Kumkufuru Roho Mtakatifu!

kukufuru

Naomba kuuliza, kwanini maandiko yanasema kwamba dhambi yoyote itasameheka isipokuwa ya kumkufuru Roho Mtakatifu, je ni kwa nini? au nini maana ya kumkufuru Roho Mtakatifu?

–Solomon

Advertisements

9 thoughts on “Kumkufuru Roho Mtakatifu!

 1. Ndugu Dikson,

  Tukiiondoa kila dhambi ndani ya huo mtazamo wa kumkufuru RM hilo tendo la kumkufuru halitakuwepo.

  Biblia inasema kama hiyo dhambi haisamehewe. Sasa Anania aliambiwa kama hamdanganye Petro bali RM ndipo akaanguka na kufa. Angelikuwa amedanganya Petro angeliomba toba, lakini kumbe allikuwa ameenda mbali pasipo kufahamu kwani kutofahamu nayo ni dhambi. Sasa Mungu hakuwa anapendelea tu kifo cha Anania, lakini ni Anania yeye ndiye alitenda ndambi ambayo haina toba, akidanganya RM. Kumkufuru RM hatuaiona kama dhambi yenyewe, lakini ni tendo fulani linalohusu dhambi dhidi ya RM.

  Kwa kuwa Anania hakupona, na mkewe safira naye hakupona, walitenda dhambi ya kifo na biblia inasema kama walidanganya RM. Hiyo dhambi haikusamehewa. Hence angalisho RM hadhihakiwe.

  Asante.

 2. HAPA NDIPO ILIPOFICHWA SIRI YA WENYE HAKI NA WASIO HAKI!!

  Naomba tumshike mkono Roho Mtakatifu alafu twende nae FARAGHA ili atujulishe
  mambo makubwa na magumu ambayo hatukuyajua!(YEREMIA 33:3).Naomba tuingie ndani ya NENO LA MUNGU kwa namna ambayo itaibua tafakari zaidi na kutupa mafunuo ya kutisha.Kumbuka Mwalimu wetu ni ROHO MTAKATIFU na mimi
  natumika kama chombo kilicho kubali kukamilishwa kwa unyenyekevu wa machozi,jasho na damu.EEH Mungu naomba UWEZA WAKO utufungue akili zetu ili tuweze kuyaelewa MAANDIKO yako.Katika MATHAYO 22:29, Yesu anasema”……..Mwapotea kwa kuwa hamyajui MAANDIKO wala UWEZA wa Mungu”.Hatuwezi kulijua NENO LA MUNGU(maandiko) kama tusipofunuliwa na ROHO MTAKATIFU(uweza wa Mungu).Wengi tumekuwa tukipotea njia na kwenda nje ya NJIA YA NENO LA KRISTO.Ni lazima tukubali kwamba BADO HATUJAJUA JINSI TUNAVYOPASWA KUJUA(1 WAKORINTHO 8:2).Na kwa yale tunayoyajua,TUNAFAHAMU KWA SEHEMU NA KUTOA USHUHUDA KWA SEHEMU(1WAKORINTHO 13:9).ROHO YA KUJITIA UJUAJI NA KIBURI CHA UZIMA KINATUFANYA TUSIWE TOFAUTI NA MAITI ZINAZO TEMBEA!Ni zaidi ya hasara kuonekana upo ndani ya wokovu kumbe ULISHA KUFA KIROHO siku nyingi,unangoja
  tu kuzikwa kimwili!!

  MASWALI YANAYOTUPA CHANGAMOTO ILIYO HAI KUHUSU WALE AMBAO TAYARI
  WAMESHA MKUFURU ROHO MTAKATIFU.

  Ni lazima tuyakabili haya MAANDIKO na wala tusijaribu kuyakwepa.
  MWANZO 6:1-2 “Ikawa WANADAMU walipoanza kizidi usoni pa nchi na wana wa kike
  walizaliwa kwao.WANA WA MUNGU waliwaona hao binti za WANADAMU ya kuwa ni
  wazuri, wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.BWANA akasema Roho yangu haitashindana na MWANADAMU milele……”
  Kuna tofauti gani kati ya WANADAMU na WANA WA MUNGU?Kwanini Mungu alikasirishwa na ndoa kati ya WANADAMU na WANA WA MUNGU?Ni kwanini Mungu
  aliwaumba WANADAMU? na kwanini aliwaumba WANA WA MUNGU?Ni nini kiini na chanzo cha kuumbwa kwa WANADAMU na WANA WA MUNGU?

