi CCM si Taifa la MUNGU MMOJA, ni ‘Taifa’ la miuungu wengi tu! Kwani mle kuna Watu wa imani mbali mbali, na Biblia inasema Imani moja, Mungu mmoja! Kuingiza Biblia na mifano ya Kiblia katika utabiri wa Kibinafsi ni kuikosea adabu Biblia ambalo ni Neno la Mungu. Mungu ni Baba yetu, Biblia inasema amtukane baba yake atauawa! kama tukimsingizia Mungu kutuambia mambo ambayo hakutumambia, ama kumbe tumeambiwa na ‘mungu’ mwingine, ni kumtukana Mungu mkuu wa kweli, na hivyo kujikuta wafu! Inawezekana nikawa nimeutupia jiwe mzinga wa nyuki, lakini jueni pia kwamba, autupiaye Mzinga wa nyuki jiwe anapaswa asimame upepo wa mbisho, nami nimesimama kunako upepo wa mbisho!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 21. Ni kweli vijembe kwenye TV, maredioni vinampa sana ibilisi nafasi ya kututhoofisha. Lakini siku chache zilizopita kulikuwa na maombi ya pamoja pale PTA , ambayo kwa kweli yameamsha ari fulani, kiu yangu yasingeshia Dar es Salaam tu, maana naona baadhi ya maeneo ne ya Dar , bado kuna ubaguzi wa kimadhehebu, tukifanikiwa kuwa na umoja wa kweli , na ikafikia siku moja wa- KRISTO wote kama mwili wa KRISTO(bila kujali MAdhehebu) Tanzania mzima tuwe na siku hata 1 tu ya kufunga na kuomba kwa kumaanisha (kama walivyofanya Esta na Mordekai na WAYAHUDI WOTE enzi za Ahasuero mfalme,na ninaomba Mungu iwepo siku kama hiyo), na siyo tusubiri kwanza tupatwe na mambo fulani kwanza ndipo tuungane,nadhani matokeo yangekuwa ya kushangaza sana Ahasuero wa taifa hili angemjua Mungu wa kweli ni yupi.Jambo lingine, ninaamini kuwa kuna watumishi wengi wanapewa jumbe kama alivyopewa ask Kakobe ,lkn kuwa na ujasiri wa kusema walichoagizwa hapo ndipo penye kazi. Lakini maombi ya umoja yana nguvu yake yatawatia ujasiri wa kufunua Mambo wanayoagizwa bila woga, na nchi yetu itapona.Na MUNGU wetu ataheshimiwa .

 22. Nashukuru kwa michango yenu. Nimependa huu ujasiri wa Askofu Kakobe kama kiongozi wa dini, na sana sana kama huu ujumbe umetoka kweli kwa Mungu. Wale tuliokuwepo mwaka 1995 tunajua alitabiri nini na kikatokea nini juu ya uraisi!!!. Orbi ni kweli hatujaweza impact society ya watz kama ulivyosema ndio maana wanatufanyia mambo kama hayo. Kuna issues nyingi walizonazo walokole ambazo zinawafanya wasiwe na sauti moja na kudharauliwa na jamii pamoja na serikali. Sasa kama nyie tu hamsikilizani wenyewe kwa wenyewe, vijembe kibao kwenye TV na redioni, watu wanatafuta utajiri tu kanisani waziwazi huku washirika wakiwa masikini wa kutupwa etc etc iweje serikali iwaone nyie ni wa maana na kuwakumbuka??? HATUNA BUDI KUBADIRIKA KAMA TUNATAKA MABADILIKO!!!!

 23. Wapendwa,

  Licha ya post yangu hapo juu ningependa kusema yafuatayo kama somo kwa Wateule wa Mungu. Kutengwa na serikali kunaweza kutufunza mengi.

  1. Inawezekana kabisa serikali imeshindwa kuona umuhimu wa WAPENTEKOSTE, licha ya kuwaalika viongozi wa serikali kufungua matamasha, kufungua makanisa,Kuzindua kanda hawajaona chochote ambacho tumeipa jamii ya kitanzania “impact” yetu imekuwa ni muziki wa Injili na mapambio ! Kama kweli tungeingusa jamii kama kanisa la Matendo ya Mitume “Kila mtu akaingiwa na hofu ajabu na ishara zikafanywa na mitume” Imani yetu ya Kipentekoste imekosa hofu kabisa katika jamii ya Kitanzania leo! Mimbari nyingi zimekuwa ni kama michezo ya kuigiza, makanisa yamekuwa sehemu ya kutafuta utajiri…hakuna tofauti na “wao” Je kweli kuna kitu cha wao kufunza au kusikia toka kwetu?

  2. Lakini pia lazima tukubali “KUTENGWA” na ” KUKATALIWA” kwa wanaomkiri Yesu ni sehemu ya Imani yetu! Kama wanatutenga kwa kuogopa UKWELI ambayo tutawapa sio mbaya kabisa….Labda hawataki kusikia sauti kutoka kambi ya Wapentekoste! Kama Jamii ya Tanzania au serikali ya Tanzania imetukataa kwa sababu hiyo ni heri yetu…….Maana sisi si wa Ulimwengu huu………Kukubali na serikali inaweza kuwa ni Ishara mbaya kwa Kanisa….! Lazima tujue Hilo pia.

  3. Hebu tutumie kutengwa huku na serikali kuanza upya kuinena na kuitangaza INJILI KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIMU…..NA KUOMBA BWANA AWE PAMOJA KWA ISHARA NA MIUJIZA……..SERIKALI ITATAMBUA TUPO……Wao wenyewe watakuja kututafuta….! MBARIKIWE.

