Hakuna Mwisho wa Kusamehe!

msamaha

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,

Hakuna likizo ya kutosamehe!!!!!!!!  Chukulia  saba mara sabini iwe ktk kipimo cha siku hivyo 7×70 = 490 na je si mwaka una siku 365/366 HIVYO NI KILA SIKU KUSAMEHE TU! Ktk Mathayo. 18… Naposoma naona kama SIJUI PETRO ALICHOKA KUBOREKA/KUKWAZWA maana da! mpaka akauliza swali hili…  by the way, he was very open/sincere -I like that!

Mstari wa 21 …”’Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba”’ 

Look/feel him(Petro) at this statement yake…”’ ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba”’.. angalia kisehemu hiki kwa macho makubwa.. ‘’hata mara saba?’’!!!!!!. In other words, He was looking for a deadline/chance/ permit to say, ENOUGH IS ENOUGH brother or Sister! To hell or heaven with you, go East, I pick West, over and out, we meet in heaven or somewhere else not in hell  hopefully!!!!!!!!

Nonetheless, think about how Smart Jesus alivyommaliza na kuset standards ya sisi kufuata ktk kusamehe no matter what! Mstari 22: ‘’’Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

Fikiri sehemu hii ya jibu la Yesu  …’’Sikuambii’’…aliongea kwa kumkamia kweli kweli, kumaanisha haswaa, ku-highlight, bold and underline kweli kweli..Sikuambii….mara 7 tu bali….. kumaanisha alichosema -KUSAMEHE ni  mwanzo mwisho, day on/off as long as kuna mtu anakutibua/mnatibuana, NI KUSAMEHE TU,  shurti swala la kusamehe litekelezwe! Yesu hakuropoka au kusema kwa bahati mbaya au bila kufikiri deeply possibility ya applicability ya statement/Neno lake,  alisema kwa hakika akikomaa..Sikuambii mara 7 tu bali 7×70 = 490,  yaani unasamehe kila siku mwaka mzima hadi advance ya kusamehe, unatoa mpaka mwaka unaofuata

Kindly read the whole chapter to get the flow..  maana mstari wa mwisho unasema ivi….35  Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake, hence soma sura nzima tafadhari kupata kitu kizima.

Mathayo. 18:1-35….1  Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,2  Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,3  akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.4  Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.5  Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;6  bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.7 Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!8  Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.9  Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.10  Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.11  [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.]12  Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?13  Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea.14 Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.15  Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.16  La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.17  Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.18  Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.19  Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.21  Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?22  Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.23  Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.24  Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta25  Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.26  Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.27  Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.28  Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari29  Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.30  Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.31  Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.32  Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?34  Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.35  Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

SWALI:  Unadhani kuna jambo umetendewa baya sana sana humu Duniani na Walimwengu?Tuna options 2 tu!  

Kwanza, Mstari 22: ‘’’Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali(Samehe) hata saba mara sabini. 

Pili, 35  Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake 

Sasa, The choice is yours, mimi nimechagua kusamehe kila Mtu na kila kitu.Amen

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

4 thoughts on “Hakuna Mwisho wa Kusamehe!

 1. Mungu akubaliki hapa haitaji majadiliano hapa tumwombe Mungu atupe neema ya kutendea kazi ebu fikili mtu kama Stephano anapigwa kwa mawe kisha anasema baba uwasamehe maana hawajui watendalo ebu tuwe watendaji wa Neno balikiwa ameni

 2. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu. kweli umetukumbusha kitu ambacho nikigumu sana. Mungu anipe neema ili niweze kusamehe na kusahau

 3. Oooh!nimeipenda hii tena sana!na ya2pasa Mungu a2saidie maana ckuhizi wapendwa 2mekosa uvumilivu!Neno limekuja kwa wakati mwafaka!na naamini litame2ponya wengi!Barikiwa Kaka!

 4. Asante Seleli kwa Kunikumbusha neno muhimu kiasi hiki.
  Hii ni mojawapo ya zawadi nzuri za rohoni ambazo umewahi kunipa binafc (sisemei mioyo ya wengine)

  Cha msingi na juu ya hili, tujizoeshe kusamehe na KUACHILIA sbb ukilishikilia jambo ht km umesamehe linaleta uchungu moyoni ambao utakurudisha kwenye kutosamehe kila unapojaribu kulikumbuka sbb kwa ukubwa wa chukizo au maudhi moyo huumia.

  Asante tena mpendwa Mungu wa mbinguni akulipe ukiwa hai.

  Gladys

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s