  MITHALI 16:4 “BWANA amefanya kila kitu kwa KUSUDI LAKE.Naam,hata WABAYA kwa SIKU YA UBAYA”
  WABAYA ni watu wa namna gani? na Hiyo SIKU YA UBAYA ni ipi?kwahiyo kuna WAZURI na SIKU YA UZURI?JE! Mungu aliumba WATU WABAYA na WATU WAZURI?Kama jibu ni ndiyo, KUSUDI LAKE lilikuwa ni nini??

  ZABURI 58:3 “WASIO HAKI wamejitenga tangu kuzaliwa kwao.Tangu TUMBONI
  WAMEPOTEA wakisema UONGO”.
  Hao WASIO HAKI ni kina nani? na kwanini walijitenga tangu kuzaliwa kwao?Mtu anawezaje kupotea tangu akiwa tumboni mwa mama yake tena kwa kusema UONGO? Ina maana kuna watu walifundishwa kusema UONGO tangu wakiwa tumboni mwa mama zao? Je tutakuwa sahihi tukisema kuna watu walifundishwa kuishika KWELI tangu wakiwa tumboni mwa mama zao kama ilivyo kuwa kwa Yohana
  mbatizaji? kwahiyo kumbe duniani kuna WENYE HAKI na WASIO HAKI?kwanini watu
  wote tusiwe WENYE HAKI kwasababu wote tuliumbwa na Mungu??

  MITHALI 24:16 “……MWENYE HAKI huanguka mara saba,AKAONDOKA TENA, bali
  WASIO HAKI hukwazwa na mabaya”.Tuunganishe na MITHALI 14:9 “WAPUMBAVU
  huidharau hatia.Bali UPO UPENDELEO kwa WENYE HAKI”.Pia tuunganishe na MAOMBOLEZO 3:22 “Ni HURUMA za Bwana kwamba hatuangamii kwa kuwa
  REHEMA zake hazikomi”
  Je tunaweza tukasema kwamba WENYE HAKI wana UPENDELEO unaoitwa REHEMA ZISIZOKOMA?? Na WAPUMBAVU( watu wabaya) hawana UPENDELEO unaoitwa REHEMA?? Je hawa WATU WABAYA(WAPUMBAVU) ndiyo watu wanaoitwa WASIO HAKI? Nini kiini na chanzo cha huu UPENDELEO kwa WENYE HAKI?

  YUDA 1:4,12,13,19 “Kwa maana kuna WATU WALIOJIINGIZA KWA SIRI,WATU WALIOANDIKIWA TANGU ZAMANI HUKUMU HII,makafiri, WABADILIO NEEMA YA MUNGU WETU KUWA UFISADI NAO HUMKANA YEYE ALIYE PEKE YAKE MOLA, NA BWANA WETU YESU KRISTO.WATU HAWA NI MIAMBA YENYE HATARI KATIKA
  KARAMU ZENU ZA UPENDO…..NI NYOTA ZIPOTEAZO AMBAO WEUSI WA GIZA NDIYO AKIBA YAO WALIOWEKEWA MILELE.WATU HAO NDIYO WALETAO MATENGANO,WATU WA DUNIA HII TU,WASIO NA ROHO.
  Ndugu yetu Yuda alizungumza maneno mazito mno.
  Hawa watu waliojiingiza kwetu kwa siri na huku walishaandikiwa hukumu ni kina nani?
  Je hawa ni watu ambao walishamkufuru Roho Mtakatifu kwahiyo hukumu yao ilishapitishwa?? kumbe kuna NYOTA zipoteazo ambazo zilishatayarishiwa giza la milele? Kumbe kuna watu wa dunia hii ambao kamwe hawawezi kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu?? Je wanapojumuika nasi katika ibada zetu na kujifanya wananena kwa Lugha huko ndiyo kumkufu(kumtukana) Roho Mtakatifu??