 24. Wapendwa,

  Tunahitaji ujasiri namna hii ambao umepotea kwa watumishi wengi Tanzania, Watumishi wengi wamekuwa waoga kabisa kusema wanachokiamini, kuanzia kukemea dhambi ndani ya familia zao, ndani ya nyumba ya Mungu, na hata ngazi ya taifa, na kwa matokeo hayo tunaona Kanisa la Mungu limefika wapi leo, na taifa la Tanzania liko wapi, huhitaji macho ya kiroho kuona taifa la Tanzania limekwama, kuangia juu kabisa hadi kwa mwanamchi wa hali ya chini…..hakuna MATUMAINI

  Kwa kiongozi wa nchi anayewatawala wananchi wa kila aina inashindikana kabisa kukubali kwamba ameshindwa kuchagua mwakilishi katika kundi la wananchi wanokadiriwa kuwa milioni 10! Serikali ya Tanzania ingeinga hata nchi nyingine basi Kenya, Africa Kusini ambayo katiba yao iliweza kubeba mwakilishi katika kila kundi la la Jamii……Kwetu kama ni kweli inasikitisha kama ni kweli kuna wawakilishi hata wa Waganga wa Kienyeji….sisemi wasiwasiwakilishwe………lakini Kwa nini ukatee mwakilishi kutoka kundi kubwa linajulikana nchini kama Wapentekoste?

  Na kwa wale wanaosema kazi yetu sio katika mimbari ya siasa, nataka kusema Bunge la Katiba sio siasa ni uwakilishi wa kutaka kutengeza na kuandaa mstakabali wa Taifa letu, kwetu sisi hata kujadili utaratibu wa kuendesha Huduma zetu kisheria….maana tunatenda kazi ya Bwana chini ya mamlaka…..!

  Ubarikiwe Mtumishi wa Mungu Kakobe, Naamini kabisa kila kitu kinaonyesha wazi hakuna gundi tena inayoweza AU itakayoweza kuishikamanisha CCM…..na kwa kulidharau kundi ambalo limekuwa likimlilia Mungu kwa maombi usiku na mchana kwa ajili ya Taifa, naamini kabisa huu ndio mwanzo wa kuanguka Chama Tawala.

 25. Kwanza nimpongeze Askofu Kakobe kwa ujasiri, hawa a ndio akina Elia wa leo wenye ujasiri wa kusema na serikali bila kumung”unya, hata kwa gharama ya kifo, maana ukweli unauma. Niseme Mungu amtie nguvu mtumishi huyu kwa kujitoa .

 26. safi sana mtumishi wa Mungu Kakobe,bila shaka umefuata kielelezo cha Daniel Vs Mfalme Nebukadreza!! Safi sana.

  Kamau,

  Ongera kwa michango mizuri. Umeiweka sawa kabisa.

  Lakini ningependa kuwaomba wapentekoste wote, endeleeni kuliombea bunge la katiba linaloendelea , kwani mambo yakiharibika uwa wanao suffer ni walala hoi, hao wakubwa wala hautawasikia. lakini pia hata km Mhe. Rais kwa bahati mbaya au kwa kukusudia kawaacha nje, si wapo wawakilishi wengne wa madhehebu ya wajumapili, watumieni hao kuwasilisha mapendekezo yenu.

  – tusisahau biblia inasema adui mpende, waombeeni wanaowaudhi! Hakuna haja ya kuendelea kulaumu, tuliombee bunge la katiba linaloendelea positively ili lifanye maamuzi ynye maslai kwa watanzania wote.

  -ubarikiwe mtumishi wa Mungu Kakobe kama unaliombea Bunge la Katiba POSITIVELY.ikumbukwe nikwa maslai ya watanzania wote.

  -Na kwa kweli malumbano yanayoendelea sasa kwny vikao vinavyoendelea, Mungu na aingilie kati! maombi ya wacha Mungu ni muhmu kunusuri hali iliyopo.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu liongoze Bunge la Katiba.

  Amen.

 27. Naomba kumjibu Mashurano hapo juu.
  Unaposema ya Kaisari mpeni Kaisari naona huelewi maana yake. Katiba ni sehemu ya utawala inayomhusu kila raia awe mpagani au muumini wa dhehebu lolote. Ndio maana madhehebu yote yameshiriki. Usichokifahamu wewe ni kuwa wachawi na waganga wa nchi hii wanaogopa uwepo wa watu wa Mungu kwenye bunge la katiba kwa sababu katiba ikishatungwa kinachobakia ni kuitii tu bila ubishi.

  Mambo ya Kuhubiri injili yako chini ya sharia pia. Ndio maana hata kufungua huduma unaambia usajiliwe na msajili wa vyama. Msajili yumo ndani ya katiba na anafanya kazi kwa mujibu wa katiba.

  Hata ukiandaa mkutano wa injili unatakiwa kuzingatia sharia ikiwamo kupata vibali kadha wa kadha.

  Hongera sana Kakobe kwa kutoa tamko la maana kuliko yote yaliyotolewa na wapentekoste.

  Wapentekoste acheni kushabikia matamasha huku mnatengwa kwenye mambo ya maana!

 28. Mpeni Mungu yaliyo yake Mungu na mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari. Kwangu mimi kama ningekuwa mchungaji ningesema” maadam Injili ya Yesu inapigwa” Lakini huku sitaki naa kule nataka ndiyo shida yetu cc wanadamu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s