  HEBU TUZAME NDANI KIDOGO.
  Yesu alikuwa ana maanisha nini aliposema kuwa kuna watu wanalitaja sana jina lake
  na kulitumia wanapotoa unabii, mapepo na kufanya miujiza lakini kweli ni kwamba wanatumia nguvu nyingine na hivyo hawatambui katika ufalme wake?Ni watu wa namna gani hawa ambao Yesu anawaita MBWAMWITU WAKALI waliovaa mavazi ya kondoo?(MATHAYO 7:15-23).Yesu anasema wazi kabisa kwamba HAKUNA MBWAMWITU anayefanya biashara ya kutoa mapepo kwa kutumia nguvu za ROHO
  MTAKATIFU kwasababu kwa kufanya hivyo atakuwa ameukana (ameufitini) ufalme
  wa shetani.Kwa hiyo wanapoigiza kwamba wanatoa mapepo kwa nguvu za ROHO
  NTAKATIFU na huku wanafanya michezo ya kishetani wanakuwa wanamdhihaki na
  kumtukana Roho Mtakatifu na huku ndiyo kumkufuru Roho Mtakatifu.Kwahiyo HATA WENYE HAKI akifanya hivyo ATAKUWA AMEMKUFURU ROHO MTAKATIFU.
  kama Mtumishi wa Mungu aliye hai anatoa mapepo kwa nguvu za Roho Mtakatifu alafu wewe unawaambia watu kuwa anatumia nguvu za shetani na ukasema hivyo ukiwa na lengo la kuharibu huduma ya huyo mtumishi huku unajua kabisa anatumia
  nguvu za Mungu,huko ni KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU.(TAFAKARI-MATHAYO
  12:22-32).
  SIKILIZA kwa makini,WENYE HAKI WANA UCHAGUZI WA KUMKUFURU AU KUTOMKUFURU ROHO MTAKATIFU lakini WASIO HAKI HAWANA CHOICE.
  HAWANA JINSI AMBAYO WANAWEZA KUMUUNGA MKONO ROHO MTAKATIFU
  WALA KUMPOKEA.WAO WANANENA,KUTABIRI NA KUONGOZWA NA ROHO WA SHETANI ambaye huwashukia kama vile sisi tunavyoshukiwa na ROHO MTAKATIFU!!Si kila mtu anaweza kupata neema ya wokovu na wala hatuwezi kumlazimisha Mungu iwe hivyo.Ndiyo maana Yesu alikuja KUWASHA MOTO kuwatenga WENYE HAKI WAWE MBALI NA WASIO HAKI.Inawezekana wewe ni MWENYE HAKI lakini wazazi wako na ndugu zako ni WASIO HAKI.Unatakiwa uendelee kuwapenda lakini
  ukweli ndio huo.Mtu yeyoye asiye haki hawezi kumuongelea Roho Mtakatifu kwa mema.Kwanza hamjui,kazi za Roho Mtakatifu kwake ni kama maigizo tu(LUKA 12:49-53).

  ANANIA na SAFIRA hawakumkufuru Roho Mtakatifu bali walimdanganya Roho Mtakatifu wakidhani wanamdanganya Mtume Petro! Walikuwa na nafasi ya kutubu
  dhambi yao ya kusema uongo lakini kwa kuwa walikuwa wamedhamiria kutotubu KIFO CHA GAFLA KIKAWAKUMBA ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE.Tunaposema
  uongo tunakufa kiroho kwahiyo tunatakiwa kutubu ili tuhuishwe kiroho na kurudishwa zizini na kama tukigoma kutubu alafu kifo cha kimwili kikatukuta,tunaenda moja kwa moja KUZIMU!(MATENDO 5:1-11).

  Sililiza maneno ambayo YESU anawaambia WENYE HAKI, “……NINYI MMEJALIWA KUIJUA SIRI YA UFALME WA MUNGU, BALI KWA WALE WALIO NJE YOTE HUFANYWA KWA MIFANO, ILI WAKITAZAMA WATAZAME WASIONE NA WAKISIKIA
  WASIKIE WASIELEWE. WASIJE WAKAONGOKA , NA KUSAMEHEWA”MARKO 4:11,12.

  Kwahiyo WASIO HAKI(walio nje) HAWAJAJALIWA(hawajapewa neema) kuijua SIRI
  YA UFALME WA MUNGU.WANATAZAMA LAKINI HAWAONI!WANASIKIA LAKINI
  HAWAELEWI!Kuna tofauti ya milele kati ya MANABII WANAOSEMA UONGO AMBAO NI WATUMISHI WA MUNGU ALIYE HAI(YEREMIA 23:16-22) NA MANABII WA UONGO(MATHAYO 24:24,25).MANABII WA UONGO walizaliwa wakiwa tayari
  wameshafundishwa uongo.Ni watu WASIO HAKI ambao kazi yao ni kuua maono
  na kuharibu hatima ya maisha ya WANA WA MUNGU lakini Mungu ameshawahukumu(ZABURI 58:3-11).Manabii wa uongo humkufuru ROHO MTAKATIFU kwa namna ya kutisha sana.Wajumbe wote wa shetani ni manabii wa uongo wanaoongozwa na ROHO YA BABA WA UONGO INAYOMKUFURU ROHO MTAKATIFU(YOHANA 8:42-44).

  SI KAZI RAHISI KWA MWANA WA MUNGU ANAYEONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU, KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU.NI MPAKA AAMUE KUMKANA YESU NA KUJIUNGA NA SHETANI.

 3. Johnstone,

  Nakubaliana na wewe kama kuukana wokovu ni mojawapo wa kumkufuru RM. Lakini unalolisema halikamiliki kwani sione kama ni kuukana wokovu kabla au baada ya kuupata.
  Pia mtu anaweza kuwa hakuukana wokovu yaani anafahamu kama Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na anazijua kazi Yesu alizozifanya msalabani, lakini anatumbukia ndani ya kumkufuru RM.
  Kwa mfano Anania na Safira walimkufuru RM kwa kumdanganya. Lakini ukichunguza vizuri utagundua kama walikuwa wakristo. Walikwama tu wakajikuta ndani ya uongo usiyo na msamaha yaani kumdanganya RM; ndiyo maana wakafa. Hence, kuna namna nyingi ya kumkufuru RM: kumtukana, kumdanganya, kumpinga, kumdharau, kumshakia, …

  Asante

  Asante.

 4. Shalom wapendwa ,
  kumkufuru roho mtakatifu kuko kwa aina nyingi, kazi za roho mt ziko nyingi sana, hapa endapo hukutii,kusema au kuwazia vibaya kazi za roho mtakatifu,hiyo dhambi haisameheki, Tunatakiwa kuiheshimu uweza wa mungu .

  mbarikiwe.

 5. Asante kwa swali lako zuri.Maana ya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu maana yake ni kwamba unaamua kuuacha wokovu na kuona kazi yote aliyo ifanya Yesu msalabani kuwa ni bure yaani nisawa na kuukana wokovu.Hii ni kwasababu mtu anapo okoka anampokea Roho Mtakatifu nahivyo akiukana wokovu ni kwamba ana mkana Roho Mtakatifu.amen barikiwa sana

 6. Ndugu Solomon,

  Shukran kwa swali lako, pia kwa wenzangu ambao walikujibu. Mungu awabariki. Ninafika leta mchango wangu licha ya kuwa wengi walichanga kwa namna hiyo.

  Jaribu kusoma hizi shahiri :

  « Marko 3 :
  22 Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, ANA BEELZEBULI, NA, KWA MKUU WA PEPO HUWATOA PEPO.
  23 Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?
  24 Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;
  25 na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
  26 Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.
  27 Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.
  28 Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;
  29 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu HANA MSAMAHA hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
  30 KWA VILE WALIVYOSEMA, ANA PEPO MCHAFU.”

  na

  “1 Yohana 5:
  5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye AAMINIYE ya kwamba YESU NI MWANA WA MUNGU?
  6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.
  7 NAYE ROHO NDIYE ASHUHUDIAYE, KWA SABABU ROHO NDIYE KWELI.
  8 Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.
  9 Kisha wako watatu washuhudiao DUNIANI, Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
  10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. ASIYEMWAMINI MUNGU AMEMFANYA KUWA MWONGO, KWA KUWA HAKUUAMINI HUO USHUHUDA AMBAO MUNGU AMEMSHUHUDIA MWANAWE. »

  Fanya connection ya hayo maneno. Nafasi nyingi neno moja likijifunzwa nje ya mantiki yote huwa inaleta tatizo kwa kulielewa.
  Hapo hatika Injili jinsi ilivyoandikwa na Marko pamoja na fasi nyingine kunapopatikana ile tamko « kumkufuru Roho Mtakatifu », utaona ile tamko iko katika maneno yasiyo mepesi sana lakini yanayoeleweka kiasi. WALE AMBAO HAWATASAMEHEWA NI WOTE WANAOSEMA KAMA YESU ALITENDA MIUJIZA KWA NGUVU ZA PEPO CHAFU.
  Sasa ukiiconnect na hiyo uliosoma ndani ya kitabu cha 1 Yohana, utaona Roho mtakatifu ndiye mshuhuda HAPA DUNIANI kama Yesu ni mwana wa Mungu. Pia asiyemwamini ule ambaye Roho Mtakatifu anaeshuhudia amefanya huyu ROHO MATAKATIFU KUWA MWONGO, wakati andiko limetangulia na kuthibithisha kama Roho ni Kweli.
  Kama umedaka vizuri, utaona kama kumkufuru Roho Mtakatifu ni kumfanya mwongo/ kupinga anachoshuhudia/ Kuwa na msimamo kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu/Kumdharau na kumwita Mwana wa Yusufu/Kutoamini kama miujiza yake ni ya ki Mungu/Kupindisha ukweli wa Roho Mtakatifu.
  Na ukiendelea kusoma utagundua maneno mengine kama kutoamini kama Yesu Kristo ndiye njia, kweli na uzima, nk
  Hayo mambo yote hayana msamaha kwani yanapinga ule ushuhuda wa Roho Mtakatifu.

  Na baraka kutoka Mwenyezi Mungu ziwe nyingi kwako.

 7. Jesus said this because some people were saying “he has an evil spirit in him” read more:

  “THE GOSPEL OF MARK”

  The Unforgiveable Sin (3:22-30)

  INTRODUCTION

  1. During His earthly ministry, Jesus faced great opposition from
  religious leaders…
  a. By Pharisees and Herodians who plotted to destroy Him – Mk 3:6
  b. By scribes from Jerusalem, who accused Him of using demonic power
  – Mk 3:22

  2. In our text for this lesson, Jesus easily answered the scribes’
  charge…
  a. For Satan to cast out demons defeated his (Satan’s) own purpose
  – Mk 3:23-26
  b. On the contrary, casting out demons was integral to defeating
  Satan – Mk 3:27

  3. On this occasion Jesus mentioned an “unforgiveable sin”…
  a. Blasphemy against the Holy Spirit – Mk 3:28-29
  b. For which there is no forgiveness – cf. Mt 12:31-32

  [These words of Jesus have troubled many, who wonder if they have
  committed this “eternal sin” (ESV) that “never has forgiveness”. Let’s
  first seek to identify exactly what was…]

  I. THE UNFORGIVEABLE SIN THEN

  A. WHAT WAS THIS SIN…?
  1. Jesus described it as blaspheming the Holy Spirit – Mk 3:29
  a. Blaspheme – “to speak reproachfully, rail at, revile,
  calumniate, blaspheme” – Thayer
  b. Thus to speak evil of the Holy Spirit in some way
  2. Mark reveals exactly how they spoke evil of the Spirit – Mk
  3:30
  a. “because they said, ‘He has an unclean spirit.'”
  b. By attributing Jesus’ power to cast out demons to Beelzebub
  (Satan), they spoke evil of the Holy Spirit by whom Jesus
  cast out demons – cf. Mt 12:28
  3. In effect, they were calling the Holy Spirit a demon; in so
  doing…
  a. They denied the evidence that Jesus was truly from God
  b. They deprived themselves of evidence to believe in Jesus
  c. They divested all hope of forgiveness that comes only
  through Jesus
  — The unforgiveable sin was to believe that the Holy Spirit was
  in fact Satan!

  B. CAN IT BE COMMITTED TODAY…?
  1. “Probably not. It was a sin committed when Jesus was on earth
  performing miracles. Since He is not physically on earth today,
  casting out demons, the same possibility of blaspheming the
  Holy Spirit does not exist.” – Believer’s Bible Commentary
  2. “People who worry that they have committed the unpardonable sin
  have not done so. The very fact that they are concerned
  indicates that they are not guilty of blasphemy against the
  Holy Spirit.” – ibid.
  3. From the NET Bible: “Three things must be kept in mind…”
  a. “The nature of the sin is to ascribe what is the obvious
  work of the Holy Spirit (e.g., releasing people from Satan’s
  power) to Satan himself”
  b. “It is not simply a momentary doubt or sinful attitude, but
  is indeed a settled condition which opposes the Spirit’s
  work, as typified by the religious leaders who opposed
  Jesus”
  c. “A person who is concerned about it has probably never
  committed this sin, for those who commit it here (i.e., the
  religious leaders) are not in the least concerned about
  Jesus’ warning”
  — Even if it can be committed today, if you worry that you have,
  you haven’t!

  [Speaking of “unforgiveable sins”, we do well to review how we can still
  fall into a condition where forgiveness is not possible as long as we
  remain in it…]

  II. THE UNFORGIVEABLE SIN TODAY

  A. WHAT IS THIS SIN…?
  1. There is a sin by which we “crucify again” the Son of God – He
  6:4-6
  2. There is a sin for which there “no longer remains a sacrifice
  for sin” – He 10:26-31
  — This sin is one in which there is no hope for forgiveness!

  B. HOW DO WE COMMIT IT…?
  1. Note carefully that it is an ongoing sin, a condition of
  rebellion against God
  a. Committed openly – cf. He 6:6
  b. Committed continually – cf. He 10:26 (“go on sinning”, ESV,
  NASB)
  c. Committed willfully – cf. He 10:26 (“deliberately”, ESV,
  TNIV)
  d. Committed knowingly – cf. He 6:4; He 10:26
  2. A spiritual condition in which one is doing grave things – He
  10:29
  a. Trampling the Son of God underfoot
  b. Treating the blood of the covenant (Jesus’ blood) a common
  thing
  c. Insulting the Spirit of grace
  3. A spiritual condition that left unchecked has grave
  consequences
  a. Fearful expectation of judgment – He 10:27
  b. Fiery indignation – He 10:27
  c. Worse punishment than death – He 10:28-29
  d. Vengeance and judgment by the Lord upon His people – He 10:
  30-31
  — It is any sin that we knowingly refuse to repent of, despite
  many opportunities!

  CONCLUSION

  1. Many today worry about blaspheming the Holy Spirit…
  a. A serious sin indeed, but likely cannot be replicated today
  b. If one worries about it, they are certainly not guilty of it!

  2. People should be more concerned about any sin…
  a. They knowingly commit
  b. They refuse to give up

  Whether one is obeying the gospel of Christ for the first time, or has
  already “tasted the heavenly gift” (He 6:4) and “received the knowledge
  of the truth” (He 10:26), all sins are “unforgiveable” unless we repent.

  Are we willing to let the goodness of God lead us to repentance…? –
  cf. Ro 2:4-5

  http://executableoutlines.com/mark/mk3_22.htm

 8. Mungu akubariki kwa kuuliza swali hili nami napenda kujibu kama ifuatavyo kwanza usome injili ya (Mathayo sura 12:-22…32) hapo unapata chanzo kwa nini Yesu alisema hivyo unaona ni viongozi wa dini ya kiyahudi wenye kufundisha watu habari za Mungu wanapinga utendaji,uponyaji wa Mungu wakisema Yesu ile nguvu ya uponyaji inatoka kwa shetani. kwa leo tunaweza kuwalinganisha watu walioamini na kuona matendo makuu ya Mungu kisha wakaanguka na kusema hakuna wokovu,kukataa miujiza ya ki Mungu,kwa sababu ya anguko la dhambi watu wanamna hiyo biblia inasema hawawezi kusamehewa soma waebrania 6:-4,6/10:-26)

  kwa hiyo nawasihi watu wote mliomwamini Yesu kuishi maisha matakatifu na yenye kumpendeza Mungu na yenye hofu ya Mungu kwani kuwa na wokovu wa kifafa unaweza kuombewa msamaha lakini mungu akakutataa kama alivyo mukataa mfalme sauli aliposhindwa kutii maagizo ya Mungu soma (1samweli 16:-1) leo watu wengi wanaishi maisha yasiyo nuru ya ulimwengu mimi nasema wanajidanganya nafsi zao wenyewa Mungu hafichwi kitu muulize mfalume daudi alitenda dhambi kwa sili,alimua uria kwa sili bali mungu alijua tuishi maisha ya kumhofu Mungu wakati wote balikiwa wote ni mimi shahidi wa YESU stephen ngulloh

 9. solomon,

  Ubarikiwe . Umeuliza swali nzuri sana!

  Mtazamo wangu ni huu:

  Kwanza kabisa maana ya neno , kukufuru ni: kunena kinyume cha Mungu.

  Hivyo basi, Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni hali ya kutokufanya ungamo na toba ya dhambi uliyofanya pale RM anapotushawishi. yaani RM ananena moyoni mwako hutubu wewe unasema “hii sio dhambi sitotubu”. Híi ni ile hali ambayo mtu ukubuhu ktk dhambi kiasi cha kuona kuwa dhambi aitendayo sio dhambi na hivyo kutoona haya ya kuungama na kutubu kwa dhati.

  Tukumbuke kuwa RM ana kazi kama kitabu cha Yohana Mtakatifu kisemavyo ni :kutuhakikishia kwa habari ya Dhambi, haki na hukumu. Hivyo basi tunapokosa mguso wa RM ndani ya mioyo yetu na hivyo kutokufanya toba. Hapo ndipo tunapokuwa tumefikia hali ya kumkufuru RM.

  Barikiwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s